Home → ushauri
→ Mimba kuharibika na Sababu zake

Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu waawake wengi wamekuwa wakaiharibikiwa na mimba bila kujua sababu.
Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba.
1.Mama anapokuwa na matatizo uvimbe (fibroid), huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara.
2. Uzito mkubwa (unene)
Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda.
3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara
Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika.
4. Utoaji mimba
Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi tisa, hivyo epuka kutoa mimba.
5. Matumizi ya Pombe,Sigara
Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya k?kumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo.
6. Magonjwa sugu
Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia.
Mimba kuharibika na Sababu zake  Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu waawake wengi wamekuwa wakaiharibikiwa na mimba bila kujua sababu. Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba. 1.Mama anapokuwa na matatizo uvimbe (fibroid), huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara. 2. Uzito mkubwa (unene) Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda. 3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika. 4. Utoaji mimba Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi tisa, hivyo epuka kutoa mimba. 5. Matumizi ya Pombe,Sigara Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya k?kumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo. 6. Magonjwa sugu Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia.
Artikel Terkait
ULISHAWAHI KUKUTANA NA MTU MWENYE UPENDO WA KWELI??? Ipo siku utakutana na mtu tofauti na ulivyozoea kuona au kusikia. Haitakuwa kwa sababu ya tabasamu lao au ucheshi wao au kwa jinsi ya kuongea kwao au kusema majina yao. Ni kwa sababu ya njia itakayo kufanya wewe ujisikie tofauti. hutaogopa kupenda na kupendwa. Siku moja utakutana na Upendo utakaoufurahia. Hutaweza kufikiria mara mbili. Hutaweza kuwa na wasiwasi kwamba anakupenda au hakupendi. ‘Utafahamu tu. Kwa mtu huyu hutaweza kuficha tabia yako. hutaficha madhaifu yako na usumbufu wako. hutakuwa na mawazo ya itakuwaje kama ata kupandia kichwani. hutakuwa na maswali ya kujua muhimu wake na hutakuwa na labda. Wakati ukikutana na mtu huyu hutaingiwa na woga. hutaweza kufikiri fikiri kitu chochote. hutaweza kufikiria upendo wake kwako. Na wakati anaposema hawezi kwenda mahali , utafahamu kuwa ni kweli. Wakati huo hutasikia kukosa kitu ndani ya moyo wako, hutasikia upweke, hutaweza kusikia chochote kinyume na upendo uliopo. Ipo siku , mtu fulani atabadilisha maisha yako. kwa sababu atakuonyesha upendo wa kweli ni upi na maana ya upendo ni nini, unaonekanaje. Atakuonyesha kuwa upendo hauna mwisho. na hutamkimbia , na hutaweza kutaka faida zaidi. hutapigwa na wala kupata maumivu yasio na msingi. Ipo siku Hutaogopa kupata maumivu. Hutaogopa kuacha tena. kwa kupoteza kipande cha moyo wako na roho yako. hutaogopa tena kutoa na kutoa upendo wako . Siku moja utapumua kwa urahisi kwa kufahamu kuwa huyo mtu hataondoka . Utapumua vizuri kwa kujua kwamba upendo huo utadumu. Huyo mtu hatakutelekeza na wala hataweza kukukimbia. Utafahamu toka moyoni mwako kwamba upendo huo hautakuumiza. Utaweza kuishi, kucheka, kulia na kupumua kwa urahisi ukiwa pembeni ya mtu huyo. Utajifahamu na kujiona vizuri. Utaweza kumuonyesha makovu, na vidonda ulivyonavyo na kwa kuwa vimepona. Utaweza kumuonyesha mtu huyo moyo wako wote kwa kujua kuwa hawezi kukuacha. Ipo siku utajikuta unaamka mikononi mwake, ukiwa karibu yake kwa upendo , katika maisha yako. hutakuwa na wasiwasi . hutaogopa. hutasikia uzito wa kupumua tena. Utahisi upendo ndani yako. mwisho utagundua Upendo halisi. Washirikishe wengi. ... Read More
AINA 10 ZA WANAUME AMBAO WANAWAKE HUJUTIA WAKIWA NAO  1. Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband). HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea. 2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake. 3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband). Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke. 4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband). Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida. 5. Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband). Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao. 6. Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband). Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena. 7. Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband). Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa. 8. Mume Mtalii (Visiting Husband). Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto. 9. Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke. 10. Mwanaume Mbahili (Miserly Husband). Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake. ... Read More
HESABU YA KUONGEZA Niwapo hisabatini, Hufikiri akilini, Kuongeza umakini, Jawabu kulibaini. Jawabu hilo halani, Hukaa makinikoni, Linafaa maishani, Hapa hapa duniani. Ingawa jana nyumbani, Siku niliyobaini, Hata leo furahani, Nakuweka pongezini. Kijana huyu nyikani, Akiwa hisabatini, Kanuniye mkononi, Kaifikiri kichwani. Ndipo nilipobaini, Kafika hisabatini, Kasogea nyongezani, Hapa hapa duniani. Kafika hisabatini, Kashikilia kanuni, Kuingia umrini, Kakaa makinikoni. Hesabuye kabaini, Kamjalia Manani, Kaingia furahani, Yamfaa maishani. Nyongezaye umrini, Hapa hapa duniani, Ufurahi maishani, Singie ubazazini. Sivutwe hisabatini, Duara kulibaini, Ukaidai kanuni, Ukokotozi pupani. Sivutwe hisabatini, Maumbo kuyabaini, Kuchora karatasini, Ukafika ushenzini. Hari yako maishani, Tuliza kichwa nyumbani, Makinika ubwabwani, Ukishibishe tumboni. Busara zako kichwani, Ziongeze kwa makini, Ufike makinikoni, Utulie furahani. Nyongezayo umrini, Ikufae maishani, Hapa hapa duniani, Sichenge msikitini. Wasalamu tamkoni, Nalitoa mdomoni, Ukae mshawashani, Vilevile moralini. Sijiweke haramuni, Kulazimisha kanuni, Iliyo hisabatini, Ukae makinikoni. Na kwa kheri tamkoni, Naitoa mdomoni, Naenda zangu nyumbani, Nikae pumzikoni. UJUMBE Shamsa Cyprian ... Read More
Hivi unazijua Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda Kwa Dhati??  Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu! ... Read More
Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi. MSOME SAIKOLOJIA YAKE Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira. MRUHUSU AKUJIBU Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. EPUKA MARUMBANO Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano. MUOMBE MSAMAHA Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.” Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: