Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA ISHIRINI.
“Catherine siku uliyoondoka ndani ya begi lako uliacha kitabu chako cha kumbu kumbu, niliweza kusoma matukio yote ambayo uliwahi kukutana nayo hapa shuleni.
Nilijua kwamba ulibakwa na Maloya, nilijua kwamba uhusiki na kifo cha Candy ingawa mwanzo nilikuwa nikikutilia hofu, nilijua jinsi ulivyokuwa na wakati mgumu sana kwa ajili yangu.
Mambo mengi sana hukutaka niyajue lakini kupitia kitabu chako kile niliweza kuyafahamu nilijua hata mpango wako wa kutaka kupoteza mawasiliano na mimi kisa ikiwa ni ule ujauzito.
Vyote hivyo vilikuwepo ndani ya kitabu chako cha kumbukumbu.”
Niliinamisha uso,
“Baada ya muda tulitangaziwa kwamba unatafutwa na polisi, mwalimu alikuwa akipenda sana kutuletea habari zinazohusiana na kesi ya Candy na hadi mwisho nilipata taarifa kwamba umekamatwa Dar na umeletwa huku Mwanza na kufunguliwa kesi, moyoni mwangu niliumia sana niliazimia kukusaidia kwa namna yoyote ile.
Nilifanya mawasiliano na mama yangu mkubwa Happiness ambaye ni mama yake na Martha.”
Moyo ulinipasuka paa, sikuwa najua kitu hiko.
“Niliongea naye nilimwelezea kila kitu nikampatia na kile kitabu chako cha kumbukumbu, aliguswa sana na shida zako na aliamua kukusaidia.”
“Tunashukuru mungu kwamba kila kitu kilienda sawa na Mungu alionekana na hatimaye leo umeachiliwa huru.
Lakini kilichonipa furaha kabisa ni kwamba ujauzito haukuwa ni wa Maloya ulikuwa ni wa kwangu, sorry Candy kwa kukatisha masomo yako.”
“Naomba nikupe kitu ambacho kinawakilisha ombi langu langu la msamaha kwako aliongea kwa uzuni na kwa sauti ya kilio.”
Niliinama tu nilishindwa la kusema.
Niliziba macho yangu na kiganja changu nikibaki nimejiinamia,
“Catherine” aliniita Martin,
“will you marry me?”
Nilitoa kiganja kilichokuwa kimefunika macho yangu
“Say whaaat!!” Alikuwa ameshikilia pete ambayo ilionekana imenakshiwa na madini ilionekana kuwa pete ya thamani sana.
“Yes” aliongea kwa kunong’ona.
Machozi yalinitoka upya, nilimtizama baba yangu alikuwa akilia, shangazi yangu naye pia.
“Yes Martin niko tayari”, nilijibu kwa sauti ya upole.
Alipiga magoti na kunivalisha pete ile kidoleni kwangu ilikuwa ni furaha kubwa kwangu na si kwangu peke yangu bali kwa wote.
“Catherine” wakili Happiness aliniita,
“baada ya dhiki huja faraja” alisema.
“Niwatakie maisha mema ila naitwa Happiness Lutabenza niliolewa miaka kadhaa iliyopita na Denis Lutabenza na kufanikiwa kupata mtoto mmoja tu Martha kabla mume wangu hajafariki. Nampenda sana mwanangu Martin kwa sababu yupo karibu nasi hasa na binti yangu nah ii ni sababu niliamua kukusaidia kwa nguvu zote yani IN THE NAME OF LOVE.” Hapo alicheka.
Nilishituka sana Martin alikuwa akiitwa Martin Lutabenza.
“Martin ni mtoto wa mdogo wa marehemu mume wangu, David Lutabenza.”
Tuliachia tabasamu wote.
Ulikuwa mwanzo wa maisha ya furaha.
Nampenda sana mume wangu Martin maisha yangu yote.
>>>>>>>>>>>>>>>>>> MWISHO<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
Napenda kuwashukuru watu wote ambao mlikuwa pamoja namI tangu mwanzo wa hii hadithi hadi hapa tumefikia mwisho.
Mungu azidi kuwabariki sana natumaini kwamba kuna kitu mmekipata, yani hamkutumia muda wenu bure mmesoma na mmepata kitu.
Lengo kubwa la kuandika hadithi hii ni kwamba kuna vitu nilikuwa nataka mvione.
Watoto wana ndoto nzuri lakini wazazi ndiyo chanzo cha kufeli kwa ndoto za wanafunzi na za watoto wengi.
Inatia huzuni sana,
Tunazaa watoto kwa sababu tunataka kuwa wazazi, lakini mara zote wazazi wengi sana wanakimbia majukumu ya kuwa wazazi.
Watoto wana mahitaji mengi sana.
Ili mtoto aweze kufikia ndoto zake mzazi anahitajika kujitoa kwa hali na mali, ili mtoto huyo aweze kufanikiwa.
Watoto wengi sana wakiharibikiwa mara zote tumekuwa tukiwatupia lawama huku tukiangalia sababu chache tu ambazo zinaonekana lakini tukiacha sisi wenyewe wazazi tunashindwa kujibebesha lawama kwamba sisi ndio tunahusika katika namna zote.
Hata hivyo lawama kubwa nazipeleka kwao wazazi kwasababu wao wanahusika
Watoto wanahitaji muda,
Wanahitaji mtu wa kuwajali,
Wanahitaji mapenzi,
Wanahitaji kuongozwa,
Wanahitaji ulinzi,
Wanahitaji maombi,
Wanahitaji kupata muda wa kupumzisha akili,
Wanahitaji kuchanganyika na watu,
Wanahitaji kusikilizwa,
Wanahitaji uhuru,
Wanahitaji amani na kujifunza.
Watoto wakipata hayo yote ni vigumu sana kwa mtoto kupoteza ndoto zake maana mtoto huyo atakuwa anajitambua kwa sababu tayari ana mahitaji yake yote ya msingi.
Kama wazazi tumekuwa tukifikiria kwamba watoto wanahitaji mavazi, elimu, malazi na chakula basi.
Lakini hayo yote hayatoshi na ndiyo maana ndoto za watoto waliowengi zinaishia njiani.
Watoto wanakuhitaji sana mzazi.
*Mwisho*
RIWAYA: HIGH SCHOOL SEHEMU YA ISHIRINI. “Catherine siku uliyoondoka ndani ya begi lako uliacha kitabu chako cha kumbu kumbu, niliweza kusoma matukio yote ambayo uliwahi kukutana nayo hapa shuleni. Nilijua kwamba ulibakwa na Maloya, nilijua kwamba uhusiki na kifo cha Candy ingawa mwanzo nilikuwa nikikutilia hofu, nilijua jinsi ulivyokuwa na wakati mgumu sana kwa ajili yangu. Mambo mengi sana hukutaka niyajue lakini kupitia kitabu chako kile niliweza kuyafahamu nilijua hata mpango wako wa kutaka kupoteza mawasiliano na mimi kisa ikiwa ni ule ujauzito. Vyote hivyo vilikuwepo ndani ya kitabu chako cha kumbukumbu.” Niliinamisha uso, “Baada ya muda tulitangaziwa kwamba unatafutwa na polisi, mwalimu alikuwa akipenda sana kutuletea habari zinazohusiana na kesi ya Candy na hadi mwisho nilipata taarifa kwamba umekamatwa Dar na umeletwa huku Mwanza na kufunguliwa kesi, moyoni mwangu niliumia sana niliazimia kukusaidia kwa namna yoyote ile. Nilifanya mawasiliano na mama yangu mkubwa Happiness ambaye ni mama yake na Martha.” Moyo ulinipasuka paa, sikuwa najua kitu hiko. “Niliongea naye nilimwelezea kila kitu nikampatia na kile kitabu chako cha kumbukumbu, aliguswa sana na shida zako na aliamua kukusaidia.” “Tunashukuru mungu kwamba kila kitu kilienda sawa na Mungu alionekana na hatimaye leo umeachiliwa huru. Lakini kilichonipa furaha kabisa ni kwamba ujauzito haukuwa ni wa Maloya ulikuwa ni wa kwangu, sorry Candy kwa kukatisha masomo yako.” “Naomba nikupe kitu ambacho kinawakilisha ombi langu langu la msamaha kwako aliongea kwa uzuni na kwa sauti ya kilio.” Niliinama tu nilishindwa la kusema. Niliziba macho yangu na kiganja changu nikibaki nimejiinamia, “Catherine” aliniita Martin, “will you marry me?” Nilitoa kiganja kilichokuwa kimefunika macho yangu “Say whaaat!!” Alikuwa ameshikilia pete ambayo ilionekana imenakshiwa na madini ilionekana kuwa pete ya thamani sana. “Yes” aliongea kwa kunong’ona. Machozi yalinitoka upya, nilimtizama baba yangu alikuwa akilia, shangazi yangu naye pia. “Yes Martin niko tayari”, nilijibu kwa sauti ya upole. Alipiga magoti na kunivalisha pete ile kidoleni kwangu ilikuwa ni furaha kubwa kwangu na si kwangu peke yangu bali kwa wote. “Catherine” wakili Happiness aliniita, “baada ya dhiki huja faraja” alisema. “Niwatakie maisha mema ila naitwa Happiness Lutabenza niliolewa miaka kadhaa iliyopita na Denis Lutabenza na kufanikiwa kupata mtoto mmoja tu Martha kabla mume wangu hajafariki. Nampenda sana mwanangu Martin kwa sababu yupo karibu nasi hasa na binti yangu nah ii ni sababu niliamua kukusaidia kwa nguvu zote yani IN THE NAME OF LOVE.” Hapo alicheka. Nilishituka sana Martin alikuwa akiitwa Martin Lutabenza. “Martin ni mtoto wa mdogo wa marehemu mume wangu, David Lutabenza.” Tuliachia tabasamu wote. Ulikuwa mwanzo wa maisha ya furaha. Nampenda sana mume wangu Martin maisha yangu yote. >>>>>>>>>>>>>>>>>> MWISHO<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<< Napenda kuwashukuru watu wote ambao mlikuwa pamoja namI tangu mwanzo wa hii hadithi hadi hapa tumefikia mwisho. Mungu azidi kuwabariki sana natumaini kwamba kuna kitu mmekipata, yani hamkutumia muda wenu bure mmesoma na mmepata kitu. Lengo kubwa la kuandika hadithi hii ni kwamba kuna vitu nilikuwa nataka mvione. Watoto wana ndoto nzuri lakini wazazi ndiyo chanzo cha kufeli kwa ndoto za wanafunzi na za watoto wengi. Inatia huzuni sana, Tunazaa watoto kwa sababu tunataka kuwa wazazi, lakini mara zote wazazi wengi sana wanakimbia majukumu ya kuwa wazazi. Watoto wana mahitaji mengi sana. Ili mtoto aweze kufikia ndoto zake mzazi anahitajika kujitoa kwa hali na mali, ili mtoto huyo aweze kufanikiwa. Watoto wengi sana wakiharibikiwa mara zote tumekuwa tukiwatupia lawama huku tukiangalia sababu chache tu ambazo zinaonekana lakini tukiacha sisi wenyewe wazazi tunashindwa kujibebesha lawama kwamba sisi ndio tunahusika katika namna zote. Hata hivyo lawama kubwa nazipeleka kwao wazazi kwasababu wao wanahusika Watoto wanahitaji muda, Wanahitaji mtu wa kuwajali, Wanahitaji mapenzi, Wanahitaji kuongozwa, Wanahitaji ulinzi, Wanahitaji maombi, Wanahitaji kupata muda wa kupumzisha akili, Wanahitaji kuchanganyika na watu, Wanahitaji kusikilizwa, Wanahitaji uhuru, Wanahitaji amani na kujifunza. Watoto wakipata hayo yote ni vigumu sana kwa mtoto kupoteza ndoto zake maana mtoto huyo atakuwa anajitambua kwa sababu tayari ana mahitaji yake yote ya msingi. Kama wazazi tumekuwa tukifikiria kwamba watoto wanahitaji mavazi, elimu, malazi na chakula basi. Lakini hayo yote hayatoshi na ndiyo maana ndoto za watoto waliowengi zinaishia njiani. Watoto wanakuhitaji sana mzazi. *Mwisho*
Artikel Terkait
Story - - - - - NI WEWE TU PENINA Sehemu ya pili (2) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp___0769673145 Ilipoishia........ Katika bar moja iliyopo maeneo ya sinza kikao kimoja kilikuwa kikiendelea, na huku kilichokuwa kikipangwa Katika kikao kile ni namna ya kulivunja na kuliharibu penzi la Penina na Frank. Mzee Joel ambaye ni baba yake Penina, pamoja na Angel ambaye ni mdogo wake Penina pamoja na vijana wengine watatu wa kiume na mmoja wa kike, ndio waliokuwa wahusika wakuu wa kikao kile. *********ENDELEA ******** "sitaki mwanangu aolewe na yule mlala hoi kwa namna yoyote Ile naomba muyakatishe mpenzi yao, nitawapa pesa yoyote mnayotaka." alisikika mzee Joel akiwaambia vijana wake. "hamna shinda mzee wetu kuanzia Sasa tupo Katika mipango ya kuliharibu penzi hilo usijali mzee wetu." kijana mmoja aliyeitwa zaza ndio alisikika akiwaambia mzee Joel maneno hayo. "nitafurahi Sana kama hili likifanikiwa siwezi kukubali mwanangu aolewe na yule mnuka jasho." mzee Joel bado alizidi kuongea kwa jazba. "baba hata mimi nakuunga mkono Dada hawezi kuolewa na yule mnuka shombo." aliongea Angel naye kumuunga mkono baba yake. "hamna shida mzee Joel tutafanya mnayotaka." akaongea Zaza. "bas Sawa ngoja niwape pesa ya maji ili muweze kuianza kazi Mara moja." akaongea mzee Joel na kutoa pesa kias cha shilingi laki mbili na kumkabidhi Zaza agawane na wenzake. "Asante Sana mzee wetu na kuanzia Sasa sisi tunaianza Kaz." akaongea Zaza huku akipokea pesa zile, na Kisha wakaagana na mzee Joel na kuondoka.* Katika ukumbi mmoja wa starehe mziki wa taratibu ulikuwa ukipigwa kwa utaratibu wa hali juu kabisa, huku watu wawili wanaopendana kupita maelezo wakiwa ndani ya ukumbi huo huku wakiburudika na mziki mwororo uliokuwa ukipigwa Katika ukumbi ule, watu hao ni Penina pamoja na Frank. "Frank nakupenda Sana mpenzi wangu sijui nifanye nini ili ujue ni kwa kiasi gani, nafahamu jinsi baba yangu anavyokuchukia Ila yeye hawezi kuwa chanzo cha mimi kutokukupenda wewe, hakika nakupenda Sana." aliongea Penina maneno hayo akimuambia Frank na kujilaza kifuani mwake. "nafahamu Penina ni kwa kiasi gani unanipenda na pia unatambua ni kwa kias gani mimi nakupenda, napenda nikuahidi tu kuwa NI WEWE TU PENINA hakuna mwingine zaidi yako." Frank naye alimwambia Penina maneno hayo ambayo yalimfanya Penina azidi kutoa tabasamu tamu usoni mwake na kuzidi kumvuruga Frank, ambaye alijiona ni mwanaume mwenye bahati Sana kuwa na msichana mrembo kama Penina. Kama Kuna zile sifa wanaume huzitafuta kwa wanawake bas Penina alikuwa nazo na zingine za ziada. "yaani mpenzi wangu kila nikikuangalia nakuwa na maswali mengi ya kijinga ya kukuuliza kwa jinsi tu ulivyo mzuri." aliongea Frank akimwambia Penina. "hahahaaaa maswali gani hayo mpenzi wangu hebu niulize moja." akaongea Penina na kumtaka Frank amuulize moja. "swali moja ambalo huwa najiuliza kila ninapokuona huwa najiuliza hivi wewe ulizaliwa na mwanadamu au Mungu ndio alikutengeneza mwenyewe alafu akakuleta duniani?" akauliza Frank huku akiwa anamtazama Penina. "hahahaaaa Frank mpenzi wangu mi nimezaliwa na mwanadamu kama wewe." akajibu Penina huku akicheka kwa maneno ya Frank. "najua wewe umezaliwa na mwanadamu kama mimi Ila wewe ni mrembo Sana Sana sanaaa." akaongea Frank huku akizidi kumsifia Penina. Penina naye alifurahi Sana na kuzidi kuwa na furaha zaidi kwa sifa alizokuwa akipewa na Frank. "Asante Sana mpenzi wangu kwa sifa zote ulizonipa ila Kuna kitu nataka nikuambie." akaongea Penina na kumtizama Frank. "kitu gani tena mpenzi wangu?" akahoji Frank huku akiwa ametumbua macho. "mbona umeshtuka hivyo Sasa?" Penina akamuuliza Frank baada ya kumuona ametumbua macho. "lazima nishtuke si unajua tena namna navyokupenda isije ikawa ni kitu kibaya." Frank akamjibu Penina. "usijali mpenzi sio kitu kibaya na nina Imani utafurahia." Penina akamwambia Frank kumtoa hofu. "ok niambie bas ni kitu gani?" akahoji Frank huku akionekana kuwa na haraka ya kutaka kujua. "nataka siku chache zijazo tufunge ndoa alafu tufanye harusi kubwa ili tuwakomeshe maadui zetu ambao hawataki kutuona tukiwa pamoja.." Penina ndio alimwambia Frank ambaye alikuwa kimya kumsikiliza. "kweli mpenzi wangu hata mimi nimeshaliwaza hilo tatizo lipo kwangu, bila Shaka unatambua hali iliyopo Katika familia yetu, hatuna uwezo kipesa hivyo nahitaji muda zaidi kulitimiza hilo Penina." Frank akamwambia Penina huku akiwa amepoteza tabasamu usoni mwake. "Frank mpenzi wangu ondoa Shaka kuhusu hilo mimi nina uwezo wa kulisimamia hilo mwanzo mpaka mwisho, na kuthibitisha hilo hapa nimekuja na funguo nne, moja ni ya duka kubwa la kuuza bidhaa za jumla na moja, mwingine ni wa gari kubwa la kubebea mizigo, mwingine ni wa nyumba mpya niliyowanunulia wazazi wako kama zawadi ya kunizalia mwanaume anayenipenda kwa dhati na mwingine ni wa gari ndogo nililokununulia wewe mpenzi wangu. " alimaliza Penina kumwambia Frank maneno hayo na kumuacha akiwa mdomo wazi. " waooow ni ngumu Sana kuamini ila acha niamini tu, Asante Sana mpenzi wangu." alisema Frank huku akimkumbatia Penina na kumshushia mabusu mfululizo. "usijali mpenzi wangu ila nataka utambue nayafanya yote haya kwasababu nakupenda Sana, lakini pia ni moja wapo ya maandalizi ya harusi yetu." Penina akamwambia Frank huku akiwa amejilaza kifuani mwake. "nashukuru Sana Penina mpenzi wangu kusikia hivyo na mimi nikuahidi kuwa na wewe mpaka mwisho wa uhai wangu hakika ni wewe tu Penina." Frank akamwambia Penina huku akiwa amemkumbatia kwa nguvu. Wakati huo tayari Muda ulikuwa umeenda Sana na tayari ilikuwa ni saa moja usiku, hivyo Frank na Penina waliondoka kurudi nyumbani huku Penina akimuahidi Frank kumkambidhi vitu vyote alivyomwambia siku inayofuata. Penina alimfikisha Frank nyumbani kwake, Frank akashuka kwenye gari na kumuuga mpenzi wake Penina. Kisha Penina akageuza gari na kuondoka. Baada ya Penina kuondoka tu, Frank kabla hajapiga hata hatua moja kuondoka pale, ghafla alishtukia amezungukwa na vijana watatu wa kiume waliokuwa wamevalia miwani nyeusi kila mmoja. Na hata Frank alipowaangalia hakuweza kuwafahamu. ....... Itaendelea. ... Read More
*LOVE BITE EP 03* ILIPOISHIA………. Mawazo yalirudi tena kwenye ile picha na kuamua kuificha bila kuichoma moto kama alivyotaka mwanzo kufanya. Badala yake alienda sehemu ambayo kulikuwa na hati ya nyumba yake na kuiweka ile picha katikati. Ni kweli Prisza alikuwa anampenda na hawakuwahi kuachana. Ni muingiliano tu wa maisha ndi uliowatenganisha. Moyo wake aliona kama si haki kuichoma ile picha kwakua bado alikua na nafasi ndani ya moyo wake japokuwa kuonana na msichana huyo ni ngumu sana. Hata alipomaliza chuo alijitahidi kumtafuta bila mafanikio. Mpaka muda huu anajitegemea ni kipindi kirefu cha miaka sita tuko walipokutana na Prisca kwa mara ya mwisho. Mawazo ya msichana huyo wa kwanza katika maisha yake yalimchanganya kichwa na hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokea na kuanzisha ukurasa mwengine wa maisha yake kwenye mapenzi na shani Baada ya usafi huo wa kabati lake, aliamua kujilaza kitandani na usingizi ukamchukua. SONGA NAYO………… Siku ya pili yake Jothan alienda kazini kama kawaida. Alifanya kazi zake na baada ya kurudi kazini alimkuta Shani amejaa tele nyumbani kwake. “karibu mume wangu “ alikaribisha Shani na kumfuata Jothan na kumpokea mizigo yake. “ahsante.” Aliongea Jothan na kumkabidhi mizigo yake Shani. “una oga kwanza au unakula ndio uende kuoga?” aliuliza Shani baada ya kurudi pale alipokuwa Jothan. “vyovyote tu mke wangu. Maana nahisi joto na hata njaa pia ninayo.” Aliongea Jothan na kumfanya Shani atabasamu. “kaoge kwanza, maana ukiwa vizuri hata chakula kitashuka barabara.” Alishauri Shani na mawazo yake yakapitishwa moja kwa moja na Jothan. Alipotoka kuoga Jothan, alirudi mezani na kukuta Shani ameshaandaa mapocho pocho ya kila aina yaliyochafua meza. “unajua mke wangu, hata niwe na njaa vipi, kama wewe upo nyumbani basi hudiriki kuitunza hiyo njaa kwa sababu unajua sana kupika mke wangu. Muda mwengine naomba nipate na njaa ya ajabu ili nikifakamie kisawasawa chakula chako.” Aliongea Jothan na Shani akabaki anatabasamu na kumuangalia Jothan kwa mapozi. Mapenzi moto moto kutoka kwa Shani yalizidi kupamba moto. Muda wote Shani alijitahidi kumuweka Jothan kwenye kundi la wanaoyafurahia mapenzi. Jothan alijisikia raha kutokana na Shani kila wakati kutokana na mauzo anayoyapata kuwa na msichana High classic. Walitamani kila saa wawe karibu na kulishana ndio style iliyowavutia watu wengi waliowashuhudia wawili hao walionyesha kupendana sana. Siku moja Jothan akiwa anatoka kazini, ghafla aliona gari likiwa limepaki pembeni na kuna msichana akihangaika kulishughulikia lile gari. Jothan alipaki gari lake pembeni na kushuka kwa ajili ya kutoa msaada. Alipomfika eneo la tukio, yule dada aligeuka kumuangalia Jothan na wote wakajikuta wanapigwa na butwaa. “JOTHAN!!” aliita yule dada kwa sauti kubwa iliyoambata na mshangao mkuu. “PRISCA!!” hata jothan naye alilitaja jina la yule msichana na kumfanya Prisca kujiachia na kupitisha mikono yake mgongoni mwa Jothan kupitia kweye makwapa yake kama ishara ya kumkumbatia. Jothan naye akampokeaa vizuri kwa kuzungusha mikono yake kwenye kiuno namba 6 cha Prisca. Baada ya kusalimiana, wakaona haitoshi. Waliacha gari zao pale pale na kutafuta sehemu tulivu na kukaa kwa ajili ya kupigiana story mbili tatu kutokana na kukumbukana kupita kiasi. “ ahsante mungu kwa kunikutanisha na kipenzi changu jamani,.. jothan milima haikutani ila binaadamu tunakutana. Leo hii kauli hiyo ndio naikubali kwa asilimia zote.” Aliongea yule dada huku akionyesha furaha ya wazi juu ya Jothan ambaye wakati huo alikua na tabasamu la usoni lakini kichwani alikua kwenye msongo wa mawazo. Anampenda Prisca lakini kwa sasa Shani amechukua nafasi kubwa kwenye moyo wake kutokana na kumpa kila anachokihitaji tena kwa wakati. Alikiri kuwa kwa sasa Prisca alizidi uzuri na kumfunika hata Shani. Maana Shani alikuwa ameridhika na kuzidi kuwa mnene kiasi japokuwa sio kigezo cha kupunguza uzuri wake. Ila Prisca alikuwa mwembaba lakini aliyekuwa na figa iliyojichonga kama glasi ya wine. Kwenye kiuno alikuwa mnene na kufaya hipsi zake kuonekana sana. Pia kijungu cha wastani kilichotupiwa huko nyuma ndio kilizidi kumpa maksi zaidi na kumfanya azidi kuonekana special na wanaume wote wanaojua viwango vya wanawake wazuri na wenye mvuto katika muonekano wa macho ya marijali. Kiuno kilichoingia ndani na muinuko wa kibinda ndio kilitengeneza namba 6. kiuno hicho mungu kawapendelea wasichana wachache sana. Hata wachina wameshindwa kutengeneza dawa ya kutengeneza kiuno hicho. Sura ya mviringo iliyokuwa na macho yenye kilevi bila ya kunywa kileo chochote ndio kilikuwa kivutio kingine. Ukiachana na weupe halisi ambao ulikuwa kiasi na kufanana na maji ya kunde, pia vijisima vidogo mashavuni vilivyojitokeza kila akifanya tendo lolote liliousumbua mdomo wake vilimfanya mtu yeyote kutamani kumuangalia usoni. Uso uliombwa na haya mbele ya mwanaume ndio ulikuwa kivutio hasa kwa mvulana mwenye kutafuta mtu wa kuweka ndani na kuoa kabisa. Mambo yote hayo ndiyo aliyokutana nayo Jothan baada ya kukutana na Prisca kwa mara nyingine baada ya muda mrefu. Hata yeye mwenye alikutana na majaribu hayo aliyoyafananisha na majaribu ayapatayo mwanamke mjane baada ya kusikia sauti ya mwanaume tajiri aliyekuja kumfariji na kwa kumuahidi kumuoa na kuwa tayari kuwalea watoto wake. Alijikaza kiume na kujaribu kuyaficha madhaifu yake yaliyomkumba na kujifanya yupo kawaida. “Hata mimi nimefurahi kukuona, za miaka?” aliongea Jothan na kumuangalia Prisca ambaye alikua na furaha wakati wote huo toka wameonana. “vipi, leo maaskari hawaji??” aliuliza Prisca na kucheka. “leo hakuna mwanafunzi hapa..au wewe mwanafunzi?..maana siku ile nilikataa kuwa mimi ni mwanafunzi halafu wewe ukajitambulisha kuwa mwanafunzi.” Aliongea Jothan na kufanya kicheko kitawale kwa sekunde kadhaa kati yao. “tumetoka mbali sana Jothan, leo naona kabisa kuwa mungu katufanya tusahau kipindi chote ambacho hatukua pamoja.” Aliongea Prisca huku akionyesha wazi kuwa bado alikuwa na mawazo ya mapenzi juu ya Jothan. “hata mimi naona kama vile hatukuonana siku mbili kwa jinsi siku ya leo ilivyofukia mashimo ya miaka mingi niliyoishi bila kuiona sura yako.” Aliongea Jothan na kumuangalia Prisca aliyekuwa na kila kitu cha kutalii umuangalipo usoni. “nikuulize swali Jothan?” Aliongea Prisca na kumfanya Jothan kushangaa kidogo baada ya kuombwa ruhusa ya kuulizwa kitu. Alifikiria kwa nukta kadhaa kisha akaruhusu kusikia kitu alichotaka kuuliza Prisca. “umeshaanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwengine zaidi yangu?” Aliuliza Prisca swali hilo huku akiwa kawaida na kuonyesha wazi kuwa lile swali linahitaji majibu sahihi na yenye utashi juu yake. Jothan hakuamini kama swali lile lingekuja mapema kabla hajaliandalia maandalizi yoyote ya kujibu. Ubongo wake ulikimbia kwa kasi kutafuta jibu la kumpa kati ya ukweli au kumuongopea kwakua wakati huo swala la kumuepuka au kumpotezea msichana huyo aliyeonja penzi lake toka hajakuwa sister du kama hivi sasa. Elimu ya msichana huyo na maisha mazuri anayoishi pia vilikuja kwenye ubongo wake na kufanya machaguo kuwa mengi. Yaani kama ni mtihani, basi lile swali lilikuwa katika mfumo wa matiple choice tena lililokuwa na mfumo wa A,B,C,D,E na F.. “sina.” Alijibu Jothan huku moyo wake ukimuuma kumkana Shani. “wooh… ni wazi hii couple Mwenyezimungu amekuwa akiismamia kwa kipindi kirefu. Unajua kuwa hata mimi nilikuwa naamini kuwa kuna siku tutakuja kuonana tena. Ndio maana sikuona uzito wowote kuwakataa wanaume wengi huku nikiwa sijui ni lini tutakutana. Roho ingeniuma sana ungeniambia kuwa kuna mwengine umeshampa moyo wako.” Aliongea Prisca bila kujua kuwa huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe. Maneno hayo yalimfanya Jothan ajione kuwa hakuwa na makosa kumuongopea kwa sababu angemwambia ukweli chochote kingeweza kutokea na kusababisha maongezi ya amani kati yake na Prisca kutoweka. “unataka kuniambia kuwa mpaka hivi sasa hauna mtu mwengine aliyerithi mikoba yangu?” aliuliza Jothan kimitego. “hakuna… yaani toka uliponiacha sijaguswa na mtu mwengine. Yaani hata kama ungekuwa umenifunga luku basi zingesoma unit zile zile ulizoziacha.” Aliongea Prisca na kumfanya Jothan kutabasamu. Waliongea mengi na kila mmoja alifurahia uwepo wa mwenzake pale. Waliachana baada ya kumrekebishia Prisca gari lake na kila mmoja kupata mawasiiliano yote ya mwenzake. Waliachana na ahadi ya kukutana naye tena walikubaliana kuwa watapeana taarifa kwenye simu. Siku hiyo iliwekwa kwenye Diary ya Jothan ambaye alikuwa anatemba nayo kwenye mkoba wake wa kazini. Usingizi ulikuja ukiambata na ndoto iliyojirudia kuanzia mwanzo hadi pale walipoachana. Aliamka asubuhi na kukuta Shani ameshamuandalia maji ya moto kwa kuwa asubuhi hiyo ilikuwa na kiubaridi kidogo. Alipoamka tu aliletewa nguo za bafuni pamoja na mswaki ambao ulisha wekwa dawa kabisa. Alipokuwa bafuni mawazo yaligeuka upande wa pili na kumfanya amuwaze pia Shani kwa jinsi alivyokuwa akitimiza wajibu wote kama mke bora anavyotakiwa kufanya. Kila aliloliwaza kutendewa na msichana basi Shani alikuwa wa kwanza kufanya hata kabla hajaambiwa fanya. Hayo na mengine mengi ndio yalimfunga Jothan na kuyatuliza macho yake kwa wasichana wengine na kumfanya kuwa mtiifu kwa kurudi nyumbani mapema. Na kama anataka kupata moja moto maja baridi basi hutoka na mpenzi wake huyo ambaye alimfanya kuinjoy kwa kuwa sehemu nyigi walizoingia hakukua na mtu mwenye demu mkali kama wake. Alimaliza kuoga huku kichwani hakujua jibu nini kati ya A au B. kuna wakati alitamani kuyaweka kuwa yote ni majibu. Kuna wakati alitamani arushe shilingi ila alishindwa kumjua nani amuweke mwenge na nani amuweke bichwa. Prisca ndio msichana waliyebikiriana kwakua yeye hakuwahi kufanya mapenzi kabla kutokana na ulinzi thabiti wa wazazi wake alipokuwa anasoma. Na Prisca ndiyo yeye aliyekata utepe. Shani ndio mpenzi wake wa ukubwani ambaye anamuonjesha matamu ya ndoa hata kabla hajafikia maamuzi ya kuoa. Hata sasa anaanza kuonekana na kitambi kidogo kwa sababu ya raha azipatazo kwa mpenzi wake huyo. Japokuwa walikuwa wapenzi kwa kipindi kirefu, lakini hawakuwahi kukaa pamoja hata wiki moja kwa sababu kila mmoja alikuwa anaishi na wazazi wake. Ila Shani na yeye wamekuwa wakilala pamoja mara tatu kwa wiki. “itakavyokuwa ndio hivyo hivyo.” Aliongea Jothan baada ya kuona anaisumbua akili yake bila majibu sahihi. Siku waliyo ahidiana kukutana kati ya Jothan na Prisca iliwadia huku kila mmoja akiwa amewasili bila kukosa huku wakiwa wamejitupia vitu vya thamani kila mmoja. Make up na mpangilio wa nguo alizovaa Prisca zilimfanya kuonekana katika muonekano mwengine wa kuvutia zaidi. Jothan hakuamini kuwa ndiye yeye alikuwa analala kwenye kifua cha yule msichana zamani. Pia hakuamini kuwa huyo msichana ndiye aliyekuwa akilipigania penzi lake miaka yote japokuwa walikuwa hawajaonana miaka mingi. Walikutana huku kila mmoja akiwa ameshuka kwenye gari lake na kwenda kwenye hotel moja yenye hadhi hapa Dar. Walipata chakula cha mchana na baadae wakaenda kwenye swimming pool kuogelea. Hamadi !, Macho yalimtoka Jothan baada ya Prisca kuvua nguo zake na kubaki na nguo ya ndani huku juu kukiwa na sidiria ndogo iliyobana maziwa yake na kuyafanya yapande juu na kuonekana sehemu kubwa ya maziwa iliyoteganishwa na msitari mmoja kati kati kuwa wazi. Jothan hakuona ubaya kuvua nguo na yeye na kubaki na boxer na kujumuika naye kwenye swimming pool huku wakiwa peke yao eneo hilo lililokuwa na mabwawa mengi ya kuogelea. Waliogelea na kujikuta michezo yote wanacheza. Kuanzia bembea, mpira wa pete na mwisho wakamaliza na mchezo usio hitaji kocha wala mashabiki japo kuwa unapendwa na watu wengi hapa duniani. Ukiwa mtoto unaambiwa kuwa mchezo huo ni mmbaya lakini ukikuwa bila kufundishwa unajikuta unacheza huku ukijilaumu kwa nini hukuanza kucheza toka mwanzo. Hawakujua walitumia muda gani kwakua taa za ile hotel ziliwaka muda wote na kufanya mtu asitambue wakati kama hajaangalia saa. Mndinyo wa kitanda murua cha hotel hiyo ndio sababu iliyowafanya kudumu muda mrefu huku kila mmoja akiwa ame miss raha za mwenzake. Mechi hiyo ya marudiano ilikuwa kali na kila mmoja alikiri kuwa walihitaji kuwa karibu na kucheza kila mara. Baada ya muda, Jothan aligutuka kuwa hiyo siku ndio siku Shani alikuwa analala kwake. Aliamka fasta na kutupa macho yake kwenye saa ya ukutani “MUNGU WANGU…. SAA SABA USIKU?” Alishtuka kimoyo moyo na kutaja alichokiona kwenye saa. Aliamka ili aenda kuoga kwa ajila ya kwenda nyumbani kwake. “vipi darling, unaenda wapi tena… mwenzio nahitaji kimoja tu cha mwisho.” Alidakwa mkono kimahaba na Prisca aliyekuwa ameyarembua macho yake na kuonyesha ishara zote za kuhitaji kipindi cha pili baada ya mapumziko. “najisikia uchovu ndio maana nilikua nataka kwenda kuoga.” Aliongea Jothan huku akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya Shani kugundua usaliti alioufanya siku ile. “twende wote babie, tukirudi mpango mzima au…” aliongea Prisca na kumfanya Jothan azidi kuchoka. “poa.. twende.” Alikubali kishingo upande na wote wakaenda kuoga na uchokozi alioufaya Prisca huko bafuni ikiwafanya mchezo huo kuanzia huko huko bafuni na kumalizikia kitandani wakiwa hoi na usingizi wa muda wote waliokuwa wakicheza cheza ulikuja na kuwafanya wapate usingizi mnono. Saa nne asubuhi ndio waliachia kitanda na kwenda kuoga. Walipofungua mlango walikutana na wahudumu waliokuwa wakigonga kwa ajili ya kufanya usafi. Walieda kupata supu kutokana na kupotelewa na nguvu nyingi masaa kadhaa yaliyopita. Baada ya hapo. Walijiandaa na kila mmoja akapanda kwenye gari lake huku Prisca akionyesha wazi kuwa aliufurahia uzinduzi wa uhusiano yao uliofanyika kwenye kitanda cha hotel ya SERENA. Jaothan akiwa kwenye gari lake, aliiona simu yake aliyoiacha makusudi kwa ajili usumbufu pindi awapo na Prisca. Alikuta missed call zaidi ya kumi na tano na sms sita zote zikiwa za Shani na zikionyesha kuwa na wasi wasi juu ya usalama wake. Alihuzunika sana kwa kosa alilolifanya japokuwa hakupanga kulala nje. Maisha ya kuendesha mioyo miwili hakuwahi kuishi na tayari kwa siku hiyo aliona adha yake na kutamani kuchuja na kuwa na mmoja tu. Ni nani ambaye angestahili kubaki na ni nani atoke ndio swali lililokosa majibu kwakua wote alikuwa anawakubali kwa wakati wao. Alivyolala na Prisca alikuwa kama alikuwa anamfungua kwa mara ya kwanza hali iliyomfanya aamini kuwa hakutumika muda mrefu. Aliona sio sawa kumuacha msichana huyo mwenye ndoto naye nyigi za maisha yao toka walipokuwa wanasoma. Na Shani hakustahili kutendewa unyama wowote kwakua hata yeye hajawahi kumfanyia unyama wowote zaidi ya kumfariji anapokuwa ana huzuni na daima aliisimamia furaha yake hata ikibidi kuenda kinyume na matakwa ya dini kwa kukubali kuishi nae bila ndoa. Akiangalia kila mmoja alionyesha kumpenda kwa wakati wake na hawakuwa tayari kumuachia. Ila yeye swali la NIMPENDE NANI lilimsumbua kuliko hata DIAMOND. Aliamua kuwasha gari lake na kuelekea nyumbani. “oooh.. ahsante mungu. Umekumbwa na nini kipenzi changu?.” Aliongea Shani baada ya kuupokea mkoba wa Jothan. Hali hiyo ilimshangaza Jothan kwakua hakutegemea mapokezi kama yale. “samahani mke wangu, sikukupa taarifa kuwa ofisini kuliandaliwa warsha na nikaenda kwa kudhani itaisha siku hiyo. Hata hivyo simu yangu niliisahau kwenye gari na kunifanya nisizione missed call zako mapema.” Aljiuma uma Jothan mbele ya Shani ambaye wakati huo ndio kwanza alikuwa anamvua viatu baada ya kukaa kwenye moja ya masofa yaliyokuwa pale sebuleni. “sawa mpenzi wangu. Nimefarijika tu wewe kurudi salama.. maana nilikuwa na wasi wasi juu ya uzima wako tu.” Aliongea Shani na kumuonyesha Jothan jinsi anavyomjali. “samahani sana mpenzi wangu, nitajaribu kukupigia simu kwa kila siku nitakayochelewa kurudi nyumbani.” Aliongea Jothan na kukiri kuwa amefanya makosa makubwa ambayo hata yeye mwenyewe hakuyategemea. Siku hiyo ilipita kwa Jothan kulala muda mrefu kutokana na uchovu wa jana yake. Asubuhi aliamka na kukuta ameandaliwa nguo za kuvaa kwa ajili ya kwenda kazini zikiwa zimepigwa pasi kabisa. Aliwekewa maji ya uvugu vugu kwa ajili ya kuoga kisha kifungua kinywa matata kilikuwa tayari mezani kinamsubiria yeye tu. “ashante mke wangu.” Alishukuru Jothan baada ya kumaliza kunywa chai. “usijali mume wangu, nakutakia safari njema. Take care honey.” Aliongea Shani na kumfungulia mlango wa gari Jothan. Jothan alifika kazini mapema na kufanya kazi zake kama kawaida. Saa nane alitoka kazini na kurudi nyumbani. Alikuta ameandaliwa chakula cha mchana mezani lakini Shani hakuwepo kwakua ilikuwa ni siku ya kwenda kwao. Alijihisi mpweke na alitamani Shani angekuwepo kwake moja kwa moja. Alikata shauri baada ya kula chakula na kuamua kumtafuta mpenzi wake kwenye simu. “hallow” alipokea Shani kwa mapozi. “I miss u babie, unaweza kuja tutoke baadae kidogo tukale mbuzi maeneo ya Facebook pub?” aliongea Jothan. “noo babie, leo nimeenda kwa mama. Sio vizuri kuonyesha tabia mbaya mbele yake ya kurudi usiku. We vumilia babie. Kesho tutakuwa wote.” Aliongea Shani kwa pozi zilizomfanya Jothan kushindwa kukata simu hata kama maneno ya msingi ya kuongea nae yameisha. “basi sawa. Sijui lini utanipeleka kwa mama.” Aliongea Jothan huku anatabasamu. “si wewe mwenyewe tu hujaamua. Ukiamua hata leo nakuleta huku.” Aliongea Shani huku akionyesha wazi kuwa alikua anacheka. “nitakuja tu mine, si unajua mambo mazuri hayahitaji haraka.” Aliongea Jothan na kukata simu. Siku ya pili yake walitoka pamoja na kwenda kula bata maeneo hayo na kurudi mida ya saa tano usiku. Alipokuwa kazini, alisikia simu yake ikiita kwa mlio tofauti. Kabla hata hajasoma jina la mpgaji wa hiyo simu. Tayari alishamtambua kwakua aliihifadhi namba ya mtu huyo kwa mlio tofauti kwa makusudi. “haloo.” Aliipokea ile simu. “haloo babie, I miss u.” sauti nyororo ya kike ilisikika upande wa pili. “I miss u too Prisca, niambie.”aliongea Jothan huku akiangalia wafanya kazi wenzake waliokuwa bize wakifanya shughuli zao. “hata kunitafuta wangu,.. yaani kama uliniroga mwenzako siku ile. Yaani sijielewi mpaka hivi leo.” Aliongea Prisca kwa sauti ya mahaba. Jothan aliangalia na kuona soo kuendelea kuongea maneno yale mbele ya wafanyakazi wenzake. “sema nini babie, nitakupigia nikiwa free. Now nipo kazini halafu nina kazi nyingi.” Aliongea Jothan kwa sauti ya chini. “sawa wangu, baadae.” Aliitkia Prisca na kukata simu. Jothan alifanya kazi zake na kurudi nyumbani kwake. Baada ya kupata chakula cha mchana, alijitupa kitandani na kuchukua simu yake na kumpigia Prisca. “haya lete maneno.” Aliongea Jothan baada ya Prisca kupokea simu. “nina hamu ya kuonana na wewe babie… sihitaji kuwa mbali na wewe hata kwa dakika moja kwa jinsi nillivyozimika mbaya.” Aliongea Prisca kwa sauti iliyomshinda mwana dada wa kipindi cha ala za roho kinachoruka usiku kwenye kituo cha clouds fm. Sauti ilipenya vizuri kwenye masikio ya Jothan na kuhisi labda Prisca alichanganya sauti ya Loveness love (Diva) na wema sepetu. “tupange week end, sababu katikati ya wiki ni majanga.” Aliongea Jothan. “poa, ijumaa si ulisema unatoka mapema. Unaonaje kama tukikutana siku hiyo.” Aliongea Prisca na wazo lake likapitishwa moja kwa moja na Jothan. Siku ya ijumaa ilipofika. Jathan alimpa taarifa Prisca na wakakutana maeneo ya Peacock hotel iliyopo maeneo ya mnazi mmoja. Jothan alifika na kumkuta Prisca alishafika muda mrefu kidogo na tayari alishaagiza kinywaji na alikua anakunywa taratibu. Alipofika, alipokelewa kwa kukumbatiwa na Prisca na kupewa mabusu matatu matakatifu kwenye mashavu yake na moja likiwa sawia mdomoni mwake. Baada ya salamu hiyo adhimu. Walimuita muhudumu aliyekuja haraka na kumpa oda yao. “tuchukue chumba sasa hivi au baadae?” aliuliza Prisca baada ya kumaliza kula. “hapana, leo sijisikii vizuri kabisa na sipo tayari kushiriki tendo lolote Prisca.” Aliongea Jothan na kumfanya Prisca apigwa na butwaa. Maana alijiandaa kabisa kupata mechi nyingine siku hiyo. “kwanini babie….unaumwa???” aliuliza Prisca kwa mshangao. “siumwi, ila mayo wangu unanisuta kila siku nikiongea na wewe kwenye simu au nikikutana na wewe. Najihisi sifanyi fair kwa nikitendacho.” Aliongea Jothan huku sura yake ikionyesha wazi kuwa hakuwa na furaha ingawaje aliingia kwa muonekano wa mtu aliyefurahia uwepo wao pale. “jamani, tatizo ni nini wangu, mbona una nifumba fumbo ambalo sijui nitalifumbua vipi?…naomba uniambie ukweli kuliko kuniweka mwenzako kwenye uzio wa alama ya kuuliza.” Aliongea Prisca huku akionyesha wazi kubadilika kutoka katika hali ya furaha aliyokuwa nayo mwanzo na kuungana na Jothan. “Prisca, hivi bado unanipenda?” aliuliza swali Jothan lililomfanya Prisca apigwe na bumbuwazi kwakua hakulitegemea lile swali. “nakupenda sana tena zaidi ya niwezavyo kuelezea kwa ulimi wangu. Ndio maana nikaweza kukaa kipindi kirefu bila ya kuwa na mtu mwengine japokuwa ni wengi walikuwa wanakuja kunitongoza na bado sikuona umuhimu wa kuanzisha mapenzi mapya kabla mapenzi yako wewe na mimi kufa.” Aliongea Prisca na kumuangalia Jothan aliyekuwa makini kumsikiliza. “hata mimi nakupenda Prisca, ila mimi ni msaliti na sio mwema kwako hata kidogo. Cha kwanza nimekuwa muongo kwa kukuongopea toka siku ya kwanza tulipokutana kwa mara ya pili ukubwani. Cha pili sistahili kuwa wako kwakua tayari nimeshakuharibia mipango na malengo yako kwa kipindi krefu Prisca.” Aliongea Jothan huku akionyesha wazi kuwa alikuwa katia wakati mgumu kufunguka yale yaliyomjaa moyoni. “sikueliwi Jothan.. naomba nidadavulie uyasemayo.” Aliongea Prisca huku akionyesha kuchaganyikiwa. “kwanza naomba unisameha Prisca kwa haya nitakayokuambia. … nilifanya makosa makubwa siku ile kwa kutokuambia ukweli kuwa tayari nina msichana na ninaishi naye. Nampenda sana ingawaje sikuweza kutoka kwenye mitego yako siku ile kwakua wewe ndio wa kwanza kukaa moyoni mwangu na chembe chembe za upendo juu yako ndizo zilizonisukuma mpaka kukuongopea na kukuambia kuwa sina mtu. Siwezi kuweka mafahari wawili kwenya zizi moja. Na kumuacha Shani ni kitu kisichowezekana kwakua ananionyesha mapenzi zaidi ya niliyowahi kufikiria mapenzi kuwa hivyo. Maamuzi yangu ni kwamba. Kuanzia leo sahau kuwa na mimi ni mpenzi wako…. Niwie radhi kwa hili.” Aliongea Jothan huku machozi yakimlenga lenga. Hakika ni uamuzi mgumu aliouchukua kwakua aliamini ilikuwa ni mtihani mkubwa katika mapokezi ya mlengwa. Alipoinua macho yake kumtazama Prisca, tayari mashavu ya prisca yalishalowana kwa machozi huku macho yakiwa mekundu. Kilio cha kwiki kilianza kusikika na kumfanya Jothan kuingiwa na imani baada ya kumtaza mpenzi wake huyo anaye amua kumuacha bila kosa lolote. ITAENDELEA ... Read More
Story....... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na moja (11) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp....... 0769673145 Ilipoishia......... Upande wa Nolan yeye alipanga lazima amfundishe adhabu baba yake kwa namna yoyote ile. "Wewe ni baba yangu ndio sikatai, umenitunza vizuri, umenipa elimu ya kutosha Sawa, lakini kwa unyama huu unaotaka kuufanya hakika sitakuacha lazima nitaenda sambamba na wewe." alijisemea Nolan akiwa chumbani kwake akipanga mipango yake. Lakini pia Nolan aliapa kama asipofanikisha ndoa ya Frank na Penina bas atajiua. *********Endelea ******** Nolan alivunja kibubu chake cha kuhifadhia pesa na kugundua pesa iliyopo huko ni ndogo Sana na haitatosha kutimiza mipango aliyoipanga. Nolan aliamua kuwa mwizi wa ghafla kwa ajili tu ya kutimiza anachokitaka. Lakini hata hivyo hakuenda kuiba sehemu nyingine yoyote, aliamua kumuibia baba yake ikiwa ni njia moja wapo ya kumkomesha baba yake. Nolan alikuwa anajua baba yake ana tabia ya kuhifadhi pesa chumbani kwake. Na baada ya Nolan kugundua kuwa baba yake hayupo haraka akaamua kwenda chumbani kwake na kumuibia pesa kiasi cha shilingi million hamsini. Baada ya zoezi hilo, Nolan alichukua kiasi cha fedha kati ya zile alizomuibia baba yake na Kisha zingine akazificha sehemu ambayo mtu mwingine hawezi kuziona. Kisha Nolan akatoka nje na kuchukua gari Lake na kuondoka nyumbani Muda ule ule. * Mzee Joel alitia nanga Katika kikosi kimoja kilichojulikana kwa Jina la the killer (wauaji) Baada ya kufika mzee Joel alielezea shida Zake zilizompwleka pale na Sasa akitaka Frank pamoja na Nolan wauwawe Mara moja. Mzee Joel alitoa picha ya Nolan pamoja na ya Frank na kumkambidhi mkuu wa kikosi kile cha the killer. "mzee tunahitaji pesa kiasi cha shilingi million thelathini ili kuitimiza kazi yako." akaongea mkuu wa kikosi kile kumwambia mzee Joel. "hakuna tatizo kuhusu pesa nyie fanyeni kazi niliyowapa." akaongea mzee Joel. "Sawa kuanzia Sasa kazi imeanza na tutakuletea majibu Muda si mrefu." mkuu yule wa kikosi cha the killer akamwambia mzee Joel. Mzee Joel aliweza kuondoka huku akiwa na uhakika wa Kaz yake kufanyika kwa ufasaha Sasa. Mkuu wa kikosi kile cha the killer aliwateua vijana wanne kwenda kuanza kazi ya kummaliza Nolan na Kisha wengine wanne akawatuma kwa Frank. * Katika hoteli ile ya kifahari Penina na Frank wakiwa wameketi kitandani wakitizama tv, ghafla bila kutarajia walishtukia kumuona Nolan akigonga mlango. "Eeh kaka mbona umekuja bila taarifa?" akauliza Penina kwa mshangao baada ya kufungua mlango. "lazima nije ghafla na taarifa zangu ziwe za ghafla kwasababu nataka nifanye kitu cha kuwafurahisha, na hivi nimekuja kuwaambia mjiandae tuondoke tayari nimeshawakatia tiketi za kwenda South Africa (Afrika kusini)" akaongea Nolan kumwambia Frank na Penina. Zilikuwa taarifa za ghafla kwa kina Penina na Frank, lakini hata hivyo hawakuwa na namna ilibidi waanze kujiandaa kwa ajili ya safari yao waliyoandaliwa na Nolan. * Vijana wanne waliopewa kazi ya kumuangamiza Frank walichunguza wakachunguza na hatimaye wakafinikiwa kupajua nyumbani kwa kina Frank. Na bila kupoteza muda wakavamia nyumbani kwa kina Frank na kuwaweka chini ya ulinzi Wazazi wake Frank pamoja na mdogo wake Frank. Vijana wale wakawaamuru Wazazi wake Frank waseme sehemu alipo Frank la sivyo watawaangamiza. Wazazi wake Frank kwa kuogopa kuuwawa wakajikuta wakitaja sehemu aliyopo Frank. Vijana wale bila kuchelewa waliachana na Wazazi wake Frank wakaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea sehemu aliyopo Frank ambapo ni Katika hoteli moja ya kifahari. * Frank pamoja na Penina walimaliza kujiandaa na moja kwa moja wakatoka ndani ya chumba kile na kuelekea mpaka nje ya hoteli ile na kuingia kwenye gari la Nolan. Lakini wakati huo huo vijana wale wanne wa the killer walikuwa tayari wameshawasili kwenye gari lile na waliweza kumuona Frank pamoja na Nolan ambao ndio walikuwa wakiwatafuta wawamalize. Mmoja kati ya vijana wale wanne wa the killer alitoa simu yake na kuwapigia wale vijana wengine wanne waliokuwa wakimtafuta Nolan, na kuwaeleza sehemu aliyoonekana Nolan pamoja na Frank. Vijana wale waliokuwa wakimtafuta Nolan nao walianza safari ya kutoka sehemu nyingine waliyokuwa wakimtafuta Nolan na kushika njia ya kuelekea Katika hotel waliyoelekezwa na wenzao. Wakati huo huo Nolan aliliondoa gari pale hotelini na kuanza safari ya kuelekea Katika uwanja wa ndege. Vijana wale wanne wa the killer nao wakawasha gari Lao na kuanza kuwafuatilia ili waweze kujua wanaelekea wapi na kama ikiwezekana wakaulie huko huko. Safari ikiwa inaendelea, ghafla Nolan aliona gari moja nyekundu ikiwa nyuma na kuitilia mashaka kuwa inawafuatilia. Nolan aliamua kufanya kitu ili apate uhakika kama gari lile linawafuatilia au haliwafuatilii. Nolan alipunguza mwendo wa gari Lao ili lile gari jekundu lililokuwa nyuma yao liwapite. Lakini cha kushangaza gari lile halikuwapita nalo pia lilipunguza mwendo na kwenda taratibu pia. Nolan akaamua kuongeza mwendo wa gari Lao ili kuliacha gari lile, lakini pia gari lile liliongeza mwendo na kuwa Sawa Sawa kabisa na gari la kina Nolan. Nolan hapo Sasa ndio akapata jibu kuwa asilimia Mia moja hilo gari jekundu linawafuatilia vibaya mno. "hawa hawanijui ngoja niwaoneshe mimi ni nani." akajisemea Nolan kimoyo moyo na hapo hapo akaongeza mwendo wa gari Lao ili kuliacha gari lile lililokuwa likiwafuatilia. Wakati huo huo kile kikosi cha pili cha the killer kiliwasili pale hotelini na kuwapigia wenzao simu ambao ni wale wanaowafuatilia wakina Nolan, na kuwatarifu kuwa tayari wameshafika. Kikosi kile cha kwanza kikawapa maelekezo ya sehemu walipo wakiwa bado wanawafuatilia wakina Nolan. Kikosi kile cha pili bila kupoteza Muda nacho kikatoka pale hotelini na kuanza kuwafuatilia wakina Nolan pia. Wakati hayo yote yanaendelea Frank na Penina walikuwa wakicheka na kufurahi kwenye gari bila kufahamu chochote kinachoendelea, na hata Nolan hakutaka kuwaambia chochote kwa kutokutaka kuwavuruga Katika safari yao. Nolan bado alizidi kujaribu kulipoteza gari lile lakini bado hakufanikiwa. Nolan alifika kwenye mataa ya kuongozea magari na baada ya Nolan kuvuka tu kwenye mataa yale, zikawaka taa nyekundu kuashiria magari yaliyokuwa yakitoka upande ule wa kina Nolan yasimame kwa dakika kadhaa. Lakini Nolan wao walikuwa tayari wameshavuka lakini vijana wale wa the killer walikuwa bado hawajavuka hivyo ikawabidi wasimame. Nolan aliweza kugundua kuwa gari lililokuwa likiwafuatilia limesimamishwa kwenye mataa. Lakini Nolan akataka kuwafahamu ni wakina walikuwa wanawafuatilia. Nolan alipaki gari pembeni Kisha akawashusha Frank na Penina na kuwapakiza kwenye tax iliyokuwa pembeni yao, na kuwakabidhi kila kitu kilichostahili kwenye safari yao na kuwataka watangulie na kuanza safari yao. Penina na Frank walishangazwa Sana na maamuzi ya Nolan lakini hata hivyo Nolan hakutaka wamuulize swali lolote, alimwamuru dereva wa tax ile awashe gari na kuondoka. Kisha Nolan naye akaingia kwenye gari yake na kugeuza kuwafuata vijana wale wa the killer na wakati huo walikuwa tayari wameshaungana wote kwa maana ya kikosi kile cha kwanza kilichokuwa kikimtafuta Nolan na kile cha pili kilichokuwa kikimtafuta Frank. ............ Itaendelea ... Read More
CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SITA (06) ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO: Siku ya pili, vicent alitoka mapema nyumbani, aliwahi shule kabla hata ya rafiki zake. Hii yote ni kutokana hata usingizi haukupatikana,kutokana na mawazo aliyo nayo. Alikuta baadhi ya wanafunzi wapo darasani, Alifika akakaa kwenye kiti na kufungua begi,kuchukua kitabu na kuanza kusoma. Ila hata sijui nini kilimtuma kutazama mbele maaana alijikuta anatoa macho. ENDELEA....... Alijikuta Anatoa macho, baada ya kuona,marafiki zake nao wamewahi shule. Aiseeee vicent alichekaaaa sana, mpka akajishika tumbo. "hadi nyinyi mmewahi leo aaah kweli mtihani siyo poa".aliongea vicent huku anawatazama kwa zamu. "mimi mwenyewe sijaamini nilivyo kuona ndo maana nikasimama mlangoni nihakikishe ni wewe au hahhhhhah".aliongea Richard huku anaelekea kule alipo vicent.ila cha kushangaza suma akuchangia neno zaidi ya kuachia tabasamu na kutembea kwenda walipokuwa wenzake. "aiseeee kama tuliambizana yani"aliongea tena vicent. Hapo suma ndo na yeye akanyanyua,mdomo wake na kuongea. " hivi unajua kwanini nimeshindwa kuongea chochote?,nikwasababu naona uchuro hapo nje nimekutana na rich, hapa nakuona wewe, nikawa najiuliza hivi hawa waliambizana nini mimi wamenichunia ila nimewabamba".aliongea suma,huvu anavuta kiti anakaa. "hii ili iweje sasa imetokea tu"alijibu richard. "sisi hatuwezi kukufanyia hivyo kwasababu sote ni wamoja". Alisema vicent, suma hakuwa na neno. " oyaa tusomeni basi kabla muda wa kwenda mstalini aujafika"aliongea tena vicent. "poa mwanangu umeongea point" alijibu suma.basi kikapita kimyaa,kila mtu alifanya yakeee kwa muda huo. ******* Mwezi ulipita,hatimae miezi, na si vicent, wala niram aliye kumbuka kama walishawahi kuonana. Basi ilikuwa weekend, moja walionekana marafiki, watatu wakiwa wamesimama stendi ya mabasi,si wengine bali ni vicent, richard na suma wakiwa wamevalia nguo za nyumbani.ilibaki kama wiki mbili wafanye mtihani. Ilionyesha kuwa walikuwa wamelewa kwenye maongezi sasa sijui vicent, walikuwa wanasubiri usafiri maana vicent hakuwa na gari siku hiyo. Mara gaflaa walishtushwa na sauti, nyororo iliotokea,barabarani. "vicentiiiiiiiiiiiii" ilikuwa sauti ya niramu, aliekuwa ndani ya range nyekundu, huku akiwa amependa,kupindukia wanasemaga kadamshi, ile mbayaaaa. Wote macho yalikuwa mbele,ila hakuna mtu alieshtuka kama vicent, maana akutegemea kuonana na binti yule ana muwaza siku zote. Na ilikuwa muda Awajaonana. Kiukweli vicent, moyo ulikuwa unampenda mbio vibaya.ila alijikaza, huku nyuma suma pamoja na richard, aisee!! Macho yaliwatoka maana walishindwa kuelewa, wanae muona machoni mwao, ni jini au malaika. Vicent alijikongoja mpaka kwenye dirisha la gari, na kumsababishia niram. " mambo niram siamini kama ni wewe, kumbe unani nakumbuka? ".alijikuta anaongea mfululizo vicent huku akiuliza, swali humohumo. "poa vicent, nakukumbuka sana vp leo huna usafiri? Maana naona kama mpo wenyewe mnasubiri usafiri? ".aliuliza niram,huku macho akiwaelekezea wakina rich. "aaah ndiyo tunamsubiri dereva tax mmoja hivi,katuambia hayupo mbali".alijibu vicent huko akiangalia huku na kule kama anaetafuta kitu. "haah kwani mnaelekea wapili niwape lifti?maana mimi naelekea mbezi"aliuliza niram. Vicent akapiga mahesabu ya haraka,alafu akaongea. "aaah! Wale wanarudi nyuma ila mimi naenda kunduchi" alijibu vicent. Ila wadau ngoja niwaambie kitu, vicent ameongopa, kwasababu wenzie wanaenda kawe sawa yeye anaenda kunduchi, ila njia ni ileile wameachwa wakina suma, yeye angeendelea mbele, ila aliamua kusema vile ili aweze, kutupa ndoano Kiulaini. Tuendelee, basi niram akamwambia "basi twende nikupe lifti waage wenzio".vicent akachomoka na kuwafata, wenzie alimkuta suma anashauku si mchezo. " vipi yule ndo yule demu uliesema? Na anaelekea wapi ili atupe lift basi kama vipi" alijikuta anaongea maneno,mfululizo na swali juu. "hamna aendi huko kaniambia nimsindikize kariakoo".aliongea vicent huku anageuka nyuma, akagongana macho na niram,wote wakatabasamu. "duuuh mwana kwahiyo umetuacha? ".aliongea richard huku anakazia macho kwenye gari. "aaah aina jinsi ila chukueni hii mpande tax".alisema vicent huku anazamisha mkono mfukoni na kutoa noti tatu za elfu kumi akamkabidhi suma. Suma alizichukua na kuzitia mfukoni. "oyaaa Usikose kutupigia ukifika home"alisema rich. Na suma akadakia. "ndiyo utupe data zote maana duuuh! Mpaka nakuonea wivu".vicent hakutia neno aliishia kutabasamu huku Anaendelea kutembea, basi aliingia ndani ya gari, huku ukimya mwingi ulitawala.vicent akaona avunje ukimya, "basi nilijua utanisahau kabisa".aliongea Vicent Huku ametoa tabasamu hafifu usoni mwake, Huku macho yanatazama mbele. "Ooooh!!Hapana siwezi kukusahau,mtu muhimu Kama wewe Kwa ule Msaada wako ".aliongea Niram,huku anamwangalia Vicent, macho yakakutana, wote wakatabasamu, Niram akageuka mbele na kuendelea, kuushika usukani akizidi kukanyaga mafuta. "hahhhhah!! Ni kweli niram lakini Siyo wote wanao kumbuka fadhila".aliongea Vicent ,Huku kimoyomoyo akiomba wasifike haraka. "haaahhh sawa bwana Wala ujaongopa, ".aliongea niram,huku akizidi kuuchapa mwendo, na bahati nzuri hakukuwa na foleni. "niram nikuombe kitu Kama hutojali? ".aliuliza Vicent Huku amemgeukia kabisa, aliongea Kwa sauti nzito, tens yakubembeleza. "usijali Kama kipo Ndani ya uwezo wangu ntakupa".alijibu niram. Vicent hakaona asizubae Sana, akasema alilokusudia."nilikuwa naomba unisaidie namba yako ya simu ili niwe nawasiliana nawe hata kukujulia Hali,maana tushakuwa marafiki".aliongea Vicent,kwa umakini wa hali ya juu ili asije kukosea step,akamkwaza Niram. " Ooooh!! Wala usijali Kwa hilo".alisema niram, huku anamtajia namba zake. Vicent aliziandika kwenye simu yake. " asante sana".alishukuru vicent. "asante nawe kwa kushukuru".alijibu niram, mara ikawa kama vituo viwili vicent ashuke. "sasa niram mie nashuka hapo kituo kinachofuata utaniacha hapo" aliongea vicent, lakini kama ungemuona moyoni mwake, alichukia kupita kiasi, alitamani wazunguke mpaka alfajiri. Duuuuh kweli mapenzi siyo poa wadau. "haaah ni hapo oky sawa"alijibu niram, na alipofika, akakanyaga break, na kusimamamisha gari. "oooh!!asante sana umenifaa mungu akufikishe salama".aliongea vicent huku anafungua mlango wa gari na kushuka. "haya asante ufike salama pia".alijibu niram, akawasha gari na kuishia, vicent alibaki anampungia mkono, mpaka alipo ishia. Kiukweli ile siku aliiona ya bahati sana kwake, hakika alikuwa na furaha mno. Alifika kwao. Akagonga geti likafunguliwa, alikuta mlinzi akamsalimu, na kuingia ndani hakumkuta yeyote ndani zaidi ya house girl. Alimsalimia akajitupa kitandaniii , pwaaaaaaah!! Aliangalia sana juu vicent, hakika kuwa na namba ya niram,kwake ilikuwa ni furaha tupu. ********* Vanessa alikuwa mezani wakipata chakula cha usiku, maana leo ilikuwa weekend kwahiyooo alikuwa mwenyewe jikoni, ila leo mawazo yalipungua kwani mawasiliano yalikuwa kama zamani na hadi asubuhi ya siku hiyo, vicent alimuaga kuwa atatoka na wakina richard. Mara ghafla alishtukia, akizibwa macho. "mmmh juliana nini bwana,ebu acha mzaha njoo ule"aliongea vanessa. " mmmh dada kwahiyo wewe mtu wako wa karibu ni Vanessa tu? ".aliuliza kwa manung'uniko Clara. Mdogo wake wa nne akitoka huyo ndo juliana, kumbuka wakiume ni wawili kwenye familia yao na ndio wakwanza na wapili. "hamna mamy wote nawapenda ila nilijua yeye, kaa chini ule mdogo wangu".aliongea Vanessa kwa sauti ya kubembeleza,huku akimvuta akae. Basi mambo yakaisha,walikula kwa furaha, wazazi na kaka zao hawakuwepo, walibaki wenyewe. ********* Niram alikuwa chumbani kwake akijisomea, wakati huo alikuwa ameshakula, alikuwa kitandani miguu kuegemeza ukutani, muda wote alikuwa mtu mwenye tabasamu usoni, kilicho mfurahisha akijulikani Mara ghafla simu ikaanza kuita...... Itaendelea CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SABA (07) ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: Niram alikuwa chumbani kwake akijisomea, wakati huo alikuwa ameshakula, alikuwa kitandani miguu kuegemeza ukutani, muda wote alikuwa mtu mwenye tabasamu usoni, kilicho mfurahisha akijulikani Mara ghafla simu ikaanza kuita. endelea........ Mara gafla akaona simu inaanza kuita. Niram akaangalia mpigaji, akaona namba ngeni. " mmh! Atakuwa Nani huyu?".alijiuliza niram, alitafakari Sana maana sikawaida kupigiwa na namba ngeni, baada ya kutafakari kwa muda.akaamua kupokea. "hellow".aliitika niram. "hallow Niram huko poa?, Vicent hapa". Ilisikika sauti upande wa pili."oooh! Vicent nashukuru mungu niko poa sijui wewe ulifika salama? ".alijibu niram nakupachika swali. "nilifika salama niram hofu ilikuwa kwako".alisema vicent. "namimi nashukuru mungu nimefika salama".alijibu niram kwa sauti nyororo kabisa. ****** Vanessa alikuwa ndani kwake akaona mbona muda unaenda sana,na ajaona msg wala simu kupigwa kutoka kwa vicent. Alikaa akasubiri na kusubiri weeeeh lakini ikawa kimya. "mmmh!! Ina maana itakuwa ajarudi bado huko alipoenda"alijisemea mwenyewe, akaona muda unaenda lakini simu aipigwi. "mmh ngoja nipige"aliamua apige yeye, akachukua simu yake na kuipiga. Jibu alilokutana nalo ni NAMBA UNAYOPIGA INATUMIKA KWA SASA.. "mmmh saa tano hii au ndo amerudi hivyo anaongea na wenzie kuwa julisha kuwa amerudi?".alijiuliza jibu akakubaliana kuwa anawasiliana na rafiki zake. ****** Huku vicent akiwa anaongea, akaona kama kuna mlio wa simu nyengine kuingia akaiangalia , alipoona mpigaji kuwa ni Vanessa akaendelea kuongea. Simu iliita mpka ikakata. Waliongea mengi na baadae niram akaaga kuwa anahitaji kupumzika. Basi waliagana na simu ikakatwa. Baada ya hapo alipiga simu kwa Vanessa,huku Akiwa ameshaupanga uongo wa kumwambia. "hellow baby mbona kimya, na napiga unatumika?".aliongea vanessa mara baada ya kupokea simu. "aaah amna nilikuwa naongea na mzee maana mchana,hakuwa na nafasi ndo kunitafuta sasahivi".alijibu vicent kwa ujasiri wa hali ya juu,bila kubabaisha maneno. "oooh kumbe haya niambie mizunguko ilikuwaje? ".Aliuliza Vanessa huku alibadili mikao ya kila aina Hapo kitandani. "ilikuwa poa sema nimechoka sana".alijibu vicent huku akijifanya anapiga mihayo. "oooh basi pumnzika baba angu tutaongea kesho".aliongea Vanessa kwasauti fulani hivi ya madeko. "sawa mama ntakuchek kesho ulale salama"alimaliza kuongea vicent akakata simu. Alienda moja kwa moja bafuni akaoga, maana choo kilikuwa ndani kwake humohumo. Alipomaliza alitoka sebleni muda ulikuwa umeenea sana ila alikuwa bado ajala, alikuta msichana ameshaenda kulala,aliwasha taa ya sebuleni akachukua sahani jikoni nakuenda kula chakula. Mara ghafla akasikia mlango unafunguliwa alikuwa mama yake, "yani wewe Bwana mi nilivyorudi nikaambiwa upo ndani nikajua ushakula".aliongea mama yake vicent,huku anavuta kiti pale sehemu ya kulia chakula akakaa. "hapana mama uwezi amini yani nilipitiwa na usingizi nikalala ndo nimeshtuka sasa hivi".aliongopa vicent, aisee huyu jamaa hatari."ooooh pole baba ni uchovu tu huo"aliongea kwa huruma mama yake. "asante mama".alijibu vicent huku anafakamia wali kwa maini. Basi waliongea mengi mama mtu alinyanyuka, na kuenda kulala. "ukimaliza usisahau kuzima taa baba".aliongea mama yake. "sawa mama ntaizima".vicent alikula akashushia juisi, akaelekea kwenye swichi akazima taa na kuenda kulala. ******* Pilikapilika zilikuwa zinaendelea, katika nyumba ya kina niram.ilikuwa Jumapili kulikuwa na ugeni mkubwa kwao, kuna ndugu zao walikuja.basi yalipikwa masontojoo siyo ya kawaida. Zilisagwa juisi za matunda basi ilikuwa tafrani. Niram akutulia alikuwa bize vibaya. "niram ebu kuongezeae chumvi kwenye biriani kule".ilikuwa sauti ya mama yake. "sawa mama".alijibu huku anaacha alichokuwa anafanya na kwenda kuweka chumvi kwenye chakula. Kila kitu kilikuwa sawa sasa niram alikuwa chumbani anajiandaa akaoge. ******** Suma alipoona ajapigiwa jana, akaona isiwe kesi ngoja amchek yeye maana umbea ulikuwa unamuwasha mtoto wa kiume huyu. Akukubali kitu kimpite hivihivi,yani alikuwa tofauti na richard mwenzie hakuwa mpenda kufuatilia yasiyo muhusu. Basi aliweka vocha akampigia "oyaaa mwanangu unayumba"haliongea suma ."hamna nilichoka sana yani uwezi amini ".alijibu vicent. "eeeh ilikuwaje jana na yule mtoto mzuri?".aliongea suma huku akitegesha masikio vizuri kupata udaku "hahhhhah suma eeh nna kazi kama unataka kuhusu hiyo stori ntakupigia baadae " "ok poa basi usisahau ".alijibu suma huku anakata simu. Ila suma akakumbuka kitu ayaaaaaah!! Daaah!!.Nimesahau kumuuliza Kitu, yeye na haraka zake mpaka nimesahau".aliongea suma huku anamlaumu vicent,kwa uamuzi wa kukata simu haraka. "anyway nitamchek baadae".aliongea suma, mara kisimu chake kikaanza kuita."duuuh huyu somoe ana mpya gani nae mi leo nnampango wa kuonana na hadijaa".alijiseme suma kimoyomoyo ,huku anaangalia ile simu bila kuipokea. Labda niwafafanulie vijitabia vya huyu ismail au kwa ufupi ndo unaweza kumuita suma. Yani suma yupo tofauti na wenzake, suma kwanza ni mwingi wa habari,anapenda kujua mambo ya watu ni mwongeaji mno kuliko wenzake.ajatulia hata kidogo isimpitie sketi mbele yake lazima amfate tu, ila richard na vicent wapo tofauti sana na yeye, richard ana mahusiano na binti mmoja anasoma, shule tofauti na yao. Na ni huyohuyo tu ndo yupo nae. Lakini suma weeeeeeh!! Mwiko mkubwa tena uchuro, kutulia na mwanamke mmoja. Basi baada ya simu kukata akaizima na kuendelea na mambo mengine. ******* Ilikuwa ni mida ya jioni. Wageni wameshaondoka, nyumbani kwa kina niram. Na mama yake kama unavyomjua mtu wa pilikapilika usiseme, alikuwa ameshaenda kuzurura muda mrefu. Aaaaah ahhh!!,sijui muhindi gani huyu mwenye tabia za Kiswahili.ok tuachane nae tuendelee. Basi niram alikuwa amekaa sebuleni peke yake, maana mdada wa kazi hupendelea kukaa ndani kwake kama kazi ameshazimaliza. Basi alijikuta mpweke sana na alijikuta anatamani, kuongea na vicent,ili apate kampani na kupoteza muda kidogo. Hata sijui ni kwanini alimuwaza vicent kuwa ndio mtu pekee wa kumtoa upweke. Hata mimi sijui,ila tutajua hivi karibuni. Basi aliingalia simu kwa muda nakujifikiria ampigie au atulie asimpigie. Basi nafsi ya niram ikawa inashindana,moja inamwambia piga nyengine, inamwambia usipige ila akiwa katika mgongano wa kutoa maamuzi nini afanye, gafla akaona kitu moyo ukapiga paaaaah!!! .alishindwa kuamini alichokiita. Itaendelea.... ... Read More
*MWAGIA HUMO HUMO EP 02* Sehemu Ya Pili (2) Lakini pamoja na yote sikuwa na sifa ya kumteka mwanaume kimapenzi zaidi ya kunionja na kuniacha. Wasiwasi wangu huenda mwili wangu hauna asali itakayo mfanya mwanaume yoyote atakaye nionja anirudie mara mbili. Basi baada ya kupokea aligeuka na kuondoka kurudi ofisini kwangu. Nilipofika mlangoni nilikumbuka kitu nilitaka kumuuliza bosi, niligeuka ili nimuulize kitu. Niligeuka ghafla na kukutanisha macho na bosi ambaye kumbe nyuma yangu alikuwa akinifuatia. Maskini kaka wa watu alishtuka mpaka akadondoka chini, nilijikuta namuonea huruma. Nilirudi hadi chini alipokuwa amekaa bila kuonesha kujinyanyua, mwili wake haukuwa mkubwa sana nilimshika mkono ili kumnyanyua. “Hapana Manka nitanyanyuka mwenyewe.” “Hapana bosi naomba unipe mkono,” nilimwambia kwa sauti ya huruma yenye kubembeleza. Alinipa mkono na kumnyanyua, baada ya kunyanyuka nilitoa kitambaa changu na kumfuta sehemu yenye vumbi. “Tosha Manka sehemu zingine nitafuta mimi.” “Hapana bosi ni wajibu wangu kufanya hili.” Aliniacha nimfute kisha nilimtengenezea kiti na kumuomba akae. “Unaweza kukaa.” Bila kuongeza neno alikaa kwenye kiti chake huku uso wake ukionesha aibu imemtawala. “Pole bosi,” nilimwambia kwa sauti ya chini. “Asante.” “Hukuumia?” “Nipo sawa.” “Pole sana.” “Asante Manka, nipo sawa kaendelee na kazi.” Niligeuka na kuondoka hata nilichotaka kumuuliza nilikiacha na kupanga kumuuliza kupitia simu yangu ya mezani. Nilitoka hadi ofisini kwangu kuendelea na kazi, kabla ya kuanza kazi nilijikuta nikijiuliza kilichomdondosha bosi wangu ni nini. Wasiwasi ulikuwa uleule bosi kapagawa na mimi, kitu ambacho sikutaka kinitokee kwa muda ule kwani ilikuwa mapema sana. Niliamini kabisa bosi kwa mtazamo wa nje alikuwa amepata bonge la mwanamke, lakini ndani sikuwa na sifa zile za kukaa na mwanaume kwa muda mrefu. Niliyapuuza na kuendelea na kazi, nilikumbuka kuna kazi nilitaka kupata maelekezo kwa bosi. Nilimnyanyua simu kumpigia baada ya kuita kwa muda ilipokelewa. “Haloo bosi.” “Ooh..Aah…Nani Manka,” maskini bosi wangu alionesha kiwewe bado hakijamtoka. “Bosi mbona hivyo?” “Aah, kawaida tu, unasemaje?” “Ok, bosi nilikuwa nauliza hii kazi ya malipo kuna maandishi ya mkono nayo niyaandike?” “Hakuna tatizo, yaandike kama ilivyoandikwa.” Nilikata simu na kuendelea ka kazi yangu kama kawaida, baada ya muda nikiwa bize simu ya mezani iliita, nilinyanyua na kupokea. “Haloo bosi.” “Ndiyo Manka jiandae tukapate lunch.” “Nashukuru bosi.” Baada ya kukata simu, niliangalia saa kubwa ya ukutani iliyokuwa mbele yangu, ilionesha ni saa saba kasoro kumi mchana. Nilimalizia kazi yangu ili nipate muda wa kwenda kula, nikiwa bado nimeinama nikirekebisha tatizo la kisarufi nilishtuliwa na sauti ya bosi. “Manka tunaweza kwenda.” “Hakuna tatizo bosi, namalizia kurekebisha sarufi.” “Utamalizia tukirudi.” Nilisave kisha nilizima computer na kunyanyuka, nilijitengeneza vizuri nguo niliyovaa. Kwa chati nilimuona bosi wangu koo likimcheza kama mtu mwenye kiu kikali. Baada ya kuhakikisha nipo sawa tulitoka hadi kwenye gari lake kisha tulikwenda kwenye moja ya hoteli ya kifahari ambayo ilinikumbusha mbali enzi nipo kwenye ndoa yangu. Tulipofika Mateja alionesha kutojiamini sana kwangu kitu ambacho sikuamini mwanaume kama yeye kuwa katika hali ile. Sikuwa na sifa kubwa zaidi ya mwanamke aliyepoteza matumaini ya kupata hadhi mbele ya mwanaume. Niliamini kaniona kwa nje hanijui ndani nilivyo ndio maana ananipapatikia. Nilijua akikipata anachokitafuta kwangu pengine ndiyo siku ya kunifukuza kazi, lakini sikuwa na jinsi kila mwanaume mwenye pesa aliamini mwanamke sahihi wa kukaa naye ni mimi. Baada ya kuketi kwenye viti vyetu muhudumu alifika na kutaka oda zetu. “Manka agiza chochote ukitakacho kwa bei yoyote.” “Asante, nataka kula unachokipenda wewe,” utanishangaa kwa nini nimesema vile, nilifanya vile ili kumtoa wasiwasi na kumfanya awe huru kwangu japo si katika suala la mapenzi. “Hapana Manka nataka wewe leo ndio uchague chakula tutakacho kula.” “Sawa,” nilichagua chakula ambacho wote tulikuwa. Baada ya chakula wakati wa kunywa vinywaji Shaka aliniuliza. “Samahani.” “Bila samahani.” “Manka, umeolewa?” “Sijaolewa.” “Una mchumba sina?” “Sina.” “Rafiki wa kiume?” “Sina.” “Manka mbona unanidanganya.” “Kweli bosi.” “Hivi Manka kwa umbile alilokujali muumba usiwe na mwanaume?” “Si kwamba sijawahi mwanaume ila kwa sasa sina.” “Kweli?” “Kweli kwa nini nikufiche ili iwe nini?” “Mara nyingi watu wamekuwa si wakweli.” “Huo ndio ukweli wangu.” “Kwa nini mrembo kama wewe huna rafiki wa kiume?” “Sina bahati nimeamua kuishi peke yangu.” “Ina maana hata ombi langu litagonga ukuta?” “Ombi gani?” “Kwa vile huna mtu nilifikili unafaa kuwa mke wangu.” “Aaah, bosi,” kauli ile ilinishtua sikupenda kuisikia masikioni mwangu. Sikuwa na jibu la moja kwa moja, moyo mapigo ya moyo walinienda mbio na machozi yalinitoka. Mateja alishtuka kuniona nikitoka machozi badala kumpa jibu lake. “Manka vipi?” “Hataa,” nilitikisa kichwa. “Mbona machozi yanakutoka.” “Kauli yako imenishtua.” “Kivipi?” “Sikutegemea kuniambia neno hilo mapema kiasi hiki.” “Manka, penzi limuingiapo mtu huwa kama kichaa aliyekatikiwa na mishipa ya fahamu. Niyasemayo si mimi ni moyo wangu naomba unihurumie.” “Ni kweli, lakini sina bahati kila siku mapenzi limekuwa likinitesa.” “Kivipi?” “Mpaka leo sijajua sababu ya kuachwa na wanaume.” “Ni wazi wote waliopita walikuwa na tamaa ya kukujua ulivyo na si mapenzi ya dhati. Lakini nakuamini mimi ndiye mwanaume sahihi kwako.” “Hiyo kauli kwangu nimeizoea, lakini mwisho wa siku mambo huwa kinyume.” “Niamini Manka, nitakuwa mume mwema.” “Mmh nitashukuru, lakini usinitende utaniumiza.” “Siwezi.” Baada ya chakula tulirudi ofisini, hatukufanya sana kazi Mateja alikuwa na uchu wa fisi. Aliniomba tufunge ofisi twende tukastarehe, sikuwa na pingamizi nilifunga kazi na kuongozana naye kwenye gari lake. Mateja alinipeleka kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano. Kwa vile shida yake niliijua sikushtuka kumsikia akiuliza chumba cha VIP, baada ya kulipia tulikwenda kwenye chumba kilichokuwa ghorofa la pili. Chumba kilichokuwa cha kifahari, ambacho kilikuwa kipo katika hadhi ya juu. Katika maisha yangu sikuwahi kuingia kwenye chumba kizuri kama kile. Chumba nilikiona kilikuwa kinapendeza lakini wasiwasi wangu bosi wangu atakipata alichokifikilia kukipata mwilini mwangu. Sikutaka nami kijiweka nyuma kwani nilikumbuka kauli za Bi Shuu mama mlezi wangu shangingi mstaafu, kuwa niwapo mbele ya mwanaume nijionesha nipo tayari kumpa kile anachokitaka. Siku zote aliniambia nijiamini ili kumfanya mwanaume naye ajiliuze mara mbili mbili ataniingiaje. Sikupoteza wakati baada ya kuingia tu chumbani nilivua nguo zote na kubakia kama kuku aliyenyonyolewa. Sikuchelewa kumsaula na yeye tukawa sale sale maua. Nilitembea kama miss kuelekea kwenye kabati kuchukua taulo kwa makusudi nimuoneshe umbile langu ambalo mwanzo huwa utata kwa wanaume. Lakini wakiisha nipata nakuwa kama Big G iliyotafunwa na kuisha utamu mwisho wake hutemwa. Kwa kweli sikupenda kutongozwa siku moja na siku hiyo hiyo kumvulia mwanaume nguo ya ndani. Niliamini kabisa kujilahisi vile lazima thamani yangu ingepungua lakini kama ningemzungusha, kidogo thamani yangu kwake ingepanda. Nilijua lazima ataniona maharage ya Msanga maji nusu kijiko. Lakini sikuwa na jinsi kutokana na njia aliyotumia kwa kweli nilijikuta siwezi kuuruka mtego wake mwepesi. Sikuwa ndege mjanja lakini nilinaswa kijinga sana, japo sikujua tatizo langu lakini nilipokuwa natembea na kumuachia umbile la nyuma lililokuwa linawatesa wanaume wengi. Niliinama makusudi kama najikuna mguu ili tu nizidi kumpagawisha. Kitu kilichofanya Mateja azidi kuwa katika wakati mgumu, wakati nafungua kabati nitoe taulo Mateja alikuwa tayari yupo nyuma yangu na kunikumbatia kwa nyuma. Nilijua uzalendo ulikuwa umemshinda, mambo yalianzia pale. Tulianza kubadilishana mate palepale kwenye kabati, baada ya muda aliona anachelewa, mwanaume alinibeba juujuu mpaka kitandani. Kwa vile mchicha ulikuwa umeishakolea nazi tuliumwaga juu ya ubwabwa na kuanza kujimegea tataribu. Mateja alionekana ana pupa kama mamba mwenye njaa, hakuchelewa kukifikisha chombo ukingoni mwa bahari. Baada ya mapumziko mafupi tulirudi ndani ya ngarawa kuendelea na safari, katika vitu ambavyo katika maisha yangu nilikuwa sivipendi ni usumbufu ndani safari. Ooh geuka hivi, lala hivi, inama hivi, nyanyuka hivi, kwa upande wangu niliona usumbufu lakini nilivumilia kwa vile ndiyo ilikuwa siku yetu ya kwanza kukutana. Kama ningekuwa nimemzoea ningempasha, kwani hakuna starehe ya mapenzi mpaka kusumbuana kumgeuza mwenzako kituko,ile kwangu sikuona mapenzi zaidi ya adhabu. Siku zote niliamini baada ya safari ndefu mtu humwaga mzigo na kutelemka. Siku ile tulikaa kaa mpaka saa tatu usiku baada ya kuoga na kula alinirudisha nyumbani. Kabla ya kuondoka Mateja aliniahidi vitu vingi ikiwemo kunijengea nyumba kuninunulia gari na kuyabadili maisha yangu kwa ujumla. Siku ile moja tu alinipatia laki tano taslimu, sikuamini niliona miujiza kupata raha na kiasi kikubwa cha pesa kama kile. Nilipofika nyumbani nilimkuta Bi Shuu yupo chumbani kwake, Nilifungua mlango wa chumba changu na kuingia ndani. Nilipowasha taa nilishtuka kumuona Bi Shuu kanisimamia nyuma, akuzungumza chochote ila alinikata jicho kali. “Shikamoo Bi Shuu” “Hainisaidii kitu” “Mbona hivyo mama yangu” “Kazi gani ya kutoka saa moja asubuhi kurudi saa tano za usiku?” Mmh, makubwa nimekuwa mtoto mdogo wa kuwa chini yake kwa kila kitu. Nilijua uchawi wa Bi Shuu ni nini, niliinama na kuchukua mkoba wangu na kufungua. Nilihesa nyekundu tano na kumpa. “Za nini?” “Katumie tu” “Za kodi?” “Walaa, nimekutunuku tu mama yangu.” “Kweli!?” “Kweli unafili uliyonifikiza madogo” Bi Shuu alifurahi na kunikumbatia na kusahau aliyobwatuka muda mfupi, baada ya kunipandisha na kunishusha alisema. “Weee mwana kulikoni” “Kaa chini nikupashe kazi imekuwa kaziiiii” “Usiniambie” “Habari ndiyo hiyo shilingi moja kwa sekunde ndio mpango” “Wacha wee leo Mchaka kawa mzaramu” “Umenifundisha wewe, ngoja nikaoge nikupashe upashike” Nilimuacha Bi Shuu chumbani kwangu akizirudia kuzihesabu pesa nilizompa mimi nikaenda kujimwagia maji. Nilipotoka kuoga nilimkuta akinisubiri kwa hamu kubwa. “mmhu, hebu nipe raha” “Bi shuu nitakueleza yote kesho” “Mwana wee siwezi kulala mpaka unipe siri ya rangi nyekundi kupendeza na kusikitisha” Huku nikijifuta maji nilimueleza yote bila kumficha hata moja, mwisho wa yote nilielezea masikitiko yangu ya bahati ya kupendwa na mkosi wa kuachwa. “Bi Shuu, japo nimepata lakini wasiwasi wangu sichelewi kumwagwa” “Kwani una tatizo gani?” “hata silijui hakuna hata mwanaume mmoja aliyenieleza tatizo langu” “Mmh, kuna umuhimu wa kulifanyia kazi” “Siamini kama tatizo langu litaisha” “Hebu kila ukiwa na huyu bwana msikilie na muulize an apenda nini chochote usimnyime” “mmh, Bi Shuu wanaume wengine waharibifu ukimchekea anakuharibu” “Sio unavyo fikiria’ “Kuna nini wanaume wanacho taka zaidi ya kuwaharibu wanawake, sijazaa babu wee cha kuwekewa matambala” “Sina maana hiyo si wote wana penda mchezo huo.” “mmh, nitamsikiliza” “Sasa mwana wee lala nakuomba muheshimu mpenzio kama Mungu wako huoni muda si mrefu nasi tutatembelea gari” “Ndicho ninachokiomba, sijui yatakuwa yale yale.” “Basi mwali lala usingizi unono.” “Nawe pia Bi shuu” Bi Shuu aliniaga na kuondoka na kuniacha nikimalizia kujifuta maji ili nilale. ****** Siku ya pili wakati namalizia kujipodoa kabla ya kwenda kujifusha udi kwa Bi Shuu simu ya Mateja iliingia, niliipokea na kuzungumza naye. “Haloo ma’ Sweet.” “Ooh, ma honey girl.” “Ni mimi, mhu baba nipe habari naona simu za asubuhi asubuhi?” “Aah, kawaida ila kuna dereva nimemtuma atakupitia muda si mrefu.” “Hakuna tatizo Sweet.” Baada ya Mateja kukata simu, kwa vile nilikuwa tayari nimeisha jipodoa nilikwenda chumbani kwa Bi Shuu. Kabla ya kuingia nilikutana na moto uliokuwa ukinukia vizuri, harufu ya asubuhi ile ilikuwa zaidi na ya jana yake Niliingia na kumkuta akiweka udi kwenye kitezo, aliponiona alitabasamu na kusema. “Haya mwali jifushe uwahi kazini.” Niliinama na kufunikwa shuka ili moshi wote wa harufu nzuri uishie kwenye nguo na mwilini, baada ya muda alifunua shuka na kuninusa kama mbwa anayesaka chakula jaani. Asikuambie mtu Bi Shuu havumi lakini yumo, mtu mzima lakini ovyooo. “Umevaa kufuri gani?” Bi Shuu aliniuliza swali ambalo sikufikiria kuniuliza. “Nyeupe.” “Hebu nione.” Mmh, makubwa nilinyanyua gauni na kuiona nilikuwa nimevaa kufuli la mikanda ‘Bikini’. “Mwali ndio nini?” Bi Shuu alishtuka. “Mbona umeshangaa?” “Unakwenda kwenye starehe au kazini?” “Kazini.” “Sasa mbona umevaa kufuri kama unakwenda kwenye kilimo cha mihogo.” “Babu weee kwenda na wakati.” “Acha ushamba vaa kufuri la kawaida, hilo kufuri unalivaa siku unayokutana na mpenzi ukitoa nguo tu akiona anaingia kimuhemuhe.” Mmh, sikutaka kubishana naye nilirudi hadi chumbani kubadili kufuri, wakati namaliza kuvaa honi ya gari ilipigwa nje nilijua mtu aliyetumwa kunifuata amefika. Nilikimbilia chumbani kwa Bi Shuu kumuaga. “Bi Shuu naondoka.” “Umebadili kufuri?” “Ndiyo.” “Hebu nione.” Nilinyanyua tena gauni na kunitazama, nilikuwa nimevaa ya kawaida tena ya rangi nyekundu, alipoiona alisema. “Ewaaa, sasa hapo ndipo nilipopataka.” “Basi nawahi kuna mtu ananisubiri hapo nje katumwa na mzee,” nilisema huku nikiteremsha gauni ili niwahi nje. “Wee Manka ndio nini?” “Vipi tena Bi Shuu mwenzio nachelewa kazini.” “Hebu jifushe na hiyo kufuri linukie.” Nilirudi haraka na kuchutama kwenye kitezo kwa kulitanua gauni langu moshi wote uingie chini. Baada ya kufanya yote niliyoelekezwa na Bi Shuu nilimuaga kwa kumbusu kisha nilipitia mkoba wangu na kutoka nje. Nilimkuta gari likinisubiri, niliingia kwenye gari na gari liliondoka. “Mambo?” “Poa, sijui yako?” “Hata mimi ipo poa.” Safari iliendelea hadi ofisini, nilipofika nilipita moja kwa moja hadi ofisini kwa Mateja, alivyokuwa ameisha ingia ofisini. Baada ya kufungua mlango wa ofisi niliingia huku nikiachia tabasamu pana na kutanua mikono yangu, Mateja aliponiona alizunguka meza yake kunipokea. Tulikutana katikati na kukumbatiana. Tuliporomosheana mabusu moto moto huku tukigandisha midomo kwa muda na kubadilisha mate. “Mmh, tosha,” nilisema huku nikijitoa mikononi kwa Mateja. “Mhu, za nyumbani?” “Mmh, mzuri sijui kwako?” “Kwangu ilikuwa ngumu kidogo kutokana na kuwa na wakati mgumu baada ya kukuota tupo pamoja niliposhutuka nilijikuta nipo peke yangu.” “Pole sana, basi ndio ufanye haraka kunichukua.” “Kwa mateso ya jana kuna umuhimu wa kufanya hivyo.” “Basi mengine baada ya kazi.” “Haya mama, mimi niseme nini.” Nilimbusu tena na kurudi kuendelea na kazi yangu, baada ya kukaa kwenye kiti nilijikuta nikikumbuka jinsi bosi wangu Mateja alivyochanganyikiwa na mimi. Nilimbusu tena na kurudi kuendelea na kazi yangu, baada ya kukaa kwenye kiti nilijikuta nikikumbuka jinsi bosi wangu Mateja alivyochanganyikiwa na mimi. Pamoja na furaha ile bado wasiwasi wangu ulikuwa nini hatima yangu kwake, nitaendelea naye au ndiyo atanitosa kama waliotangulia. Wazo la awali lilikuwa kuomba msaada kwa Bi Shuu ili niweze kumdhiniti. Niliendelea na kazi zangu kama kawaida, muda wa mchana tulikwenda kula pamoja kama wapenzi wasiojificha. Siku ile baada ya kurudi nyumbani aliniomba tuwe wote usiku wa siku ile, sikumkatalia kwa vile ndiye aliyekuwa mmiliki wa mwili wangu. Usiku alinipitia na kuondoka kwenda kulala naye mpaka asubuhi, kaonja kaona tamu sasa anataka kula kabisa. … Ni kweli nilifurahi kulala na Mateja mpaka asubuhi kuonesha jinsi gani alivyopagawa kwangu, lakini usiku kwangu ulikuwa wa karaha sana yaani mambo nisiyoyapenda ya kusumbuana wakati wa mapenzi yalijirudia tena. Nilishindwa kumkatalia kwa vile alikuwa bosi wangu kwa kuogopa kufukuzwa kazi na maisha ya kutangatanga yalinichosha. Usiku mzima kugeuzwa kama chapati ooh geuka hivi, lala hivi fanya hivyo, basi kero mtindo mmoja. Nilijiuliza bila kunisumbua vile hawezi kukidhi haja zake, mpaka kunakucha nilikuwa nimekasirika mtoto wa kike kila kona ya mwili iliniuma hayakuwa mazoezi bali adhabu ya mapenzi. Asubuhi Mateja alifurahi sana na kuniahidi kabla ya yote kukibadili chumba changu kwa kuninunulia sofa za nguvu, alinipa pesa nyingi za kutumia na kunirudisha nyumbani. Huwezi amini nilipofika nyumbani nilimkuta Bi Shuu akinisubiri, kutokana na uchovu nilimsalimia na kuingia ndani nijilaze. Kabla sijabadili nguo na kuvaa kanga nyepesi Bi Shuu aliingia. “Mankaaaaa,” aliniita kimbea. “Unasemaje Bi Shuu,” nilimuuliza huku nikimuangalia jicho zito la usingizi. “Mmh, sikuwezi.” “Kwa nini Bi Shuu?” “Mambo yako mazito.” “Mmh kawaida tu, vipi ushakunywa chai?” “Nilikuwa nakusubiri wewe.” “Mimi kwa sasa hivi siwezi nimechoka sana.” “Eeeeh Manka weee, mlikuwa mnakomoana.” “Wee Acha tu,” niliona kama ananichelewesha kulala kutokana na umbea wake wa utu mzima. Nilivuta pochi na kutoa noti kadhaa za kumi kumi na kumpatia Bi Shuu bila kuzihesabu. “Za nini?” “Za kwako.” Bi Shuu alichanganyikiwa na kunivamia kwa furaha na kujitahidi kunibeba japo uzito wangu ulikuwa mkubwa. Kweli pesa sabuni ya roho Bi Shuu alipagawa na kuniona kama malaika niliyetumwa kuja kumpa furaha ya asubuhi ile. “Bi Shuu niache nipumzike.” “Mwali weee lala, tena utakutana nimekuandalia chakula kizuuuri.” Bi Shuu alitoka na kuniacha nikimalizia kuondoa nguo mwili kisha kuchukua kanga nyepesi kisha kujitupa kitandani. Nililala kwa muda wa saa zaidi ya nane kutokana na uchovu wa mbilinge za Mateja usiku kucha. Majira ya jioni Mateja alifanya kweli kwa kuleta sofa za nguvu kitu kilichofanya Bi Shuu kunipa chumba kikubwa cha nyumba kubwa. Niliamini ule ulikuwa mwaka wangu wa mimi kurudi katika maisha ya kutanua. Niliamini muda si mfupi lazima niwe na gari langu mwenyewe. Baada ya kukipamba chumba changu na kupendeza Bi Shuu aliniweka chini na kunipa somo. “Manka Mungu akupe nini, ukishikwa shikamana mwali wee.” “Hata mimi najua Bi Shuu.” “Unaonekana mwanzo ulikuwa ukifanya makusudi mbona sasa hivi mwanaume kapagawa muda si mrefu utakuwa dunia ya wenye nazo.” “Ndio maana yake.” “Basi Manka nitakuongezea vikorombwezo akigusa amenata.” “Usiniambie!” “Kwanini wazee wenzangu pamoja na umri wangu wakionja wanapagawa itakuwa wewe ukioga maji yanatelemka.” “Tena kweli ufanye haraka maana ameisha tangaza ndoa.” “Basi hiyo kazi niachie.” Mateja alinipigia simu kuwa siku ile angekuja kulala ili jumatatu twende kazini pamoja nami sikumkatalia. Kweli usiku alikuja kulala kwenye chumba changu kilichokuwa na hadhi kubwa kwa mtu yoyote. Kama kawaida ya usiku wa jana yake yalijirudi ya kusumbuliwa lala hivi geuka hivi fanya hivi, basi taabu mtindo mmoja. Na siku ile nilivumilia lakini moyoni nilijisemea siku nyingine nitampasha kweli wake hawezi kunigeuza kama mwanasesele na kunichezea apendavyo. Nikajikuta siyachukia mapenzi na kuyaona kwangu ni karaha na si starehe, mwanaume alikuwa akipanda juu ya mnazi hashuki mpaka nahisi kichefuchefu. Niliamini kabisa alitaka kunikomoa kwa vitu alivyonipa, kwangu sikuona mapenzi zaidi ya mateso. Uvumilivu uliponishinda nilianza kuwa mkali kwa kumgomea kwa usumbufu wake kwa kumueleza makavu kuwa sitaki kama hawezi kifo cha mende tuache. Mateja alinielewa na kustarehe bila usumbufu, nilishangaa kumbe anaweza kukwea mnazi bila kujifunga kamba za miguu. Kilichonishangaza ndani ya mapenzi yetu yaliyochukua miezi minne, Baadhi ya mambo yalianza kutoonesha dalili zozote za kutimiza ahadi yake. Siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo uhusiano na Mateja ulivyozidi kulega, hata kuwa pamoja baada ya kazi ikafutika kila muda alionekana yupo bize. Kitendo cha kutokuwa karibu na Mateja kilimshtua sana Bi Shuu kwani hata vizawadi navyo vilikatika. Siku moja aliniweka chini na kuniuliza. “Manka kulikoni?’ ”Hata mimi sijui.” “Manka kila siku hujui wakati unaharibu.” “Bi Shuu unanilaumu bure.” “Hivi kama na huyu atakuacha unafikiri utampata nani?” “Bi Shuu nimejitahidi kwa kila ulilonifundisha nililifanya lakini matokeo yake ndio hayo lazima kuna mkono wa mtu.” “Manka kuna kitu gani alichokipenda Mateja hukumpa?” “Mmh, kila kitu nimempa.” “Kweli?” “Kweli kabisa, nikudanganye ili iweje.” “Sasa itakuwa nini?” “Hata mimi sijui, huu utakuwa ni mkosi tu” “Basi naomba kesho ukienda kazini niitie Mateja.” “Mmh, sijui kama atakuja, lakini nitafikisha ujumbe.” Siku ya jumatatu nilikwenda kazini kama kawaida huku nikifikilia jinsi ya kufikisha wito kwa Mateja wa kuitwa Bi shuu. Hakuwa Mateja niliyekuwa namfahamu. Ilionesha mapenzi yalikwisha kabisa. Kila alipoingia ofisini alinisalimia lakini hakuna kilichoendelea. Nilipomuuliza alinijibu kwa kifupi “Nipo bize,” nilijikuta nikiiona kazi ngumu kama si Bi Shuu ningeacha kazi kutokana na kujiona sina thamani tena kwa Mateja. Siku moja roho iliniuma sana baada ya msichana mmoja kuingia ofisini kwa Mateja bila kumuulizia kwangu kama ilivyokuwa kwa wateja wengine. Niliacha kazi zangu na kumfuata ndani, nilipoingia ofisini mbona lilinishuka mtoto wa kike. Niliwakuta wamekumbatiana na Mateja huku midomo yao ikiwa imegandiana. Nilitamani ardhi ipasuke inimeze, nilisimama kama sanamu nisijue cha kufanya, machozi yalinitoka bila kizuizi, pamoja na kuniona hawakushtuka ndio kwanza walizidisha kutomasana kimahaba. Niliona wazi kabisa penzi langu na Mateja limefika ukingoni. Nilirudi ofisini kwangu na kukaa chini kazi ilikuwa chungu nilijikuta nikilia peke yangu, nilitamani kuondoka niiache kazi. Lakini niliyakumbuka maneno ya Bi Shuu kuwa siku zote penzi tamu ni lile lisilo sukumwa ninalosukumwa lina kasoro. Nikiwa nimeinama nafuta machozi nilishtushwa na sauti ya Mateja. “Manka.” Bila kuitika nilinyanyua uso kumuangalia huku kitambaa kikiwa karibu na macho kufuta machozi. Mateja alikuwa amesimama mbele ya meza yangu akiwa ameshikana kimahaba mmoja alimshika mwenzake mkono shingoni na mwanaume kiunoni. “Vipi mbona unalia?” Mateja aliniuliza kwa kunikujeli, sikumjibu niliendelea kufuta machozi. “Manka huyu ndiye mke wangu mtalajiwa.” Sikumjibu niliinama chini na kulia kilio cha kwikwi ambacho Mateja na mpenzi wake hawakukijali. Niliwasikia wakiondoka, niliwasindikiza kwa macho mpaka walipotoweka, baada ya kutoweka machoni mwangu nilijikuta nikijiuliza nalia nini kwani tukio lile halikuwa la kwanza upande wangu kutendewa. Ni kweli lazima moyo uniume kutokana na ahadi nzuri za Mateja ambazo nilijua zitanibadilisha katika maisha yangu. Ndoto yangu ya mchana ya kumiliki gari na nyumba iliyeyuka kama bonge la mafuta katika kikaango cha moto. Baada ya muda Mateja alirudi na kunipita kuingia ofisini kwake bila kunisemesha jambo lolote. Nilikumbuka wito niliopewa na Bi Shuu wa kwenda kuzungumza naye juu ya matatizo yangu, kila nilipotaka kumwambia moyo ulisita na kuamua kuipotezea tu. Muda wa kutoka nilijikuta nikijikaza kike na kumueleza. “Samahani bosi.” “Bila samahani,” Mateja alinijibu kistaarabu. “Bi Shuu alikuwa anakuita.” “Bi shuu naye ana shida gani tena?” “Hata sijui.” “Mmh, yule bibi na umri wake yuko vile wakati wa usichana wake alikuwaje?” “Mmh, sijui.” “Basi mwambie nitamtembelea wikiendi.” Jamani kauli ya Mateja ilinipa matumaini labda atarudisha moyo wake, siku zote nilimuamini Bi Shuu kwa maneno yake matamu yaliyojaa misemo nahau na methani ili kumlainisha mtu. “Jamani bosi kwa nini usiende leo?” “Manka nipo bize sana atanisamehe, lakini mwambie sijamdharau nitaitikia wito wake.” ITAENDELEA ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: