NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 09
Mara nikaona akishtuka na kuanza kuongea kwa Lugha ya Kiarabu huku akichoma ubani kwa wingi ndani ya chetezo, moshi ulijaa mle chumbani hadi nikapiga chafya.
Akafunika kile chetezo na chumba kikawa na hewa kama mwanzoni. Akaniambia alifanya vile ili kuhakikisha anafukuza majini na mizimu mibaya iliyoingilia maongezi yangu na yake mle ndani. Akanieleza hiyo ndiyo sababu pia hata makanisa ya Kikatoliki wakati wa ibada lazima kwanza ubani ufukizwe.
Hapa ndiyo nikamuomba anielezee kuhusu mizimu maana aliishia kwenye majini tu na nilipanga kuwa akimaliza kuhusu viumbe hao anielezee tena kuhusu malaika, angalau nijue kabla muda wangu wa kufa haujafika.
Akasema; “Mizimu, kama ilivyozoeleka ni roho za watu waliokufa ambao huamshwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ahadi, viapo, visasi na ibada za mizimu ndiyo huzifanya roho hizi zirudi duniani na kuwasumbua wahusika.
Hapo kwenye ibada za mizimu, akafafanua kuwa watu wengine huabudu watu waliokufa ambapo kwa kufanya hivyo huziamsha roho zao zilizo ahera na kuzifanya ziwe na nguvu kiasi cha kuja tena duniani, ikiwa marehemu alikuwa muovu basi mzimu wake utarudi na kufanya uovu zaidi na kama marehemu alikuwa mtu wa kutenda wema basi mzimu wake utakuwa ni wa wema zaidi.
Kwenye suala la visasi akasema, inawezekana mtu aliuawa kwa dhuruma hivyo mzimu wake utarudi na kuja kuwaangamiza wabaya wake.
Suala langu na mzimu wa Jay Love lilidondokea kwenye sababu ya ahadi na viapo alivyokula na mke wangu Rabia.
Nikamuona ananitazama kama ananionea huruma na kuniambia; “Sasa ngoja nikupunguzie huu mzigo wako,” sikujua alikuwa anamaanisha mzigo gani?
No comments:
Post a Comment