Home → ushauri
→ UNAYAJUA HAYA ILI UFURAHIE MAPENZI YAKO??

1.FANYA UCHAGUZI SAHIHI
Hapa ndipo watu wanapotakiwa kutumia akili zao mpaka zile za akiba, ukikosea hapa ni rahisi sana kuvurunda hapo baadaye. Uhusiano wenye nguvu, hujengwa na penzi la kweli. Acha kukurupuka, lazima ujihakikishie kwamba uliyenaye ni chaguo kutoka ndani ya moyo wako.
Najua una maswali; kwamba utawezaje kumjua mwenye mapenzi ya kweli, hiyo ni mada ambayo nimeshaandika mara kadhaa katika ukurasa huu na gazeti damu na hili, Ijumaa. Kimsingi, kwa kufuata maelekezo hayo, mwenzi ambaye unatarajia kuwa naye katika maisha ya ndoa hapo baadaye, lazima msingi uwe ni uchaguzi sahihi.
Sikia, watu wengi waliokuwa na fedha, wamefilisika baada ya kuoa/kuoleawa na wenzi ambao si sahihi. Aidha, wapo wenye mafanikio makubwa sana, ambayo wameyapata baada ya kuoa/kuolewa na wenzi sahihi. Rafiki zangu, si jambo rahisi kumpata yule aliye sahihi. Inahitaji utulivu.
Yapo mengi sana ambayo unapaswa kuyaangalia, ambayo nimekwishaeleza sana katika makala zangu zilizopita. Wakati nahitimisha kipengele hiki, shika neno moja tu; unapomchagua mwenzi wa maisha yako, hakikisha ni yule aliye sahihi! Tuendelee na kipengele kingine.
2. JIELEZE
Migogoro mingi baina ya walio kwenye uhusiano husababishwa na wenzi kutowafahamu vyema wenzao. Usiingie katika mkumbo huu, ni suala la kujieleza tu. Kumweleza mpenzi wako ulivyo, kutamfanya ajue vitu unavyopenda na usivyopenda. Aidha, kama unao udhaifu wowote wa kiafya na kadhalika, mweleze mwenzako.
Kumweleza kutamfanya ajiamini kuwa anapendwa. Kunaonesha unavyojiamini na unayetaka mwenzako ashirikiane na wewe katika hali uliyonayo. Si vibaya mwenzio kukufahamu kwamba una hasira sana. Yes! Maana akishajua hilo, ataacha utani unaokaribia kukuudhi maana anajua vizuri kuwa una hasira za karibu.
Ipo mifano mingi sana, lakini kikubwa cha kushika katika kipengele hiki ni kuwa mkweli kwa mwenzako kuhusu maisha yako. Acha kumdanganya kwamba familia yenu ina uwezo mkubwa, wakati ni wa kawaida. Kuwa mkweli, mapenzi si utajiri, ni hazina iliyojificha ndani ya moyo.
Kama anakupenda, anakupenda tu! Siku akigundua kwamba unamdanganya, pendo lake litapungua kwa kiasi kikubwa sana. Jieleze kwa uwazi na ukweli kutoka ndani ya moyo wako. Naye atakuheshimu na utakuwa umetengeneza mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye ndoa isiyo na migogoro.
3. MPE UHURU
Wengi wanaamini kumbana mpenzi ni njia sahihi ya kumfanya awe mwaminifu, si kweli. Kuna wenye tabia ya kuvizia simu za wenzao na kuzipekua, si utaratibu mzuri. Mpe uhuru, usimbane! Kuonesha kumwamini sana mpenzi wako, kunamfanya naye aishi ndani ya uaminifu.
Kumchunga hakumnyimi kuendelea na mambo yake, sana sana atafanya kwa siri kubwa. Kumpa uhuru, kutamwogopesha, atajua yupo na mwaminifu ndiyo maana hafuatiliwi, hapo utakuwa umechochea naye awe mwaminifu kama wewe.
4. ACHA PAPARA
Katika hatua za mwanzo kabisa za uhusiano wenu, hutakiwi kuwa na papara katika jambo lolote. Kila kitu kifanywe kwa utaratibu. Huna sababu ya kurukia mambo, hasa makubwa.
Wengi wamekuwa na haraka sana ya kukutana kimwili, haya ni makosa makubwa sana. Haraka ya nini kama unatarajia awe wako wa maisha. Ngoja nikuambie rafiki yangu, unapoanza kuulizia mapema mambo ya faragha, unamfanya mwenzako ashindwe kukuamini.
Kwanza, atahisi wewe upo kwa ajili ya kutaka kujistarehesha tu, lakini pia anaweza kufikiria kwamba unapenda sana mambo ya chumbani. Kumfanya agundue kasoro hiyo ni tatizo kubwa sana kwako.
Hata hapo baadaye mtakapoingia kwenye ndoa, ni rahisi zaidi kukumbuka mambo ya zamani, kwamba yupo na mtu anayependa sana mambo ya mahaba. Kwa maneno mengine, hata akihisi tu au kusikia kwamba una mtu mwingine pembeni, atapeleka moja kwa moja hisia zake kwenye kuamini moja kwa moja juu ya jambo hilo.
Papara si jambo jema kabisa kwa mwenzi ambaye unatarajia awe wako wa maisha. Tulia, mchunguze kwanza. Kumbuka unatakiwa kufikiria kuhusu mustakabali wa maisha yako ya baadaye, kama ndivyo, huna haja ya kuharakisha mambo ya mapenzi.
5. JENGA URAFIKI
Ukitaka kutengeneza uhusiano wenye nguvu, basi zingatia zaidi urafiki. Kumfanya mwezi wako rafiki ni silaha kubwa na yenye nguvu katika kuuimarisha uhusiano.
Mwenzi wako anapojiona kama rafiki, anakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza chochote, ikiwemo matatizo na migongano mbalimbali kama rafiki zaidi.
Hawezi kukuficha siri zake. Atakuwa na wewe muda wote na atakusogeza karibu yake kwa kila kitu. Hata penzi lenu pia litakuwa na nguvu zaidi. Urafiki ni kila kitu ndugu zangu.
Acha tabia ya kumkaripia mpenzi wako, jenga mazoea ya kujadiliana zaidi kuliko kutumia kauli za ukali. Rafiki zangu, yote hayo niliyoyazungumza yanajengwa na jambo moja tu; urafiki!
6. MSIFIE
Wengine wanaweza kushangazwa na kauli hiyo, lakini nataka kuwaambia kuwa kati ya mambo muhimu kabisa kumfanyia mpenzi wako na kulifanya penzi kuwa jipya ni kumsifia. Unapomwambia mwenzako kauli nzuri za kumbembeleza kuwa yeye ni mzuri, anakuvutia kwa kila hali, unajenga penzi.
Unamfanya anajihisi wa thamani, atajiamini kuwa yeye ni mkamilifu, si kwa watu wanaomzunguka pekee, bali hata wewe ambaye umemchagua na kumfanya awe wako.
Kama huna utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, huu ni wakati wako wa kufanya hivyo kwa lengo la kuzidisha mapenzi na kuyapa nguvu.
7. SAIDIA KUKUZA UHUSIANO WENU
Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha penzi linazidi kukua siku hadi siku. Kwa maana hiyo, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unakuwa mstari wa mbele kukuza uhusiano wenu.
Kuna mambo mengi sana ambayo yakifanyika, yanakuza uhusiano. Vipo vitu vya kufanya, kutoka pamoja ni njia mojawapo ya kukuza uhusiano. Rafiki zangu, mnapokwenda katika matembezi, husaidia kubadilisha mapenzi na kuonekana mapya.
Si lazima kwenda nje ya mji, kikubwa ni kuzingatia mfuko wako. Hata mkienda mahali pa kawaida tu, mkanywa juice na keki, bado ni nafasi nzuri kwenu ya kukuza uhusiano huo.
Kila mmoja ana wajibu wa kufanya hivyo, lakini hutakiwi kumsubiri mwenzako afanye, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unamfanya mwenzi wako afurahie uhusiano wenu. Kufanya hivyo, kutampa deni na yeye la kufanya hivyo kwako.
8. MFANYE NAMBA MOJA
Kuna baadhi ya marafiki wana fikra potofu (hasa wanaume). Hawa wanaamini kumpa mwanamke nafasi katika maisha ni kumfanya akukalie. Si kweli. Mwanamke unapompa nafasi ya kwanza, anaufurahia uhusiano wenu.
Anajiona mwenye hadhi kubwa zaidi kwako, hutafuta njia za kukufanya umpende maradufu, kuliko kumuacha akijiona hana nafasi.
Ongozana na mpenzi wako kwenye kumbi za burudani, mialiko ya sherehe mbalimbali, lakini pia mpe kipaumbele kwa kila kitu. Hili halihitaji elimu ya darasani. Chunguza wenzako wanaowapa wenzi wao kipaumbele wanavyoishi.
Achana na mifumo ya kizamani, ukimpa mwenzako usawa anajiona ana nafasi kwako na thamani katika uhusiano mlionao.
9. MPE NAFASI
Hapa hakuna kitu kikubwa sana, ni kiasi cha kumpa nafasi katika mambo yako muhimu. Mathalan unataka kununua kiwanja Gongo la Mboto; Hata kama umeshaweka kila kitu sawa, lakini kumshirikisha tu, kutamfanya ajione mwenye nafasi kubwa kwako.
Hili si kwa wanaume pekee, hata wanawake nao wanapaswa kutoa vipaumbele kwa wanaume zao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza ladha ya mapenzi kwa wapendanao.
Inawezekana elimu hii imekupitia kushoto, hebu jaribu uone mafanikio yake.
Kumpa nafasi mwenzako katika mambo yako, tafsiri yake ni kumuamini na kumfanya azidi kujiamini kwako. Ni rahisi sana, lakini habari njema kwako ni kwamba, atakusikiliza kwa kila kitu, maana anajiona yeye ni sehemu yako kikamilifu.
10. MTAMBULISHE
Mapenzi ya siri yana ukomo wake marafiki zangu. Ngoja niwaambie, unapokuwa unapenda mapenzi ya siri sana, unampa wakati mgumu mwenzako.
Ni rahisi kufikiria kwamba, unafanya hivyo kwa kuwa ama hujiamini au una mtu mwingine. Weka mambo hadharani. Mtambulishe mwenzi wako kwa marafiki zako.
Jiamini, unapokutana na mtu uliyesoma naye zamani au kuishi naye sehemu moja, mwambie kwamba uliyenaye ni mwenzako na unatarajia kuingia naye kwenye ndoa.
Kufichaficha kunaondoa utamu wa mapenzi. Kunazidisha maswali ambayo hayana majibu. Kama yapo ni huyo mwenzako kujijibu mwenyewe. Kwa kawaida, hatajipa majibu mazuri.
Yatakuwa ya kinyume – yenye tafsiri mbaya. Kwamba yawezekana hutaki kumtambulisha kwa kuwa una mtu mwingine. Je, ni kweli? Kama ndivyo huna sababu ya kumpotezea muda mwenzako. Kama si kweli, basi amka. Gundua kwamba ulikuwa unafanya makosa na uanze ukurasa mpya.
11. GUSIA MAMBO YA KIIMANI
Kuzungumzia mambo ya dini kulingana na imani yenu, kutamsogeza mwenzako kwenye ukweli kuwa una lengo naye la kuungana katika maisha ya ndoa. Angalizo kwako ni kwamba, wakati unamweleza hayo, iwe kweli yanatoka ndani ya moyo wako.
12. WAHUSISHE VIONGOZI WA DINI
Ikiwa uhusiano wenu umekomaa, unatakiwa kuwashirikisha viongozi wa dini. Angalia mazingira, unaweza kwenda naye, au kwenda mwenyewe na kuwaeleza nia yako. Waambie wakuombee au wawaombee ili uhusiano wenu uwe na nguvu.
Kumbuka ndoa ni tendo la heri, hivyo shetani naye hutumia nafasi hiyo kuwaharibia! Kumuingiza Mungu katika uhusiano wenu kuna maana, mtakuwa katika ulinzi wenye nguvu zaidi.
Yamkini pia, kama uliyenaye si chaguo kutoka kwa Muumba atamuengua mikononi mwako na kukupeleka palipo sahihi. Usiogope, nenda kaonane na viongozi wa dini na uwaeleze kinagaubaga.
13. KAMILISHA TARATIBU ZA KIFAMILIA/KIMILA
Ikiwa una uhakika kuwa mwenzako ndiye uliyemkusudia (zaidi kwa wanaume) wajulishe wazazi wako, kisha anza taratibu za kimila na kifamilia. Tuma wazee wapeleke posa, lipa mahari, halafu sasa anza kutimiza maagizo mengine yote utakayoagizwa.
Ni njia ya kuelekea kwenye ndoa. Uhusiano wenye baraka za wazazi, si tu kwamba unakuwa na nguvu, bali una radhi za wazazi wenu wa pande zote mbili. Je, kwa hali hiyo uhusiano wenu hautaimarika? Bila shaka utazidi kuchanua.
14. JADILINI KUHUSU NDOA
Hii ni hatua ya muhimu kabisa katika kuelekea kwenye ndoa. Mnapaswa kuijadili ndoa yenu ni ya namna gani? Kama imani zenu zimetofautiana, nini kifanyike? Pindi mtakapojadiliana, mtaweza kupata muafaka juu ya ndoa ambayo ni sahihi kwenu.
Ndugu yangu, usilazimishe kumbadilisha mwenzako akufuate katika imani yako kama yeye hataki au pengine kuna vipingamizi katika familia yao. Kila mmoja wenu anapaswa kuweka hoja mezani na mnazijadili kwa mapana yake na mwisho muafaka utapatikana, mtaoana.
Hakuna kinachoshindikana katika majadiliano, tumia lugha nzuri kumshauri mwenzako ili ajue unamjali hivyo ni rahisi kuridhia ulichomshauri. Ieleweke tu ndoa yoyote mtakayokubaliana kupitia majadiliano yenu, basi itadumu kuliko mkitumia njia ya kulazimishana.
(b) Kwa wanandoa hapa sasa mnisome kwa makini maana wengi wamekuwa wakifeli katika hatua hii kutokana na kujisahau. Mikikimikiki ya maisha inapoibuka inaweza kuwafanya kila mmoja wenu akawa na maamuzi yake katika maisha hata kama mwanzoni (kabla ya ndoa) dhamira yenu ilikuwa njema.
Siku ya leo, Lets Talk About Love itakumegea vipengele sita ambavyo kimsingi ukivisoma kwa makini itakuwa ni dozi sahihi kama mwanandoa kuweza kujua siri hizi muhimu za kufurahia mapenzi yenu na nikushauri kuitumia kila siku.
15. WEKENI MIPANGO PAMOJA
Wanandoa wengi wamekuwa wakijisahau pindi wanapokuwa ndani ya ndoa. Inawezekana awali walikuwa na mikakati mizuri lakini baadaye mmoja wao huanza kujiamulia bila kumshirikisha mwenzake. Tatizo hili lipo zaidi kwa wanaume, mfumo dume unachukua mkondo wake. Utakuta mwanaume anafanya maamuzi peke yake akiamini yeye ndiyo kila kitu.
Jeuri hii inakuja hasa pale mwanaume anapoamini kuwa yeye ndiyo chanzo cha fedha wanayotaka kufanyia kitu fulani. Ataamua bila kumshirikisha mkewe kwa kuwa fedha anakuwa nazo yeye bila kujua mipango yote inapaswa kuzungumzwa pamoja kabla ya kufanya maamuzi.
Ndoa ni makubaliano baina ya watu wawili hivyo basi, katika kila jambo la maendeleo litafanikiwa pale tu mtakapolipanga pamoja. Ndugu yangu, acha kujiona wewe ni zaidi katika ndoa kutokana na kipato ulichonacho. Fedha si lolote si chochote katika maisha ya ndoa. Fedha zisibadilishe maamuzi ya mipango yenu, kila mnachotaka kukifanya basi mkifanye pamoja.
16. TUMIA MAJADILIANO ZAIDI
Yamkini wote wawili mlifanya majadiliano kabla ya kufikia maamuzi ya ndoa, basi ni wajibu wenu kuishi katika majadiliano kila siku. Wapo watu wasiopenda kuona ndoa za watu zinakuwa na furaha. Wataingilia na kuwafanya mgombane. Inawezekana pia mkapishana kauli katika mazungumzo, busara huhitajika.
Kutofautiana kwa kauli pamoja na vitu vingine, vinaweza kumalizwa kwa njia ya majadiliano. Jadilini katika lugha nzuri itakayomfanya mwenzio aone thamani yake.
Mkijadili yote kwa uyakinifu, mwisho mtagundua kumbe kilichokuwa kinawatatiza ni kitu kidogo ambacho hakikuhitaji nguvu kubwa kukitatua. Mnapojadiliana ni rahisi pia kutambua kosa lilikuwa wapi au lilisababishwa na nani, hivyo ni rahisi kumuepuka.
17. PALIZI YA NDOA
Kama ilivyo kwa mazao yakiwa shambani yanavyohitaji kupaliliwa ili yaweze kushamiri, vivyo hivyo katika ndoa. Ndoa inapaswa kupaliliwa kila siku. Jaribu kila wakati kusoma alama za nyakati, vitu gani anavipenda mwenzako basi umfanyie kila wakati.
Mfano unaweza kupanga siku moja katika wiki ukamchukua mkeo au mumeo na kumtoa nje kimatembezi. Ndoa hupaliliwa na vitu kama hivyo. Zawadi za hapa na pale zisipungue, acha kuishi kwa mazoea eti kwa kuwa tayari ni mkeo au tayari ni mumeo.
Unapoipalilia ndoa katika staili za zawadi, mitoko na vitu vingine huifanya ionekane mpya kila siku. Mnunulie mkeo au mumeo vazi unaloona linaendana na wakati mlionao.
18. KINYWA CHENYE LADHA
Inawezekana ukaona labda nazungumzia kitu cha kawaida sana, lakini kama ukitafakari kwa kina na kwa mapana yake, utagundua kwamba ni mjadala wenye maana katika ndoa.
Hata kwenye Kitchen Party, sherehe za ndoa n.k, suala la kinywa chenye ladha nzuri huzungumzwa sana, ila hapa nitakuongezea baadhi ya vitu vingine usivyovijua.
Kwa kawaida, wanawake ndiyo ambao huaswa zaidi katika kuwa na kauli nzuri kwa waume zao. Wanaume wamesahaulika kabisa. Wanaonekana kama wao hawana wajibu wa kuwa na kauli nzuri kwa wake zao; jambo hili si la kweli hata kidogo.
Wote wanapaswa kuweka masikilizano kwa kauli ya pamoja, huku kila mmoja akiwa na shabaha ya kuhakikisha mwenzake haudhiki na maneno yake. Ni jambo jepesi sana – kuwa na ulimi wenye ladha.
KUJITAMBUA kwamba unayezungumza naye ni mke/mumeo. Hebu jiulize, ikiwa mwanzoni wakati wa uchumba wenu mliweza kuwa na kauli nzuri, kila mmoja akiwa na hamu ya kumsikiliza mwenzake muda wote, iweje katika ndoa?
Jibu la swali hili litakuwa mwongozo mzuri zaidi wa kuinakshi ndoa yenu kuwa bora yenye furaha siku zote. Ndugu zangu, furaha ndiyo kila kitu katika uhusiano wowote ule. Kukiwa na furaha, hakuwezi kuingia tatizo lolote. Litapitia wapi, wakati mioyo ina amani?
Ikiwa kinyume chake, ni rahisi hata kugombana, maana hata mgombanishi hupata nafasi zaidi sehemu isiyo na amani, isiyo na majadiliano, pasipo na maelewano. Usikubali kuwa katika ndoa ya namna hiyo.
19. EPUKA MANENO YA KUUDHI
Kipengele hiki hakina tofauti sana na kilichopita, lakini hapa kuna la zaidi la kuongezea. Kuna wakati wenzi wanaweza kuingia katika mtafaruku ambao chanzo chake ni cha ajabu kabisa! Kwa mfano, unakuta mpenzi anamwambia mwenzake: “Mh! Na wewe unanuka sana mdomo!”
Kauli gani hiyo kwa mpenzi wako? Mwanaume unalala naye kila siku, kwa nini umwambie ananuka? Wewe ukifanya hivyo, huko nje wamuambieje? Kwanza kama ni kweli ana tatizo hilo, ni jukumu lako kumtibu, lakini pia kumtunzia siri.
Kama nje anachekwa, ndani ya familia pia anachekwa, wapi atapata faraja? Yapo maneno mengi sana yenye kuudhi, lakini hapa nitataja machache. Wengine wanawaambia wenzao wananuka kikwapa, hawajapendeza, hawana akili nk.
Haya ni maneno ya kuudhi. Hebu fikiria kauli kama hii mtu anamtamkia mkewe! “Yaani kweli wewe huna akili, kitu kidogo kama hicho kweli unaweza kukosea? Ndiyo maana wenzetu wanafanikiwa kimaisha, wanatuacha. Sijui nilikutana na wewe wapi?...maisha yangu yanazidi kuwa giza tu, nikiwa na wewe!”
Acha maneno ya kufuru, kwani siku zote hukuona upungufu wake? Kuwa makini na kauli zako. Ndoa yako utaivunja wewe mwenyewe, pia kama ni kuijenga, utaijenga wewe mwenyewe!
20. UBORA KATIKA TENDO LA NDOA
Hapa ndipo panapotakiwa kupewa heshima kubwa zaidi kuliko vipengele vyote vilivyotangulia. Katika masomo yaliyopita, nimewahi kufafanua hili kwa undani zaidi, leo nitagusia juu juu tu!
Rafiki zangu, tendo la ndoa ni la heshima. Halitaki papara na linatakiwa kupewa nafasi na kila mmoja kuridhika. Acha kujifikiria mwenyewe, maana hapa ndipo panapopatikana mianya ya kutoka nje ya ndoa.
Hakikisha mwenzako anaridhishwa na wewe mnapokuwa chumbani. Tafuta elimu zaidi ya kufurahia tendo hilo ili mwenzako awe na sababu ya kuwa na wewe. Sikia nikuambie, tendo la ndoa kwa wanandoa hasa waliozoeana linachosha!
Huu ni ukweli ambao wengi wanaupinga. Yes! Linachosha na kukikanaisha. Hakuna kipya. Mwanaume yule yule. Kitanda kile kile, chumba kile kile. Lazima umchoke.
Hata hivyo, ukiwa mbunifu utaendelea kumuona mwenzako mpya kila siku. Badilisheni mazingira, tafuteni muda wa kutoka pamoja angalau mara moja ndani ya miezi mitatu – kwa mwaka mara nne.
Yapo mengi sana, elimu hii ni pana, hasa kama utakuwa mbunifu na mwenye kuisaka kila siku. Rafiki zangu, nadhani mnafahamu namna inavyokuwa vigumu kueleza kila kitu hapa gazetini, lakini kikubwa cha kumalizia mada hii ni hiki; unapokuwa na mwenzako faragha, ujue kuwa anategemea zaidi wewe kumfanya afurahie tendo hilo.
Ukijua hivyo, naye akajua hivyo, furaha ya tendo la ndoa itadumu siku zote za ndoa yenu.
UNAYAJUA HAYA ILI UFURAHIE MAPENZI YAKO??  1.FANYA UCHAGUZI SAHIHI Hapa ndipo watu wanapotakiwa kutumia akili zao mpaka zile za akiba, ukikosea hapa ni rahisi sana kuvurunda hapo baadaye. Uhusiano wenye nguvu, hujengwa na penzi la kweli. Acha kukurupuka, lazima ujihakikishie kwamba uliyenaye ni chaguo kutoka ndani ya moyo wako. Najua una maswali; kwamba utawezaje kumjua mwenye mapenzi ya kweli, hiyo ni mada ambayo nimeshaandika mara kadhaa katika ukurasa huu na gazeti damu na hili, Ijumaa. Kimsingi, kwa kufuata maelekezo hayo, mwenzi ambaye unatarajia kuwa naye katika maisha ya ndoa hapo baadaye, lazima msingi uwe ni uchaguzi sahihi. Sikia, watu wengi waliokuwa na fedha, wamefilisika baada ya kuoa/kuoleawa na wenzi ambao si sahihi. Aidha, wapo wenye mafanikio makubwa sana, ambayo wameyapata baada ya kuoa/kuolewa na wenzi sahihi. Rafiki zangu, si jambo rahisi kumpata yule aliye sahihi. Inahitaji utulivu. Yapo mengi sana ambayo unapaswa kuyaangalia, ambayo nimekwishaeleza sana katika makala zangu zilizopita. Wakati nahitimisha kipengele hiki, shika neno moja tu; unapomchagua mwenzi wa maisha yako, hakikisha ni yule aliye sahihi! Tuendelee na kipengele kingine. 2. JIELEZE Migogoro mingi baina ya walio kwenye uhusiano husababishwa na wenzi kutowafahamu vyema wenzao. Usiingie katika mkumbo huu, ni suala la kujieleza tu. Kumweleza mpenzi wako ulivyo, kutamfanya ajue vitu unavyopenda na usivyopenda. Aidha, kama unao udhaifu wowote wa kiafya na kadhalika, mweleze mwenzako. Kumweleza kutamfanya ajiamini kuwa anapendwa. Kunaonesha unavyojiamini na unayetaka mwenzako ashirikiane na wewe katika hali uliyonayo. Si vibaya mwenzio kukufahamu kwamba una hasira sana. Yes! Maana akishajua hilo, ataacha utani unaokaribia kukuudhi maana anajua vizuri kuwa una hasira za karibu. Ipo mifano mingi sana, lakini kikubwa cha kushika katika kipengele hiki ni kuwa mkweli kwa mwenzako kuhusu maisha yako. Acha kumdanganya kwamba familia yenu ina uwezo mkubwa, wakati ni wa kawaida. Kuwa mkweli, mapenzi si utajiri, ni hazina iliyojificha ndani ya moyo. Kama anakupenda, anakupenda tu! Siku akigundua kwamba unamdanganya, pendo lake litapungua kwa kiasi kikubwa sana. Jieleze kwa uwazi na ukweli kutoka ndani ya moyo wako. Naye atakuheshimu na utakuwa umetengeneza mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye ndoa isiyo na migogoro. 3. MPE UHURU Wengi wanaamini kumbana mpenzi ni njia sahihi ya kumfanya awe mwaminifu, si kweli. Kuna wenye tabia ya kuvizia simu za wenzao na kuzipekua, si utaratibu mzuri. Mpe uhuru, usimbane! Kuonesha kumwamini sana mpenzi wako, kunamfanya naye aishi ndani ya uaminifu. Kumchunga hakumnyimi kuendelea na mambo yake, sana sana atafanya kwa siri kubwa. Kumpa uhuru, kutamwogopesha, atajua yupo na mwaminifu ndiyo maana hafuatiliwi, hapo utakuwa umechochea naye awe mwaminifu kama wewe. 4. ACHA PAPARA Katika hatua za mwanzo kabisa za uhusiano wenu, hutakiwi kuwa na papara katika jambo lolote. Kila kitu kifanywe kwa utaratibu. Huna sababu ya kurukia mambo, hasa makubwa. Wengi wamekuwa na haraka sana ya kukutana kimwili, haya ni makosa makubwa sana. Haraka ya nini kama unatarajia awe wako wa maisha. Ngoja nikuambie rafiki yangu, unapoanza kuulizia mapema mambo ya faragha, unamfanya mwenzako ashindwe kukuamini. Kwanza, atahisi wewe upo kwa ajili ya kutaka kujistarehesha tu, lakini pia anaweza kufikiria kwamba unapenda sana mambo ya chumbani. Kumfanya agundue kasoro hiyo ni tatizo kubwa sana kwako. Hata hapo baadaye mtakapoingia kwenye ndoa, ni rahisi zaidi kukumbuka mambo ya zamani, kwamba yupo na mtu anayependa sana mambo ya mahaba. Kwa maneno mengine, hata akihisi tu au kusikia kwamba una mtu mwingine pembeni, atapeleka moja kwa moja hisia zake kwenye kuamini moja kwa moja juu ya jambo hilo. Papara si jambo jema kabisa kwa mwenzi ambaye unatarajia awe wako wa maisha. Tulia, mchunguze kwanza. Kumbuka unatakiwa kufikiria kuhusu mustakabali wa maisha yako ya baadaye, kama ndivyo, huna haja ya kuharakisha mambo ya mapenzi. 5. JENGA URAFIKI Ukitaka kutengeneza uhusiano wenye nguvu, basi zingatia zaidi urafiki. Kumfanya mwezi wako rafiki ni silaha kubwa na yenye nguvu katika kuuimarisha uhusiano. Mwenzi wako anapojiona kama rafiki, anakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza chochote, ikiwemo matatizo na migongano mbalimbali kama rafiki zaidi. Hawezi kukuficha siri zake. Atakuwa na wewe muda wote na atakusogeza karibu yake kwa kila kitu. Hata penzi lenu pia litakuwa na nguvu zaidi. Urafiki ni kila kitu ndugu zangu. Acha tabia ya kumkaripia mpenzi wako, jenga mazoea ya kujadiliana zaidi kuliko kutumia kauli za ukali. Rafiki zangu, yote hayo niliyoyazungumza yanajengwa na jambo moja tu; urafiki! 6. MSIFIE Wengine wanaweza kushangazwa na kauli hiyo, lakini nataka kuwaambia kuwa kati ya mambo muhimu kabisa kumfanyia mpenzi wako na kulifanya penzi kuwa jipya ni kumsifia. Unapomwambia mwenzako kauli nzuri za kumbembeleza kuwa yeye ni mzuri, anakuvutia kwa kila hali, unajenga penzi. Unamfanya anajihisi wa thamani, atajiamini kuwa yeye ni mkamilifu, si kwa watu wanaomzunguka pekee, bali hata wewe ambaye umemchagua na kumfanya awe wako. Kama huna utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, huu ni wakati wako wa kufanya hivyo kwa lengo la kuzidisha mapenzi na kuyapa nguvu. 7. SAIDIA KUKUZA UHUSIANO WENU Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha penzi linazidi kukua siku hadi siku. Kwa maana hiyo, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unakuwa mstari wa mbele kukuza uhusiano wenu. Kuna mambo mengi sana ambayo yakifanyika, yanakuza uhusiano. Vipo vitu vya kufanya, kutoka pamoja ni njia mojawapo ya kukuza uhusiano. Rafiki zangu, mnapokwenda katika matembezi, husaidia kubadilisha mapenzi na kuonekana mapya. Si lazima kwenda nje ya mji, kikubwa ni kuzingatia mfuko wako. Hata mkienda mahali pa kawaida tu, mkanywa juice na keki, bado ni nafasi nzuri kwenu ya kukuza uhusiano huo. Kila mmoja ana wajibu wa kufanya hivyo, lakini hutakiwi kumsubiri mwenzako afanye, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unamfanya mwenzi wako afurahie uhusiano wenu. Kufanya hivyo, kutampa deni na yeye la kufanya hivyo kwako. 8. MFANYE NAMBA MOJA Kuna baadhi ya marafiki wana fikra potofu (hasa wanaume). Hawa wanaamini kumpa mwanamke nafasi katika maisha ni kumfanya akukalie. Si kweli. Mwanamke unapompa nafasi ya kwanza, anaufurahia uhusiano wenu. Anajiona mwenye hadhi kubwa zaidi kwako, hutafuta njia za kukufanya umpende maradufu, kuliko kumuacha akijiona hana nafasi. Ongozana na mpenzi wako kwenye kumbi za burudani, mialiko ya sherehe mbalimbali, lakini pia mpe kipaumbele kwa kila kitu. Hili halihitaji elimu ya darasani. Chunguza wenzako wanaowapa wenzi wao kipaumbele wanavyoishi. Achana na mifumo ya kizamani, ukimpa mwenzako usawa anajiona ana nafasi kwako na thamani katika uhusiano mlionao. 9. MPE NAFASI Hapa hakuna kitu kikubwa sana, ni kiasi cha kumpa nafasi katika mambo yako muhimu. Mathalan unataka kununua kiwanja Gongo la Mboto; Hata kama umeshaweka kila kitu sawa, lakini kumshirikisha tu, kutamfanya ajione mwenye nafasi kubwa kwako. Hili si kwa wanaume pekee, hata wanawake nao wanapaswa kutoa vipaumbele kwa wanaume zao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza ladha ya mapenzi kwa wapendanao. Inawezekana elimu hii imekupitia kushoto, hebu jaribu uone mafanikio yake. Kumpa nafasi mwenzako katika mambo yako, tafsiri yake ni kumuamini na kumfanya azidi kujiamini kwako. Ni rahisi sana, lakini habari njema kwako ni kwamba, atakusikiliza kwa kila kitu, maana anajiona yeye ni sehemu yako kikamilifu. 10. MTAMBULISHE Mapenzi ya siri yana ukomo wake marafiki zangu. Ngoja niwaambie, unapokuwa unapenda mapenzi ya siri sana, unampa wakati mgumu mwenzako. Ni rahisi kufikiria kwamba, unafanya hivyo kwa kuwa ama hujiamini au una mtu mwingine. Weka mambo hadharani. Mtambulishe mwenzi wako kwa marafiki zako. Jiamini, unapokutana na mtu uliyesoma naye zamani au kuishi naye sehemu moja, mwambie kwamba uliyenaye ni mwenzako na unatarajia kuingia naye kwenye ndoa. Kufichaficha kunaondoa utamu wa mapenzi. Kunazidisha maswali ambayo hayana majibu. Kama yapo ni huyo mwenzako kujijibu mwenyewe. Kwa kawaida, hatajipa majibu mazuri. Yatakuwa ya kinyume – yenye tafsiri mbaya. Kwamba yawezekana hutaki kumtambulisha kwa kuwa una mtu mwingine. Je, ni kweli? Kama ndivyo huna sababu ya kumpotezea muda mwenzako. Kama si kweli, basi amka. Gundua kwamba ulikuwa unafanya makosa na uanze ukurasa mpya. 11. GUSIA MAMBO YA KIIMANI Kuzungumzia mambo ya dini kulingana na imani yenu, kutamsogeza mwenzako kwenye ukweli kuwa una lengo naye la kuungana katika maisha ya ndoa. Angalizo kwako ni kwamba, wakati unamweleza hayo, iwe kweli yanatoka ndani ya moyo wako. 12. WAHUSISHE VIONGOZI WA DINI Ikiwa uhusiano wenu umekomaa, unatakiwa kuwashirikisha viongozi wa dini. Angalia mazingira, unaweza kwenda naye, au kwenda mwenyewe na kuwaeleza nia yako. Waambie wakuombee au wawaombee ili uhusiano wenu uwe na nguvu. Kumbuka ndoa ni tendo la heri, hivyo shetani naye hutumia nafasi hiyo kuwaharibia! Kumuingiza Mungu katika uhusiano wenu kuna maana, mtakuwa katika ulinzi wenye nguvu zaidi. Yamkini pia, kama uliyenaye si chaguo kutoka kwa Muumba atamuengua mikononi mwako na kukupeleka palipo sahihi. Usiogope, nenda kaonane na viongozi wa dini na uwaeleze kinagaubaga. 13. KAMILISHA TARATIBU ZA KIFAMILIA/KIMILA Ikiwa una uhakika kuwa mwenzako ndiye uliyemkusudia (zaidi kwa wanaume) wajulishe wazazi wako, kisha anza taratibu za kimila na kifamilia. Tuma wazee wapeleke posa, lipa mahari, halafu sasa anza kutimiza maagizo mengine yote utakayoagizwa. Ni njia ya kuelekea kwenye ndoa. Uhusiano wenye baraka za wazazi, si tu kwamba unakuwa na nguvu, bali una radhi za wazazi wenu wa pande zote mbili. Je, kwa hali hiyo uhusiano wenu hautaimarika? Bila shaka utazidi kuchanua. 14. JADILINI KUHUSU NDOA Hii ni hatua ya muhimu kabisa katika kuelekea kwenye ndoa. Mnapaswa kuijadili ndoa yenu ni ya namna gani? Kama imani zenu zimetofautiana, nini kifanyike? Pindi mtakapojadiliana, mtaweza kupata muafaka juu ya ndoa ambayo ni sahihi kwenu. Ndugu yangu, usilazimishe kumbadilisha mwenzako akufuate katika imani yako kama yeye hataki au pengine kuna vipingamizi katika familia yao. Kila mmoja wenu anapaswa kuweka hoja mezani na mnazijadili kwa mapana yake na mwisho muafaka utapatikana, mtaoana. Hakuna kinachoshindikana katika majadiliano, tumia lugha nzuri kumshauri mwenzako ili ajue unamjali hivyo ni rahisi kuridhia ulichomshauri. Ieleweke tu ndoa yoyote mtakayokubaliana kupitia majadiliano yenu, basi itadumu kuliko mkitumia njia ya kulazimishana. (b) Kwa wanandoa hapa sasa mnisome kwa makini maana wengi wamekuwa wakifeli katika hatua hii kutokana na kujisahau. Mikikimikiki ya maisha inapoibuka inaweza kuwafanya kila mmoja wenu akawa na maamuzi yake katika maisha hata kama mwanzoni (kabla ya ndoa) dhamira yenu ilikuwa njema. Siku ya leo, Lets Talk About Love itakumegea vipengele sita ambavyo kimsingi ukivisoma kwa makini itakuwa ni dozi sahihi kama mwanandoa kuweza kujua siri hizi muhimu za kufurahia mapenzi yenu na nikushauri kuitumia kila siku. 15. WEKENI MIPANGO PAMOJA Wanandoa wengi wamekuwa wakijisahau pindi wanapokuwa ndani ya ndoa. Inawezekana awali walikuwa na mikakati mizuri lakini baadaye mmoja wao huanza kujiamulia bila kumshirikisha mwenzake. Tatizo hili lipo zaidi kwa wanaume, mfumo dume unachukua mkondo wake. Utakuta mwanaume anafanya maamuzi peke yake akiamini yeye ndiyo kila kitu. Jeuri hii inakuja hasa pale mwanaume anapoamini kuwa yeye ndiyo chanzo cha fedha wanayotaka kufanyia kitu fulani. Ataamua bila kumshirikisha mkewe kwa kuwa fedha anakuwa nazo yeye bila kujua mipango yote inapaswa kuzungumzwa pamoja kabla ya kufanya maamuzi. Ndoa ni makubaliano baina ya watu wawili hivyo basi, katika kila jambo la maendeleo litafanikiwa pale tu mtakapolipanga pamoja. Ndugu yangu, acha kujiona wewe ni zaidi katika ndoa kutokana na kipato ulichonacho. Fedha si lolote si chochote katika maisha ya ndoa. Fedha zisibadilishe maamuzi ya mipango yenu, kila mnachotaka kukifanya basi mkifanye pamoja. 16. TUMIA MAJADILIANO ZAIDI Yamkini wote wawili mlifanya majadiliano kabla ya kufikia maamuzi ya ndoa, basi ni wajibu wenu kuishi katika majadiliano kila siku. Wapo watu wasiopenda kuona ndoa za watu zinakuwa na furaha. Wataingilia na kuwafanya mgombane. Inawezekana pia mkapishana kauli katika mazungumzo, busara huhitajika. Kutofautiana kwa kauli pamoja na vitu vingine, vinaweza kumalizwa kwa njia ya majadiliano. Jadilini katika lugha nzuri itakayomfanya mwenzio aone thamani yake. Mkijadili yote kwa uyakinifu, mwisho mtagundua kumbe kilichokuwa kinawatatiza ni kitu kidogo ambacho hakikuhitaji nguvu kubwa kukitatua. Mnapojadiliana ni rahisi pia kutambua kosa lilikuwa wapi au lilisababishwa na nani, hivyo ni rahisi kumuepuka. 17. PALIZI YA NDOA Kama ilivyo kwa mazao yakiwa shambani yanavyohitaji kupaliliwa ili yaweze kushamiri, vivyo hivyo katika ndoa. Ndoa inapaswa kupaliliwa kila siku. Jaribu kila wakati kusoma alama za nyakati, vitu gani anavipenda mwenzako basi umfanyie kila wakati. Mfano unaweza kupanga siku moja katika wiki ukamchukua mkeo au mumeo na kumtoa nje kimatembezi. Ndoa hupaliliwa na vitu kama hivyo. Zawadi za hapa na pale zisipungue, acha kuishi kwa mazoea eti kwa kuwa tayari ni mkeo au tayari ni mumeo. Unapoipalilia ndoa katika staili za zawadi, mitoko na vitu vingine huifanya ionekane mpya kila siku. Mnunulie mkeo au mumeo vazi unaloona linaendana na wakati mlionao. 18. KINYWA CHENYE LADHA Inawezekana ukaona labda nazungumzia kitu cha kawaida sana, lakini kama ukitafakari kwa kina na kwa mapana yake, utagundua kwamba ni mjadala wenye maana katika ndoa. Hata kwenye Kitchen Party, sherehe za ndoa n.k, suala la kinywa chenye ladha nzuri huzungumzwa sana, ila hapa nitakuongezea baadhi ya vitu vingine usivyovijua. Kwa kawaida, wanawake ndiyo ambao huaswa zaidi katika kuwa na kauli nzuri kwa waume zao. Wanaume wamesahaulika kabisa. Wanaonekana kama wao hawana wajibu wa kuwa na kauli nzuri kwa wake zao; jambo hili si la kweli hata kidogo. Wote wanapaswa kuweka masikilizano kwa kauli ya pamoja, huku kila mmoja akiwa na shabaha ya kuhakikisha mwenzake haudhiki na maneno yake. Ni jambo jepesi sana – kuwa na ulimi wenye ladha. KUJITAMBUA kwamba unayezungumza naye ni mke/mumeo. Hebu jiulize, ikiwa mwanzoni wakati wa uchumba wenu mliweza kuwa na kauli nzuri, kila mmoja akiwa na hamu ya kumsikiliza mwenzake muda wote, iweje katika ndoa? Jibu la swali hili litakuwa mwongozo mzuri zaidi wa kuinakshi ndoa yenu kuwa bora yenye furaha siku zote. Ndugu zangu, furaha ndiyo kila kitu katika uhusiano wowote ule. Kukiwa na furaha, hakuwezi kuingia tatizo lolote. Litapitia wapi, wakati mioyo ina amani? Ikiwa kinyume chake, ni rahisi hata kugombana, maana hata mgombanishi hupata nafasi zaidi sehemu isiyo na amani, isiyo na majadiliano, pasipo na maelewano. Usikubali kuwa katika ndoa ya namna hiyo. 19. EPUKA MANENO YA KUUDHI Kipengele hiki hakina tofauti sana na kilichopita, lakini hapa kuna la zaidi la kuongezea. Kuna wakati wenzi wanaweza kuingia katika mtafaruku ambao chanzo chake ni cha ajabu kabisa! Kwa mfano, unakuta mpenzi anamwambia mwenzake: “Mh! Na wewe unanuka sana mdomo!” Kauli gani hiyo kwa mpenzi wako? Mwanaume unalala naye kila siku, kwa nini umwambie ananuka? Wewe ukifanya hivyo, huko nje wamuambieje? Kwanza kama ni kweli ana tatizo hilo, ni jukumu lako kumtibu, lakini pia kumtunzia siri. Kama nje anachekwa, ndani ya familia pia anachekwa, wapi atapata faraja? Yapo maneno mengi sana yenye kuudhi, lakini hapa nitataja machache. Wengine wanawaambia wenzao wananuka kikwapa, hawajapendeza, hawana akili nk. Haya ni maneno ya kuudhi. Hebu fikiria kauli kama hii mtu anamtamkia mkewe! “Yaani kweli wewe huna akili, kitu kidogo kama hicho kweli unaweza kukosea? Ndiyo maana wenzetu wanafanikiwa kimaisha, wanatuacha. Sijui nilikutana na wewe wapi?...maisha yangu yanazidi kuwa giza tu, nikiwa na wewe!” Acha maneno ya kufuru, kwani siku zote hukuona upungufu wake? Kuwa makini na kauli zako. Ndoa yako utaivunja wewe mwenyewe, pia kama ni kuijenga, utaijenga wewe mwenyewe! 20. UBORA KATIKA TENDO LA NDOA Hapa ndipo panapotakiwa kupewa heshima kubwa zaidi kuliko vipengele vyote vilivyotangulia. Katika masomo yaliyopita, nimewahi kufafanua hili kwa undani zaidi, leo nitagusia juu juu tu! Rafiki zangu, tendo la ndoa ni la heshima. Halitaki papara na linatakiwa kupewa nafasi na kila mmoja kuridhika. Acha kujifikiria mwenyewe, maana hapa ndipo panapopatikana mianya ya kutoka nje ya ndoa. Hakikisha mwenzako anaridhishwa na wewe mnapokuwa chumbani. Tafuta elimu zaidi ya kufurahia tendo hilo ili mwenzako awe na sababu ya kuwa na wewe. Sikia nikuambie, tendo la ndoa kwa wanandoa hasa waliozoeana linachosha! Huu ni ukweli ambao wengi wanaupinga. Yes! Linachosha na kukikanaisha. Hakuna kipya. Mwanaume yule yule. Kitanda kile kile, chumba kile kile. Lazima umchoke. Hata hivyo, ukiwa mbunifu utaendelea kumuona mwenzako mpya kila siku. Badilisheni mazingira, tafuteni muda wa kutoka pamoja angalau mara moja ndani ya miezi mitatu – kwa mwaka mara nne. Yapo mengi sana, elimu hii ni pana, hasa kama utakuwa mbunifu na mwenye kuisaka kila siku. Rafiki zangu, nadhani mnafahamu namna inavyokuwa vigumu kueleza kila kitu hapa gazetini, lakini kikubwa cha kumalizia mada hii ni hiki; unapokuwa na mwenzako faragha, ujue kuwa anategemea zaidi wewe kumfanya afurahie tendo hilo. Ukijua hivyo, naye akajua hivyo, furaha ya tendo la ndoa itadumu siku zote za ndoa yenu.
Artikel Terkait
ULISHAWAHI KUKUTANA NA MTU MWENYE UPENDO WA KWELI??? Ipo siku utakutana na mtu tofauti na ulivyozoea kuona au kusikia. Haitakuwa kwa sababu ya tabasamu lao au ucheshi wao au kwa jinsi ya kuongea kwao au kusema majina yao. Ni kwa sababu ya njia itakayo kufanya wewe ujisikie tofauti. hutaogopa kupenda na kupendwa. Siku moja utakutana na Upendo utakaoufurahia. Hutaweza kufikiria mara mbili. Hutaweza kuwa na wasiwasi kwamba anakupenda au hakupendi. ‘Utafahamu tu. Kwa mtu huyu hutaweza kuficha tabia yako. hutaficha madhaifu yako na usumbufu wako. hutakuwa na mawazo ya itakuwaje kama ata kupandia kichwani. hutakuwa na maswali ya kujua muhimu wake na hutakuwa na labda. Wakati ukikutana na mtu huyu hutaingiwa na woga. hutaweza kufikiri fikiri kitu chochote. hutaweza kufikiria upendo wake kwako. Na wakati anaposema hawezi kwenda mahali , utafahamu kuwa ni kweli. Wakati huo hutasikia kukosa kitu ndani ya moyo wako, hutasikia upweke, hutaweza kusikia chochote kinyume na upendo uliopo. Ipo siku , mtu fulani atabadilisha maisha yako. kwa sababu atakuonyesha upendo wa kweli ni upi na maana ya upendo ni nini, unaonekanaje. Atakuonyesha kuwa upendo hauna mwisho. na hutamkimbia , na hutaweza kutaka faida zaidi. hutapigwa na wala kupata maumivu yasio na msingi. Ipo siku Hutaogopa kupata maumivu. Hutaogopa kuacha tena. kwa kupoteza kipande cha moyo wako na roho yako. hutaogopa tena kutoa na kutoa upendo wako . Siku moja utapumua kwa urahisi kwa kufahamu kuwa huyo mtu hataondoka . Utapumua vizuri kwa kujua kwamba upendo huo utadumu. Huyo mtu hatakutelekeza na wala hataweza kukukimbia. Utafahamu toka moyoni mwako kwamba upendo huo hautakuumiza. Utaweza kuishi, kucheka, kulia na kupumua kwa urahisi ukiwa pembeni ya mtu huyo. Utajifahamu na kujiona vizuri. Utaweza kumuonyesha makovu, na vidonda ulivyonavyo na kwa kuwa vimepona. Utaweza kumuonyesha mtu huyo moyo wako wote kwa kujua kuwa hawezi kukuacha. Ipo siku utajikuta unaamka mikononi mwake, ukiwa karibu yake kwa upendo , katika maisha yako. hutakuwa na wasiwasi . hutaogopa. hutasikia uzito wa kupumua tena. Utahisi upendo ndani yako. mwisho utagundua Upendo halisi. Washirikishe wengi. ... Read More
VITU VIZURI 60 VYA KUMWAMBIA MSICHANA UMPENDAE:  Ninamaanisha kuwa maneno matamu.Wakati kijana uko kwenye process ya kutafuta na kujaribu kuuteka moyo wa msichana, unatakiwa kujifunza kutumia maneno matamu.Na lazima ujue kuwa sio kila neno unalotumia litagusa moyo wa mwanamke unayemtaka,Lakini maneno matamu yanafanya kazi ya kushangaza . Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. watu wengi pia huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza. sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unaempenda na unahitaji awe wako milele. 1.Macho yako ni mazuri , yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama. 2,Unanifanya niwe mwanaume bora , kwa hio nastahili mapenzi yako. 3.Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu. 4.Wewe ni mzuri na ni mrembo naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua. 5.Unapotabasamu huzuni kwangu hupotea , ghafla nakuwa mtu wa furaha. 6.Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani , lakini umenichagua mimi. 7.Hapana.wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo. 8.Ninapokushika nashisi kulegea kwenye magoti. 9.Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako,ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu. ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu. 10.Siamini , maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi. 11.kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda , natamani niwe na wewe milele. yaani wasife. 12.Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja. 13.Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda,nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia. 14.Kukutana nawe ni kitu ambacho hakijawahi kutokea. 15.Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia , hapo hupotea kabisaaa. 16.Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi. 17.Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama haitatosha kukupenda. 18.Napata furaha nikiwa na wewe. 19. Napenda kutumia muda na wewe. 20.Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa. 21.Natamani maishsa yangu yote nikuone ukiwa na furaha. 22.Usibadilike nakupenda jinsi ulivyo. 23.Nikiwa na wewe nafurahi kama mtoto. 24.Napenda nywele zako. 25.Napenda nikukumbatie ninapokuaga. 26.Natamani kukubusu kila sehemu ya mwili wako. 27.Naanza siku na wewe ndani ya mawazo yangu, na ninamaliza siku na wewe kwenye ndoto zangu. 28. ukiwa na mimi huwa natamani kusimamisha muda, maana muda unakwenda haraka. 29.Nikisikia sauti yako asubuhi , siku nzima ni mtu wa furaha. 30.Tabasamu lako zuri linanifanya niyeyuke. 31.Unaponiaga napata shida kukuruhusu uende. 32. Umenielewa vizuri, ni kama unasoma mawazo yangu. 33.Mungu alikupendelea kukuumba, akili na kila ulichonacho. 34.Najivunia kuwa na wewe na ninafurahia. 35.Napenda unavyosema unanipenda. 36.Mapenzi yetu ni kama mawimbi ya bahari, wakati mwingi hutulia, na wakati mwingine huvuma,lakini yanarudi palepale. 37.mapenzi yetu yawe kama ua rose ambalo halina miiba. 38.Najua kwa nini watu wanatutazama , ni kwa sababu wewe ni mzuri kuliko mwezi. 39.Muda utakuwa hauna thamani endapo sitatumia na wewe. 40.kama siku yangu ingeanza na busu lako, nisingehitaji kahawa. 41.Kama ningeambiwa nielezee rangi, basi ningeenda kwenye rangi za rainbow, kwa sababu wewe ni mzuri.ni wa muujiza. 42.Mimi bila wewe ni mbaya, lakini ni mzuri nikiwa na wewe. 43.Tukishikana mikono na mioyo yetu inashikana,na nafsi zetu zinapatana . 44.Siku ya kwanza tulipokutana, nilijua ipo siku tutakutana tena, na nafurahi imetokea. 45.Nafurahi tumekua pamoja, sina cha kukosa hata kidogo. 46.Moyo wangu unapumua kama ndege, kila unapotabasamu. 47.Kila ninapokuwa nimeshuka moyo, nikikusikia wewe moyo wangu unapata nguvu. 48.Shika mikono yangu nami nitashika moyo wako, tunza kwa maisha yote. 49.Maisha yote , milele yote,isio na mwisho, toka nimekutana na wewe maneno yote yana maana. 50.Siku naona kama mwaka, na siku inapita kama sekunde. 51.Natamani ningekuwa kama pweza mwenye mikono mingi ili nikukumbatie na mikono myote. 52.Siamini katika nafsi mpya, lakini baada ya kukutana na wewe nimeamini, natamani kama ningeweza kurudi nyuma na kutengeneza kitu. 53.Sitaweza kukutoa kwenye mawazo yangu , kwa maana nakuhitaji uwepo. 54.Kuna wakati nahisi upweke, kwa wakati huo, basi huamua kukupigia simu na kusikia sauti yako. 55.Ninapokutizama namuona mungu jinsi alivyokuumba na kukubariki. 56.Unanifanya niwe wa muhimu . 57.Ni siri ambayo inanifanya nikutazame zaidi kwa kila siku. 58.Kuongea na wewe kila siku unanifanya nikufahamu zaidi na zaidi. 59.Moyo wangu nakupa,nipe moyo wako ili tuifungie kwa pamoja, na tutupe ufunguo mbali. 60.Nakuhitaji muda wote, siku , mwaka na hata milele. ... Read More
Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa njia 10 muhimu  Mwanamke ni kiumbe anayependa kuonyeshwa mapenzi kila wakati. Kumtongoza mwanamke kunaweza kuwa kazi ngumu sana usipozingatia mambo kadhaa muhimu. Ukitaka kuweza kumtongoza mwanamke lazima ujue anachotaka yeye. Waweza kushangaa kwamba wanachotaka wanawake ni vitu vidogo ambavyo waweza timiza ili kuweza kumfanya akukubali hata kuzungumza na wewe. Waweza kumtongoza mwanamke ukizingatia mambo yafuatayo Msikilize mwanamke unayemtongoza Wanawake hupenda mtu ambaye anawasikiliza kwa kila jambo wanachosema. Ni muhimu unapopatana na mwanamke sharti uwe makini na anacho simulia. Kuwa mtu ambaye anauliza maswali na anaye taka kujua zaidi juu ya huyu mwanamke. Muulize kazi anayofanya, anakoishi, na mwonyeshe kwamba unamsikiliza kwa kuuliza swali unapotaka ufafanuzi. Mwanamke huskia ako huru kwa mwanamme ambaye anamsikiliza kwa maana hii huonyesha mwanamume anamdhamini huyo mwanamke. Kwa kumwonyesha kwamba wewe una nia ya kujua mahitaji yake, kwa matendo yako, si maneno yako, kutakusaidia kumwonyesha kwamba wewe ni mtu anayeweza kuwa naye maishani mwake. Kuweka kipaumbele mahitaji yake na kumsikiza kutakusaidia kwa kumtongoza mwanamke huyo. Mwanamke hupenda mtu mwenye kujiamini Unapomwongelesha mwanamke lazima uwe mtu mwenye kujiamini. Ujasiri na kujiamini ni kitengo kikubwa kinachofafanua mwanamume. Unapomwongelesha mwanamke lazimi uonyeshe ujasiri mbele yake. Kama Warren Farrell, Ph.D., anavyosema “Jambo linalomvutia mwanamke kwa mwanamume ni mwanamume mwenye ujasisiri”. Ujasiri utamvutia mwanamke kwa kujua mwanamume anazungumza na kujibeba kwa ujasiri. Mwanamke hupenda kuwa karibu na mwanamume anayevutia Kuvutia kwa mwanamume huja kwa njia kadhaa. Mwanamke hupenda mwanamume ambaye hachoshi kwa hadithi zake, ni mcheshi, anachangia kwa mazungumzo kati yao na anaye hakikisha kwamba mwanamke anajiskia huru kwa maongezi. Kama mwanamume, hakikisha unatoa mifano inayoendana na maongezi mliyo nayo. Hakikisha mnayoyaongelea yanachangiwa na nyinyi wawili. Mwanamume aliemcheshi na mwenye kumvutia mwanamke kwa anavyoendeleza mazungumzo ndie aliye na nafasi kubwa ya kumpata mwanamke anayetarajia ama aliye na hamu naye. Kumbuka kwamba usiwe ni wewe pekee unayeongea, mwachie pia mwanamke achangie pia. Ukizingatia haya, mwanamke hujiskia yuko huru nawe na anaweza ongelea chochote. Mwanamke hapendi mtu mwenye haraka Haraka hapa ina maana, kwa kutongoza mwanamke lazima uwe mtu mwenye subra sana. Kinachomfanya mtu awe na hamu ya kuwa na mwingine ni matarajio anayopata rohoni. Unapopatana na mwanamke kwa wakati wa kwanza, usimwonyeshe kwa umbele unachotaka, lakini taka kumsikiliza, mjue jina, anachofanya kazini, na mambo mengine kwanza. Kwa kufanya haya mwanamke ataona kwamba unahamu naye na kwamba atajiskia wa maana kwako. Jambo hili litakusaidia sana kwa kutongoza huyo mwanamke. Kitu cha muhimi ni kwanza upate kuwa marafiki na mwanamke yule ili uweze kupata nafasi nzuri ya kumtongoza. Ubinafsi wa kipekee Mwanamke hupenda vitu vya kipekee sio vitu vinavyoigwa kwingine. Usije ukafanya ama ukanena kama mwanamume mwingine ili kumshinda huyo binti. Kuwa na ubinafsi wako, fanya mambo yako kwa kipekee. Kuiga wengine hakutakusaidia kwani mwanamke atakuona kama mtu asiyejiamini. Mwanamke hupenda manamume ambaye ni tofauti na wanaume wengine ambao amewahi kutana nao hapo mwanzo. Ni vizuri kuwa na vitu ambavyo ni vya kipekee kwako. Kama sauti yako, vile wacheka vile wamtizama mwanamke yule, vile wavaa, vile umejipaka manukato mazuri. Upekee huu hukupa nafasi ya mbele kwa mpango wako wa kumtongoza mwanamke yule. Mavazi na usafi Mwanamke hupenda usafi sana. Ukitaka mwanamke aweze kuvutiwa nawe lazima uvae vizuri na uwe safi. Kuvaa vizuri, nguo zinazokufanya upendeze huwa njia moja ya kuvutia wanawake. Pia kuwa makini na usafi. Kuoga vizuri, kujipaka manukato yanayo vutia, kuweka nywele, nguo safi husaidia sana kwa kukupa ujasiri wa kumwendea mwanamke uliye na hamu naye. Sio lazima uvae mavazi ghali, lakini valia kwa kupendeza. Mwanamke hupenda mtu anayejiamini katika alichovalia. Muziki Kwa miaka mingi muziki umejulikana kuwa chombo cha kuonyesha mapenzi ama kama namna ya kumtongoza mwanamke. Mwanamke hupenda kuonyeshwa kwamba ni mtu wa thamani kwa mwanamume. Muziki waweza kukusaidia kuweka mazingira yenye utulivu na yenye riwaya ya mahaba. Kumbuka kumzingatia wakati unaweka muziki ule, jua mbeleni muziki anaopenda na fanya hima kwamba unamtumbuiza na aina hizo kwa kikamilifu. Ukifanya hivyo, mwanamke ataoona kwamba unathamini. Weka muziki wenye utulivu, wenye mahaba na wenye kumsifu mtu wa kike na uzuri wake kwa kumwonyesha mapenzi. Bidii ya kuwa makini kwa mwanamke na kumpa pongezi wakati wowote Mwanamke ni kiumbe anayependa kusifiwa na kupongezwa sana. Kwa mwanamume ni muhimu kwamba kwa kumtongoza mwanamke, kumbuka kila wakati kumpongeza kwa kuvaa kwake, nywele, viatu, anavyong’aa. Ni muhimu kumwonyesha kwamba umefurahia bidii yake ya kuvaa vyema na kuhakikisha anakaa vyema mnapokutana. Mwanamke hujiskia mwenye thamana sana kwa kujua kwamba kuna mwanamume amemwona anakaa sawa. Mwambie wapenda alivyosongwa, anavyotoa busu, anavyocheka, na kila kidogo anachofanya. Utashangaa kwamba yaweza onekana ni mambo madogo lakini huchangia katika kutongoza mwanamke. Mpikie chajio mwanamke unayemtongoza Kama mwanamume hakuna kitu cha muhimu kama kumpikia mwanamke uliye na macho kwake. Mwanamume ajuaye kupika huwa anawavutia wanawake sana. Unaweza kumwalika mwanamke kwako ka chajio. Fanya hima ukajua chakula anachopenda binti unaye mtarajia, ukahakikisha umepika chakula kitamu na kinachovutia kwa kuangalia na harufu tamu. Mwandalie mezani pamoja na kinyuaji. Kuwa umehakikisha kuna mazingira yenye utulivu na pia weka mziki wenye mahaba. Mwanamke hujihisi mwenye thamani sana. Hapa utakuwa umejiongezea pointi kadhaa kwa mpango wako wa kumtongoza binti yule. Zawadi Kila mwanamke hupenda kupata zawadi wakati wowote. Kama mwanamume itakusaidia pakubwa kwa mpango wako wa kumtogoza binti yeyote. Zawadi zaweza kuwa tofauti. Waweza mtumia maua ya waridi kazini, ukakumbuka kumtumia chokoleti wakati wa wapendanao, ukamtumania kahawa asubuhi akiingia kazini. Kwa kufanya vile, mwanamke hujiskia wa dhamana na anayependwa. Wanawake pia hupenda kupelekwa mahali pa zuri ambapo anaweza kujibinjari. Mpeleke densi, mpeleke mahali mkala chajio, mpeleke mbugani kwa wanyama ama kwa safari. Kufanya vile kutakupatia pointi nyingi kwa mtazamo wako wa kumtongoza mwanamke yule. Kama kawaida wanawake na wanaume huwa na hamu ya kujuana na kuishi maisha pamoja. Katika kumtongoza mwanamke lazima kwanza mwanamume afahamu nini mwanamke yule anachopenda. Pia inabidi mwanamume pia kumpa sikio binti yule wakati wowote wanapozungumza na kuuliza mwaswali asipoelewa kitu. Mpe wanamke pongezi wakati wowote mnapopatana, mpe pongezi kwa kusukwa vizuri, kupaka kucha vizuri, kuvaa nguo vizuri, tabasamu lake na anavyocheka. Mara kwa mara mpe zawadi za hapa na pale. La muhimu sana ni mwanamke huvutiwa na mwanamume anaye jiamini. Ukiwa mwanamume ambaye anajiamini, itamfanya mwanamke yule kujiskia huru kuwa karibu nawe na hio itakusaidia katika hali ya kumtongoza. ... Read More
JINSI YA KUISHI NA MPENZI MPENDA PESA   HAPA tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu. Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki zangu, kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana. Suala la kusaidiana si la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote, kwa mwanaume au mwanamke. Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha! Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana. Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri.” Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni ndiyo. Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha. Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na fedha, ukiona mpenzi wako anaweka fedha mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha. Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze ukweli kisha muangalie namna nyingine ya kumsaidia. Itakuwa siyo busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande zote mbili. Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akutoe ‘out’, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au laah. Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka? Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu? Kimsingi ukiwa na mpenzi mwenye tabia ya kutaka kukuomba fedha kila wakati tena katika matumizi mengine ambayo siyo ya msingi, mbinu zifuatazo ni muhimu kuzifuata. Twende tukaone. MWELEZE UKWELI Kama huna fedha wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana fedha au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi. JENGENI KUSAIDIANA Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake. Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna fedha zinavyokuwa hazitoshi na ataweza kubana matumizi. ACHA UFUJALI Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa fedha kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa unazo! Unachotakiwa ni kudhibiti mapema matumizi yako hata kama fedha itakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu. BAKI NA HILI Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, bali kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie. Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo epukana na tabia hiyo. ... Read More
Jinsi ya Kuomba Msamaha MACHAGUO YA UPAKUAJI Podikasti Makala Nyinginezo SOMA KATIKA Amkeni! | Septemba 2015 UNAWEZA KUWA NA FAMILIA YENYE FURAHA Fuata Mwongozo wa Mungu ili Uwe na Ndoa Yenye Furaha Kujiuliza maswali mawili rahisi kunaweza kuisaidia ndoa yako. AMKENI! Viwango Vinavyomfaa Kila Mtu, Nyakati Zote—Upendo Upendo unaotajwa mara nyingi katika Biblia si ule wa kimahaba au kimapenzi. HABARI NJEMA KUTOKA KWA MUNGU! Kanuni za Biblia Zinatunufaishaje? Yesu alieleza kwa nini tunahitaji mwongozo na ni kanuni gani mbili za Biblia zina umuhimu mkubwa. Kuwafundisha Watoto Unyenyekevu Je, Inafaa Kujihatarisha Kwa Kusudi la Kujisisimua? Watoto Wanapoondoka Nyumbani Umuhimu wa Kazi za Nyumbani Kuomba msamaha kunaweza kuzuia ugomvi CHANGAMOTO Muda mfupi tu uliopita wewe na mwenzi wako mmetoka kubishana. Kisha unajiambia hivi: ‘Sihitaji kumwomba msamaha. Kwa sababu si mimi niliyeanzisha ugomvi!’ Mmeacha kuzungumzia jambo hilo, lakini hali si shwari. Unafikiria kuomba msamaha lakini unaona huwezi kusema, “samahani.” KWA NINI HILO HUTUKIA Kiburi. “Wakati mwingine si rahisi kusema ‘samahani’ kwa sababu sitaki kujishushia heshima,” anakiri mume anayeitwa Charles. * Kiburi kinaweza kukufanya uone aibu kukubali kwamba umechangia tatizo. Mtazamo. Unaweza kuhisi kwamba kuomba msamaha kunahitajika tu pale unapokosea. Mke anayeitwa Jill anasema hivi: “Ni rahisi kwangu kusema ‘samahani’ ninapojua kwamba nimesababisha tatizo. Lakini, ikiwa sote tulisema mambo yasiyofaa, ni vigumu kufanya hivyo. Kwa nini niombe msamaha ikiwa sote tuna makosa?” Unaweza kujitetea ikiwa unahisi kwamba mwenzi wako ndiye mwenye makosa. “Unapoamini kabisa kwamba hujafanya kosa lolote, unaonyesha huna hatia kwa kukataa kuomba msamaha,” anasema mume anayeitwa Joseph. Malezi. Huenda ulilelewa katika familia ambayo halikuwa jambo la kawaida kuomba msamaha. Ikiwa ndivyo, huenda hukujifunza kukubali makosa yako. Kwa kuwa hukuzoea kufanya hivyo tangu utotoni, ni vigumu kwako kuomba msamaha ukiwa mtu mzima. MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA Mfikirie mwenzi wako. Jaribu kukumbuka jinsi ulivyohisi vizuri ulipoombwa msamaha na mtu fulani. Kwa nini basi usimfanye mwenzi wako ahisi hivyo? Hata ikiwa huamini kwamba ulikosea, unaweza kuomba msamaha kwa ajili ya maumivu ambayo mwenzi wako amepata au kwa sababu ya usumbufu wowote uliotokana na matendo yako. Maneno hayo yanaweza kumsaidia mwenzi wako ahisi vizuri.— Kanuni ya Biblia: Luka 6:31 . Zingatia ndoa yako. Ona kuomba msamaha kuwa ushindi katika ndoa yako na si kushindwa. Zaidi ya yote, mtu anayeendelea kukasirika ni “mgumu kuliko mji wenye nguvu,” inasema Methali 18:19 . Inaweza kuwa vigumu kurudisha amani katika hali hiyo. Pia, unapoomba msamaha unazuia kosa kuwa kikwazo. Ukifanya hivyo, unatanguliza ndoa yako badala ya hisia zako.— Kanuni ya Biblia: Wafilipi 2:3 . Uwe mwepesi kuomba msamaha. Ni kweli kwamba ni vigumu kuomba msamaha ikiwa hujakosea. Lakini makosa ya mwenzi wako hayapaswi kuwa kisingizio cha kuendelea kuwa na tabia mbaya. Hivyo, usisite kuomba msamaha ukifikiri kwamba muda ukipita kosa hilo litasahaulika. Unapoomba msamaha unafanya iwe rahisi pia kwa mwenzi wako kuomba msamaha. Na kadiri unavyoomba msamaha ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kufanya hivyo tena wakati mwingine.— Kanuni ya Biblia: Mathayo 5:25 . Onyesha kwamba unajali hisia za mwenzi wako. Kutetea kosa lako si sawa na kuomba msamaha. Kusema kwa kejeli, “samahani kwa kuwa naona unakwazika haraka kwa sababu ya jambo hili,” si njia ya kuomba msamaha hata kidogo! Kubali makosa yako na utambue kwamba umemuumiza mwenzi wako, hata kama unaona hakuwa na sababu ya kukwazika. Tambua ukweli. Kubali kwamba utafanya makosa. Kwa kweli, kila mtu hukosea! Hata kama unafikiri huna hatia, tambua kwamba kuna uwezekano umechangia jambo hilo. Biblia inasema hivi: “Mtu wa kwanza katika kesi yake ni mwadilifu, mwenzake huingia naye hakika humchunguza kwa undani.” ( Methali 18:17 ) Itakuwa rahisi kwako kuomba msamaha ikiwa una maoni yaliyosawazika kuhusu mapungufu yako ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: