NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 25 “Haya haya anzeni kwenda, lakini shehe usisahau ile dawa bwana niletee,” alisema yule afande huku akiagana na shehe nikatambua kumbe wamejuana na tayari amekuwa mteja wake. Ama kweli inachekesha, pamoja na misukosuko yote ile lakini Mungu ameonesha neema yake kwa kunitoa lupango, labda hakutaka nifie mle ndani itakapofika kesho asubuhi. Shehe alitusindikiza kwa gari yake hadi nyumbani kwangu, nilishangaa kutoona ule mzimu wa Jay Love ambao ulikuwa unatoa harufu kali, kwa kifupi kulikuwa safi. Niligundua hiyo ilikuwa ni kazi ya Shehe nikamshukuru na kwenda naye kando nikiomba anielezee kinagaubaga nini kilichotokea. Hapo ndiyo nikagundua kuwa kumbe mzimu wa Jay Love ili kuhakikisha unakumbukwa na Rabia ulimpeleka Rabia kuchora tattoo yenye jina lake kifuani kwake, tena yule shehe alisema tattoo hiyo aliijua baada ya kuwauliza dada zake ambao walikiri kuwa alikuwa nayo. Shehe alisema kuwa alihakikisha anachoma picha zote za Jay Love alizokuwa nazo Rabia, lakini kazi kubwa ni kumfanya Rabia apoteze kumbukumbu zote za Jay Love na kuhakikisha ile tattoo inaharibiwa na kusomeka vingine ili hata kama Rabia akiiona asilitaje jina la Jay Love ambaye hata kwa kutajwa tu kutamfanya aamke kuzimu na kurudi tena, safari hii akiwa hazuiliki.

at 12:47 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top