SHORT STORY HUZUNI YANGU B mzee wa utam😋 ✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾 STORI hii imeshika nafasi ya pili katika shindano la hadithi fupi katika page ya jamvi la simulizi. Niwashukuru wote mliopiga kura. Na hata wale ambao kwa namna yoyote ile mlishindwa kupiga kura. Hadithi zote zilisomwa bila kujulikana waandishi wake hadi pale matokeo yalipotangazwa. Ilifana sana. Pia kwa fursa hii, nampongeza TUNU WA J. Ndiye aliibuka kidedea. Kelvin Kagambo naye si haba. Kura yangu nilimpa yeye bila kujua. Ilikuwa ni katika simulizi ya PANDE MBILI ZA MAISHA. “Jifunze kukabiliana na huzuni kama huna uwezo wa kuigeuza kuwa furaha. Usiyatafsiri machozi ya mtu kama maumivu ndani ya moyo wake. Vilevile usikitafsiri kicheko cha mtu kama furaha ndani ya moyo wake." Ni moyo wangu na fikra zangu juu ya mengi niyaonayo na ninayoendelea kuyaona katika ulimwengu huu. Nafsi yangu imekuwa ikitaabika kila niyaonapo kwa macho yangu na hata kwa kusimuliwa. Yanaumiza na kuichumbua nafsi yangu. Kila kukicha na hata pale jua lichweapo, yamekuwa yakizidi kujidhihirisha machoni pangu kwa kasi kubwa mno. Macho yangu yakalia machozi ya kawaida yasiyoonyesha rangi ukiyamwaga juu ya karatasi lakini kadri siku zisogeavyo, si machozi tena ndani ya mboni zangu. Yamekuwa machozi ya damu. Yanachafua popote pale yadondokeapo. Moyo wangu umekuwa wa kuhangaika kuitafuta furaha lakini imekuwa vigumu furaha hiyo kupatikana. Nikaelemewa maumivu ikanibidi kuwageukia marafiki zangu baada ya kuwakosa ndugu zangu tangu nikiwa na umri wa miaka tisa baada ya ajali mbaya ya meli katika ziwa Victoria. Hakuna asiyeikumbuka ajali hiyo ya Mv Bukoba. Tulikuwa tukielekea katika harusi ya shangazi yangu lakini meno yangu yakapoteza mg’ao kutokana na ajali ile. Nikaokolewa na wavuvi ambao nao baada ya kunifikisha nchi kavu hawakuwa na msaada mwingine tena kwangu. Uso wangu ukayajenga makunyanzi nikiwa na umri mdogo. Tabasamu likanipotea na kubaki nikiliona kwa wengine. Macho yangu yakapoteza nuru pale marafiki niliowadhania, waliponitema mate kutokana na hali yangu. Hakuna aliyehitaji kunitazama hata kwa bahati mbaya. Waliogopa uchakavu wangu wa mwili mpaka mavazi. Hatua zangu zikageuka sumbuko kwa wengine kutokana naharufu niliyokuwa nikiitoa katika mwili wangu. Harufu hiyo ilitokana na kidonda nilichokipata baada ya pikipiki kuniunguza kwa bomba la kutolea moshi. Jamii ilikuwepo wakati nikiungua lakini wakakosa kauli vinywani mwao. Wakawa zaidi ya mabubu ilihali ndimi zao zilikuwa zikiyateta maneno kabla ya mimi kupatwa na hilo. Aliyenisababishia ajali akatokomea na kuniacha katika hali ya maumivu yasiyoelezeka. Nikabaki mwenye katika kisiwa cha baridi pasipo msaada wa joto. Baridi ikaikomaza ngozi yangu na hatimaye ikazoea. Nikalisahau joto na kutamani kuishi katika baridi kila wakati. Kwasababu maisha ni sawa na hadithi ya kuwa lazima uweke kituo na mikato, baada ya baridi likaja joto. Likaniunguza kadri lilivyoweza. Ngozi yangu maji ya kunde ikabadilika na kuwa nyeusi hapana shaka kama mkaa. Hali hiyo nayo nikaizoea na kuitamani kila wakati. Lakini bado haikuwa mwisho wa huzuni yangu. Ikanyesha mvua. Sikuwa na makazi maalum hivyo nikakosa pa kuziweka mbavu zangu kwa ajili ya usingizi ili kupata mapumziko ya mchana kutwa kuzunguka huku na kule kukamilisha maisha yangu ya hapa ulimwenguni. Nikaizoea mvua na lakini sikuitamani kwasababu hiyo ilinizidishia tabu mno. Umri wangu ulizidi kusonga na hatimaye nilitimiza mika kumi na mbili. Kuongezeka kwa umri wangu haukuwa mwisho wa mateso yangu bali ilikuwa kama ndiyo nayo yanaongezeka. Kutokana na kutamani kuoga na kuvaa kama ilivyokuwa kwa wengine niliokuwa sichoki kuwatumbulia macho, ikanibidi kuomba kazi ya kuosha vyombo kwa mama ntilie. MUNGU ni mwema pamoja na kwamba mateso yangu ya miaka mitatu iliyokuwa imepita ni yeye pia aliyekuwa akiniongoza ili mimi kuendelea kuishi. Nasema hivyo kwasababu nakumbuka siku moja nilifanikiwa kupata chuma chakavu nyingi na baada ya kutafuta mteja nilifanikiwa kumpata. Alikuja na gari ili kubeba. Tukaongozana naye ili niende kupima ni kilo ngapi aweze kunipatia fedha yangu. Lakini kwa bahati mbaya tukapata ajali mbaya mno ila cha kushangaza niliweza kusalimika bila hata kuchumbuka kidole. Hakika ni zaidi ya kumbukumbu yenye kunistaajabisha fikrani mwangu. Wenzangu watatu pamoja na dreva ambaye ndiye alitakiwa kunilipa, wakanitangulia na kuniacha ulimwenguni nikizidi kupumua na kuivuta hewa safi pasipo malipo yoyote. Hapo ndipo huwa nawaona wapuuzi wale wote wenye viburi kisa wanamiliki. Hapo ndipo nawaona wapuuzi wale wote wenye kuishia kunung’unika kisa wamekosa mali. Niseme maisha ni sawa na daraja barabarani. Yupo aliyepata mali akapoteza macho yake. Iko wapi faida ya macho yake? Hawezi kuviona vitu vizuri na hata vibaya. Atabaki kunusa ilihali kaa ukitambua vipo visivyonusika. Vinahitaji macho. Kwanini unung’unike kwa kukosa leo ilihali bado unavyo viungo vyako ambavyo kesho waweza kuvitumia kutafuta mali ikusababishayo kunung’unika? UVUMILIVU na SUBIRA. Nilibahitika kupata kazi ya kuosha vyomba. Niliifanya kazi ile moyo mmo

at 8:01 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top