Home → Love sms
→ *⚱YAJUE ANACHOTAKA MUMEO / MKEO⚱*
_Wakati mwengine watu walioko kwenye ndoa hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu na waume zao na akatokea jamaa na kumhakikishia kumpatia kila anachotaka, wanakubali mara moja bila kujua kwamba wao ni wake za watu ama wapenzi wa watu na kujikuta wanajenga mazoea🎈🎈🎈_ .
_Utakuta wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini bado wanafanya usaliti. Hii ni kutokans na tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta wanatafuta wanaume wengine huku wakidai kuwa, wanatafuta ladha tofauti💙💚🧡_ .
_Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia, unaweza kumkuta ana mwanamke bomba tu mwenye kila kigezo, lakini bado anakuwa na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje💕💕💕_ .
_Kuna kila sababu ya kila mmoja kujitambua na kuitambua thamani yake. Wewe kama ni mke wa mtu, ridhika na hali aliyonayo mumeo, fedha isikufanye ukapoteza utu wako, ukamsaliti mtu ambaye ulimuahidi kumtunzia penzi lake. Vivyo hivyo kwa mwanaume, ridhika na penzi unalolipata kutoka kwa mkeo/mpenzi wako. Mademu wa nje hawana maana kwako zaidi ya kukuingiza katika matatizo unayoweza kuyaepuka💖💖💖_ .
_Kusalitiana kwa wanandoa kumekuwa kukitokea kutokana na kuwepo kwa mazingira fulani ambayo baadhi yao wamekuwa wakishindwa kujizuia nayo hivyo kujikuta wanatoka nje ya ndoa zaidi_ 🖤🖤🖤.
_Ila sasa nalazimika kwa nguvu zote kuwashauri wale walio katika uhusiano wa kimapenzi, namaanisha wapenzi wa kawaida, wachumba ama wanandoa, tusiwe na tamaa za kijinga na kufikia hatua ya kuwasaliti wenza wetu🦜🦜🦜_ .
_Hivi unajisikiaje unapomvulia nguo mtu ambaye wala hana ‘future’ na wewe eti kwa sababu ya fedha? Hivi na wewe ukifanyiwa hivyo na mwenza wako utajisikiaje? Elewa maumivu utakayoyapata pale utakaposikia wenza wako ana uhusiano na fulani ni hayo hayo atakayoyasikia mwenza wako🌹🌹🌹_ .
_Kuwa muaminifu, ridhika na unachokipata kwake, muoneshe mapenzi ya dhati naye atafanya vivyo hivyo na kujikuta mnayafurahia maisha yenu⛺⛺⛺_ .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: