NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 15
Tukiwa tumeketi kila mmoja akiushangaa mzimu ule, ghafla kama ukashtuka hivi ukasimama kwa nguvu na kutaka kunivamia.
Nikashangaa kuona ukikwama kama vile umefungwa na mnyororo kila ulipotaka kuvuka mchoro wa kingo za pentagram.
Shehe akaniambia nisiogope chochote mzimu huo hauwezi kutoka kifungo hicho, akaniambia kuwa uliweza kuzinduka kwa sababu Rabia aliukumbuka na akanisisitiza kuwa laiti kama Jay Love atasauliwa kichwani mwa Rabia basi mzimu wake utakuwa hauna nguvu yoyote na utarudi kuzimu ulipotoka.
Akaniambia hata kuhusu manabii na Mtume Muhammad (S.A.W) na Yesu Kristo, kuwa wanakumbukwa sana ndiyo maana wanaishi na kuwatendea miujiza na neema watu wawaaminio.
Akadai kuwa hapo kabla kulikuwa na mizimu mingi iliyopanda daraja na kuabudiwa kama Miungu, ikiwemo; Baali, Zeus, Titan, Herdes na mingine mingi, lakini baada ya dini ya Kikristo na hatimaye Uislamu kuingia, Miungu hii ikasahauliwa na hatimaye mizimu yao ikaishiwa nguvu na kurudi kuzimu.
Nikamuuliza kuhusu mchoro huo wa pentagram na vitunguu saumu akanieleza yafuatayo…
No comments:
Post a Comment