'SOMA STORY HII FUPI KISHA UJIFUNZE' *INAITWA* _______MSOMI!?.________ SEHEMU: Mwanzo/Mwisho.... __UTANGULIZI__ MSOMI;Ni neno ambalo linawafanya watu hususani vijana ambao wameweza kufika vyuo vikuu kuwa watu wa majigambo sana mbele ya jamii zao na hata wengine udiriki kufikia hatua ya kusahau marafiki zake ambao alicheza nao ilimradi tu anamarafikia zake wasomi, Na pia vijana wengi wanapofika vyuoni hubadirika kabisa tabia... TUWEMO KATIKA MKASA HUU WENYE UHALISIA WA KWELI... Ilikuwa ni siku ambayo nilikua mtaani kwetu baada ya kupata likizo fupi,kijana mmoja ambaye nilikuwa nimecheza nae mpira kipindi cha nyuma nikiwa katika shule ya primary alinifuata na kutaka kusalimiana na mimi kitendo cha kunifuata nilitoka katika kiti ambacho nilikuwa nimekaa kijana huyo akuonekana kuwa na wazo lolote kunihusu mimi kwani baada ya kutoka katika kiti hicho alinipa mkono ili niweze kusalimiana nae lakini sikudhubuti hata kidogo kwamaana alionekana mchafu ukilinganisha kwa jinsi nilivyokuwa mimi. 'Denisi mbona uko hivyo siku hizi au kwasababu uko chuo nini'!?. Kijana huyo aliongea huku akiwa anaonekana waziwazi kuwa amechukizwa kitendo hicho,mimi kwenye nafsi yangu ilifurahi sana baada ya kuona kijana huyo aliyeonekana kunishadadia kuona kuwa amechukizwa na hicho kitenda na kweli kijana huyo aliondoka na kuniacha nikiwa naendelea kuchati na wasomi wenzangu. Baada ya muda nilirudi nyumbani kitendo cha kuingia ndani mama alianza kulalamika huku akilaani vitendo vyangu 'Jamani mwanangu huoni haya unashika simu za laki tano na pia unavaa nguo za fasheni huku ukijua wazi maisha tulionayo sisi mimi na babaako tumekusomesha kwa shida ila leo hii unadiriki kutotutumia pesa japo kidogo maana najua wazi ulipata mkopo'!?. Mama aliongea huku akionekana kuchukizwa na hicho kitendo. 'Mama ehee mimi sina hela labda mpaka niajiliwe ndo nitaanza kutoa hela mama,mjini kupendeza mama ama unataka mwanao nivae nguo zilizochakaa'. Nilimjibu mama huku nikiwa nimemtazama usoni kwa kumuhesabu. 'Mwanangu mpaka unafikia hatua ya kunijibu hivyo kwanza unajua wazi nyumba hii inavuja kitendo cha kutuma hela japo kidogo watengeneze bati ni kazi kwako kweli babaako anahaki ya kukukataa kwa tabia zako hizo'!?. Mama aliongea huku akiwa anaonekana kuchukizwa na majibu yangu mimi nikiwa sina ili wala lile niliingia ndani baada ya kuingia ndani nikimkuta Baba akiwa amekaa sebuleni nilisarimu baada ya kumsalimia nilimpita na kwenda chumbani. _MWISHO WA LIKIZO_ Nikiwa najiandaa kwa safari ya kwenda kwenye kituo cha mabasi ili niweze kupanda basi la kwenda Mwanza na hatimae niende moja kwa moja katika chuo ambacho nilikuwa nasomea CHUO CHA SAUTI, na kweli basi nilipata baada ya kufika katika kituo cha mabasi nilipanda basi na hatimae niliweza kufanikiwa kufika katika Chuo hicho,baada ya kufika chuoni niliweza kukutana na marafiki zangu tulipeana ongera nyingi za kufanikiwa kufika chuoni na baada ya kupeana ongera nyingi kila mwanafunzi wa chuo alienda mpaka kwenye Mabweni ambayo yalikuwa karibu na sehemu ya chuo. 'Jamani leo hii kuna nguo fulani na imetoka na ni bonge la nguo hakika ukilivaa lazima mademu wakukubari!?.Alikuwa ni kijana mmoja ambaye alikuwa rafiki angu aliongea huku tukiwa tunasukumizia mizigo kuingia ndani ya chumba hicho na baada ya kusema hivyo alinipa simu ake kweli nguo ilionekana kutoka ilikuwa ni nzuri sana. 'Kijana kwasasa mkopo wa serikali haujatoka hivyo sijui mademu watatukomaje sasa'!?. Nilimjibu huku nikiwa naonekana mwenye shauku ya kuipata hiyo nguo.'Usiwe na shaka kuna kampuni imejitokeza kuwa itakuwa inakopesha wanafunzi wa vyuo vikuu na baada ya kumaliza unarudisha mkopo huo'. Rafiki angu huyo aliongea huku akiwa anatoka kwenye chumba hicho na kunivuta na mimk kunitoa nje sikuweza kujua tunaenda wapi na mara kwa mbele niliweza kuona jengo kubwa rafiki angu aliniingiza kwenye ilo jengo. Baada ya kufika wafanyakazi wa sehemj hiyo walituchangamkia sana na rafikia angu cha ajabu alidai kuwa anataka mkopo wa milioni moja na nusu waliweza kumpatia na mimi kuona hivyo na mimj niliomba mkopo huohuo cha ajabu sheria ya kampuni hiyo aikuwa ngumu sana kwa wanafunzi kwani ulikuwa unawapa namba za simu na namba za akaunti za chuo, kila mtu alitoka na kitita cha hela nyingi tuliingia supermarket na kununua nguo zilizokuwa zimeingia baada ya kununua tulibakiwa na kiasi fulani cha pesa hivyo kila mtu alitoka kwenye supermarket hiyo, Kitendo cha kutok katika supermarket wingu lilitanda kukaonekana kuwa kutakuwa na mvua ya hatari sana na kweli mvua ilianza kunyesha ya hatari sana. Ilitubidi kurudi kwenye supermarket hiyo baada ya kuingia mara simu angu ilianza kuita baada ya kuitazama ilikuwa ni simu kutoka kwa mama nilijua wazi kuwa anataka hela hivyo ikanibidi kuiweka blacklist ili akipiga simu yake isifanikiwa kunifikia. Na kweli baada ya kufanya hivyo sikuweza kusikia tena simu ake na kipindi hicho mvua iliendelea kunyesha ila baada ya masaa mawili ilikatika baada ya kukatika tulitoka katika supermarket hiyo na kuelekea mpaka kwenye chumba ambacho tulikuwa tunalala. Na hatimae niliweza kuitoa namba ya mamangu blacklist cha ajabu baada ya kuitoa nilikuta ujumbe wa kustaajabiaha ambao ulisema hivi'DENISI WAZAZI WAKO ATUNAO TENA DUNIANI'!?. Kitendo cha kuoma ujumbe huo mara akili alibadirika palepale na kuanza kujifikilia jinsi ya vifo vya wazazi wangu vilivyotokea. Nilizitazama hela nilizokuwa nazo baada ya kuzitazama nikitoka katika chumba hicho huku nikimuacha rafikj angu aliyekuwa akipnekana kuchoka nilipanda bajaji mpaka kwenye kituo cha mabasi na kwa bahati nzuri niliweza kukuta basi moja tu lililokuwa likija Bukoba hivyo nililipanda baada ya kulipanda nilikuja nalo mpaka kwenye kituo cha mabasi ya Bukoba baada ya kufika nilikodi pikipiki mpaka nyumbani na kweli nilikuta nyumba yetu imebomoka na baada ya kufika katika sehemu hiyo nilianza kulia na kila mtu alionekana wazi kunisota miili ya mamaangu ilitolewa kwenye nyumba hiyo baada ya maji kupungua katika sehemu hiyo. Nilitoa hela ili watu waweze kuwazika wazazi wangu baada ya kuonekan wazazi wangu kutoa harufu mbaya, nilihuzunika sana na sikuwa na jinsi ya kufanya ila niliyakumbuka maneno ya mama mpaka leo hii nikiwa mtaani huwa nakumbuka maneno yake kwamaana baada ya wazazi wangu sikuwa na nauli ya kurusi chuo na nilichukia chuo hadi leo hii nayaandika haya MSOMI NI ILE YA MTU KUSOMA MANENO YA MTU, na vijana wengi tunapotoshwa sana baada ya kufika chuo na kujiona kuwa wewe ni mtu wa tofauti katika jamii... JIFUNZE; Tabia ambazo unazikuta katika sehemu fulani kama hazina tija jitahidi kuachana nazo tafuta tabia ambazo zina maana ili ziweze kukusaidia maishani mwako na yasije kukutokea mambo yaliyonitokea mimi!!?... Ukipenda story kama hizi karibu kwenye page yangu inayoitwa STORY ZA KUSISIMUA&MIKASA #KARIBUNI_NYOTEEEE#

at 1:09 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top