UVUMILIVU KATIKA NDOA Mume na Mke wote wanatakiwa kuvumiliana na kusubiriana. Hakuna mwanaadamu aliyekamilika. Kama walivyo na udhaifu wanawake, Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: "Kuweni wema kwa wanawake kwani wameumbwa kutokana na sehemu ya juu ya ubavu, na sehemu iliyopinda kuliko zote katika ubavu ni sehemu ya juu. Kwa hiyo kama utataka kuinyoosha utaivunja, na kama utaiacha hivyo hivyo itaendelea kupinda. Kwa hiyo wawaidhini wanawake (waonyeni) kwa kadiri iwezekanavyo." (Bukhari na Muslim). Hadithi hii inathibitisha kuwa hapana mtu atakayedumu na mkewe, kama hapatakuwa na uvumilivu. Mwanaume asitegemee mkewe kuwa na msimamo kama ule wake, ajue kuwa kila mmoja, kulingana na nafasi yake ana umbile tofauti. Vile vile wanaume wana udhaifu wao. Takriban kila mtu hakosi udhaifu ambao si wenye kumpendezesha mwenziwe. Kama wanaume walivyosisitizwa kuwavumilia wake zao kwa udhaifu kama huu na wanawake pia hawana budi kuwavumilia waume zao endepo watakuwa na udhaifu usiipendeza. Hivyo ifahamike kuwa Maisha ya ndoa yanahitaji subira ya hali ya juu na kujitoa au kujitolea kwa namna ya kipekee. Ubinafsi na umimi ndio chanzo kikubwa sana cha kusambaratisha ndoa. Ndoa inaweza kufanya maisha yakawa mepesi au magumu kutegemeana na wahusika wenyewe. Wepesi huja pale kila mmoja anapojitahidi kutekeleza wajibu wake ipasavyo. Hata hivyo wanandoa hawapaswi kuingia kwenye ndoa na mategemeo makubwa sana kiasi ambacho yasipofikiwa inakuwa ndio chanzo cha migogoro. ⏬⏬ In shaa Allah 🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺

at 9:33 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top