Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA PILI.
Nilifanikiwa kupanga vitu vyangu katika mpangilio uliopendeza mbele za macho yangu baada ya hapo nilijiandaa kwa ajili ya ratiba za siku hiyo. Uniform mpya zilinipendeza hakika, sketi yangu fupi nyeusi iliyochanua vyema, shati langu jeupe la mikono mirefu, tai ya pundamilia, soksi ndefu zilizonifika magotini na viatu nilipendeza sana.
Muda ulipokaribia mimi na Candy tuliongozana hadi mstarini na baada ya matangazo machache tuliruhusiwa kuingia madarasani. Candy aliniongoza mpaka kwenye darasa letu.
Ili ndilo darasa lako aliongea kwa dharau na kisha akaondoka kwa hatua za mikogo, nilibaki nikimtazama mpaka alipopotelea. Hakika Candy ni msichana mzuri niliwaza.
Dakika moja ya kumshangaa Candy ilipoisha niliamua kuingia darasani na wakati huo wakati naingia darasani nilijigonga kwenye paji la uso mlangoni. Nilihisi maumivu makali.
Madaftari mawili ambayo hayakutosha kwenye kibegi changu cha mgongoni yalidondoka. Nilichutama ili kuyaokota na hapo nilijigonga tena na safari hii sio kwenye mlango tena bali ni mtu alikuwa amenigonga, nilikasirika sana. Nikageuka kwa ghadhabu ili nimuone ni nani ambaye amenigonga nilikutana na sura nzuri ya kiume iliyopambwa na tabasamu laini, hakika sikuwahi kukutana nalo katika maisha yangu yaliyopita.
“Sorry” alisema kwa sauti tamu.
“Aaaanh usijali nilikua nakusaidia kuokota madaftari yako lakini kwa bahati mbaya nikakugonga samahani kwa hilo.”
“usijali na asante sana” nilisema.
Aliniokotea madaftari yangu na kisha akanikabidhi, “wewe ni mgeni mahali hapa sijawahi kukuona.”
“Ndio nimehamia jana”
“Karibu sana”
“Asante” nilisema.
“Unasoma combination gani?”
“Niko ECA”
“Wooow karibu kwenye darasa letu”
“Asante”
“Naitwa Martin, sijui wewe unaitwa nani?”
“Naitwa Catherine.”
“Catherine karibu sana.”
“Asante.”
Alinishika mkono na kuniongoza darasani, alisimama mbele ya darasa na kuongea kwa sauti nzuri ya kiume.
“Hello class huyu ni mwanafunzi mpya atajitambulisha anahitaji ushirikiano wenu.” Akaniachia nafasi nijitambulishe mbele ya darasa.
Nikasema kwa uwoga hali nimeshikwa na aibu za kike.
“Hello class naitwa Catherine nimetokea Kibasila” nilishindwa kuendelea, watu walicheka na kisha wakanikaribisha. Nilioneshwa sehemu ya kukaa pembeni yangu aliketi msichana mzuri alinisalimia “hello naitwa Martha karibu sana.” Nilitabasamu na kisha nikamwambia asante.
Ghafla mwalimu aliingia akiwa mwenye ghadhabu, tulisimama kumsalimia.
Hakujibu salamu yetu alianza kufoka “kama hujafanya assignment simama hivyohivyo na kama umefanya kaa chini.”
Nilijikuta nimesimama peke yangu.
“All eyes on me.” Nilihisi nimejisemea mwenyewe lakini kumbe niliongea kwa sauti darasa zima wakacheka, nikatoa macho hali nimeachia mdomo.
Mwalimu aliniuliza “je wewe ndio ambaye ujafanya kazi yangu ni kitu gani kimekufanya usifanye assignment?”
Nilishikwa na kigugumizi, “Eeeeh aaanh mimi ni mgeni”
“ahaaa” alisema mwalimu yule ambaye baadae nilikuja kumtambua kama Mr. Maloya.
“Kaa chini” nikakaa.
Alianza kufundisha huku akitumia muda wake mwingi kunitazama, sikujua kwa sababu ya ugeni wangu au vipi.
Tuliendelea na vipindi mpaka wakati wa mapumziko ulipofika. Darasa zima waliondoka.
Nilibaki peke yangu nisijue wapi pa kuelekea. Na wakati nimeinama nikifuta viatu vyangu nilisikia nimeguswa begani kwangu.
Kwa kuwa sikuwa nimemzoea mtu yeyote nilijua lazima ni Candy ambaye amenipitia kwa ajili ya mapumziko.
“Candy” niliita huku nikigeuka, hakuwa Candy nilikutana na sura nzuri ya kiume.
“Martin hapa”
niliachia tabasamu.
“oooh Martin” nilishindwa kuendelea.
“Mbona uko hapa peke yako?” aliuliza.
“Sijui nielekee wapi” nikasema.
“Aaanh ngoja twende restaurant” nikanyanyuka tukaongozana.
Tulipofika niliagiza maziwa na slace tatu za mkate.
“Unayaonaje mazingira ya shule yetu” aliuliza.
Kabla sijamjibu msichana ambaye alikuwa mmoja kati ya wanafunzi alifika mezani kwetu.
“Wewe ndio Catherine si ndio?” aliuliza.
“Ndio” nilimjibu
“Academic master kasema upeleke barua zako za uhamisho ofisin kwake sasa hivi.” Alisema.
“Asante kwa taarifa” nilijibu.
Nilinyanyuka haraka bila kuaga na kuelekea yalipo mabweni yetu. Nilipofungua nilishangaa kumkuta Candy amelala usingizi, nikashangaa wakati wa mapumziko Candy amelala kwa uchovu gani?
Sikumtilia sana maanani kwa vile nilikuwa mgeni, nikachukua barua zangu na kuzipeleka panapohusika na kisha kurejea darasani. Masomo ya siku hiyo yaliendelea kama kawaida. Muda wa vipindi ulipoisha nilirejea bwenini na wakati huo Candy ndio alikuwa akiamka, tulipata chakula cha mchana na kisha kwenda kwenye michezo. Wakati wa jioni ulipofika tuliingia kwenye kusali. Nilikaribishwa vizuri sana nilijihisi ni mmoja kati yao. Nilipata faraja mno kwa vile nilikuwa nikikubalika kila sehemu. Maisha ya shule yaliendelea vizuri.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
>>>>>>>>>>>>>>>>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: