Home → simulizi
→ Love story:ANKO INATOSHA
Mwandishi:JAFARI MPOLE
Sehemu:15
ILIPOISHIA.:..
...akajikuta akidondosha chozi huku akigeuka kumtazama anko ambaye bado alikuwa
anakoroma usingizini...
ENDELEA NAYO LEO...
Hakuweza kuamini Eliza kwa kile alichokiona ingawa nafsi yake ilikuwa inamsuta na kuanza kujilaumu mwenyewe,aligeuka tena kutazama zile dawa,machozi yakazidi kumtiririka baada ya moyo wake kulipokea lile jambo kwa uhalisia halisi,"ANKO AMEATHIRIKA?AH
AH AH !NIMEKWISHA JAMANI UUUWIH..!!"alisema Eliza kwa sauti ya chini ikiambatana na kilio ambacho kilimfanya anko Tony aamke kutoka usingizini,alishangaa kumuona Eliza mule chumbani asubuhi ile akiwa yupo kwenye hali ya huzuni,.
"vipi Eliza,mbona upo hivyo,unaumwa?"alisema anko Tony akinyanyuka kutoka kitandani.Eliza hakutaka tena swali,maelezo wala stori,alichomwambia anko wake ni kuwa chai tayari,na yeye akageuka na kuondoka mule chumbani kwa anko.
."huyu ananini leo mbona kanuna hivyo?"alisema anko ingawa haikumshtua sana ile hali ya Eliza,akatabasamu tu huku akigeuka mezani kuchukua mswaki,wakati ananyanyua mswaki wake akaziona zike dawa alizokunywa,akakumbuka kuwa kumbe jana yake alisahau kuziweka mahala pake ili mtu yeyote asiweze kuziona,hakika alishtuka hasa baada ya kukumbuka kuwa ni muda huohuo tu ndio alitoka Eliza mule chumbani kwake,tena akawa amebadilika gafla tofauti na siku zote.
"mmh...atakuwa ameziona hizi dawa nini!?!"alibaki ameduwaa anko bila ya kupata jibu.
Eliza hakuwa na raha hata kidogo pale mezani huku
wenzake wenzake wakiendlea kula,hata kupeleka kitu mdomoni hakuweza,huzuni ilimjaa,nafsi yake inaulaumu moyo kumuweka moyoni anko Tony na kumruhusu autumie mwili autakavyo, hakika alikuwa akihofia juu ya afya yake,.Hali ile hata mama yake aliielewa hakusita kumuuliza mwanaye.
"Eliza,vp mbona huonekani kufurahi,wenzako tunakula wewe hata mkate umekushinda,una nini? unaumwa?"aliuliza mama mtu.
"na kweli hata mimi namuona leo si kawaida yake,eti shosti,vipi?"alisema Rose hju akimshika bega Eliza.
"ah..sijisikii vizuri,nahisi homa inanianza mama"alisema Eliza kujaribu kuwadananya,hakuwa mwenye kuumwa kweli.
"nilijua tu,na ulivokuwa muoga wa dawa wewe ndo umeamua kunyamaza kimya,unajitafutia matatizo wewe mtoto shauri yako,mwanamke mzima unaogopa dawa,muone vile...sasa utaongozana na Rose mpaka hospitali ukapime,Rose umsindikize hoapitali huyu cha uwoga na hakikisha anafika huyu na anapima maana kazidi uoga mwenzenu,loh..utakuja utuletee matatizo humu ndani,muone vile,"alisema mama Rose huku akinyanyuka na kubeba mkoba wake akatoa noti mbili za elfu kumi na kumkabidhi Rose.
"shika hii hela ya hospitali kama atapimwa mtachukua dawa sawa,mimi natoka kidogo ntarudi badae jioni"
"sawa mama,ngoja tumalizie hapa nimpeleke huyu"alisema rose na mama yake akaondoka.
Hakuna yeyote aliyekuwa akijua lolote kuhusu akifikilia Eliza kwa muda ule,wote walikuwa wakijua kuwa alikuwa akiumwa kweli,na kweli baadaye wakajiandaa Rose na Eliza na kuanza safari ya kuelekea hospitali huku wakimuacha ruth aendelee na kazi ndogondogo za ndani.
Safari ya kuelekea hospitali haikuwa na shaka kwake,moyoni alikuwa na lake jambo,njiani walikutana na Zuhura akitoka kwao,walikaribiana na kuanza kupiga umbea kdogo.
"haya shoga zangu vip mbona wawili wawili tena mmepooza kwema!"aliuliza zuhura.
"mh..mwenzangu hata siyo kwema,shosti hapa anaumwa,hata chakula kashindwa kula ndo namsindikiza hospitali hapa akapime ajue ni maralia ama nini!"alisema rose.
"mh na kweli maana siyo kawaida yake kupooza,pole mpenzi"alisema Zuhura kumfariji Eliza ambaye muda wote hakuweza hata kusema neno,kwakuwa hakuwa na safari ya umuhimu sana,zuhura akaungana na wenzake na kuwa watatu wakaelekea hospitali kama kimsindikiza mwenzao Eliza anayesadikika kutojisikia vema.
Njiani walikuwa wakipiga stori tu huku muongeaji mkubwa akiwa ni zuhura muda wote,mpaka wakakaribia nje kidogo na hospitali,ndipo Eliza akawasimamisha wenzake na kuwaekeza jambo wenzake baada ya kukaa kimya muda wote tangu mwanzo wa safari akiwa anatafakari jambo.
"jaman hebu subirini kidogo,kabla hatujaingia ndani kwa dokta nataka nitoe wazo,sisi ni wanawake,mnaonaje tukaenda kupima afya zetu tujue kwanza tupo salama au laa,halafu tukimaliza hapo nitapima malaria,au mnasemaje!"alisema Eliza kuwapa ushauri, wenzake wakatazamana kwanza,hakika lilikuwa wazo
zuri,waliliafiki na wakamuelewa,taratibu wote wakaingia hospitali kwa lengo la kupima kujua yao afys. Walifika kwa daktari na zoezi hilo halikuchukua muda,dakhka 30
zilìwatosha wote kuchukuliwa damu zao na kupimwa,majibu yakawa tayari na wote wakaingia kwa dokta na kukaa kusikiliza majibu yao.
"sawaa,majibu yenu tayari na ninayo hapa,sasa kwa kawaida majibu ni siri ya mtu mwenyewe,nyie mnaonaje aanze mmoja mmoja au?"alisema daktari.
"ah dokta mimi naona ungetuambia tu kwa pamoja ili tujijue,sisi ni ndugu"alisema Rose na wenzake wakakubali,daktali akafungua karatasi yake.
"sawa,majibu yenu haya hapa..Rosemary Peter majibu yako yanayabeba pia majibu ya wenzako wote,namaanisha kuwa majibu yako ndio hivyo ilivyo kwa Elizabeth Peter na Zuhura Juma...Rosemery... una maambukizi ya virusi,namaanisha unaishi na virusi vya UKIMWI"
"NINI?"alishangaa Rose kuambiwa vile.
"ndio ukweli ulivyo na ndivyo iko ivyo kwa wenzako wote,wote mmeathirika"
"ati nini??"alihaki Zuhura huku Eliza akiwa tayari kashapata jibu sahihi la kile alichokuwa akikifikira tokea mwanzo,alibaki kudondosha tu machozi baada ya kuambiwa wote watatu ni waathirika.
"haiwezekani kabisa...mimi rose..,nimeathrika? ah ah
ah"zìlikuwa ni sauti za vilio mule ndani,hakuna aliyeamini anachoambiwa,ingawa eliza alilifahamu hilo lakini alishindwa kujizuia kuendelea kulia,daktari aliwafariji na kuwapa maelezo na namna ya kuishi na kujizuia kuendelea kuwaambukiza wengine,alikaa nao kwa muda kidogo na kuwatoa ile imani ya kujiona ndio umefika mwisho maisha yao,hata walipotoka hospitali wote mioyo yao ilikuwa imedhoofika.
Hakuna aliyekuwa anaongea njiani pindi walipokuwa wanarudi kwao,safari yao ilikomeshea kwa akina Zuhura,wakaingia chumbani kwa zuhura na kukaa mule wakitazamana kwa masikitiko na majonzi yakianza kutawala tena huku akijikaza Eliza taratibu,akawatazama wenzake..
"Rose ndugu yangu,hakuna haja ya kulia kiasi hicho,mambo mengi hapa kati yamepita ambayo tulikuwa hatufahamu ila sina budi kuyaanika hayo mambo kila mtu ajue ukweli na hii nikutokana na siri ambayo tulikuwa tukijidanganya sisi wenyewe..."
SIRI GANI HIYO?TUKUTANE SEHEMU YA MWISHO YA STORY YETU,...
Love story:ANKO INATOSHA Mwandishi:JAFARI MPOLE Sehemu:15 ILIPOISHIA.:.. ...akajikuta akidondosha chozi huku akigeuka kumtazama anko ambaye bado alikuwa anakoroma usingizini... ENDELEA NAYO LEO... Hakuweza kuamini Eliza kwa kile alichokiona ingawa nafsi yake ilikuwa inamsuta na kuanza kujilaumu mwenyewe,aligeuka tena kutazama zile dawa,machozi yakazidi kumtiririka baada ya moyo wake kulipokea lile jambo kwa uhalisia halisi,"ANKO AMEATHIRIKA?AH AH AH !NIMEKWISHA JAMANI UUUWIH..!!"alisema Eliza kwa sauti ya chini ikiambatana na kilio ambacho kilimfanya anko Tony aamke kutoka usingizini,alishangaa kumuona Eliza mule chumbani asubuhi ile akiwa yupo kwenye hali ya huzuni,. "vipi Eliza,mbona upo hivyo,unaumwa?"alisema anko Tony akinyanyuka kutoka kitandani.Eliza hakutaka tena swali,maelezo wala stori,alichomwambia anko wake ni kuwa chai tayari,na yeye akageuka na kuondoka mule chumbani kwa anko. ."huyu ananini leo mbona kanuna hivyo?"alisema anko ingawa haikumshtua sana ile hali ya Eliza,akatabasamu tu huku akigeuka mezani kuchukua mswaki,wakati ananyanyua mswaki wake akaziona zike dawa alizokunywa,akakumbuka kuwa kumbe jana yake alisahau kuziweka mahala pake ili mtu yeyote asiweze kuziona,hakika alishtuka hasa baada ya kukumbuka kuwa ni muda huohuo tu ndio alitoka Eliza mule chumbani kwake,tena akawa amebadilika gafla tofauti na siku zote. "mmh...atakuwa ameziona hizi dawa nini!?!"alibaki ameduwaa anko bila ya kupata jibu. Eliza hakuwa na raha hata kidogo pale mezani huku wenzake wenzake wakiendlea kula,hata kupeleka kitu mdomoni hakuweza,huzuni ilimjaa,nafsi yake inaulaumu moyo kumuweka moyoni anko Tony na kumruhusu autumie mwili autakavyo, hakika alikuwa akihofia juu ya afya yake,.Hali ile hata mama yake aliielewa hakusita kumuuliza mwanaye. "Eliza,vp mbona huonekani kufurahi,wenzako tunakula wewe hata mkate umekushinda,una nini? unaumwa?"aliuliza mama mtu. "na kweli hata mimi namuona leo si kawaida yake,eti shosti,vipi?"alisema Rose hju akimshika bega Eliza. "ah..sijisikii vizuri,nahisi homa inanianza mama"alisema Eliza kujaribu kuwadananya,hakuwa mwenye kuumwa kweli. "nilijua tu,na ulivokuwa muoga wa dawa wewe ndo umeamua kunyamaza kimya,unajitafutia matatizo wewe mtoto shauri yako,mwanamke mzima unaogopa dawa,muone vile...sasa utaongozana na Rose mpaka hospitali ukapime,Rose umsindikize hoapitali huyu cha uwoga na hakikisha anafika huyu na anapima maana kazidi uoga mwenzenu,loh..utakuja utuletee matatizo humu ndani,muone vile,"alisema mama Rose huku akinyanyuka na kubeba mkoba wake akatoa noti mbili za elfu kumi na kumkabidhi Rose. "shika hii hela ya hospitali kama atapimwa mtachukua dawa sawa,mimi natoka kidogo ntarudi badae jioni" "sawa mama,ngoja tumalizie hapa nimpeleke huyu"alisema rose na mama yake akaondoka. Hakuna yeyote aliyekuwa akijua lolote kuhusu akifikilia Eliza kwa muda ule,wote walikuwa wakijua kuwa alikuwa akiumwa kweli,na kweli baadaye wakajiandaa Rose na Eliza na kuanza safari ya kuelekea hospitali huku wakimuacha ruth aendelee na kazi ndogondogo za ndani. Safari ya kuelekea hospitali haikuwa na shaka kwake,moyoni alikuwa na lake jambo,njiani walikutana na Zuhura akitoka kwao,walikaribiana na kuanza kupiga umbea kdogo. "haya shoga zangu vip mbona wawili wawili tena mmepooza kwema!"aliuliza zuhura. "mh..mwenzangu hata siyo kwema,shosti hapa anaumwa,hata chakula kashindwa kula ndo namsindikiza hospitali hapa akapime ajue ni maralia ama nini!"alisema rose. "mh na kweli maana siyo kawaida yake kupooza,pole mpenzi"alisema Zuhura kumfariji Eliza ambaye muda wote hakuweza hata kusema neno,kwakuwa hakuwa na safari ya umuhimu sana,zuhura akaungana na wenzake na kuwa watatu wakaelekea hospitali kama kimsindikiza mwenzao Eliza anayesadikika kutojisikia vema. Njiani walikuwa wakipiga stori tu huku muongeaji mkubwa akiwa ni zuhura muda wote,mpaka wakakaribia nje kidogo na hospitali,ndipo Eliza akawasimamisha wenzake na kuwaekeza jambo wenzake baada ya kukaa kimya muda wote tangu mwanzo wa safari akiwa anatafakari jambo. "jaman hebu subirini kidogo,kabla hatujaingia ndani kwa dokta nataka nitoe wazo,sisi ni wanawake,mnaonaje tukaenda kupima afya zetu tujue kwanza tupo salama au laa,halafu tukimaliza hapo nitapima malaria,au mnasemaje!"alisema Eliza kuwapa ushauri, wenzake wakatazamana kwanza,hakika lilikuwa wazo zuri,waliliafiki na wakamuelewa,taratibu wote wakaingia hospitali kwa lengo la kupima kujua yao afys. Walifika kwa daktari na zoezi hilo halikuchukua muda,dakhka 30 zilìwatosha wote kuchukuliwa damu zao na kupimwa,majibu yakawa tayari na wote wakaingia kwa dokta na kukaa kusikiliza majibu yao. "sawaa,majibu yenu tayari na ninayo hapa,sasa kwa kawaida majibu ni siri ya mtu mwenyewe,nyie mnaonaje aanze mmoja mmoja au?"alisema daktari. "ah dokta mimi naona ungetuambia tu kwa pamoja ili tujijue,sisi ni ndugu"alisema Rose na wenzake wakakubali,daktali akafungua karatasi yake. "sawa,majibu yenu haya hapa..Rosemary Peter majibu yako yanayabeba pia majibu ya wenzako wote,namaanisha kuwa majibu yako ndio hivyo ilivyo kwa Elizabeth Peter na Zuhura Juma...Rosemery... una maambukizi ya virusi,namaanisha unaishi na virusi vya UKIMWI" "NINI?"alishangaa Rose kuambiwa vile. "ndio ukweli ulivyo na ndivyo iko ivyo kwa wenzako wote,wote mmeathirika" "ati nini??"alihaki Zuhura huku Eliza akiwa tayari kashapata jibu sahihi la kile alichokuwa akikifikira tokea mwanzo,alibaki kudondosha tu machozi baada ya kuambiwa wote watatu ni waathirika. "haiwezekani kabisa...mimi rose..,nimeathrika? ah ah ah"zìlikuwa ni sauti za vilio mule ndani,hakuna aliyeamini anachoambiwa,ingawa eliza alilifahamu hilo lakini alishindwa kujizuia kuendelea kulia,daktari aliwafariji na kuwapa maelezo na namna ya kuishi na kujizuia kuendelea kuwaambukiza wengine,alikaa nao kwa muda kidogo na kuwatoa ile imani ya kujiona ndio umefika mwisho maisha yao,hata walipotoka hospitali wote mioyo yao ilikuwa imedhoofika. Hakuna aliyekuwa anaongea njiani pindi walipokuwa wanarudi kwao,safari yao ilikomeshea kwa akina Zuhura,wakaingia chumbani kwa zuhura na kukaa mule wakitazamana kwa masikitiko na majonzi yakianza kutawala tena huku akijikaza Eliza taratibu,akawatazama wenzake.. "Rose ndugu yangu,hakuna haja ya kulia kiasi hicho,mambo mengi hapa kati yamepita ambayo tulikuwa hatufahamu ila sina budi kuyaanika hayo mambo kila mtu ajue ukweli na hii nikutokana na siri ambayo tulikuwa tukijidanganya sisi wenyewe..." SIRI GANI HIYO?TUKUTANE SEHEMU YA MWISHO YA STORY YETU,...
Artikel Terkait
*LOVE BITE EP 04* ILIPOISHIA…… Aliongea Jothan huku machozi yakimlenga lenga. Hakika ni uamuzi mgumu aliouchukua kwakua aliamini ilikuwa ni mtihani mkubwa katika mapokezi ya mlengwa. Alipoinua macho yake kumtazama Prisca, tayari mashavu ya prisca yalishalowana kwa machozi huku macho yakiwa mekundu. Kilio cha kwiki kilianza kusikika na kumfanya Jothan kuingiwa na imani baada ya kumtaza mpenzi wake huyo anaye amua kumuacha bila kosa lolote. SONGA NAYO…………….. Machozi na kilio cha kwikwi kiliendelea kwa dakika kadhaa, Prisca alimuangalia Jothan ambaye alikua ana muonea aibu wakati huo. Hakuamini kuwa ndiye yeye aliyetamka maneno yale,. “kwanini mimi?…. kwanini Jothan umeamua kuzichezea hisia zangu kwa miaka yote hiyo niliyokuwa na wewe kumbe ulikuwa huna malengo ya kuwa na mimi. Kwanini Jothan umeamua kunifanyia hivyo?” aliongea Prisca huku analia. “sorry Prisca. Unafikiri ningefanyaje kwa hali niliyokuwa nayo hivi sasa. Sina jinsi japokuwa bado nakupenda sana. Ningekuwa mtu mwengine hivi sasa ningeendelea kuwachanganya wote wawili. Ila roho huwa inanisuta kufanya hivyo kwakua hata mimi sihitaji kuchezewa hisia zangu. Naomba kubaliana tu na maamuzi yangu japokuwa unaumia.” Aliongea Jothan huku na yeye akijifuta machozi yaliyomdondoka kutokana na hali aliyokuwa nayo Prisca inavyosikitisha. “thank you for everything.” Aliongea Prisca na kunyanyuka na kuondoka. Alimuacha Jothan ambaye alijiinamia na kujilaumu kwa alichokifanya. Akili nyingine ilimwambia kama mwanaume wa ukweli na mwenye msimamo basi alifanya maamuzi sahihi na ya busara. Alirudi nyumbani na kumkuta Shani amejaa tele nyumbani kwake. Alipofika tu, Shani alimfuata na kumkumbatia. Ingawaje Jothan alijichekesha, lakini Shani aligundua kuwa hakuwa sawa. “una nini mume wangu?. Aliuliza Shani baada ya kumuangalia usoni Jothan. “kawaida tu mke wangu.. kwani naonyesha nina tatizo?” aliuliza Jothan kuhakikisha alichokisikia kutoka kwa Shani. “sura yako inaonyesha kama ullikuwa unalia au ulikuwa unahuzunika muda si mrefu.” Aliongea Shani na kumfanya Jothan kumuangalia usoni Shani. “kichwa kilikua kinanigonga sana, hata hivyo sasa hivi niko sawa.” Aliongopa Jothan “pole mume wangu, kama bado kinaendelea we niambie nikununulie panadol au nikusindikize hospital… usidharau mume wangu.” Aliongea Shani huku akionyesha kwa alikua anajali sana afya ya mwenzi wake. “usijali, niko sawa tu.” Aliongea Jothan na kuingia chumbani kwake. Alijilaza na kuwaza yaliyotokea muda mfupi uliopita. Aliamua kupiga moyo konde na kuona yote yalikuwa ni majaribu tu. Maisha yalikuwa mazuri huku kila mmoja akifurahia uwepo wa mwenzake. Hata Jothan mwenyewe alikiri kuwa uamuzi wake ulikuwa sahihi sana kumchagua Shani katika maisha yake badala ya Prisca ambaye mpaka kipindi hicho alikuwa ameshakatisha mawasiliano naye. Shani naye alijitahidi kuhakikisha anafanya yale yote apendayo Jothan na kumteka Jothan kisawa sawa. Ilkuwa akiongelewa mwanamke bora basi Jothan alilipitisha jina la Shani bila kuangalia kuwa alikuwa na nani au alizungukwa na wasichana wazuri. Alitumia muda mwingi kuwa karibu na Shani. Hata kama alikua anataka kwenda kutanua, basi Shani alikuwa ubavuni kila walipoenda. Siku moja ambayo ilikua ni mwisho wa wiki, Jothan aliamua kulala tu Jumaapili hiyo kutokana na uchovu aliokuwa nao wa jana yake kwakua walienda club yeye na Shani na kurudi asubuhi kabisa. Nyumbani kwake aligonga hodi mgeni mmoja wa kike na kufunguliwa mlango na Shani ambaye alishaamka na alikuwa anfanya usafi nyumbani kwake. “za saa hizi dada.” Alisalimia yule mgeni ambaye alionyesha wazi kuwa alikua amechoka kutokana na mimba kubwa aliyokuwa nayo. “salama tu.” Alijibu Shani na kumsikiliza huyo msichana shida yake. “sijui nimemkuta mwenye nyumba hii?” aliuliza yule dada na kumuangalia Shani aliyekuwa makini akimsikiliza. “mwenyewe kalala, ila naweza kukusaidia kama hutajali kunieleza shida yako.” Aliongea Shani na kumuangalia yule dada. “ni vyema kama nita onana nae mwenyewe.” Aliongea yule dada na kumfanya Shani amkaribishe ndani. Kwakua Shani alikua anaandaa chai, hakuona ubaya kuandaa ya kutosha na kumkaribisha yule mgeni aliyekunywa chai kama anafukuzwa kutokana na njaa aliyokuwa nayo. Shani aligundua njaa aliyokuwa nayo mgeni huyo na kumuongezea vyakula mpaka alipohakikisha ameshiba ndio akaamua kumfuata na kumuuliza maswali machache wakati wanamsubiri bwana mkuwa aamke. “tunsubiri aamke, si unajua alikesha jana kwa hiyo sio vizuri kumuamsha mtu akiwa katika uchovu kama huo.” Aliongea Shani na wazo hilo likapitishwa na yule mgeni. Jothan aliamka na kwenda kuoga. Alivaa nguo zake nyepesi na kwenda sebuleni na kumkuta mgeni aliyekuwa anamsubiri. Yule dada alipogeuza shingo kumuangalia Jothan, macho yalimtoka na kujikuta mshangao mkuu umempata. “wewe, umefuata nini nyumbani kwangu?” aliuliza Jothan kwa hasira. Yule mgeni hakua na la kujibu zaidi ya kujiinamia. “na wewe unawakaribishwa watu humu ndani wengine ni nyoka kama huyu mwanamke.” Aliongea Jothan na kumuweka Shani kwenye bumbuwazi. “mbona sielewi, maana mimi aliniambia ni mgeni wako ndio maana nikaona si vibaya kumkaribisha ndani.” Alijitetea Shani. “mimi simjui huyu, .. kwani wewe msichana unaitwa nani?” aliuliza Jothan na kwenda kukaa kwenye moja ya sofa za pale sebuleni. “BAHATI.” Alijibu yule mgeni kwa aibu na kuangalia chini. “WHO A BAHATI BAY THE WAY??” Aliongea Jothan na kumfanya Bahati kupiga magoti mbele yake na kuanza kulia kwa uchungu. “sihitaji kupigiwa magoti mama, mpigie magoti mungu wako na umuombe msamaha kwa ulichokitenda kwangu mimi.” Aliongea Jothan na kumuinua Shani pale chini. “naomba unisamehe, nimehadaika tu na jiji na hivi sasa limeshanifunza Jothan.” Aliongea Bahati huku analia. “leo hii unamjua Jothan wewe?.. si ulikua hunijui wewe?.. nani kakutajia jina langu?” aliuliza Jothan maswali mfulumizo yaliyomshinda Bahati kujibu na kubaki analia tu. “nyamaza kulia dada, kwani tatizo ni nini?.. niewekeni wazi jamani.” Aliongea Shani baada ya kukaa kimya muda mrefu. “sikiliza mke wangu, huyu dada ni mpumbavu na hana akili hata kidogo. Alikuwa na matatizo ya macho yaliyomsababishia upofu na hakuwa anaona hapo mwanzo. Mimi kwa imani yangu nikamchukua kutoka kwa mama yake Arusha na kuja naye hapa Dar kwa nia njema ya kumtibu. Sikuhitaji chochote kutoka kwake. Ila malipo aliyokuja kunilipa haki ya mungu kanifanya moyo wangu uwe na sugu na kuwa mgumu kuwasaidia wengine. Yaani alipopata macho ndio akaniona mimi takataka baada ya bosi wangu kumtaka. Siku niliyokutana naye akajifanya sauti yangu kaisahau. Yaani hata nilipojitambulisha bado akijifanya hanijui. Nikasamehe na kuachana naye, bado akaona haitoshi akaamua kunifanyia fitina mpaka nikafukuzwa kazi bila kosa. Sasa huyu utamuita mtu au kiatu tena kisichokuwa na kamba?” Aliongeea Jothan maneno yaliyomchoma Bahati na kumfanya aanze kulia kwa sauti kubwa zaidi ya aliyokuwa analia. “msamehe mume wangu, mungu kakujaalia umepata kazi nyingine. Na hujui kakuepusha na nini kukutoa kule. Na huyu adhabu yake ndio hii. Maana amepewa mimba na ametimuliwa. Hana msaada mwingine zaidi yako wewe. Msamehe tu mume wangu.” Aliongea Shani na kumsogelea Jothan aliyekuwa kafura kwa hasira na kuanza kumshika shika. Jothan alivuta pumzi ndefu kisha akamuangalia Bahati. “ni msaada gani unaotaka kutoka kwangu?” aliuliza Jothan na kumfanya Bahati kufuta machozi. “naomba unisaidie kunipeleka tu Arusha kwa mama yangu.” Aliongea Bahati huku analia. Kauli hiyo iliwaigia wote wawili. Ghafla walishangaa kumuona Jothan machozi yanamtoka kwa jinsi alivyokuwa anamuonea imani msichana mzuri walivyomtumia vibaya na kuwa kama kituko. Hakua Bahati yule kipofu mwenye bashasha usoni kila wakati. Sasa hivi mashavu yalimuingia ndani, nywele zake hazitazamiki mara mbili. Ngozi yake ilijaa makovu ya kupigwa kila sehemu. Jothan alijikuta ameguswa na kuanza kulia kwa sauti. Alinyanyuka huku analia na kumfuata Bahati na kumuinua kichwa chake na kuitazama sura yake iliyokuwa imelowa machozi na kuvimba kutokana na kulia kwa muda mrefu. “utakaa hapa mpaka utakapojifungua na kurudisha afya yako… pole sana kwa yaliyo kukuta.” Hatimaye aliongea maneno hayo yaliyomfanya Bahati kumkumbatia Jothan bila kujali uwepo wa mke wake pale. Wali muhurumia Bahati na kumpa chumba mule ndani. Siku tatu baadae, Bahati alipatwa na uchungu na kumuwahisha hospitali ya kulipia iliyopo kinondoni. Uchungu ulidumu kwa siku mbili mfululizo na kwa bahati nzuri Bahati alifanikiwa kujifungua salama mtoto wa kike. Aliwashukuru sana Shani na Jothan kwa utu wao waliouonyesha juu yake, maana walikuwa nae bega kwa bega na kuhakikisha kuwa anajifungua salama. Baada ya miezi mitatu kupita, Jothan aliamua kumsafirisha Bahati na kumrudisha kwao Arusha. Alilazimika kwenda naye kwakua Bahati hakua anapajua kutokana na hali yake ya upofu aliyokuwa nayo mwanzo. Walipofika Arusha mjini, Jothan alikodi taksi iliyowafikisha mpaka nyumbani kwa kina Bahati. Ilikuwa zaidi ya furaha kwa mama yake Bahati baada ya kumuona mwanaye akiwa anaona . alimfuata na kumkumbatia. “karibuni…. Karibuni nyumbani.” Alikaribisha mama huyo kwa Furaha. “ahsante, tumeshakaribia.”aliongea Jothan na kuingia ndani. Kwa furaha ya ajabu, mama huyo alikuwa anatabasamu kila muda kutokana na kumkumbuka mwanaye. Wakati wanaendelea na stori za kawaida. Ghafla mlango ulianza kugongwa kwa nguvu. Mama yake Bahati alitoka na kwenda kumsikiliza mtu anayegonga mlango. Alikaa huko kwa dakika kadhaa. Na baadae alirudi huku akiwa hana furaha kama aliyokuwa nayo mwanzo. “samahani baba, namchukua huyu tukatete kidogo.” Aliongea mama yake Bahati. “hamna shida mama.” Aliongea Jothan na kumfanya Bahati anyanyuke na kumfuata mama yake.. “mwanangu, aliyekuja kugonga ni mwenye nyumba. Amesema kuwa ametuchoka kutokana na kutomlipa kodi yake kwa muda mrefu. Yaani nimechanganyikiwa hata sijui tutafanyaje.” Aliongea mama yake Bahati baada ya kumuita mwanaye chemba. “usijali mama, nililijua hili ndio maana nikamuelezea Jothan mapema. Ametuahidi kutusaidia.” Aliongea Bahati na kumfanya mama yake amuangalie. “kwani, wewe na huyo Jothan mkoje?” Alijikuta mama yake Bahati anauliza swali lile kutokana na kutoelewa mazingira na makubaliano ya kumponyesha mtoto wake macho na kumrudisha akiwa na mtoto. “ni story ndefu mama, ila kifupi ni mkombozi wangu na wewe pia. Naweza sema hivyo.” Aliongea Bahati. “kwa hiyo unataka kusema kuwa hata huyu mtoto si wa kwake.” Aliuliza mama yake Bahati. “ndio mama.” Aliongea Bahati kimkato huku akitaka kumuonyesha mama yake ni jinsi gani asivyotaka kuaonngelea ile mada kwa muda ule. Baada ya muda Bahati alirudi sebuleni alipomuacha Jothan na mama yake akaenda kuandaa chakula cha jioni. “mbona hivyo, kwema?” aliuliza Jothan baada ya Bahati kurejea pale. “sio kwema, kama nillivyokuambia siku ile. Mama kashindwa kulipa kodi hivyo mwenye nyuumba anataka hela yake au tuhame.” Aliongea Bahati na kumuangalia Jothan. Baada ya chakula cha usiku, Jothan alimkabidhi mama yake Bahati fedha tasilimu shilingi laki saba kwa ajili ya kulipa deni la laki nne analodaiwa na hiyo nyengine kwa ajili ya mkataba mpya. Mama yake Bahati alifurahi kidogo machozi yamtoke na kumuombea sana dua za mafanikio Jothan. “naomba niwaache, naenda kulala Hotel na mungu akipenda kesho ndio safari yangu ya kurudi Dar-es-salaam” aliongea Jothan baada ya kuangalia saa yake ya mkononi na kumuonyesha kuwa ilishatimu saa tatu kamili. “sawa mwanangu. Mungu akutangulie katika kila jambo lako.” Aliongea mama yake Bahati na jothan akatoka huku Bahati akimsindikiza. “nakushukuru kwa yote ulioamua kuyafanya katika maisha yangu. Nakuomba usichoke kuwasaidia wasiojiweza kama nilivyokuwa mimi japokuwa nilikuumiza… kwa mungu kuna fungu lako Jothan.” Aliongea Bahati walipokuwa njiani wakisindikizana. “usijali, hata mimi naamini mambo yangu yananinyookea kwakua nakigawa kidogo kwa wenzangu wenye shida. Yale yalikuwa maneno tu tena kwa sababu nilikuwa na hasira. Mimi sina kinyongo na wewe. Moyo wangu mweupe na nakuombea pia maisha mazuri na ya furaha na mtoto wako. Naamini hutofanya makosa tena kwakua umeshajifunza.” Aliongea Jothan huku wakiikaribia bara bara. Baada ya kufika kituoni, waliagana huku Bahati machozi yanamtoka kwakujua kuwa ule ulikuwa mwisho wa kuonana na mwanaume huyo wa ajabu maishani mwake. Aliondoka huku kila baada ya hatua moja akigeuka nyuma kumtazama Jothan. Kwa mbali kulikuwa na gari linakuja spidi upande aliokuwa Bahati. Jothan alipotupa macho yake kuitazama ile gari ilikaribia kabisa kumgonga Bahati ambaye wakati huo Bahati hakuiona ile gari kwakua likua bize kumuangalia Jothan. Aliamua kutupa begi lake na kumkimbilia Bahati, alipofika tu alimsukuma na kwa bahati mbaya ile gari ilikuwa inajaribu kumkwepa Bahati na kumgonga Jothan. “MAAAMAAAAAA!” Alipiga kelele Bahati baada ya kumshuhudia Jothan akianguka chini baada ya kugongwa. Damu nyingi zilikuwa zinamtoka puani na mdomoni. Yule dereva aliyemgonga Jothan, alisimamisha gari na kumuingiza Jothan pamoja na Bahati na safari ya kuelekea hospitali kwa ajili ya kujaribu kuokoa maisha ya Jothan ilianza mara moja.. Walipofika hospitali, walipokelewa haraka na Jothan akakimbizwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. “jamani kwa hali ya mgonjwa wenu, anatakiwa kufanyiwa operation haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha yake.” Aliongea daktari na wote wakakubaliana kuwa tendo lile lifanyike. Bahati alikuwa mtu wa kulia tu usiku nzima. Alijua yeye ndio sababu iliyomsababishia Jothan kugongwa na lile gari.. Alilia na kumuomba mungu asimchukue Jothan. Alirudi nyumbani asubuhi na kumtaarifu mama yake juu ya kilichotokea. Mama yake alisikitika sana na kwenda hospitali ambapo walikaa kwa masaa manne bila kuruhusiwa kumuona mgonjwa. Walirudi nyumbani na kurudi tena hospitalini jioni ambapo waliruhusiwa kuingia ndani na kumkuta yule mtu aliyemgonga Jothan akwa pale hospitalini. Bahati alimuelekeza mama yake kwa yule mtu aliyeonekana na moyo wa pekee kwa kukubali kuisimamia afya ya Jothan kwa kipindi chote atakacholazwa pale hospitalini. “kwa maelezo ya dokta, amesema kuwa atarejewa na fahamu kiasi katikati ya wiki hii,.. ila itachukua muda mrefu kurudiwa na kumbukumbu.” Aliongea yule jamaa alyemgonga baada ya kujitambulisha kwa jina la Saimon. Baada ya taarifa zile, walikubaliana na kuondoka huku zoezi la kumuangalia Jothan likiwa linaendelea kila siku. Baada ya wiki mbili jothan alifumbua macho. Lakini hakuweza kuongea na hakuwa na kumbukumbu yoyote. “kwa hiyo dokta tunaruhusiwa kuondoka naye” aliuliza Saimon baada ya daktari kuridhika na maendeleo ya Jothan. “mnaruhusiwa, ila kwa masharti. Msimsumbue kwa kumlazimisha akumbuke kitu chochote. Maana kumbukumbu zake zitakuja taratibu kutokana na mazingira katika ubongo wake.” Aliongea dakrari katika moja ya kuwapa maangalizo juu ya mgonjwa wao. “sawa, sasa inaweza kuchukua muda gani hadi kurudiwa na fahamu zake sawa sawa?” aliuliza Bahati. “inaweza kuchukua miezi sita, nane au mwaka mzima kutokana na ukubwa wa tatizo lenyewe.” Aliongea daktari na kuwafanya wote waliokuwa pale waishiwe nguvu. Walikubaliana waondoke naye na kwenda kukaa kwa kina Bahati huku Simon akiwaambia kuwa atakuwa pamoja nao katika kila hali. Kutokana na kuchanganyikiwa siku aliyopata ajali Jothan, Bahati hakuokota kitu chochote alichokuwa amebeba Jothan siku ile. Hivyo hakuwa na mawasiliano angalau amjulishe Shani juu ya ajali iliyompata mpenzi wake. Siku zilikatika kwa kasi bila Jothan kuonyesha dalili zozote za kukumba yaliyokuwa nyuma. Hata jina lake tu alianza kulizoea baada ya Shani na mama yake kulitamka kila mara. Kwa upande wa Bahati alijisikia raha kumuuguza Jothan kwakua alikua analipa fadhila kwa yale aliyomtendea. Alihakikisha kuwa kila alichokihitaji mgonjwa wake basi alikua anakipata kwa wakati. Aliamua kurudia kazi yake ya kuuza maua ili alishe familia inayomkabili. Baada ya miezi sita kupita, Jothan alianza kuonekana kukumbuka kidogo kidogo. Aliweza hata kuuliza kuwa yupo wapi na ni nini kilichomleta pale. Alitamani kwenda kazini tena kama zamani. “PRISCA…… PRISCA” Alisikika Jothan usiku akilitaja jina la mwanamke huyo mara kadhaa. Bahati ambaye alikua amekaa kimya wakati wote, aliamka kutoka kwenye godoro la chini alipolala na mtoto wake na kumsogelea Jothan. Alishangaa kumuona Jothan akitokwa machozi. “mimi ni Bahati “ alijitambulisha Bahati mbele ya Jothan ambaye alikua macho usiku huo huku akitokwa na machozi. “yupo wapi Prisca.” Aliuliza Jothan na kumfanya Bahati ashtuke kidogo kwakua hakulifahamu jina hilo.. “Prisca mimi simjui… au ndio Shani ana majina mawili?” aliuliza Bahati na kumfanya Jothan afikirie kwa muda mrefu. “Shani.. Shani… ndio nani huyo?” aliuliza Jothan huku akionyesha kutokuwa na kumbukumbu nae. “si yule aliyekuwa unaishi nae kabla ya kuja huku ?” aliongea Bahati na kumfanya Jothan avute taswira juu ya mtu huyo aliyekuwa anamzungumzia Bahati. “huyo simkumbuki, yupoje kwani?” aliuliza Jothan na kumuangalia Bahati ambaye wakati huo alikuwa mbele yake akiongea kwa sauti ya taratibu kwa kuwa usiku ulikuwa tayari ni mkubwa. Hivyo sauti zao zilipea na kusikika kila mahali mule ndani. “ni mnene kiasi, mweupe na ana shepu Fulani hivi .. anapenda kuvaa ma wigi ya rihanna.” Alijaribu kumkumbusha Jothan kwa kumtajia muonekana halisi wa mtu huyo. “huyo simukumbuki,….. ninaye mkumbuka mimi ni msichana mzuri niliyeanza naye mapenzi toka tukiwa shuleni. Ni msichana mzuri sana. Na kila siku zilivyozidi kujongea, basi uzuri wake ulikua unaongezeka kila siku iendayo kwa Mungu. Nalikumbuka jina lake huyo dada. Anaitwa Prisca. Ila sijui muonekano wake kwa sasa. Labda ikitokea kuonana nae.” Aliongea Jothan huku akijaribu kuvuta hisia zake juu ya msichana huyo anaye mkumbuka kwa machache tu. “daktari alituambia kuwa tusikusumbue kwa kukumbusha ya nyuma. Ila utakumbuka taratibu. Ni vyema ulale Jothan ili uipumzishe akili yako.” Aliongea Bahati na Jothan akakubaliana nae. Kila siku ambayo Bahati alikua anarudi kutoka katika mihangaiko yake, aliutumia muda huo kupiga stori mbali mbali na Jothan. Wakati mwengine alimtembeza sehemu kadhaa maarufu. Kila akipata fedha nyingi, basi humchukua Jothan na kumpeleka shooping kwa ajili ya kumnunulia nguo. Baada ya miezi miwili kupita, Jothan alirejewa na fahamu zake kamili. Alikumbuka kila kitu. Hata siku aliyokuwa anataka kurudi Dar na kupata ajali ya gari pia aliikumbuka. Alimkumbuka pia Bahati ambaye wakati huo alikuwa naye bega kwa bega wakishirikiana na Simon ambaye alikua anakuja kumtembela mara kwa mara na kumuachia chochote kitu. Siku moja Jothan akiwa barazani anapunga upepo, alifuatwa na Bahati aliyekuwa amebeba Juice glasi mbili na kumkabidhi moja. Aliipokea na Bahati akakaa karibu yake. “lete story” aliongea Jothan baada ya kumuona Bahati kama alikua ana kitu Fulani alichokuwa anataka kumwambia. “nina mpya basi, zaidi kama hutojali. Nilikuwa nahitaji ushauri kutoka kwako.” Aliongea Bahati na kumtazama Jothan. “ulikuwa au unahitaji ushauri kutoka kwangu.” Aliongea Jothan kimzaha. “naomba unishauri,.. Simon ameniambia kuwa ananipenda na yupo tayari kufunga ndoa na mimi. Wewe kama wewe unamuonaje Simon. Anafaa kuwa mume wangu?” alifunguka Bahati na kumuangalia Jothan aliyekuwa anamuangalia pia. “kwa muda mfupi toka nimfahamu huyo mtu, sina shaka naye hata kidogo. Maana alikuwa na uwezo wa kukimbia siku ile aliyonisababishia ajali au hata kunikimbia hospitali. Lakini mpaka sasa ametupa hela nyingi kwa ajili yangu. Huwezi jua Bahati, si ajabu Mungu kamkutanisha na wewe kupitia mgongo wangu. Cha msingi zisikilize hisia zako maana wewe ndio utakuwa naye kipindi hicho mimi nitakapokuwa mbali na wewe. Kama na wewe unampenda na yeye yupo tayari kumlea mtoto wako ni dhahiri shahiri kuwa na yeye anakupenda pia.” Jothan aliongea maneno yaliyomkuna sawasawa Bahati. Alibaki anatabasamu na kumuangalia Jothan ambaye naye alikua anatabasamu pia. “nilikuwa nampenda muda mrefu sana, sema nashukuru sana kuwa hata yeye kumbe alikua ananifikiria.” Alingea Bahati. “hongera. Nilitaka kurudi Dar wiki hii, ila kama ndoa iatapangwa mapema basi nitasubiria mpaka muoane.” Aliongea Jothan na kumfanya Bahati afurahi kupita kiasi. Siku ya harusi kati ya Bahati na Simon iliwadia na maharusi walionekana kupendeza kupita kiasi. Jothan alilifurahia tukio lile baada ya Bahati kuonekana kubadilika na kuwa mwema na mtu mwenye jitihada kama alivyokuwa zamani. Baada ya siku mbili, Jothan aliaga na kurudi Dar. Kwakua hakuwa mgeni wa jiji, alitambua magari ya kinondoni na kuelekea kwake. Alifika nyumbani kwake na kukuta kufuli nje ya geti lake. Hakuwa na jinsi zaidi ya kukaa pembeni kwenye Café iliyokuwa inatazamana na geti lake ili Shani atakaporudi aweze kukutana naye. Alikaa mpaka saa mbili usiku, lakini hakukuwa na dalili za mtu yeyote kufika pale. Aliamua kwenda kulala Gesti kutokana na uchovu wa safari aliokuwa nao. Aliamka asubuhi na kupata chai, baada ya hapo akaelekea nyumbani kwake. Pia alikuta geti likiwa limepigwa kufuli kama ilivyokuwa jana yake. Aliamua kumfuata dalali mmoja aliyekuwa ameweka benchi lake pembeni ya nyumba yake na kumuuliza. “samahani mzee Sadi, hivi huyu mke wangu ana muda gani toka afunge hili geti?” aliuliza Jothan baada ya kusalimiana na mzee huyo aliyemzoe kwa muda mrefu akiwa pale nje na kufanya shughuli zake za udalali wa nyumba,viwanja na vyumba vya kupangisha. “hivi hauna habari?” aliongea mzee Sadi na kumshangaa sana Jothan kwakua alikua anajua kila kitu. “sina habari yoyote mzee wangu. Nimeingia jana tu kutoka Arusha, hivyo sina habari yoyote mie!!.” Aliongea Jothan kwa mshangao mkuu. Alianza kuhisi jambo baya linaweza kuwa lilimkumba Shani kipindi ambacho alikuwa hayupo. “mbona hii nyumba imeshauzwa miezi miwili iliyopita?… tena matangazo yalibandikwa muda mrefu. Sema wenye nyumba bado hawajahamia. Si unajua watu wenye fedha zao bwana?.” Aliongea yule dalali na kumfanya Jothan apigwe na bumbu wazi. “OOOOH MY GOD……..WHY ME?????” Alijikuta nguvu zinamuishia Jothan na kukaa chini. Aliiangalia nyumba yake aliyoijenga kwa gharama kubwa na machozi yalianza kummiminika kama maji. ITAENDELEA ... Read More
Story...... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na tatu (13) Ilipoishia....... Mzee Joel ndio hakuamini baada ya kuingia ndani na kukuta vijana wote wamelazwa chini alafu kidogo hivi akatokeza Nolan akiwa amepigilia suti nyeusi Kisha akamwambia baba yake ambaye ni mzee Joel, "naenda kwenye kikao cha harusi ya Penina na Frank na kama utahitaji kadi unijulishe nikuletee ya kwako." ***********Endelea ********* Nolan baada ya kumuambia baba yake maneno hayo aliingia kwenye gari na kuondoka. Nolan alifikia sehemu ambayo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kutengeneza kadi za harusi. Nolan alitengeneza kadi za harusi zisizopungua Mia moja hamsini kwa ajili ya harusi ya Penina na Frank. Kadi hizo hazikuwa za kuchangia harusi ya Frank na Penina bali kadi za mualiko. Nolan alijipanga kusimamia kila kitu Katika harusi ya Penina na Frank hivyo yeye alitengeneza kadi ambazo ni kama kiingilio cha kuhudhuria harusi hiyo bila kuchangia chochote. Nolan baada ya kukamilisha zoezi la kutengeneza kadi zile akaanza kutafuta ukumbi Mkubwa wenye hadhi ya kufanyia sherehe ya harusi ya Frank na Penina. Nolan alifanikiwa kuupata ukumbii ambao aliuhitaji na baada ya hapo Nolan akaanza kuzigawa kadi zile kwa watu mbali mbali ikiwemo na marafiki pia. Nolan moja kwa moja aliwasili nyumbani kwa kina Frank na kuwakuta Wazazi wake Frank ambao walimpokea kwa furaha Sana. "kikubwa kilichonileta hapa ni kuhusu harusi ya mtoto wenu Frank pamoja na mdogo wangu Penina, napenda kuwaafahamisha kuwa taratibu za harusi ya ndugu zetu hawa inaendelea vizuri na hapa nimewaletea kadi za mualiko." alianza kuongea Nolan baada ya kukaribishwa ndani na Wazazi wake Frank huku akiwakabidhi kadi zile Wazazi wake Frank. "Asante Sana kijana wetu na hongera Sana kwa hapa ulipofikia Mungu azidi kukusimamia zaidi na zaidi." wakaongea Wazazi wake Frank huku wakimshukuru Sana Nolan. "msijali Sana hii kazi ilikuwa lazima niifanye na lazima nitaitimiza, na kingine ninachotaka kukifanya kwa Sasa nataka niwahamishe hapa nyumbani kwenu niwapelekee sehemu mkakae hapo kwa siku kadhaa mpaka pale harusi ya mtoto wenu itakapokamilika, nafanya hivi kwa sababu ya usalama wenu kwasababu kuna vita kubwa inaendelea. " akaongea Nolan na kutoa maelezo hayo ambayo Wazazi wake Frank walikubaliana nayo bila wasi wasi wowote. Wazazi wake Frank pamoja na Mdogo wake Frank walijiandaa na kuondoka na Nolan ambaye aliwapeleka Katika hotel moja iliyopo nje kidogo ya jiji la dar es salam na kuwataka wakae hapo kwa wiki tatu kabla ya harusi ya Frank na Penina na gharama zote atazisimamia yeye Nolan. Nolan baada ya hapo alishika njia ya kurudi nyumbani kwa ajili ya kwenda kupumzika kidogo. * Dickson aliwasili Tanzania kwa Mara nyingine tena Ila awamu hii alikuwa na vijana wake wanne alioongozana nao. Baada ya kuwasili uwanja wa ndege moja kwa moja Dickson pamoja na vijana wake walichukua gari ndogo na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mzee Joel.* Mzee Joel alizidi kuchanganyikiwa baada ya kumaliza siku ya pili Sasa bila kumuona Penina na wala hajui ni wapi Penina alipo. Jambo hilo lilimvuruga Sana mzee Joel na kumfanya ashindwe hata kula chakula anachopikiwa na mkewe. Mzee Joel pia aliweza kuwasiliana na mkuu wa kikosi cha the killer na kumueleza jinsi vijana wake walivyoshindwa kuifanya kazi waliyoagizwa na kujikuta wakipokea kichapo kikali kutoka kwa Nolan. Mkuu yule wa kikosi cha the killer aliyejulikana kwa Jina la buffalo alipigwa na butwaa baada ya kupewa taarifa zile na mzee Joel. buffalo hajawahi kuamini kama kuna mtu yoyote anayeweza kupambana na vijana wake na akawaweza, hivyo taarifa zile zilimshangaza Sana. Buffalo akaamua ni lazima amjue huyo kijana ni nani aliyeweza kuwatandika vijana wake. "mzee hiyo kazi niachie mimi nitapambana nae mwanzo mwisho." akaongea buffalo kumwambia mzee Joel. Mzee Joel aliweza kumuelewa buffalo na kukataa simu na kumsubiri buffalo aingie kazini mwenyewe kwasababu yeye ndio mtu pekee Sasa aliyebaki wa kumtegemea. Dakika chache baada ya mzee Joel kuongea na buffalo, mzee Joel alipata taarifa kuwa kuna wageni nje wanahitaji kuonana na yeye. Mzee Joel alitoa ruhusa wageni hao wakaribishwe ndani. Kitendo bila kuchelewa wageni wale walifunguliwa geti na kukaribishwa mpaka ndani. Mzee Joel alishtuka baada ya kuona ugeni wenyewe ni wa Dickson pamoja na vijana wake wanne. "karibuni karibuni Sana." akaongea mzee Joel huku akijaribu kujichekesha japo hakuwa na amani hata kidogo. "hatuna haja ya kukaa mzee Joel, tumekuja kumchukua Penina nataka kujua kama inawezekana au haiwezekani?" akauliza Dick huku akionesha dhahiri kupandwa na hasira. "inawezekana kijana wangu tafadhali kaeni kidogo bas." akaongea mzee Joel kwa upole. "nimeshakuambia hatuna haja ya kukaa sisi tumekuja kumchukia Penina tu." akaongea Dick kwa msisitizo. "kijana wangu Dick naomba nipe muda wa siku mbili tu nitakuwa tayari nimeshakamilisha hili swala." akaongea mzee Joel kuwaambia wakina Dick. "Mzee umenipotezea Muda na umekula pesa zangu nyingi Sana, Sasa naondoka na kesho nitarudi unikabidhi Penina la sivyo pesa zangu utarudisha na utalipa Muda wangu nilioupoteza kwa ajili yako." akaongea Dick kwa jazba na kuondoka pamoja na vijana wake na kumuacha mzee Joel akitokwa na jasho jembamba. Baada ya dakika chache wakina Dick kuondoka Nolan naye aliwasili nyumbani na kumkuta baba yake akiwa na mawazo tele huku pembeni akiwa chupa ya pombe kali. "Baba shikamoo" akasilimia Nolan lakini alijua baba yake hataitikia salamu yake. Mzee Joel kweli hakuitikia salamu ya Nolan alibaki akimtizama tu kwa hasira. Nolan naye hakujali alitoa kadi tano za harusi ya Penina na Frank na kumwekea baba yake kwenye Meza iliyokuwa mbele yake. "karibu Sana Katika harusi ya Penina na mpenzi wake wa Muda mrefu Frank, wewe pamoja na rafiki Zako mnakaribishwa. " Nolan ndio alimwambia baba yake mzee Joel baada ya kumuwekea kadi zile kwenye Meza iliyokuwa mbele yake, Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake. ............ Itaendelea ... Read More
Story....... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya Tatu (3) BY GIVAN IVAN Ilipoishia........ Baada ya Penina kuondoka tu, Frank kabla hajapiga hata hatua moja kuondoka pale, ghafla alishtukia amezungukwa na vijana watatu wa kiume waliokuwa wamevalia miwani nyeusi kila mmoja. Na hata Frank alipowaangalia hakuweza kuwafahamu. .......... .. Endelea............ "tulia hivyo hivyo na sikiliza tunachokuambia." akaongea kijana mmoja huku akiwa ametoa kisu na kumuwekea Frank shingoni. Frank naye alikuwa kimya na kuwasikiliza walichokuwa wanataka kumuambia. "sikiliza wewe kijana wewe bado mdogo Sana, hivyo bas tunakusihi uachane na Penina haraka iwezekanvyo, hili ni onyo tu tunakupa na ukikaidi bas shingo yako tutaikata kama ya kuku." akaongea kijana ambaye alikuwa kiongozi wa wenzake, kijana huyo aliitwa Zaza. Baada ya Zaza kumwambia Frank maneno yale ya kumtisha aliondoka na wenzake na kuingia kwenye gari moja nyeusi iliyokuwa imepaki pembeni Yao, Kisha gari likaondolewa kwa kasi ya ajabu huku dereva wao akiwa ni mwanamke anayejulikana kwa Jina la Melissa, moja Kati ya vijana waliopewa kazi nzito ya kuliharibu penzi la Frank na Penina. Frank alianza kuingiwa na hofu na kujiuliza "ni nini tena kinaendelea juu yake? " Frank alijivuta na kuondoka sehemu Ile na kuingia nyumbani kwao akiwa mnyonge kuliko kawaida yake. " eeh kaka vip mbona mnyonge hivyo kulikoni tena? " akauliza Angel mdogo wake Frank. " aah kuna vijitu vinataka kuniharibia siku hapo nje." akajibu Frank na kuketi kwenye kigoda. "watu gani tena hao mwanangu?" akauliza pia mama yake Frank. "mama kuna watu hapo nje wamenisimamisha na kunitishia niachane na Penina la sivyo wataniua." akaongea Frank kuwaambia wazazi wake wakiwa wamepigwa na butwaa. "haa mwanangu katoe taarifa haraka polisi kwa usalama wa maisha yako." akaongea baba yake Frank kumpa ushauri mtoto wake. "Polisi siendi baba nachojua mimi Penina ni mpenzi wangu nampenda na yeye ananipenda, yoyote atakayeingilia penzi langu na Penina ama zake ama zangu na kukuonesha mfano naanza na hawa walionitisha leo." akaongea Frank kwa jazba Kisha akanyanyuka na kuondoka kuelekea chumbani kwake. "kuwa makini mwanangu tusije tukakupoteza mapema." akaongea baba yake Frank, lakini Muda huo Frank alikuwa ameshatoweka mbele ya macho yao. "Mimi ni mwanaume rijali nitakubalije kutenganishwa na Penina kirahisi hivi?" alikuwa Frank akijiuliza swali hilo huku akizunguka zunguka chumbani kwake. "naamini hakuna mwenye uwezo wa kunitenganisha mimi na Penina isipokuwa Mungu tu." akaongea Frank huku sasa akiwa amejilaza chali kitandani kwake.* Hatimaye Penina naye aliwasili nyumbani na Muda huo ikiwa ni majira ya saa tatu usiku. Geti lilifunguliwa na taratibu Penina akaingiza gari ndani na kulipaki sehemu yake, Kisha yeye akashuka na kuanza kuelekea ndani Katika jumba la kifahari kwa mwendo madaha kama kinyonga. Lakini kabla hajaingia ndani alikutana na baba yake mlangoni ambaye alionesha wazi kuwa alikuwa anamsubiri Penina. "shikamoo baba!" akasalimia Penina, lakini baba yake badalaa aitikie salamu ile akamuuliza Penina, "umetoka wapi usiku huu?" "nilikuwa na mpenzi wangu Frank kuna sehemu tulienda ndio narudi Sasa hivi." Penina akamjibu baba yake bila uoga. "wewe ni Mara ngapi nimekukataza kurudi nyumbani kwangu usiku? Na si nimeshakuambia uachane na huyo chokora wako?" akauliza baba yake Penina huku akiwa amezira. "Kwa kosa la kurudi nyumbani usiku naomba unisamehe baba yangu, Lakini muda si mrefu nitakuondolea hii kero ya kurudi nyumbani usiku kwasababu mimi na huyo mpenzi wangu unayemuita chokora tumeshaanza harakati za kufunga ndoa na tutahamia kwetu muda si mrefu." akaongea Penina kumuambia baba yake bila uoga wowote. "hivi wewe mpumbavu unajua unaongea na nani? Maana naona unaropoka ropoka tu kama umekunywa maji machafu." akaongea baba yake Penina. "ndio najua naongea na nani, najua naongea na wewe hapo baba yangu kipenzi tena nakupenda Sana lakini najua wewe hunipendi." akaongea Penina maneno hayo ambayo yalimfanya baba yake apoe kidogo. "hapana mwanangu sio kwamba sikupendi, nakupenda sana tena Sana Ila huyo unayemuita Frank mi ndio ananikera kupita maelezo yaani nikimuona nahisi hata kutapika." akaongea baba yake Penina kwa upole kidogo. "Baba unataka niachane na Frank?" akauliza Penina. "ndio mwanangu tena nitafurahi Sana na nitakupa zawadi kubwa Sana." akaongea baba yake Penina. "ok bas subiri kidogo." akasema Penina Kisha akaondoka kwa Kas mpaka jikon ambapo alichukua kisu na kurudi nacho mpaka kwa baba yake. Wakati hayo yote yanatendeka Noel ambaye ni kaka yake Penina alikuwa akiyashuhudia yote hayo. "kama unataka niachane na Frank niue kwasababu hiyo ndio njia pekee." akaongea Penina huku akimkabidhi baba yake kisu kile. "haa mwanangu Sasa huu utoto gani unaleta mbele yangu?" akauliza baba yake huku akikitupa kisu kile pembeni. "sio utoto baba bali namaanisha ninachokiongea, na kama umeshindwa kutekeleza nilichokuamuru bas tambua hakuna wa kunitenganisha na Frank na siku si nyingi tutafunga pingu za maisha, na sitojali kama wewe utaudhuria ama hutoudhuria." akaongea Penina kumuambia baba yake Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake. Nolan naye alitoka sehemu aliyokuwepo akisikiliza malumbano ya Penina na baba yake na kumfuata Penina chumbani kwake. Huku nyuma baada ya Penina kuondoka, baba yake alitoa simu yake na Mara moja akampigia Zaza. "hallow mzee Joel.!" akaongea Zaza baada ya kupokea simu. "Zaza nisikilize kwa makini, Penina na yule chokora wapo Katika mipango ya kufunga ndoa, Sasa nachotaka mfanye ni kuwatenganisha kwa namna yoyote ile, mnachotakiwa kufanya ni kumteka nyara huyo chokora alafu mkamtupe mbali kabisa sehemu ambayo mnajua anaweza chukua hata mwaka mmoja Kuja kuonana na Penina tena. " akaongea mzee Joel kwa kusisitiza (mzee Joel ni baba yake Penina) " Sawa hamna shida mzee wetu tutafanya hivyo." akajibu Zaza. "ok bas fanyeni haraka iwezekanavyo kama mtahitaji pesa zaidi mtanijulisha." mzee Joel akamwambia Zaza na kukataa simu. * Penina baada ya kuingia chumbani kwake ghafla kaka yake naye akaingia pamoja naye. "hee kaka kumbe ulikuwa nyuma yangu?" akahoji Penina kwa mshangao. "ndio na pia nilikuwa nasikiliza malumbano yenu mzee." akaongea Nolan ambaye ni kaka yake Penina. "yaani kaka wewe acha tu, baba angejua navyompenda asingenifanyia hivi anavyonifanyia." akaongea Penina kwa huzuni kumuambia Nolan. "Ila mdogo wangu usijali wewe simamia kile unachokiamini na mimi nitakuwa nyuma yako kukusaidia." akaongea Nolan kumtia moyo Penina. "nashukuru kaka kusikia hivyo angalau wewe ndio uko upande wangu." akaongea Penina kumshukuru kaka yake. "usijali mdogo wangu wewe lala kwa amani tutaonana kesho." akaongea Nolan na kuondoka chumbani kwa Penina.* Kwa upande wa kina zaza usiku ule ule walianza kupanga mikakati ya kumteka Frank na kwenda kumtupa mbali kabisa na jiji la dar es salam. Lakini hii ilikuwa kazi ngumu Sana ambayo walihitaji pesa za kutosha na pia wachore ramani ya sehemu watakayoenda kumtupa Frank. ....... Itaendelea ... Read More
Story......... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya Sita (6) By GIVAN IVAN PHONE & whatsapp ____0769673145 Ilipoishia........ "Eeh Mungu Kwanini unaniacha niteseke hivi? Kama huu ndio mwisho wa maisha yangu bas naomba unichukue haraka usiniache nife Katika mateso makali kiasi hiki." akajisemea Frank kwa sauti ya chini akimuomba Mungu wake. Lakini hata hivyo baada ya masaa mawili mbele, aliweza kupita mzee mmoja aliyekuwa akichunga ngombe, karibu na sehemu Ile aliyotupwa Frank na pia akaweza kumuona Frank akiwa amelala pale chini akiwa hajiwezi kwa lolote. ***********Endelea ******* Mzee yule aliweza kumsogelea Frank na kumfungua kitambaa cheusi alichofungwa usoni. "kijana umepatwa na nini." akauliza mzee yule baada yule baada ya kumfungua Frank usoni. "kwa kwa kwani ha ha hapa ni wapi?" akauliza Frank kwa taabu badala ya kujibu swali aliloulizwa. "hapa ni tabora kwani umepatwa na nini?" akajibu mzee yule na kumuuliza tena Frank. Frank hakuamini kusikia eti yupo tabora, akamwambia mzee yule, "nimetekwa na Kuja kutupwa huku tafadhali naomba nisaidie nina njaa Sana." aliongea Frank kwa taabu kumuambia mzee yule. "ooh pole Sana kijana wangu, wewe kwenu wapi?" akauliza mzee yule huku akimfungua Frank kamba za miguuni pamoja na mikononi. "Tafadhali mzee wangu naomba nisaidie nipate hata maji ya kunywa nakufa mzee wangu." akaongea Frank kwa uchungu Sana. Mzee yule alimwonea huruma Frank kwa jinsi alivyokuwa anaongea na hali mbaya aliyokuwa nayo. Mzee yule alimbeba Frank na kumpeleka mpaka kijumba chake kilichotengenzwa kwa nyasi huku pembeni yake kukiwa na zizi kubwa la ngombe. Mzee yule baada ya kufika alimlaza Frank chini kwenye ngozi ya ngombe, Kisha akamletea maziwa na kuanza kumnywesha Frank. Frank aliweza kupata nguvu kidogo baada ya kunywa maziwa karibia Lita mbili. Baada ya hapo mzee yule alimletea Frank nyama iliyochomwa na kumkambidhi Frank. Frank alianza kula nyama Ile ambayo hakujua ni ya mnyama gani. Baada ya masaa kadhaa Frank aliweza kurudia kwenye hali yake ya kawaida, lakini sasa mawazo yakaanza kumtawala kwa kumkumbuka mpenzi wake Penina. Frank alianza kukumbuka jinsi alivyoongea na Penina kwenye simu na kukubaliana kukutana baada ya dakika kadhaa, lakini pia akakumbuka namna alivyotoka nje kumsubiri Penina lakini baada ya hapo hakukumbuka tena kilichotokea mpaka pale alipokuja kushtuka na kujikuta yupo kwenye gari na baadae kujikuta yupo pale msituni na kusaidiwa na mzee yule. Lakini Frank alikumbuka pia alikuwa na simu lakini alipoitafuta mfukoni hakuiona. Frank alihuzunika sana kwa hichi kilichomtokea, hakujua ni wakina nani wamemfanyia kitendo kile. Frank bado alikumbuka mengi Sana aliyokuwa ameongea na Penina, lakini Sasa alikuwa akiwaza kama ataweza kukutana tena na Penina. "kijana, kijana, kijana" Frank alishtushwa na sauti ya mzee yule ikimuita na hapo na hapo ndio akatoka kwenye mawazo Yale na kumuitikia mzee yule. "naam mzee wangu." akaitikia Frank na kumtizama mzee yule. "inaonekana una mawazo Sana nimekuita zaidi ya Mara tano bila mafanikio una matatizo gani kijana wangu." Akauliza mzee yule huku akionekana kumhurumia Sana Frank. "Mzee wangu nina matatizo makubwa Sana." akaongea Frank huku akitokwa na machozi. "mzee wangu yaani kuna watu wanataka kuniangamiza kwasababu tu ya mwanamke." akazidi kuongea Frank kwa uchungu. "hebu nyamaza bas unielezee vizuri na uniambie unaitwa Nani, jikaze wewe ni mwanaume." akaongea mzee yule huku akimpiga piga Frank mgongoni. "kwanza kabisa mimi naitwa Frank na sababu kubwa ya mimi kuwa hapa Sasa hivi ni kwasababu ya mapenzi." akaongea Frank na kumsimulia mzee yule simulizi fupi ya mapenzi yake na Penina huku pia akimuelezea jinsi ambavyo mzee Joel baba yake Penina hataki yeye Frank amuoe mtoto wake Penina. "pole Sana kijana wangu Frank, lakini nataka nikuambie tu kama kweli huyo mwanamke anakupenda kutoka moyoni, lazima atakusubiri mpaka pale utakaporejea." akaongea mzee yule kumpa moyo Frank. "mimi kweli yule mwanamke ananipenda Sana, lakini atajuaje niko hai mpaka Sasa?" akaongea Frank na kuhoji. "kijana acha kuwa na mawazo potofu kinachotakiwa kwa Sasa na ufanye kazi upate pesa ya kurudi dar es salam shilingi elfu sabini." akaongea mzee yule kumuambia Frank. "lakini hapa inaonekana ni msituni kabisa Nitapata wapi kazi Sasa.?" akahoji Frank kwa mshangao. "ndio hapa ni msituni hujakosea tena huku ni msituni ndani ndani kabisa na kutoka hapa kuelekea tabora mjini ambapo ndio kuna magari ya kuelekea dar es salam kwa miguu huwa tunatumia siku Tatu." akaongea mzee na kumuacha Frank akiwa ametumbua macho. "kwani hamna magari?" akahoji Frank. "huku msituni magari yatoke wapi kijana unataka kuchanganyikiwa.?" mzee yule akamuuliza Frank kwa mshangao. "mpaka hapa mzee wangu nishachanganyikiwa." akaongea Frank huku akiwa ameshika kichwa. "sikiliza kijana nikuambie, wewe ni mwanaume na siku zote mwanaume huwa hakati tamaa, pumzika hapa kwangu kwa siku mbili nikuandae uweze kuanza safari ya kuelekea tabora mjini kwa ajili ya kurudi kwenu wewe sio wa kuishi huku msituni. " akaongea mzee yule kumuambia Frank ambaye alikuwa kama haamini kilichomtokea. * *******Dar es salam ****** " yes Dickson habari yako? " " Habari yangu nzuri Sana hamjambo huko? " " hatujambo kabisa Dickson uko wapi? " " kwa Sasa niko Kenya kuna biashara nafanya halafu kesho nitakuja Tanzania. " " ooh Safi Sana Dick na pia karibu Sana nyumbani uje umuone mpenzi wako." "Ok Asante Sana nitakuja kumuona mpenzi wangu usijali." "Sawa bas nakutakia Kaz njema na safari njema." "Asante mzee Joel." Hayo yalikuwa mazungumzo ya mzee Joel pamoja na kijana mmoja kutoka nchi Norway aliyeitwa Dickson (Dick) ambaye ndio mzee Joel anatarajia aje amuoe mtoto wake Penina. "Kesho kuna mgeni maalumu atakuja hapa nyumbani nataka mumpokee kwa heshima na adhabu ya kutosha mmesikia?" akaongea mzee Joel akiwaambia watoto wake watatu, Nolan, Irene, Penina pamoja na mke wake ambao wote walikuwa sebuleni. "mgeni kutoka wapi na ni wa jinsia gani?" akahoji Nolan baada ya kuhisi kitu. "nimesema kuna mgeni anakuja na nataka mumpokee kwa heshima ya hali ya juu hayo maswali mengine sihitaji kuulizwa." akaongea mzee Joel kwa msisitizo. "ok Sawa." akajibu Nolan na kunyamaza.* Katika familia ya kina Frank furaha ilitoweka kabisa Katika nyumba yao kutokana na kutoweka kwa Frank na ikiwa imetimia wiki moja bila kujulikana alipo Frank.* Siku aliyokuwa anaisubiri mzee Joel ya kukutana na kijana mzungu anayeitwa Dick hatimaye iliwadia. "Penina mwanangu naomba nisikilize na unielewe mimi kama baba yako, Frank nimepata taarifa zake kuna sehemu ameonekana huko arusha akiwa na mwanamke mwingine Sasa ya nini kungangania mwanaume ambaye hajatulia?" akaongea mzee Joel na kumuuliza Penina ambaye alibaki kimya tu. "Mwanangu ngoja nikuletee mwanaume mzuri ambaye anaendana na wewe, mzuri kama wewe na mwenye elimu kama wewe achana na yule muokota makopo Frank." akaongea mzee Joel kumwambia Penina, lakini Penina bado alikuwa kimya tu akimtizama baba yake bila kumjibu kitu. Lakini mzee Joel hakujali ukimya wa Penina, yeye aliingia kwenye gari na kwenda kumpokea Dick Kuja kumuona Penina. Baada ya mzee Joel kuondoka. Machozi yalianza kutiririka usoni mwake baada ya kumkumbuka mpenzi wake Frank. Baada ya masaa mawili mbele mzee Joel alirejea nyumbani akiwa pamoja na mgeni wake. Geti lilifunguliwa na mlinzi na gari likaingia mpaka ndani na kupaki sehemu yake. "karibu Sana kuwa huru." akaongea mzee Joel huku akimfungulia Dick mlango wa gari. ........ Itaendelea ... Read More
HOUSE GIRL DIARY; NAITWA RAYA NI HOUSE GIRL MSTAAFU! Nilikua mgeni katika ile nyumba, ingwa haikua mara yangu ya kwanza kufanya kazi za ndani lakini bado nilikua ninaogopa ogopa Dada (Mama mwenye nyumba) alionyesha mkali sana kwani ile kuingia tu alishanipa mashariti elfu kidogo. Nilishaambiwa sehemu ambazo siruhusiwi kukanyaga, vitu ambavyo siruhusiwi kugusa na majina ya kuwaita wote mule ndani. “Sitaki unite Mama unanizeesha unafikiri mimi naweza kuzaa kinyago kama wewe!” Hiyo ndiyo ilikua kauli yangu ya kwanza kukaribishwa nayo mara tu baada ya kumsalimia na kumuita Mama. Kweli hakua mtu mzima, lakini kwakua katika nyumba niliyoondoka nilikua nimezoea kumuita bosi wangu Mama nilijua ni heshima nayeye atapenda kuitwa hivyo. “Huko ulikotoka kwanini ulifukuzwa?” Aliniuliza kwa hasira, sijui hata nilimfanya nini lakini alionekana na kisirani chake tu. “Sikufukuzwa dada niliamua tu kuondoka, walikua …” “Eeeeh! Mimi si shoga yako kuanza kuniambia matatizo yako, nyamaza nishakuambia sitaki kukusikia, nenda jikoni huko! Unajua kupiga au niwakufundishwa kila kitu!” Alinikatisha kabla ya kujielezea kisha kuendelea kufoka. Nilimuambia najua akaniambia niingie jikoni kuanza kazi. Ulikua mchana kwani niliondokea kwa Shangazi yangu (si Shangazi kweli ni mtu ambaye alinilete tu mjini). Niliingia jikoni na kukuta lundo la vyombo, sikua na haja ya kuelekezwa, nilishakua House Girl mzoefu hivyo nilijua nini cha kufanya. Nilianza kuosha na ulipofika wakati wa kupika nilimuuliza tunapika nini. Nashukuru safari hii alinijibu vizuri hivyo nilichukua kile nilichelelekezwa na kumpikia. Kutokana na kelele za nyumba niliyotoka na uzungu wa Bosi wangu wa zamani nilikua najua kupiga si kitoto, ile milenda milenda yangu ya kijijini niliiacha huko huko hivyo nilipompikia tu na kuweka chakula mezani, alikifurahia ingawa hakusema chochote lakini hakulalamika, hiyo ilikua dalili njema kwangu. Katika nyumba niliyotoka baada ya kuwatengea chakula nilikua nasubiri mpaka wamalize kula, hii ni kwasababu kama kikitokea kitu cha kutumwa basi niwepo kuwasikiliza. Huwa nasimama pembeni kama wale madhouse girl wa kwenye TV kusubiria mpaka mabosi wangu wamalize kula ndiyo huingia jikoni na kujitengea chakula changu. Nilishazoea hivyo na kwakua ilikua ndiyo nyumba yangu ya kwanza nilijua labda mjini kote ndiyo hali ilivyo. “Unasubiri nini hapo si uende jikoni huko ukajipikie au wewe huli?” Aliniuliza kwa hasira, nilitaka kumjibu kumuelezea nilivyozoea lakini hakutaka kusikiliza, jicho alilonikata niliondoka kama chizi nikikimbia. Nilifika jikoni na kupakua chakula, nilikaa chini ili kula. Lakini kabla hata sijafikisha tonge mdomoni alikuja, alikua kasimama pembeni yangu. “Ndiyo unafanya nini?” Aliniuliza, macho yake yalikua katika chakula. “Nakula ma…dada…” Kidogo nisahau na kumuita Mama. “Pumbavu unakula nini? Yaani unakula chakula ambacho ninakula mimi! Hivi una akili kweli unataka kuwa sawa na mimi, nikulipe elfu thelathini na chakula ule kama mimi!” Aliongea kwa hasira, alikipiga teke chakula kisha kutoka, alirudi na ndoo ya dagaa na kunirushia. “Kuna ndoo ya dona iko hapo, pika ugali wako ule. “Aliongea kwa hasira huku anaondoka, alienda kwa sekunde kadhaa na kurejea. “Upike mwingi kuna mwenzako anatoka shule atakuja kula na wewe!” aliondoka na kuniacha pale. Nilianza kuchambua Dagaa ambao wengi walikua wameoza, unakutana na wadudu kabisa. “Haya mapya! Nimeruka mkojo nimekanyaga mavi!” Niliendelea kujiongelesha huku nikichambua dagaa ambao walishaanza kunitia kichefuchefu. Huko nilikotoka nilikua nanyanyaswa lakini angalau nilikua nakula chakula cha mabosi wangu hata kama nilikua nalia jikoni! *** Jioni jioni hivi kama saa kumi na nusu watoto wake walikuja, walikua watatu. Mmoja mkubwa kuliko wenzake Jackline na wengine wadogo Joan na John, hawa walilingana kwani walikua mapacha. Baada ya kubadilisha nguo niliambiwa niwatengee chakula, nilifanya hivyo kwa kuweka sahani tatu mezani. Lakini Jackline ambaye alikua na miaka kumi hakukaa mezani, alikuja jikoni ambapo nilikua naandaa chakula cha usiku. “Wewe ndiyo Dada mpya, shikamoo…” Alinisalimia tena kwani alishanisalimia wakati nawafungulia geti ili waingie. Niliitikia kwa wasiwasi kwani nilishaambiwa nisiongee na wanae hivyo niliogopa hata kumjibu salamu. “Chakula changu kiko wapi?” Aliuliza, huku akikaguakagua vyombo. “Chakula si nimeshawatengea sebuleni?” Niliuliza kwa mshangao, hasira zilinipanda kidogo kwani nilishajua kuwa kumbe mbali na kudili na Bosi kichomi basi ningedili na mtoto mdogo kama yule ambaye ana kisirani. “Baba amesafiri mimi siruhusiwi kula sebuleni nnatakiwa kula na wewe!” Sikumuelewa niliuliza mata mbilimbili ndipo kwa utulivu kabisa alinieleza kuwa yule hakuwa Mama yake mzazi bali ni Mama wa kambo hivyo kila Baba yake anaposafiri yeye haruhusiwi kula chakula sebuleni na wengine mpaka anaporejea. Chakula anachokula ni cha Dada wa kazi. Kusema kweli hilo lilikua jingine jipya, labda kwakua nilikua sijafanya kazi katika nyumba ambayo Bosi ana mtoto wa kambo. Niliwaza kile chakula ambacho nilipika kwaajili yangu, nikawaza wale dagaa kisha nikamuangalia yule mtoto na kumuambia. “Jack, si unaitwa Jack… “Nilimuuliza. “Ndiyo Dada!” Alijibu kwa upole. “Huwezi kula kile chakula, hata mimi kimenishinda, hembu ngoja nikutengee kingine, mbona kiko kingi tu watamwaga hawa!” Niliongea huku nikimtafutia sahani ili kumpakulia chakula lakini alikataa katakata, aliniambia nitapigwa sana kama nikila chakula kingine. Alinionea huruma mimi pia nakuniambia hata Dada mwingine alifukuzwa kazi kwakua alikua ananipakulia chakula cha wengine. Alionyesha kuogopa mpaka na mimi nikaogopa kwa namna alivyokua anaogopa. “Huyu ni mwanamke wa namna gani mbona yuko hivi!” Niliwaza nikimuangalia Jackline, alikua kachoka lakini alijitahidi kuonyesha yuko sawa, mara kwa mara alikua akitabasamu huku akijilazimisha kucheka. Aliniongelesha ongelesha kutaka urafiki, kweli nilimuonea huruma machozi yalinilengalenga. Kwangu ule ulikua ni mtihani mpya ambao sikujua nitaumalizaje. *** Siku mbili baadaye Baba mwenye nyumba alikuja, huyu yeye niliambiwa nimuite Baba na nilifanya hivyo bila kuuliza maswali. Alikua ni kijana tu wa makamo au sijui niseme mtu mzima mwenye muonekano wa kijana. Alikua mchangamfu na alipokuja kila mtu alikua na furaha, si Jackline au watoto wake wengine nyumba ilikua kama imemwagiwa gunia la furaha. Hakukua na kupika mara mbilimbili, hata mimi niliambiwa nikae kwenye meza kubwa, hakukua na kutumwa tumwa kwani Baba akiwepo wakati wa kula ni kula na wote alituchukulia kama wanae. Ilikua ni kama unaishi katika nyumba nyingine tofauti kabisa, Dada alikua mchangamfu akiongea kwa kucheka mara kadhaa akimkumbatia Jackline. Hata mimi alinitambulisha kwa bashasha akinisifia kwa ufanyaji kazi wangu. Kweli nilishangaa “Mbona sielewe, huyu Mama yako wa kambo mbona kama anabadilika sana kama si yeye?” Nilimuuliza Jackline, alijiibaiba kukaa jikoni wakati wenzake wakiangalia TV, Baba yake akiwepo alikua haruhusiwi kufanya kazi yoyote. “Nimeshamzoea, anaigiza tu Baba akiwepo?” “Kwahiyo Baba yako hajui chochote?” “Hapana, nilishamuambiaga zamani lakini hakuniamini, niliishia kupigwa tu. Nilimuambia Mama kwanza aliposema kwa Baba akaambiwa nina wivu hivyo kukatazwa hata kuja kuniona, ilileta ugomvi mkubwa siku hizi kila nikilalamika naambiwa nimetumwa na Mama kuja kumfitinisha Mama Mdogo…” “Mama yako wewe yuko wapi? Kwanini huendi kuishi na Mama yako?” Yuko kijijini, waligombanaga na Baba zamani, hawakuoana, Baba alinichukua nikiwa mdogo na kunileta hapa, mimi sijui mambo hayo ila Mama yangu naongea naye tu kwenye simu mara moja moja lakini simkumbuki hata sura, hata sijui mimi mambo yao.” Aliongea kana kwamba ni mtu mzima, alionyesha kupitia mambo mengi na hakukua na mtu wa kumsikiliza. Nilipokuja kufuatilia nilikuja kugundua kuwa Mama yake na Baba yake hawakua wapenzi, ni watu tu walikutana na mimba ilipotokea basi Mama yake alivyokua akidai matumizi kipindi hicho ashaoa aliamua kumnyang’anya mtoto kwa nguvu. Kwao ni Iringa hivyo alimnyang’anya na kumchukua kipindi akiwa na miaka minne na tangu wakati huo alikua akiwasiliana naye kwa simu tu. Ana Mama yeka mkubwa, Dada wa Mama yake ambaye yuko Dar lakini naye haruhusiwi kumuona kwani ndiyo alimuambia kuhusu manyanyaso na kumuambia Mama yake ambaye alipoongea na Baba yake ukawa ugomvi mkubwa. Sikua na la kuongea zaidi ya kunyamaza tu kwa namna alivyokua akiongea ni kama alishakata tamaa ya maisha muda mrefu, sikujua ni kwa namna gani naweza kumsaidia kwani hata mimi nilikua na matatizo yangu. Usiku wakati wa kulala sikuolazwa stoo kama kawaida, hapana, niliambiwa natakiwa kulala katika chumba kimoja na Jack. Ulikua ni utaratibu wao, Baba akiwapo na mimi nakua mtoto na lala chumba kimoja na Jack. Usiku baada tu ya kuingia Jack alizima taa, nilishangaa kwani hata kitandani nilikua sijafika, nilimuuliza kwanini anazima, nikihisi labda ni Mama yake hapendi. Nilisogea na kuwasha, alishtuka, ni kitu amcho hakukitegemea. Alikua anavua nguo ili kuvaa nguo za kulalia, nilipowasha taa tu alianza kujificha kama vile anaona aibu. Nilishangaa kwani mimi ni mwanamke mwenzake, “Dada zima taa, zima taaaa!” Alipiga kelele, alionyesha kushtuka akijificha, lakini badala ya kuficha hata sehemu za siri alikua anaficha mgongo wake. Nilitaka kuzima lakini kabla ya kufanya hivyo macho yangu yalitua katika mgongo wake, ulikua kama ramani ya Tanzania, ulijaa makovu mengi ya fimbo, mengine mabichi kabisa kama vidonda. Sikuzima, sasa nilijua sababu ya yeye kuzima taa hakutaka nione makovu. Nilisogeza macho mpaka kwenye mapaja na sehemu za siri huko ndipo kuliharibika zaidi. Hapo ndiyo nilijua ni kwanini mara kwa mara huwa anakunja uso hata akiegemea sehemu au kugusa mapaja yake. Nilimsogelea na kumkalisha chini, alianza kulia kabla ya kusema chochote. “Kwanini humuambii Baba yako, kwanini humuonyeshi haya makovu? Akiona atakuamini!” Niliongea kwa hasira, sikua na muda pale lakini kwa upendo aliokua nao yule Baba sidhani kama angeweza kumuona mwanae katika hali ile na kunyamaza kimya. “Namuambia Baba yako, hii kazi ishanishinda, ngoje nifukuzwe lakini niondoke na huyu Sherani!” Niliongea huku nikinyuka kwenda kumgongea Baba yake, tayari walishaingia chumbani kulala. Jack alinifuata akilia kunibemebeleza ili nisiende akiogopa kuwa atamuua lakini sikujali, nilijua ni uoga ambao mimi kama mtu mzima nisingeweza kuuruhusu. Ushahidi alikua nao na hakukua na haja ya kuendelea kuteseka hata siku moja katika nyumba ya Baba yake. Alinisihi sana lakini sikumsikiliza, nilitoka mpaka sebuleni, alinifuata akiwa vilevile uchi kasahau kuvaa nguo, analia, nilielekea mpaka mlangoni kwa wazazi wake. Bado alikua analia, huku akiongea kwa kunong’ona. “Dada Raya, Dada Raya usimuambie, usiongee chochote, mimi niko sawa niliumia Shuleni, sio Mama aliyenipiga, ni ukorofi wangu tu!” Alipiga kelele kuniomba nisiseme. ITAENDELEA… (Hiki ni kisa cha kweli ingawa majina yaliyotumika hapa hayahusiani na wahusika. Hii ni sehemu tu ya simulizi kutoka kwa wadada wakazi “House girls” ambazo nitakua nikiwaletea. Je unadhani kama Raya atagonga mlango na kumshitaki Mama wa kambo, je Baba Jack akiambiwa atachukua hatua gani, kesho si mbali sana tukutane kwa sehemu ya pili hapahapa kwenye ukurasa huu…” ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: