SMS Tamu za mahaba.......  Nakupenda sana mwandani wangu ndiyo maana moyo wangu hupatwa kidonda ninaokuona na mwingine hasa anapokuwa hana sifa, nahisi kama anakutumia wewe kama mdori wake wa kumfurahisha. Uwe makini ua la moyo wangu. Mpenzi wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka moyo na akili yangu pia. Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia, fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu, fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo kwa kukutumia sms mpenzi wangu, Nakutakia usiku mwema Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo kama ukiwa mbali "NIACHE NIKUPENDE SWEET"

at 1:48 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top