JAMANI BABA Sehemu 10 ILIPOISHIA “Oooh ! Sasa?” “Kuhusu kukutana nje ya hapa nyumbani?” “Ee, ndiyo .” “Nije wapi sasa ? Halafu leo naomba unikate kiu kwelikweli mpenzi wangu.” SEPA NAYO SASA . .. “Hilo wala si ombi ni jukumu langu mimi kama mpenzi wako , mimi kama mkata kiu wako na mimi kama mumeo mtarajiwa, ” alisema Masilinde huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi ya ajabu kwani alikuwa bado hajaamini kama amefika mahali binti mbichi kabisa , aliyeumbwa akaumbika kama Mwaija anafikia hatua ya kuomba kukatwa kiu na yeye . “Sasa sikia , ulizia watu Kwasandarusi ni wapi , watakuonesha mimi utanikuta nimekaa nje .” “Sawa baby ,” alijibu bila woga Mwaija .Mwaija alifunga nyumba huku sauti ya mama yake ikisikika masikioni mwake . ..“ Mimi nakwenda msibani tena, naomba usitoke nyumbani Mwaija .” “Sawa mama .” “We sema sawa mama halafu nirudi nikute haupo.” “Haitatokea mama. ” “Sawa .” “Aah! Sasa nikianza kuogopa maneno ya mama nitalala na kiu yangu, ye’ ikifika usiku atakatwa kiu, mimi je ?” alijipa moyo Mwaija huku akianza safari ya kuelekea Kwasandarusi.. . “Eti we mtoto, hujambo ?” “Sijambo, shikamoo.” “Marahabaa . Eti Kwasandarusi wapi ?” “Pale penye mikokoteni nje ,” alijibu mtoto mmoja aliyekuwa akicheza mtaani . “Haya asante ee?” alishukuru Mwaija . Mwaija alitembea kuelekea Kwasandarusi , kwa mbali alimwona mama yake wa kambo amekaa nje kwenye fomu ... “Nikifika nitamwonesha maajabu , nitamkumbatia, ” alisema moyoni Mwaija . “Kweli , alipofika, wakati Masilinde anasimama ili kumkaribisha, Mwaija akamvaa na kumkumbatia kisha mabusu mfululizo yakafuatia ... “Mmm.. .mwaaa ... mmmmmwaaa ... mmmmwaaa!” Masilinde tayari alishafika kitandani kihisia japokuwa mabusu yale yaliwashangaza wengi kwani waliowaona walibaini tofauti kubwa ya umri kati ya Masilinde aliyeonekana kama ana miaka 50 na Mwaija aliyeonekana ana miaka kama 20 tu! “Yule si kama mtoto wake?” alisema mzee mmoja akiwa jirani na eneo la waliposimama wawili hao .. . “Yahe siku hizi ukifuata umri utaachwa! We angalia wapi umelenga ,” alisema mwenzake wakiwakodolea macho akina Masilinde. “Nikwambie kitu my love,” alianza kusema Mwaija. “Nambie tu. ”“ Mama alinionya kuhusu kutoka nyumbani.” “Kwa hiyo?” “Kwa hiyo twende haraka , kila kitu kiende haraka ili niwahi kurudi kabla hajarudi. ” “Sawa . Sasa unaona lile geti la mwisho pale?” “Ndiyo.” “Ile ni gesti , inaitwa Kichapo! Nenda pale ingia mimi nakuja nikukute imesimama mapokezi , sawa?” “Sawa ,” alisema Mwaija akiwa ameshaanza kutembea kuelekea kwenye gesti hiyo ya Kichapo. “Hodi. ..hodi wenyewe,” Mwaija alibisha hodi baada ya kuhisi ukimya umetawala . “Karibu, ” sauti ya mwanaume ilisikika kutokea ndani. Mwaija alisimama mapokezi. .. “Kuna mtu kaniambia nije nimsubiri hapa mapokezi,” alisema Mwaija akiwa anaogopaogopa... “Nani, au Masilinde?” mtu wa mapokezi alimuuliza. “Mh ! Mi simjui jina . ” “Sasa we utakujaje na mtu humjui jina ?” “Hayakuhusu ,” alikuja juu Mwaija .. . “Halafu pamoja na kuja kumsubiri mtu, we mtoto umeumbika kweli ungekuwa na mtu kama mimi ungefaidi. Ningekununulia simu ya maana, viatu vizuri , yaani ungependa mwenyewe, ” alisema yule mtu wa mapokezi. “Sina shida navyo,” alijibu Mwaija , safari hii akionesha hasira za waziwazi . Mtu wa mapokezi aliposikia mlio wa viatu alijikausha akijua aliyemtuma Mwaija kumsubiri hapo anaingia ... “Karibu sana. ” “Asante . Kuna chumba ?” “Kipo. ” “Naomba. ” Masilinde alichukua chumba akazama ndani na Mwaija. .. “Eti baby, we unaitwa nani?” aliuliza Mwaija mara baada ya kukaa tu. “Kwani vipi dear, hujui jina langu ?” “Silijui . Nani ataniambia na kwa ajili ya nini ?” Masilinde alipiga hesabu za haraka akagundua kuwa, kuuliza kwa Mwaija kumekuja kwa kuambiwa na mhudumu wa gesti hiyo. .. “Huyu haiwezekani tumeingia chumbani kukaa tu, anaulina naitwa nani? Lazima kaambiwa jina langu na yule kijana. Na kama ni kweli kwa kamwambia kwa sababu gani na ili iweje ?” alijiuliza Masilinde.. . “Mimi naitwa Mathayo, ” Masilinde alilitaja jina lake la kwanza ambalo alijua muhudumu wa gesti halijui. “Ooo! Maana yule kaka kaniuliza umekuja kumsubiri nani? Nikasema simjui jina , akasema au Masilinde nini ? Sasa nikawa najiuliza inawezekana ukawa unajulikana kwa jina hadi gesti?” “Simjui mimi na ni mara yangu ya kwanza kuingia humu . Kumbe mzuri kidogo, si tutakuwa tunakujakuja hapa mara mojamoja?” aliuliza Masilinde...“ Wewe tu baby wangu,” alisema Mwaija huku bila soni wala haya akianza kumvua nguo Masilinde ili akatwe kiu . itaendeleaaa

at 12:32 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top