Riwaya: SARAI SEHEMU YA PILI(02) ***Ilipoishia*** jeny aliendelea kuandaa karanga kisha akazifunga kwenye mifuko....ghafla alimuona sarai kaamka na kuja upande wa nje huku anatembea.....jeny alistuka sana....alianza kuwa na wasiwasi huenda amezaa jini.....sarai alizipiga hatua mpaka kwa mama yake..kisha akaanza kumsaidia mama yake kufunga karanga kwenye mifuko....yawezekana vipi mtoto miezi minne(4) atembee kama mtoto wa miaka minne....wakati akijiuliza mara ghafla... ***Endelea*** wakati akijiuliza mara ghafla.........sarai aliongea akamwambia mama yake""kwa nini unanitazama kwa uwoga!!!!? kisha sarai akaketi na kuanza kumsaidia mama yake kufunga karanga...jeny aliendelea kufunga karanga lakini uwoga ulitawala fikra zake....baada ya muda kupita walimaliza kufunga karanga.......jeny aliniandaa ili aende kwenye bihashara....alipomaliza kuandaa vitu vyake vyote alimchukuwa sarai...lakini Sarai alikataa kuindoka na mama yake akabaki nyumbani akiwa kitandani....jeny aliamua kuondoka huku akili yake ikiwaza...""baada ya nusu saa itanibidi nirudi ili nimnyonyeshe sarai.... alipofika eneo lake la bihashara....alipanga karanga pamoja na matunda juu ya meza......jeny alistahajabu sana siku hiyo wateja walikuwa walinunua matunda pamoja na karanga kwa mfululizo.......kabla ya nusu saa meza ilibaki tupu...jeny alistahajabu sana"" siamini siku zote watu walininyanyapaa mimi na mwanangu pamoja na bihashara yangu....lakini leo nimepata wateja wengi kwa mfululizo!!......jeny alifunga bihashara yake na kuanza kurudi nyumbani..... siku iliyofuata pia jeny aliuza bidhaa akamaliza mapema.....ikawa ni kila siku anauza na kumaliza mapema....wateja waliongezeka..... baada ya mwezi mmoja kupita, mtaji wa jeny uliongezeka mara mia zaidi alipata pesa za kutosha kwa sababu alikuwa akizitunza.... siku moja jeny alipata wazo la kuanzisha duka la kuuza nafaka.....duka lile lilimpatia fedha za kutosha.......baada ya miezi sita sarai alizidi kukua.... *************** siku zilisonga hatimae jeny aliamua kuliboresha duka lake...likawa ni duka la bidhaa za jumla na rejareja.....alipata wateja wengi sana......watu wenye maduka yaliyokuwa jirani.. walianza kumuonea wivu..kwa sababu wateja waliingia na kutoka kwa mfululizo..... sikumoja majira ya usiku jeny alimuogesha sarai. kisha akampa chakula jeny alianza kumzoea sarai..hakushangazwa na tena na maajabu ya sarai.....baada ya sarai kumaliza kula jeny alimlaza kitandani.....kisha wakalala.. ************** Upande mwingine walionekana watu watatu wamebeba madumu.....watu hao walionekana kuwa na wasiwasi !!!! macho yao yalitazama huku na kule kwa hofu kubwa.....walizipiga hatua kuelekea nyumbani kwa jeny....watu hao walihisi kuwa jeny ni mchawi kutokana na muonekano wa mtoto wake Sarai......walipofika walifungua madumu hayo yaliyokuwa na petroli na kuanzaj??nnnnnnnnnn?n??nnn?nnnnnnnn?n???n? kuimwagia nyumba ya jeny kwa kuizunguka kila upande.....walipohakikisha wamemwaga mafuta pande zote....waliamua kuichoma moto nyumba ya jeny......kisha wakakimbia na kutokomea..... moto ulianza kuwaka kwa kasi kutokana na upepo uliokuwa ukivuma nje' jeny alihisi hewa kuwa nzito chumbani kwake...alipofumbua macho aliogopaaa sana kuona moto umetanda ndani ya nyumba.....jeny alianza kupiga kelele za kuomba msaada......kisha akamchukua sarai na kumtoa upande wa nje ya nyumba....jeny aliungua baadhi ya sehemu za mwili wake lakini alijitahidi mpaka akafanikiwa kumuokoa sarai na kumtoa upande wa nje.....ghafla alikumbuka kuwa chumbani kwake kulikuwa na pesa za mauzo ya wiki nzima alizokuwa amepanga kuzipeleka benki.....akakimbia mbio kurudi upande wa ndani ili aone kama ataweza kuzitoa pesa hizo......alipoingia ndani moto ulikuwa umesha tanda ukiambatana na moshi mzito.....alijitahidi akaingia chumbani akafanikiwa kuzitoa pesa zile..kisha akakimbia kutoka nje...ghafla bati lilidondoka na kumkandamiza...kwa sababu mbao zilizokuwa zimeshikilia bati ziliunguwa hivyo hazikuweza kustahimili uzito wa bati..... punde majirani walifika na kuanza kutoa msaada wa kuzima moto...walijitahidi lakini walishindwa...waliamua kupiga simu kwenye shirika la msaada ZIMAMOTO....punde walifika bila kuchelewa wakaanza kuzima moto...baada ya nusu saa walifanikiwa kuuzima moto huo.....kisha wakaingia ndani ili utoa vitu ambavyo havikuungua sana....walipoingia ndani waliweza kumuona jeny kateketea kwa moto na kubaki mifupa......lakini maiti ya sarai haikuonekana kabisa.... wakati jeny anamtoa sarai nje hakuna aliyemuona hivyo haikujulikana ni wapi sarai alipo.... ITAENDELEA...... usikose kufatilia simulizi hii ya kusisimua. .. ASANTENI.

at 7:06 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top