[9/26, 08:31] ‪+255 714 435 449‬: NIPE BHANA Sehemu ya 05 Mwandishi:Mmaka Watsapp:0714435449 ...........ilipoishia......... Wakati naanza kukojoa nikatazama barabarani na kwa mbali nikaona difenda ya polisi ikija kwa kasi eneo tulipo huku askari watatu wakiwa nyuma ya gari huku wameinyoosha mitutu yao Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwangu ambapo akili ikaniambia ndo hivyo usha kamatwa unaenda kufia jela Basi wazo lika nijia napiga kelele Nyokaaaa!!!!..... Nyokaaaaaaa!!!!!!!!...... Nakufaaa jamani .........nisaidieni............ Nikaanza kukimbia kwa kasi niki tokomea katikati ya vichaka vilivyo ndani ya pori lile nene ... Wakati uwo gari la polisi likikaribia lilipokuwa gari letu....... .............endelea........ Kwakweli nilitimua mbio ambazo tangu nizaliwe sikuwahi kukimbia kiasi kile kila hatua niliyo piga nilikanyaga majani na vichaka ambavo vilitoa sauti iliyoonesha kana kwamba kuna mtu alikuwa nyuma yangu akinifukuzia basi bila kuangalia nyuma kwa woga nilizidi kuongeza kasi nikikukumbana na vichaka vyenye miiba iliyoishia kurarua sehemu mbalimbali za mwili wangu ikiacha michiri ya damu na kuchana nguo nilizokuwa nimevaa Sikutaka kuangalia nyuma kujua kilicho endelea zaidi nilizidi kutimua mbio kwa kasi muda nao ulizidi kusonga na mwendo wangu ulizidi kupungua huku jua kali likinichoma na kusababisha nihisi kiu Nilizidi kukimbia lakini ikafika wakati mwili ukakataa pumzi ikapungua njaa na kiu pamoja na jua kali vyote kwa pamoja vikaanza kunisha mbulia, sikuwa na budi kusimama nikatafuta sehemu yenye kivuli ndani ya kichaka kidogo na kutulia Nikaangalia sehemu niliyotoka hakukuwa na dalili ya kiumbe chochote kunifuata hapo ndo nikaamini ni maruweruwe yaliyonifanya nidhani kuna mtu alinifuata nyuma kwa kasi kwakuwa nilishaiacha mbali barabara kiasi cha kutoiona tena niliona bora nijipumzishe kidogo katika kivuli cha kichaka kile ubaya ni kwamba ndani ya pori lile hakukuwa na miti mikubwa ya kivuli bali vichaka vidogo vya miiba na majani marefu Nilijilaza chini ya kivuli kile nikiwaza juu ya hatima ya maisha yangu yaliyo haribiwa na mapenzi nikiwaza nimeshakuwa muhalifu kwa kumwaga damu na sasa kila kona natafutwa kama gaidi pia kuhusu kibarua changu cha kuuza vinyago kahela kidogo nilicho kipata sasa itabaki kuwa historia pia wazo kuhusu umaskini ulioitawala familia yangu kijijini kwetu manushi ilizidi kunimaliza nguvu kwani mimi ndiye nilikuwa tegemeo la familia nikiwasomesha wadogo zangu na kumuhudumia mama yangu aliye jihusisha na shughuli za kilimo Hakika nilizidi kuchoka na kutokana na uchovu niliokuwa nao usingizi ulinipitia Polisi baada ya kufika eneo lilipo kuwa gari nililopanda nikielekea nyumbani Arusha walimtaka dereva awape taarifa zote kuhusu abiria waliopanda basi lile wakiwataka abiria wote waliotoka kujisaidia kurejea ndani ya gari kila mmoja akitakiwa kukaa kwenye siti yake na kuonesha tiketi yake ambapo abiria walifanya kama walivyoagizwa na baada ya kukaa kulionekana siti moja iliyobaki wazi yaani haikukaliwa ambapo askari mmoja alihoji na kujibiwa na mmoja wa abiria kwamba kuna kijana mmoja alitoka kujisaidia vichakani lakini ghafla alipiga kelele akilalamika nyokaa!!! na kuanza kutimua mbio akitokomea ndani ya vichaka Polisi nao waliomba kujua jina la mtu huyo na kuambia aliitwa Samweli Joseph "Ni mrefu wastani na maji ya kunde?" aliuliza mmoja wa askari wale na kujibiwa ndio na msichana aliye kuwa amekaa pembeni yangu "Sasa huyu ndiyo muhalifu aliye sababisha mauaji ya kikatili ya baba na mwanawe mbele ya hadhara bila woga wowote na alikuwa akijaribu kutorokea kijijini kwao mkoani Arusha" askari anaongea maneno ambayo yanamfanya kila abiria aliye kuwa ndani ya gari lile kubaki mdomo wazi kwa woga wasiamini kama walisafiri na mtu katili aliyefanya mauaji ya kutisha kiasi kile "Asanteni kwa msaada wenu sasa mnaruhusiwa kuendelea na safari na samahanini kwa kuwachelewesha kwani jukumu letu sisi kupambana na wahalifu kama hawa na kuwafikisha katika vyombo vya dola" Wasafiri wote wanaitiaki asante askari wanaacha gari liendelee na safari na kufikisha taarifa makao makuu kwamba mtuhumiwa amekimbilia mapori ya muheza baada ya kugundua polisi walilifuata gari alilopanda Mkuu wa polisi anatuma kikosi cha askari tano kinachoingia ndani ya pori hilo na kuanza msako wa kunitafuta Nikiwa nimejilaza baada ya kipitiwa na usingizi ghafla nilihisi kitu kizito cha baridi kikinigusa mkono wangu na kuanza kupanda taratibu mpaka kifuani nikasogeza mkono kama nikikisogeza kwa pembeni baada ya kuhisi ni tawi la kichaka kile lilisukumwa na upepo na kunigusa lakini nilipogusa tawi lile nilihisi ulani flani na utelezo hapo ikanibida nifungue macho kutazama kwani nilijizuia kufungua nikiamini iwapo nitafungua nitapoteza usingizi ambao niliufanya kama kitulizo cha mawazo kwa wakati ule Kwa kweli baada ya kufungua macho nilitaka kuzumia baada ya kuona nyoka mkubwa aina ya black mamba akiwa kifuani kwangu ananitaza huku kakitoa kilimi chake nje nyoka yule baada ya kuona nimefumbua macho na kustuka alinnyanyua kichwa chake tayari kunishambulia, hapo kengere ya hatari ikagonga kichwani mwangu ambapo kwa kasi ya ajabu na ujasiri ambao sikujua nilipoutoa niliishika shingo ya nyoka yule na kunyanyuka naye kwa kasi kisha nikamrusha juu kwa nguvu ambapo alianguka katikati ya majani marefu umbali kama wa mita kumi kutoka nilipo Basi nami kwa kasi ya ajabu nikatoka nduki kuiokoa roho yangu lakini nilipigwa na butwaa baada ya kugeuka nyoma na kumuona nyoka yule anakuja kwa kasi ya ajabu huku ameinua shingo yake akibakiza mta mbili tu anifikie nilikusanya nguvu zote na kuongeza kasi ambapo niligeuka nyuma na kumuona nyoka yule akipambana kujaribu kuniuma miguuuni lakini alikikosa kutokana na hatua nilizopiga Nilizidi kuongeza mwendo na kuwa mwangalifu nikimkwepa nyoka yule ambaye hakuchoka kabisa kutaka kuniuma na wala hakuonesha dalili ya kupunguza mwendo kwa kukata tamaa lakini kama unavyojua ujanja wa nyoka nyasi basi ndivyo ilivyo kuwa kwani nyoka yule alizidi kuja kwa kasi na kufika usawa wangu ambapo alinipa kazi ya kumkwepa nikisaidiwa na visiki vilivyo mpunguza mwendo kwa kujigonga kwani aliupimia mguu wanguu wangu tu Nilizidi kukimbia kwa kasi nikimuomba mungu aniokoe katika masaibu yale lakini ghafla mbele yangu niliona mteremko mkali ambapo chini kulionekana mbali sana kukijaa majabali makubwa Nilijitajidi kupiga breki kwa nguvu zote nikijishika na vichaka ili kuupunguza mwendo hatimaye nilifanikiwa ikiwa ni baada ya kutegwa na kisiki kilichokuwa mbele yangu na kurushwa pembeni kidogo na mwanzo wa mteremko ule niligugumia kwa maumivu makali ikiwa ni baada ya kucha kadhaa kutoka katika vidole vya miguu yangu lakini cha kumshukuru mungu ni kwamba nyoka yule alipitiliza moja kwa moja na kuangukia katika mteremko mkali ambao sijui kama alipona Hakika sijui viatu vilinitokaje miguuni na viliangukia wapi lakini maumivu makali ya kutolewa kucha tena bila ganzi ndiyo yaliyo nisurubu kwa wakati ule lakini sikuwa na budi kujikaza kutafuta sehemu yenye makazi kwa ajili ya kujisitiri kwani nisingeweza kulala ndani ya pori lile lanye wanyama hatari ikiwa tayari ilisha timia saa kumi jioni Nilianza kutembea pekupeku kwa kuchechemea nikitobolwa na miiba midogo midogo ambayo niliichomoa mguuni taratibu na kuendelea na safari Nilizidi kutembea nikimuomba mungu japo nipate sehemu yenye usalama ya kulala kwa usiku tu asubuhi niendelee na safari nisiyo kuwa nikiujua mwisho wake lakini mungu si athumani hatimaye ilifika saa kumi na mbili jioni kijua kikimalizia kuzama ambapo kwa mbali niliona mashi ukitoka kwenye vijumba vidogo vilivyo enyekwa kwa nyasi hapo matumaini ya kupata msaada kidogo yakanijia Nilianza kuongeza mwendo kuelekea zilipo nyumba zile japo niliumia lakini maumivu hayakuwa chochote kwa wakati ule kwani nilitaka niwahi kufika kabla jua alijazama ambapo ingekuwa rahisi kupata msaada kwani kama giza lingeingia basi nisinge pokelewa wakidhani labda ni mwizi au mchawi kutokana na jinsi nilivyoonekana Nilizidi kuongeza mwendo ambapo kwa mbali nilimuona mtu akipasua kuni..... Je nini kitaendelea ? Usiikose sehemu ya (06) Itaendelea..... [9/26, 10:03] ‪+255 714 435 449‬: NIPE BHANA sehemu ya 06 Mwandishi:Mmaka watsapp:0714435449 .........ilipoishia........ Nilianza kuongeza mwendo kuelekea zilipo nyumba zile japo niliumia lakini maumivu hayakuwa chochote kwa wakati ule kwani nilitaka niwahi kufika kabla jua alijazama ambapo ingekuwa rahisi kupata msaada kwani kama giza lingeingia basi nisinge pokelewa wakidhani labda ni mwizi au mchawi kutokana na jinsi nilivyoonekana Nilizidi kuongeza mwendo ambapo kwa mbali nilimuona mtu akipasua kuni..... ........endelea........ Kwa kweli baada ya kumuona mtu yule kwa mbali ni kama nguvu mpya zilinijia nikajikuta nazidi kuongeza mwendo japo miguu ili andamwa na majeraha hatimaye nilifika karibu na alipokuwa mtu yule ambapo baada ya kusikia sauti ya nyasi kavu zikikanyagwa aliweka shoka lake nyuma yake na kugeuka akinitazama Nami kidogo hofu ili nijia kutokana na mwonekano wa mtu yule ambaye sikuweza kuiona sura yake vizuri zaidi ya nguo alizovaa nikajikaza kiume nikijisemea liwalo na liwe bora nifie mikononi mwa binadamu wenzangu kuliko kuliwa na wanyama wa porini baada ya kufika karibu kabisa na mwanaume yule niliweza kumtazama vizuri usoni na kugundua alikuwa mzee kama wa miaka hamsini na tano kutokana na mikunjo iliyokuwa usoni mwake na nyele nyeupe kiasi zilizochafuka zilizo mjaa kichwani "Shikamoo babu" nilimpa salamu mzee yule ambapo hakunipa jibu lolote zaidi ya kuchukua shoka lake kwa tahadhari na kubeba baadhi ya vikuni alivyo pasua akianza kupiga hatua kuondoka kwa kweli baada ya kuona babu anaondoka nilijua nisipofanya jambo la ziada nitafia katikati ya pori lile ukichangia njaa niliyokuwa nayo pamoja na majeraha yaliyo zidi kunipa wakati mgumu kadiri muda ulivyo zidi kwenda nilijikokota mpaka nikafika mbele yake na kusimama nakupiga magoti " Samahani babu mimi sina ubaya kwako bali ni matatizo tu yamenikuta na kunifanya niwe katika hali hii najitaji msaada wako babu yangu hapa nilipo nina majeraha makubwa mwilini pamoja na njaa na kiu nipo tayari kufanya lolote utakalo naomba tu unihifadhi kwa leo hii" niliongea maneno kwa utulivu na upole wa hali ya juu ambapo mzee yule alinitazama kwa kitambo kidogo na kusema "unabahati sana kijana nilizani ni hawa wezi wa mazao hapa kijijini nilipanga kukufanyia kitu kibaya sana lakini muonekano wako unaonesha kuna matatizo unapitia nyanyuka mjukuu wangu twende kwanza ukapumzike mengine tutaongea zaidi kesho" maneno ya babu hakika yalinipa furaha ambayo sikuwi kupata maishani nikajiona kama nimezaliwa upya kwani wakati wote nilijua maisha yangu yalifika mwisho "nashukuru sana mzee wangu naamini mungu atakurudishia mema mengi maishani mwako" "usijali mjukuu wangu sisi kama binadamu inatupasa kusaidia mimi natimiza tu"alinijibu mzee yule na kunitaka nifuatane naye tulianza kutembea katika vichochoro vilivyo katika nyasi ndefu hatimaye tukatokezea nje nyumba kubwa kiasi iliyo ezekwa kwa nyasi mzee yule akatupa chini kuni alizobeba na kuliegemeza jembe kwenye ukuta nje ya nyumba ile kisha akanitaka nifuatane naye ndani ya nyumba kwa sababu nje tayari kulikuwa na giza nene tukaingia ndani ya nyumba ile tukifikia katika sebule iliyo katikati ya vichumba viwili vilivyo tazamana "karibu kijana jisikie huru hapa uko salama japo huku sisi hatunaga umeme jitahidi uzoee " anaongea mzee yule akinikaribisha kukaa kwenye kigoda sebuleni pale kisha anaita "We mama Zena uko wapi sa hivi mumeo nimefika hata maji ya kunywa hunipi" "abee mume wangu nipo huku chumbani na Zena tunamalizia kufunga mboga" inasikika sauti ya mwanamke ikijibu kutoka chumbani "haya njoo huku na vikombe viwili kuna mgeni" "sawa mume wangu" mara pazia chakavu la moja ya chumba linafunguliwa na anaonekana mwanamke wa umri kama miaka arobaini aliye jaliwa umbo la asilia la kiafrika pamoja na sura ya kuvutia akija tulipokaa na babu na akiwa ameshika jagi la plastiki lililo jaa maji pamoja na bilauri mbili zachuma "karibu mume wangu"anasema mama yule baada ya kumaliza kumimina maji kwenye moja ya glasi na kumkabidhi mume wake huku akinitaza kwa macho yaliyo jaa maswali ana mimina maji kwenye glasi nyingine na kunikabidhi kisha naye ana chukua kigoda na kukaa "mume wangu kulikoni ugeni huu" anasema mama yule akinitazama "huyu kijana inaonekana ametoka mjini na kuna matatizo yamempata hapa alipo anahitaji msaada" "inaonekana au ndiyo yaliyo msibu au hebu atueleze mwenyewe maana wewe naona kama unachukulia mzaha swala hili kumkaribisha mtu usiye mjua alafu usiwe na uelewa kuhusu tatizo lake hebu kijana tueleze" ndiyo hivyo kama alivyo sema babu mimi nimetoka mjini na nimefika hapa kutokana na matatizo niliyokumbana nayo hapa nilipo nahisi maumivu mwali mzima na njaa kali naomba msaada wenu japo nijisitiri kwa siku kadhaa hali ya ikitengamaa nita tafuta njia nyingine ya kuondoka... inatosha kijana ... we mwanamke hivi uoni mumeo na mgeni tunahitaji maji ya kuoga hebu nenda haraka katutayarishie mama zena anaondoka na kuniacha na babu aliye jitambulisha kwa jina la mzee Saidi "Hivi huyu Zena yuko wapi yani mda wote nimefika mpaka sasa hajani salimia wala kunipa pole we!! Zena" "abeee baba!!!" inaitika sauti nyororo ya kike sauti ikitokea chumbani "njoo hapa" "sawa baba nakuja" pazia linafunguliwa ninabaki mdomo wazi baada ya kumuona msichana mwenye uzuri usio elezeka haukuwa wa sura tu bali hata umbo alikuwa ni zaidi ya mwanamke kwa kweli msichana yule alikuwa mzuri sijawahi kuona japo aliishi mazingira ya kijijini lakini haikuwa sababu ya kuuficha urembo wake aling'aa bila kutumia kipodozi chochote kwenye ngozi yake nyeupe kiasi hakika kwa uzuri aliokuwa nao akiwa kijijini basi niseme angeingia mjini na kutumia vipodozi vya kisasa pamoja na kuvaa mavazi wanayo vaa dada zetu basi angepanga msururu wa wanaume ambao wange lihitaji penzi lake " shikamoo baba"inasikika sauti kutoka kwa msichna yule sauti ninayoweza kusema ni ya kumtoa nyoka pangoni kama walivyo zoea kuiita vijana wa mjini "marahaba mama ina maana siku hizi salamu mpaka nikuombe" "hapana samahani baba nilikuwa nafunga mafungu ya mbogo chumbani sikujua kama ulishafika" anajibu binti mrembo Zena huku akinitizama kwa vimacho vya kuibia vya aibu "na huyu mgeni mbona hujamsalimia au hujafunzwa kupokea wageni" "ahaaa!!! shikamoo kaka" ana kurupuka binti yule akinisalimu na kutazama pembeni kwa aibu akinipa mkono "marahaba hujambo mwaya"ninaitikia na kuupokea mkono wake uliokuwa mlaini kama pamba "sijambo kaka.. mi naitwa Zena wewe unaitwa nani" anasema binti yule sasa akijikaza kunitazama uso akiin'gata midomo yake kwa aibu ikiwa in baada ya baba yake kumtazama kwa jicho kali mara ya kwanza alivyo nisalimia na kuatonitazama "mbona mi tayari nilishakujua mda mrefu"nilimtania nikionyesha tabasamu naye alilipokea tabasamu langu na kunirudishia la kwake lililonifanya nizidi kuamini kweli kuna baadhi ya viumbe mungu kawapendelea ni siseme mengi juu ya vishimo mashavuni, macho ambayo akitabasamu hujiweka katika hali ya kuvuti pamoja na midomo midogo laini iliyo pambwa na meno meupe "muongo umenijulia wapi"aliniuliza kwa sauti laini ya kudeka "si hapa hapa au"nina mjibu na kisha wote kwa pamoja tunacheka binti yule akinipasia mkono na kuniambia na mvunja mbavu "we Zena katayarishe chakula na umuambie mama yako amtayarishie mgeni sehemu ya kulala" tunastushwa na sauti ya mzee Saidi ambaye muda wote tunaongea alikuwa akiibonyeza simu yake aina ya Nokia tochi "sawa baba ngoja niwaache" anasema Zena na kuondoka akiniacha na mzee Saidi ninaoga , tunakula cha usiku kisha tunaagana wakinielekeza chumba changu cha kulala...... je nini kita fuata usikose sehemu ya (07) Alafu naona kama wengi hawasomi hadithi hii kwa kuzani haina maadili lakini ukweli ni kwamba hadithi hii ina mafunzo mengi ambayo tunaweza kukutana nayo katika maisha yetu ya kila siku.. itaendelea.........

at 11:07 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top