Home → ushauri
→ HATUA KUMI ZA KUCHAGUA MCHUMBA

Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.
Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.
Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.
Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.
Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.
Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.
Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.
Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye.
Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea.
Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.
Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.
KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.
Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.
PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.
TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.
NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.
Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.
TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.
Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.
Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.
SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.
Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.
SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana
NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.
TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.
KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.
Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.
HATUA KUMI ZA KUCHAGUA MCHUMBA  Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni. Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi. Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake. Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli. Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa. Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake. Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy aliwahi kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao. Nia ya swali lake ilikuwa ni kuniomba njia za kumtambua mwanaume mkweli bila kufanya naye mapenzi? Aliuliza hivyo huku akiwa na hoja kuwa wanaume wengi hawako tayari kuwa na uhusiano na msichana bila kufanya naye mapenzi na wakati huo huo huficha tabia zao chafu wakilenga kumnasa wamtakaye. Binafsi nafahamu kuwa kuna wanawake/wanawake wengi ambao hujiingiza katika mapenzi kwa kutekwa na hadaa za mwili na kujikuta wanacheza mchezo wa kitoto wa pata potea. Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya. Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi. KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye. Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure. PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake. TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka. NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia. Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia. TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa. Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa. Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha. SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda. Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu. SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe. TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana. KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake. Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.
Artikel Terkait
Tatizo la Ugumba kwa wanawake  Ugumba ni hali ya mwanamke kushindwa kushika ujauzito. Linaweza kuwa tatizo pia kwa mwanaume lakini katika makala hii tutaona nini kinasababisha tatizo hili kwa upande wa wanawake. Nini husababisha ugumba kwa wanawake? Mayai kutokomaa ipasavyo: Tatizo la mayai kutokukomaa vema ndilo chanzo na sababu kuu ya wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito na hii inachukua karibu asilimia 30 ya wanawake wote wagumba. Habari njema ni kuwa tatizo hili linaweza kurekebishwa kirahisi ikiwa mwili utapewa vile viinilishe mhimu vinavyokosekana hadi kupelekea mayai kutokomaa vizuri. Vinavyosababisha mayai ya mwanamke kutokomaa vema: (1) Matatizo ya kihomoni Matatizo katika homoni ndicho chanzo kikuu cha mayai kutunga bila kukomaa vizuri. Hatua za ukomaaji wa mayai zinategemea uwiano mzuri wa homoni na namna zinavyotegemeana katika kufanya kazi. Jambo lolote linalovuruga homoni kubaki katika uwiano wake sawa na wa kutegemeana na wenye kufanya kazi ipasavyo linaweza kupelekea utungaji wa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Kuna sababu kuu mbili zinazosababisha matatizo katika homoni: Ufanyaji kazi usioridhisha wa hypothalamus Hypothalamus ni sehemu ya mbele ya ubongo ambayo ina jukumu la kutuma ishara (signals) kwenda katika tezi ya pituitari ambayo yenyewe tena hutuma uchochezi wa kihomoni kwenda kwenye ovari katika mfumo wa F.S.H na L.H ili kuanzisha ukomaaji wa mayai. Ikiwa hypothalamus inashindwa kufanya kazi zake vizuri kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa ndiyo kutakuwa ni matokeo yake. Tatizo hili linachukuwa asilimia 20 katika kesi za mayai kushindwa kukomaa kiasi kinachohitajika. Ufanyaji kazi usioridhisha wa tezi ya pituitari Kazi kubwa ya tezi ya pituitari ni kuzarisha na kutoa homoni mbili maalumu kwa ajili ya mfumo wa uzarishaji kufanya kazi zake vizuri ambazo zinajulikana kitaalamu kama ‘Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ na ‘Luteinizing hormone (L.H)’. Mayai yatashindwa kukomaa vizuri ikiwa ama L.H au F.S.H zinatengenezwa chache sana au nyingi sana kuliko inavyohitajika. Hili linaweza kutokea kama sababu ya ajari, uvimbe au kama usawa usio sawa wa kikemikali katika pituitari. (2) Kovu katika Ovari Uharibifu au ajari katika ovari unaweza kupelekea kuzalishwa kwa mayai ambayo hayajakomaa. Kwa mfano, upasuaji mkubwa, uvamizi au upasuaji wa mara nyingi wa uvimbe katika ovari unaweza kusababisha kapsuli ya ovari kupata majeraha au makovu na hivyo kwa namna moja ama nyingine kuweza kuzuia utungwaji wa mayai ambayo hayajakomaa vema. Pia maambukizi katika njia ya uzazi yanaweza kupelekea tatizo hili. (3) Dalili za mwanzo za kukaribia kufunga kuzaa (Menopause) Hii huchangia kwa asilimia chache na kwa sasa halielezeki kisawasawa. Kwamba wanawake wengi wanapokaribia umri wa kuacha kuzaa kuanzia miaka 40 kwenda juu baadhi yao hutokewa na tatizo la kutunga mayai ambayo hayajakomaa vema. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao mapema kabla ya umri uliozoeleka yaani miaka 40 kwenda juu. Kwa sababu hiyo inadhaniwa kwamba uwezo wao wa asili katika kuzalisha mayai unakuwa umepunguwa na wengi wao huwa ni wale walikuwa wakijihusisha zaidi na michezo ya kukimbia au wale wenye historia ya muda mrefu ya kuwa na uzito pungufu na wafanyaji sana wa mazoezi. Tatizo hili pia linaweza kuwa ni la kurithi. (4) Matatizo kwenye kijishimo yai (follicle) katika ovari: Ingawa kwa sasa bado hili nalo halielezeki, hiki kijishimo yai kwa kitaalamu kinajulikana kama ‘’follicle’’ ndicho hupasuka na yai kutoka. Kuna baadhi ya kina mama wanapata dalili za kijishimo yai kutokupasuka “unruptured follicle syndrome” na matokeo yake kila mwezi mama anazalisha yai kama kawaida lakini hiki kijishimo yai kinashindwa kupasuka. Hivyo yai linabaki ndani ya ovari na utungaji wa mimba unashindwa kufanyika. Kinachosababisha ufanyaji kazi dhaifu wa mirija ya uzazi (Fallopian Tubes): Magonjwa katika mirija ya uzazi yanahusika na ugumba kwa karibu ya asilimia 25 ya wanawake wote wagumba. Hali yenyewe inatofautiana toka kwa mmoja hadi kwa mwingine kutoka kugandana au kunatana kidogo hadi kuzibika kabisa kwa mirija. Matibabu ya mirija iliyozibika huhusisha upasuaji au usafishaji wa mwili kwa kula vyakula na vinywaji maalum kwa muda wa majuma kadhaa. Sababu kubwa zinazopelekea kuzibika au kunatana kwa mirija ya uzazi ni pamoja na zifuatazo: (A) Maaambukizi Maambukizi katika njia ya uzazi ambayo yamesababishwa ama na bakteria au virusi na ambayo kwa kawaida ni magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya tendo la ndoa, maambukizi haya kwa kawaida husababisha muwasho au kuungua na kupelekea makovu na uharibifu. Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na mengineyo yanaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa wanawake wengi hasa ikiwa hayatatibiwa mapema. (B) Magonjwa yasiyo ya kawaida Magonjwa yasiyo ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa kidole tumbo (appendicitis) na uvimbe katika utumbo mpana (colitis), magonjwa ambayo husababisha muwasho au kuungua chini ya uvungu wa utumbo mkubwa na kuiathiri mirija ya falopiani na kama matokeo yake makovu na kuzibika kwa mirija ya uzazi hutokea. (C) Upasuaji uliopita Upasuaji una chukua nafasi kubwa katika kusababisha ugumba kutokana na matokeo yake ya kusababisha magonjwa ya mirija ya uzazi na uharibifu utokanao na huo upasuaji. Upasuaji katika utumbo mkubwa unaweza kupelekea kunatana au kugandana kwa mirija ya uzazi kutakakopelekea mayai kushindwa kusafiri kirahisi katika mirija hiyo ya uzazi. (D) Mimba kutungwa nje ya mji wa uzazi: Hii ni wakati mimba inapotungwa katikati ya mirija ya uzazi yenyewe. Katika hali kama hii hata kama kutatokea bahati kiasi gani bado kunaweza kusababisha uharibifu katika mirija na hali hii ni moja ya hali mbaya sana kiafya na kimaisha. (E) Hali ya kurithi Kwa nadra au kwa asilimia fulani ndogo baadhi ya wanawake huzaliwa na hali ya kuwa na mirija isiyo ya kawaida kwa uzazi na kwa kawaida hali hii huambatana na mji wa uzazi usio wa kawaida pia. . (5) Sababu za kitabia: Inajulikana wazi kwamba baadhi ya tabia na namna tunavyoishi kunaweza kupelekea wanandoa wakashindwa kupata mtoto. Kwa bahati nzuri nyingi kama si zote ya hizo tabia zinaweza kurekebishika au kuachwa kabisa na kupelekea siyo tu kuwa na uwezo wa kuzaa bali pia kuwa na afya nzuri kwa ujumla. Sababu hizo za kitabia ni pamoja na zifuatazo: Lishe na mazoezi Ili mfumo wa uzazi uwe na uwezo mzuri unahitaji vitu viwili mhimu, lishe kamili na mazoezi. Wanawake wenye uzito uliozidi sana au wenye uzito pungufu sana wanaweza wakapatwa na tatizo la kutopata ujauzito kirahisi. Uvutaji sigara Uvutaji wa sigara una mchango mkubwa na ugumba. Uvutaji sigara husababisha uzarishwaji wa mbegu chache kwa mwanaume (lower sperm count) kwamba mwanaume anatoa mbegu chache sana ama pungufu wakati huo huo uvutaji sigara huchangia katika tatizo la kutoka kwa mimba, kuzaa kabla ya miezi 9 (njiti), na kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo kwa wanawake. Unywaji pombe Unywaji pombe kupita kiasi una mchango mkubwa sana katika ugumba na hii hata ikitokea mama akapata ujauzito kama bado anaendelea kunywa pombe inaweza kupelekea matatizo hata kwa mtoto mtarajiwa. Unywaji pombe pia huchangia uzarishwaji wa mbegu chache kwa wanaume. Madawa ya kulevya Utumiaji a madawa ya kulevya kama bangi na mengine ya kujidunga kwa sindano kunaweza kuwa sababu ya kuzalisha mbegu chache kwa wanaume. Utumiaji wa dawa za kulevya kama ‘Cocaine’ kwa mama mjamzito kunaweza kusababisha mtindio wa ubongo na matatizo katika figo kwa mtoto mtarajiwa. Matumizi ya madawa ya kulevya inafaa yaepukwe wakati wa kutafuta ujauzito na wakati wa ujauzito. Utowaji mimba Utowaji mimba wa mara kwa mara pia unahusika sana na tatizo la ugumba kwa karibu ya asilimia 20. Utowaji mimba unaweza kusababisha makovu katika mji wa uzazi na hata kuharibika kabisa kwa mji wa uzazi ikiwa utowaji huo haukufanyika kitaalamu au unafanyika mara kwa mara. (6) Sababu za ugumba za kimazingira: Uwezo wa kushika ujauzito unaweza pia kuathiriwa kutokana na kuwa karibu na baadhi ya kemikali au sumu katika maeneo ya kazi au makazi. Vitu viwezavyo kusababisha mabadiliko, dosari za kuzaliwa, utokaji mimba, au utasa huitwa ‘Sumu kwa mfumo wa uzazi’. Kamikali zifuatazo zinahusishwa na ugumba au utasa: Risasi (Lead) Kuwa karibu na kemikali au sumu zinazounda risasi kunaweza kuwa sababu ya ugumba. Risasi hupelekea kuzalishwa kwa mbegu zisizo za kawaida kwa wanaume zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘teratospermias’ na inafikirika pia kuhusika na utokaji mimba kusiko kwa asili (artificial abortion). Baadhi ya matibabu na madawa ya hospitalini Kuwekwa kwenye matibabu yanayohusisha mionzi (x-rays), mionzi ya kawaida au hata ile ya kutibia kansa (chemotherapy), kunaweza kusababisha matatizo katika uzarishwaji wa mbegu kwa mwanaume na wakati huo huo kuchangia kwa sababu kadhaa zinazopelekea kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Pia matumizi ya dawa za kuzuia ujauzito kwa muda mrefu yamekuwa yakihusishwa na ugumba kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado kuna mjadala mkubwa katika hili. Ethylene Oxide Hii ni kemikali inayotumika kusafishia vifaa vya upasuaji, pia hutumika katika kutengeneza baadhi ya sumu za kuua wadudu. Ethylene oxide inaweza kupelekea matatizo katika uzazi hasa katika miezi ya mwanzo mwanzo ya ujauzito na inahusishwa sana na tatizo la utokaji mimba katika miezi ya mwanzo ya ujauzito (early miscarriage). Dibromochloropropane (DBCP) Hii pia ni kemikali au dawa inayotumika katika kuua wadudu, ikiwa unafanya nayo kazi kila mara inaweza kusababisha kutungwa kwa mayai yasiyokomaa vizuri, kuelekea mapema kwa ukomo wa kutokuzaa kabla hata ya miaka 40 au 45 (early menopause) na kadharika. (7) Sababu zingine zinazoweza kusababisha ugumba kwa mwanamke: Karibu asilimia 10 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya mji wa uzazi usio wa kawaida (abnormal uterus). Hali zingine ni pamoja na uvimbe katika kizazi, kugandana au kunatana kwa mji wa uzazi na mirija ya uzazi. Karibu asilimia 3 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya matatizo ya ute usio wa kawaida katika mlango wa kizazi (femaleís cervical mucus). Ute ute huu unahitaji kuwa na hali fulani maalumu kwa mbegu za kiume kuweza kuogelea kirahisi katikati yake. Chanzo kikubwa cha tatizo hili ni usawa usio sawa wa homoni za kike ambapo homoni ya uzazi ya kike iitwayo ‘estrogen’ yaweza kuwa ni chache sana au homoni nyingine iitwayo ‘progesterone’ yaweza kuwa ni nyingi sana tofauti na inavyohitajika. Vitu vya kuepuka kwa mtu mwenye tatizo la ugumba: ChipsiVinywaji baridiKaffeinaNyama nyekunduVilevi ... Read More
Hivi unazijua Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda Kwa Dhati??  Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu! ... Read More
Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati ANAVYOKUTAZAMA Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda. MIPANGO Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu. ATAONESHA HUZUNI Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. ATAKUAMINI Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake. ATAKUPA NAFASI Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake. UTAKUWA MWANAFAMILIA Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao. ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo. ATAKUSAIDIA Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani. ATAJITOLEA Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati. ATAAMBATANA NAWE Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu. KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!! ... Read More
JIFUNZE KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPENZI YA DHATI NA WEWE: Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi". Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. MTU AMBAYE HAKUPENDI KWA DHATI: ==> Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako. ==> Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?" Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo". Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu. ==> Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo. ==> Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie. ==> Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. ===> Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo. MTU ANAYEKUPENDA KWA DHATI: ==> Hachoki kukwambia NAKUPENDA, kwani anajisikia raha sana pale atamkapo neno hilo juu yako kwahiyo unaweza ukawa kama wimbo wake kwako. ==> Anajivunia kuwa na wewe na atapenda kukupa sifa nzuri kila mara, yani Hachoki kukusifia. Atakushauri pale unapokosea ili uwe katika njia nzuri. Unaponuna atajua cha kufanya ili wewe ufurahi na kurudi kwenye hali ya kawaida. ==> Hachoki kukuombea mema na kukutakia mafanikio. ==> Atapenda kukueleza ukweli kila mara ili uweze kujenga uaminifu na imani juu yake. ==> Wewe utakuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake, atakuthamini na kukujali. Tatizo lako litakuwa sawa na tatizo lake, atakupa ushauri bila kuchoka. ==> Kabla ya kumuuliza swali kuwa "je unanipenda?" atakuwa ameshakujibu tena kwa hisia nzito kuwa "nakupenda sana mpenzi wangu". ==> Hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, kwakuwa wewe ndiye furaha yake. ====> Thamani yako ni kubwa sana kwake, anakuona mpya kila siku na hachoki kuvutiwa na wewe. Anakupenda kwa kumaanisha na si kukupenda kimazoea tu. Neno NAKUPENDA litamtoka moyoni na ataridhihirisha kwa kinywa chake. Mtambue mtu huyu kuwa anakupenda kwa dhati. NB: Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Si vyema kutumia mapungufu ya mwenzio kama fimbo katika mapenzi, cha muhimu ni kumuelimisha na kumuelekeza ili muweze kwenda sambamba. Nadhani baadhi ya maswali ya wadau yatakuwa yamejibiwa na hiyo mada. Kama kuna nyongeza au swali lolote kuhusiana na hiyo mada tuambiane hapa na kupatiana majibu hapa hapa wadau. ... Read More
Mbinu Tata Za Kumfanya Mwanamke Ajigonge Kwako Kirahisi  #1 Mfanye mwanamke ajieleze kwako Unaweza kumuuliza swali kama “Ni kitu gani ambacho kinakufanya unique/tofauti na wengine?” Ama kumwambia, “Wewe unakaa mdogo sana kiumri kwangu. Ni kitu gani ambacho uko nacho ambacho kitaziba pengo hilo?” Ataanza kukupatia sababu ambazo anajiona kuwa yeye ni unique – kiufupi atakuwa akijaribu kujieleza zaidi ili ajipendekeze kwako/ umpende zaidi. Yaani atakuwa anajaribu kuhakikisha kuwa unaridhika na kila kitu ambacho atakwambia. Na uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa kadri mwanamke anavyokuwa mrembo ndivyo zaidi utakavyohitajika kumfanya ajihitimishe kwako, usiogope kumuuliza maswali ambayo yatamlazimu ajihitimize kwako. Muulize maswali mazito. Muulize maswali ambayo itakuwa ngumu kwake kujihitimu kwako. Na kitu cha kufurahisha kuhusu wanawake warembo, ni kuwa wamezoea kufukuziwa na wanaume kiasi cha kuwa ukianza kuuliza maswali na kujihitimu kwako, atafall na wewe zaidi. Hii ni kwa sababu hawajazoea kuulizwa maswali kama hayo. Hawajazoea kuambiwa, “Wewe si mwanamke type yangu.” ama, “Ningekutongoza lakini unanikumbusha ndugu yangu wa kike mdogo.” Pia unapaswa kuhitimisha wanawake kulingana na ladha yako. Labda kwa mfano hupendi wanawake wanaovuta sigara, kunywa pombe nk, basi mhitimishe kwa kutumia mambo haya. Usimfiche. Mwambie ukweli. Kumwambia mambo kama haya kutamfanya ajue vigezo vyako. Unampa challenge na yeye kutaka kutimiza vigezo vyako. Mbinu hii ni rahisi ya kumuwin kirahisi na kumfanya akufukuzie. #2 Tumia Mwili wako Mara ya kwanza unapoongea na mwanamke huwa anaangalia kando. Wewe ndie uko wazi, unaongea na yeye, unamwangalia, lakini yeye ameangalia kando kabisa. Hapo kuna ile hisia ambayo inakuja ndani yako kuwa huyu mwanamke hamakiniki na wewe kabisa. Well, hapa ndipo unatumia mbinu funge ya kuiga vile ambavyo anafanya yeye. Wakati umemuapproach, si lazima umuangalie mzima mzima kwanza, unaweza kuangalia kiupande. Na akiongea kitu ambacho umependezwa nacho, unaweza kutumia mwondoko wazi kwa kuangalia upande wake. Na akisema kitu ambacho hujapenda basi tumia mwondoko funge kwa kuangalia kando. Mbinu hii hufanya kazi kwa kuchukua atenshen na umakinifu wa mwanamke. Atamakinika kwa kila neno ambalo atakwambia. Mwishowe itajeuka kuwa ni yeye ndiye anayekufukuzia na wala si wewe. Mbinu hii pia inampa confidence ya kutamka mambo ambayo si rahisi kutamkwa na mwanamke hivihivi. #3 Ongea Kwa Kujiamini na Amri Ndani yake Katu mwanamke hawezi kukufukuzia kama utatumia toni saidizi kama, “Mambo waendeleaje?” ambapo sentensi kama hii toni ya sauti inapanda mwishoni. Kama vile unauliza swali. Matumizi ya sentensi hizi zitakufanya uonekane mtu mdhaifu, mhitaji, na utafanya wanawake wakukimbie. Lakini ukitumia toni saidizi zilizovunjwa kwa mwanamke kama, “Hey! Njoo hapa! Waendeleaje!” unatoa sauti ya kuamrisha na ya kutoa maelekezo. Na kwa kuwa uasili wa mwanamke ni kufuata amri, atakujibu kwa kutafuta toni saidizi ili aweze kujihitimisha kwako. Atakwambia, “Mmh, jina langu ni Mamito?” huku akitaka umthibitishe. So, ukimwambia, “Sasa, mpangilio wako ni upi!? kwa toni saidizi iliyovunjwa, atakujibu... “Mmh, mimi mwanafunzi nasomea...huu ni mwaka wangu wa...” Kiufupi hapa anajaribu kujieleza zaidi kwako kulingana na vile sauti yako ilivyotoka. [Soma: Jinsi ya kuwa mwanaume bora ya wote] #4 Weka nafasi na Pozi Katika Maongezi yako Unapoongea na mwanamke, hutaki kuona umepalilia maongezi bila mpangilio, badala yake huwa unataka nafasi angalau kurudi nyuma kiasi kuyapa maongezi yenu nafasi ya kupumua. Unaruhusu kuwe na angalau kimya ndani yake. Kimya ambacho kinaenda polepole. Na nafasi ambayo utampa mwanamke nafasi ya kujileta kwako ili kuteka atenshen yako. So mpe mwanamke nafasi ya kujiekeza kwako, na utagundua kuwa mwanamke huyu anakusaidia pakubwa kuyafanya maongezi yenu yanawiri. Atafurahi kukupa namba yake ya simu kwa kuwa anakufukuzia. Atafurahi kukutana na wewe katika deti ya pili. Na hatakutatiza zile nyakati za mwisho mwisho za kumuomba penzi. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: