OFA OFA OFA. SIMULIZI: JINA LA URITHI SEHEMU YA KUMI NA TATU(13) ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪ yule mwanakijiji aliyekabidhiwa dawa,,akazipiga hatua huku akiangaza angaza macho yake kumchagua mwanakijiji mmoja! mkusanyiko wa wanakijiji ulikuwa mkubwa,,,kiasi kwamba Jogolo alikuwa amezungukwa na umati huo,, yule mwanakijiji akasita! kuendelea kutembea,,akageuka na kurudi ule upande aliokuwepo mwanzo,,Jogolo hakuwa na wasiwasi,,aliamini huenda ameamua kumchagua mtu kati ya waliokuwa amesimama nyuma ya Jogolo.... lakini mwanakijiji huyo aka,ipiga hatua n akusimama mbele ya jogolo,,akaanza kuvua nguo na kuifungua dawa hiyo....macho yakamtoka Jogolo!! KIZAA ZAA!!!!!!! ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪ Jogolo akaingiwa na hofu akajaribu kutoweka kimiujiza lakini ikashindikana,,,hii ni kwa sababu dawa ile ya kichawi inanguvu kuliko nguvu alizokuwanazo yeye mwenyewe,,na kwa sababu tayari alikuwa ameshamkabidhi mtu mwingine ile dawa,,,kwa sasa hawezi kufanya chochote. mwanakijiji akazipiga hatua mpaka karibu kabisa na Jogolo,,kisha akakifungua kile kitambaa cheusi kilichokuwa na dawa ndani yake,,, akaichukua dawa hiyo ili ammwagie Jogolo mwilini,, ghafla,,likatokea tetemeko la ardhi,,likiambatana na mvua kubwa,,,waanakijiji wakaingiwa na hofu ,,,punde si punde dawa ile ikaishiwa nguvu ni baada ya kunyeshewa na mvua. ************************************ upande mwingine ulionekana mzimu wa muanzilishi wa ukoo wa Laula, mzimu huo ulikuwa ndani ya umbile la mtoto Laula....ukitazama kwa harakaharaka huwezi kutambua kuwa kunamzimu ndani ya mwili wa mtoto . Laula akazipiga hatua na kuingia katikati ya mji.. wakati huohuo kule kijijini ,,mvua iliendelea kunyesha,,wanakijiji waliendelea kuhofia maisha yao,,,ilinyesha mfululizo takribani dakika tano mfululizo...ghafla ikaacha kunyesha,,ukimya ukatawala kila mmoja alimtazama mwenzake usoni kwa macho ya uwoga Jogolo pia hakuamini kilichotokea. akajisemea moyoni,,"laiti kama mvua isingenyesha ningekuwa marehemu sasahivi! Jogolo aliongea maneno hayo huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu....Jogolo akasema,,"kunajambo nataka niwaeleze,,,dawa hii tayari imeshaharibika...kwa sababu imenyeshewa na mvua,,hivyo kunajambo mbadala lahitajika lifanyike haraka iwezekanavyo. wanakijiji waliendelea kubaki kimya,,hakuna aliyethubutu hata kufungua mdomo wake kuongea jambo ama kuuliza swali lolote. Jogolo akasema,,"usiku wa leo nitafanya jambo fulani,,lakini jambo hilo litafanyika makaburini,,ni lazima kaburi la muanzilishi wa ukoo wa Laula lifukuliwe. Wakati huo huo upande mwingine alionekana Laula akizipiga hatua kuifuata barabara ya vumbi,,,barabara hiyo ilikuwa na kilima kiasi....alitembea mfululizo kwa mwendo wa saa nzima,,,ghafla akaona njia panda! akaangaza macho yake kuzitazama njia hizo mbili.....akaamua kuifuata njia moja akazipiga hatua kadhaa kisha akatoweka kimiujiza! Ilipofika nyakati za usiku wa manane...akaonekana Jogolo akiwa makaburini,,tayari kuianza kazi ya kufukua kabuti la muanzilishi wa ukoo wa Laula.. bila kuchelewa akaanza kulifukua kaburi hilo....na baada ya dakika kadhaa akawa amemaliza kulifukua na kutoa udongo wote ndani ya kaburi hilo,,,akafanikiwa kuona baadhi ya mifupa ya muanzilishi wa ukoo wa Laula...akachukua fuvu la kichwa pamoja na mfupa mmoja wa uti wa mgongo..kisha akatoka ndani ya kaburi hilo kimiujiza...na kaburi likajifukia lenyewe... Jogolo akatoweka kimiujiza,,akajitokeza kule kijijini....mbiu ikapigwa,,wanqkijiji wote wakatoka kwenye majumba yao,,wakakusanyika sehemu moja.... Jogo akasema uwashwe moto mkubwa kwa ajili ya kuianza kazi ya kuangamiza ule mzimu.... ndani ya dakika kadhaa zikakusanywa kuni nyingi,,na moto ukawashwa.... Jogolo akausogelea moto huo akiwa kashikilia lile fuvu pamoja na mfupa wa uti wa mgongo....akavirusha ndani ya moto huo,,,kisha akachukua kisu akajitoboa kwenye mkono wake,,akanyunyizia damu yake kwenye moto huo,,kisha akazipiga hatua kadhaa kurudi nyuma. ukimya ukatawala kwa dakika kadhaa....wakisubiri kuona nini kitandelea.... punde si punde,,,ule moto ukazimika,,giza totoro likatawala! wanakijiji wakaingiwa na hofu kupita kiasi,,kwa mbali ukaonekana mwanga ukitokea upande mwingine kuja ule upande walipokuwa wamekusanyika wanakijiji....wakati wanatahamaki mara ghafla. akaanza kudondoka mwanakijiji mmoja baada ya mwingine...jambo hilo lilizua taharuki!!! wanakijiji wakaanza kupiga kelele....Jogolo akafungua mdomo wake kufanya jambo flani,,,huenda ikasaidia......kisha akachukua mchanga na kuuweka mdomoni....akatema mchanga huo na kuurusha ule upande unapotokea ule mwanga!!! mara ghafla!!!'' PATASHIKA! ITAENDELEA..... ITAENDELEA.....

at 11:50 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top