Home → ushauri
→ Jinsia ni nini?
Jinsia ni mahusiano ya kijamii na kiutamaduni yanayozingatia mgawanyo wa majukumu kwa kuangalia jinsi (Ke na Me).
Jinsia inachangia kuwepo kwa tofauti kati ya mwanaume na mwanamke katika mgawanyo wa majukumu kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.
Kwa njia hii majukumu, kazi, matarajio, haki, vikwazo, nafasi, fursa pamoja na huduma mbalimbali zinatambuliwa kwa kutegemea jinsi ya mtu.
Uchambuzi wa Kijinsia ni nini?
Uchambuzi wa kijinsia ni uchambuzi unaohusisha aina na mbinu mbalimbali zinazotumika katika kufuatilia na kuelewa tofauti za kimaisha kati ya wanaume na wanawake, wavulana na wasichana, na mahusiano kati yao yanayojumuisha upatikanaji wa fursa na rasilimali, majukumu yao, pamoja na changamoto zinazowakabili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: