NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 08
Nikiwa najisikia kukosa amani kwa kutazamwa na majini huku nikiongeza maarifa mapya nilivyofundishwa na Shehe, nikaketi kwa adabu zaidi.
“Nisamehe kwa kilichotokea lakini ilikuwa lazima nikuoneshe kwa vitendo ili ujue mimi siyo kama wengine wanaowaongopea watu,” alisema Shehe akanishika mkono wangu na kuangalia viganja vyangu vya mkono.
Akavaa miwani yake na kufuatilia vizuri michirizi kwenye mikono yangu akaniambia; kwenye mkono kila mchirizi una maana yake. Akasema huu wa juu aliouita namba 1. unahusiana na masuala ya mapenzi ‘heartline’ 2. Unahusiana na akili ‘headline’ 3. Unahusiana na maisha ‘lifeline’ 4. Unahusiana na zari, bahati, gundu na vitu vingine kama hivyo huu unaitwa, ‘fateline’.
“Mara nyingi mstari huu wa ‘fate’ hutakiwa kuwa mng’avu sana ukimaanisha bahati njema lakini ukiwa umekolea rangi na kukata mstari namba 1 wa mapenzi ‘heartline’ na mstari namba 2 wa akili ‘headline’ kama huu wako basi maisha yako ya mapenzi na akili zako zitapewa mtihani na gundu hadi kupelekea kifo,” alisema hivyo yule Shehe, lakini alishangaa baada ya kuona mstari huo ukiwa haujaukata mstari namba 4 yaani mstari wa maisha ili kuthibitisha kwamba nitakufa. (nimeambatanisha picha ya kiganja changu hapo juu)
Akaniambia tangu aanze kazi yake hajawahi kuona kiganja kama changu kwa kuwa hakioneshi kufa kwangu kwenye gundu litakalonikuta na badala yake nitakufa kwa kawaida tena uzeeni.
Akaniambia japo ninatakiwa kufa ndani ya siku 10, lakini sitakufa, swali likawa je, nitakuwa wapi muda wote huo?
Itaendelea..
share stori hii watu wajue kuzisoma alama za mikono yao.
No comments:
Post a Comment