CHOMBEZO: NILAMBE HUMOHUMO By *🅱 professional love* SEHEMU YA PILI Unadhani nilifanikiwa kuinua domo langu na kumwambia japo ninakupenda tu? Thubutu! Kila nilipojitahidi kusema sasa nimwambie, ulimi ulikuwa mzito na pale ulipokuwa mwepesi maneno yalifanya mgomo!  Mgomo ulipojisahau yalitoka maneno mengine tofauti kabisa na ninakupenda!  Mpaka muda wa maongezi niliomuomba tuongee unakwisha na yeye kuniaga sikuwa nimemwambia lolote la maana. Nilibaki nimeduwaa kwa muda wakati wakati akiyoyoma na kunipa nafasi ya kuyafaidi maungo yake kwa nyuma.  Ghafla akageuka na kunitazama.  Macho yetu yakagongana.  Akatahayari, labda kwa vile alivyogundua kwamba alikuwa akitazamwa kifisifisi. Akageuza na kurudi kwa madaha akitumia hatua zilezile za miss Tanzania wa mwaka huu mpaka pale nilipokuwa nimesimama. Akaniangalia kwa muda kabla hajaniuliza kwa wasiwasi. ‘’Una nini Ibra?’’ “Sina kitu Shamsa!’’ ‘’Kweli?’’  “Haki ya Mungu vile!’’ “Au nimekukatili?! Bado hujamaliza kiu yako ya maongezi na mimi?” “Nilishamaliza kabisa. Amini nilitaka tu kujua kidogo kuhusu utendaji kazi wa Socket Bracker na vitambuzi vya Short, lakini jinsi ulivyonielekeza inatosha kabisa. Ahsante sana Da! Shamsa, Mungu akujaalie!” “Amina” Akajibu akitabasamu, wasiwasi ukiondoka pole pole. Dimples zake zikabonyea na kukitonesha kidonda changu tena. Mshituko mdogo nilioutoa ambao nilijitahidi kuuficha asiuone, ukawa umeurudisha wasiwasi wake kwangu tena.  ‘’Sikiliza Ibra!’’ akaniambia kama aliyechoshwa na kitu fulani.  “Mimi ni mwanadamu mwenye hisia timilifu kama wewe! Kama una lolote ambalo labda unahisi litahitaji msaada wangu we niambie tu. Acha kuteseka kipumbavu na njaa na wakati chakula unachodhani ni cha watu kipo karibu yako! Huwezi jua may be Mungu amepanga kukuokoa kwa chakula hicho.!”  Akazidi kunionyesha kwamba yuko tayari kwa lolote binti wa watu. Masikini laiti angelijua jinsi alivyozidi kuniweka mbali kwa kauli ile, asingeendelea. “Da’ Shamsa, msaada niliouhitaji umekwisha nisaidia, tena umenisaidia kiukamilifu. Nikiwa na tatizo jingine nitakwambia tu. Naomba nawe usichoke kupokea miito yangu!” ‘’Usijali!’’ akaniwahi kwa pupa. Ukapita ukimya mfupi tukiwa bado tumesimama hivyo hivyo tukiangaliana kwa zamu tena kwa wizi, mwishowe Shamsa akaniita tena. ‘’Ibra?” Sasa alinitulizia macho usoni moja kwa moja. ‘’Naam!’’ Nikaangalia pembeni, nikisugua vidole vyangu kama jinga vile ‘’Au… Au… Au unanipenda na unashindwa kuniambia?” “Mmmm, mmmm!” Nikatikisa kichwa kushoto na kulia kukataa. Shamsa akanipuuza na kuendelea “Kama umenipenda niambie tu. Niambie dia, niambie nijue! Hizi ni zama za ukweli na uwazi niambie usiogope!’’  Ooops! nikashusha pumzi ya faraja ndani kwa ndani, kwa namna ya mtu aliyeshusha mzigo mzito. Shamsa aliamua kuweka ile Msondo ngoma wanaita mambo hadharani. Ndiyo! Alikuwa amegusa mzizi, amegusa pale nilipotaka aguse.  Pengine ingelikuwa wewe ilikuwa ni kiasi cha kuongeza maneno machache tu ndio ni kweli ninakupenda, lakini kutokana na uzuri wako, uwezo wako kiakili na kifedha nimekuwa nikihofia kukwambia kwa kuwa nilijua utanikataa na hivyo nitaaibika lakini ninakupenda sana na ninataka uwe mpenzi wangu please please naomba upokee ombi langu na kunipokea mimi mwenyewe,  Lakini kwangu thubutu! Haikuwa hivyo nikajichekeshachekesha kiwazanga pale huku nikiona aibu kupindukia pengine kwa Shamsa kuligundua lile lililomo moyoni mwangu, nikaropoka.  “Hapana Da’ Shamsa! Wewe ni dada yangu, kwamwe siwezi kukutamkia maneno kama hayo, nikiwa na mengine nitakwambia si hili!’’ Nilizidi kujiweka mbali na kujikaanga kwa mafuta yangu mwenyewe.  Shamsa akaniangalia vizuri asiamini lile nililoongea, kutaka uhakika akaniuliza tena. ‘’Unasemaje?”  Nikarudia nilichokisema awali mithili ya muigizaji aliyeiva vyema baada ya kumeza scripts kikamilifu. Nikaona Shamsa akiishiwa nguvu kwa staili ileile ya kukata tamaa, alipogundua nimemgundua katika hilo, haraka akajirekebisha na kusema.  “Ok! Nafurahi kwa mawazo yako yaliyokwenda shule Ibra, laiti kama wanaume wote wangelikuwa kama wewe…! Ndio maana ninakupenda Ibra, wewe sio muhuni, hupendi mambo ya kipumbavu!  Angelikuwa mwanaume mwingine, tayari angeisha nitongoza zamani. Lakini wewe akah! Keep it up. Keep it real Ibra. Endelea na moyo wako huo huo siku moja nitakuja kukupa tuzo. Bye!’’ Akaondoka bila kunipa nafasi ya kujibu tena, nadhani maneno yale aliyasema kwa uchungu kiasi cha machozi kumlenga na nilihisi aliondoka upesi akihofia kulia mbele yangu! Kulia? Nikajiuliza kwa mshangao, kwa ajili yangu! Maana yake nini? Sikupata jibu! Niliendelea kumwangalia mpaka alipotoweka kwenye upeo wa macho yangu. Ndio kwanza nikapambazukiwa na ukweli wa kile nilicho kifanya.  “Shit!” Nikaguta ghafla nikijipiga makonde ya nguvu kichwani. “Nimefanya nini sasa? Ama kweli mimi ndio mjinga wa wajinga No! Mwenyekiti wa wajinga. Mtoto tayari alishakaa katika laini namba moja, mie nimemrudisha line namba ziro! Tena ziro pointi ziro tano! Kamwe siistahili kusamehewa!” Nikajiambia nikizidi kujipiga makonde kichwani.  ‘’We vipi Ibra?’’ sauti niliyoifahamu sana ikanishtua kutoka nyuma yangu. Nikageuka haraka huku nikitahayari mithili ya mtu aliyefumaniwa, ni kweli rafiki yangu Yusuph alikuwa amenifumania, nikijipiga makonde kichwani kama chizi. “Vipi nini?” Nikasaili kipumbavu nikizidi kuona hatia na kuongeza  “Mbona mie mambo yangu yako safi?  ‘’Unahakika ni safi?’’ Akimu akanitulizia macho asiyapepese walau kiduchu.  Nikazidi kuona soo.  “Sikiliza Ibra, mimi ni rafiki yako wa damu, rafiki wa dhati rafiki wa kufa na kuzikana. Unaponificha jambo ni kama unajificha mwenyewe!” ‘’Hakuna Akimu! Hakuna kabisa. Nothing!” ‘’Kweli?’’ ‘’Kweli tupu! ‘’Sasa mbona unajipigapiga makonde kichwani huku ukikita miguu chini utafikiri umepoteza kitu fulani kama sio kufeli mitihani!” Eh! Hii kali! Nikawaza. Kumbe nilikuwa nikikitakita na miguu chini? Sekunde kadhaa zikapita huku Akimu akiniangalia na mimi nikiangalia chini kwa tahayari wakati huo kichwa changu kikizunguka kutafuta jambo la kumuongopea Akimu, sikulipata. “Ukingali unajaribu kunificha Ibra! Any way haya ni maisha yako. Wewe ni mwamuzi wa mwisho kwayo. Ukiona ninastahili kuambiwa utaniambia, Ukiona sistahili usiniambie na sitolalamika kwaheri!”. Akimu akamaliza na kuondoka kwa haraka kama alivyoondoka Shamsa. Nahisi nae aliongea kwa uchungu kwa kuwa tangu nianze masomo yeye ndio amekuwa rafiki na mwandani wangu mkuu.  Sasa nitawakorofisha watu wangapi jamani? Kwa kule tu kukataa kwangu kusema ukweli! Kwa Shamsa naweza kustahimili kuishi bila ya kuwa na mahusiano nae mazuri. Lakini Akimu?! Itanichukua muda gani kutengeneza urafiki mzuri na bora kama yeye?  Liwalo na liwe! Nikaanza kumkimbilia huku nikimwita, alikuwa amefika mbali kidogo, aliposikia akasimama na kugeuka . ‘’Unasemaje?” Akaniuliza nilipo mfikia. “I am so sorry kaka!’’ ‘’Samahani ya nini Ibra?! Si umesema hakuna kitu?” ‘’Nilikuwa wrong Akimu, nina tatizo! Tena tatizo kubwa!’’ ‘’Tatizo la mapenzi sio? Linamuhusu Shamsa bila shaka!’’ Nikasikia moyo unafanya pah! Amejuaje? Nikatikisa kichwa chini na juu kuafiki, ’’Nilijua tu lipo tatizo, nikashangaa na kuchukia ulipotaka kunificha. Ulipotoka bwenini nilikuwa na shida na wewe, nikawa nimekufuatilia ili nikujuze shida yangu. Nikakukuta na Shamsa, na kutokea hapo nimeshuhudia kila lililojiri baina yenu ingawa sikuweza kusikia maneno mliyokuwa mkizungumza!’’ Unaona? Siku nyingine mtu unaweza kufungwa hivi hivi. Kumbe amenichora A to Z halafu mie nakomaa tu hakuna kitu, hakuna kitu!  “Haya niambie ni tatizo gani?  Nikabakia nikiumauma meno kwa muda nisijue nianzie wapi. Maana haya matatizo mengine wewe unaona tatizo, hali mwenzako haoni kama ni tatizo. Nikaamua kumweleza ukweli. ‘’Tatizo ni Shamsa Akimu, Nampenda sana, tena sana !’’ “Amekukataa? kwa kadiri nilivyoona na ninavyohisi kama sio kufahamu Shamsa nae anakupenda kupita kiasi, kwani bado haujamwambia kama unampenda?” ‘’Bado!’’ ‘’Sasa tatizo liko wapi si ungemwita ukamwambia?! We mwambie tu Shamsa zungu yule hana tatizo!’’  “Tatizo lipo hapo kwenye kumwambia!” “Unaogopa?” ‘’Naweza kusema hivyo, maana naweza kujipanga kwa sasa namwambia nikikutana nae tu nageuka zezeta kama sio bwege. Kujiamini kote kunatoweka na maneno yanakimbia kabisa!’’ Akimu akatabasamu. ‘’Wakati mwingine unapaswa kujiamini Ibra!’’ “Tatizo ni kwamba…” Nikamkumbusha kwa karaha, ’’Sio kwamba sijiamini, najiamini sana lakini ninapofika mbele yake tu ndipo hali hii inapo jitokeza! Unaweza kudhani Shamsa anadawa vile!’’ “Huko unakoenda mbali Shamsa hana dawa. Tatizo liko kwako tu tatizo ni kwamba hujiamini! Hilo tu. Lakini sio lazima umtongoze kwa kuongea nae, ziko njia nyingi za kufikisha ujumbe wako,  Nikazibuka masikio. “Kama zipi?” “Unaweza kumuandikia barua, ukamnunulia kadi za mapenzi, ukamtumia mauwaridi mazuri yenye ujumbe mzuri na hata kumwandikia sms za mapenzi na ujumbe ukafika, akaelewa na mkawa wapenzi. Shamsa hana ubavu wa kukukataa wewe Yule, sure am telling you!! ‘’Kumbe?!” “Eeh!’’ Akakubali kwa msisitizo. Moyo wangu ukazizima kwa furaha nikajua naweza kutumia moja wapo kati ya njia hizo, mambo yakajipa na nikaweza kummiliki Shamsa Nuhu moja kwa moja.  ‘’Ila’’ Akimu akanizindua tena, “Itakubidi usubiri muhula huu wa mitihani uishe ili usichanganye mapenzi na masomo. Ukianza wewe kuvichanganya vyenyewe vitamalizia, na hupata zaidi ya hasara!’’ ‘’Nitasubiri!” Nikamwambia “Good!’’ Akashangilia baadae akaniambia lile alilokuwa akinitafutia, nami nikampa ushauri alioutaka. Mpaka tunaagana tabasamu lilikuwa bado limeupamba uso wake.

at 8:52 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top