Thursday, November 16, 2017

Riwaya: SAFARI YA MSITU WA SIRI SEHEMU YA NNE (4) ***Tulipoishia*** Upande mwingine David alionekana akizidi kuingia ndani ya pori...." pori lile lilionekana kuwa na msitu wenye miti mikubwa sana..mara ghafla alimuona swala yule,, kwa sasa swala yule hakuwa mbali na pale alipokuwepo David..kisha alivuta upinde ule kumlenga swala yule....ile anataka uachia mshale swala alitimua mbio na kutokomea ndani zaidi kunako msitu huo... David alichukia sana....akaamua kuingia ndani zaidi kunako msitu huo....mara ghafla kilipita kiumbe mbele yake kwa kasi ya hajabu akuweza kukitambua kiumbe kile.. ***Endelea*** Alistuka! sana kisha akawa katika hali ya umakini zaidi,, ikasikika sauti yenye mngurumo wa ajabu ambao hakuwahi kusikia sauti ya mnguromo huo tangu kuzaliwa kwake.... alipotazama kwa mbele aliona kunamnyama"" ,,alipomtazama vizuri" aligundua kuwa ni NGIRI. alisogea taratibu ili kumnasa mnya yule..mara ghafla..mnyama yule alipitiwa na kiumbe cha ajabu ambacho hata David hakukiona viziri wala hakuweza kutambua ni kiumbe cha aina gani!''',, kiumbe kile kilitenganisha katikati ya mwili wa yule NGILI. nakisha kutoweka na upande mmoja ambao ni sehemu ya kuanzia tumboni kuelekea nyuma.. kikaacha upande mmoja ambao ni sehemu ya kuanzia tumboni kuelekea kichwani...Damu zilimrukia David aliogopa sana..baada ya kuona hivyo alitimua mbio bila kujua ni wapi anaelekea alikimbia huku ameushikilia baraabara upinde wake",, ******* baada ya kukimbia umbali mrefu huku akiwa anatokwa na damu kwenye baadhi ya sehemu za mwili wake..majeraha hayo aliyapata kwa sababu alikuwa anapita kwenye vichaka vyenye miba pasipo yeye kujua kutokana na hofu na uwoga aliokuwanao hivyo hakuweza kuhisi maumivu hata kidogo kwa wakati ule,, "" alipunguza mwendo kisha akatazama nyuma huenda akakiona kiumbe hicho....lakini hakuona chochote.. wakati David anakimbia kwa ajili ya kuokoa maisha yake kumbe ndio alikuwa anazidi kuingia ndani zaidi kunako msitu ule,,"" alipotaamaki hakuweza kukumbuka ni njia ipi aliyoingianayo hivyo alikuwa kama mtu aliyepotea njia... alitembea kwa hatua za kunyata huku akigeuza-geuza shingo yake kila upande,,"" alifanya hivyo mara zote kipindi anazipiga hatua...mara kiumbe kile cha ajabu kikapita tena" mbele yake kwa kasi ya ajabu david hakuweza kukitambua kiumbe hicho kutokana kilikuwa kinapita kama upepo( vup) aliingiwa na uwoga kisha mapigo yake ya moyo yalianza kupiga kwa kasi ya ajabu....aliamua kutimua mbio,, safari hii alikimbia huku anapiga kelelele...nakufaaaaa!!! nisaidieni..aliomba msaada pasipo mafanikio yoyote...alipiga kelele hizo ili kama kuna mtu yupo karibu na maeneo hayo aweze kumsikia huenda akampa msaada...Lah!hasha!!"",, kelele zile hazikusaidia chochote"",, hakuna mtu aliyesikia kelele zile kwa sababu David alikuwa ndani zaidi kunako msitu ule hivyo kelele zile hazikuweza kutoka nje ya msitu",, ************ Hakuna binadamu yeyote aliyewahi kuingia kwenye MSITU huo kisha akatoka Yuhai",, inasadikika kuwa ndani ya msitu huo ,, kuna kiumbe wa ajabu. inasemekana miaka mingi iliyopita"",, yapata takribani zaidi ya miaka mia moja kulikuwa na watu",,jamii ya kabila la ""WACHEDA"" watu hao walikuwa wakiabudu mti""..Mti huo ulikuwa Katikati ya mstu..ambapo David yumo.... watu hao jamii ya kabila la WACHEDA waliuita Mti huo MUNGU wao.. hivyo walikuwa wakifanyia makafara na matambiko,,""na kuomba katika mti huo... ilitokea siku moja kuna mtu mmoja alikwenda msituni humo na kuukata mti ule...baada ya kuukata..alipata lahana muda huohuo"" kisha alibadilika na kuwa kiumbe wa ajabu...Tangu siku hiyo hakuwahi kuonekana tena...hata ndugu jamaa na marafiki zake hawakuwahi kujua ni wapi alipokwenda hivyo alibakia msituni humo maisha yake yote...basi kuanzia sikuhiyo alikuwa anauwa chochote kinachoonekana kuingia kwenye msitu ule...alifanya hiyo kwa Wanyama na Binadamu mpaka kizazi chaJamii yote ya kabila la WACHEDA kilikwisha nakutoweka kabisa... ************ David alikuwa katika wakati mgumu sana na hatari kubwa ndani ya msitu ule..alichoka kukimbia akaamua kupumzika chini ya mti..baada ya dakika kadhaa aligundua kuwa hapo alipoketi sio salama..yani pako wazi sana hivyo alihofia kuwa huenda kiumbe kile kitamuona kwa urahisi na kumdhuru.. alijisogeza huku anatambaa utadhani mtoto wa miezi tisa""",,,David alijisogeza kunako kichaka kidogo ili ajifiche.. lakini kabla hajafanya hivyo..ghafla kiumbe kile kikajitokeza tena"" kikapita kwa kasi ya ajabu!! David alinyanyuka haraka kutoka pale chini kisha akaanza kutimua mbio tena...alikimbia sana huku asijue nini cha kufanya...wakati anakimbia mara ghafla alikanyaga sehemu iliyotitia akadondoka kisha akatumbukia ndani ya shimo refu sana Tiiiiiiii akapoteza fahamu. ITAENDELEA.......

No comments:

Post a Comment