USINISAHAU, Siwezi irudisha hatua yangu nyuma japo mbele napaogopa kusogea,sitamani kukumbuka japo nafurahia yaliopita,usije ukanisahau nilikupa yasiyo sahaulika, Haikuwa mara yako ya kwanza kunitoa machozi ila bado nilifurahia penzi,kuna wakati sitamani urudi ila natamani kukuona, nafsi imejawaha na hamaniko, kiapo cha penzi nimekisaliti, Najua sikuwa mpole bali nilikuwa mkarimu,hofu yangu ilikuwa si kuumia ila ni kukukosa pindi nitakapokuumiza,Umizo limeishinda furaha, teke penzi nikalipiga. Ila huwezi amini kinywa changu kitakachokuambia,pigo ulilopata limetoka kwa mwanamke mwenzio aliyeondoka na moyo wangu wa huruma na kuniachaa na ukarimu pekee. Unaweza ukamlaumu lakini adhabu ya mateso nipe mimi, maana kwa moyo wake wa kike hatoweza kuvumilia, Naomba usinisahau, hadithi nzima ya penzi iko ndani ya macho yangu nitazame. Macho yametawaliwa na furaha iliyojificha na maumivu yaliodhihirika,amini chozi hukata kauli ya uchungu, tamu husafiri na neno lisilofika mwisho kwa furaha, Upole wa jicho lenye mchozi ni ukatili wa ulimi kuhukumu kosa lisilo na tuhuma ya kweli, kuna wakati ni rahisi kuzungumza na moyo lakini pindi moyo unapojibu yale mazungumzo uliyozungumza hisia za kweli hudondosha chozi, Mkono wako ulifurahisha shavu langu,mara zote ila pindi ulipoinua kibao kunizaba, machozi yalikukatisha makosa yangu kutamka,Hakika ulimaanisha upendo,udhaifu wangu kwako niliuona pindi chozi langu lilipodondoka pia na kukosa mfutaji. How can i stop crying? how can i shade my tears? no i cant, nikifuta chozi nahisi nakutoa shavuni pindi unapotaka kunipiga busu la upendo Hakuna neno tamu litakalo toka kwenye kinywa pasipo kuwepo afanyaye neno kuwa tamu, moyo wako ni shahidi wa upendo, mbali nami ukaenda Tafadhali naomba USINISAHAU. Ila utakapotaka kunisahau,kumbuka kila dakika na sekunde inaumuhimu kwenye penzi, inaweza kuangamiza au kuokoa, shika moyo wako fumba macho kisha vuta kumbukumbuku ya siku nilikueleza nakupenda kwa unyenyekevu na wewe, siku uliyonijibu umekubali, utaona heshima na furaha ambayo hutoipata kokote zaidi ya kwangu. I MISS YOU by *🅱 professional love*

at 8:53 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top