Nazungumza na wale WANAWAKE ambao huruhusu akili yao kuchotwa na TAMAA ZA DUNIA! Vile ambavyo MUNGU amemuumba mwanamke ni wazi kabisa yeye ndiye aliye na jukumu la kulea watoto lakini wako wanawake wao wanajiita wa kisasa HUZITELEKEZA FAMILIA ZAO NA KUANGUKIA KATIKA ANASA... Mwanamke mwenye akili kamwe hawezi kumuacha mtoto wake na kuambatana na DUNIA laa kama mtoto huyo amejitambuwa Yaani kufikia miaka 18, Vile ambavyo umeweza kuikimbia FAMILIA yako ndivyo ambavyo laana itakuwa juu yako, Unamuachiaje watoto wako mwanaume hata kama ni baba yao? Mwanaume kuitunza familia ni andiko lakini Swala la kulea ni la mama, ndo maana hata Biblia imesema MWANA MPUMBAVU NI MZIGO WA MAMAYE... Hata wahenga nao walisema ASIYE FUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA ULIMWENGU yote haya huyajui? Nikiri kabisa NDOA iko na changamoto lakini hupashwi kuwaza UBAYA wa baba yao bali inua huruma juu ya uzao wa tumbo lako laa kama uliwanunua watoto hao na hukuwabebea mimba miezi 9, ukajifungua kwa uchungu halafu unasahau mateso yale ila unayatazama mateso yahusuyo NDOA? Mungu akusaidie urejeshe akili yako maana kwa akili hiyo nikukosee adabu WEWE NI KILAZA! MITHALI 14:1 Biblia inasema; "Kila mwanamke aliye na HEKIMA hujenga nyumba yake, Bali aliye MPUMBAVU huibomoa kwa mikono yake mwenyewe" Mungu awabariki wanawake wote wanaosimamia nafasi yao na heshima kwao kuitwa mama, Kuujuwa umuhimu wako kama mwanamke ni rehema maana wapo wasoijuwa heshima hiyo.

at 6:06 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top