Home → simulizi
→ KURUDI KWA MOZA: 39 Walifika kituoni na kushuka kisha safari ya kuelekea kwenye maombi ikaanza sehemu yenyewe haikuwa mbali na kituo cha basi, wakati wanakaribia kufika Salome alimuomba mama yake kuwa aende dukani kununua maji mara moja kwani alikuwa na kiu sana, Neema alikubali kisha Salome akaanza kwenda dukani ambako napo hapakuwa mbali sana, ni nyuma kidogo tu na walipokuwa. Neema akaona kama mwanae anakawia dukani na kuamua kumfata, ile anafika dukani tu alishtukia akiwa nyumbani kwake tena bado yupo chumbani kitandani yani ndio anaamka. Neema alishangaa sana na kujiangalia mara mbili mbili, ni kweli alikuwa ametoka kuamka ysni hata kuoga alikuwa hajaoga, “Jamani haiwezekani, yani iwe sijaamka mpaka muda huu kweli!” Akachukua na simu yake kuangalia saa, akaona ni saa tano asubuhi na kuzidi kushangaa kwani hata kwakama kwa kawaida hana tabia hiyo ya kulala mpaka saa tano asubuhi, mara nyingi akichelewa sana basi anaamka saa mbili ila siku hiyo ilimchanganya zaidi, akajaribu kukumbuka kuwa alishajiandaa na Salome walikuwa wanaenda kwenye maombi na mara ya mwisho Salome alimuomba kuwa anaenda kununua maji halafu alikawia sana dukani, ila alipomfata dukani ndio akajikuta yupo kitandani tena akiwa naio kwanza anaamka, akajiuliza “Hivi naota au ni kitu gani? Lakini sioti jamani mbona nilikuwa macho jamani ndoto gani hii?” Neema alijiuliza maswali kadhaa bila ya majibu, akaamua kutoka ili ajaribu kuona kama anaota au la. Alitoka na kumkuta Salome akiwa anaandaa kifungua kinywa, na alipomuona tu alimuamkia, Neema alishangaa sana na kumuuliza Salome, “Inamaana bado hatujaonana?” “Tumeonana muda gani tena mama? Si ndio umetoka kuamka?” Neema akaganda kwa muda kisha akamwambia Salome, “Hivi mimi na wewe hatujaenda mahali leo?” “Mama unaota ua?” “Sijui mwanangu, yani sijui kabisa ila ninachojua ni kuwa tulijiandaa kwenda kwenye maombi, na tulifika kabisa ila wewe ukataka kununua maji, nimekufata gafla nikajikuta kitandani ndio naamka” Salome alicheka sana, kisha akamuangalia mama yake na kumwambia, “Mama jamani mbona vichekesho hivyo yani uende mahali halafu ujikute gafla umelala ndani yani ndio unaamka! Unaona hilo jambo linawezekana kweli?” “Hata mimi nashangaa mwanangu, yani sielewi kabisa” “Hiyo ni ndoto mama isikupe presha” “Yani hata sijui, sijui kabisa yani” “Usijali mama ni ndoto hiyo” Neema alikaa kwenye kochi sasa, huku akiwa na mawazo tele kuhusu yale mauzauza aliyoyapata maana hakuelewa kama ni ndoto au ni kitu gani. Alijifikiria sana bila ya majibu, wakati anawaza vile akashtuliwa na Salome na kumwambia, “Natoka mama” Alitaka kuongea jambo ila hakuweza kuongea chochote zaidi ya kumuitikia mwanae tu kuwa wataonana badae. Ndugu wa mama Jack leo waliendelea kufanyiwa dawa na Yule mganga, Yule mganga aliwaambia kuwa anaona kitu sio cha kawaida kimefanyika kisha akawaambia, “Inaonekana mama Jack katolewa kafara na rafiki yake” Wakashangaa sana, na kuuliza kuwa ni rafiki yake yupi ambaye kamtoa kafar mama yao, “Huyo rafiki yake anaitwa Rose” Watoto wa mama Jack wakashangaa sana kwani mama yao siku zote alikuwa akimsifia huyo Rose ingawa hawakujua kuwa Rose anapatikana sehemu gani. Yule mganga aliendelea kuongea, “Yani huyo Rose anapenda sana mambo ya waganga wa kienyeji ndiomana kajikuta kamtoa rafiki yake kafara, mama yenu kosa lake ni kumsindikiza huyu Rose kwa mganga yani huyo Rose anapenda sana mambo ya waganga ndio yanayomghalimu.” Walimshangaa mtoto mmoja wa mama Jack akishindwa hata kuendelea kumsikiliza mganga bali aliinuka na kuondoka zake. Alienda moja kwa moja nyumbani kwao na kuchukua simu ya mama yake kisha kupekua jina la Rose, na alipolipata alimpigia simu, “Hallow” “Samahani nani mwenzangu?” “Najua mama una shida, mimi ni mganga wa kienyeji. Naomba tukutane nikusaidie” “Jamani umejuaje dah! Nashukuru sana, nielekeze ulipo nije” Basi Yule kijana akamuelekeza Rose mahali ambapo yeye aliona panafaa kukutana na huyo Rose kwani alikuwa na uchungu sana wa mama yake kutolewa kafara ukizingatia maiti ya mama yake ilifika kwao na kutoweka kwahiyo mama yao walijua tu amekufa ila hata nafasi ya kuzika mwili wa mama yao hawakuipata, yani kijana huyu alijikuta ana uchungu uliopitiliza moyoni mwake haswaa swala la kumfikiria Rose. Rose muda aliokuwa nyumbani kwake na mawazo sana kuhusu kutoweka kwa Sara ndio muda aliopigiwa simu na Yule kijana kwahiyo alihisi kupata mkombozi ukizingatia hakutaka kuchukua hatua ya kutoa wale misukule wake kwavile anahisi kuwa atapata matatizo ndiomana alikuwa anaogopa kuwatoa, kwahiyo ile simu aliona kama ya ukombozi kwake. Alijiandaa haraka haraka na kutoka, ila sebleni alikuta watoto wake wale mapacha wamekaa na baada ya salamu walimuuliza mama yao, “Mama, Sara kaenda wapi?” “Jamani Sara ni mtu mzima, mimi siwezi jua alipoenda” “Mama, Sara hajatoka humu ndani. Tumeenda kumuuliza mlinzi kasema hajatoka, tumemuangalia chumbani kwake hayupo pia. Sara kaenda wapi mama?” “Jamani hebu subirini hadi jioni moune hatorudi, mtoto wa kike yule labda karuka ukuta huko kaenda kwa wanaume” Kisha akatoka zake na kuwaacha, walijiuliza sana maswali ni kwanini mama yao kawajibu kirahisi kiasi kile maana swala la kutokuonekana kwa Sara ilitakiwa hata yeye ashtuke lakini cha ajabu yeye alikuwa akiwajibu kirahisi rahisi tu, wale mapacha walijiuliza sana kuhusu ndugu yao na kukosa jibu. Mama yao alipoondoka, Ana nae alienda sebleni, ikabidi kaka zake wamuulize yeye, “Sara kaenda wapi?” “Sara!!! Sijui mimi” “Ana, ulisema kwa uzuri kabisa unataka kuacha uchawi, Sara haonekani ndani. Mlinzi hajamuona akitoka, na kama angeenda mahali kwa hakika angetuaga hata simu yake ipo ndani, Sara yuko wapi?” “Jamani sijui, mtanilaumu bure tu” Hawa mapacha waliwaza sana cha kufanya ila hawakuwa na jinsi maana hakuna mwenye uhakika wa alipo Sara. Salome leo alienda kumtembelea Mishi na kumshtua sana kwani hakutegemea kutembelewa tena na Salome, aliamini kuwa ameshamalizana nae, kwahiyo kitendo cha kumuona kaenda tena kumtembelea kilimshangaza sana, akashindwa hata kumkaribisha, “Usishikwe na uoga Mishi, ila kilichonileta leo ni jambo moja tu. Kwanini unataka kumdanganya mzee wa watu?” “Kumdanganya nini?” “Si unataka kumwambia kuwa mimba hiyo ni yake!” “Tafadhali naomba nisaidie, sitaki kuumbuka mimi, sitaki watu wajue kuwa nilibakwa ndiomana nataka kumwambia kuwa mimba ni yake” “Msamaha wangu kwako ni kumwambia ukweli, yani wewe mueleze ukweli wote. Anakupenda, kukuacha hawezi, nataka tu ajue mtu anayempenda ni mtu wa aina gani, usimdanganye kuhusu mimba uliyobeba, mwambie ukweli wote” Mishi alikuwa kimya tu maana huu ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwake, na alijua kama atamwambia huyo mzee ukweli basi ni lazima huyo mzee akikutana na mama yake Mishi atamueleza halafu yeye alitaka iwe siri, ‘Nihurumie tafadhali” “kama husemi, nitakuumbua. Nakupa siku moja tu ya kumwambia mzee wa watu ukweli” Ilibidi Mishi akubali kuwa atamueleza Yule mzee ukweli wa mambo ingawa alikuwa anaumia sana. Neema alikuwa anajiuliza hadi kwenda kuoga tena alikuwa anawaza, ila badae akakata shauri na kwenda kuoga halafu akarudi akiwa anaendelea na mawazo yake, watoto wake wale mapacha walitoka shule na kumkuta mama yao pale sebleni akiwa na mawazo, mmoja akaanza kumuuliza mama yao, “Kumbe msharudi ile safari na dada” Akili ikamzinduka kidogo na kufanya awaulize vizuri hawa watoto wake, “Hivi asubuhi ni nani kawaamsha na kuwaandaa muende shule?” “Si wewe mama” “Hivi nilirudi tena kulala?” “Mama jamani, ulisema wewe na dada Salome mnatoka, tena hadi ukatuelekeza mahali tutakuta funguo ndiomana tumekuuliza mmesharuudi tayari” Neema alipata kidogo mwangaza wa jambo amabalo lilitokea ingawa bado alikuwa haelewi kuwa kama jambo hilo limetokea ni hakika limemtokea yeye pamoja na Salome sasa iweje salome amwambie kuwa alikuwa anaota? Aliwaza sana, kisha akachukua simu yake na kuamua kumpigia mama Pendo ili amshirikishe hilo swala, alimpigia na kumuelezea kila kitu jinsi ilivyokuwa, kwakweli mama Pendo alishangaa sana na kuhisi kuwa huenda ni stori za kusadikika, “Una uhakika na hayo mambo kuwa uliondoka kweli nyumbani” “Nina uhakika, hata wanangu hawa wadogo wamenithibitishia hilo” Akamueleza jinsi wanae mapacha walivyomwambia, yani bado mama Pendo ilikuwa ngumu kuelewa kwani mazingira ya tukio lenyewe yalikuwa ni ya utata sana, “Sasa mi ninachoona niongee na mtumishi aje hapo nyumbani” “Kwakweli utakuwa umenisaidia sana ukifanya hivyo, haya mambo ni ya ajabu kwangu hadi sielewi nianzie wapi na niiishie wapi” “Pole ndugu yangu, au nije mwenyewe kuwachukua” “Hata hivyo ni sawa ili nimwambie Salome asitoke” “Basi nitaangalia litakalo wezekana” Neema aliongea sana na huyu rafiki yake, basi alivyokata simu likamjia tukio la kukumbuka kuwa alishawahi kumjuangalia mwanae Salome na kumuona kama kafanana na Moza, hofu ikamshika na kujisemea, “Hapana haiwezekani, Moza aklishakufa na mwanangu yupo hai. Haiwezekani kwakweli” Alikuwa anajiuliza na kujijibu mwenyewe ila alipatwa na mawazo sana huku akimngoja mwanae arudi kwa siku hiyo na kumwambia kuhusu ujio wa mama Pendo kuwapeleka kwenye maombi au ujio wa mtumishi kumuombea Salome. Ana wakati anaongea na kaka zake alikosa raha kabisa maana yeye alionekana anajua fika alipo dada yao Sara ukizingatia nyumba nzima hakujulikana alipo. Ikabidi ainuke na kwenda chumbani kwake kufanya dawa zake. Alifika na kuzianza dawa zake, alifanya kwa muda kidogo na kumuona kuwa dada yake Sara ni miongoni mwa misukule ya mama yao. Alishtuka sana Ana na kushangaa kwanini mama yao kafikia hatua hiyo maana aliona sasa ni hatua mbaya yani mama yao hata afikie kumuweka kama msukule mtoto wake mwenyewe, maana misukule aliyokuwa anatunza mama yake ilikuwa ni tofauti na misukule ya watu wengine maana hii ililishwa kichawi na ilimsaidia kichawi kupata nguvu za ziada kiasi kwamba ni ngumu sana kwake kuitoa misukule hiyo kwani itamgharimu maisha yake yote, kwahiyo kitendo cha mama yao kumuweka Sara msukule kilimchanganya sana Ana na kumshangaza, akamuangalia mara mbili mbili dada yake alivyokuwa akisononeka na kumuonea huruma ila hata yeye Ana hakuwa na uwezo wa kuwatoa watu kwenye kile kichumba ambacho mama yao aliwahifadhi. Kisha akajaribu kuangalia kuwa mama yao ameenda wapi, alimuona yupo porini ambapo hata njia hakuielewa halafu alikuwa akishangaa shangaa, mara wakatokea vijana watatu na kumbana, kile kitendo kilimfanya Ana atupe dawa zake zote kwa kushtuka kwani alijua wazi kuwa mama yao yupo hatarini. Rose alienda hadi mahali ambapo alielekezwa na Yule kijana ila alifika jioni maana sehemu yenyewe ilikuwa ni safari ya mbali sana, alishangaa sehemu yenyewe ilikuwa kimya kabisa, akaanza kushangaa shangaa, mara walikuja vijana nyuma yake wakamfunga mdomo, mikono na miguu na mwisho wakamfunga macho, “Mama mpumbavu sana wewe na habari zako za kupenda waganga, umemuua mama yangu na wewe ni lazima ufe” Rose hakuweza kujitetea wala nini maana wale vijana walikuwa wamemziba mdono kwa kitambaa, kisha wakaanza kumpiga ambapo walimpiga sana, halafu wakakubaliana kuwa wambake, walifanya kazi ya kumbaka kwa zamu, Rose alilia sana na kujilaumu moyoni kufika sehemu bila ya tahadhari. Wale vijana walimpiga sana Rose, kisha wakataka kumchinja kwani lengo la mtoto wa mama jack ni kumuona huyu mtu anayeitwa Rose akifa kama alivyokufa mama yao, ingawa mama yao alikufa kichawi ila walitaka huyu mtu wamuue kimacho macho. Alishika kisu sasa akitaka kumchoma, wakati amekiinua ili amchome alishtukia mkono wake ukishikwa na kuzuiwa kumchoma, alipogeuza macho aangalie ni nani alimuona ni binti amabaye mama yao alimsaidia usiku ambapo kesho yake ndio alitokomea nae. Itaendelea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: