STORY :HIGH SCHOOL SEHEMU YA KWANZA. Jina langu ninaitwa Catherine Kindamba, Ilikua ni siku ya jumanne nilipowasili shuleni Hans pope Academy mkoani Mwanza kutoka Dar es salaam. Nilimaliza kidato cha nne katika shule ya secondary Canossa na kupata division one na kisha kuchaguliwa kujiunga katika shule ya secondary Kibasila kwa mchepuo wa ECA, yani Economics, commerce na Accountancy. Baba yangu hakuyapenda kabisa mazingira ya pale Kibasila, hivyo aliamua kuniamishia Hans pope Academy Mwanza. Ni kiasi kama mwenzi wa pili niliamia shuleni hapo. Mimi ni msichana mpole na mwenye ushirikiano na wenzangu. Ninapenda dini na kulelewa kimaadili. Marafiki wawili tu Winnie na Angel walitosha kuifanya jamii yangu ndogo. Daima sikupenda company ya wavulana kwakuwa sikupenda vile baba alivyokuwa akimfanyia mama, hali iliyopelekea kuwepo kwa migogoro isiyoisha pale nyumbani. Pamoja na hayo yote baba yangu ambaye alikuwa mhasibu wa pale bandarini pamoja na mama yangu ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi ya Academy International school niliyosoma hapo awali walinipenda sana nikiwa kama mzaliwa wa pekee. Mazingira ya shule mpya ya Hans pope Academy yalikuwa mazuri niliyapenda. Ilifika jioni saa moja nikaingia chumba nilichopangiwa katika jengo lililoitwa white house nikalala fofofo. Saa kumi na mbili kamili ya alfajiri nilishtushwa na mlio wa kengele, nilishuka dekani kwangu na hapo ndipo niligundua kuwa sikuwa peke yangu. Kilikuwa ni chumba kidogo kizuri kilichopangiliwa vizuri, cha watu wawili. Kulikuwa na makabati mawili makubwa yaliyojigawa ukutani, meza ya kusomea na madirisha mapana ambayo yaliweza kuingiza mwanga na hewa safi. Katika kitanda cha chini alikuwepo msichana ambaye pamoja na kuwa alikuwa bado usingizini haikuniwia vigumu kujuwa kuwa huyu kiumbe aliyeko mbele yangu ni mzuri na mrembo wa kutosha kutwaa taji la miss Dunia. Ninajiamini kuwa mimi ni mzuri huyu msichana hakika alikuwa shani mbele ya macho yangu. Nilimsanifu kuanzia sura yake zuri, lips zake ambazo kwa juu zilichora kama umbo la kopa, rangi yake nyeupe ya kung’aa, ngozi yake laini, shape yake, hakika huyu msichana alikuwa ni mzuri sana. Nilimuangalia hadi macho yangu yalipotosheka kisha nikasimama tu nisijue nini cha kufanya nikageuka kwenda sehemu ambayo niliweka mabegi yangu. “wewe ni nani” sauti tamu ilipenya katika masikio yangu. Niligeuka kwa mshituko na kutazama pale sauti ilipotokea. Yule mrembo wa dunia alikuwa bado amelaa alikuwa akiniangalia macho yake makubwa na matamu yalitosha kunihakikishia kuwa huyu msichana aliumbwa kwa utulivu zaidi. “aaaaah aaaaa mimii” nilishikwa na kigugumizi sikujua nimjibu nini kile kitu kilinichanganya. “naitwa Catherine Catherine Kindamba” hatimaye niliweza kuongea na kujitambulisha. “Catherine unafanya nini hapa” aliongea huku akinyanyuka kutoka kitandani. “mimi ni mgeni nimefika hapa jana usiku, nimehamia” niliongea “mmmh” alinitazama kwa Dharau huku akibetua midomo yake. “Catherine karibu” “Ahsante” nilijibu “Sasa umeamka saizi unaenda wapi” aliniuliza. “aaaaah nimesikia kengele nataka nijue ni nini kinaendelea” “oooh sasa hivi ni mda wa jogging kama unapenda nenda ila sio lazima sana unaweza kubaki hapo ukijiandaa kwa ajili ya kuingia darasani, mi pia nipo siendi jogging.” “Aaaaah sawa hata mimi pia sipendelei jogging acha nipange vitu vyangu” niliongea. “ooooh unsoma Combination gani?” aliniuliza “niko ECA” nilijibu “ooooh” “wewe je unaitwa nani” nilimuuliza “naitwa Candy, niko HGE na ukipenda unaweza kuniita Queen Candy” alisema. Hakika nilijua kwamba huyu msichana aliyekuwa mbele yangu ni mtu mwenye Dharau sana hata hivyo sikuwa na papara dharau zake hazikuwa kitu kwangu lakini katika siku hizo za mwanzo ilikuwa ni hali ya kawaida tu kwakuwa nilihitaji kuijua shule vizuri sikumtilia maanani sana. <<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA >>>>>>>>>>>>>>>>>

at 11:12 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top