Home → Love sms
→ MWANAMKE UBUNIFU
SIVYO UTAACHWA KWENYE MATAA
CHUKUA UTUNDU HUU UKAKUSAIDIE
๐๐✊๐๐✊๐๐✊๐✊๐✊๐
leo nakuongezea utundu mwanakwetu kwani ukisikia mwanamke ni kitulizo cha mume mithali ya kiu kwa maji baridi ya mtungini hivyo kumlea mume asikwapuliwe na mapaka shume si lele mama yataka ufanye kazi khasa kazi ya malezi maana hapo ndipo tofauti ya wanawake inapotofautishwa na hiyo ndo hulka
kwanza bi mdada mume uandaliwa tangu anapoamka kitandani kamwe maji ya kukoga mume hayanyooshewi kwa kidole cha shahada ati maji hayo humo kwenye ndoo nenda kaoge khaa we wapi? maji ya kukoga mume uyaandae mke tena uyaandae kulingana na hali ya hewa wakati huo ipoje ni joto au baridi.. maji yatie viungo vyake bibi, maji yanaungwa bibi weeee yaunge kwa ASUMINI,VILUA,MAWARDI,VILANGILANGI,KARAFUU, maji yanukie sio maji wakoga huku wabana pua uvundo si uvundo maji yananuka moshi khaa! bibi taulo la mume na lako liwe safi sio taulo mpaka rangi haijulikani, taulo mpaka wiki halijafuliwa hahahahhahaa utakimbiwa bibi we.
waungwana mke na mume uoga pamoja huko bafuni ni full kubebishana,kusuguana, kumwagiana maji. kusuguana migongo hadi raha.lkn mume yuko bafuni we mke uko bize na fatuma gulu cjui filamu ya uhuru,mke bize na taarab huna uwazalo,waungwana bafuni wanaenda na VISOSI vyao special. na wanaojua maana mpaka viti spesho wanavyo majumbani hivyo huvioni mpaka muda wa kwenda kuoga wapendanao
bi mdada mfanye mumeo aone adhabu kuishi mbali na wewe japo kwa siku moja. lkn we hata ukisafiri mwezi mume haoni pengo la kutokuwepo kwako nyumbani khaa!!! we una hasara. malezi bibi malezi mume hafugwi kama kuku wa kijijini upo dada.
vitu hivi vidogo vidogo ndo vinafanya watu wadate mpaka mawifi wahashumu kua si bure labda kaka yao labda kazugwa,ubunifu bibi weeee ndo silaha ya kuwakata denge vizabizabina na makurumbembe.
USIPOWEZA KUKITUNZA JIANDAE KUKUTUNZIA WANAOJUA KUTUNZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: