Home → simulizi
→ RIWAYA: DAMU YA MWANANGU
SEHEMU YA KUMI NA MOJA(11)
*****ILIPOISHIA******
akaingia ndani ya kichaka hicho!
Nyamwela akaona huo ndio muda muafaka wa kutimua mbio...akafungua mlango taratibu akatimua mbio na kutokomea porini akajificha nyumba ya mti mkubwa,,akawa anachungulia kule barabarani,,akamuona ye dereva anatokea kichakani na kuingia ndani ya gari,,,,akaliwasha gari hilo akaliondosha kwa mwendo wa kasi!
Nyamwela akaonekana akitimua mbio kutokea porini kuja upande wa barabara..alikimbia huki akipiga mayowe,,kuashilia dereva asimamishe gari hilo...lakini akastaajabu kuona dereva huyo anaendelea na safari,,badala ya kurudi alipotoka!
Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa...akabaki kasimama katikati ya barabara huku kajishika kichwani! akaamua kuketi chini ya mti uliokuwepo kando ya barabara! akisubiri msaada wa lifti kwenye gari lolote litakalokatiza katika barabara hiyo.
*****ENDELEA******
Nyamwela.aliketi hapo chini ya mti kwa masaa mengi mfululizo..lakini hakuona dalili zozote za gari kupita katika barabara hiyo!
akaamua kunyqnyuka na kuzipiga hatua akitembea katikati ya barabara.....alitembea umbali mrefu kiasi....
wakati huohuo,,alionekana yule dereva wa taxi,,akiwa kalipata lile basi,,na kuchukua begi la Nyamwela,,akaingia nalo ndani ya taxi..akafunga milango na kufungua zipu ya begi hilo! akastaajabu kuona noti nyingi za shilingi elfu kumi kumi,,pamoja na nguo..akatoa nguo hizo na kuzitupa nje...akachukua pesa zote akazificha chini ya kiti alichokuwa amekalia!....
akalitupa begi nje! akaliondosha gari lake kwa kasi ya ajabu...kuifuata njia ya kurudi.......
Upande mwingine alionekana Nyamwela akiendelea kuzipiga hatua katikati ya barabara,,,akiwa kaweka mikono yake nyuma huku uwo wake ukionyesha kugubikwa na mawazo mazito!
punde si punde akaona,ile taxi ikimpita kwa kasi ya ajabu,,akajisemea moyoni,,"nashukuru hajanitambua,,angenidai pesa yake ya nauli....Nyamwela alijisemea maneno hayo huku akiendelea kuzipiga hatua,,,
alitembea umbali mrefu,,hatimae giza likaanza kutanda!
akatazama huku na kule hakuona dalili zozote za mqkazi ya watu kuwepo jirani na eneo hilo!
akaamua kupanda juu ya mti kwa lengo la kujihifadhi,,na kuepuka wanyama wakali,,kwa sababu eneo hilo limezungukwa na misitu yenye wanyama wakali!
alikesha usiku kucha akiwa juu ya mti huo,,hatimae pakakucha...akatelemka kutokq juu ya mti huo,,na kuifuata barabara,,,akawa anatembea kando ya barabara hiyo,, huenda akapata msaada lift ya gari lolote litakalo katiza katika barabara hiyo! kwa mbali akaliona moja kati ya mabasi ya kampuni ya basi alilolipanda jana...akafurahi,,,akiamini huenda akapata msaada...
akaingiza mkono wake mifukoni mwa suruali aliyokuwa ameivaa,,akatoa tiketi akaishikilia mkononi,,kisha akanyoosha mkono wake akiashilia dereva alisimamishe gari hilo!
dereva akapunguza mwendo hatimae gari likasimama...Nyamwela akaingia ndani ya basi hilo akaonyesha tiketi yake,,kisha akatoa maelezo kuwa jana alisahau begi lake katika moja ya mabasi ya kampuni hiyo....
dereva akamuonea huruma akasema nitakupa msaada wa lift ufike dar es salaam,,huenda begi lako limehifadhiwa katika ofisi zetu..
Nyamwela akasimama na kusikilia bomba, safari ikaendelea...
baada ya mwendo wa lisaa limoja kupita,,,Nyamwela akaona nguo zinazofanaan na nguo zake alizoziweka ndani ya lile begi!
lakini akapuuza,,ghafla akaona lile begi likiwa limetupwa kando ya barabara,,na linqonyesha halina kitu ndani yake!
Nyamwela akapaza.sauti na kusema,,"simamisha gari nimeliona begi langa tumelioita.
abiria wakamshangaa,,,ghafla ikasikika sauti,ya abiria mmoja akisema,,"bila shaka mtu huyu karukwa na akili,,atakuwa kachanganyikiwa!
abiria wengine wakadakia na kumuunga mkono abiria aliyesema hivyo!
Nyamwela akaendelea kusisitiza jamani simamisha gari begi langu tumeshalipita na nimeliona kwa macho yangu...
aliongea maneno hayo huku akimvuta dereva,,,
dereva huyo akaamua kusimamisha gari na kumfukuza Nyamwela atoke ndani ya gari,,akisema,,"sina uhakika kama unaakili timamu,,yani unanivuta,,wakati naendesha gari,,huoni kuwa unaweza kusababisha ajali? haya toka haraka ndani ya gari.
Nyamwela hakujali akashuka na kutimua mbio kurudi walipotoka...alikimbia kwa kasi,,hatimae akalikaribia lile begi! akaliokota!! macho yakamtoka,,begi hilo lilikuwa tupu,,halikuwa na kitu chochote ndani yake!,,Nyamwela akaanza kulia huku anacheka,,vyote kwa pamoja!!!! alipogeuza shingo yake kulitazama.lile basi,,kama bado limesimama,,,mara ghafla!!!!
TAHARUKI!
ITAENDELEA..........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: