Tuesday, December 5, 2017

NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 17 Nilishangazwa na maneno hayo na tulikaa hadi asubuhi, wazo likawa moja tu, kumpigia mkwe wangu yaani mama yake Rabia ili tuzungumzie suala hili. Kidogo nilikuwa nina imani kwa kuwa nilikuwa nina uhakika mzimu wa Jay Love nimeufungia vyema chumbani kwangu hivyo hauwezi ukawa karibu na Rabia tena. Kweli tulikubaliana hivyo lakini nilimpigia simu mke wangu ambaye alionekana kuwa na hamu ya kuniona mimi zaidi, nikatambua kuwa kweli hapo mwanzo alikuwa akipelekwa na nguvu za Jay Love. Tulikutana tukashinda mchana kutwa tukikumbushia penzi letu, lakini baadaye nilimuita mkwe wangu pembeni na kumuelezea nilichokifanya, lakini kumbe Rabia alisikia yote tuliyokuwa tukiyazungumzia. Kuanzia jinsi nilivyomuona akaingia na Jay Love hotelini kuanzia siku ya kwanza hadi hivi juzi. Kwa penzi na kumbukumbu nzito alizonazo juu ya Jay Love, Rabia alishindwa kabisa kujidhibiti akafanya hima kuwataarifu polisi maana alishajua kuwa mzimu wa Jay Love ulikuwa chumbani kwangu. Kwake yeye hakuuona kama mzimu bali aliuona kama mpenzi wake aliowahi kumpenda kwa dhati hapo kabla na mimi akinichukulia kama mpita njia tu, si mumewe kama nilivyostahili. Hiyo ilionesha jinsi ambavyo ule usemi wa penzi la dhati hutokea mara moja tu. NAJUA WANAWAKE WENGI HAPA MTAKUBALI KUWA MWANAUME ULIYEMPENDA KWA DHATI MWANZONI, HAWEZI KUFANANA NA WENGINE WOTE ULIOPENDANA NAO BAADAYE BILA KUJALI HUYO WA KWANZA ALIKUUMIZA KIASI GANI. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Rabia.

No comments:

Post a Comment