Home → ushauri
→ Kuna aina nyingi ya masikitiko lakini sikitiko lenye kuubomoa moyo na kuusababishia kutokaa sawa Sawa ni sikitiko la mahusiano pale unapoachana na mtu ambaye bado unampenda... Inauma sana ila huwa inatokea maana hayo ndo maisha, Kuachana kuna nguvu ya ajabu ambayo huleta maumivu makali moyoni hasa ukikumbuka zile siku zilivyokuwa zenye Furaha na Amani! Upendo siku zote hautoshi na Ukiwa kwenye upendo haimaanishi utakuwa na furaha siku zote maana Mapenzi ni ya wawili na kila mmoja ana makuzi yake hivyo ni vyema kuzikubari nyakati pindi zinapokujia, Unaweza kuendelea kumpenda mtu hata kama anakuumiza japo moyoni huwezi kuwa kama ulivyokuwa kipindi hajaanza fujo zake... Kwa hiyo kwa sehemu fulani unaweza kumuacha aende, Muda gani ni sahihi? Huwezi kujuwa maana dhoruba za MAPENZI huja pasipo taarifa, Hilo nalo ni sikitiko jingine Kwani kuishi katika penzi Ukiwa na wasiwasi wa kutojuwa usalama wa penzi lako ni shida, Siku zote UPENDO hauhesabu lakini ukiishi katika mapenzi bila kuhesabu iko siku utatakiwa kuhesabu na ushindwe kuijuwa hesabu na hapo ndipo utashindwa mtihani ulio mbele yako.
Team Brayton Offical Love
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: