Home → simulizi
→ NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 24
Nikiwa nimebakiza masaa takribani kumi na nane sasa, kabla sijafikia kiama changu, nilishtukia nikiitwa nje ya selo na afande mmoja.
Nilipotoka nikapelekwa moja kwa moja hadi chumba cha mkuu wa kituo huko nilishangaa kukutana na Rabia na Shehe, Rabia akionekana analia kwa furaha tofauti na siku chache nyuma.
Akaruka na kunikumbatia kwa nguvu huku akiangusha kilio mfululizo, machozi yake niliweza kuyahisi yakitiririka na kunilowesha bega langu akitamka maneno haya; “Nisamehe mume wangu, sijui nini kilinikuta.. naomba nisamehe,”
Maneno yake yalinichoma moyoni yakanikumbusha enzi penzi langu na Rabia likiwa changa na jinsi alivyoonesha kunipenda kwa kumtazama kwenye macho tu. Siku hiyo sikuelewa nini kimetokea lakini nilijua anazungumza kutoka moyoni.
“Haya, yatosha sasa naomba ukae,” alizungumza mkuu yule wa kituo akimwamrisha Rabia ambaye hata hivyo alitumia muda kuniachia.
Akasogeza kiti na kukaa karibu kabisa na mimi akinishika mkono. Nilimtazama Shehe, akanikonyeza na kunionesha ishara ya dole gumba kuwa kila kitu kipo sawa. Kwa ishara ile nikajua aliupata ujumbe wangu na alimponesha Rabia; kivipi! Sikujua.
“Mr Denis, tumekagua sana nyumbani kwako lakini hatukuweza kuona kitu chochote kinachotoa ushahidi kama ulimuua mtu, ingawa tulichokiona kinaonesha kuna mambo ya kishirikina ulikuwa unayafanya.
“Hatujui ni nini na hatutaki kujua kwa sababu serikali haiamini katika ushirikina, na kama huyu bibie ambaye ni mkeo ndiye alitupa taarifa na leo ana kanusha basi hatuna shaka na hivyo basi kuanzia hivi sasa upo huru kuondoka,” alisema yule afande nikiwa sijaamini bado.
Nikamtazama mke wangu akaniangukia kifuani na kulia zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: