Home → Love sms
→ *πΉπΉ MKE MWENYE SIFA HIZI NI KITULIZO CHA MUME πΉπΉ*
π½π₯π₯π
Haiba na urembo wa mke unazidi pale mwanamke anapokuwa na maneno machache mdomoni
Hasemi ila mazuri
Hana kelele
Hana lawama nyingi Mume akipandisha sauti hashindani nae
Mpole ila si mjinga
π½π₯
Thamani ya mwanamke huongezeka zaidi akiwa mchamungu
Mwanamke muumini anapendeza zaidi kwa mumewe
Mume anamuonea haya sana mwanamke muumini
Anasema nae kwa heshima
Mwanamke muumini ana subira
Mdomo wake umejaa shukran
Anadhibiti hasira zake
Anazuia mdomo wake
Hajivuni
Anajishusha
π½π₯π
Mwanamke muumini hawi kero kwa jirani zake
Ana subira juu yao
Haanzishi magomvi
Haishindani nao kwenye shari
Hajifakharishi kwao
π½π₯π
Mwanamke muumini mdomo wake umejaa dhikir, kusema yalo sawa.
Siyo kudumu na nyimbo(mipasho) au mafumbo na kejeli.
π½π₯π
Mwanamke muumini humkuti kwenye baraza za umbea
Hakai barazani na kumteta kila anaepita njia
Hadhuruli au kupenda safari ziso na faida.
Hutulia nyumbani
Hatoki ila kwa dharula
Na hatoki ila kwa ridhaa ya mumewe
π½π₯π
Mwanamke muumini hamsugui roho mumewe
Hatishii kuondoka
Hadai talaka bila sababu za kisheria
Humtoa hofu mumewe kwa kuthibitisha penzi lake kwa mumewe (kwa maneno na vitendo)
π½π₯π
Mwanamke muumini anaelewa mtoaji rizki ni Allah
Basi si mchoyo nyumbani kwake
Mkarimu kwa jamaa na wageni wote.
Anaheshimu watu
Anajiheshimu pia.
π½π₯π
Mwanamke muumini ni liwazo njema kwa mumewe.
Mume akihuzunika humfariji
Akikasirika humpoza
Ni mwanamke ambaye mume akimtazama anafurahi
Ni mwanamke mwenye kutosheka na hali yake.
Hana tamaa
Khofu yake iko kwa Allah.
π½π½π₯π₯π₯π₯π½π½
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: