Home → ushauri
→ AINA KUMI ZA WANAWAKE WANAOPENDWA NA WANAUME
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale WENYE MSIMAMO, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
WAPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.
WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.
MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.
WA WAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.
WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.
MARIDADI
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si washamba [nieleweke]. Wanapendeza kwa muonekano.
WANAORIDHIKA
Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.
WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
AINA KUMI ZA WANAWAKE WANAOPENDWA NA WANAUME Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale WENYE MSIMAMO, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio. WAPENDA USAWA Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50. WANAOJUA MAPENZI Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani. MARAFIKI Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani. WA WAZI Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo. WANAOJITEGEMEA Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja. WASIO NA PRESHA Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi. MARIDADI Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si washamba [nieleweke]. Wanapendeza kwa muonekano. WANAORIDHIKA Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke. WA MMOJA Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
Artikel Terkait
HIVI UNAIJUA MAANA YA MAPENZI VIZURI AMA.......???  Jina mapenzi limeweza kupewa maana nyingi kulingana na maongezi yanayozunguka jina hilo. Mapenzi yaweza kusemwa kwamba ni jina linaloonyesha hisia za mtu iwe mahaba, pendo kwa mtu ama upendo wa Mungu. Mara nyingi watu wengi hukosea kwa kuchambua mapenzi katika mahaba pekee. Watu wengi hudhania mapenzi huwa yanahusisha moyo wa binadamu, lakini hakika ni kwamba huhusisha ubongo wa mwanadamu. Kuna aina nyingi za mapenzi ambazo binadamu huonyesha katika maisha yao wanapoendelea na shughuli zao za kila siku. Kama binadamu sisi husahau aina nyingine za mapenzi kwani wengi wetu hawajui neno mapenzi lina maana nyingi. Kwa kufafanua mapenzi yapo na aina zifuatazo Mapenzi ya kimwili (Eros) Aina hii ya mapenzi ni ya kimahaba. Kwa mfano mwanamume kumtamani mwanamke ama vile vile mwanamke kumtamani mwanamume kwa hamu ya ngono. Hapa mapenzi huwa yanayoendelezwa na hisia za kumtaka yule mwingine kimapenzi. Hii ndio aina ambayo watu wengi duniani hudhani ndio maelezo kamili ya mapenzi ill hali hii ni moja yapo ya zingine nyingi. Aina hii ya mapenzi ni muhimu kwa watu wanaoanza kutongozana ama watu wanaofikiri kuwa katika uhusiano. Mapenzi ya Urafiki (Philia) Aina hii ni ambayo inavutiwa na mtu kukufanyia kitendo kizuri ama kukusaidia ama ni mtu mzuri kwa ujumla. Mapenzi hapa yaweza kuwa kwa ndugu ama rafiki yako mzuri. Mapenzi haya huwa sana ambapo mtu wanashiriki maadili sawa na mwenzake na kwamba hisia zao sinaambatana ama mmoja anapokea matendo sawia na yale anamwelekezea yule mwenzake. Mapenzi ya aina hii yanaenziwa sana duniani. Wataaluma huamini kwamba mapenzi ya urafiki husaidia kutoa tamaa ya mwili na kuzingatia kufahamiana zaidi kwa marafiki na dunia kwa jumla. Mapenzi ya Familia(Storge) Aina hii ya mapenzi ni inayoonekana na wazazi kwa watoto wao na pia kutoka kwa watoto kwa wazazi. Aina hii hutofautiana na ya urafiki kwani haizingatii kile mtu anachokutendea bali uhusiano wa kidamu na vile wazazi na watoto wao wanavyotegemeana. Sifa za binafsi hazizingatiwi hapa ili wazazi waonyeshe wanao hisia hizi. Uhusiano wao huchangia kwa mapenzi haya. Mapenzi haya huhusishwa na mtu kujiskia yuko huru na salama. Mapenzi ya Kujitolea(Agape) Aina hii ya mapenzi inazingatia asili, mapenzi kwa Mungu au miungu na mapenzi kwa usiowajua. Hii ni mapenzi ya kujitolea kwa ubinafsi ama mapenzi ya ubinadamu. Aina hii inahusishwa na kuto tarajia malipo au kitu chochote kwa matendo unayoyafanya. Yaani ni mapenzi yakujitolea mhanga. Aina hii ya mapenzi hutusaidia kuwapenda watu tusiowajua na kusaidiana kibinadamu kwa hali yoyote ile. Dunia yastahili kuwa na aina hii kwa wingi ili tukaweza kukaa kwa amani na furaha. Mapenzi kwa Mungu ama niungu pia huwa katika aina hii. Kumwabudu Mungu aliye binguni ni mfano mmoja wa kueleza aina hii. Mapenzi Changamfu (Ludus) Aina hii ya mapenzi ni mapenzi yasio na dhamira yoyote na ma mzaha tu. Mapenzi haya hayana masharti hata kidogo. Mfano wa aina hii ya mapenzi ni kama mtu anovyomtongoza mwingine, kupinga densi na kucheza. Aina hii ya mapenzi haina mambo mengi kwani huwa ni kawaida tu. Aina hii huwa sawa kwa watu wanaojitosheleza kimaisha. Aina hii ya mapenzi huwa gumu wakati mtu mmoja hufasiri kwamba mwingine ana hamu ya kimwili. Inafaa watu waweze kuelewa kama wanahamu zaidi na raha na kufurahi tu. Mapenzi Madhubuti(Pragma) Aina hii ni mapenzi ambayo yako na msingi wa wajibu wako kwa mwingine na wa kuzingatia maslahi ya mwingine ya siku za usoni. Mfano mwema ni kwa wapenzi ambao wako katika ndoa. Aina hii inahusishwa na uvumulivu na maelewano kati ya walio katika ndoa. Aina hii ya mapenzi hukuzwa kwa muda wa miaka kadha na ndio maana yaitwa madhubuti ya ka kudumu. Mvuto wa kimwili sana hauzingatiwi katika aina hii ya mapenzi bali kujengana kimawazo na kufanya maisha yao kuwa bora zaidi. Kinyume na aina zingine za mapenzi mapenzi madhubuti huzingatia pande zote mbili za wapenzi wawili. Lazima wewe wanapendana ama kuwa na mafikira na dhamira sawia. Mapenzi ya Kibinafsi (Philautia) Mapenzi haya ni ya mtu binafsi. Aina hii ya mapenzi huwa ina matokeo mawili, yaweza kuwa nzuri ama ya kudhuru. Upande mbaya wa aina hii huwa kwa ile hali ya ubinafi, kutafuta umaarufu na kutafuta utajiri na hufanya mtu kujiona ana dhamana kuliko mtu mwingine yeyote. Upande huu hufanya mtu akajiona yuko mkubwa kuliko mungu. Pia kuna upande mzuri wa aina hii ya mapenzi ambao inahusiana na mtu kujijua, kwa kufahamu uwezo wako na kujidhamini kwa uzuri wako na unachoweza kufanya. Kwa uhusiano wowote, huwezi kumpenda mwingine kama wewe mwenyewe hauna mapezi ya kibinafsi. Kwa kujipenda kwanza ndio tunaweza kupenda wengine na kuwatunza vizuri maishani. Aina hii ni muhimu sana kwa maisha ya kila mwanadamu. Mapenzi ya kibinafi humsaidia mtu kujua mazuri na mabaya na kupanga maisha yake kwa nji inayostahili. Mapenzi ya kibinafsi humwongezea mtu hali ya kujiamini na kujidhamini. Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi huweza kuelewana sana na watu wengi kwa vile kwa kujidhamini watu pia hukudhamini. Hii husaidia kwa vile mnaelewana na watu kazini, nyumbani na mahali pengine ambapo mnapatana. Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi hawahitaji kujigamba ili watu wawajue ama kujionyesha kwa watu. Uzuriwao hujionyesha kwa wanayofanya na wanavyoongea. Watu wanaojipenda kibinafsi huwa wako huru kwa mambo mapya na uwazi. Uchambuzi na ufahamu wa mapenzi ni nini husaidia kila mwanadamu kutambua aina gani anafaa kuwapa watu kwa kila wakati na aina gani ya mapenzi kutupilia mbali. Mwanadamu anaweza penda ila kwa hiari yake. Haina maana lazima mtu akupende ndio umpende nawe. Kila mwanadamu anauwezo wa kumpenda mwingine ama kitu anachotaka hata kama yeye mwenyewe hajapatiwa mapenzi hayo. Lazima kama mwanadamu kufanya mapenzi kama kitu cha kawaida kwa kila tunachofanya maishani. Iweke iwe sehemu ya maisha yako na utu wako. Pia ni muhimu kuwa na aina hizi zote za mapenzi kwa uhusiano kwa kila siku na watu wengine ilituweze kuishi maisha marefu. Kama binadamu, mapenzi ya muhimu sana ni yale ya kujitolea na yale ya kibinafsi. Unapokuwa na mapenzi yasiyo tarajia kitu chochote na mapenzi yako mwenyewe ndio utaweza kuwapa watu mapenzi hayo mengine. Tukiweza kushikilia aina zote zingine za mapenzi kwa mahusiano yetu basi tutakuwa na maisha marefu na yenye kufana. Mapenzi ni kitu muhimu maishani na ni sharti yaenziwe na kila mwanadamu. ... Read More
Je Wajua Kwanini Wanawake Hula Vyakula vya Ajabu Ajabu Wakiwa Wajawazito?  Tabia hii inayojulikana kwa Kiingereza kama “Pica” inatokana na mtu kutamani kula vitu vyenye virutubisho kidogo sana au visivyo na virutubisho vya aina yoyote kwa mwili. Tamaa hizi huwa zinawapata watoto au mama mjamzito kutafuna vitu ambavyo kimsingi si chakula – kama udongo au chaki. Jina hili la pica ni aina ya ndege ambaye anajulikana kwakuwa anakula kitu chochote, hana anachochagua. Ni kweli kwamba wajawazito wengi hupata hamu ya kula vitu ambavyo si vyakula walivyozoea kula mara kwa mara wakiwa si wajawazito; wengi wao ni rahisi kuwaelewa kwa sababu hukimbilia mchele, barafu na vinginevyo ambavyo si vitu vibaya kula. Kwa watoto, hii ni tabia iliyozoelekakwakuwa inawatokea watoto wengi ambao ni kati ya asilimia 25 na 30% ya watoto wote; lakini kwa wanawake wajawazito, inatakiwa iwe kwa kiwango cha chini zaidi. Nini kinasababisha tabia hii kwa wajawazito? Sababu ya baadhi ya wanawake kuwa na tabia hii wakati wa ujauzito haijulikani hasa. Kwa sasa hakuna sababu maalumu, lakini kwa mujibu wa Jarida la Chama cha Watu Wanaoishi na Ugonjwa wa Kisukari nchini Marekani, tabia hii yawezekana ikasababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Baadhi wanadai kwamba hali hii inaashiria kwamba mwili unajaribu kupata vitamini na madini mengine yanayokosekana kwenye chakula cha kawaida ambacho mtu anakula. Muda wingine tabia hii yawezaikatokana na kuumwa viungo au akili kwa muda mrefu. Baadhi ya vitu vya ajabu ambavyo wajawazito hupenda kula Vitu vinavyopendwa zaidi na wajawazito wengi ni udongo, uchafu. Vitu vingine ni njiti za kiberiti zilizochomwa, mawe, mkaa, barafu, dawa ya meno, sabuni na mchanga. Mjamzito anapokula vitu hivi hujisikii raha kana kwamba amekula chakula chenye faida kubwa kwake na kwa mtoto aliye tumboni. Kuna hatari yoyote kwa mtoto aliye tumboni? Kula vitu ambavyo si vyakula kimsingi ni jambo linaloweza kusababisha madhara kwa mjamzito mwenyewe na mtoto aliye tumboni. Kula vitu hivi kunaweza kuharibu mfumo wa kawaida wa kunyonya virutubisho kutoka kwenye vyakula na kusababisha mwili wako upungukiwe na madini muhimu unayoyahitaji kwa afya yako na ya ukuaji wa mtoto vilevile. Tabia hii ni hatarishi sana kwakuwa vitu ambavyo si vyakula vinaweza kuwa na viambata ambavyo ni sumu au vyenye vijidudu vinavyoathiri mwili. Kudhibiti tabia hii Usihamaki unapojikuta unatamani vitu vya ajabu ajabu wakati wa ujauzito: inatokea sana na si jambo la kushangaza kwako pia. Jambo la muhimu ni kumjulisha muuguzi wako au wahudumu wa kliniki unayohudhuria kujua maendeleo yako ya mtoto tumboni ili akuelimishe na ahakikishe kwamba una uelewa kuhusu hatari zinazoambatana na tabia hiyo. Baadhi ya mbinu za kutumia kushinda tamaa hizo Mtaarifu mhudumu wako wa afya kwenye kliniki unayohudhuria na muangalie kumbukumbu za ukuaji wa mtoto tumboni pamoja na hali yako ya kiafyaFatilia kiwango chako cha madini ya chuma mwilini pamoja na kiwango cha vitamini na madini mengine unayotakiwa kulaOmba ushauri kuhusu kitu gani uwe unakula ili kubadili ili kuepuka vitu vya ajabu (waweza kumung’unya/ kutafuna vitu kama pipi au ‘big g’ isiyo na sukariMwambie hata rafiki yako mmoja kuhusu hamu hizi na umtake awe anakukataza unapokula vitu vya ajabu ... Read More
NAOMBA MSIJE KWENYE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YANGU, NJOONI KWENYE MSIBA WANGU. Baada ya kukaa kwenye ndoa takriban miaka 10 kasoro miezi miwili wakafanikiwa kupata watoto wawili wa kwanza angel na wa pili baraka. jamaa akakaa na mkewe wakapanga mipango mizito sana kuhusiana na tukio lingine zito baada ya tukio lao la harusi.yaani kusheherekea miaka 10 ya ndoa yao. Lakini akajisemea, ngoja nipime kiwango cha uaminifu alichonacho mke wangu kabla ya hiyo sherehe haiwezekani kwamba kuna usalama kabisa maana ktk miaka yote nimekuwa MTU wa kazini,safarini in short sina muda mwingi wa kukaa na familia yangu....na kama atavuka hili jaribu basi naweka nadhiri mbele za mbingu nitamtafutia zawadi nzuri ambayo hajawahi kuona na hatokuja kuisahau Akawaambia marafiki zake nataka nifanye party ya kusheherekea miaka kumi ya ndoa yangu nahitaji kampani yenu,walifurahi sana marafiki zake hususani wafanyakazi wenzake. Kamati zikaundwa mara moja,lakini baba angel aliendelea na upelelezi wa kumjaribu mkewe pasipo kujua huyo mkewe aitwaye Elizabeth. Mama angel aliendelea kualika marafiki zake,wazazi wake wakawa wanasubiria kwa hamu kubwa hilo tukio wakimbariki mwenyezi Mungu kwa kuendelea kustawisha ndoa ya mtoto wao.huku asijue mmewe ana nini ndani ya moyo wake. Baba angel akafanya usajili wa line mpya ya tigo asiyoijua mkewe. Akasajili kwa kubuni jina la #Asajile_mwasilu ambaye alikuwa anahisi anatembea na mkewe maana mara kadhaa alishazikuta msg za ajabu kwenye simu ya mkewe kama za mtu na mpenzi wake na alipoichunguza kwenye tigo pesa usajili ukaonyesha jina la Asajile mwasilu. akawa akichat na mkewe mara kwa Mara, kupitia hiyo namba mpya...... siku moja mkewe akaangalia hiyo namba kwenye usajili akaona jina la "Asajile mwasilu" waooooo ooh my dear,akafurahi basi mwenyewe! Akaamua kupiga simu,mumewe hakupokea akakata akamwambia nitext niko mahali hatutaweza kuelewana. Kumbuka Wakati huo mumewe yupo kazini........akamwambia tuendelee kuchat My nikupendae uko wapi mpenzi wangu nikufuate sasa hivi,maana nilivyofrahi kuona SMS yako mungu anajua!namba zako zote baba angel alifuta kwenye simu yangu,na wewe ndio hujanitafuta tena..... baba angel akajibu, we taratibu,si unajua umeolewa wewe unifuate wapi? mumeo alinipigiaga simu kwamba angenifanya kitu kibaya Sana iwapo ningeendelea kuwa na mawasiliano na wewe basi nikaogopa mwenyewe ndio maana nikajikaliaga kimya. Ooh pole my sweet, ndio walivyo wanaume wasiojitambua hawa,yaani yeye anadhani anaweza kunichunga eti! Anasahau kwamba uanaume sio kuchunga mke uanaume ni kumhudumia vzur mkeo kitandani huo ndio ulinzi tosha. Yaani kusema ule ukweli,sijawahi kupata mwanaume wa kunihudumia vile nitakavyo zaidi yako,uko wapii? Mama angel akaendelea kufunguka. Mh!baba angel akajikuta anaishiwa pozi vibaya mno huku mapigo ya moyo yanayoambatana na ghadhabu yakikitesa kifua chake ambacho hata pumzi ilikuwa ni shida kutoka hakuamini kwamba huyo anaechat naye ni mkewe.......akamjibu kwa kicheko cha uongo Hahaaaaaa ina maana unataka kusema jamaa hayuko vzur kitandani?? Na vipi angel hajambo??? Ndio maana nakuuliza uko wapi this time nikufate?maana umelandisha mtoto mpaka sio vizuri,wewe mwanaume una damu kali,wakati mwingine mpaka naona aibu kumwita mume wangu baba angel maana ukweli Mimi ndio naujua....ila yeye hajui kitu anajua ni wake. Baba angel akawazaa wee huku mipango ya sherehe akiona ikiyeyuka taratibu kadri alivyokuwa akiendelea kuchati na mkewe... Akakaa katibu dakika 10 bila kusema chochote akiwaza je ni kweli angel sio wangu???mh! Hawa wanawake vipii?? akatazama saa yake akaona ni saa 8 za mchana akajisemea pale ofsini "hivi mke wangu ana roho mbaya kiasi hiki Kumbe nalea mtoto asie wangu?? Akafungua kwenye gallery akatazama picha za mtoto wake huyo mzur akaendelea kujipa moyo......... Akamrudia mkewe akamwambia Wacha buana uko naye angel hapo?? Mama angel akajibu yes, jamaa akajibu tena "Mi mwenyewe nimekumiss sana na nimemmis sana mwanangu natamani nimwone tu lakini naangalia usawa wa mfuko hauko sawa sana...... Mkewe akajibu hebu ngoja nipe dakika sifuri......... Haraka haraka mama angel akampigia simu mumewe kwa namba yake ya siku zote. "Samahani baby unamkumbuka neema msimamizi wa send off yangu?? Jamaa kwa unyonge huku akijikaza kusikiliza uongo wa mkewe akajibu ndio namkumbuka amefanya nini? Nilikuwa nampa taarifa ya party yetu kumbe alipata ajar yuko nyumbani, sasa nimeona wacha nikamwangalie kabisa sasa hivi naomba hela kidogo..........jamaa akamtumia tsh. laki moja na nusu na msg juu akimhimiza kuwahi kurudi. Vipi uko na angel hapo?? Mama akajibu ndio nikupe uongee naye?? basi akampa simu wakaongea na baba yake...... Akachukua simu mama yake akamwambia mumewe " halafu naenda nae angel mara moja! Jamaa akajibu hamna shida. Upesi mama angel akamwandikia sms anaedhani ni Asajile mchepuko wake kumbe ni mumewe huyo huyo akamtext sasa enda mahali tafuta guest nzur nakutumia elfu 80 sasa hivi Jamaa akajibu waooo ndio maana sijawahi kuacha kukupenda Elizabeth wangu.....basi ntakwambia nikipata. Ila uje na angel Baada ya dakika kama 30 Elizabeth akawa amejiandaa na kumuandaa mwanaye huku akimuahidi house girl kana kwamba atarudi saa 2 usiku....... Jamaa mida kama ya saa 10 jioni akamtext wife njoo hapa...........kuna Lodge inaitwa shelisheli unaijua?wife akaitikia yes.....basi njoo ni chumba namba 6 ghorofa ya 6 ila usimwache mtoto pls. Muda wote huo baba angel alikuwa ameshika kitambaa mkononi maana haipiti sekunde asipojifuta machozi machoni alikuwa akilia tu kwa jinsi alivyokuwa akimpenda mkewe.akajifikiria kuwa ,kwanini Mungu alimficha hilo jambo lililo moyoni mwa mkewe??kwanini Mungu ameruhusu alee mtoto asiye wake?? Kufika hapo Ni kama mwendo wa dakika 20 kwa toyo,basi Mama angel akaona achukue hiyo bodaboda awahi na kweli akawa amewahi.......akaingia hiyo hotel akaenda sehemu ya lift akafika chumba gorofa ya 6 akaenda chumba namba 6 Taratibu akafungua mlango mgongoni akiwa na angel akakuta hakuna mtu kumbe jamaa kaingia kidogo uani Dakika mbili hivi jamaa akawa anatokea kutoka uani Ile kufungua mlango Mama angel hakuamini alichokikuta maana tayari kwenye ubongo wake alikuwa amemtengeneza Asajile.....lakini sio Asajile aliyemkuta........ aligongana USO kwa USO na mumewe wanaetarajia kufanya sherehe ya ndoa yao wiki kama mbili zijazo. Mama angel alipiga yowe yesuuuuu huku akitaka kukimbia kutoka nje........mumewe akamkamata mkono wake akamtuliza na kumwambia "usiogope uko kwenye mikono salama ya baba wa watoto wako kaa utulie! Ooh my god sijui nimefanya nini Mimi!?mkewe alijisemea huku akionyesha kuchanganyikiwa. Wakati huo angel yuko kwa baba yake akistaajabu kuhusu kinachoendelea......... Ilimchukua kama dakika 20 mpaka kutulia mama angel Mumewe akaongea maneno mafupi tu..... MKE WANGU, USIJE UKADHANI MIMI NIPO GIZANI KABISA NISIJUE HATA HATA KIDOGO ULICHONACHO MOYONI MWAKO. AKAONGEA KILUGHA KUMKWEPESHA MTOTO ASIELEWE......LAKINI AKIWA NA MAANA KWAMBA TANGU HUYU MTOTO AMEZALIWA,MOYONI MWANGU NILIJUA SIO MTOTO WANGU,HATA WIFI ZAKO, shemeji zako WAZAZI WANGU WALINIAMBIA HILI JAMBO,NA LISEMWALO LIPO.......mama angel akazidi kupigwa butwaa Akaendelea kumsimulia mkewe....... SIKU MOJA NILIOTA NDOTO MTOTO ANAUMWA,NA TULIPOENDA HOSPITALI ETI KATIKA VIPIMO IKAONYESHA WANAPIMA DNA NIKAKASIRIKA,MBONA MNAMPIMA DNA WAKATI HUYU NI MGONJWA ANAHITAJI VIPIMO VINGINE? YULE DR AKANIAMBIA NITULIE KWANI ANAJUA AFANYACHO NIIKAMKA,NILIPOMPIGIA SIMU MTUMISHI WA MUNGU MMOJA AKANIAMBIA MTOTO SI WANGU LAKINI NISICHUKUE UAMUZI WOWOTE MBAYA BADALA YAKE NIENDELEE KULEA MAANA MALIPO NI KWA MUNGU. Elizabeth, umenitonesha tena kidonda mke wangu, Asante umemleta angel kwa baba yake Asajile lakini hayupo,bado nabaki Mimi ndiye baba yake Mungu atanilipa kwa uaminifu wangu......nashkur kwa uongo wako,asante kwa hela uliyonitumia ya chumba, nataka nikwambie nimefanya kama ulivyonipa maelekezo....... Wakati huo mama angel analia tu hakuna mfano,anaona hata aibu kusema nisamehe,alichojibu ktk kulia kwake ni "Naona nafsi yangu inahukumiwa mno kuliko maneno unayoniambia.....najua mwisho wa ndoa yangu ni hapa hakuna jinsi,siwezi kujitetea mume wangu!naiona jehanamu hii hapa,ninauona ubaya wa kufuga dhambi sasa,hapa ndio naamini hakuna siri duniani,haiwezekani ukafanya kitu ukajua haitajulikana. Niko tayari uniambie chochote na sitapinga,nimeaibika mbeke ya mwanangu Mwanangu nimeaibika mbele ya mume wangu anipendaye na nimeaibika mbele za mbingu na dunia..........nitaficha wapi USO wangu mie?? Jamaa akamwambia mkewe najuta kukujaribu mke wangu najuta kuupima uaminifu wako,ila namshukuru Mungu amenipa kifua kikubwa cha kukabiliana na mambo MAZITO. Lakini wakati mwingine namshukuru Mungu tu maana kila jambo lina makusudi....... Wakatoka pale hotelini wakaingia ndani ya gari ambayo baba angel alikuja nayo wakarudi nyumbani. Usiku mzima mwanamke hakulala usingizi akidhani labda mumewe angemuua hata mtoto........asubuhi kulipokucha jamaa alipowahi kazini mwanamke akaanza kupitia message walizokuwa wanachat na mmewe akaona ni kama yupo uchi tu.......akaenda kununua vidonge duka la dawa baridi akameza akafa huku akiacha ujumbe usemao KUHUSU KUFA KWANGU ASILAUMIWE MTU YEYOTE ILA NILAUMIWE MIMI NAPENDA NIWEKE HADHARANI KILA KITU,KUHUSU MTOTO WANGU ANGEL SIO WA MUME WANGU,JAPO KWA KIPINDI CHOTE ALIKUWA ANAJUA NI WAKE.......BABA YAKE ANAITWA ASAJILE MWASILU......ALINIPA MIMBA NIKIWA NDANI YA NDOA YANGU....... NATUBU KWA WAZAZI WANGU NA WAZAZI WA MUME WANGU MNIOMBEE NIENDAKO NIPUNGUZIWE ADHABU YA KABURI,MWISHO NAWAOMBA MSIJE KWENYE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YANGU,NJOONI MSIBANI. Mwisho sitaki kueleza nini kilitokea kwenye mazishi na msiba kwa ujumla wake Lakini jamaa anaendelea kulea mtoto asiye wake na mtoto wake. Kwenye mazishi alisikika akilia akisema najuta kwanini nilipima uaminifu na msimamo wa mke wangu,yamkini mpaka leo angekuwa hai............... BAADA YA MAZISHI MAKABURINI BABA ANGEL ALIMPELEKEA KARATASI KAKA YAKE AMBAYE NDIYO ANGETOA SHUKRANI KWA WATU NA MATANGAZO MACHACHE YA NINI KINGEENDELEA BAADA YA PALE,BASI AKASOMA ILE KARATASI KWAMBA "TUNAPENDA KUWATAARIFU KWAMBA ILE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YA BABA ANGEL PAMOJA NA MKEWE AMBAYE NI MAREHEMU SASA ILE TAREHE IPO PALEPALE ATAFANYA NA WATOTO WAKE ITAAMBATANA NA KUMSHUKURU MUNGU KATIKA YOTE MAANA IMEANDIKWA "SHUKURUNI KWA KILA JAMBO"........... Siku ya sherehe yenyewe watu walifika kwa wingi sana hamna mfano na miongoni mwao ni baba angel original yaani Asajile....... Itaendelea next time Ila jueni kuwa shetani yuko kaz ... Read More
*SIMULIZI DARASA* *STORY FUPI* *USIMDHARAU USIYEMJUA* Msichana mmoja alikuwa amempenda kijana mmoja mtanashati na mcha Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana baada ya muda. Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule kwa dhati. Alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauri kuhusu mipango ya maisha na alikua akimuombea kila alipopata nafasiya kuomba. Siku moja binti alikua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa…hivyo akaalika marafiki zake, na watu wengine muhimu akiwemo mpenzi wake. Wageni wote walifika kwa wakati isipokua yule kijana alichelewa kidogo… Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake.. Akamsifia sana, akasema atamvalisha pete ya uchumba soon, na akasema siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa nafsi yake. Baadae kijana akaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho… Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya yule msichana kumsifia sana. Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu akataka kujua kilichokua ndani ya mfuko..mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate..!! Lahaula… watu wote wakastaajabu.. mkate??? Lakini kabla hajasema lolote kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza kulia.. akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha..!! Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate na kuutupa.!! Maskini..yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota.. Kisha akarudi high table na kusema “baby nakushukuru kwa yote..Huenda umenidharau kwa kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii. Lakini kama ungetambua thamani ya zawadi hii, usingefanya haya..” Kisha akafungua ule mkate na kutoa vitu viwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday. Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema “Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote. Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili kuelekea ndoto yetu ya ndoa.. ..Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona mkate, badala ya pete hii ya thamani iliyokua ndani.. Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata.. Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza..” Kisha akachukua mkate wake, huyoo akaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late.. MORAL OF THE STORY..! Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje.. Mungu huangalia thamani ya kitu ndani lakini Wanadamu huangalia nje.. Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi kuonekana.. Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa kutizama umbo la nje.. Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua haukua mkate wa kawaida… kuna vingi vya thamani ndani yako. Wote wanaokudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima..!! 🌹TUELIMISHANE MEMA🌹 Subra ndio inayotakiwa katika maisha. *akida* ... Read More
Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi. MSOME SAIKOLOJIA YAKE Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira. MRUHUSU AKUJIBU Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. EPUKA MARUMBANO Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano. MUOMBE MSAMAHA Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.” Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: