Home → simulizi
→ Sitaki tena – 06
Ilipoishia..,
bado haikusaidia kumjua ni nani
lakini ulikuwa ni mwili wa mtu
pale chini ambao kwa namna
moja au nyingine sikuweza
kuutambua mara moja,
kwa ushupavu wa halmashauri ya
kichwa changu ikanituma
nichukuwe panga na ku..
Endelea.,
Nichukuwe panga na kuchana
kipande cha nguo yake,nikafanya
hvyo kisha kile kitambaa
nikakificha katika pindo la nguo
yangu ya ndani halafu safari
ikaendelea,nilikatiza msituni bila
kuogopa kitu chochote na wala
kumuogopa yeyote hatimaye
baada ya kukimbia mda refu
nikahisi kama kitu kigumu
nakanyaga chini,furaha na amani
vikaanza kutawala ndani ya moyo
wangu kwani nilikuwa tayari nipo
katika barabara ya lami,akili ikawa
katika kukisia ni upande gani ndo
utakuwa unaelekea Dar na
upande gani utakuwa unarudi
Mbeya,nikiwa bado natafakari
likapita basi la
kwanza,nikashindwa
kulisimamisha nikaamua kusubiri
gari nyingine,kwani sikuwa hata
na nauli hvyo nikaamua nijifiche
niweze kudandia gari lolote
litakalopita kwa mwendo mdogo.,
Baada ya kukaa pale takribani
lisaa moja na nusu bila ya kuona
gari lolote hatimaye nikaliona gari
kubwa likiwa linakuja kwa
kujikongoja.,
"Kama kufa wacha nife tu.,lakini
hili gari siliachi.." nilijisemea
kimoyomoyo huku nikijiweka
tayari kwa kurukia lile gari aina ya
roli,huku mikuki na mishale
pamoja na lile panga nikilitupia
msituni,kitendo cha lile gari kufika
karibu yangu kikawa kosa kubwa
sana kwangu kwani ndani ya mda
mchache nikawa tayari nipo
nyuma ya lile lori lililokuwa
limebeba mbao.,
Kwa ujasiri niliokuwa nao
nikaingia mpaka mule ndani ya
lile lori kwa nyuma ambapo
sikumuona mtu yeyote kisha
nikarudishia mlango na kujilaza
kwenye zile mbao huku nikiwa
sina uhakika na ninapoenda,
"Sijui ndo litaishia morogoro au
ndo la Iringa hili gari?" hayo ni
kati ya maswali yaliyokuwa
yameandama ndani ya kichwa
changu,huku safari ikiendelea
taratibu baada ya mwendo mrefu
kidogo, ghafla gari likasimama
kwa mbali nikahisi sauti ya watu
wanajibizana kwa nje.,
"Hapana mkubwa mzigo wetu
hauwezi kuzidi kiasi hicho"
hapohapo jibu likanijia kuwa
tutakuwa tumefika maeneo ya
mizani,
"Embu fungua nyuma tuhakikishe
maana tani zimezidi na kama
hutaki paki pale gari yako
uandikiwe faini"
Wakiwa bado wanabishana pale
tayari kwenye gari nikawa
natetemeka mwili mzima huku
nywele zikinisimama na akili
ikinituma nifungue mlango,
nikisema nijifiche nyuma ya mbao
siwezi kwani ni kweli kulikuwa na
mbao nyingi kiasi kwamba nilipata
kanafasi kadogo sana ka kujificha,
"Mungu saidia.! Mungu saidia.!
Saidia jamani.!"
Ndio maneno niliyokuwa naomba
nisiweze kukamatwa kwani nia
yangu nikufika Dar,
Mda si mrefu nikaskia
mungurumo wa gari kuwashwa
kuashiria safari inaendelea moyo
wangu ukawa na furaha upya
nikajihisi ni mtu tofauti sana
duniani tena aliye na bahati
mbaya kupelekwa gerezani lakini
aliyejawa na bahati nzuri uraiani,
Nikiwa sina hata lepe la usingizi
huku safari ikiendelea niliweza
kushuhudia tena kwa mara
nyingine kuki kuchwa kwani
mwanga ulikuwa umeshatoka
kuashiria kuwa ni alfajiri,gari nalo
likatembea ka mwendo kidogo
kisha likasimama, sauti na
makelele ya watu ndio
yalichochea hisia zangu,niliweza
kutoa jicho langu kupenyeza
kwenye kauwazi ka mlango
nikaweza kushuhudia watu mbali
mbali,moja kwa moja nikapata
wazo la kuangalia kile kipande
cha nguo nilichokikata kule kwa
yule mtu msituni alikuwa ni nani,
Taaratibu mkono wangu ukaanza
kupenyeza mpaka kwenye upindo
wa nguo yangu ya ndani
nikakichukuwa kile kitambaa na
kukiangalia.,
"Mamaa..! mamaa..! nimeuwa
tena mungu wangu..!
Nisamehe Pendo..! Sijakusudia
mimi..! Maaaaa aaaaaaah..!"
Kumbe kile kilikuwa nikipande
cha nguo cha rafiki yangu
niliotokanaye gerezani 'Pendo'..
wakati nikiendelea kutoa sauti kali
nikahisi kunawatu wamezisikia
kelele zangu hivyo nikasikia
mlango unafungulia eneo
nililokuwa..,
"Sauti inatokea humu ndani
bwana, tena ni sauti ya kike."
aliongea mmoja ya watu
waliokuwa wanazungumza nje ya
lile lori nililokuamo ndani.,
"Mtoeni.!, mtoeni.! Tena anasema
ameua,embu mkamateni
tumpeleke polisi.."
Nilibaki nimezubaa huku nikiwa
sijitambui kipi cha kufanya,nikawa
natetemeka sana huku nikiishiwa
na pumzi,nahisi mapigo ya moyo
yalizidiwa kasi kwani nilijihisi
napata joto ghafla huku kijasho
chembamba kikiambatana na
mchozi uliokuwa unanitoka mithili
ya maji yakifata mkondo wake,
sikuwa na jinsi tena kwani
niliamini ndoto zangu za kuwa
uraiani zimekwisha na sijui
ntawaambia nini Gervas na mama
yangu endapo watasikia nipo tena
gerezani,
Huku kojo likiwa linanimwagika,
ukakamavu na ujasiri wote
ukinitoka nilijikuta natoa tena
sauti ya ukali.,
"Sio mimi..! Sio mimi..! Jamani
msinikamate.."
Huku nikinyosha mikono yangu
miwili kuelekea ile sehemu
niliyoamini ni mlango,taratibu
nikaanza kufungua ili nijisalimishe
ile namalizia kufungua tu tu nikawa
tayari nipo mikononi mwa raia
nisiowafahamu lakini walikuwa ni
wanaume wamevalia sare ambazo
sikuweza kuzitambua mara moja
huku juu wakiwa na mashati
meupe na wengine masweta
mekundu kutokana na hali ya
baridi kali lililokuwa limezunguka
maeneo haya,
Ilikuwa ni mchana tulivu kwani jua
lilikuwa si kali sana kutokana na
kaubaridi katika huu mji,wale
wenye hasira wakaanza
kunishambulia kwa kunipiga
makofi huku wengine
wakinishambulia kwa matusi
makubwa ya nguoni huku
wakiniburuza mithili ya mzoga
aliyeoza anayeenda
kutupwa,nilipiga kelele lakini
haikusaidia nilivutwa sana na wale
vijana..
"Wauaji kama nyinyi ndo
tunaowatafuta" aliongea mmoja
wa wale watu huku wakiwa
wamenichania vipande vya nguo
yangu, nilikuwa sina tena ujanja
na pia kulikuwa hakuna tena
muujiza utakaotendeka kwangu ili
niweze kujikomboa katika mikono
ya wale watu nisiowafahamu
walioonekana makatili wasio na
huruma hata kidogo.,
Waliniburuta kwa mwendo mrefu
sana,huku umati wa watu
ukifurika kunishuhudia,
walipokezana kunishika na
kunivuta,huku nikiwa bado nalia
na kung'ang'ania nisiweze
kupelekwa kituoni,
Nikiwa naendelea kulia huku
nguvu zikiniishia na kuacha
wafanye wanachokitaka,nikahisi
pumzi zimeniisha kwani kwa sasa
nilikuwa nahema juu juu huku
damu zikinimwagika pembezoni
mwa mdomo wangu, maji
machafu pamoja na matope
vilitawala mwilini mwangu huku
sura ikiwa imenivimba sana,
niliamini hata nikiendelea kulia
haitasaidia chochote,na pale
malengo yangu yalikuwa
yamefikia tamati kwani nilikuwa
nikipelekwa polisi,
Tukiwa njiani mwa safari huku
kipigo kikinizidia katika mwili
wangu huku macho yangu
yakiangaza huku na kule kupata
japo msaada wowote ndipo
yakakutana uso kwa uso na kibao
kilichoandikwa,
'TOSAMAGANGA HIGH SCHOOL'
Halmashauri ya kichwa changu
ikafanya kazi fasta hapo hapo
nakugundua kuwa wale si raia
wakawaida kama nilivyodhani bali
walikuwa ni wanafunzi katika kile
kijiji tena katika shule anayosoma
Gervas japokuwa sikumuona
katika wale watu waliokuwa
wakinipiga lakini niliamini lazima
alikuwa akisoma katika shule ile
kama alivyonielezea hapo awali
kwamba anasoma shule ya
wavulana tupu iliopo Iringa na
inaitwa 'Tosamaganga' hayo yote
aliniambia kipindi kile nipo
gerezani,
"kabla hamjanifikisha huko
kituoni naomba mniitie Gervas
Phota nimuage"
Niliposema hivyo tu wale jamaa
waliokuwa wamenishikilia
wakaniacha ghafla kwa mshangao
huku wengine wakiamini huenda
nilikuwa nimejifanyisha nimeua ili
niweze kuonana na Gervas na
wengine wakijiuliza nimemjuaje
Gervas? Wakanikazia macho,
"Gervas.? Mbona sisi hatumjui"
Walinijibu huku wengine
wakinicheka na kunisonya kwa
dharau,
"We dada una mashetani au
kichaa enhh.. Unamuitaji nani?"
jibu alilonipa mmoja wa wale
watu lilinifanya niingiwe na woga
huku meno yakiumana nakuhisi
labda Gervas alinidanganya
anasoma shule hii lakini
haiwezekani.,
Hasira zilizidi kunipanda kwani
kipigo kiliongezeka mara mbili ya
pale huku damu nyingi
zikiendelea kunimwagika, ghafla
nikasikia kama mlio wakengele
ukipigwa pembeni ya shule huku
watu waliokuwa wamevalia kofia
wakiwa wako na virungu
mikononi wakinifuata pale
nilipokuwa nimeburuzwa na wale
wanafunzi,hofu ilizidi kutanda
kwenye ubongo wangu,mwili
ulininyong'onyea kuona wale
watu wamevalia sare kama polisi,
kila walipokaribia lile eneo ndipo
nilitamani nife hapohapo,nikiwa
nagala gala pale chini huku wale
wanafunzi wakianza kutawanyika
kwa kuwaogopa wale watu huku
wakiniacha peke yangu nilianza
kujisogeza kwa mwendo wa
taratibu huku nikitumia magoti na
makalio yangu kujisogeza mpaka
nikaona chupa ya soda,nikaivunja
ili niweze kujiua kabla ya wale
askari hawajanifikia, nikiwa nataka
kuanza zoezi la kujiua mara yule
askari akawa ameshanikaribia na
kunipokonya ile chupa.,
"niache nife..,niacheni jamani..!
Nikiwa nimeshakata tamaa tena
ya kuishi,kwa haraka nikaweza
kuyakodoa macho yangu na
kumuangalia mtu aliyenipora ile
chupa niliyokuwa nimeivunja
vunja na kuacha ncha kali
nikitaka kujiua,nikaangalia mara
mbili mbili nikagundua kuwa yule
hakuwa askari polisi kama
nilivyodhani bali alikuwa ni mmoja
kati ya wale walinzi wa ile shule
waliokuja kutawanya na
kuwakamata wanafunzi sugu
waliokuwa nje ya shule mda wa
masomo,
"Pole sana binti angalia sana siku
nyingine watakuja kukubaka wale
wanafunzi wavuta bangi wale...!"
nilishangaa sana yule mlinzi
kunipora kisha akaniacha na
kuendelea kuwafukuza wanafunzi
wengine,nilijawa na nguvu na
furaha ya ajabu nakujiona ni mtu
wa bahati tena ya mtende, watu
wengi walinishangaa sana hilo
sikujali kwani maisha ya kupigwa
kama yale nilishayazoea tangu
kipindi kile nipo Gerezani.
Huku nikiwa nimelowa damu na
kuchanika karibu nguo yote
nliokuwa nimeivaa, nliweza
kujikokota chini chini mpaka eneo
la nyuma na ile shule kisha
nikaegemea chini ya mti mkubwa,
kwa uchovu na maumivu
niliyoyapata yalinifanya nianze
kunyemelewa na kausingizi
japokuwa kulikuwa na baridi kali
sikuwa na jinsi yoyote
yakukabiliana nalo,
"Twende bwana au unapenda
kubaki hapa porini..? Mi
nakuacha...Hapana.,
Pendo usiniache..! Pendo
usiniache...! Usiniache..!
Usiniache...! Usiniache..!
Peeeendooooooooo.......!"
Ghafla nikashtuka nakuanza
kuhema kwa kasi huku
nikitetemeka Levina mimi kumbe
ilikuwa ni ndoto tena nilikuwa
nikiota nipo na marehem pendo
kule msituni,usingizi ukanikata
nakuanza kuangaza kila upande
nakuona giza limeanza kutanda
lakini upande wa mbele yangu
kulikuwa na taa kali zilizomulika
ile shule, nikaanza kusogelea
taratibu kwa kuzunguka yale
majengo yaliokuwa yamewekewa
uzio huku nikitafuta lango la
kuingilia, hatimaye nikagundua
geti lilipo,walinzi takriban watatu
walikuwa wametanda pale lango
la kuingilia hivyo nikatafuta eneo
la choo kwani niliamini kukijua
choo itakuwa ni njia nyepesi ya
kuingia ndani ya ile shule, haraka
haraka macho yangu yakaweza
kuona wanafunzi wakiongozana
wakiingia kwenye jengo lingine
lililoonekana si kubwa sana kama
majengo mengine huku wakiingia
na kutoka, haraka haraka kwa
ujasiri na kwa shauku niliokuwa
nayo ya kutaka kupambana
mpaka nimuone Gervas nikawa
na nguvu ya ajabu yakuweza
kuruka ukuta japokuwa haukuwa
mrefu sana ndani ya dakika
chache nilikuwa tayari nipo
kwenye kale kajengo kalichokuwa
na vyoo vingi vyote vikiwa na
milango nikaingia choo
kimojawapo na kujifungia huku
nikishuhudia hamna mtu ndani,
harufu kali ya kinyesi na mikojo
katika vile vyoo nilipokuwamo
ndani havikunizuia hata kidogo
kuondoka mule ndani,niliweza
kutulia kimya huku nikiombea aje
kati ya Gervas au mwanafunzi
yeyote nimuulizie Gervas, mpaka
nikajishangaa kwa jinsi nilivyokuwa
sina woga wowote,
Ghafla nikasikia sauti ya kama
mtu anakuja,nikazidi kukaa kimya
ndani ya choo huku nikijiuliza
ntaanzaje mara ile sauti ya mtu
akiingia na kuanza kukojoa
mlango wa pembeni yangu,
nikafungua mlango wangu
taratibu na kuanza kunyata
kuelekea mlango aliokuwepo
huku akili ikinituma nimuwahi na
kumnyamazisha kabla hajashtuka
na kuanza kupiga kelele,
" Shhh..usiniogope wala
usikimbie..Naitwa Levina
natokea..."
Kabla sijamaliza kujitambulisha
yule mwanafunzi akawa
ameshanitambua..
" We si yule dada ambaye
nimetoka kuskia stori yako sa hivi
kwa wenzangu kuwa umepigwa
na kukuburuzwa mchana kutwa
pale nje na umeokolewa na
walinzi..?"
"Ndio mimi ila nipo hapa kwa
msaada mmoja tu, unamfahamu
Gervas Phota..?"
"Namfahamu na ninasoma naye
lakini yupo Chumbani anaumwa
leo siku ya pili yupo kitandani.."
"Tafadhali nisaidie kwa hili nenda
kaniitie mwambie Levina, nipo
hapa hapa chooni kwenye
mlango huu nawasubiria
mtanikuta.."
Ndani ya mda mfupi nikawa tayari
nimeshayazoea mazingira ya kile
choo ikiwa ni pamoja na harufu
kali ya mule ndani, niliweza
kujifungia mlango mmojawapo
kwa mda mrefu tangu nimefika
bila ya hata mtu yoyote kujua,
mara nikasikia sauti ya watu
wanaongea kwa nje huku sauti
kama niliyokuwa naifahamu
nilianza kuingiwa na furaha na
amani isiyokuwa na kifani kwani
niliamini Gervas ndiye mkombozi
wangu na anayepajua mpaka
nyumbani kwetu kwani nilikuwa
nimeshapasahau hadi jina la
mtaa,sikutaka kujitokeza hvyo
nikavuta subira huku nikiisikia ile
sauti kwa umakini taaratibu
nikaweza kuitambua kuwa
haikuwa sauti ninayoifahamu hata
kidogo na hata maongezi
waliokuwa wanaongelea
hayakuwa yakiunafunzi hivyo
halmashauri ya kichwa changu
ikapambanua fasta na kujua kuwa
wale watakuwa ni walinzi kwani
walikuwa wanaongelea mambo ya
kifamilia na kikazi tena kazi ya
ulinzi, moyo ulianza kuniripuka
kwani walikaa mda mrefu huku
wakipiga story na hata wanafunzi
walipokuja nilisikia wakiwaamkia
na kujisaidia na kuondoka
zao,kwa ujumla nililegea sana na
akili ilishaanza kuchoka,nikiwa
bado nipo nao wale walinzi
chooni huku wakinogewa na stori
ila mlango nilikuwa nao tofauti
bila ya wao kujua ghafla nikasikia
sauti kali iliyotokea upande wa nje
huku ikilitaja jina langu.,
"LEVINAAAA...! LEVINAAA...!
LEVINAAA...!
" YUPO MLANGU UPI
UMESEMA..?"
Nilitamani niweze kutoka lakini
haikuwezekana kutokana na wale
walinzi kukaa mda mrefu
wakipiga stori, hakika ile sauti
ilikuwa ni ya Gervas akiongea na
mwenzake huku nikihisi
ameshakaribia kuingia mule
chooni,ghafla nikasikia ukimya
umetanda halafu yakafuatia
maswali kutoka kwa wale walinzi
wakimuuliza Gervas,
"Levina..! Levina ndo nani? Na
mbona mwenzako amenyoosha
kidole mlango huo ambao
umefungwa..?
Kuna nani...?"
*************************
*** Je? Ndoto za Levina kumpata
Gervas zitatimia?
*** Itakuwaje akikamatwa wakati
ile ni shule ya Wavulana tupu?
Inaendelea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: