SIMULIZI YA KUSISIMUA... Ndoa Yangu Inanitesa part 7 Nilitulia kidogo nikaendelea, “Moyo wangu unasononeka sana. Laiti ningelijua nisingeoa, maisha gani haya yananitesa kiasi hiki?”Nilijikuta nikilia ovyo kama toto jinga lenye kudeka ovyo.Kilio changu lilikuwa rohoni.na aliyejua alikuwa muumba pekee.Getruda alikuja kunibembeleza kwa hofu kwamba ningechukua maamuzi ya kijinga tena. Aliniandalia chakula mezani.Tulisali kisha tukala . Saa nane mchana baada ya kupata mlo wa mchana nilimuaga Getruda nikiwa naelekea ofisini kumueleza Mzee Jophu yaliyosibu katika unyumba wangu. Lakini cha kushangaza Mzee Jophu baada ya kumueleza kila kitu,nilimuona uso ukiwa umejawa furaha badala ya kunionea huruma. Hali hiyo aliisubiri kwa hamu hata hivyo alishanga kuona mimi kuchelewa kumuelezea shida zangu toka mwanzoni.Alijifanya kama hataki kuchangia mapenzi ilinimuone mtu mwema, “Sasa Jophu unakataa nini na wakati nimekuambia mke wangu hajaguswa” “Inamaana siku zote hizo mlikuwa mkilala tu?” “Ndio”nilimjibu nikahisi machozi yakinilengalenga, hata hivyo nilijikaza kiume. “Matatizo haya yalikupata muda gani?” “Siku ya kwanza toka nifunge ndoa na mke wangu” “Usinitanie Sweedy. Ulijaribu kwenda hospitali?” “Ndio.Nilichunguzwa kwa makini.Daktari alinieleza kwamba nilipigwa sindano yenye sumu.Nilikataa kwani sijawahi kupigwa sindando yeyote toka uliponiajiri. Na sasa ni miaka karibu ishirini na tano. Nakumbuka sindano ya mwisho nilichomwa nikiwa na chuoni. Na siku nyingine niile nilipokuja kutolewa damu” “Kutolewa damu si kupigwa sindano labda una matatizo mengine kiafya.Vipi kuhusu chango?” “Sina chango,mzee”Nilimjibu nikiwa nimetizama chini. “Mzee, naomba unisaidie kuokoa jahazi la ndoa yangu”Nilimweleza nikimpigia magoti.Sikuwa najua kwamba mzee Jophu ndiye aliyetuma watu wanipige sindano ya kuua uume wangu.Wakidai wana nitoa damu ilinikapimwe virusi vya ukimwi.Hata hivyo ilikuwa kazi kumgundua mbaya wangu,jinsi alivyoonyesha kutokutaka kuchukua jukumu la kumridhisha mke wangu. “Mkeo atakubali kwenda kupima damu zetu?” “Sina uhakika kama atakubali au laa. Ni vizuri kimpigie simu”Nilitoa simu yangu ya kiganjani na kubonyeza namba za Getruda, mke wangu. “Hallo, mpenzi”alipokea tu baada ya kuona namba zangu juu ya kioo cha simu yake. “Oooo!, vipi upo salama.” “Ndio. Sijui wewe” “Shwari kabisa.Mmmm…utakubali kupima Virusi vya ukimwi?” “Tangu lini kigori akawa na Ukimwi?” “Sijambo la ajabu kwani ukimwi unaambukizwa kwa kujamiana tu?”Getruda aitafakari akajiona kweli alibugi sana. “Sawa, nimekubali kupima afya kwa manufaa yetu sote” “Ok, jiandae nakuja sasa hivi nyumbani” “Ok, bye bye”Alinaga na kukatasimu. “Nilimtizama mzee Jophu na kumwambia, “Amekubali kupima” Kwambali niliona tabasamu la mzee Jophu lililonifanya nione meno yake ya rangi rangi, nafikiri kutokana kunywa maji ya Arusha tokea utotoni mwake. “Sasa Sweedy”Alitulia kidogo na kukohoa kinafiki,nilimtizama kwa makini niwezekujua alichotaka kusema,aliendelea “Kwa vile wewe ni rafiki yangu sina budi kukusaidia.Ila nakuomba usimweleze mtu yeyote ‘Especial my wife’,Umenielewa. Narudia tena naomba iwe siri moyoni mwetu” “Sawa, mzee.Usihofu kitu”nilimjibu kwa upole kabisa. Mzee Jophu aliongea moyoni akiwa amejawa furaha kubwa mno, “Kile nilichokitaka kimekamilika. Sasa kazi kwangu kurina asali nitakavyo”” Mzee Jophu kunajambo la muhimu nimelikumbuka. Nilimdanganya kuwa nilimwagikiwa na tindikali. Akikuuleza mueleze ni kweli”Nilitulia kidogo, ingawa alijaribu kuficha furaha niliiona , Nikatulia kama niliyewaza kitu ,Machozi yakaniwakia pale nilipokumbuka nguvu zangu nilipokuwa Nchini Thailand “Lakini boss na shindwa kujua ugonjwa huu niliupata wapi na nani aliyeniletea” “Usijali muombe mungu akuondolee. Hatamimi ninafanya tu, kwa vile wewe rafiki yangu wa damdam, lakini kwa maulana ni dhambi kuzini nje ya ndoa,” Mzee Jophu aliongea ilinimuone mtu wa busara kama alivyoonekana kuwa ni mtu wa busara kumbe ni muungwana wa ngozi tu, lakini rohoni ni muuwaji. Maneno yake ilikuwa vigumu kumgundua kuwa yeye ndiye mbaya wangu, aliyeamua kunitesa iliamfanye mke wangu wake. Mazungumzo yetu ya ofisi yalikuwa ya muda mrefu. Tulipo maliza jioni iliwadia tuliongozana na Mzee Jophu moja kwa moja hadi nyumbani kwangu. “Lakini Sweedy kama ameoa mke mwenye uso wa mbuzi mimi sitamkubali atakuwa wako mwenyewe” “ Hakika mke wangu utamkubali. Amekamilika kila idara. Utamsahau mama Jacob nakuambia” Nilimueleza. “Yote tisa, kumi tutaona. Nitaamini unajua kuchagua,” “Lako jicho, yanini ni kusifie?” Niliposema, nilitamani Mzee Jophu ardhike na ombo la Getruda, lakini kitu kilichoniuma zaidi ni jinsi gani ningemuunganisha mwanaume mwenzangu na mke wangu niliyemlipia mahari. “Inawezekana huyu mshenzi akamkataa mke wangu. Midomo yake imejaa dharau”nilijisemea kimoyomoyo huku nikibonyeza kitufe cha geti. Getruda Kimario alifika getini na kufungua, mtu wa kwanza kuingia akiwa Mzee Jophu.Shauku yake haikufichika ,alimtupia Getruda jicho la lilo jaa ubembe.Ni hapo ndipo nilipohisi Mzee Jophu kumkubali mke wangu. Alikuwa na shauku ya kumbusu Getruda, nikipindi kirefu toka wapoteane pale ofisini kwake, na Getruda alimkumbuka kuwa yule alikuwa yule aliyempa mama yake mzazi shilingi laki tano za kitanzania iliamuowe yeye. Walitupiana macho yaliyojaa furaha macho ya matamanio ya Getruda yalizidi kumchanganya Jophu. Aliyekuwa na shauku kuupitisha usiku mwanana na binti aliyemlipia shilingi laki tano. Aliamini alikuwa na haki yakujivinjari jasho lake. Mwanzoni nilihisi hawakumbukani,kumbe kumbukumbu alikuwa nazo na alishuhudia mama yake akipokea hizo hela. Ulifikia muda muafaka wakuweka mambo hadharani ili nitatuliwe shidayangu. Kabla sijazungumza chochote nilipandisha pumzi na kushusha kwa nguvu kama mtu aliyechoka na pilika pilika za kutwa nzima ,”ooooooophhhh!”Kisha nikasema kwa sauti ya chini kama mgonjwa,ni kweli niliyotaka kusema yaliniuma sana. “ Nafikiri mke wangu nilisha wahi kukutajia jina la rafiki yangu kipenzi. Ila ni vema nikalirudia leo ukiwa una muona . Aliye kaa hapa mbele ndiye Mzee Jophu. Sio Mzee kweli ni kwaajili ya mali zake ndio maana watu wanampa jina la heshima ya mzee. Huyu ndiye mwa ndani wangu ukimuona yeye ndio umeniona mimi. Shida zake ni zangu, zangu ni zake,”Nilikohoa kidogo ni kumgeukia mzee Jophu. Kijasho kilizidi kuchuruzika kwa kasi kuliko mwanzoni, nilihisi midomo kufa ganzi na kuwa mizito, nilijikuta sauti ikipotea ghafla pale nilipofikiria kumuachia mzee Jophu mke wangu.Tena hajawahi kuguswa na mtu yeyeto maishani. Kwa kweli inatia uchungu sana heri ningekuwa nimezaliwa na udhaifu huo kuliko kunikuta nikiwa mtu mzima. “Mzee Jophu huyu ni mke wangu, kwa upande mwingine naweza kusema ni mkeo. Nina matatizo ya,,,,,,” hasira kali iliniingia moyo nikashindwa kumaliza, nilijikuta nikiangua kilio. Moyo uliuma sana. “Kweli kweli na muachia Jophu kigoli wangu?”Nilimtizama Getruda kama vile nikimuaga, sikuweza kukwepa jambo hilo tena.Kwa kuwa lilishakuwa kero katika familia yetu. “Naomba uwe karibu na mke wangu, kama ulivyo karibu na mkeo, lakini,,,,,,,,,,naomba unifichie siri yangu, heshima iwepo msije mkachukulia muda huo kunidharau, nami sikupenda kuwa hivi,,,”Nilikokoteza maneno kwa ujasiri . “Ok, nashukuru kumfahamu mkeo, na nitaendelea kumfahamu vizuri, zaidi kadri siku zinavyo zidi kwenda” Mzee Jophu aliongea huku akinyanyuka kuelekea alipo Getruda. Alinishika mkono na kuunyanyua usawa wa midomo yake, hakuchelewa nilisikia sauti ya busu kwenye kiganja cha mke wake wangu. Busu hilo lilimchanganya mke wangu na kujikuta mwili ukimsisimka, vinyweleo na nywele zilisimama kwa shoti ya busu la mzee Jophu.Nilibaki nimeduwa, midomo ikiwa wazi kama sekunde kadhaa.Bila hofu wala haya, walijikuta wamekumbatiana na Mzee Jophu alisogeza midomo yake karibu kabisa na sikio akimnong’oneza. “Kweli kwenye miti hakuna wajenzi, nitakutunza kama mlima Kilimanajaro unavyotunza Seluji yake, nitakupa chochote unachotaka, ikiwezekana nitakuoa kabisa, nakupenda siko tayari kukuacha, naamini unanipenda” Sauti ya Mzee Jophu ilizidi kumtekenya Getruda, alijikuta akitikisa kichwa ishara ya kukubali.Alishindwa kujizuia kutoa sauti za kizizima, taratibu kwa jinsi maneno ya Jophu yaliyokuwa yakipenyeza sikioni angali yana uvuguvugu, kwa wimbi lenye joto nadhifu.Mzee Jophu alimwachia na kuketi karibu nae. Mambo yote niliyaona. Kwa jinsi roho ilivyoguguna niliondoka sehemu ile na kuingi chumbani, nilimpenda sana mke wangu, sikupenda awe mke wa shirika wala sikupenda kuona akishikwa shikwa na mtu zaidi yangu. Japo nilikuwa na wivu lakini nilishindwa kwa sababu nilipata udhaifu, ikanilazimu kuvumilia na kuhamisha macho, na kutizama pembeni.Pia hilo lilinishinda nikaamua kujiondokea kiunyonge kama kifaranga asiye na mama. Kuondoka kwangu, ulikuwa mwanya wa Jophu na mke wangu kupanga mambo yao. By brayton starpoz

at 9:13 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top