HEBU TUJARIBU KUFUATILIA HAKA KA HADITHI KATAMU KULITOKEA Tawala Mbalimbali Katika Nchi Ya WAKALDAYO Ambayo ilikuwa na wafalme mbalimbali kulingana na majimbo husika.Siku Moja Mfalme na malkia wa jimbo moja liitwalo MEDIANI walishauliana Kupata Ua Moja zurii ndani ya nyumba yao.Walipofikia Makubaliano kweli ua likapatikana Wakasemezawa wao kwa Wao hili ua litatuongezea familia nyingine ya kifalme hapa maana walikubaliana falme yoyote ile itakayokuja kuwatembelea na endapo mtoto wa kiume wa falme ile akilipenda hilo ua nalo likampenda basi wataluhusu lichukuliwe na huyo mtoto wa kiume wa falme nyingine na kuunganisha Undugu. Ki Ukweli Walitumia muda mwingi kulijali lile ua pindi lilipokuwa dogo ili litowe mizizi komavu liweze kutafuta maji yake chini na liendelee kuchipua.Walitumia mda mwingi kuligharamikia na uangalizi wa hali ya juu atimae ua lilikuwa likapendeza likachanua.Tawala mbalimbali zilipita na kuliona Wengi walilitamani wakataka hata kulichukua lakini mfalme alisema ua langu bado dogo halijakomaza mizizi vizuri subirini pindi likikomaa na wakati ukifika basi tutaliluhusu lichague nani kati ya nyinyi mnaokuja kulitaka aondoke nalo. Baada Ya miaka ishirini na kidogo Ua lilikuwa limekomaza mizizi vizuri limechanua vzr linanukia na kupendeza.Pindi lilipokuwa likitambaa hapa na pale kila mmoja alitoa macho kushuhudia uzuri wake.malkia na mfalme wakasemezana wao kwa wao,Sasa Ua letu limekuwa ni wakati wa kuruhusu Kuchukuliwa mtoto wa mfalme Yoyote wa kiume atakaeleta barua kuwa wamekubaliana na ua letu kuwa limchukue ni wakati wa kukubali. Haikupita miezi ufalme jilani Ulikuja kutembelea katika Jimbo La MEDIANI wakiwa familia nzima yaani watoto wa mfalme wa kike na wakiume wote kwa pamoja na wafanyakazi.walipofika katika ule mji walistaajabu kuona uzuri wa lile ua kila mmoja alivutiwa nalo Mtoto Wa Kwanza wa ufalme ule ulioenda kutembelea alimnon'goneza baba yake kuwa baba sasa nimeshakuwa nina nyumba yangu nina kila kitu nataka niongee na hili ua likikubali naomba umpe taarifa mfalme wa hii nnchi kuwa nalichukua ua lake nikakaenalo nyumbani kwangu.Kweli ua lilipomuona yule kijana lilichanua zaidi likajipuliza huku na kule kuonyesha furaha na ishara ya kumkubali yule kijana.Ama hakika kijana alifurahi sana kuona amekubalika.Wafalme waliongea huko atimae wakapatana dhamani ya kuondoka na lile ua hatimae ua liling'olewa kutoka katika falme ya mediani kuelekea katika falme ya huyo baba ake na kijana sherehe ilifanyika na undugu ukaonganishwa. MWANA wa Mfalme alielichukua lile ua alifika akaliweka ndani Mwake hakika alijiskia raha maana lilikuwa linapendeza na kuvutia.Alianza kutumia gharama zake kubwa kulituza maana alijua mizizi bado haijaanza kwenda chini kutokana na kuwa wamelin'goa sehemu yake na kulileta sehemu nyingine.Lakini Ilipita Mwaka yule kijana akajua sasa hapa ua langu limekomaa na litakuwa limezoea mazingira aliliacha aone je linauwezo wa kusimama na likapendeza kama alivyolikuta kwao? Cha ajabu kila alipokuwa akiludi kutoka katika pilika pilika alikuta ua linazidi kudhoofika.Mtoto wa mfalme alihuzunika sana kuona ua linashindwa kuchanua vzr kama alivyolikuta kwao alijikuta anaanza kulichukia.Katika mizunguuko yake ya huku na huko alipita na kuona maua mengine azuri yanajitunza vzr alivutiwa nayo alijikuta muda mwingi anapoteza kukaa kalibu na yale maua ya nje kutokana na ua lake ndani kushindwa kuchanua na kumelemeta kama zamani.Muda Mwingine mtoto wa Mfalme alipikua akikaa peke ake alijikuta anajusemea Mwenyewe"Ua langu nimeliachia kila kitu ndani,Nimelipa kila kitu ndani nimelipa udongo nzuri,Mbolea,Maji, n.k lakini sijui kwanini limeshindwa kuvitumia ili liendelee kupendeza kama zamani?.Nitakaa na kutamani haya maua ya nje Mpaka lini?.Ona yanavojitunza mpaka raha hutumia kile kidogo yanachokipata kuendelea kujibolesha lakini ua langu nimelipa vyote limeshindwa kujiboresha"sijui nifanye nini..? Wazo Likamwijia na kusema nenda kaliambie Ua lako Unapenda Liweje Acha tamaa kutamani vya nje na wakati unajua kabisa Uwezo Wa ua lako kupendeza kama zamani upo likumbushe nini unapenda kutoka kwake huenda limesahau Ulilipendea Nini. Mtoto Wa mfalme baada ya kupata wazo hilo Siku Moja jioni alitumia muda mzuri huo wa kulikumbusha ua lake nini kilichomvutia kutoka kule kwao mpaka kuleta ndani ya nyumba.toka siku hiyo ua halikusahau kile ambacho anapenda mtoto wa mfalme.lilifanya kila jitihada na likaanza kupendeza kama zamani.Ama hakika mfalme alitokea tena kulipenda ua lake.Je unajua nini kilitokea.Mtoto wa mfalme hakutamani tenaa Maua Ya nje FUNDISHO LANGU _______________________ Je Ua ni nani.....? 👉 Ua ni binti kutoka katika ufalme wa Mediani Je Wafalme wa Mediani ni akina nani?? 👉Wafalme wa Mediani Ni Wazazi wa huyo binti ambae ni Ua Je Mtoto wa Mfalme ni nani?? 👉Ni mume wa huyo binti kutoka falme ya Mediani ambae amehusika kama ua NINI MAANA YA KISA HIKI 👉Ukweli ni kwamba wanawake wengi wanajisahau sana pindi wanapoingia katika ndoa na kusahau ni nini kilichomvuta mme wake mpaka akapendwa.Wamesahau wao kama ni ua linalotakiwa kupendeza ndani ya nyumba kila mara ili kumvutia mmewe lakini badala yake wamepoteza ule uzuri wao waliokutwa nao hawajijali tena na wameona kuvishwa pete ndio kumaliza kila kitu 👉Ukweli ni kuwa mwanamke anatakiwa awe mlembo ili kuendelea kumvutia mumewe kila mara.Ndoa pekee isikufanye umemaliza kila kitu Angalia nini kilichompata yule binti baada ya kuacha kujijali tena Ndicho kinachofuata pia kwa kuacha kwako kujijali.usipoteze ule mvuto wako uliokutwa nao kwa wazazi eti kisa umeolewa. 👉Kama ukiendelea kuvutia daima hakika mmeo hana sababu ya kusema apate tamaa kwa wengine na wakati wewe umewazidi mvuto Hebu jiulize umeshaenda sokoni kununua kitu halafu mmeshapatana na bei na muuzaji lakini ghafla ukatupia macho pembeni kwa muuzaji mwingine ukaona kitu kile kile lakini kinaonekana kina ubora kuliko ulichokuwa unataka kununua je nini kinafuata ni jukumu la kuacha kununua ulichopatana nacho na kufuata kile kilichonona Ndivyo ilivyo ukipoteza ubora wako kama mke kinachofuata jilani yako anaeendelea ku maintain ubora wake atakusaidia majukumu 👉Pia na nyinyi waume si busara sana kuanza kuvutika na vya nje na wakati unao uwezo wa kumwambia mkeo vile unavyopenda awe.Usimuonee aibu ni jukumu la kukaa na kumuambia yule ni mke wako au ukishindwa kumwambia fanya jukumu la kumnunulia vitu ambavyo unavutiwa navyo na kuona akitumia katika kujiremba unapendezwa navyo.Hii itakusaidia kujenga familia bora yenye amani na upendo Muda wote USISAHAU Hata vitabu vitakatifu Vinakusisitiza wewe Mwanamke Uwe Pambo Ndani Ya nyumba hili ni jukumu lako la kwanza kama mke..............

at 11:44 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top