Home → simulizi
→ KURUDI KWA MOZA: 6
Wakati anataka kutoka akasikia sauti,
“Moza lala”
Akashtuka sana na kugeuka ili aone sauti inatokea wapi, ila hakumuona mtu yoyote akataka akafungue malango tena, kasikia
“Moza lala”
Safari hii ile sauti ilimwambia kwa ukali kidogo. Moza alizidi kupatwa na uoga hadi akawaza kutoroka kwenye ile nyumba ila atatorokaje usiku huo na kuna mlinzi getini, yani akawa na mawazo mbali mbali mpaka akajihisi kuchanganyikiwa. Ila bado alikuwa na wazo la kwenda sebleni kukaa lakini sauti ile ilizidi kumwambia moza alale, alipoona ile sauti inazidi maana ilianza kuongea kama mwangwi,
“Moza lala, Moza lala, Moza lala”
Uoga ulimjaa Moza hadi akataka kutoka kwa nguvu ila alipofungua mlango ulikuwa mgumu na ile sauti ilizidi kumsihi alale, Moza alitetemeka zaidi akataka kupiga kelele ili afunguliwe mlango ila moyo mwingine ukamwambia ukipiga kelele ndio utamshtua mwenye nyumba kuja kukuadhibu, akaamua kwenda kukaa kitandani huku akiombea asilale ila sauti ya kumsihi kulala ilizidi na kumtia hofu zaidi. Alipotaka kuinuka tena muda huu alishtukia akipigwa kibao kilichomuangusha hadi chini halafu taa ya chumbani ilizimwa yani hapo ndio uoga zaidi ukamshika na kujikuta akishindwa kuinuka pale chini ila cha kumshangaza wakati anaogopa sana, usingizi ukampata pale pale.
Wakati amelala akajiona yupo mahali chini ya mti halafu kaja Yule dada anayeongeaga kati ya wale wadada watano, akaanza kuongea nae ila leo Moza hakuweza kujibu wala kuuliza swali.
“Moza, ni mbishi sana wewe ndiomana nimekufanyia hivi. Yani hujui kutofautisha kati ya mtego na kitu cha kweli. Yule mama angetaka ulale ili akufanyie mambo mabaya unafikiri angeongea kwa sauti kubwa vile? Kaongea kwa sauti kubwa sababu amejua wewe ni mbea na utasikiliza tu kwahiyo alikuwekea mtego, na usingelala ndio angejua kama ni mbea kweli maana kwanini unasikiliza maongezi yao? Halafu kwa sheria za huyu mama amfanyiagi kitu mbaya mtu akiwa amelala, ndiomana hata jana hakukufanya lolote sababu ulilala ila ungekuwa macho ungepatwa na makubwa. Usifikirie siku zote nitaweza kukusaidia, nimeweza leo sababu ile juzi uliunguza mboga kwahiyo nimepata nguvu. Jifunze kuelewa mitego Moza, tutakupoteza na wewe. Usifikirie ni rahisi hivyo kutoroka kwenye hii nyumba. Kitabu nilichokwambia kipekue kesho uanze kukisoma ndio kitakusaidia sana kwenye mambo yote ya kufanya. Halafu unatakiwa kuwa makini sana kwenye kila kitu unachofanya, yani fikiria kabla ya kutenda jambo lolote. Kwasasa lala tu”
Huyu mdada aliondoka, ila ni usingizi mzito sana ulimshika Moza wakati huo.
Kuja kushtuka ilikuwa ni kumeshakucha, akaamka pale chini na kujishangaa shangaa kuwa imekuwaje mpaka akalala hapo chini, akaanza kukumbuka matukio na kukumbuka kuwa mara ya mwisho alinaswa kibao na kuanguka hapo chini kisha kukawa na giza kubwa lililompa uoga na kupitiwa na usingizi kwa uoga, pia akakumbuka alivyoota. Akainuka pale chini haraka haraka baada ya kukumbuka kuwa alitakiwa kuadhibiwa, akatoka sebleni ila nyumba ilikuwa kimya kabisa yani ilionyesha hapakuwa na mtu yeyote mule ndani.
Akasogea mezani ambapo alikuta ujumbe, ‘UPIKE WALI, MAHARAGE NA SAMAKI’ akaelewa kuwa ujumbe huo umeachwa na mama mwenye nyumba, hivyo akahisi kuwa huenda nyumba nzima wameondoka na hivyo kwenda kuoga na kuanza kufanya kazi za hapa na pale mule ndani hadi alipoanza kupika kile chakula alichoagizwa.
Alipomaliza kupika alikiandaa kabisa mezani ila alikuta ujumbe mwingine ‘TENGENEZA NA JUISI YA MATUNDA YAPO KWENYE FRIJI’ akaangalia kulia na kushoto, mbele na nyuma na kujiuliza,
“Mbona ujumbe huu sikuukuta mwanzoni? Humu ndani si nimebaki mwenyewe? Au sikuangalia vizuri!”
Akajiuliza bila ya jibu kama kawaida kisha akaanza kuiandaa hiyo juisi na kuiweka kwenye friji, ila aliporudi mezani alikuta ujumbe mwingine ‘CHEMSHA MAJI YA KUOGA YA ANA UMUWEKEE KWENYE CHUPA’ hapo uoga ukamshika na kuanza kuhisi tofauti, kisha akajiuliza,
“Mbona huyo Ana hajawahi kusema nimchemshie maji ya kuoga? Huu ujumbe ananiwekea nani? Siwezi kwakweli, naogopa. Inamaana sikuuona pia?”
Alikuwa na mashaka sana ila akaenda kuchemsha hayo maji na kuyaweka kwenye chupa, alipomaliza alirudi tena mezani na kukuta ujumbe mwingine ‘DEKI TENA NYUMBA’
Aliogopa sana sasa hivi na kuamua kukimbilia nje hadi kwa mlinzi huku akihema juu juu, Yule mlinzi alimuuliza,
“Humo ndani sielewi”
“Huelewi nini?”
“Nimebaki peke yangu ila nakutana na ujumbe mezani, kila nikifanya nakuta ujumbe mwingine. Naogopa kwakweli”
Yule mlinzi alianza kucheka sana kisha akamuuliza,
“Kwahiyo wewe unahisi ni nini?”
“Nahisi labda ni jinni”
“Usinichekeshe wewe, hivi jini unalijua wewe? Ushawahi kuona jini?”
“Sijawahi”
“Sasa unaogopa nini?”
“Naona mambo ya ajabu, ukizingatia ndani nipo mwenyewe”
“Upo mwenyewe wapi wewe, fanya tu ujinga wako uone. Mama yupo ndani leo hajatoka”
Moza akapumua kidogo na kujiona kama mjinga, kwani alihisi mitego ya Yule mama iliendelea kwahiyo ikabidi ajipange na majibu kama mwenye nyumba akimuuliza.
Moza alirudi ndani sasa na kuanza kudeki, na alipomaliza Rose alitoka ndani na kwenda sebleni ila Moza hakuonyesha kushtushwa sababu ameshaambiwa na mlinzi kuwa Rose yupo ndani, huyu mama alimuangalia Moza na kumuuliza
“Mbona hujashtuka?”
“Nishtuke nini sasa mama?”
“Ushtuke kuniona”
“Sijashtuka sababu nilijua tu kuwa upo ndani”
“Umejuaje”
“Nilipoona ujumbe mara ya kwanza, na nilipoona mara ya pili nikajua tu kuwa upo ndani”
Rose akacheka kisha akamwambia Moza,
“Unajifanya mjanja eeh wakati ushafanya umbea kwanza, nilitaka leo kukufundisha kazi za kufanya maana ni uhakika hujui kazi za kufanya ndiomana unapata na muda wa kufanya umbea. Laiti kama ungekuwa na kazi za kufanya basi umbea usingefanya. Haya nenda kamwagilizie maua maji, na nikitoka nikute yamelowana haswaaa”
Moza alitoka nje na kwenda kufunga mpira na kuanza kumwagilia maua, wakati anamwagilia kuna sauti ikamtuma kupekua ua moja wapo, akahisi kama kuchimba mzizi wa lile ua. Ikabidi amwagilie kwanza ili pakilowana achimbe mzizi huo aone ni nini na kwanini hisia zake zinamtuma afanye hivyo.
Palivyolowana, akaitwa na Rose kwani Ana alikuwa tayari amesharudi. Moza alivyofika pale, akashangaa kumuona Ana akiwa amebeba mwenyewe begi lake halafu Yule mama alimwambia kwa ukali,
“Hivi Moza huoni mtoto anahangaika na begi, si umpokee”
Moza akataka kumpokea lile begi Ana, ila Ana akawa mkali sana na kumkatalia kisha akamwambia mama yake
“Hili lidada limbea sana, lisije likafungua begi langu bure. Siwezi kumruhusu tena abebe begi langu”
Ana akaondoka zake, Rose akamuangalia Moza na kumfokea pale,
“Unaona sasa faida ya umbea wako, hadi mwanangu hakutaki yani wewe sijui kama mwezi huu utamaliza humu ndani. Umbea wako utakuwa umekuponza, haya kaendelee na umwagiliaji huko, sasa ole wako nisikie unafanya umbea hadi kwenye maua yangu”
Moza akataka kutoka, wale mapacha nao walirudi na walikuwa wakilalamika njaa sana,
“Ila chakula nimeshaandaa mezani”
“Hivi wewe Moza si nishakwambia kaendelee na umwagiliaji, mtu gani wewe hujielewi. Kwani hawa wakilalamika njaa ni wanakulalamikia wewe? Wewe ndio unaetafuta chakula humu ndani au? Hebu nenda zako huko”
Moza akondoka kwa aibu maana hakutegemea kama muda huu huyu mama angesema hivi.
Alienda tena kwenye ile bustani ya maua na kuendelea kumwagilia,ila bado mawazo yake yalimtuma kwenye lile ua ili afukue mzizi ajue kuna nini ila akakumbuka ile sauti ya mwenye nyumba kuwa ole wako nisikie unafanya umbea kwenye maua yangu,ile kauli ikawa inamrudia ila akajisemea.
“Kwani mimi natafuta umbea au nataka kuangalia mizizi ya lile ua? Kwani kuangalia mizizi ni umbea nao? Hapana bhana si umbea, nataka tu kuridhisha roho yangu maana inanituma niangalie mizizi ya ua lile, mbona haujanionyesha ua lingine zaidi ya lile! Huu si umbea bhana”
Yani alikuwa anajihoji mwenyewe na kujijibu mwenyewe basi aliacha kumwagilia na kwenda kufukua, alipokuwa anafukua hakuona mizizi kama alivyodhani ila alichokiona alistaajabu sana kwani alikuta mfuko na kitu kimefungwa kama mpira akataka kukifungua ila akajua akifungua hapo atabambwa kwahiyo akakificha kwenye nguo zake ili akakifungue ndani akiingia chumbani kwake kulala.
Tangu amkificha kile kimfuko nguvu ya kumwagilia ilimuisha kabisa na akajisikia hamu ya kuangalia kuna nini ila akajikaza kuwa ataenda kuangalia ndani. Roho yake ikamtuma kuwa akipeleke chumbani kwake kabisa, basi akaacha tena kumwagilia na kuanza kutembea ili apelike ule mfuko ndani ila kadri alivyokuwa anatembea nguvu zilikuwa zinamuisha, yani mpaka anaingia chumbani kwake alianguka kabisa ndipo alipotoa ule mfuko haraka haraka, ila alipoutoa tu na kuutupia pembeni nguvu zake zilirejea tena na kumfanya awe na mashaka zaidi kuhusu ule mfuko,
“Kilichomo humu kwenye mfuko si kimpira kama ninavyodhani ila nadhani kuna kitu kingine haiwezekani nguvu ziniishe kiasi hiki, lazima niangalie kuwa ni nini”
Ila muda huo akaitwa na Sara na kumfanya ainuke na kwenda alipo Sara ambapo alienda moja kwa moja chumbani kwa Sara, alifikiwa na swali,
“Jana ulikuja na nani hapa nyumbani?”
“Jana?”
“Ndio jana, usijipumbaze”
“Aaah nilikuja na mtoto mmoja hivi anaitwa Salome”
“Ni nani huyo mtoto?”
“Kwani wewe kakwambia nani kama nilikuja nae?”
“Moza, unafikiri umbea unauweza peke yako tu? Usitake kujua kaniambia nani, ila nijibu huyo mtoto ni nani na anamahusiano gani na familia yetu?”
“Ila kwanini umeniuliza hivyo Sara?”
“Moza, usiniulize maswali ila nijibu nilichokuuliza”
“Kwakweli sijui nikujibu vipi hilo swali lako, ila Yule mtoto ni wa bosi wangu wa zamani yani mwanzoni nilikuwa nafanya kazi kwao. Nimekutana nae buchani sasa nikamlete ili apafahamu ninapoishi kwasasa”
“Mama anajua kama uliwahi kufanya kazi kwa mama wa huyo mtoto?”
“Hajui, kwani kuna uhusiano gani kati yenu na huyo mtoto?”
“Sitaki maswali Moza, ila hili swala lazima mama nimfikishie maana umemleta mtu bila ruhusa ya mama. Vipi baba alimuona?”
“Alimuona ndio wakati namsindikiza”
“Yani wewe Moza wewe unatafuta mabalaa ambayo huwezi kuyatatua. Sikia nikwambie ujue kama ulikuwa hujui, Yule mtoto aliwahi kusingiziwa baba kuwa mtoto wake yani ilitokea mtafaruku mkubwa sana hapa nyumbani. Kipindi hicho hadi mama akaanza kutafuta mtoto kwa haja zote ndio baada ya miaka kadhaa akampata Ana. Sasa mama ana hasira sana na familia ya Yule mtoto halafu wewe unaenda kumchukua na kumleta nyumbani”
“Lakini mimi nilikuwa siyajui yote hayo, na kama ndio hivyo mbona Salome hakuonyesha kama anapafahamu hapa?”
“Sikia Moza, kwanza Yule haitwi Salome nadhani hilo jina wamempa ukubwani. Alikuwa anaitwa Maria, mamake anapajua hapa vilivyo na hawezi kusogelea hapa. Yule mtoto hapajui hapa, usijaribu tena kumleta Yule mtoto kwenye nyumba hii”
“Lakini ningependa unieleweshe zaidi, mbona kafanana sana na baba”
“Moza Moza, naenda kukusemea kwa mama maana naona unazidi kuchokonoa mambo”
“Tafadhali, naomba unisamehe”
“Unamuogopa eeh”
“Ndio namuogopa”
“haya, kaendelee na shughuli zako”
Moza alitoka mule chumbani kwa Sara na kwenda jikoni kuosha vyombo ambavyo tayari walikuwa wamelia chakula, hapo akawaza tena kuhusu Salome kuwa Yule baba inasemekana kasingiziwa lakini inaonyesha wazi Salome ni mtoto wa Patrick, ila kwanini Patrick mwenyewe anauwalakini kuhusu mtoto wake huyo na kwanini Salome alibadilishwa jina kama ni kweli alibadilishwa jina, alitamani kujua kwa undani zaidi ambapo alijua wa kumjibu mwingine ni mama yake Salome ambaye ni Neema.
Alitamani apate muda wa kwenda kuzungumza na Neema ili ajue kwa undani zaidi,
“Lakini umbea huu loh hata kuacha sitamani, najikuta tu natamani kujua sijui nifanyeje masikini Moza mimi”
Kumbe maneno hayo aliongea kwa sauti ya kusikika, akasikia sauti ikimwambia, ilikuwa ni sauti ya Rose,
“Haya ni nini unachotamani kujua?”
Moza akashtuka na kumjibu kwa uoga uoga,
“Hakuna kitu mama”
“Usinichekeshe Moza, wakati nimekusikia kila kitu. Niambie unachotamani kukijua ili nikusaidie ukijue”
“Hakuna kitu mama”
“Hakuna kitu eeeh!”
“Ndio mama hakuna kitu”
“Mimi nakiona kipo”
Rose alimshika mkono Moza na kuanza kumkokota, kwakweli Moza alishikwa na uoga kwani moja kwa moja Rose alimpeleka Moza kwenye kile chumba chenye chumba kidogo ndani kisha akamwambia,
“Unataka kujua kilichopo mule eeeh!”
Moza alikuwa kimya tu,
“Najua unajiuliza kuwa ukubali au ukatae, huku moyo wako mwingine ukitamani kujua siri iliyomo kwenye chumba kile. Haya chukua funguo hapo juu”
Rose alimwambia Moza kwa kumkaripia ambapo Moza alichukua funguo huku akitetemeka,
“Haya fungua sasa”
Moza alianza kufungua huku akitetemeka kwani alihisi kama hapelekwi nay eye kwenye chumba hiko basi ataona vitu vya ajabu, ila leo tofauti na siku ile aliyotaka kuchungulia kwani alipigwa na shoti ila leo hakupigwa na cheche yoyote. Na alipofungua tu alijiona yupo nje,
“Umeona sasa, huu ni mlango wa kutoka nje. Sasa wewe ulikuwa unafikiria ni nini?”
“Hapana mama, sijafikiria chochote”
“Haya tuzunguke tukaingie ndani”
Wakazunguka na kuingia ndani tena, kisha Rose akamuuliza moza,
“Sasa una amani eeh”
Moza aliitikia kwa kichwa tu kuwa ameridhika, Rose alicheka na kumuacha moza anaenda jikoni ambapo alienda kumalizia vile vyombo vyake ila alikuwa na mawazo mengi sana.
Moza aliingia chumbani kwake ila bado alikuwa na maswali mengi sana, kwanza kabisa alijiuliza kuhusu chumba alichopelekwa ambacho mlango wa ndani ulimtoa nje,
“Mmmh huyu mama hajanifanyia mtego kweli, mbona kama chumba sio kile? Nahisi kanifanyia mchezo Yule mama lakini kwanini anifanyie mchezo wakati mimi si chochote wala lolote kwenye hii familia”
Wazo lingine likamjia ni kuhusu Ana maana siku hizi Ana hakutaka kitu chochote afanyiwe na Moza jambo ambalo lilimchanganya pia. Wakati anawaza hayo, mlango wake uligongwa alipoenda kufungua alimkuta mama mwenye nyumba ambaye alimwambia
“Dawa yako inachemka”
Huyu mama akaondoka, Moza akatoka na kwenda jikoni huku akiangalia hiyo dawa aliyoambiwa inachemka iko wapi maana hakubandika dawa yoyote kwahiyo ule usemi wa dawa yako inachemka kwa muda huo hakuelewa alijua ni dawa kweli.
Moza alivyoona hakuna dawa inayochemka alirudi tena chumbani,muda huu akili ikamtuma achunguze ule mfuko alioutoa kwenye maua. Akuchukua ule mfuko na kuanza kuuchunguza kwa kuufunua ambapo kweli alikuta kama mpira wa makaratasi umefungwa fungwa. Moza akaanza kufungua ila kadri alivyofungua ndivyo nguvu zilivyomuisha, hadi mwishoni akaanguka kabisa na kuwa kimya hapo hapo.
Itaendelea kesho usiku kama kawaida…..!!!!!!
KURUDI KWA MOZA: 6 Wakati anataka kutoka akasikia sauti, “Moza lala” Akashtuka sana na kugeuka ili aone sauti inatokea wapi, ila hakumuona mtu yoyote akataka akafungue malango tena, kasikia “Moza lala” Safari hii ile sauti ilimwambia kwa ukali kidogo. Moza alizidi kupatwa na uoga hadi akawaza kutoroka kwenye ile nyumba ila atatorokaje usiku huo na kuna mlinzi getini, yani akawa na mawazo mbali mbali mpaka akajihisi kuchanganyikiwa. Ila bado alikuwa na wazo la kwenda sebleni kukaa lakini sauti ile ilizidi kumwambia moza alale, alipoona ile sauti inazidi maana ilianza kuongea kama mwangwi, “Moza lala, Moza lala, Moza lala” Uoga ulimjaa Moza hadi akataka kutoka kwa nguvu ila alipofungua mlango ulikuwa mgumu na ile sauti ilizidi kumsihi alale, Moza alitetemeka zaidi akataka kupiga kelele ili afunguliwe mlango ila moyo mwingine ukamwambia ukipiga kelele ndio utamshtua mwenye nyumba kuja kukuadhibu, akaamua kwenda kukaa kitandani huku akiombea asilale ila sauti ya kumsihi kulala ilizidi na kumtia hofu zaidi. Alipotaka kuinuka tena muda huu alishtukia akipigwa kibao kilichomuangusha hadi chini halafu taa ya chumbani ilizimwa yani hapo ndio uoga zaidi ukamshika na kujikuta akishindwa kuinuka pale chini ila cha kumshangaza wakati anaogopa sana, usingizi ukampata pale pale. Wakati amelala akajiona yupo mahali chini ya mti halafu kaja Yule dada anayeongeaga kati ya wale wadada watano, akaanza kuongea nae ila leo Moza hakuweza kujibu wala kuuliza swali. “Moza, ni mbishi sana wewe ndiomana nimekufanyia hivi. Yani hujui kutofautisha kati ya mtego na kitu cha kweli. Yule mama angetaka ulale ili akufanyie mambo mabaya unafikiri angeongea kwa sauti kubwa vile? Kaongea kwa sauti kubwa sababu amejua wewe ni mbea na utasikiliza tu kwahiyo alikuwekea mtego, na usingelala ndio angejua kama ni mbea kweli maana kwanini unasikiliza maongezi yao? Halafu kwa sheria za huyu mama amfanyiagi kitu mbaya mtu akiwa amelala, ndiomana hata jana hakukufanya lolote sababu ulilala ila ungekuwa macho ungepatwa na makubwa. Usifikirie siku zote nitaweza kukusaidia, nimeweza leo sababu ile juzi uliunguza mboga kwahiyo nimepata nguvu. Jifunze kuelewa mitego Moza, tutakupoteza na wewe. Usifikirie ni rahisi hivyo kutoroka kwenye hii nyumba. Kitabu nilichokwambia kipekue kesho uanze kukisoma ndio kitakusaidia sana kwenye mambo yote ya kufanya. Halafu unatakiwa kuwa makini sana kwenye kila kitu unachofanya, yani fikiria kabla ya kutenda jambo lolote. Kwasasa lala tu” Huyu mdada aliondoka, ila ni usingizi mzito sana ulimshika Moza wakati huo. Kuja kushtuka ilikuwa ni kumeshakucha, akaamka pale chini na kujishangaa shangaa kuwa imekuwaje mpaka akalala hapo chini, akaanza kukumbuka matukio na kukumbuka kuwa mara ya mwisho alinaswa kibao na kuanguka hapo chini kisha kukawa na giza kubwa lililompa uoga na kupitiwa na usingizi kwa uoga, pia akakumbuka alivyoota. Akainuka pale chini haraka haraka baada ya kukumbuka kuwa alitakiwa kuadhibiwa, akatoka sebleni ila nyumba ilikuwa kimya kabisa yani ilionyesha hapakuwa na mtu yeyote mule ndani. Akasogea mezani ambapo alikuta ujumbe, ‘UPIKE WALI, MAHARAGE NA SAMAKI’ akaelewa kuwa ujumbe huo umeachwa na mama mwenye nyumba, hivyo akahisi kuwa huenda nyumba nzima wameondoka na hivyo kwenda kuoga na kuanza kufanya kazi za hapa na pale mule ndani hadi alipoanza kupika kile chakula alichoagizwa. Alipomaliza kupika alikiandaa kabisa mezani ila alikuta ujumbe mwingine ‘TENGENEZA NA JUISI YA MATUNDA YAPO KWENYE FRIJI’ akaangalia kulia na kushoto, mbele na nyuma na kujiuliza, “Mbona ujumbe huu sikuukuta mwanzoni? Humu ndani si nimebaki mwenyewe? Au sikuangalia vizuri!” Akajiuliza bila ya jibu kama kawaida kisha akaanza kuiandaa hiyo juisi na kuiweka kwenye friji, ila aliporudi mezani alikuta ujumbe mwingine ‘CHEMSHA MAJI YA KUOGA YA ANA UMUWEKEE KWENYE CHUPA’ hapo uoga ukamshika na kuanza kuhisi tofauti, kisha akajiuliza, “Mbona huyo Ana hajawahi kusema nimchemshie maji ya kuoga? Huu ujumbe ananiwekea nani? Siwezi kwakweli, naogopa. Inamaana sikuuona pia?” Alikuwa na mashaka sana ila akaenda kuchemsha hayo maji na kuyaweka kwenye chupa, alipomaliza alirudi tena mezani na kukuta ujumbe mwingine ‘DEKI TENA NYUMBA’ Aliogopa sana sasa hivi na kuamua kukimbilia nje hadi kwa mlinzi huku akihema juu juu, Yule mlinzi alimuuliza, “Humo ndani sielewi” “Huelewi nini?” “Nimebaki peke yangu ila nakutana na ujumbe mezani, kila nikifanya nakuta ujumbe mwingine. Naogopa kwakweli” Yule mlinzi alianza kucheka sana kisha akamuuliza, “Kwahiyo wewe unahisi ni nini?” “Nahisi labda ni jinni” “Usinichekeshe wewe, hivi jini unalijua wewe? Ushawahi kuona jini?” “Sijawahi” “Sasa unaogopa nini?” “Naona mambo ya ajabu, ukizingatia ndani nipo mwenyewe” “Upo mwenyewe wapi wewe, fanya tu ujinga wako uone. Mama yupo ndani leo hajatoka” Moza akapumua kidogo na kujiona kama mjinga, kwani alihisi mitego ya Yule mama iliendelea kwahiyo ikabidi ajipange na majibu kama mwenye nyumba akimuuliza. Moza alirudi ndani sasa na kuanza kudeki, na alipomaliza Rose alitoka ndani na kwenda sebleni ila Moza hakuonyesha kushtushwa sababu ameshaambiwa na mlinzi kuwa Rose yupo ndani, huyu mama alimuangalia Moza na kumuuliza “Mbona hujashtuka?” “Nishtuke nini sasa mama?” “Ushtuke kuniona” “Sijashtuka sababu nilijua tu kuwa upo ndani” “Umejuaje” “Nilipoona ujumbe mara ya kwanza, na nilipoona mara ya pili nikajua tu kuwa upo ndani” Rose akacheka kisha akamwambia Moza, “Unajifanya mjanja eeh wakati ushafanya umbea kwanza, nilitaka leo kukufundisha kazi za kufanya maana ni uhakika hujui kazi za kufanya ndiomana unapata na muda wa kufanya umbea. Laiti kama ungekuwa na kazi za kufanya basi umbea usingefanya. Haya nenda kamwagilizie maua maji, na nikitoka nikute yamelowana haswaaa” Moza alitoka nje na kwenda kufunga mpira na kuanza kumwagilia maua, wakati anamwagilia kuna sauti ikamtuma kupekua ua moja wapo, akahisi kama kuchimba mzizi wa lile ua. Ikabidi amwagilie kwanza ili pakilowana achimbe mzizi huo aone ni nini na kwanini hisia zake zinamtuma afanye hivyo. Palivyolowana, akaitwa na Rose kwani Ana alikuwa tayari amesharudi. Moza alivyofika pale, akashangaa kumuona Ana akiwa amebeba mwenyewe begi lake halafu Yule mama alimwambia kwa ukali, “Hivi Moza huoni mtoto anahangaika na begi, si umpokee” Moza akataka kumpokea lile begi Ana, ila Ana akawa mkali sana na kumkatalia kisha akamwambia mama yake “Hili lidada limbea sana, lisije likafungua begi langu bure. Siwezi kumruhusu tena abebe begi langu” Ana akaondoka zake, Rose akamuangalia Moza na kumfokea pale, “Unaona sasa faida ya umbea wako, hadi mwanangu hakutaki yani wewe sijui kama mwezi huu utamaliza humu ndani. Umbea wako utakuwa umekuponza, haya kaendelee na umwagiliaji huko, sasa ole wako nisikie unafanya umbea hadi kwenye maua yangu” Moza akataka kutoka, wale mapacha nao walirudi na walikuwa wakilalamika njaa sana, “Ila chakula nimeshaandaa mezani” “Hivi wewe Moza si nishakwambia kaendelee na umwagiliaji, mtu gani wewe hujielewi. Kwani hawa wakilalamika njaa ni wanakulalamikia wewe? Wewe ndio unaetafuta chakula humu ndani au? Hebu nenda zako huko” Moza akondoka kwa aibu maana hakutegemea kama muda huu huyu mama angesema hivi. Alienda tena kwenye ile bustani ya maua na kuendelea kumwagilia,ila bado mawazo yake yalimtuma kwenye lile ua ili afukue mzizi ajue kuna nini ila akakumbuka ile sauti ya mwenye nyumba kuwa ole wako nisikie unafanya umbea kwenye maua yangu,ile kauli ikawa inamrudia ila akajisemea. “Kwani mimi natafuta umbea au nataka kuangalia mizizi ya lile ua? Kwani kuangalia mizizi ni umbea nao? Hapana bhana si umbea, nataka tu kuridhisha roho yangu maana inanituma niangalie mizizi ya ua lile, mbona haujanionyesha ua lingine zaidi ya lile! Huu si umbea bhana” Yani alikuwa anajihoji mwenyewe na kujijibu mwenyewe basi aliacha kumwagilia na kwenda kufukua, alipokuwa anafukua hakuona mizizi kama alivyodhani ila alichokiona alistaajabu sana kwani alikuta mfuko na kitu kimefungwa kama mpira akataka kukifungua ila akajua akifungua hapo atabambwa kwahiyo akakificha kwenye nguo zake ili akakifungue ndani akiingia chumbani kwake kulala. Tangu amkificha kile kimfuko nguvu ya kumwagilia ilimuisha kabisa na akajisikia hamu ya kuangalia kuna nini ila akajikaza kuwa ataenda kuangalia ndani. Roho yake ikamtuma kuwa akipeleke chumbani kwake kabisa, basi akaacha tena kumwagilia na kuanza kutembea ili apelike ule mfuko ndani ila kadri alivyokuwa anatembea nguvu zilikuwa zinamuisha, yani mpaka anaingia chumbani kwake alianguka kabisa ndipo alipotoa ule mfuko haraka haraka, ila alipoutoa tu na kuutupia pembeni nguvu zake zilirejea tena na kumfanya awe na mashaka zaidi kuhusu ule mfuko, “Kilichomo humu kwenye mfuko si kimpira kama ninavyodhani ila nadhani kuna kitu kingine haiwezekani nguvu ziniishe kiasi hiki, lazima niangalie kuwa ni nini” Ila muda huo akaitwa na Sara na kumfanya ainuke na kwenda alipo Sara ambapo alienda moja kwa moja chumbani kwa Sara, alifikiwa na swali, “Jana ulikuja na nani hapa nyumbani?” “Jana?” “Ndio jana, usijipumbaze” “Aaah nilikuja na mtoto mmoja hivi anaitwa Salome” “Ni nani huyo mtoto?” “Kwani wewe kakwambia nani kama nilikuja nae?” “Moza, unafikiri umbea unauweza peke yako tu? Usitake kujua kaniambia nani, ila nijibu huyo mtoto ni nani na anamahusiano gani na familia yetu?” “Ila kwanini umeniuliza hivyo Sara?” “Moza, usiniulize maswali ila nijibu nilichokuuliza” “Kwakweli sijui nikujibu vipi hilo swali lako, ila Yule mtoto ni wa bosi wangu wa zamani yani mwanzoni nilikuwa nafanya kazi kwao. Nimekutana nae buchani sasa nikamlete ili apafahamu ninapoishi kwasasa” “Mama anajua kama uliwahi kufanya kazi kwa mama wa huyo mtoto?” “Hajui, kwani kuna uhusiano gani kati yenu na huyo mtoto?” “Sitaki maswali Moza, ila hili swala lazima mama nimfikishie maana umemleta mtu bila ruhusa ya mama. Vipi baba alimuona?” “Alimuona ndio wakati namsindikiza” “Yani wewe Moza wewe unatafuta mabalaa ambayo huwezi kuyatatua. Sikia nikwambie ujue kama ulikuwa hujui, Yule mtoto aliwahi kusingiziwa baba kuwa mtoto wake yani ilitokea mtafaruku mkubwa sana hapa nyumbani. Kipindi hicho hadi mama akaanza kutafuta mtoto kwa haja zote ndio baada ya miaka kadhaa akampata Ana. Sasa mama ana hasira sana na familia ya Yule mtoto halafu wewe unaenda kumchukua na kumleta nyumbani” “Lakini mimi nilikuwa siyajui yote hayo, na kama ndio hivyo mbona Salome hakuonyesha kama anapafahamu hapa?” “Sikia Moza, kwanza Yule haitwi Salome nadhani hilo jina wamempa ukubwani. Alikuwa anaitwa Maria, mamake anapajua hapa vilivyo na hawezi kusogelea hapa. Yule mtoto hapajui hapa, usijaribu tena kumleta Yule mtoto kwenye nyumba hii” “Lakini ningependa unieleweshe zaidi, mbona kafanana sana na baba” “Moza Moza, naenda kukusemea kwa mama maana naona unazidi kuchokonoa mambo” “Tafadhali, naomba unisamehe” “Unamuogopa eeh” “Ndio namuogopa” “haya, kaendelee na shughuli zako” Moza alitoka mule chumbani kwa Sara na kwenda jikoni kuosha vyombo ambavyo tayari walikuwa wamelia chakula, hapo akawaza tena kuhusu Salome kuwa Yule baba inasemekana kasingiziwa lakini inaonyesha wazi Salome ni mtoto wa Patrick, ila kwanini Patrick mwenyewe anauwalakini kuhusu mtoto wake huyo na kwanini Salome alibadilishwa jina kama ni kweli alibadilishwa jina, alitamani kujua kwa undani zaidi ambapo alijua wa kumjibu mwingine ni mama yake Salome ambaye ni Neema. Alitamani apate muda wa kwenda kuzungumza na Neema ili ajue kwa undani zaidi, “Lakini umbea huu loh hata kuacha sitamani, najikuta tu natamani kujua sijui nifanyeje masikini Moza mimi” Kumbe maneno hayo aliongea kwa sauti ya kusikika, akasikia sauti ikimwambia, ilikuwa ni sauti ya Rose, “Haya ni nini unachotamani kujua?” Moza akashtuka na kumjibu kwa uoga uoga, “Hakuna kitu mama” “Usinichekeshe Moza, wakati nimekusikia kila kitu. Niambie unachotamani kukijua ili nikusaidie ukijue” “Hakuna kitu mama” “Hakuna kitu eeeh!” “Ndio mama hakuna kitu” “Mimi nakiona kipo” Rose alimshika mkono Moza na kuanza kumkokota, kwakweli Moza alishikwa na uoga kwani moja kwa moja Rose alimpeleka Moza kwenye kile chumba chenye chumba kidogo ndani kisha akamwambia, “Unataka kujua kilichopo mule eeeh!” Moza alikuwa kimya tu, “Najua unajiuliza kuwa ukubali au ukatae, huku moyo wako mwingine ukitamani kujua siri iliyomo kwenye chumba kile. Haya chukua funguo hapo juu” Rose alimwambia Moza kwa kumkaripia ambapo Moza alichukua funguo huku akitetemeka, “Haya fungua sasa” Moza alianza kufungua huku akitetemeka kwani alihisi kama hapelekwi nay eye kwenye chumba hiko basi ataona vitu vya ajabu, ila leo tofauti na siku ile aliyotaka kuchungulia kwani alipigwa na shoti ila leo hakupigwa na cheche yoyote. Na alipofungua tu alijiona yupo nje, “Umeona sasa, huu ni mlango wa kutoka nje. Sasa wewe ulikuwa unafikiria ni nini?” “Hapana mama, sijafikiria chochote” “Haya tuzunguke tukaingie ndani” Wakazunguka na kuingia ndani tena, kisha Rose akamuuliza moza, “Sasa una amani eeh” Moza aliitikia kwa kichwa tu kuwa ameridhika, Rose alicheka na kumuacha moza anaenda jikoni ambapo alienda kumalizia vile vyombo vyake ila alikuwa na mawazo mengi sana. Moza aliingia chumbani kwake ila bado alikuwa na maswali mengi sana, kwanza kabisa alijiuliza kuhusu chumba alichopelekwa ambacho mlango wa ndani ulimtoa nje, “Mmmh huyu mama hajanifanyia mtego kweli, mbona kama chumba sio kile? Nahisi kanifanyia mchezo Yule mama lakini kwanini anifanyie mchezo wakati mimi si chochote wala lolote kwenye hii familia” Wazo lingine likamjia ni kuhusu Ana maana siku hizi Ana hakutaka kitu chochote afanyiwe na Moza jambo ambalo lilimchanganya pia. Wakati anawaza hayo, mlango wake uligongwa alipoenda kufungua alimkuta mama mwenye nyumba ambaye alimwambia “Dawa yako inachemka” Huyu mama akaondoka, Moza akatoka na kwenda jikoni huku akiangalia hiyo dawa aliyoambiwa inachemka iko wapi maana hakubandika dawa yoyote kwahiyo ule usemi wa dawa yako inachemka kwa muda huo hakuelewa alijua ni dawa kweli. Moza alivyoona hakuna dawa inayochemka alirudi tena chumbani,muda huu akili ikamtuma achunguze ule mfuko alioutoa kwenye maua. Akuchukua ule mfuko na kuanza kuuchunguza kwa kuufunua ambapo kweli alikuta kama mpira wa makaratasi umefungwa fungwa. Moza akaanza kufungua ila kadri alivyofungua ndivyo nguvu zilivyomuisha, hadi mwishoni akaanguka kabisa na kuwa kimya hapo hapo. Itaendelea kesho usiku kama kawaida…..!!!!!!
Artikel Terkait
CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA KWANZA (01) Ilikuwa alfajiri moja nyepesi, katika jiji la dar-es-salaam, katika mtaa mmoja tulivu sana mbezi beach, dio kwanza nikama pilika zilikuwa zinaanza, yalionekana magari machache ya kifahari, yakikatiza kwenye viji barabara vya mtaa, na kupoteea barabara kuu, watu wakikwep foleni kwa kuwai makazini na mashuleni, au sehemu mbali mbali za kijamii, mapema namna hii, huku watu wachache walio tembea kwa miguu wakionekana wakitembea haraka kuelekea barabarani, Ndani jumba moja la kifahari lililo zungukwa na uzio(fensi) wa ukuta mkubwa, ilisikika sauti ya msichana mmoja, mrembo mwenye asili ya Kihindi akiongea na mama yake, ilionekana alikuwa anataka kutoka. "mama mi naondoka naenda shule, maana kuna mitihani muhimu nawahi ingekuwa bila ya hiyo mitihani nisingeenda" alisikika binti mwenye sauti kinanda, akimwambia mama yake, ambae pia, ni mwenye asili ya Kihindi,japo alionekana ni mama wa makamo, lakini akika alifanana na binti yake., maana unge weza kuona uzuri wa mama huyu, japo tayari alisha kuwa mkubwa, "basi haya, chukua gari hiyo nyeusi, uwahi mwanangu" alisema mama huyu huku anawonyeshawanae funguo ya hili gari alilo mtajia, "hapana mamy, ntaomba lifti huko huko, leo sijisikii kuendesha" alijibu binti mrembo, huku akichukuwa begi lake juu ya meza na kuanza kuondoka, akiufwata mlango mkubwa wa kutokea nje. "haya basi baadaye mwanangu, jitazame huko uendako" aliongea mama huku anamsindikiza kwa macho binti yake, ambae toka akiwa mdogo amekuwa nae makini sana, ungesema amezaliwa peke yake, "ok mumy" alijibu binti chotara, huku anainua mkono wake na kuchezesha vidole, akimaanisha ana mpungia mkono mama yake, kisha akatoweka. Naam huyu ni binti mrembo NIRAM, ni binti wakihindi, mwenye sura nzuri ya kuvutia, macho ya duara, pua iliyochongoka vizuri, mwenye midomo mipana ambayo kila anapo tabasamu, basi uacha vijishimo mashavuni mwake, alikuwa na urefu wa futi tano, na pointi kadhaa, kifua cha wastani na tumbo dogo, kiuno chake kilibeba makalio ma nene kihasi na pia, vi hips vya kumwagika vilivyojazia na kuchomoza pembeni, vilizidi kumpendezesha, asa anapokuwa katika mwendo, kiufupi mdau wa story hii, ilikuwa si rahisi upishane nae, ushindwe kumgeukia, iliuone uumbaji. Huyu anaitwa Niram Popat, baba yake ni mfanya biashara mkubwa, na kwa sasa yupo nchini Uingereza, kwa shughuli zake za kibiashara, binti huyu akualiwa peke yake, Niram alikuwa na kaka yake, ambae kwa sasa yupo chuo kikuu cha Indira Gandhi nchini india akijichukulia masters yake, kifupi katika familia yao wamezaliwa wawili tu! yani yeye na kaka yake, Niram alipendwa kuliko kawaida. Hiyo ndo historia fupi ya niram, ebu tuendelee na kisa hiki cha Chaguo langu, Niram alitembea taratibu akiongozana na watu waliokuwa wanaelekea huko kwenye kituo cha dala dala, dakika chache baadae, Niram alifika kituoni, nakuwakuta watu wengi wakisubiri usafiri,binti huyu, alijitenga pembeni kabisa na abiria wengine, usafiri ilionyesha ulikuwa wa shida sana siku hiyo, maana magari yalifika pale yakiwa yamesha jaa, hivyo waliofanikiwa kupanda, walijibana kama nyanya kwenye matenga, Niram alijikuta ana kumbuka gari ambalo amelikataa nyumbani,”haaa, kwanini niliamua hivi?” alijilahumu binti huyu mzuri, ambae asilimia tisini ya wanaume waliokuwepo pale, walikuwa wanamkodolea macho, wakisanifu uumbaji, Lakini wakati anawaza hayo,mara ghafla ilisimama range nyeusi, mbele yake na paka shushwa vioo, ilionekana sura moja matata sana, ya mwanaume mtanashati, hakika alifaa kuitwa handsome wa Kiafrika "hellow" yule kijana ndani yagari alimsabahi Niram, nae akajibu kwa kichwa, yule jamaa akatabasamu kidogo, "naweza kukupa lifti? Aliuliza kijana yule. na Niram akuwa mbishi, aliitikia kwa kichwa kama kawaida yake, hapo ukafunguliwa mlango Niram akaingia. na kufunga mlango, sasa akawa ametulia kwenyeseat yake, huku macho mbele, akitegemea kuona gari linaondoka, na maswali yanaanza, lakini zika pita dakika kadhaa na gari halikuondoka. Muda wote haku endesha gari, alikuwa ameduwaa, kumshangaa msichana alie ingia garini mwake. Alizidi kushangaa "sorry kaka mimi nashuka vituo vinne mbele ndipo ilipo shule yetu"aliongea niram. Maskini kijana yule aligutuka, akababaika huku anaondoa gari, "oooh! aaagh sawa unasoma shule ipi dada?" aliongea huku gari ikienda taratibu "shadhiliya slamic internation school" alijibu Niram, "ooh ile shule ya kiislam "aliuliza kijana. "yap! nasoma kidato cha tano pale" alijibu niram "ok mi mwenyewe nasoma pale st joseph international school kidato cha sita "alisema kijana "aah kumbe" alisema Niram kwa uchangamfu kidogo, akiona kuwa yupo na mwanafunzi mwenzie, "ndiyo ninaitwa Vincent, sijui naweza kulijuwa juna lako kama hutojali?" aliuliza Vincent huku anatabasamu, kidogo wengee lilianza kumtoka, "mimi naitwa Niram..” alisema Niram lakini kama alistuka kidogo, “ooh! kaka nishushe unapitiliza" aliongea niram kwa mshtuko "ooh sorry, kwa kweli" alijibu Vincent,huku ana peleka mguu wake wkulia katikati na kukanyaga bleack, akippunguza mwendo na kuweka gari pembeni ya barabara, kisha akasimama, Niram alishuka, na akashukuru Vincent kwa kupitia kwenye dirisha la upande aliokaa, na kuondoka zake. Vicent alibaki kaduwaa, maana alishangazwa na uzuri wa aina yake, kwa yule msichana. "daah nimesahau kuomba namba" alijilahumu Vicent, lakini hakuwa na lakufanya, akawasha gari akasepaaa. Anaitwa Vicent Ngosha, ni mtoto wa mzee Emanueli Ngosha mfanya biashara mkubwa nchini Tanzania na nje ya nchi.Vincent alikuwa ni mvulana wa kisukuma, mama yake ni muhaya, Vicent ni mtoto pekee kwenye familia yao, ni familia yenye uwezo mkubwa, baba yake alikuwa mkoani kibiashara, hivyo alibaki pale nyumbani na mama yake, pamoja na house girl, Vicent alifika shuleni akiwa na mawazo lukuki, “ok! mdau huu nimwanzo wa mkasa huu wakusisimua, ...... CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA PILI (02) ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA : Anaitwa Vicent Ngosha, ni mtoto wa mzee Emanueli Ngosha mfanya biashara mkubwa nchini Tanzania na nje ya nchi.Vincent alikuwa ni mvulana wa kisukuma, mama yake ni muhaya, Vicent ni mtoto pekee kwenye familia yao, ni familia yenye uwezo mkubwa, baba yake alikuwa mkoani kibiashara, hivyo alibaki pale nyumbani na mama yake, pamoja na house girl, Vicent alifika shuleni akiwa na mawazo lukuki. ENDELEA......... Vincent alifika shule akiwa na mawazo kibao. Aliwaza kwamba alikutana na jini au mtu wa kawaida, hakika alikuwa hayupo sawa alishachanganywa na mtoto wa Kihindi, akujua afanye nini ili aweze kuwa karibu na binti yule, akika Vicent likuwa katika wakati mgumu, alijikuta anatembea bila kujielewaakinyoosha moja kwamoja mpaka darasani, “dah! nime kuwa mjinga sana, ninge omba namba, mbona demu alikuwa poa kabisa” alijilahimu Vicent, akiwa amekaa kwenye kiti chake, na kuegemea meza, kama vile anataka kulala, "hey! niggar vipi mbona umezubaa mwanangu?, yani tumekutafuta pande zote, mpaka kule bustanini, kumbe umekuja kujichimbia class, tena hata assemble ukuja" Vicent aligutushwa kidogo na kuinua kichwa kumtazama alie msemesha, japo sauti alisha itambua, kuwa alikuwa Richard, ni rafiki kipenzi wa vicent, nikama Vicent aliganda kidogo, akimtaza Richard, ambae alishangazwa na rafiki yake,Richard akageuka nakumtazama kijana mwingine alie kuwepo pembeni yake, "vipi Rich mbona leo amepoa sana, yani kama amemwagiwa maji, unanini wewe?" alidakia suma rafiki yake mwengine. maana awakumuelewa mwenzao, Vincent akujuwa amjibu nani kati yao, na awajibu nini, hivyo aliishia kutabasamu kisha akajikohoza kidogo, na kuanza kuwaambia "yani leo najiona kama nipo ndotoni, kwa nilichokutana nacho" ilikuwa sauti iliyo jaribu kuonyesha msisitizo wakile anacho kiongea, "hahahahaha! kashaanza sound zake huyu" alisema suma, huku wote wanacheka,kabla mmoja wao ajakumbuka jambo, "hoya! alafu nimekumbuka, Vannessa alikuwa anakuulizia" aliongea Richard, kama unge msikia unge juwa kuwa huyo Vannesa, alikuwa anainshu muhimu sana na Vicent, maana aliongea kwa msisitizo, "mmh! yani huyo Vanessa naomba usinitajie, maana leo ana nafasi ya kuzungumziwa hapa" alisema Vincent, ila kabla ya kuongeza neno, mara ikasikika "waoooh! jaman baby nilikutafuta huko nje kotesijakuona" wote watatu wakageuza shingo zaona kutazama upande wa mlangoni sauti iliko tokea, macho yao yaka mshuhudia binti mrembo wa ki afrika, alie kuwa anatembea taratibu kuja pale walipo kuwepo wakina Vicent, huyu ni Vanessa alie zungumziwa, “mpaka nikawa na wasi wasi kuwa leo auto kuja” aliongea tna Vanessa, kwa sauti iliyojaa furaha na mania moyoni, Wakati hiuo tayariwanafunzi walishaanza kuingia darasani, Vanesa alienda moja kwa moja mpaka kwa Vicent na kumkumbatia kwa furaha, lakini cha kushangaza kijana huyu akuonyesha ushirikiano, ushirikiano kwa mrembo Vanessa, "baby una nini leo?" alihoji vannessa.kwa mshngao huku anajitoa kwenye kumbatiao lake kwa Vicent, "sina kitu"lilikuwa jibu la mkato,toka kwa Vicent, "sasa kwanini huko hivyo?" aliuliza tena Vanessa, kwa sauti iliyoanza kubadirika na kunyongea, huku wezao wakiwatazama, yani Richard na Ismail wenyewe wana mwita Suma, “nimekuambia niko sawa, unielewi wewe unataka nikuambieje” safari hii Vicent aliongea kwa sauti ya juu, iliyo jaa ukali wa wazi, kihasi cha kulitikisa darasa zima, sekunde kadhaa, wtu wote kimya, wakigeuza shingo zao na kuwatazama wakina Vicent, kwa mshangao. Kitendo hiki akikuwashangaza walewanafunzi wenzao peke yao, ata Richard na Ismail, nao walishangaa, Vanesa alitanzana chini kwa aiu, maana macho yake haya kuweza kutazama, macho ya wanafunzi wenzake me darasani, tenamacho hayo yalishindwa kuya zuwia machozi, ambayo yalianza kumtoka, akika binti huyu, akashindwa kuendelea kusimama mbele ya mvulana ambe sikuzote ame nae karibu, hivyo akageuka na kuondoka zake, huku anakimbia, akielekea nje ya darasa, "una nini mwanangu, mbona kama umeurugwa?" alihoji Richard, huku suma akidakia "mbona si kawaida yako mshikaji wangu" akika wakina Suma walionekana kusikitishwa na kitendo kile, ambacho awakukitarajia, kutokana na ukaribu wa wawili awa, hapo Vicent alikuwa ametulia nikama anawaza jambo, kisha akainua usowake taratibu, "sikilizeni niwaambie washakaji, mimi toka zamani niliwaambia kuwa, Vanesa simpendi, nyie mkasema ooh! mkubalie sijuwi hooooh! mtoto mzuri yule, et! shule nzima wanamfukuzia, bahati imekuja kwako, mala ooh! sasa nimegundua leo kuwa, mwanamke ninaempenda yupo, tena nimemuona, kwa macho yangu" alijibu vincent.marafiki zake wakatazamana kwa mshngao, huku wakimsikia Vicent anaendelea, "leo nimekutana na mwanamke ambae naweza sema ni wa ndoto zangu, sijawahi kujihisi hivi kabla, ila kwasasa ndo naanza kuhisi nimependa kwa mara ya kwanza" Vicent alizidi kuwashangaza marafiki zake, lakini kabla ajawaeleza zaidi juu ya mtoto wa Niram, mara Mwalimu akaingia darasani, na mazungumzo yakaisha kwa muda huo. ****** Vanessa ni binti mmoja mzuri mwenye sura ya duara macho ya kusinzia ana kimdomo furahi hivi cha rangi ya pink, nyuma amefungashia balaha, kiasi cha kupendezwa na kunguo yoyote atakayo ivaa, kifupi kila mwanaume, iwe mtaani au hapa shuleni, alikuwa anammezea mate, na rangi yake ya chocolate ndo kabisa, ilichangia uzuri wake kwa kwa kihasi kikubwa, ikichangia na urefu wake wa wastani,ila binti huyu Vannesa alivutiwa sana vincent mpaka akawa anashindwa kujizuia, japo alikuwa akisumbuliwa na wanaume wengi hadi walimu ila yeye limfanya Vicent kuwa ndie mwanaume wa ndoto zake, Vannesa alijitahidi kufanya kila njia na ushwishi, mpaka akafanikiwa kumfata na kumwambia, ukweli kijana huyu, Ilikuwa ni vigumu kwa vicent kukubali, maana hakuwahi kumpenda msichana, na hakujua afanye nini, ila vishawishi vilimfanya akubali, kwa maana yeye aliona labda ndo inavyokuwa mapenzi yapo hivyo, japo alisumbuliwa na wanawake wengi, ila vicent akuwahi kujihusisha na msichana yeyote yule. Kwahiyo Vanessa ni mwanamke wake wa kwanza, kimahusiano, lakini leo tangu amekutana na Niram alijihisi tofauti, yani kama kuna kitu kina Uchoma moyo wake, hapo ndipo alipojua kuwa, kumbe sasa huku ndiko kupenda kwenyewe, maana ukiachilia kuwa alisha ona waschana wazuri wengi katika maisha yke, yaliki yule binti alimwingia sana moyoni mwake, na kuivuruga hakiri yake, Vanessa aliingia darasani kwao, huku akifuta machozi, kwakutumia kitambaa chakechepe, akiofia wenziewasije wakaona, na kugundua kuwa alikuwa analia, hilisiyo darasa ambalo Vincent yupo, maana walisoma madarasa tofauti, licha ya kuutamachozi na kujaribu kujizuwia kulia, lakini aikuwezekana, maana donge la uchungu lilikuwa lime laa shingoni mwa Vanessaalijikuta anashindwa na kuendelea kuangua kilio cha kwikwi, Vanesa aliwai kwenyekiti chake na kukaa, huku akijizima uso kwakuegemea kwenye meza, akizuwia na mikono yake miwili, ilimuuma sana binti huyu, akika machungu haya ya ghafla, sizani kama nitaweza kuya eezea, "nimemkosea au anipendi tena" alijiwaziwa kimoyo moyo, binti huyu, huku machozi yakizidi kutililika machonimwake na kulowesha mikono yake,mala akastuka kunamtu akimshika begani,aka jifutamacho ziharaka na kumtazama alie mshika begani, "Vanessa una nini, mbona unaonekana kama umetoka kulia" aliuliza Maria, rakifi yake na Vanessa, huku anakaa chini kwenye kiti chakee, pembeni ya Vanessa alimwangalia rafiki yake kwa macho yenye majonzi, hakika kama ungemuona usingetofautisha na mtu aliefiwa, alinyongea kupita kiasi."Maria sijui nimemkosea nini vicent amenikaripia kama mtoto mdogo" aliongea Vanessa kwasautia mbayo nikama kilio kilitaka kurudi upyaa, ila alijitahidi kukizuwia, akaendelea kuzungumza "nilimtafuta sana nje, sikumuona, baada ya kuzunguka kwa muda mrefu, ndo likanijia wazo la kumfata darasani kwao, hakika niliingia kwa bashasha ila nikapokelewa kwa hasira na dharau" mpaka hapo Vanessa alishindwa kuendelea nakuanza kulia kwa kwikwi, ilibidi Maria aanze kumbembeleza kwa kumpiga piga mgongoni, inaonyesha wanafunzi wengine awakujuwa kunacho endelea kwa Vanessa, maana kila mtu aliendelea na mambo yake,******** Mida ya saa nne, ndani ya viunga vya Shadhiliya slamic internation school, yani shuleni kwa kina Niram, mambo yalikuwa shwari, ulikuwa wakati wa mapumziko, wanafunzi walikuwa wametawanyika kwenye viunga vya shule, mida hii binti mrembo Niram, alikuwa na rafiki zake watatu ndani ya canteen ya shule, wanapata chai, mara Niram akawa kama amekumbuka jambo fulani. "jamani mwenzenu leo nimepewa lift na kijana mmoja wa Kiswahili, lakini mzuri sijapata kuona" kabla ajamaliza kuongea binti Niram, akadakia shira huyu nae ni jamii ya kina Niram yani ni muhindi pure kasoro, hawa wengine hajra na Salma, ni tofauti, wakati Salma alikuwa mpemba mweusi, ila Hajra alikuwa Mwarabu kabisaaaaa, "ahhhhh usitake kusema umempenda mswahili, hivi mzee Popat uta mbebea mbebeo gani?, si ata kuchinjaa" alisema Shira, na hapo vikafata vicheko kwa woteee, kasro Niram peke yake ambae alisema, "wala sina mpango huo, ntampeleka wapii mimi, ila nimemsifiatu! sababu katika wavulana niliowai kuwaona, kwa hapa mtanzania, yule kaka ni handsome sanaa" alisema Niram huku anawaangalia marafiki zake, ambao wakakubaliana nae, kwakiikisa vicwavyao juu chini, na wakati huo kengele ya darasani ikagongwa, wakasimama tayari kwa kuanza safari ya kuingia darasani itaendelea ...... ... Read More
Story....... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya Tatu (3) BY GIVAN IVAN Ilipoishia........ Baada ya Penina kuondoka tu, Frank kabla hajapiga hata hatua moja kuondoka pale, ghafla alishtukia amezungukwa na vijana watatu wa kiume waliokuwa wamevalia miwani nyeusi kila mmoja. Na hata Frank alipowaangalia hakuweza kuwafahamu. .......... .. Endelea............ "tulia hivyo hivyo na sikiliza tunachokuambia." akaongea kijana mmoja huku akiwa ametoa kisu na kumuwekea Frank shingoni. Frank naye alikuwa kimya na kuwasikiliza walichokuwa wanataka kumuambia. "sikiliza wewe kijana wewe bado mdogo Sana, hivyo bas tunakusihi uachane na Penina haraka iwezekanvyo, hili ni onyo tu tunakupa na ukikaidi bas shingo yako tutaikata kama ya kuku." akaongea kijana ambaye alikuwa kiongozi wa wenzake, kijana huyo aliitwa Zaza. Baada ya Zaza kumwambia Frank maneno yale ya kumtisha aliondoka na wenzake na kuingia kwenye gari moja nyeusi iliyokuwa imepaki pembeni Yao, Kisha gari likaondolewa kwa kasi ya ajabu huku dereva wao akiwa ni mwanamke anayejulikana kwa Jina la Melissa, moja Kati ya vijana waliopewa kazi nzito ya kuliharibu penzi la Frank na Penina. Frank alianza kuingiwa na hofu na kujiuliza "ni nini tena kinaendelea juu yake? " Frank alijivuta na kuondoka sehemu Ile na kuingia nyumbani kwao akiwa mnyonge kuliko kawaida yake. " eeh kaka vip mbona mnyonge hivyo kulikoni tena? " akauliza Angel mdogo wake Frank. " aah kuna vijitu vinataka kuniharibia siku hapo nje." akajibu Frank na kuketi kwenye kigoda. "watu gani tena hao mwanangu?" akauliza pia mama yake Frank. "mama kuna watu hapo nje wamenisimamisha na kunitishia niachane na Penina la sivyo wataniua." akaongea Frank kuwaambia wazazi wake wakiwa wamepigwa na butwaa. "haa mwanangu katoe taarifa haraka polisi kwa usalama wa maisha yako." akaongea baba yake Frank kumpa ushauri mtoto wake. "Polisi siendi baba nachojua mimi Penina ni mpenzi wangu nampenda na yeye ananipenda, yoyote atakayeingilia penzi langu na Penina ama zake ama zangu na kukuonesha mfano naanza na hawa walionitisha leo." akaongea Frank kwa jazba Kisha akanyanyuka na kuondoka kuelekea chumbani kwake. "kuwa makini mwanangu tusije tukakupoteza mapema." akaongea baba yake Frank, lakini Muda huo Frank alikuwa ameshatoweka mbele ya macho yao. "Mimi ni mwanaume rijali nitakubalije kutenganishwa na Penina kirahisi hivi?" alikuwa Frank akijiuliza swali hilo huku akizunguka zunguka chumbani kwake. "naamini hakuna mwenye uwezo wa kunitenganisha mimi na Penina isipokuwa Mungu tu." akaongea Frank huku sasa akiwa amejilaza chali kitandani kwake.* Hatimaye Penina naye aliwasili nyumbani na Muda huo ikiwa ni majira ya saa tatu usiku. Geti lilifunguliwa na taratibu Penina akaingiza gari ndani na kulipaki sehemu yake, Kisha yeye akashuka na kuanza kuelekea ndani Katika jumba la kifahari kwa mwendo madaha kama kinyonga. Lakini kabla hajaingia ndani alikutana na baba yake mlangoni ambaye alionesha wazi kuwa alikuwa anamsubiri Penina. "shikamoo baba!" akasalimia Penina, lakini baba yake badalaa aitikie salamu ile akamuuliza Penina, "umetoka wapi usiku huu?" "nilikuwa na mpenzi wangu Frank kuna sehemu tulienda ndio narudi Sasa hivi." Penina akamjibu baba yake bila uoga. "wewe ni Mara ngapi nimekukataza kurudi nyumbani kwangu usiku? Na si nimeshakuambia uachane na huyo chokora wako?" akauliza baba yake Penina huku akiwa amezira. "Kwa kosa la kurudi nyumbani usiku naomba unisamehe baba yangu, Lakini muda si mrefu nitakuondolea hii kero ya kurudi nyumbani usiku kwasababu mimi na huyo mpenzi wangu unayemuita chokora tumeshaanza harakati za kufunga ndoa na tutahamia kwetu muda si mrefu." akaongea Penina kumuambia baba yake bila uoga wowote. "hivi wewe mpumbavu unajua unaongea na nani? Maana naona unaropoka ropoka tu kama umekunywa maji machafu." akaongea baba yake Penina. "ndio najua naongea na nani, najua naongea na wewe hapo baba yangu kipenzi tena nakupenda Sana lakini najua wewe hunipendi." akaongea Penina maneno hayo ambayo yalimfanya baba yake apoe kidogo. "hapana mwanangu sio kwamba sikupendi, nakupenda sana tena Sana Ila huyo unayemuita Frank mi ndio ananikera kupita maelezo yaani nikimuona nahisi hata kutapika." akaongea baba yake Penina kwa upole kidogo. "Baba unataka niachane na Frank?" akauliza Penina. "ndio mwanangu tena nitafurahi Sana na nitakupa zawadi kubwa Sana." akaongea baba yake Penina. "ok bas subiri kidogo." akasema Penina Kisha akaondoka kwa Kas mpaka jikon ambapo alichukua kisu na kurudi nacho mpaka kwa baba yake. Wakati hayo yote yanatendeka Noel ambaye ni kaka yake Penina alikuwa akiyashuhudia yote hayo. "kama unataka niachane na Frank niue kwasababu hiyo ndio njia pekee." akaongea Penina huku akimkabidhi baba yake kisu kile. "haa mwanangu Sasa huu utoto gani unaleta mbele yangu?" akauliza baba yake huku akikitupa kisu kile pembeni. "sio utoto baba bali namaanisha ninachokiongea, na kama umeshindwa kutekeleza nilichokuamuru bas tambua hakuna wa kunitenganisha na Frank na siku si nyingi tutafunga pingu za maisha, na sitojali kama wewe utaudhuria ama hutoudhuria." akaongea Penina kumuambia baba yake Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake. Nolan naye alitoka sehemu aliyokuwepo akisikiliza malumbano ya Penina na baba yake na kumfuata Penina chumbani kwake. Huku nyuma baada ya Penina kuondoka, baba yake alitoa simu yake na Mara moja akampigia Zaza. "hallow mzee Joel.!" akaongea Zaza baada ya kupokea simu. "Zaza nisikilize kwa makini, Penina na yule chokora wapo Katika mipango ya kufunga ndoa, Sasa nachotaka mfanye ni kuwatenganisha kwa namna yoyote ile, mnachotakiwa kufanya ni kumteka nyara huyo chokora alafu mkamtupe mbali kabisa sehemu ambayo mnajua anaweza chukua hata mwaka mmoja Kuja kuonana na Penina tena. " akaongea mzee Joel kwa kusisitiza (mzee Joel ni baba yake Penina) " Sawa hamna shida mzee wetu tutafanya hivyo." akajibu Zaza. "ok bas fanyeni haraka iwezekanavyo kama mtahitaji pesa zaidi mtanijulisha." mzee Joel akamwambia Zaza na kukataa simu. * Penina baada ya kuingia chumbani kwake ghafla kaka yake naye akaingia pamoja naye. "hee kaka kumbe ulikuwa nyuma yangu?" akahoji Penina kwa mshangao. "ndio na pia nilikuwa nasikiliza malumbano yenu mzee." akaongea Nolan ambaye ni kaka yake Penina. "yaani kaka wewe acha tu, baba angejua navyompenda asingenifanyia hivi anavyonifanyia." akaongea Penina kwa huzuni kumuambia Nolan. "Ila mdogo wangu usijali wewe simamia kile unachokiamini na mimi nitakuwa nyuma yako kukusaidia." akaongea Nolan kumtia moyo Penina. "nashukuru kaka kusikia hivyo angalau wewe ndio uko upande wangu." akaongea Penina kumshukuru kaka yake. "usijali mdogo wangu wewe lala kwa amani tutaonana kesho." akaongea Nolan na kuondoka chumbani kwa Penina.* Kwa upande wa kina zaza usiku ule ule walianza kupanga mikakati ya kumteka Frank na kwenda kumtupa mbali kabisa na jiji la dar es salam. Lakini hii ilikuwa kazi ngumu Sana ambayo walihitaji pesa za kutosha na pia wachore ramani ya sehemu watakayoenda kumtupa Frank. ....... Itaendelea ... Read More
Story....... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya nane (8) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp....... 0769673145 Ilipoishia........ Lakini Sasa watu wale ambao walikuwa ni wakina Zaza hawakujua wanamfuata nani. Wazimu wa wazimu Nolan naye alifungua mlango na kutoka kwenye gari Lake na kuanza kuwafuata wakina Zaza bila kuwa na uoga wowote.* *************Endelea ********* Zaza pamoja na wenzake walishtuka kuona Nolan anashuka kwenye gari na kuona anawafuata bila wasi wasi wowote. Na baada ya sekunde chache Nolan alikuwa mbele yao. "mnataka nini mbona tunapotezeana Muda?" Nolan akawauliza wakina Zaza huku akiwa amesimama mbele yao. "hahahaaaa Nolan kwa siku ya leo huna bahati leo umeingia pabaya." akaongea zaza huku akimsogelea Nolan. "leo hakika tutakufunza adhabu." akaongea zaza na kumshushia Nolan fimbo ya mgongo, lakini kabla fimbo Ile haijamfikia Nolan aliidaka na kuivunja. Kitendo kile kilimshtua Zaza na kumfanya akasirike kwa fimbo yake kuvunjwa. Zaza alimrushia Nolan ngumi ya uso lakini nayo pia ilikingwa vizuri na Nolan. "acha kupoteza Muda wako kupigana na mimi hata mkiwa ishirini bado hamtaniweza." akaongea Nolan kumwambia Zaza. Lakini zaza hakusikia, akachomoa kisu na kutaka kumchoma Nolan cha tumbo, lakini Nolan alimkamata mkono ule wenye kisu Kisha akamtandika ngumi tatu tumboni za haraka haraka na Kisha akauosokota ule mkono wenye kisu na kuuvunja. Zaza alijikuta akipiga kelele kwa maumivu aliyoyapata. Wale vijana wengine kuona mkubwa amevunjwa mkono nao wakachomoa visu vyao na kuanza kumfuata Nolan kwa kasi. Nolan akawaangalia na kuwapigia hesabu za haraka haraka. "wewe nitakupiga teke la tumbo, wewe wa pili nitakupiga ngumi mbili za kichwa alafu wewe wa tatu na wa mwisho nitatukutoboa kwenye paja la mguu na kisu chako mwenyewe." hizo ni hesabu za haraka haraka ambazo Nolan aliwapigia vijana wale. Na wakati huo huo vijana wale walimkaribia Nolan, na kama Nolan alivyowapigia hesabu aliwafanya vile vile na kila mmoja akadondokea upande wake. "nyie ni kina nani na mnataka nini?" Nolan akamuuliza kijana mmoja kati ya wale wanne aliowapiga. "sijui hata sisi ni wakina nani" akajibu kijana yule. "nitakuvunja shingo jibu swali nililokuuliza." Nolan akamuamrisha kijana yule. "si nimesema sijui sisi ni wakina nani." akajibu kijana yule jibu hilo ambalo lilimpelekea apokee ngumi nzito ya uso kutoka kwa Nolan. Lakini kumbe wakati Nolan anamuhoji kijana yule, kulikuwa na mwanamke mmoja ambaye ni dereva wa kina Zaza yeye alibaki kwenye gari na Nolan hakumuona. Mwanamke yule alishuka kwenye gari taratibu akachomoa kisu chake na kuanza kumsogelea Nolan taratibu bila yeye kujua. Mwanamke yule alipofika sehemu ile aliyokuwa Nolan akimuhoji kijana yule alikinyanyua kisu chake juu kwa mikono miwili na kukusanya nguvu Zake zote na kuanza kuhesabu moja mpaka tatu kwa ajili ya kumshushia Nolan kisu kile cha kichwa. Nolan akiwa bado pale chini akimhoji kijana yule ghafla alishangaa kumuona kijana yule akianza kucheka, kumbe kijana yule alimuona yule Mwanamke ambaye ni mwenzao akijiandaa kummaliza Nolan. Lakini kucheka kwa yule kijana kulimfanya Nolan ahisi kitu. Lakini kidogo hivi Nolan aliona kivuli cha mtu pembeni yake, akageuka haraka kuangalia ni nini kipo nyuma, lakini Ile kugeuka Nolan alikutana na kisu kikija kwa kasi kichwani kwake. Nolan alipojaribu kukikwepa kisu alikuwa tayari ameshachelewa, lakini kwa bahati nzuri kisu kile hakikumpata Nolan kichwani, kwani Ile kugeuka nyuma kulimfanya alindishe kichwa kidogo hivyo kisu kile kikampata Nolan bega karibu na shingo. Nolan alisikia uchungu ambao hajawahi kusikia Katika maisha yake. Lakini mwanamke yule alidhamiria kummaliza Nolan, kwani alikichomoa kisu kile kwenye bega la Nolan na kukirudishia tena pale pale na kumfanya Nolan azidi kupiga kelele kwa maumivu aliyoyapata. Mwanamke yule alikichomoa tena kisu kile na kutaka kummaliza Sasa Nolan kwa kumkata shingo. Mwanamke yule alipotaka kumkata Nolan shingo, Nolan alijijaza licha maumivu aliyokuwa nayo alikikamata kisu. Lakini kwa kukimata kisu kile alijikuta akipokea teke Zito kutoka kwa yule yule Mwanamke na kutupwa mbali. Lakini kwa kupigwa teke lile ilikuwa kama vile Nolan ameamshwa kutoka usingizini. Nolan alinyanyuka na kusimama na kumtizama mwanamke yule huku akiapa lazima amuue. "umenipiga Sana hata wewe Sasa umeisha." akaongea Nolan na kuanza kutoka mbio kumfuata yule Mwanamke. Yule Mwanamke naye akatoka mbio na kuanza kumfuata Nolan huku akiwa na kisu chake mkononi. Walipokaribiana yule Mwanamke akaruka juu huku akiwa amekielekeza kisu kichwani kwa Nolan, Nolan kuona vile naye akaruka juu zaidi ya yule Mwanamke na kupita juu kidogo ya kichwa cha Mwanamke yule na kutua nyuma ya Mwanamke yule. Bila kupoteza hata sekunde moja Nolan aligeuka na kuruka juu na kurusha teke Zito ambalo lilimpata sawia kabisa Mwanamke yule la kichwa na kumuweka chini. Nolan hakusubiri yule Mwanamke anyanyuke, akaruka tena juu na kukunja miguu na kutua kwa magoti mgongoni mwa yule Mwanamke yule na kumvunja mgongoni huku wenzake wakishuhudia lakini wasiweze kufanya lolote kwa kuwa nao walikuwa hoi kwa kichapo walichokipata kutoka kwa Nolan. "wewe lazima nikuue umenijeruhi Sana ngombe wewe." Nolan ndio alimwambia Mwanamke yule Kisha akammaliza kwa kumtandika ngumi nzito ya shingo ambayo ilimpandisha ndege ya kuzimu. Baada ya Nolan kummaliza Mwanamke yule naye alijikuta akidondoka chini na kuzimia kutokana damu nyingi iliyomwangika kutoka kwenye mwili wake. Taarifa zilienea kila mahali kwa mauaji yale yaliyotokea sehemu ile huku wengine wakiwa hoi bin taabani. Polisi pamoja na kikosi cha kutoa huduma ya kwanza kilifika pale na bila kupoteza muda, Nolan pamoja na wakina Zaza wakabebwa na kupelekwa hospital.* Mzee Joel akiwa ametulia nyumbani kwake akipata moja baridi moja ya moto, aliweza kupata taarifa Ile ambayo ilimshangaza Sana. "inakuaje wakina Zaza wako hoi na pia Nolan yupo hoi, kuna nini kilitokea?" akajiuliza mzee Joel bila kupata jibu. Huzuni ilianza upya tena kwa Penina baada ya kupata taarifa ya Nolan mtu pekee ambaye alikuwa akimtegemea kwa chochote, kuwa na yeye yuko hoi bin taabani hospitalini. Bila kupoteza Muda Penina aliingia kwenye gari Lake na kuanza safari ya kuelekea Katika hospital aliyolazwa Nolan, Penina alihisi kuchanganyikiwa hasa akifikiria mambo anayotendewa na baba yake, na pia kupotea kwa mpenzi wake Frank. Hali hiyo ilimfanya Penina akose umakini barabarani na akiwa amebakiza mita chache kufika Katika hospital aliyopo Nolan, Penina alijikuta akikosa balance na kupoteza mwelekeo na kutoka nje ya barabara na kwenda kugonga mti uliokuwa pembeni ya barabara Ile. Pale pale Penina alipoteza fahamu baada ya kugonga mti ule, na alipokuja kushtuka alijikuta yupo hospitalini. Taarifa ilimfikia mzee Joel kwamba Penina amepata ajali Muda mchache uliopita. "shit ni bora afe mtu yoyote lakini sio Penina, utajiri wangu upo kwa Penina." akaongea mzee Joel huku akitoka ndani haraka haraka na kuingia kwenye gari na kuanza kuwahi hospitalini kwenda kumuangalia binti yake Penina.* Baada ya kubangaiza huku na kule kwa siku kadhaa hatimaye Frank alifanikiwa kupata pesa ambayo aliihitaji, na bila kupoteza sekunde, dakika wala masaa, moja kwa moja Frank aliianza safari ya kurudi dar es salam huku mawazo yake yote yakiwa kwa Penina tu Mwanamke aliyempenda kwa moyo wake wote. .......... Itaendelea ... Read More
HOUSE GIRL DIARY; NAITWA RAYA NI HOUSE GIRL MSTAAFU! Nilikua mgeni katika ile nyumba, ingwa haikua mara yangu ya kwanza kufanya kazi za ndani lakini bado nilikua ninaogopa ogopa Dada (Mama mwenye nyumba) alionyesha mkali sana kwani ile kuingia tu alishanipa mashariti elfu kidogo. Nilishaambiwa sehemu ambazo siruhusiwi kukanyaga, vitu ambavyo siruhusiwi kugusa na majina ya kuwaita wote mule ndani. “Sitaki unite Mama unanizeesha unafikiri mimi naweza kuzaa kinyago kama wewe!” Hiyo ndiyo ilikua kauli yangu ya kwanza kukaribishwa nayo mara tu baada ya kumsalimia na kumuita Mama. Kweli hakua mtu mzima, lakini kwakua katika nyumba niliyoondoka nilikua nimezoea kumuita bosi wangu Mama nilijua ni heshima nayeye atapenda kuitwa hivyo. “Huko ulikotoka kwanini ulifukuzwa?” Aliniuliza kwa hasira, sijui hata nilimfanya nini lakini alionekana na kisirani chake tu. “Sikufukuzwa dada niliamua tu kuondoka, walikua …” “Eeeeh! Mimi si shoga yako kuanza kuniambia matatizo yako, nyamaza nishakuambia sitaki kukusikia, nenda jikoni huko! Unajua kupiga au niwakufundishwa kila kitu!” Alinikatisha kabla ya kujielezea kisha kuendelea kufoka. Nilimuambia najua akaniambia niingie jikoni kuanza kazi. Ulikua mchana kwani niliondokea kwa Shangazi yangu (si Shangazi kweli ni mtu ambaye alinilete tu mjini). Niliingia jikoni na kukuta lundo la vyombo, sikua na haja ya kuelekezwa, nilishakua House Girl mzoefu hivyo nilijua nini cha kufanya. Nilianza kuosha na ulipofika wakati wa kupika nilimuuliza tunapika nini. Nashukuru safari hii alinijibu vizuri hivyo nilichukua kile nilichelelekezwa na kumpikia. Kutokana na kelele za nyumba niliyotoka na uzungu wa Bosi wangu wa zamani nilikua najua kupiga si kitoto, ile milenda milenda yangu ya kijijini niliiacha huko huko hivyo nilipompikia tu na kuweka chakula mezani, alikifurahia ingawa hakusema chochote lakini hakulalamika, hiyo ilikua dalili njema kwangu. Katika nyumba niliyotoka baada ya kuwatengea chakula nilikua nasubiri mpaka wamalize kula, hii ni kwasababu kama kikitokea kitu cha kutumwa basi niwepo kuwasikiliza. Huwa nasimama pembeni kama wale madhouse girl wa kwenye TV kusubiria mpaka mabosi wangu wamalize kula ndiyo huingia jikoni na kujitengea chakula changu. Nilishazoea hivyo na kwakua ilikua ndiyo nyumba yangu ya kwanza nilijua labda mjini kote ndiyo hali ilivyo. “Unasubiri nini hapo si uende jikoni huko ukajipikie au wewe huli?” Aliniuliza kwa hasira, nilitaka kumjibu kumuelezea nilivyozoea lakini hakutaka kusikiliza, jicho alilonikata niliondoka kama chizi nikikimbia. Nilifika jikoni na kupakua chakula, nilikaa chini ili kula. Lakini kabla hata sijafikisha tonge mdomoni alikuja, alikua kasimama pembeni yangu. “Ndiyo unafanya nini?” Aliniuliza, macho yake yalikua katika chakula. “Nakula ma…dada…” Kidogo nisahau na kumuita Mama. “Pumbavu unakula nini? Yaani unakula chakula ambacho ninakula mimi! Hivi una akili kweli unataka kuwa sawa na mimi, nikulipe elfu thelathini na chakula ule kama mimi!” Aliongea kwa hasira, alikipiga teke chakula kisha kutoka, alirudi na ndoo ya dagaa na kunirushia. “Kuna ndoo ya dona iko hapo, pika ugali wako ule. “Aliongea kwa hasira huku anaondoka, alienda kwa sekunde kadhaa na kurejea. “Upike mwingi kuna mwenzako anatoka shule atakuja kula na wewe!” aliondoka na kuniacha pale. Nilianza kuchambua Dagaa ambao wengi walikua wameoza, unakutana na wadudu kabisa. “Haya mapya! Nimeruka mkojo nimekanyaga mavi!” Niliendelea kujiongelesha huku nikichambua dagaa ambao walishaanza kunitia kichefuchefu. Huko nilikotoka nilikua nanyanyaswa lakini angalau nilikua nakula chakula cha mabosi wangu hata kama nilikua nalia jikoni! *** Jioni jioni hivi kama saa kumi na nusu watoto wake walikuja, walikua watatu. Mmoja mkubwa kuliko wenzake Jackline na wengine wadogo Joan na John, hawa walilingana kwani walikua mapacha. Baada ya kubadilisha nguo niliambiwa niwatengee chakula, nilifanya hivyo kwa kuweka sahani tatu mezani. Lakini Jackline ambaye alikua na miaka kumi hakukaa mezani, alikuja jikoni ambapo nilikua naandaa chakula cha usiku. “Wewe ndiyo Dada mpya, shikamoo…” Alinisalimia tena kwani alishanisalimia wakati nawafungulia geti ili waingie. Niliitikia kwa wasiwasi kwani nilishaambiwa nisiongee na wanae hivyo niliogopa hata kumjibu salamu. “Chakula changu kiko wapi?” Aliuliza, huku akikaguakagua vyombo. “Chakula si nimeshawatengea sebuleni?” Niliuliza kwa mshangao, hasira zilinipanda kidogo kwani nilishajua kuwa kumbe mbali na kudili na Bosi kichomi basi ningedili na mtoto mdogo kama yule ambaye ana kisirani. “Baba amesafiri mimi siruhusiwi kula sebuleni nnatakiwa kula na wewe!” Sikumuelewa niliuliza mata mbilimbili ndipo kwa utulivu kabisa alinieleza kuwa yule hakuwa Mama yake mzazi bali ni Mama wa kambo hivyo kila Baba yake anaposafiri yeye haruhusiwi kula chakula sebuleni na wengine mpaka anaporejea. Chakula anachokula ni cha Dada wa kazi. Kusema kweli hilo lilikua jingine jipya, labda kwakua nilikua sijafanya kazi katika nyumba ambayo Bosi ana mtoto wa kambo. Niliwaza kile chakula ambacho nilipika kwaajili yangu, nikawaza wale dagaa kisha nikamuangalia yule mtoto na kumuambia. “Jack, si unaitwa Jack… “Nilimuuliza. “Ndiyo Dada!” Alijibu kwa upole. “Huwezi kula kile chakula, hata mimi kimenishinda, hembu ngoja nikutengee kingine, mbona kiko kingi tu watamwaga hawa!” Niliongea huku nikimtafutia sahani ili kumpakulia chakula lakini alikataa katakata, aliniambia nitapigwa sana kama nikila chakula kingine. Alinionea huruma mimi pia nakuniambia hata Dada mwingine alifukuzwa kazi kwakua alikua ananipakulia chakula cha wengine. Alionyesha kuogopa mpaka na mimi nikaogopa kwa namna alivyokua anaogopa. “Huyu ni mwanamke wa namna gani mbona yuko hivi!” Niliwaza nikimuangalia Jackline, alikua kachoka lakini alijitahidi kuonyesha yuko sawa, mara kwa mara alikua akitabasamu huku akijilazimisha kucheka. Aliniongelesha ongelesha kutaka urafiki, kweli nilimuonea huruma machozi yalinilengalenga. Kwangu ule ulikua ni mtihani mpya ambao sikujua nitaumalizaje. *** Siku mbili baadaye Baba mwenye nyumba alikuja, huyu yeye niliambiwa nimuite Baba na nilifanya hivyo bila kuuliza maswali. Alikua ni kijana tu wa makamo au sijui niseme mtu mzima mwenye muonekano wa kijana. Alikua mchangamfu na alipokuja kila mtu alikua na furaha, si Jackline au watoto wake wengine nyumba ilikua kama imemwagiwa gunia la furaha. Hakukua na kupika mara mbilimbili, hata mimi niliambiwa nikae kwenye meza kubwa, hakukua na kutumwa tumwa kwani Baba akiwepo wakati wa kula ni kula na wote alituchukulia kama wanae. Ilikua ni kama unaishi katika nyumba nyingine tofauti kabisa, Dada alikua mchangamfu akiongea kwa kucheka mara kadhaa akimkumbatia Jackline. Hata mimi alinitambulisha kwa bashasha akinisifia kwa ufanyaji kazi wangu. Kweli nilishangaa “Mbona sielewe, huyu Mama yako wa kambo mbona kama anabadilika sana kama si yeye?” Nilimuuliza Jackline, alijiibaiba kukaa jikoni wakati wenzake wakiangalia TV, Baba yake akiwepo alikua haruhusiwi kufanya kazi yoyote. “Nimeshamzoea, anaigiza tu Baba akiwepo?” “Kwahiyo Baba yako hajui chochote?” “Hapana, nilishamuambiaga zamani lakini hakuniamini, niliishia kupigwa tu. Nilimuambia Mama kwanza aliposema kwa Baba akaambiwa nina wivu hivyo kukatazwa hata kuja kuniona, ilileta ugomvi mkubwa siku hizi kila nikilalamika naambiwa nimetumwa na Mama kuja kumfitinisha Mama Mdogo…” “Mama yako wewe yuko wapi? Kwanini huendi kuishi na Mama yako?” Yuko kijijini, waligombanaga na Baba zamani, hawakuoana, Baba alinichukua nikiwa mdogo na kunileta hapa, mimi sijui mambo hayo ila Mama yangu naongea naye tu kwenye simu mara moja moja lakini simkumbuki hata sura, hata sijui mimi mambo yao.” Aliongea kana kwamba ni mtu mzima, alionyesha kupitia mambo mengi na hakukua na mtu wa kumsikiliza. Nilipokuja kufuatilia nilikuja kugundua kuwa Mama yake na Baba yake hawakua wapenzi, ni watu tu walikutana na mimba ilipotokea basi Mama yake alivyokua akidai matumizi kipindi hicho ashaoa aliamua kumnyang’anya mtoto kwa nguvu. Kwao ni Iringa hivyo alimnyang’anya na kumchukua kipindi akiwa na miaka minne na tangu wakati huo alikua akiwasiliana naye kwa simu tu. Ana Mama yeka mkubwa, Dada wa Mama yake ambaye yuko Dar lakini naye haruhusiwi kumuona kwani ndiyo alimuambia kuhusu manyanyaso na kumuambia Mama yake ambaye alipoongea na Baba yake ukawa ugomvi mkubwa. Sikua na la kuongea zaidi ya kunyamaza tu kwa namna alivyokua akiongea ni kama alishakata tamaa ya maisha muda mrefu, sikujua ni kwa namna gani naweza kumsaidia kwani hata mimi nilikua na matatizo yangu. Usiku wakati wa kulala sikuolazwa stoo kama kawaida, hapana, niliambiwa natakiwa kulala katika chumba kimoja na Jack. Ulikua ni utaratibu wao, Baba akiwapo na mimi nakua mtoto na lala chumba kimoja na Jack. Usiku baada tu ya kuingia Jack alizima taa, nilishangaa kwani hata kitandani nilikua sijafika, nilimuuliza kwanini anazima, nikihisi labda ni Mama yake hapendi. Nilisogea na kuwasha, alishtuka, ni kitu amcho hakukitegemea. Alikua anavua nguo ili kuvaa nguo za kulalia, nilipowasha taa tu alianza kujificha kama vile anaona aibu. Nilishangaa kwani mimi ni mwanamke mwenzake, “Dada zima taa, zima taaaa!” Alipiga kelele, alionyesha kushtuka akijificha, lakini badala ya kuficha hata sehemu za siri alikua anaficha mgongo wake. Nilitaka kuzima lakini kabla ya kufanya hivyo macho yangu yalitua katika mgongo wake, ulikua kama ramani ya Tanzania, ulijaa makovu mengi ya fimbo, mengine mabichi kabisa kama vidonda. Sikuzima, sasa nilijua sababu ya yeye kuzima taa hakutaka nione makovu. Nilisogeza macho mpaka kwenye mapaja na sehemu za siri huko ndipo kuliharibika zaidi. Hapo ndiyo nilijua ni kwanini mara kwa mara huwa anakunja uso hata akiegemea sehemu au kugusa mapaja yake. Nilimsogelea na kumkalisha chini, alianza kulia kabla ya kusema chochote. “Kwanini humuambii Baba yako, kwanini humuonyeshi haya makovu? Akiona atakuamini!” Niliongea kwa hasira, sikua na muda pale lakini kwa upendo aliokua nao yule Baba sidhani kama angeweza kumuona mwanae katika hali ile na kunyamaza kimya. “Namuambia Baba yako, hii kazi ishanishinda, ngoje nifukuzwe lakini niondoke na huyu Sherani!” Niliongea huku nikinyuka kwenda kumgongea Baba yake, tayari walishaingia chumbani kulala. Jack alinifuata akilia kunibemebeleza ili nisiende akiogopa kuwa atamuua lakini sikujali, nilijua ni uoga ambao mimi kama mtu mzima nisingeweza kuuruhusu. Ushahidi alikua nao na hakukua na haja ya kuendelea kuteseka hata siku moja katika nyumba ya Baba yake. Alinisihi sana lakini sikumsikiliza, nilitoka mpaka sebuleni, alinifuata akiwa vilevile uchi kasahau kuvaa nguo, analia, nilielekea mpaka mlangoni kwa wazazi wake. Bado alikua analia, huku akiongea kwa kunong’ona. “Dada Raya, Dada Raya usimuambie, usiongee chochote, mimi niko sawa niliumia Shuleni, sio Mama aliyenipiga, ni ukorofi wangu tu!” Alipiga kelele kuniomba nisiseme. ITAENDELEA… (Hiki ni kisa cha kweli ingawa majina yaliyotumika hapa hayahusiani na wahusika. Hii ni sehemu tu ya simulizi kutoka kwa wadada wakazi “House girls” ambazo nitakua nikiwaletea. Je unadhani kama Raya atagonga mlango na kumshitaki Mama wa kambo, je Baba Jack akiambiwa atachukua hatua gani, kesho si mbali sana tukutane kwa sehemu ya pili hapahapa kwenye ukurasa huu…” ... Read More
*LOVE BITE EP 05* 🌹🌹🌹🌹🌹💞💞💞🌹🌹🌹 MWISHOOOOOOO “OOOOH MY GOD……..WHY ME?????” Alijikuta nguvu zinamuishia Jothan na kukaa chini. Aliiangalia nyumba yake aliyoijenga kwa gharama kubwa na machozi yalianza kummiminika kama maji. ITAENDELEA………… Alsimama na kuamua kwenda kwa rafiki yake John ambaye alikua anakaa magomeni. Alikaribishwa ndani na mke wa rafiki yake huyo na kukutana na rafiki yake sebuleni kwake. Walikumbatiana kwa kuwa siku nyingi walikuwa hawajaonana. Kwakua muda wa msosi ulikua unakaribia, mke wa John alipakua chakula na baada ya dakika kumi waliitwa kwenye meza ya chakula. Walikula huku kila mmoja akijaribu kumuhadithia mwenzake yaliyotokea nyuma kwa kipindi chote hicho cha takribani miezi nane. Jothan ndiye alikuwa wakwanza kumuhadithia mwenzake yaliyomkuta kuanzia safari yake ya Arusha hadi kufikia pale alipoenda kwenye nyumba yake na kukuta imeuzwa na mwanamke aliyekuwa anampenda na kumuamini kupita maelezo. John alisikitika sana kuisikia story ile iliyomuumiza hata yeye. “usijali rafiki yangu,. Kuhusu pa kukaa tu. Hapa umefika maana kuna vyumba vingi vya kutosha. Sasa vipi kuhusu docomments zako muhimu kama vyeti na vitambulisho vyako?” aliuliza John kwa kugundua umuhimu wa hivyo vitu. “ndio maana nikakwambia kuwa nimechanganyikiwa sana. Yaani sijui nianzie wapi?” aliongea Jothan huku akionyesha wazi kuwa akili yake imeeshia pale kimawazo. “usijali, vitapatikana tu.” Aliongea John na kuonyesha wazi nia yake thabiti ya kumsaidia rafiki yake huyo. “vipi kazini, wameshamuajiri mtu mwengine wa kukaa katika nafasi yangu?” aliuliza Jothan huku akionyesha wazi kuwa na wasi wasi na nafasi yake ya kazi. “mbona company imeuzwa kwa mzungu ambaye kaamua kuibomoa na kujenga hotel. We ukienda utaona tu mabati yamezunguka katika jengo la ofisi yetu. Sasa angalau ungekuwa na docoments zako zingekusaidia kupata malipo na mafao yako kutoka NSSF.” Aliongea John na kumfanya Jothan ashike kichwa kwakua alikua anaamini kuwa maisha yake yanaweza kunyanyuka tena kama akivipata vitu vyake muhimu. Kadi za benk, nyaraka mbali mbali na vyeti vyake alivyovihangaikia kuvipata ndivyo vilimnyima raha Jothan. “mimi hivi sasa nimeajiriwa na kampuni ya Fast jet. Hata wewe ungekuwa na vyeti vyako tungekuwa tunafanya kazi wote . Maana watu wenye sifa kama zako wanahitajika sana pale.” Aliongea John na kumfanya Jothan ajiinamie. Walikaa pamoja na baadae Jothan alielekezwa chumba atakachukuwa analala. Usiku baada ya kula chakula, alienda chumbani kwake Jothan na kulala. Asubuhi ilipofika, John alimgongea Jothan na kumuaga. Alitoka na kwenda zake kazini. Aliandaliwa chai Jothan na shemeji yake baada ya kuamka asubuhi na kutoka sebuleni. Alikunywa chai na kwenda chumbani kwake. Alioga na kubadilisha nguo. “shemeji.. natoka kidogo.” Aliaga Jothan na kuondoka. Alienda kinondoni ili kuangalia kuwa kama watu walionunua ile nyumba yake wameshahamia. Alikuta hali ile ile ya kama alivyoiacha. Alijitahidi kumuulizia Shani kwa majirani wa pale, lakini hakuna hata mmoja aliyempa majibu chanya juu ya kumpata Shani. Roho ilimuuma kila akiitazama nyumba yake. Alilia sana na kuamua kukubali yote kuwa hata kama atalia na kumaliza machozi yake, basi hawezi kuirudisha nyumba yake. Alirudi nyumbani kwa rafiki yake aliye muhifadhi na kwenda chumbani kwake. Alikaa huko na baaae aliitwa na shemeji yake wakati wa chakula cha mchana. Walikula pamoja na rafiki yake aliwasili pale baada ya nusu saa. “leo nimechelewa kurudi kwa sababu nilikuwa nashughulikia swala lako kwa kuvitangaza vyeti vyako kwenye magazeti mbali mbali yatokayo kesho.” Aliongea John na kumfanya Jothan afurahi kusikia hivyo. Alikaa pale kwa wiki mbili zilizokwenda kwa amani. bada ya hapo, alianza kupata mitihani midogo midogo kutoka kwa Shemeji yake huyo aliyekuwa anapenda kumuonyesha tabasamu kila wakati. Kadri siku zilivyozidi kusonga mbele, ndivyo majaribu kutoka kwa shemeji yake yalivyopamba moto hadi kufikia kuingia chumbani kwake akiwa na upande mmoja wa khanga nyepesi iliyoonyesha kila kitu alichokivaa ndani. Alimuonya mara kadhaa lakini bado msichana huyo aliyekumbwa na pepo wa ngono juu yake alizidi kumuandama. Kamwe hakupenda kuwa sehemu ya tatizo . Alipenda kuwa mtatuzi wa tatizo. Baada ya kuona visa vinazidi kutoka kwa mke wa rafiki yake. Aliamua kuihama nyumba bila kumuambia rafiki yake sababu iliyomuhamisha pale nyumbani kwake kwa kuhufia kuharibu ndoa ya watu waliodumu kwa takribani miaka kumi. Japokuwa hakua na pa kwenda, ila aliamini kuwa kufanya vile basi Mungu atamnyooshea njia yake.. Fedha kidogo alizokuwa nazo zilimuwezesha kujihudumia mwenyewe na kulala gesti kwa wiki moja tu. Baada ya hapo alikuwa choka mbaya. Hakuwa na hata senti tano. Siku hiyo aliamua kuuwa winga kwa kushinda na njaa hadi kiza kilipoingia. Hakuwa na mahali pa kulala, aliamua kwenda kukaa stendi ya daladala maeneo ya kinondoni huku akimuomba mungu usiku ule ukuche akiwa salama maeneo yale. Masaa yalisogea na usiku mnene ulianza kutokea baada ya idadi ya magari kupungua huku watu waishio maeneo hayo kutoonekana nje. Hata yeye mwenyewe hakujua alipataje usingizi. Ila alishtuka baada ya kuona mwanga mkali wa taa za gari ukimulika maeneo aliyokuwa yeye. Alishtuka na kuyazuia macho yake kwa mikono kutokana na ukali wa mwanga wa taa zile. Sekunde kadhaa baadae, zile taa zilizimwa , mara akaona mlango unafunguliwa wa ile gari aina ya Range na kiatu aina ya high hills kikionekana kikikanyaga ardhi. Hali hiyo ilimonyesha kuwa mtu ashukaye kwenye ile gari ni msichana. Uteke wa mguu ule pia ulimuwezesha Jothan kupima age ya mtu anayeshuka. Wakati anausumbua ubongo wake kufikiria na kuwaza lengo la yule mtu kupaki gari lenye thamani pale, yule mtu alishuka na kufunga mlango. Kutokana na mawenge ya taa, hakuweza kumuona mtu aliyekuwa akizihisabu hatua kuelekea pale alipo. Yule dada alimsogelea mpaka pale. Hakuamini alichokiona mbele yake, alikuwa msichana wa ndoto zake toka alipokuwa anasoma. Hakujua ni kitu gani kilichomsukuma mpaka kufika maeneo yale. Ila aliamini kuwa ni Mungu pekee ndio amekisikia kilo chake na kuamua kuwakutanisha tena pale. “PRISCA???”” Alinyaanyuka Jothan na kuita kwa mshangao mkuu huku akiwa haamini macho yake kuwa yule ndiye Prisca wake wa zamani. Bila kujibu chochote, yule dada alianguka kifuani mwa Jothan huku machozi yanamtoka. Hakuamini Jothan macho yake. Alimuangalia Prisca ambaye alikua anafuta machozi yake. “tuondoke eneo hili, sio salama Jothan.” Aliongea Prisca na kumchukua Jothan na kwenda naye kwenye gari. Safari ilianza huku kila mtu akiwa amenyamaza bila kuongea chochote. Jothan alishangaa kuona gari linaelekea mtaa aliokuwa anakaa yeye zamani kabla ya nyumba yake kuuzwa. Gari lilipiga honi kwenye geti la nyumba yake Jothan. Mlinzi alifungua mlango na Jothan hakuamini kuwa mmiliki wanyumba yake ni Prisca. “siamini Prisca kama ni wewe ndio umeinunua nyumba hii?” aliongea Jothan baada ya kuingia kwenye nyumba ile ambayo haikubadilishwa kitu chochote zaidi ya rangi tu. “siku zote huwa napenda kukuona ukiwa mwenye furaha. Ndio maana niliposikia nyumba hii inauzwa ndipo niliamua kuinunua kwa sababu sikupenda ipotee kwenye upeo wa macho yako. Sio nyumba tu, na kila kilichukuwa ndani pia nimevinunua. Hata gari lako pia ukilihitaji nitakupatia kwa sababu kwa sasa halipo hapa. Nimevinunua vitu vyote hivi kwa ajili yako Jothan.” Aliongea Prisca huku machozi yanamtoka. Jothan naye hakuweza kuyazuia machozi yake na kumfuata Prisca na kumkumbatia. “moyo wa mtu ni kichaka Prisca, sikuweza kufikiria kama ipo siku Shani angeweza kuyabadili maisha yangu na kunifanya niwe hivi… nashukuru sana kwa yote uliyoyafanya kwa ajili yangu Prisca.” Aliongea Jothan maneno yale na kumfanya Prisca azidi kulia. “kesho nitachukua begi langu na kuondoka. Maana kazi yangu ya kukutafuta wewe nimeshaimaliza Jothan.” Aliongea Prisca na kumuangalia Jothan ambaye wote walikuwa wanalia wakati huo. “hapana, hutakiwi kuondoka Prisca. Na kama utaondoka basi hii numba na kila kitu kilichomo humu ndani bado vitakuwa havitoshi kutimiza furaha yangu bila ya wewe kuwa karibu yangu.” Aliongea Jothan huku analia. “mimi sio chaguo lako Jothan, siwezi kukaa karibu na wewe. Nitakuwa naumia roho tu na sitaweza kuvumilia kukuona ukiwa na msichana mwengine mbele yangu.” Aliongea Prisca huku analia kwa uchungu. “nilikosea kuchagua kwakua sikujua upi ni mchele ni zipi ni pumba. Niliacha mchele kwakua pumba zilinivutia angi yake. Leo najuta kwakua pumba zimenilaza njaa. Wewe ndio mchele wa kunifanya nishibe na kunitoa njaa hii ya kufa inayonikabili. Nakupenda sana Prisca.” Aliongea Jothan na kujikuta ameeanguka kwa magoti mbele ya Prisca ambaye wakati huo na yeye alikuwa haoni vizuri kutokana na ukungu wa machozi ulikuwa kwenye macho yake. “toka siku uliyonikana Jothan kule Peacock hotel kuwa mimi sio chaguo lako. Moyo wangu uliingia ganzi na kuamua kuishi single Jothan. Sihitaji tena kupenda kwakua nina bahati mbaya ya kupenda nisipopendwa. Sipendi kuumizwa tena kwakua maumivu yake siwezi kuyastahimili. Nikuache tu na maisha yako na mimi naiche na maisha yangu” aliongea Prisca kwa uchungu maneno yalimchoma sana Jothan ambaye bado alikuwa analowanisha viatu vya Prisca kwa machozi yake pale chini. “nisamehe mimi, nimeshajifunza Prisca,” aliendelea kuomba Jothan huku sauti iliyojaa uchungu ikiendelea kumtoka mtoto wa kiume. Nguvu ya mapenzi inaweza kuhamisha milima, wahenga walisema hayo na mimi nawaunga mkono kwa kusadiki maneno hayo. Prisca alijikuta anamnyanyua Jothan na kumkumbatia. Wote walilia sana na kila mmoja kwa muda wake alimbembeleza mwenzake kwa mumfariji. Ukurasa mpya wa mapenzi kwa wapendanao hao walioanza mapenzi toka walipokuwa shuleni yalianza kwa kasi kubwa. Hakukua na sababu ya kuchunguzana wala kupeana muda. Walikubaliana kupima ukimwi kabla ya kufanya mapenzi. Zoezi hilo lilifanikiwa kwa asilimia mia moja. Wote walikuwa wazima na mipango ya ndoa ilifanyika haraka. Vitu vyote vilivyokuwa kabatini alivikuta vile vile. Kasoro hati ya nyumba tu ambayo alirudishiwa na mpenzi wake Prisca. Alifurahi sana na kwenda kupeleka cv zake kwenye kampuni ya Fast jet. Alipata kazi haraka na kuungana na rafiki yake kipenzi John. Ndoa ya aina yake ilifungwa kati ya Jothan na Prisca. Wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walihudhuria harusi ile. Kwenye Hight table walikwepo John na mkewe, Bahati na mumewe Saimon pamoja na mama yake. Hakika furaha ambayo ilipotea kwa muda mrefu kwa Jothan ilirudi alifurahia uwepo wa watu hao muhimu katika maisha yake kwa vipindi tofauti.. Miezi saba baadae, Jothan na mkewe Prisca walikuwa wanatoka kwenye matembezi yao usiku wa saa sita. Wailpofika msasani. Walilakuta wasichana wengi walikuwa wamejiremba na kuvaa nusu uchi wakiashiria kuwa walikuwa wanauza miili yao. Jothan hakuamini kumuona Shani akiwa amejiingiza kwenye kundi hilo. Alisikitika sana kumuona Shani akikimbilia magari na kuanza kujinadi kama wafanyavyo mada wengine wanaojiuza hapo. Alisimamisha gari lake na kumuangalia mkewe ambaye alimpa ishara ya kuondoka na kumuacha mwanamke huyo na maisha yake. Walirudi nyumbani na kumshukuru Mungu kwa kuwaunganisha tena na kuyahesabu yote yaliyotokea nyuma ni mitihani tu, na wao ndio couple iliyokubaliwa na Mungu. ***********MWISHO************** Maisha ni sahani iliyojaa mazuri na mabaya. Kuna wakati unaweza kukubali kuwa maisha ni jinsi unavyoishi. Ila wapo wanaoishi nje ya malengo waliojiwekea. Hakuna anayependa kupata hasara, ila kama una muamini Mungu basi utaamini kuwa kupata hasara katika jambo Fulani ni moja ya mitihani na huenda mungu amekuEpushia kitu Fulani katika jambo hilo. Kila hatua unayopitia ni moja ya changamoto katika mafanikio yako. Ukianguka jikaze na jaribu kuruka tena hata kama utasikia maumivu. Tochi ya mungu hummulkika kila mtu isipokuwa kwa atakayekataa mwenyewe. Ridhiki ya mtu ipo kwenye mikono yake mwenyewe ndio maana huwezi kuizuia. Mungu ametoa vitu vitatu vikubwa kuliko Mali. Kwanza Mungu katoa akili za kipekee. Nikisema akili za kipekee namaanisha kuwa kila mtu Mungu kampa akili lakini hawa wenye akili za kipekee huweza kufanya mambo makubwa na ya kushangaza hali ambayo mtu uliyepewa akili ya kawaida huwezi kufanya hata kama una pesa. Pili Mungu katoa vipaji. Mtu mwenye kipaji Fulani basi huweza kufanya mambo makubwa ikiwemo kufikisha ujumbe haraka kwa watu kutokana na kukubalika na watu wengi zaidi ya mtu wa kawaida. Kimfano matangazo, tangazo hilo akipewa mtu Fulani atangaze basi muitikio utakuwa mdogo kuliko akipewa tangazo hilo Diamond, Mrisho Mpoto na wengne wengi. Kipaji ni kitu cha pekee alichotoa mungu kama zawadi kwa mtu Fulani na kama kitathaminika na yeye kukiwekea mkazo basi hiyo ndio inaweza kuwa njia ya mafanikio yake kupitia kipaji hicho. Tatu mungu katoa Moyo wa pekee. Moyo huu amewapa watu wachache. Na cha ajabu kuwa mtu mwenye moyo wa kutoa basi hutoa kitu kikubwa bila kujali kubakiwa na kidogo. Humshinda mwenye mali ambaye akitoa hata kitu kidogo huhisi anapungukiwa. Mtu mwenye moyo wa pekee hupenda kutenda mambo yanayompendeza mwenzake hata kama yanaweza kuharibu furaha yake. Hapendi kumuona mtu akilia au akihuzunika wakati yeye anaweza kumfanya mtu huyo kuwa na furaha hata kwa kumuongopea. Hawezi kula yeye kabla ya kuangalia wenzake wenye njaa. Hayo na mengine mengi kajaaliwa mtu mwenye moyo wa pekee. Na huwashinda wenye vipaji na akili za pekee. Watu hawa mungu huwajaalia kwa kuendelea kuwapa na kutia Baraka mali zao hata kama ni kidogo. Nia na madhumuni ni kujifunza kupitia burudani hii iliyowaacha watu kwenye majonzi au kufurahia mwisha mzuri wa Jothan kuwa na mtu ampendaye. *****************************************MWISHO****************************************** ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: