MAPENZI YA FACEBOOK-06 Sikutaka kukurupuka katika kufanya maamuzi, niliamua kuvuta subira huku nikiendelea kumchunguza mke wangu. Nilikuwa katika mpango mgumu sana, naweza kusema ni katika mpango uliyoshiriki katika kuushambulia moyo wangu kwa mikuki iliyonipa maumivu makali sana. Kuna kipindi nilijitahidi kuyavumilia lakini nilishindwa nilitaka kumwambia lakini pia nilisita kufanya hivyo. Nikabaki naugulia maumivu ya ndani kwa ndani. Moyo wangu ulikuwa ukiuma mithili ya maumivu ya moto wa pasi. Ama kwa hakika usikubali udhaifu wako kila mtu akaufahamu kwani utaweza kujikaribisha katika wakati wa maumivu kila siku, utakuwa ni mtu wa kukosa furaha. Hili ndilo lilikuwa kosa langu kubwa ambalo nililifanya kwa mke wangu. Aliufahamu udhaifu wangu, udhaifu ambao aliutumia katika kuuvunja moyo wangu wa mapenzi. Tukio lile la kushuhudia komenti za wanaume ambao alikuwa akiwajibu pamoja na picha zake za nusu uchi zilizidi kuniumiza sana, kila wakati tukio hilo lilikuwa likinijia katika akili yangu, nilijitahidi kusahau lakini sikuweza kabisa badala ya kusahau ndiyo kwanza nilikuwa nikiziona zile komenti za wale wanaume waliyokuwa wakimsifia, sifa ambazo nyingine sikuwahi hata kumsifia. Nilizama katika dimbwi la mawazo, nilikuwa nikiifikiria ndoa yangu, nilikuwa nikimfikiria Ester wangu. Kuna kipindi nilihisi ndoa ilikuwa ikienda kunishinda kabisa nikawaza kumuacha lakini nilipoyafikiria maswali ya ndugu na marafiki watakayoniuliza juu ya ndoa yetu kuvunjika huku sababu ikiwa ni Facebook niliacha kuwaza hivyo, nilihisi kumpenda sana mke wangu. “Kuna nini?” aliniuliza mke wangu wakati huo alikuwa bize akiperuzi simu yake. “Hakuna kitu,” nilijibu huku nikijitahidi kuigiza tabasamu, hakika iliniwia vigumu sana. “Mbona sasa huendi kazini?” “Sijisikii vizuri.” “Unaumwa?” “Hapana sipo sawa tu!” “Mmh! Mwenzetu vipi au umeshagombana huko maana,” aliniambia huku akiangua kicheko kikubwa sana. “Unacheka nini?” nilimuuliza. “Amna nimeona kituko huku Facebook,” alinijibu huku akionekana kuitazama kwa umakini wa hali ya juu simu yake. Nilizidi kujisikia vibaya sana hasa baada ya kumuona mke wangu akizidi kuwa bize na simu yake. Nilijiuliza ni nini kilichokuwa kinamuweka muda mrefu huko Facebook kiasi kwamba akawa anasahau majukumu yake mengine. Sikuweza kupata jibu kabisa. Nilichokuwa nimepanga kwa wakati huo ni kumnyang’anya simu ili niweze kuona ni kitu gani hicho kilichokuwa kikimfurahisha kiasi kwamba hata ule uwepo wangu mahali pale akawa hauthamini. Niliinuka na kumnyang’anya simu kitendo ambacho kilizua mtafaruku mkubwa sana. Sikutegemea kama kingeweza kuleta mtafaruku huo. Kwa kweli sikutaka tena kuendelea kuwa katika upole wa kiasi hicho. Moyo wangu ulivumilia matukio mengi sana ambayo kiukweli yalinitesa sana katika maisha yangu. “Naomba simu yangu tafadhali,” aliniambia huku akionekana kuchikizwa sana na kitendo nilichokifanya. “Sikupi,” nilimjibu huku nikimtazama usoni. Alioneka kuwa na wasiwasi mkubwa sana. “Mume wangu ni nini lakini?” “Nimesema sikupi.” “Kila siku ugomvi mimi nimechoka sasa,” aliniambia huku akijifanya kulia, kilio cha kinafki. Sikutaka kuyajali machozi yake, nilichokuwa nataka ni kukishuhudia hicho kituko kilichokuwa kikimchekesha mke wangu. Lahaula! Sikuamini kile nilichokuwa nakiona katika simu ya mke wangu. Alikuwa akichat na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Osman Ismail, huyu alioneka kumfahamu kabisa, nililifahamu hilo kupitia chatting zao. Osmon:Baby nimekumis sana. Ester:Nimekumis pia honey. Osmon:Uko wapi? Ester:Home. Osmon:Unafanyaje? Ester:Nipo na baba yangu. Osmon:Ok baadae basi love you. Ester:Love too Hubby. Nilizidi kupagawa kwa nilichokuwa nikikisoma kwa wakati ule, nilimtazama mke wangu, alikuwa akitetemeka sana, niliamua kumuuliza kuwa Osmon alikuwa ni nani yake kwa kweli alikosa jibu la kunipa zaidi ya yote alibaki akilia kama mtoto mdogo huku akiniomba nimsamehe kwa kile kilichokuwa kimetokea. Je, nini kitaendelea? Usikose sehemu ijayo....

at 7:27 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top