NAOMBA MSIJE KWENYE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YANGU, NJOONI KWENYE MSIBA WANGU. Baada ya kukaa kwenye ndoa takriban miaka 10 kasoro miezi miwili wakafanikiwa kupata watoto wawili wa kwanza angel na wa pili baraka. jamaa akakaa na mkewe wakapanga mipango mizito sana kuhusiana na tukio lingine zito baada ya tukio lao la harusi.yaani kusheherekea miaka 10 ya ndoa yao. Lakini akajisemea, ngoja nipime kiwango cha uaminifu alichonacho mke wangu kabla ya hiyo sherehe haiwezekani kwamba kuna usalama kabisa maana ktk miaka yote nimekuwa MTU wa kazini,safarini in short sina muda mwingi wa kukaa na familia yangu....na kama atavuka hili jaribu basi naweka nadhiri mbele za mbingu nitamtafutia zawadi nzuri ambayo hajawahi kuona na hatokuja kuisahau Akawaambia marafiki zake nataka nifanye party ya kusheherekea miaka kumi ya ndoa yangu nahitaji kampani yenu,walifurahi sana marafiki zake hususani wafanyakazi wenzake. Kamati zikaundwa mara moja,lakini baba angel aliendelea na upelelezi wa kumjaribu mkewe pasipo kujua huyo mkewe aitwaye Elizabeth. Mama angel aliendelea kualika marafiki zake,wazazi wake wakawa wanasubiria kwa hamu kubwa hilo tukio wakimbariki mwenyezi Mungu kwa kuendelea kustawisha ndoa ya mtoto wao.huku asijue mmewe ana nini ndani ya moyo wake. Baba angel akafanya usajili wa line mpya ya tigo asiyoijua mkewe. Akasajili kwa kubuni jina la #Asajile_mwasilu ambaye alikuwa anahisi anatembea na mkewe maana mara kadhaa alishazikuta msg za ajabu kwenye simu ya mkewe kama za mtu na mpenzi wake na alipoichunguza kwenye tigo pesa usajili ukaonyesha jina la Asajile mwasilu. akawa akichat na mkewe mara kwa Mara, kupitia hiyo namba mpya...... siku moja mkewe akaangalia hiyo namba kwenye usajili akaona jina la "Asajile mwasilu" waooooo ooh my dear,akafurahi basi mwenyewe! Akaamua kupiga simu,mumewe hakupokea akakata akamwambia nitext niko mahali hatutaweza kuelewana. Kumbuka Wakati huo mumewe yupo kazini........akamwambia tuendelee kuchat My nikupendae uko wapi mpenzi wangu nikufuate sasa hivi,maana nilivyofrahi kuona SMS yako mungu anajua!namba zako zote baba angel alifuta kwenye simu yangu,na wewe ndio hujanitafuta tena..... baba angel akajibu, we taratibu,si unajua umeolewa wewe unifuate wapi? mumeo alinipigiaga simu kwamba angenifanya kitu kibaya Sana iwapo ningeendelea kuwa na mawasiliano na wewe basi nikaogopa mwenyewe ndio maana nikajikaliaga kimya. Ooh pole my sweet, ndio walivyo wanaume wasiojitambua hawa,yaani yeye anadhani anaweza kunichunga eti! Anasahau kwamba uanaume sio kuchunga mke uanaume ni kumhudumia vzur mkeo kitandani huo ndio ulinzi tosha. Yaani kusema ule ukweli,sijawahi kupata mwanaume wa kunihudumia vile nitakavyo zaidi yako,uko wapii? Mama angel akaendelea kufunguka. Mh!baba angel akajikuta anaishiwa pozi vibaya mno huku mapigo ya moyo yanayoambatana na ghadhabu yakikitesa kifua chake ambacho hata pumzi ilikuwa ni shida kutoka hakuamini kwamba huyo anaechat naye ni mkewe.......akamjibu kwa kicheko cha uongo Hahaaaaaa ina maana unataka kusema jamaa hayuko vzur kitandani?? Na vipi angel hajambo??? Ndio maana nakuuliza uko wapi this time nikufate?maana umelandisha mtoto mpaka sio vizuri,wewe mwanaume una damu kali,wakati mwingine mpaka naona aibu kumwita mume wangu baba angel maana ukweli Mimi ndio naujua....ila yeye hajui kitu anajua ni wake. Baba angel akawazaa wee huku mipango ya sherehe akiona ikiyeyuka taratibu kadri alivyokuwa akiendelea kuchati na mkewe... Akakaa katibu dakika 10 bila kusema chochote akiwaza je ni kweli angel sio wangu???mh! Hawa wanawake vipii?? akatazama saa yake akaona ni saa 8 za mchana akajisemea pale ofsini "hivi mke wangu ana roho mbaya kiasi hiki Kumbe nalea mtoto asie wangu?? Akafungua kwenye gallery akatazama picha za mtoto wake huyo mzur akaendelea kujipa moyo......... Akamrudia mkewe akamwambia Wacha buana uko naye angel hapo?? Mama angel akajibu yes, jamaa akajibu tena "Mi mwenyewe nimekumiss sana na nimemmis sana mwanangu natamani nimwone tu lakini naangalia usawa wa mfuko hauko sawa sana...... Mkewe akajibu hebu ngoja nipe dakika sifuri......... Haraka haraka mama angel akampigia simu mumewe kwa namba yake ya siku zote. "Samahani baby unamkumbuka neema msimamizi wa send off yangu?? Jamaa kwa unyonge huku akijikaza kusikiliza uongo wa mkewe akajibu ndio namkumbuka amefanya nini? Nilikuwa nampa taarifa ya party yetu kumbe alipata ajar yuko nyumbani, sasa nimeona wacha nikamwangalie kabisa sasa hivi naomba hela kidogo..........jamaa akamtumia tsh. laki moja na nusu na msg juu akimhimiza kuwahi kurudi. Vipi uko na angel hapo?? Mama akajibu ndio nikupe uongee naye?? basi akampa simu wakaongea na baba yake...... Akachukua simu mama yake akamwambia mumewe " halafu naenda nae angel mara moja! Jamaa akajibu hamna shida. Upesi mama angel akamwandikia sms anaedhani ni Asajile mchepuko wake kumbe ni mumewe huyo huyo akamtext sasa enda mahali tafuta guest nzur nakutumia elfu 80 sasa hivi Jamaa akajibu waooo ndio maana sijawahi kuacha kukupenda Elizabeth wangu.....basi ntakwambia nikipata. Ila uje na angel Baada ya dakika kama 30 Elizabeth akawa amejiandaa na kumuandaa mwanaye huku akimuahidi house girl kana kwamba atarudi saa 2 usiku....... Jamaa mida kama ya saa 10 jioni akamtext wife njoo hapa...........kuna Lodge inaitwa shelisheli unaijua?wife akaitikia yes.....basi njoo ni chumba namba 6 ghorofa ya 6 ila usimwache mtoto pls. Muda wote huo baba angel alikuwa ameshika kitambaa mkononi maana haipiti sekunde asipojifuta machozi machoni alikuwa akilia tu kwa jinsi alivyokuwa akimpenda mkewe.akajifikiria kuwa ,kwanini Mungu alimficha hilo jambo lililo moyoni mwa mkewe??kwanini Mungu ameruhusu alee mtoto asiye wake?? Kufika hapo Ni kama mwendo wa dakika 20 kwa toyo,basi Mama angel akaona achukue hiyo bodaboda awahi na kweli akawa amewahi.......akaingia hiyo hotel akaenda sehemu ya lift akafika chumba gorofa ya 6 akaenda chumba namba 6 Taratibu akafungua mlango mgongoni akiwa na angel akakuta hakuna mtu kumbe jamaa kaingia kidogo uani Dakika mbili hivi jamaa akawa anatokea kutoka uani Ile kufungua mlango Mama angel hakuamini alichokikuta maana tayari kwenye ubongo wake alikuwa amemtengeneza Asajile.....lakini sio Asajile aliyemkuta........ aligongana USO kwa USO na mumewe wanaetarajia kufanya sherehe ya ndoa yao wiki kama mbili zijazo. Mama angel alipiga yowe yesuuuuu huku akitaka kukimbia kutoka nje........mumewe akamkamata mkono wake akamtuliza na kumwambia "usiogope uko kwenye mikono salama ya baba wa watoto wako kaa utulie! Ooh my god sijui nimefanya nini Mimi!?mkewe alijisemea huku akionyesha kuchanganyikiwa. Wakati huo angel yuko kwa baba yake akistaajabu kuhusu kinachoendelea......... Ilimchukua kama dakika 20 mpaka kutulia mama angel Mumewe akaongea maneno mafupi tu..... MKE WANGU, USIJE UKADHANI MIMI NIPO GIZANI KABISA NISIJUE HATA HATA KIDOGO ULICHONACHO MOYONI MWAKO. AKAONGEA KILUGHA KUMKWEPESHA MTOTO ASIELEWE......LAKINI AKIWA NA MAANA KWAMBA TANGU HUYU MTOTO AMEZALIWA,MOYONI MWANGU NILIJUA SIO MTOTO WANGU,HATA WIFI ZAKO, shemeji zako WAZAZI WANGU WALINIAMBIA HILI JAMBO,NA LISEMWALO LIPO.......mama angel akazidi kupigwa butwaa Akaendelea kumsimulia mkewe....... SIKU MOJA NILIOTA NDOTO MTOTO ANAUMWA,NA TULIPOENDA HOSPITALI ETI KATIKA VIPIMO IKAONYESHA WANAPIMA DNA NIKAKASIRIKA,MBONA MNAMPIMA DNA WAKATI HUYU NI MGONJWA ANAHITAJI VIPIMO VINGINE? YULE DR AKANIAMBIA NITULIE KWANI ANAJUA AFANYACHO NIIKAMKA,NILIPOMPIGIA SIMU MTUMISHI WA MUNGU MMOJA AKANIAMBIA MTOTO SI WANGU LAKINI NISICHUKUE UAMUZI WOWOTE MBAYA BADALA YAKE NIENDELEE KULEA MAANA MALIPO NI KWA MUNGU. Elizabeth, umenitonesha tena kidonda mke wangu, Asante umemleta angel kwa baba yake Asajile lakini hayupo,bado nabaki Mimi ndiye baba yake Mungu atanilipa kwa uaminifu wangu......nashkur kwa uongo wako,asante kwa hela uliyonitumia ya chumba, nataka nikwambie nimefanya kama ulivyonipa maelekezo....... Wakati huo mama angel analia tu hakuna mfano,anaona hata aibu kusema nisamehe,alichojibu ktk kulia kwake ni "Naona nafsi yangu inahukumiwa mno kuliko maneno unayoniambia.....najua mwisho wa ndoa yangu ni hapa hakuna jinsi,siwezi kujitetea mume wangu!naiona jehanamu hii hapa,ninauona ubaya wa kufuga dhambi sasa,hapa ndio naamini hakuna siri duniani,haiwezekani ukafanya kitu ukajua haitajulikana. Niko tayari uniambie chochote na sitapinga,nimeaibika mbeke ya mwanangu Mwanangu nimeaibika mbele ya mume wangu anipendaye na nimeaibika mbele za mbingu na dunia..........nitaficha wapi USO wangu mie?? Jamaa akamwambia mkewe najuta kukujaribu mke wangu najuta kuupima uaminifu wako,ila namshukuru Mungu amenipa kifua kikubwa cha kukabiliana na mambo MAZITO. Lakini wakati mwingine namshukuru Mungu tu maana kila jambo lina makusudi....... Wakatoka pale hotelini wakaingia ndani ya gari ambayo baba angel alikuja nayo wakarudi nyumbani. Usiku mzima mwanamke hakulala usingizi akidhani labda mumewe angemuua hata mtoto........asubuhi kulipokucha jamaa alipowahi kazini mwanamke akaanza kupitia message walizokuwa wanachat na mmewe akaona ni kama yupo uchi tu.......akaenda kununua vidonge duka la dawa baridi akameza akafa huku akiacha ujumbe usemao KUHUSU KUFA KWANGU ASILAUMIWE MTU YEYOTE ILA NILAUMIWE MIMI NAPENDA NIWEKE HADHARANI KILA KITU,KUHUSU MTOTO WANGU ANGEL SIO WA MUME WANGU,JAPO KWA KIPINDI CHOTE ALIKUWA ANAJUA NI WAKE.......BABA YAKE ANAITWA ASAJILE MWASILU......ALINIPA MIMBA NIKIWA NDANI YA NDOA YANGU....... NATUBU KWA WAZAZI WANGU NA WAZAZI WA MUME WANGU MNIOMBEE NIENDAKO NIPUNGUZIWE ADHABU YA KABURI,MWISHO NAWAOMBA MSIJE KWENYE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YANGU,NJOONI MSIBANI. Mwisho sitaki kueleza nini kilitokea kwenye mazishi na msiba kwa ujumla wake Lakini jamaa anaendelea kulea mtoto asiye wake na mtoto wake. Kwenye mazishi alisikika akilia akisema najuta kwanini nilipima uaminifu na msimamo wa mke wangu,yamkini mpaka leo angekuwa hai............... BAADA YA MAZISHI MAKABURINI BABA ANGEL ALIMPELEKEA KARATASI KAKA YAKE AMBAYE NDIYO ANGETOA SHUKRANI KWA WATU NA MATANGAZO MACHACHE YA NINI KINGEENDELEA BAADA YA PALE,BASI AKASOMA ILE KARATASI KWAMBA "TUNAPENDA KUWATAARIFU KWAMBA ILE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YA BABA ANGEL PAMOJA NA MKEWE AMBAYE NI MAREHEMU SASA ILE TAREHE IPO PALEPALE ATAFANYA NA WATOTO WAKE ITAAMBATANA NA KUMSHUKURU MUNGU KATIKA YOTE MAANA IMEANDIKWA "SHUKURUNI KWA KILA JAMBO"........... Siku ya sherehe yenyewe watu walifika kwa wingi sana hamna mfano na miongoni mwao ni baba angel original yaani Asajile....... Itaendelea next time Ila jueni kuwa shetani yuko kaz

at 2:08 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top