Home → simulizi
→ Sitaki tena – 05
Ilipoishia.,
"jamani..! jamani..! jamani..!
Nisaidieni nakufaa..! nakufaa..!"
Nikiwa bado nalia pale ghafla..
Endelea.,
Ghafla nikamulikwa mwanga
mkubwa nikaangaza huku na
huku nikaweza kuwaona watu
wakiwa wamenizunguka..
"Wewe ni nani.? Na unafanya nini
hapa?" aliongea mmoja wa watu
wale waliokuja pale nilipokuwa
baada ya kupiga makelele kwa
kuona mnyama akinifuata kumbe
hakuwa mnyama wa kunidhulu
bali alikuwa ni ng'ombe
aliyechelewa kuingizwa bandani
na katika lile eneo walikuwapo
wanaishi watu.,
"Naitwa Levina nimetokea mbeya
ila gari yetu ilipata ajali tukawa
tumevamiwa na majambazi hivyo
nikaamua nikimbilie huku
msituni..kwani hapa ni wapi?"
niliwajibu hapo hapo huku
nikishusha pumzi na kuwauliza
swali bila hata ya kuonyesha
woga wa aina yoyote,
"Hapa ni kijiji cha LIAMKENA tupo
katikati na hili pori la msitu wa
Ruaha., Haya mbebeni tumpeleke
nyumbani na wewe John swaga
huyo ng'ombe turudini
nyumbani" aliamrisha mmoja wao
kwa sauti ya juu.,
Safari ya kutoka katika ule msitu
mpaka kuingia katika kijiji cha
'Liamkena' usiku wa manane
ilifanikiwa kwani nilipofika tu
wakaanza kunitibia kidonda
changu kwa kutumia dawa za
kienyeji huku wanakijiji wengine
kutoka katika kijiji kile wakija
kunishangaa si kwakuwa nilikuwa
natisha bali walistaajabu
kuokotwa usiku wa manane
kwenye ule msitu ulioaminika
kuwa na wanyama wakali tena
wengi,
Ndani ya siku mbili nikawa tayari
nimeshazoea mazingira uku akili
yangu nashauku kubwa
nikiielekezea nyumbani na jinsi
gani ntampata Gervas na
kumshukuru kwa yote
aliyonitendea.,
Hali ya kidonda changu haikuwa
mbaya kwani kilianza kufunga
taratibu, ila wanakijiji walipenda
niendelee kubaki mpaka nipone
kabisa jambo ambalo lilipingana
na halmashauri ya kichwa
changu,
Ilipofika saa tano usiku huku kijiji
chote kikiwa kimerindima kwa
giza nene,sikuwa na hata chembe
ya usingizi, jicho langu liliweza
kupenyeza kupitia katundu
kadogo kadirisha kalichokuwa
kametengenezwa kwa kutumia
miti, niliweza kujua mara moja
sehemu ya kutokea hivyo
nikachana kipande cha gauni
langu na kukifunga katika eneo
lakidonda changu kisha
nikachukuwa mishale na upinde
huku upande wa kulia kwangu
nikashikilia panga tayari kwa
kuingia tena msituni huku
nikitafuta barabara ya
kutokea,nilifanikiwa kutoroka na
kuingia msituni,akili yangu na
mwili wangu vikawa kama
vimeshapigwa ganzi kwani sikuwa
muoga hata kidogo,nilitembea
taratibu lakini nikaona kama
nachelewa hivyo nikaanza
kukimbia wakati nakimbia niliweza
kusikia kama kuna watu
wananikimbiza nyuma yangu
kama sivyo basi ntakuwa
nimeingia katika ulimwengu wa
wanyama pori tena wale wakali
nikasimama na kujificha nyuma ya
mti kisha taratibu nikachomoa
mshale japo nilikuwa sijui
kuutumia lakini niliweza
kuuelekezea upande wa ile
sehemu niliyotoka na kuhisi kile
kitu kitakuwa kinatokea upande
huo, Niliunyosha na kufanikiwa
kuuachia,nikasikia sauti ya kike..
"Nakufaa mama niokoe..
Ooh.! Uuh.! Uuh.!" ghafla
ikafuatia mshindo kuashiria kile
kitu kimeanguka chini baada ya
kuachia mshale wangu wenye
sumu kali, bila kuwa na woga kwa
kunyemelea nikaanza kufata lile
eneo kumtambua yule mtu, huku
nikikaribia pale nimeshika panga
langu akatokea fisi maeneo ya
karibu nikamfyeka akawa
amekufa,nikaendelea na zoezi
langu la kutambua ni kitu gani
kitakuwa mbele yangu, sikuwa na
tochi,ila nilipoukaribia ule mwili
niliupapasa lakini bado
haikusaidia kumjua ni nani lakini
ulikuwa ni mwili wa mtu pale chini
ambao kwa namna moja au
nyingine sikuweza kuutambua
mara moja, kwa ushupavu wa
halmashauri ya kichwa changu
ikanituma nichukuwe panga na
ku Nichukuwe panga na kuchana
kipande cha nguo yake,nikafanya
hvyo kisha kile kitambaa
nikakificha katika pindo la nguo
yangu ya ndani halafu safari
ikaendelea,nilikatiza msituni bila
kuogopa kitu chochote na wala
kumuogopa yeyote hatimaye
baada ya kukimbia mda refu
nikahisi kama kitu kigumu
nakanyaga chini,furaha na amani
vikaanza kutawala ndani ya moyo
wangu kwani nilikuwa tayari nipo
katika barabara ya lami,akili ikawa
katika kukisia ni upande gani ndo
utakuwa unaelekea Dar na
upande gani utakuwa unarudi
Mbeya,nikiwa bado natafakari
likapita basi la
kwanza,nikashindwa
kulisimamisha nikaamua kusubiri
gari nyingine,kwani sikuwa hata
na nauli hvyo nikaamua nijifiche
niweze kudandia gari lolote
litakalopita kwa mwendo mdogo.,
Baada ya kukaa pale takribani
lisaa moja na nusu bila ya kuona
gari lolote hatimaye nikaliona gari
kubwa likiwa linakuja kwa
kujikongoja.,
"Kama kufa wacha nife tu.,lakini
hili gari siliachi.." nilijisemea
kimoyomoyo huku nikijiweka
tayari kwa kurukia lile gari aina ya
roli,huku mikuki na mishale
pamoja na lile panga nikilitupia
msituni,kitendo cha lile gari kufika
karibu yangu kikawa kosa kubwa
sana kwangu kwani ndani ya mda
mchache nikawa tayari nipo
nyuma ya lile lori lililokuwa
limebeba mbao.,
Kwa ujasiri niliokuwa nao
nikaingia mpaka mule ndani ya
lile lori kwa nyuma ambapo
sikumuona mtu yeyote kisha
nikarudishia mlango na kujilaza
kwenye zile mbao huku nikiwa
sina uhakika na ninapoenda,
"Sijui ndo litaishia morogoro au
ndo la Iringa hili gari?" hayo ni
kati ya maswali yaliyokuwa
yameandama ndani ya kichwa
changu,huku safari ikiendelea
taratibu baada ya mwendo mrefu
kidogo, ghafla gari likasimama
kwa mbali nikahisi sauti ya watu
wanajibizana kwa nje.,
"Hapana mkubwa mzigo wetu
hauwezi kuzidi kiasi hicho"
hapohapo jibu likanijia kuwa
tutakuwa tumefika maeneo ya
mizani,
"Embu fungua nyuma tuhakikishe
maana tani zimezidi na kama
hutaki paki pale gari yako
uandikiwe faini"
Wakiwa bado wanabishana pale
tayari kwenye gari nikawa
natetemeka mwili mzima huku
nywele zikinisimama na akili
ikinituma nifungue mlango,
nikisema nijifiche nyuma ya mbao
siwezi kwani ni kweli kulikuwa na
mbao nyingi kiasi kwamba nilipata
kanafasi kadogo sana ka kujificha,
"Mungu saidia.! Mungu saidia.!
Saidia jamani.!"
Ndio maneno niliyokuwa naomba
nisiweze kukamatwa kwani nia
yangu nikufika Dar,
Mda si mrefu nikaskia
mungurumo wa gari kuwashwa
kuashiria safari inaendelea moyo
wangu ukawa na furaha upya
nikajihisi ni mtu tofauti sana
duniani tena aliye na bahati
mbaya kupelekwa gerezani lakini
aliyejawa na bahati nzuri uraiani,
Nikiwa sina hata lepe la usingizi
huku safari ikiendelea niliweza
kushuhudia tena kwa mara
nyingine kuki kuchwa kwani
mwanga ulikuwa umeshatoka
kuashiria kuwa ni alfajiri,gari nalo
likatembea ka mwendo kidogo
kisha likasimama, sauti na
makelele ya watu ndio
yalichochea hisia zangu,niliweza
kutoa jicho langu kupenyeza
kwenye kauwazi ka mlango
nikaweza kushuhudia watu mbali
mbali,moja kwa moja nikapata
wazo la kuangalia kile kipande
cha nguo nilichokikata kule kwa
yule mtu msituni alikuwa ni nani,
Taaratibu mkono wangu ukaanza
kupenyeza mpaka kwenye upindo
wa nguo yangu ya ndani
nikakichukuwa kile kitambaa na
kukiangalia.,
"Mamaa..! mamaa..! nimeuwa
tena mungu wangu..!
Nisamehe Pendo..! Sijakusudia
mimi..! Maaaaa aaaaaaah..!"
Kumbe kile kilikuwa nikipande
cha nguo cha rafiki yangu
niliotokanaye gerezani 'Pendo'..
wakati nikiendelea kutoa sauti kali
nikahisi kunawatu wamezisikia
kelele zangu hivyo nikasikia
mlango unafungulia eneo
nililokuwa..,
"Sauti inatokea humu ndani
bwana, tena ni sauti ya kike."
aliongea mmoja ya watu
waliokuwa wanazungumza nje ya
lile lori nililokuamo ndani.,
"Mtoeni.!, mtoeni.! Tena anasema
ameua,embu mkamateni
tumpeleke polisi.."
Nilibaki nimezubaa huku nikiwa
sijitambui kipi cha kufanya,nikawa
natetemeka sana huku nikiishiwa
na pumzi,nahisi mapigo ya moyo
yalizidiwa kasi kwani nilijihisi
napata joto ghafla huku kijasho
chembamba kikiambatana na
mchozi uliokuwa unanitoka mithili
ya maji yakifata mkondo wake,
sikuwa na jinsi tena kwani
niliamini ndoto zangu za kuwa
uraiani zimekwisha na sijui
ntawaambia nini Gervas na mama
yangu endapo watasikia nipo tena
gerezani,
Huku kojo likiwa linanimwagika,
ukakamavu na ujasiri wote
ukinitoka nilijikuta natoa tena
sauti ya ukali.,
"Sio mimi..! Sio mimi..! Jamani
msinikamate.."
Huku nikinyosha mikono yangu
miwili kuelekea ile sehemu
niliyoamini ni mlango,taratibu
nikaanza kufungua ili nijisalimishe
ile namalizia kufungua tu..
Itaendelea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: