Riwaya: SAFARI YA MSITU WA SIRI
SEHEMU YA TANO(5)
***Ilipoishiaa***
david aliamua pumzika chini ya mti....baada ya dakika kadhaa aligundua kuwa hapo alipo keti sio salama..yani pako wazi sana hivyo alihofia kuwa huenda kiumbe kile kitamuona kwa urahisi na kumdhuru..
alijisogeza huku anatambaa utadhani mtoto wa miezi tisa""",,,David alijisogeza kunako kichaka kidogo ili ajifiche.. lakini kabla hajafanya hivyo..ghafla kiumbe kile kikajitokeza tena"" kikapita kwa kasi ya ajabu!! David alinyanyuka haraka kutoka pale chini kisha akaanza kutimua mbio tena...alikimbia sana huku asijue nini cha kufanya...wakati anakimbia mara ghafla alikanyaga sehemu iliyotitia akadondoka kisha akatumbukia ndani ya shimo refu sana Tiiiiii""""akapoteza fahamu.....
***endelea***
alipozinduka alishangaa kujikuta amelala chini alipatazama upande wa juu aligundua kuwa yumo ndani ya shimo...sasa nimefikaje humu alijiuliza David....ndipo kumbukumbu ikarudi alikumbuka kuwa alikuwa anamkimbia yule kiumbe wa ajabu ambaye hata yeye mwenyewe hakufanikiwa kukitambua kiumbe kile...aliogopa sana alipotazama vizuri aliona kama unauwazi sehem akaamua kupita kwenye uwazi huo..... aliifuata njia hiyo ambayo ilikuwa iko chini ya aridhi....wakati anazipiga hatua alikuwa anajiuliza maswali njia hii itatokezea wapi??? lakini alijipa moyo bila shaka hili ni handaki hivyo basi lazima kutakuwa na njia ya kutokezea nje..baada ya kuwaza hivyo alianza kuzipiga hatua za harakaharaka..kutokana na giza lililokuwemo humo ndani ya hiyo njia ya nini kwa chini ya aridhi...David alijingonga gonga kwenye kingo za njia ile...
**************
huko nyumbani kwa kina david....alionekana paul ameanza kuingiwa na wasiwasi...inamaana mpaka sasahivi david hajarudi atakuwa amepatwa na nini?? alijiuliza paul ambae ni mjomba wake David...wakati huo mama David alikuwa amepumzika chumbani kwake...alikuwa kasinzia kutokana na zile dawa alizopewa kule kituo cha afya zilimpelekea mwili wake kuregea hivyo tangu mda ule alikuwa bado kalala...
**********
Paul aliamua kurudi kule porini kumtafuta David""",,alimtafuta kwa muda mrefu sana bila mafanikio yoyote....paul aliwaza huenda David labda kaingia kwenye ule msitu ambao ni MSITU WA SIRI"" ,,,watu wa kijiji hicho waliuita msitu huo hivyo...kwa sababu hakuna binadamu yeyote anaejua chochote kuhusu msitu ule...kwa sababu hakuna mtu aliyeingia msituni mule akatoka salama hivyo ilibaki kuwa siri ya msitu...aaah kama atakuwa kaingia msituni mule Masikini David wangu sijui kama Yusalama"",, aliingiwa na wasiwasi akanza kuita kwa kupaza sauti...aliita hivyo mpaka sauti ilikauka....
hatimae alianza kuingia ndani ya msitu ule ili kumtafuta David huenda atamuona
***********
upande mwingine alionekana David bdo yupo ndani kwenye njia ya handaki lile...kwa mbali alianza kuona mwanga"" alipotazama kwa makini aliona ni mwanga wa Jua....akaanza kuzipiga hatua za haraka haraka kuelekea kunako mwanga huo...alipoukaribia aliona njia ikionesha upande wa nje aliona miti alifurahi sana kuisha akaifuata njia ile ili atoke nje....kabla ya kutoka aliona kitu" akakitazama kwa makini ndipo alipoona kiumbe wa ajabu..kiumbe huyo alitisha sana alikuwa anafanana na mti...ukikitazama ni mti kabisa",, lakini alikuwa na umbile la binadamu...nilistuka nikaingiwa na uwoga....huku ikiambatana na vijampo vya mfululizo (phu phu phu) nilijiuliza inamaana hiki ndicho kile kiumbe kilichokuwa kinapita kwa kasi ya ajabu mbele yangu au????kisha nikaanza kuangaza angaza macho yangu nilipo tazama kwa mbali nilistuka kuona mafuvu na mifupa mingi ya binadamu......kisha niliona mti ule ukitembea kuelekea upande niliokuwepo...wakati huu niliweza kuona vizuri mti ule waajabu ulikuwa ukitembea.....niliogopa sana nikajua leo ndio mwisho wa uhai wangu....nikafumba macho...nilipofumbua macho sikumuona kiumbe yule waajabu""" kumbe alikuwa kapitiliza na kuelekea mbele zaidi..niliogopa kutoka kisha nikaamua kubaki hapohapo....nilikaa kwa muda kama wa lisaa limoja nilipoona pako kimya nikaamua kutoka ili niondoke eneo lile"",, kabla sijafanya hivyo. niliona yule kiumbe wa ajabu anarudi huku ameninginiza kiwiliwili cha binadamu...kiwiliwili hicho kilionekana kuanzia upande wa tumboni kuelekea kichwani...bila kuwa na sehemu ya chini yani kiuno na miguu....niliogopa sana."" ,, kiumbe kile kilipokuwa kinasogea nilistuka sikuamini macho yangu kwa kile nilichokiona.....niliogopa zaidi baada ya kuona kiwiliwili hicho kilikuwa ni cha.....
ITAENDELEA........
usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua na yenye maajabu ya kutisha..
No comments:
Post a Comment