CHOMBEZO: NILAMBE HUMO HUMO SEHEMU YA nane “Mimi ni miongoni mwa watu wachache sana wasiopenda kuwakwaza wenzao hasa wewe! Kuendelea kunilaumu kana kwamba nimeua bila kunieleza nilililolifanya, hunitendei haki Shamsa! Unaniweka katika kimuhemuhe ambacho kinanifanya nishindwe kujua nastahili kuwemo katika fungu gani kati ya wastaarabu na washenzi. Tafadhali niambie, niambie tu usihofu!’’ Shamsa akashusha pumzi na kuzivuta tena akauliza “Kwa hiyo hujafanya kitu?’’ ‘’Kitu gani? kwa kadiri ninavyokumbuka na kufahamu, sijafanya lolote la kumchukiza mtu yeyote! Na kama nilivyokwambia sipendi kumkwaza mtu!’’ ‘’Kweli!?’’ ‘’Kabisa!’’ ‘’Sasa kule Chuoni ulikuwa unalia nini?” Akili ikazibuka. Macho yakazibuka pia na fahamu kufunguka. Masikio, moyo na hata vinyweleo vya mwili ambavyo wakati huu vilikuwa vikikiruhusu kijasho chembamba kupenya na kuteleza juu ya paji la uso wangu, juu ya mashavu, juu ya mikono, juu ya kila mahali, sasa nikaelewa! Kwamba Shamsa alikuwa akizungumzia kufeli kwangu. ‘’Machozi yakafurika upya katika macho yangu. Shamsa alikuwa amenitonesha donda. Amegusa mahali ambapo sikutaka paguswe. Halafu kilio kidogo kikanianguka. Nilijitahidi kukizuia mpaka nikafaulu. ‘’Mapenzi Shamsa!” Nikasema huku nikipenga kamasi na kufuta machozi ‘’Mapenzi?!” Shamsa hakuamini!. “Yeah, Mapenzi! Naweza kusema ni mapenzi kwa kila hali ndiyo yaliyonifanya nifeli. Ukweli huu huniumiza zaidi. Huniumiza kwa vile ni ukweli unaoashiria upumbavu ulikithiri nilionao. Ni upumbavu tu maana ujinga unatibika, upumbavu hautibiki!” ‘’Bado sijakuelewa!’’ Alikuwa Shamsa kwa upole kabisa. ‘’Ni mapenzi Shamsa, nilikupenda sana mfano wa maua, ninakupenda hata sasa na nitaendelea kukupenda daima!’’ ‘’Kunipenda huko ndio kukakufanya ufeli?’’ Nikatikisa kichwa juu na chini kukubali. ‘’Si kweli!’’ Akasema kwa sauti thabiti nae akitikisa kichwa kushoto na kulia kukataa ‘’Si kweli hata kidogo!‘’ Akaongezea na kuendelea ‘’Nahisi unajaribu kunificha kama sio kunichezea shere. Naomba uniambie ukweli Ibra, ili niangalie namna ya kukusaidia tafadhali!’’ Sikujua nimwambie ukweli upi ‘’Mbona hata mie ninakupenda sana na nimefaulu vizuri tu? Mbona nilikuwa nikikufikiria na kutamani kuwa nawe mahala kama hapa nikila raha na kustarehe na wewe? Mimi nina nini niweze na wewe una nini ushindwe? Hapana niambie ukweli Ibra’’ Akatua. Furaha na bashasha vikiuvaa moyo akili na mwili wangu kwa zamu. Shamsa ananipenda! Ulikuwa ukweli ulionitoa machozi ya furaha, machozi ya upendo! Upendo wa dhati. Upendo uliotukuka! ‘’Shamsa’’ Nikaita nisiamini masikio yangu, “Ni kweli unanipenda?!’’ “Ni kweli Ibra, nakupenda sana! Nakupenda mno! Nakupenda kuliko unavyofikiria. VETA nzima watu wa Compass wanajua jinsi nilivyokufa na kuoza juu yako, Najua hata wewe unanipenda tu ila hujiamini na pengine unanipenda kupita kiasi, kiasi umekuwa kama unaniogopa uongo?’’ Akasuta! Ulikuwa ukweli, ukweli halisi. Ukweli Original kama alitegemea kunisuta kule kungenifanya nione haya kama sio aibu, alikosea! Badala yake nilitahayari na kuinamisha uso kwa fedheha, nilipoinua bado alikuwa akinitazama. Nikanong’ona. “I love you Shamsa!’’ ‘’I love you too Ibra!’’ Moyo wangu ukachanua kwa raha, akili ikapigwa dafrao na furaha huku mate ya uchu kama sio utamu yakijaa mdomoni. Nikamsogelea akanisogelea! Tukakutana katikati na kukumbatiana kwa nguvu na kudumu katika hali hiyo kwa muda. Hatimaye! Nikawaza kwa furaha nikingali nimekishikilia kifua chake Hatimaye Shamsa ameanguka mikononi mwangu, Ananipenda! Kwa mara ya kwanza nimepata hifadhi katika moyo wa mwanamke!’ Ilikuwa ajabu na kweli. Tulipoachiana matendo halisi ya mapenzi yalifuatia. Tulilishana, tukacheza na kuogelea pamoja. Tulipotosheka tukarudi mchangani tena. Shamsa akaniita kwa upendo uliotukuka. Sauti yake ilikuwa tamu vibaya sana “Ibra mpenzi?” ‘’Naam!’’ ‘’Bado hujanishibisha dear!’’ ‘’Lakini biskuti, Chocolate na Ice cream hazishibishi!’’ Akatabasamu, vishimo vikatokea hapa na pale katika mashavu yake na kidevuni. “Unanielewa vizuri sana Ibra! Ni kuhusu kufelishwa na mapenzi! Hebu niambie ukweli!’’ ‘’Ni ukweli mpenzi!’’ Nikamwambia, kabla sijaanza kumsimulia safari ya maisha yangu toka Shule ya Msingi, Sekondary, hadi pale VETA. Nikamwambia jinsi nilivyokuwa nampenda na namna nilivyoshindwa kumkabili licha ya yeye kunionyesha dalili za waziwazi. Nikamwambia pia namna nilivyopateua uwanja wa fisi kama mahala mbadala, ushauri niliopewa na Akimu baadae ambapo nilijikuta nikianguka tena katika ngoma za kizaramo. Nikashindwa kujisomea, kufuatilia masomo na kuendekeza ngono, mpaka ninamaliza kusimulia, Shamsa alikuwa bado ana hamu ya kunisikiliza. “Huo ndio mkasa wangu Shamsa! Unadhani kitu gani naweza kusema kimenifelisha kama sio mapenzi?” “Duh! Pole sana Ibra una bonge la mkasa! Mkasa ambao umeusisimua moyo wangu katika namna inayonifanya nikuogope! Nikuulize swali jingine?” ‘’Uliza tu laaziz!” ‘’Mbona siku ile nilipokuuliza kama unanipenda ulikataa kata kata?” Nikatabasamu, “Mbona hilo umeshalijibu katika maelezo yako? Shamsa mpenzi nilikuwa sijiamini, nilikuwa nakuogopa! Akili zako, uzuri na uwezo wako kifedha vilinifanya niufyate, nikawa nakufa kiofisa tai shingoni!” Akacheka. Nami nikacheka. Ikawa raha juu ya raha ‘’Siku nyingine usiogope ukubwa wa samaki! Uliza bei!’’ Akasema kati kati ya kicheko, tukacheka zaidi. ‘’Lakini kufeli kwako hakutokani na mapenzi! Naweza kusema hivyo!’’ akaniambia baadae kwa uhakika kabisa. ‘’Kumbe kunatokana na nini na au nikuiteje?” ‘’Kunatokana na tamaa kali ya ngono na niite tu umalaya, kwa sababu hata ngoma unazozizingizia huzifuati zenyewe! Hii ni kwa vile hujui kucheza kabisa, unayo ifuata ni ile mijimama na kile kipindi muhimu cha kuzima ngoma uongo?” Nikashindwa kumjibu. “Mapenzi ya kweli ni zaidi ya ngono Ibra! Unadhani ni kwanini mimi imeniuma wewe kufeli? Kwanini nilikuja kukufariji katika bweni lenu? kwanini nimekuleta huku?! Sababu ni moja tu Ibra wangu. MAPENZI! Ni mapenzi ya dhati niliyo nayo kwako, hilo tu!” Akahitimisha. Alikuwa sahihi. Tuliendelea kufurahi na kula maisha pale ufukweni hata msiba wote wa kufeli ukaondoka. Nilichogundua tu ni kuwa Shamsa alikuwa mwangalifu sana wakati huu. Hakujiachia sana kama alivyokuwa akijiachia wakati ule kabla sijampa full story yangu. Jioni tuliondoka na kuelekea mabwenini. Siku ya pili yake tulikuwa kwenye hoteli moja ya kitalii huko baada ya maongezi yetu ya kawaida ndipo alipo nitwanga swali.. ‘’Sasa Ibra Chuo ndio tumemaliza, baada ya kutunukiwa shahada zetu yatupasa kuondoka. Mwenzangu una mipango gani? Mie mwenzio Mzee ameniunganishia Tanesco na mwakani nitaajiriwa!’’ Swali zito. Nikachoka kabisa, dakika zikayoyoma pasipo kujibu “Sikiliza Ibra, kufeli masomo sio kufeli maisha. Kwa hiyo usifikirie sana kuhusu hilo, mimi nina ushauri mzuri kwako!’’ Akatua na kunitazama. ‘’Enhe upi?’’ ‘’Kwanza nataka mimi na wewe tuoane unasemaje?” Sura yangu ikachanua mithili ya maua katika jua la asubuhi. Nikamwambia, “Sina kipingamizi Shamsa nakupenda mno!” Naye akatabasamu kufuatia kauli yangu hii. Akasema. ‘’Basi kama hivyo ndivyo, huna budi kujifunza udereva haraka sana, ili nimwambie mzee akuajiri katika kampuni yake. Nitamshauri akulipe mshahara mzuri sana unaonaje?” ‘’Nitashukuru kupita kiasi!” Nikasema haraka nikiwaza hata kama Lady Jay dee ataniita mwanaume kama binti na Bushoke kuniita Mume bwege shauri yao! Nitafanyaje hali nimesha ulowanya?” Nikakubali. Lakini kabla haya hayajafanyika inakubidi uanze taratibu za uchumba na kwa hili hatuna budi kwenda kupima afya zetu kwanza ili ulete barua ya posa wakati huo huo ukianza Driving School! Sawa mpenzi?!” ***HE MAMBO YA KUPIMA TENAAA…….IBRA ANALOOOO!!!!

at 3:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top