Home → simulizi
→ SIMULIZI YA KUSISIMUA... Ndoa Yangu Inanitesa part 7
Nilitulia kidogo nikaendelea, “Moyo wangu unasononeka sana. Laiti ningelijua nisingeoa, maisha gani haya yananitesa kiasi hiki?”Nilijikuta nikilia ovyo kama toto jinga lenye kudeka ovyo.Kilio changu lilikuwa rohoni.na aliyejua alikuwa muumba pekee.Getruda alikuja kunibembeleza kwa hofu kwamba ningechukua maamuzi ya kijinga tena. Aliniandalia chakula mezani.Tulisali kisha tukala .
Saa nane mchana baada ya kupata mlo wa mchana nilimuaga Getruda nikiwa naelekea ofisini kumueleza Mzee Jophu yaliyosibu katika unyumba wangu. Lakini cha kushangaza Mzee Jophu baada ya kumueleza kila kitu,nilimuona uso ukiwa umejawa furaha badala ya kunionea huruma. Hali hiyo aliisubiri kwa hamu hata hivyo alishanga kuona mimi kuchelewa kumuelezea shida zangu toka mwanzoni.Alijifanya kama hataki kuchangia mapenzi ilinimuone mtu mwema,
“Sasa Jophu unakataa nini na wakati nimekuambia mke wangu hajaguswa”
“Inamaana siku zote hizo mlikuwa mkilala tu?”
“Ndio”nilimjibu nikahisi machozi yakinilengalenga, hata hivyo nilijikaza kiume.
“Matatizo haya yalikupata muda gani?”
“Siku ya kwanza toka nifunge ndoa na mke wangu”
“Usinitanie Sweedy. Ulijaribu kwenda hospitali?”
“Ndio.Nilichunguzwa kwa makini.Daktari alinieleza kwamba nilipigwa sindano yenye sumu.Nilikataa kwani sijawahi kupigwa sindando yeyote toka uliponiajiri. Na sasa ni miaka karibu ishirini na tano. Nakumbuka sindano ya mwisho nilichomwa nikiwa na chuoni. Na siku nyingine niile nilipokuja kutolewa damu”
“Kutolewa damu si kupigwa sindano labda una matatizo mengine kiafya.Vipi kuhusu chango?”
“Sina chango,mzee”Nilimjibu nikiwa nimetizama chini.
“Mzee, naomba unisaidie kuokoa jahazi la ndoa yangu”Nilimweleza nikimpigia magoti.Sikuwa najua kwamba mzee Jophu ndiye aliyetuma watu wanipige sindano ya kuua uume wangu.Wakidai wana nitoa damu ilinikapimwe virusi vya ukimwi.Hata hivyo ilikuwa kazi kumgundua mbaya wangu,jinsi alivyoonyesha kutokutaka kuchukua jukumu la kumridhisha mke wangu.
“Mkeo atakubali kwenda kupima damu zetu?”
“Sina uhakika kama atakubali au laa. Ni vizuri kimpigie simu”Nilitoa simu yangu ya kiganjani na kubonyeza namba za Getruda, mke wangu.
“Hallo, mpenzi”alipokea tu baada ya kuona namba zangu juu ya kioo cha simu yake.
“Oooo!, vipi upo salama.”
“Ndio. Sijui wewe”
“Shwari kabisa.Mmmm…utakubali kupima Virusi vya ukimwi?”
“Tangu lini kigori akawa na Ukimwi?”
“Sijambo la ajabu kwani ukimwi unaambukizwa kwa kujamiana tu?”Getruda aitafakari akajiona kweli alibugi sana.
“Sawa, nimekubali kupima afya kwa manufaa yetu sote”
“Ok, jiandae nakuja sasa hivi nyumbani”
“Ok, bye bye”Alinaga na kukatasimu.
“Nilimtizama mzee Jophu na kumwambia, “Amekubali kupima”
Kwambali niliona tabasamu la mzee Jophu lililonifanya nione meno yake ya rangi rangi, nafikiri kutokana kunywa maji ya Arusha tokea utotoni mwake.
“Sasa Sweedy”Alitulia kidogo na kukohoa kinafiki,nilimtizama kwa makini niwezekujua alichotaka kusema,aliendelea “Kwa vile wewe ni rafiki yangu sina budi kukusaidia.Ila nakuomba usimweleze mtu yeyote ‘Especial my wife’,Umenielewa. Narudia tena naomba iwe siri moyoni mwetu”
“Sawa, mzee.Usihofu kitu”nilimjibu kwa upole kabisa.
Mzee Jophu aliongea moyoni akiwa amejawa furaha kubwa mno, “Kile nilichokitaka kimekamilika. Sasa kazi kwangu kurina asali nitakavyo””
Mzee Jophu kunajambo la muhimu nimelikumbuka. Nilimdanganya kuwa nilimwagikiwa na tindikali. Akikuuleza mueleze ni kweli”Nilitulia kidogo, ingawa alijaribu kuficha furaha niliiona , Nikatulia kama niliyewaza kitu ,Machozi yakaniwakia pale nilipokumbuka nguvu zangu nilipokuwa Nchini Thailand “Lakini boss na shindwa kujua ugonjwa huu niliupata wapi na nani aliyeniletea”
“Usijali muombe mungu akuondolee. Hatamimi ninafanya tu, kwa vile wewe rafiki yangu wa damdam, lakini kwa maulana ni dhambi kuzini nje ya ndoa,” Mzee Jophu aliongea ilinimuone mtu wa busara kama alivyoonekana kuwa ni mtu wa busara kumbe ni muungwana wa ngozi tu, lakini rohoni ni muuwaji. Maneno yake ilikuwa vigumu kumgundua kuwa yeye ndiye mbaya wangu, aliyeamua kunitesa iliamfanye mke wangu wake.
Mazungumzo yetu ya ofisi yalikuwa ya muda mrefu. Tulipo maliza jioni iliwadia tuliongozana na Mzee Jophu moja kwa moja hadi nyumbani kwangu.
“Lakini Sweedy kama ameoa mke mwenye uso wa mbuzi mimi sitamkubali atakuwa wako mwenyewe”
“ Hakika mke wangu utamkubali. Amekamilika kila idara. Utamsahau mama Jacob nakuambia” Nilimueleza.
“Yote tisa, kumi tutaona. Nitaamini unajua kuchagua,”
“Lako jicho, yanini ni kusifie?” Niliposema, nilitamani Mzee Jophu ardhike na ombo la Getruda, lakini kitu kilichoniuma zaidi ni jinsi gani ningemuunganisha mwanaume mwenzangu na mke wangu niliyemlipia mahari.
“Inawezekana huyu mshenzi akamkataa mke wangu. Midomo yake imejaa dharau”nilijisemea kimoyomoyo huku nikibonyeza kitufe cha geti.
Getruda Kimario alifika getini na kufungua, mtu wa kwanza kuingia akiwa Mzee Jophu.Shauku yake haikufichika ,alimtupia Getruda jicho la lilo jaa ubembe.Ni hapo ndipo nilipohisi Mzee Jophu kumkubali mke wangu. Alikuwa na shauku ya kumbusu Getruda, nikipindi kirefu toka wapoteane pale ofisini kwake, na Getruda alimkumbuka kuwa yule alikuwa yule aliyempa mama yake mzazi shilingi laki tano za kitanzania iliamuowe yeye. Walitupiana macho yaliyojaa furaha macho ya matamanio ya Getruda yalizidi kumchanganya Jophu. Aliyekuwa na shauku kuupitisha usiku mwanana na binti aliyemlipia shilingi laki tano. Aliamini alikuwa na haki yakujivinjari jasho lake.
Mwanzoni nilihisi hawakumbukani,kumbe kumbukumbu alikuwa nazo na alishuhudia mama yake akipokea hizo hela.
Ulifikia muda muafaka wakuweka mambo hadharani ili nitatuliwe shidayangu. Kabla sijazungumza chochote nilipandisha pumzi na kushusha kwa nguvu kama mtu aliyechoka na pilika pilika za kutwa nzima ,”ooooooophhhh!”Kisha nikasema kwa sauti ya chini kama mgonjwa,ni kweli niliyotaka kusema yaliniuma sana.
“ Nafikiri mke wangu nilisha wahi kukutajia jina la rafiki yangu kipenzi. Ila ni vema nikalirudia leo ukiwa una muona . Aliye kaa hapa mbele ndiye Mzee Jophu. Sio Mzee kweli ni kwaajili ya mali zake ndio maana watu wanampa jina la heshima ya mzee. Huyu ndiye mwa ndani wangu ukimuona yeye ndio umeniona mimi. Shida zake ni zangu, zangu ni zake,”Nilikohoa kidogo ni kumgeukia mzee Jophu. Kijasho kilizidi kuchuruzika kwa kasi kuliko mwanzoni, nilihisi midomo kufa ganzi na kuwa mizito, nilijikuta sauti ikipotea ghafla pale nilipofikiria kumuachia mzee Jophu mke wangu.Tena hajawahi kuguswa na mtu yeyeto maishani. Kwa kweli inatia uchungu sana heri ningekuwa nimezaliwa na udhaifu huo kuliko kunikuta nikiwa mtu mzima.
“Mzee Jophu huyu ni mke wangu, kwa upande mwingine naweza kusema ni mkeo. Nina matatizo ya,,,,,,” hasira kali iliniingia moyo nikashindwa kumaliza, nilijikuta nikiangua kilio. Moyo uliuma sana.
“Kweli kweli na muachia Jophu kigoli wangu?”Nilimtizama Getruda kama vile nikimuaga, sikuweza kukwepa jambo hilo tena.Kwa kuwa lilishakuwa kero katika familia yetu.
“Naomba uwe karibu na mke wangu, kama ulivyo karibu na mkeo, lakini,,,,,,,,,,naomba unifichie siri yangu, heshima iwepo msije mkachukulia muda huo kunidharau, nami sikupenda kuwa hivi,,,”Nilikokoteza maneno kwa ujasiri .
“Ok, nashukuru kumfahamu mkeo, na nitaendelea kumfahamu vizuri, zaidi kadri siku zinavyo zidi kwenda” Mzee Jophu aliongea huku akinyanyuka kuelekea alipo Getruda. Alinishika mkono na kuunyanyua usawa wa midomo yake, hakuchelewa nilisikia sauti ya busu kwenye kiganja cha mke wake wangu. Busu hilo lilimchanganya mke wangu na kujikuta mwili ukimsisimka, vinyweleo na nywele zilisimama kwa shoti ya busu la mzee Jophu.Nilibaki nimeduwa, midomo ikiwa wazi kama sekunde kadhaa.Bila hofu wala haya, walijikuta wamekumbatiana na Mzee Jophu alisogeza midomo yake karibu kabisa na sikio akimnong’oneza.
“Kweli kwenye miti hakuna wajenzi, nitakutunza kama mlima Kilimanajaro unavyotunza Seluji yake, nitakupa chochote unachotaka, ikiwezekana nitakuoa kabisa, nakupenda siko tayari kukuacha, naamini unanipenda” Sauti ya Mzee Jophu ilizidi kumtekenya Getruda, alijikuta akitikisa kichwa ishara ya kukubali.Alishindwa kujizuia kutoa sauti za kizizima, taratibu kwa jinsi maneno ya Jophu yaliyokuwa yakipenyeza sikioni angali yana uvuguvugu, kwa wimbi lenye joto nadhifu.Mzee Jophu alimwachia na kuketi karibu nae.
Mambo yote niliyaona. Kwa jinsi roho ilivyoguguna niliondoka sehemu ile na kuingi chumbani, nilimpenda sana mke wangu, sikupenda awe mke wa shirika wala sikupenda kuona akishikwa shikwa na mtu zaidi yangu. Japo nilikuwa na wivu lakini nilishindwa kwa sababu nilipata udhaifu, ikanilazimu kuvumilia na kuhamisha macho, na kutizama pembeni.Pia hilo lilinishinda nikaamua kujiondokea kiunyonge kama kifaranga asiye na mama.
Kuondoka kwangu, ulikuwa mwanya wa Jophu na mke wangu kupanga mambo yao.
By brayton starpoz
SIMULIZI YA KUSISIMUA... Ndoa Yangu Inanitesa part 7 Nilitulia kidogo nikaendelea, “Moyo wangu unasononeka sana. Laiti ningelijua nisingeoa, maisha gani haya yananitesa kiasi hiki?”Nilijikuta nikilia ovyo kama toto jinga lenye kudeka ovyo.Kilio changu lilikuwa rohoni.na aliyejua alikuwa muumba pekee.Getruda alikuja kunibembeleza kwa hofu kwamba ningechukua maamuzi ya kijinga tena. Aliniandalia chakula mezani.Tulisali kisha tukala . Saa nane mchana baada ya kupata mlo wa mchana nilimuaga Getruda nikiwa naelekea ofisini kumueleza Mzee Jophu yaliyosibu katika unyumba wangu. Lakini cha kushangaza Mzee Jophu baada ya kumueleza kila kitu,nilimuona uso ukiwa umejawa furaha badala ya kunionea huruma. Hali hiyo aliisubiri kwa hamu hata hivyo alishanga kuona mimi kuchelewa kumuelezea shida zangu toka mwanzoni.Alijifanya kama hataki kuchangia mapenzi ilinimuone mtu mwema, “Sasa Jophu unakataa nini na wakati nimekuambia mke wangu hajaguswa” “Inamaana siku zote hizo mlikuwa mkilala tu?” “Ndio”nilimjibu nikahisi machozi yakinilengalenga, hata hivyo nilijikaza kiume. “Matatizo haya yalikupata muda gani?” “Siku ya kwanza toka nifunge ndoa na mke wangu” “Usinitanie Sweedy. Ulijaribu kwenda hospitali?” “Ndio.Nilichunguzwa kwa makini.Daktari alinieleza kwamba nilipigwa sindano yenye sumu.Nilikataa kwani sijawahi kupigwa sindando yeyote toka uliponiajiri. Na sasa ni miaka karibu ishirini na tano. Nakumbuka sindano ya mwisho nilichomwa nikiwa na chuoni. Na siku nyingine niile nilipokuja kutolewa damu” “Kutolewa damu si kupigwa sindano labda una matatizo mengine kiafya.Vipi kuhusu chango?” “Sina chango,mzee”Nilimjibu nikiwa nimetizama chini. “Mzee, naomba unisaidie kuokoa jahazi la ndoa yangu”Nilimweleza nikimpigia magoti.Sikuwa najua kwamba mzee Jophu ndiye aliyetuma watu wanipige sindano ya kuua uume wangu.Wakidai wana nitoa damu ilinikapimwe virusi vya ukimwi.Hata hivyo ilikuwa kazi kumgundua mbaya wangu,jinsi alivyoonyesha kutokutaka kuchukua jukumu la kumridhisha mke wangu. “Mkeo atakubali kwenda kupima damu zetu?” “Sina uhakika kama atakubali au laa. Ni vizuri kimpigie simu”Nilitoa simu yangu ya kiganjani na kubonyeza namba za Getruda, mke wangu. “Hallo, mpenzi”alipokea tu baada ya kuona namba zangu juu ya kioo cha simu yake. “Oooo!, vipi upo salama.” “Ndio. Sijui wewe” “Shwari kabisa.Mmmm…utakubali kupima Virusi vya ukimwi?” “Tangu lini kigori akawa na Ukimwi?” “Sijambo la ajabu kwani ukimwi unaambukizwa kwa kujamiana tu?”Getruda aitafakari akajiona kweli alibugi sana. “Sawa, nimekubali kupima afya kwa manufaa yetu sote” “Ok, jiandae nakuja sasa hivi nyumbani” “Ok, bye bye”Alinaga na kukatasimu. “Nilimtizama mzee Jophu na kumwambia, “Amekubali kupima” Kwambali niliona tabasamu la mzee Jophu lililonifanya nione meno yake ya rangi rangi, nafikiri kutokana kunywa maji ya Arusha tokea utotoni mwake. “Sasa Sweedy”Alitulia kidogo na kukohoa kinafiki,nilimtizama kwa makini niwezekujua alichotaka kusema,aliendelea “Kwa vile wewe ni rafiki yangu sina budi kukusaidia.Ila nakuomba usimweleze mtu yeyote ‘Especial my wife’,Umenielewa. Narudia tena naomba iwe siri moyoni mwetu” “Sawa, mzee.Usihofu kitu”nilimjibu kwa upole kabisa. Mzee Jophu aliongea moyoni akiwa amejawa furaha kubwa mno, “Kile nilichokitaka kimekamilika. Sasa kazi kwangu kurina asali nitakavyo”” Mzee Jophu kunajambo la muhimu nimelikumbuka. Nilimdanganya kuwa nilimwagikiwa na tindikali. Akikuuleza mueleze ni kweli”Nilitulia kidogo, ingawa alijaribu kuficha furaha niliiona , Nikatulia kama niliyewaza kitu ,Machozi yakaniwakia pale nilipokumbuka nguvu zangu nilipokuwa Nchini Thailand “Lakini boss na shindwa kujua ugonjwa huu niliupata wapi na nani aliyeniletea” “Usijali muombe mungu akuondolee. Hatamimi ninafanya tu, kwa vile wewe rafiki yangu wa damdam, lakini kwa maulana ni dhambi kuzini nje ya ndoa,” Mzee Jophu aliongea ilinimuone mtu wa busara kama alivyoonekana kuwa ni mtu wa busara kumbe ni muungwana wa ngozi tu, lakini rohoni ni muuwaji. Maneno yake ilikuwa vigumu kumgundua kuwa yeye ndiye mbaya wangu, aliyeamua kunitesa iliamfanye mke wangu wake. Mazungumzo yetu ya ofisi yalikuwa ya muda mrefu. Tulipo maliza jioni iliwadia tuliongozana na Mzee Jophu moja kwa moja hadi nyumbani kwangu. “Lakini Sweedy kama ameoa mke mwenye uso wa mbuzi mimi sitamkubali atakuwa wako mwenyewe” “ Hakika mke wangu utamkubali. Amekamilika kila idara. Utamsahau mama Jacob nakuambia” Nilimueleza. “Yote tisa, kumi tutaona. Nitaamini unajua kuchagua,” “Lako jicho, yanini ni kusifie?” Niliposema, nilitamani Mzee Jophu ardhike na ombo la Getruda, lakini kitu kilichoniuma zaidi ni jinsi gani ningemuunganisha mwanaume mwenzangu na mke wangu niliyemlipia mahari. “Inawezekana huyu mshenzi akamkataa mke wangu. Midomo yake imejaa dharau”nilijisemea kimoyomoyo huku nikibonyeza kitufe cha geti. Getruda Kimario alifika getini na kufungua, mtu wa kwanza kuingia akiwa Mzee Jophu.Shauku yake haikufichika ,alimtupia Getruda jicho la lilo jaa ubembe.Ni hapo ndipo nilipohisi Mzee Jophu kumkubali mke wangu. Alikuwa na shauku ya kumbusu Getruda, nikipindi kirefu toka wapoteane pale ofisini kwake, na Getruda alimkumbuka kuwa yule alikuwa yule aliyempa mama yake mzazi shilingi laki tano za kitanzania iliamuowe yeye. Walitupiana macho yaliyojaa furaha macho ya matamanio ya Getruda yalizidi kumchanganya Jophu. Aliyekuwa na shauku kuupitisha usiku mwanana na binti aliyemlipia shilingi laki tano. Aliamini alikuwa na haki yakujivinjari jasho lake. Mwanzoni nilihisi hawakumbukani,kumbe kumbukumbu alikuwa nazo na alishuhudia mama yake akipokea hizo hela. Ulifikia muda muafaka wakuweka mambo hadharani ili nitatuliwe shidayangu. Kabla sijazungumza chochote nilipandisha pumzi na kushusha kwa nguvu kama mtu aliyechoka na pilika pilika za kutwa nzima ,”ooooooophhhh!”Kisha nikasema kwa sauti ya chini kama mgonjwa,ni kweli niliyotaka kusema yaliniuma sana. “ Nafikiri mke wangu nilisha wahi kukutajia jina la rafiki yangu kipenzi. Ila ni vema nikalirudia leo ukiwa una muona . Aliye kaa hapa mbele ndiye Mzee Jophu. Sio Mzee kweli ni kwaajili ya mali zake ndio maana watu wanampa jina la heshima ya mzee. Huyu ndiye mwa ndani wangu ukimuona yeye ndio umeniona mimi. Shida zake ni zangu, zangu ni zake,”Nilikohoa kidogo ni kumgeukia mzee Jophu. Kijasho kilizidi kuchuruzika kwa kasi kuliko mwanzoni, nilihisi midomo kufa ganzi na kuwa mizito, nilijikuta sauti ikipotea ghafla pale nilipofikiria kumuachia mzee Jophu mke wangu.Tena hajawahi kuguswa na mtu yeyeto maishani. Kwa kweli inatia uchungu sana heri ningekuwa nimezaliwa na udhaifu huo kuliko kunikuta nikiwa mtu mzima. “Mzee Jophu huyu ni mke wangu, kwa upande mwingine naweza kusema ni mkeo. Nina matatizo ya,,,,,,” hasira kali iliniingia moyo nikashindwa kumaliza, nilijikuta nikiangua kilio. Moyo uliuma sana. “Kweli kweli na muachia Jophu kigoli wangu?”Nilimtizama Getruda kama vile nikimuaga, sikuweza kukwepa jambo hilo tena.Kwa kuwa lilishakuwa kero katika familia yetu. “Naomba uwe karibu na mke wangu, kama ulivyo karibu na mkeo, lakini,,,,,,,,,,naomba unifichie siri yangu, heshima iwepo msije mkachukulia muda huo kunidharau, nami sikupenda kuwa hivi,,,”Nilikokoteza maneno kwa ujasiri . “Ok, nashukuru kumfahamu mkeo, na nitaendelea kumfahamu vizuri, zaidi kadri siku zinavyo zidi kwenda” Mzee Jophu aliongea huku akinyanyuka kuelekea alipo Getruda. Alinishika mkono na kuunyanyua usawa wa midomo yake, hakuchelewa nilisikia sauti ya busu kwenye kiganja cha mke wake wangu. Busu hilo lilimchanganya mke wangu na kujikuta mwili ukimsisimka, vinyweleo na nywele zilisimama kwa shoti ya busu la mzee Jophu.Nilibaki nimeduwa, midomo ikiwa wazi kama sekunde kadhaa.Bila hofu wala haya, walijikuta wamekumbatiana na Mzee Jophu alisogeza midomo yake karibu kabisa na sikio akimnong’oneza. “Kweli kwenye miti hakuna wajenzi, nitakutunza kama mlima Kilimanajaro unavyotunza Seluji yake, nitakupa chochote unachotaka, ikiwezekana nitakuoa kabisa, nakupenda siko tayari kukuacha, naamini unanipenda” Sauti ya Mzee Jophu ilizidi kumtekenya Getruda, alijikuta akitikisa kichwa ishara ya kukubali.Alishindwa kujizuia kutoa sauti za kizizima, taratibu kwa jinsi maneno ya Jophu yaliyokuwa yakipenyeza sikioni angali yana uvuguvugu, kwa wimbi lenye joto nadhifu.Mzee Jophu alimwachia na kuketi karibu nae. Mambo yote niliyaona. Kwa jinsi roho ilivyoguguna niliondoka sehemu ile na kuingi chumbani, nilimpenda sana mke wangu, sikupenda awe mke wa shirika wala sikupenda kuona akishikwa shikwa na mtu zaidi yangu. Japo nilikuwa na wivu lakini nilishindwa kwa sababu nilipata udhaifu, ikanilazimu kuvumilia na kuhamisha macho, na kutizama pembeni.Pia hilo lilinishinda nikaamua kujiondokea kiunyonge kama kifaranga asiye na mama. Kuondoka kwangu, ulikuwa mwanya wa Jophu na mke wangu kupanga mambo yao. By brayton starpoz
Artikel Terkait
*MWAGIA HUMO HUMO EP 03* Sehemu Ya Tatu (3) Baada ya kusema vile aliingiza mkono mfukoni na kutoa pochi alihesabu noti tatu za kumi kumi na kunipa. “Mpelekee hizi mwambie nitakuja.” Nilizipokea na kufunga kazi zangu, pamoja na penzi letu kufa bado nilipelekwa na kurudishwa nyumbani na gari. Nilipofika nyumbani nilikwenda chumbani kwangu, kabla ya kufanya kitu chochote nilivua nguo zangu na kubakia mtupu kama nilivyozaliwa mbele ya kioo kikubwa na kujitazama upya kasoro katika mwili wangu. Nilituliza macho na kuyazungusha taratibu mwilini mwangu kuangalia nina kasoro gani inayonifanya kila kukicha nipoteze wanaume. Kila hatua niliyokuwa nikipiga katika kusafirisha macho yangu nilijigundua nina sifa kubwa sana ya kuitwa mwanamke mrembo tena mwenye kumtia hamu ya mapenzi mwanaume rijali. Umbile langu kwa mimi mwenyewe kama ningekuwa mwanaume na kukutana na mwanamke mwenye umbile kama langu ningemganda kama ruba, lakini kwangu ilikuwa na tofauti kubwa sana. Baada ya kujigundua sina kasoro mwilini nilijikuta nikilia huku nikisema kwa sauti ya chini. “Hali hii mpaka lini?” ”Hali ipi?” Sauti ya Bi Shuu iliuliza nyuma yangu ilionesha Bi Shuu alikuwa ameingia kitambo bila mwenyewe kujua. Niligeuka na kwenda kujitupa kifuani kwake huku nikilia kwa uchungu. “Vipi tena mwali?” “Bi Shuu huu mkosi.” “Wa nini?” “Na Mateja kanimwaga.” “Kwa nini unasema hivyo?” Nilimweleza yaliyotokea ofisini huku nikilia. “Ulimwambia namwita?” “Amesema atakuja wikiend.” “Basi kazi hiyo niachie mimi.” “Siamini kama atakusikiliza.” “Ngoja aje, nitajua mbichi na mbivu.” “Mmh, sina matumaini.” “Hebu kaoge nikupe michapo.” Nilikwenda kuoga ili nipate michapo ya Bi Shuu ambaye alinihakikishia kunipigania mpaka mwisho. Nini kitaendelea? Tukutane wiki ijayo. Mwisho wa wiki Mateja alikuja kuonana na Bi Shuu, alipofika waliingia kwa Bi Shuu. Nilikuwa na hamu ya kusikia alitaka kumuuliza nini juu yangu, nilijitahi kusikiliza dirisha la sebuleni la Bi Shuu lakini sauti walizokuwa wakizungumza zilikuwa za chini sikuweza kusikiliza waliyokuwa wakizungumza japo kuna muda nilisikia Mateja akisema. “Ilikuwa vigumu kuja kuyasema haya kwako, kwa vile mpaka anafikia umri alionao niliamini ni vigumu kubadilika.” “Mmh kama ni hivyo nina kazi nzito, naomba unipe muda vinaonesha chukuchuku havijaungwa.” “Hapana Bi Shuu nakuheshimu sana, lakini tumechelewa ungeniita mapema tungeweza kulipatia ufumbuzi. Sasa hivi nipo katika mipango ya harusi na kila kitu kipo katika hatua za mwisho,” kauli ile ilinikata maini. “Mmh, sawa nimekuelewa.” “Basi bibie wacha nikuache tutaonana,” nilimsikia Mateja akiaga ili aondoke. “Lakini naomba usimfukuze kazi mjukuu wangu.” “Bi Shuu suala la kazi haliingiliani na mapenzi, sitamgusa katika kazi hilo usihofu.” “Kama ni hivyo nashukuru, lakini Manka kapoteza dume la haja.” “Kila kitu mipango ya Mungu.” Nilimshuhudia Mateja akihesabu nyekundu tano na kumpatia Bi Shuu ambaye alishukuru nusra amlambe viguu Mateja kwa pesa aliyompa. “Asante bwana yangu,” Bi Shuu alishukuru. “Kawaida Bi Shuu ukiwa na shida mtume Manka usiogope.” Mateja aliaga ili aondoke, nilitoka haraka dirishani kwa Bi Shuu na kukimbilia chumbani haraka. Nilijikuta nikiangua kilio kutokana na niliyoyasikia nusu kwa Bi Shuu, niliamini nilikuwa nimechelewa kuyasikia ya mwanzo kuhusu tatizo langu. Niliamini kosa lilikuwa langu nilitakiwa nimueleze mapema Bi Shuu kuhusiana na mabadiliko ya Mateja. Kwa kauli ya Mateja kama ningewahi ningeweza kulikoa penzi langu. Nikiwa nimejiinamia kitandani nilikia nilishtushwa na mlango kugongwa. Nilijua ni Bi Shuu ambaye hakutakiwa kugonga, lakini sikutaka kumlazimisha nilipaza sauti yangu ya kilio. “Ingia mlango upo wazi.” Mlango ulifunguliwa macho yangu yalimshuhudia Mteja akiingia ndani mwangu baada ya miezi sita toka alipokata mawasiliano na mimi. Alikuwa wa kwanza kuniuliza baada ya kukutana na michirizi ya machozi kwenye mashavu yangu. “Vipi Manka unaumwa?” “Ndiyo,” nilidanganya kwa vile sikuwa na cha kumwambia. “Nini tena?” “Kichwa.” “Ooh, pole sana, umemeza dawa?” “Bado.” “Basi nyanyuka nikupeleke hospital.” “Kitapoa tu.” “Basi kama utazidiwa utakwenda hospitali.” Mateja alisema huku akinisogelea mkononi alikuwa ameshikilia pochi na kunikabidhi elfu hamsini huku akisema. “Kama utazidiwa zitakusaidia kwenda hospital.” Nilitaka kuzikataa zile pesa kwa vile shida yangu haikuwa pesa bali yeye mwenyewe. Nilitaka kumuuliza tatizo langu nini lakini niliamini nilikuwa nimechelewa nilitakiwa kuuliza mapema na si muda ule ambao alinionesha mpenzi wake mbele ya macho yangu. Nilipokea zile pesa Mateja aligeuka na kuondoka akiniacha nilikilia kilio cha kwikwi, baada ya kuondoka Bi Shuu aliingia na kunisimamia kama jini la kutumwa mkono kiunoni. “Manka kwenu hakuna unyago?” Lilikuwa swali la kwanza bila kujali kilio changu. “Unyago! Ndio nini?” “Mafunzo ya msichana kujitambua na jinsi ya kumridhisha mwanaume kitabia na kimapenzi?” “Sikuwahi kuyasikia.” “Mmh, ndiyo maana.” “Una maana gani kusema hivyo?” “Umepoteza wapenzi kwa kutojua mwanamke anatakiwa kumridhisha vipi mwanaume.” “Kwani kuna kitu gani amekueleza Mateja?” “Tutazungumza na kulifanyia kazi.” Baada ya kusema vile alitoka na kuniacha na mawazo kibao juu ya maswali yake na kitu alichoambiwa na Mateja. Nilijiuliza kutopata mafunzo ya usichana yanahusiana vipi na kukataliwa na wanaume. Nilijikuta nikijizoazoa hadi kwa Bi Shuu kutaka kujua Mateja kamwambia nini. Nilipofika nilimkuta akizurudia kuzihesabu pesa alizopewa na Mateja, aliponiona aliziweka pembeni na kunitupia macho. “Mmh, mwali una jipya gani?” “Bi Shuu naomba unieleze ulichopelezwa na Mateja juu yangu?” “Nitakueleza kwa vitendo si la maneno.” “Matendo! Una maana gani?” “Nimepata sababu ya wewe kukorofishana na wanaume, inaonesha wazi hukupitia mafunzo ya usichana. Nina kazi na wewe, mi ndo Bi Shuu bwana kila mwali aliyepitia mikononi mwangu kila aliyeonja hakutema. Najua wanakutema kwa vile unawalisha vya chukuchuku.” “Vya chukuchuku! Una maana gani?” “Utajua baada ya kuviunga kisha uwaonjeshe kama hukuolewa narudi kijijini kwetu japo toka nitoke kwetu kumebakia magofu. Lakini nakuhakikishia nakutia mikononi mwangu halafu nisikie, eti bwana bwana kaniacha,” Bi Shuu alishikilia pua na kusemea puani. “Nakwambia najua kuviunga vya chunguni mpaka vya mwilini, wala hujachelewa sasa hivi mtu akigusa amenasa.” “Utafanyaje?” “Nataka uombe likizo ya mwezi mmoja tena nitakuombea mimi kwa Mateja ili niviunge viwe vitamu.” “Vitamu! Vipi hivyo?” “Nataka ukiguswa usisimke, ujue mwiko upo katika chungu au upo juu ya mfuniko, kumpa mwanaume mpaka asuse. Usilale kama gogo uoneshe basi upo safarini na si kukapua macho kama kibaka akimvizia mtu.” “Mmh, mbona umeniacha njia panda.” “Leo nataka kumbadili Mchaga awe kama Mmakonde.” Mmh, kila alilozungumza kwangu lilikuwa geni, nilisubiri niungwe ili niwe mtamu kwa mwanaume. Niliendelea na kazi yangu huku moyo ukiniuma kulipoteza penzi la Mateja, na mpenzi wake kutaka sifa kila muda wa chakula cha mchana lazima ampitie na wakitoka walikumbatiana na kuzidi kuniumiza. Lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo. Wiki moja baadaye Bi Shuu alinituma nimwite Mateja, kama kawaida nilimfikishia ujumbe wake, naye hakuwa na hiyana alikubali wito. Ilikuwa ajabu katikati ya wiki Mateja kukubali kwenda kumsikiliza Bi Shuu, tena aliniomba nikitoka kazini niongozane nae. Baada ya muda wa kazi niliongozana na Mateja hadi nyumbani, tulipofika aliingia kwa Bi Shuu na kuniacha nikiingia chumbani kwangu. Nilijikuta nikijawa na mawazo juu ya wito ule Bi Shuu alikuwa na kitu gani ambacho alichomuitia Mateja. Niliamini kabisa kama kutaka kumrudisha kwangu itakuwa ngumu kutokana na kila kitu kujionesha juu ya Mateja na mpenzi wake mpya. Nilipofika ndani hata hamu ya kuvua nguo iliniisha na kujikuta nikitoka na kujipitisha jirishani ili nisikie alichoitiwa na Bi Shuu. Lakini sauti ya Bi Shuu ilinishtua kwa kuniita, moyo ulinishtuka kutaka kujua naitiwa nini? Niliingia sebuleni na kumkuta Mateja amekaa kwenye kochi akiwa ametulia. Bi Shuu aliponiona aliniambia. “Manka kwenye friji yako kuna soda?” “Mmh, jana nilimalizia nilikuwa na mpango wa kuweka leo.” “Basi nifuatie dukani.” “Bi Shuu si lazima achana nayo,” Mateja aliingilia kati. “Hapana babu lazima unywe soda.” Siku zote Mateja hakuwa na makuu alimkubalia Bi Shuu, baada ya kupewa pesa nilipitia chupa na kwenda dukani haraka ili niwahi mazungumzo yao. Nilipofika dukani nusra nipasuke kwa hasira baada ya kukuta wateja wengi kwenye duka la Mpemba. Sikutaka kusubiri nilikimbilia kwenye grosary iliyokuwa mbali kidogo. Nilinunua soda haraka haraka na kurudi hadi karibu na nyumba na kuanza kunyata hadi dirishani ili nisikilize wanazungumza nini. Nilipofika dirishani nilimsikia Mateja akisema. “Hakuna tatizo Bi Shuu kila kitu kitakwenda kama unavyotaka.” “Kama hivyo nitashukuru.” Baada ya mazungumzo yale palipita ukimya mfupi huku sauti za nyayo zikielekea mlangoni, nilichepua mwendo hadi mlangoni na kukutana uso kwa uso na Bi Shuu. “Vipi mwali mbona umechelewa?” “Dukani kwa Mpemba kumejaa watu ilibidi nisogee mbele kwenye grosary.” Bi Shuu aliipokea soda na kuingia nayo ndani, nilibakia mlangoni nikijiuliza niingie au niende chumbani kwangu. Kupata jibu la nifanye nini lilinifanya nisimame kwa muda pembeni ya mlango. Kabla sijapata jibu nilishtushwa na sauti ya Mateja. “Manka kumbe upo hapa?” “Ndi..ndi..yo,” maskini nilipata kugugumizi cha ghafla. “Wacha niondoke zangu.” “Haya, karibu,” nilijibu kwa aibu huku nikiangalia chini. Mateja kweli alinichoka bila kuongeza neno alinitipa na kuelekea kwenye gari lake, Bi Shuu alimsindikiza mpaka kwenye gari. Nilibakia nikimsindikiza kwa macho. Baada ya Mateja kuondoka Bi Shuu alirejea, alipofika alinishangaa kunikuta nimetawaliwa na simanzi usoni mwangu. “Vipi mwali?” “Aah, kawaida tu.” “Acha kujitia ukiwa, kila kitu kina wakati wake na wakati ndio unakuja.” “Kwani Mateja kasemaje?” “Aseme nini?” “Kwa hiyo amekubali?” “Akubali nini?” “Kwani ulimuitia nini?” “Kuhusu likizo yako.” “Kasemaje?” “Amekubali.” “Naanza lini?” “Sijajua lakini amekubali.” “Mmh, haya.” Niliachana na Bi Shuu na kwenda chumbani kwangu kujiandaa na kujimwagia maji ili nipumzike. ********* Siku ya pili nikiwa ofisini niliitwa na Mateja kunitaarifu kukubaliwa likizo yangu ambayo ingeanza wiki itakayofuata kwa kukamilisha kazi zangu zote muhimu. Nilipewa pesa ya likizo na kujiandaa kwenda kwenye unyago wa kiutu uzima ili niugwe niwe mtamu mwanaume akigusa anate. Baada ya kumalizia kazi za ofisi kwa wiki niliyopewa, niliruhusiwa kurudi nyumbani kuanza likizo. Nilirudi nyumbani na kumkuta Bi Shuu ambaye kabla ya kuweka makalio chini aliniuliza. “Mmh, umepewa likizo?” “Nimepewa.” “Basi kazi yote niachie mimi.” Siku ile nilipumzika bila kugusiwa kitu chochote, lakini alfajiri niliamshwa na kupelekwa kuogeshwa maji baridi kisha nilifungwa upande wa kanga bila nguo ingine ndani. Aliniongoza hadi katika chumba kimoja cha ndani kilichokuwa kitupu. Chini kwenye sakafu kulikuwa na maji kuonesha amemwagwa, baada ya kuingizwa mule ndani wakati huo kibaridi kilikuwa kikinichanyata. Bi Shuu alifunga mlango kwa nje na kuniacha nimesimama nikijiuliza ameleta mule ndani nifanye nini? Ajabu muda ulikatika nikiwa nimesimama, miguu ilichoka na kujiuliza mbona harudi ameniweka mule ndani ili iwe nini. Kukaa chini nilishindwa kutokana chini kuwa na maji na muda ule ubaridi kilikuwa kikali sana. Niliposhika mlango ulikuwa umefungwa kwa nje nilijaribu kuita kwani nilikuwa nimechoka kusimama zaidi ya saa moja. Hakukuwa na jibu la mtu yoyote. Nilijawa na mawazo juu ya kuwekwa chenye chumba chenye maji kisha kusimamishwa kwa muda mrefu. Nilijiuliza unyago wenyewe kama ndio ule kwangu niliamini nitashindwa. Niliamua kukaa kwenye maji huku kibaridi kikizidi kunichonyota, kutokana na uchovu nilijiegemeza kwenye ukuta na usingizi ulinipitia. Nilishtushwa na maji ya baridi niliyomwagiwa ndoo nzima, Bi Shuu alikuwa mbele yangu akiwa amekunja uso kwa hasira na kunifokea kwa sauti ya juu. “Haya ndiyo yanakufanya ukose wanaume kila kukicha, mwanamke mvivu kama nini, kukuacha muda mfupi umeshindwa kuvumilia na kuuchapa usingizi kwenye maji.” “Samahani Bi Shuu.” “Haya fanya usafi haraka,” alisema huku akinitupia tambara kukausha maji. Nilichukua tambara na kuanza kufanya usafi kwa kukamilia maji kwenye ndoo mpaka nilipokausha, Bi Shuu alirudi na mkeka ambao aliutandika kisha alitoka na kurudi na chai. Tulikunywa chai kisha aliniacha nipumzike kwa kuniacha na kipande cha kanga tu. Jioni ilipofika Bi Shuu aliingia ndani na kuniketisha kitako na kuanza kuniuliza maswali. “Manka kitu gani wakati wa mapenzi hukipendi?” “Mmh, vingi lakini tabia ya wanaume kunisumbua wakati wa kilimo huna sikupendi.” “Mmh, kingine?” “Ni hilo hilo tu.” “Nimekuelewa, kuna vitu vingi vya kike vimekupita kushoto, siku hizi wanaume hawapendi mwanamke anayelala kama gogo, husisimki wala hutingishiki.” “Bi Shuu nitikisike vipi au nisisimke vipi?” “Ndiyo maana leo umo humu ndani, ukitoka utajua unasisimka vipi na unatikisika vipi?” “Mmh, haya.” Mmh, hukuwepo ila malaika wako alikuwepo, sikujua alichonipa Bi Shuu kilikuwa adhabu au mateso. Niliwekwa mikao ambayo haikuwa tofauti na ile niliyokuwa nikiwakatalia wanaume, kila nilipotegea nilitandikwa bakora ya mgongo iliyotua sawia kwenye mgongo mtupu. Kila siku nilikuwa nikifanyishwa mazoezi yagumu ya viungo ambayo yalikuwa mateso mazito, kuna kipindi nilifikiria kumwambia bora aniache nilivyo kuliko mateso yale. Lakini Bi Shuu alikuwa mkali kama pilipili hakutaka mchezo hata kidogo hata nilipochoka bado alinilazimisha huku akisema. “Kushinda kuchoka ndiyo siri ya kumkata kiu mwanaume.” Nilibebeshwa mzigo kichwani nikiwa mtupu na kuanza kuchomwa na sindano kiunoni kitu kilichinifanya nishtuke kwa kuchezesha kiuno. Haikuishia hapo nililazwa chini na kubebesha mzigo kiunoni na kuendelea kuchomwa na kitu cha ncha ambacho kilinifanya nijinyonge nyonge bila kupenda. Niliendelea na mazoezi makali chini ya kungwi wangu Bi Shuu huku akinipa mbinu nyingi za kumchanganya kimapenzi mwanaume. Kuna mambo mengine siwezi kuyasema gazetini lakini Bi Shuu koma. Toka nizaliwe sikuwahi kukutana na mwanamke Shankupe kama yeye. Mtoto wa kike nilifundishwa maneno ya kusema mtu akiwa juu ya mnazi wangu, pumzi za kutoa wakati mwiko upo ndani ya chungu na akianza kugeuza maini nilitakiwa nilegee vipi huku macho na pumzi nizifanye vipi. Najua mwenzangu mie mwenye viuno kama vimefungwa mbao na wakati wa mapishi unatulia unasubiri mtu amwage mzigo akimaliza anyanyuke. Lakini ukikutana na bibi huyu lazima bwana akutaje jina. Mwezi mmoja mtoto wa kike nilipikwa nikapikika, baada ya mafunzo mazito Bi Shuu kwa ushambenga wake alinitafutia mwanaume ili kutaka kunipima baada ya mazoezi. Sikukataa kwa vile nilijua kile ndicho kipimo, mtoto wa kike nilijiandaa kuonesha kilichoniweka ndani kwa mwezi mzima. Cha ajabu Bi Shuu alitaka mchezo ule nichezee chumbani kwake, mmh, makubwa madogo yana nafuu. Sikutaka kumbishia kwa vile nilikuwa na usongo na mafunzo ya Bi Shuu ambayo yalinifanya nijiamini na kumtamani mwanaume nimtoe kamasi nyembamba. Baada ya kijana aliyechaguliwa na Bi Shuu kufika alikaribishwa chumbani kwa Bi Shuu, nilijikuta nikiwa na usongo na yule kijana ambaye alikuwa mmoja wa vijana walioninanga sijui kucheza nilipokutana naye siku ya kwanza. Baada ya kuingia ndani nilimpokea juu juu na kumtoa nguo maungoni kama kuku aliyechinjwa na kunyonyolewa manyoya. Baada ya kumuandaa mtoto wa kike huku mwili ukinisisimka baada ya kukiona kijiti cha kupokezana kwenye mbio fupi. Mtoto wa kike nikiwa nataka kufanya mtihani wangu wa kwanza kwa umakini mkubwa huku nikipitia hatua moja baada ya nyingine. Nilimlamba mwili mzima kama mama mbuzi akimsafisha mwanaye baada ya kumzaa, nilijua kutumia ulimi wangu. Nilipofika kwenye shina la mnazi mtoto wa kike nilitulia kwa muda huku vidole laini na ulimi ukifanya kazi yake. Mara nilimuona kijana wa watu akitetemeka kama amekunywa coka ‘ngriiiiiiiiii’, maskini kumbe alikuwa akilia chozi lisilo na msiba. Kijana wa watu naye akabadili upepo na kunirudishia mashambulizi. Mtoto wa kike nilipoguswa nililegea na kuzitoa pumzi huku jicho likipoteza kiini cheusi. Kwa mara ya kwanza niligundua kumbe mwili kila sehemu una raha yake kuishinda nyingine. Kama nilivyofundishwa na Bi Shuu kila nilipoguswa nilisema neno lake. Baada ya mshike mshike wa maandalizi cha chakula, hatimaye kiliiva na kutengwa mezani. Nilimpokea juujuu huku nilionesha jinsi gani mtoto wa kike nilivyoshikika, mtoto wa kike sikuwa na haraka nilifuata mwiko ulivyogeuza maini ili kumfanya mpigaji na mwimbaji wasitofautiane. Mtoto wa kike nilimaliza maneno yote mdomoni, sikuamini kutatalika kama bisi kwenye chungu cha moto. Mpaka mchezo unakwisha nilikuwa nipo hoi kwani niliamini vilikuwa vitamu kijana wa watu kila alipomaliza alileta sahani aongezewe. Nami nilimpakulia naye alijilia huku akigugumia kama dume la njiwa lenye wivu. Huku nikilia mara nne kwa utamu wa msiba. Lazima niseme ukweli kuna kipindi nilitaka kunyanyua mikono, maji yalikuwa shingoni, nyonga iligoma kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kuyakata mawimbi. Bi Shuu alinieleza kumfurahisha mwanaume si nyonga tu, hata kujua kuyapangilia maneno hasa kumsifia hakuna mwanaume kama yeye pia anajua kumshikisha punda adabu kwa kumtandika bakora balabala. Baada ya nyonga kugoma na kukiona kiuno kikiwaka moto, nilitumia sauti kumsindikiza mwenzangu mpaka alipofika juu ya mnazi. Kijana wa watu hakuamini ilibidi aniulize. “Manka, kumbe mambo unayaweza mbona ulikuwa uninikatili, mambo haya ungenipa tokea zamani sasa hivi ungekuwa mke wangu.” “Nilikulisha vya chukuchuku lakini sasa vimeungwa ndio maana unaviona vitamu.” Kijana wa watu bila kutegemea alinipa elfu 50 kama asante ya kumpa penzi tamu ambalo alikiri hakuwahi kulipata kwa mwanaume yoyote. Baada ya kuondoka na kuniacha nimejilaza baada ya kuhisi uchovu kila kona ya mwili kutokana na mshike mshike wa kufanya majaribio ya vitendo. Bila ya kujigeuza usingizi mzito ulinipitia juu ya kitanda cha Bi Shuu. Nilishtuka baada ya masaa matatu nikiwa nausikia mwili mchovu kila kona, Bi Shuu aliniamsha na kukuta ameniandalia maji ya kuoga. Nilioga kupunza uchovu na kurudi ndani ambako chakula kilikuwa tayari. Tulikula pamoja kisha tulipumzika sebuleni, cha ajabu niligundua Bi Shuu akiniangalia kwa kuniibia kitu kilichonifanya nimuulize. “Bi Shuu vipi?” “Kuhusu nini?” “Naona kama unanivizia kunitazama kuna nini si uniambie.” “Mmh, kweli ulikuwa na usongo.” “Wa nini Bi Shuu?” “Kazi umeifanya vizuri japo kuna kipindi ulichemsha.” “Ulijuaje?” “Nilikuwepo muda wote toka unaanza mpaka unamaliza, kwenye maandalizi nakupa mia kwenye sauti na pumzi sabini kwenye mchezo wenyewe hamsini.” “Jamani Bi Shuu kujitahidi kote unanipa hamsini.” “Manka kwanza nashangaa mtu ulikuwa hujui lolote umeweza kupata hamsini wengi huwa chini ya hapo.” “Bi Shuu kama nina hamsini nimeweza kupewa zawadi nikipata mia itakuwaje?” “Mia kupata ni kazi kwa vile maungo yako yalikakamaa muda mrefu lakini utaweza kufika hata sabini kwa bidii yako.” “Mapungufu yangu ni nini?” “Kutumia nguvu nyingi ambazo hukufanya upumue kwa kasi sana kitu kinachokufanya uchoke sana, pia papala ya kukata nyonga. Mwanzo uliweza kwenda sawa lakini ulipoanza kuchoka alifanya bora liende. Lakini mwanzo ni mzuri. Kwa uwezo wako huo na kuonesha ulikuwa makini kwa kuyashika mafunzo, inaonesha nikikuongezea matirio kama kwenye mpira ni ujanja wa kuweza kumsoma mwanaume. Kila mwanaume ana amambile tofauti na mwenzake na wengine wana nguvu kama kirafu unatakiwa kufanya nini.” “Bi Shuu nitashukuru nimeteseka sana, kwa nini sikuyapata mafunzo haya mapema ili kuweza kumdhibiti Mateja,” Nilijikuta nikidondosha chozi kulikumbuka penzi la Mateja nililolipoteza kutokana na kutokujua sheria za kitandani na kunifanya niendeshe ovyo na kusababisha ajali za kutoelewa alama za kitandani. “Manka usiwe kama kipofu aliyefumbua macho na kumuona chura na kuamini hakuna kama chura chini ya jua, mbona kuwa wanaume zaidi ya Mateja” “Bi Shuu ni kweli usemayo lakini Mateja niliamini ni mwanaume sahihi kwangu.” “Ni kweli, lakini kisicho riziki hakiliki we jipange ukikolea utamu nakuhakikishia nitakutafutia bwana Mateja cha mtoto. Kwanza nataka niyafanyie kazi makosa madogo madogo ambayo yatakufanya kila atakaye gusa atangaze ndoa. Nataka umlize mwanaume kama mtoto mdogo, umeisha ona mtoto akinyang’anywa ziwa jinsi anavyolia?” “Ndiyo.” “Basi nataka mwanaume chozi limtoke, kuna vitu vidogo wanawake hawajui, vitu hivyo ukimfanyia mwanaume kama ameoa lazima aitelekeze nyumba yake. Mchele mmoja lakini unatofautiana katika mapishi, hii nyumba jasho la mwili wangu pale nilipompata mume wa mtu. Leo hii naishi kwangu nawe nataka uwe mara mbili yangu.” “Bi Shuu mbona wasichana hatuna vitu hivi?” “Siku hizi uzungu umetawala na kujikuta wakipoteza vitu vingi vya kumfurahisha mwanaume. Kumfurahisha mwanaume kitandani si kigezo pekee cha kuilinda nyumba yako. Kuna vitu vingi ambavyo vipo nje ya kitanda. “Kuna wasichana wengi wana nyonga laini kama unakula keki lakini wana mapungufu kama chujui la nazi ambayo hayawezi kumfanya atulie kwa kwenye ndoa yake. Kama tabia yako nzuri ulichanganya na machejo ya kitandani hata utakita hata ndege utanunuliwa japo mwenzio hana uwezo wa kununua baskeri.” “Mbona hujanifunda na hivyo?” “Siwezi kukuichanganya kimoja kimoja, kwanza tunatengeneza mtego akiingia anase, ukimaliza mafunzo ya mwili tunarudi tena kilingeni ili mumeo aone tofauti ya magumegume na mwanamke.” “Bi Shuu mbona nimechoka sana.” “Umelia mara ngapi?” “Mara nne.” “Mara ya mwisho ulilia mara ngapi ulipokutana na mwanaume kabla ya leo?” “Mara mbili sijawahi kulia zaidi ya hapo.” “Ndio maana, lazima uchoke umeukamua mwili sana na shughuli haikuwa ya kitoto kuna kipindi kidogo nisimamishe mpambano mlikuwa kama mnataka kutoana roho.” “Bi Shuu umejuaje?” “Nikuambie mara ngapi nilikuwa nafuatilia toka mwanzo mpaka mnamaliza” “Jamani Bi Shuu kumbe ulikuwa unanipiga chabo,” Mbona niliona aibu mtoto wa kike, jamani bibi huyu ana mambo kumbe mwenzie nahenyeka yeye anapiga chabo. “Sasa ningejuaje mapungufu yako.” “Mmh, makubwa madogo yana nafuu.” “Na hayo mengine lini maana muda wa kurudi kazini umekaribia.” “Wiki iliyobakia inatosha, kapumzike jioni kama kawa mpaka kieleweke.” “Wacha nikalale naona mwili sio wangu, kwenye pesa hiyo chukua nusu niachie nusu” “Asante mwali, nina imani sasa umeamini nilichokisema kinatimia” “Wee mwisho Bi Shuu je, ungenikamata ndio unavunja ungo naona kila aliyenionja angeniganda kama ruba.” Baada ya mazungumzo nilimuomba Bi Shuu nikapumzike mwili ulikuwa na uchovu, nilikwenda chumbani kwangu kulala kwa kulifungulia feni mpaka mwisho mtoto wa kike nilijiachia kitanda kizima. ******* Kama kawaida Bi Shuu aliniamsha kwenye chakula cha mchana na baada ya chakula cha mchana nilioga na kupanda tena kitandani. Sikuamini mwili kuchoka kiasi kile, Bi Shuu alinieleza ni kutokana na kuzoea kulala kama gogo kitandani lakini siku ile niliushughulisha mwili hata kumwaga machozi manne kitu ambacho hakikuwa kawaida yangu. Nilipogusa kitandani usingizi haukuchelewa kunichukua, Bi Shuu aliniamsha saa mbili za usiku nilikwenda kuoga kisha nilipata chakula cha usiku. Baada ya chakula nilipumzika kidogo na kuingizwa unyagoni kumalizia muda ulipobakia kwa kunipa mbinu za kummiliki mwanaume kwa sauti na matendo huku tabia ikiwa ndiyo uliyochukua sehemu kubwa. Katika mafunzo siku moja alinipa nipike chakula baada ya kupika tulikula wote, kesho yake alinipa nipike tena chakula kilekile, lakini hakunipa chumvi. Nilipomuuliza alisema nipike vile vile na muda wa kula nilishindwa kumuelewa baada ya kunieleza nipakue, nilipakua na kukila bila chumvi. Tulikula wote bila kujua chakula kile kwa nini tulikila bila chimvi. Sikutaka kumuuliza kwa vile hakikuwa kingi tulikuwa na kukimaliza wote. Baada ya chakula usiku Bi Shuu akiwa ameniweka chini aliniuliza. “Manka kuna tofauti gani ya chakula ulichopika jana na leo?” “Tofauti yake cha jana kina chomvi lakini cha leo hakina chimvi.” “Kipi chakula kizuri?” “Cha jana.” “Kwa sababu gani?” “kina chumvi lakini cha leo hakina chimvi.” “Mbona umekila.” “Nilishindwa kuelewa ulikuwa na maana gani.” “Lakini bila hivyo usingekula?” “Nisingekula.” “Unajua nilikuwa nina maana gani?” “Hata sijui” “Hii nakuonesha yaisha ya ndani ya ndoa, wanawake wengi wanawalisha wanaume chakula kisicho na chumvi. Wapo wanaokosa uvumilivu huvunja ndoa lakini wanaoburuzwa na mapenzi hula chakula kisicho na chumvi kila siku na kuishia kunung’unika moyoni.” “Lakini Bi Shuu kama mkewe hamuwekei chumvi anashindwa vipi kuchukua mwenyewe kuweka kwenye chakula” “Swadakta swali zuri, ndio maana kukuweka huku ndani vitu vingi huvifanya kwa mafumbo jibu lake huwa ndio maisha yako ndani ya mahusiano yako. Chakula na chumvi sikuwa na maana hiyo bali kukueleza matatizo ndani ya nyumba nyingi wanawake wengi ndoa zao uziondoa chumvi bila wao wenyewe kujua” “Kivipi?” “Nyumba nyingi mwanzo wa mapenzi huwa moto moto kama kumpokea mpenzio akirudi kumtengea chakula kula pamoja kuoga pamoja kuwa karibu yake kumpoza uchovu wa kutwa nzima ambao ndiyo tiba ya mwanaume kutoitafuta faraja nje ya ndoa yake. “Wengi baada ya muda baadhi ya vitu hundoka kabisa na ndoa kuendeshwa kimazoea, moyoni lazima utasema hivi nisivyofanya kuna nini kwani hawezi kufanya mwenyewe. Kuacha kuyafanya hayo ni sawa kuondoa chumvi kwenye mahusiano yako na kumfanya mpenzio kula chakula kisicho na chumvi. “Wengi huvumilia na kuumia moyoni lakini wasio na uvumilivu huitafuta chumvi hiyo nje ya ndoa. Hapo ndipo tatizo linapoanza na kuipoteza ndoa yako bila kujua tatizo ni wewe mwenyewe. Kuondoa baadhi ya vitu ndani ya ndoa yako kama kutompokea mumeo au kutokula na kuoga pamoja ni vitu vinavyo mwanaume huona vya kawaida lakini ni ufa mkubwa katika ndoa. “Penzi halizeeki bali mwili ndio unazeeka, vyote nilivyokueleza usikipunguze hata kimoja ukiingia katika ndoa yako. Nakuhakikishia bwana atakaye kuoa watu watasema umemuwekea libwata, limbwata mwali ni kumlea mumeo kama mtoto. Nina imani umenielewa” “Mmh, kweli nimekubali Mungu kakujalia kumtengeneza mwanamke, nina imani ungenieleza kwa maneno ningekuelewa nusu lakini kwa vitendo nimekuelewa zaidi. Asante Bi Shuu” “Nashukuru kuonesha ni muelewa na mtu mwenye usongo na mafunzo” “Lazima Bi Shuu niwe na usongo nimeteseka sana” Nilimalizia mafunzo huku akilekebisha mapungufu aliyoyaona kwenye mtihani wangu wa kwanza.” Nilikuwa sijawahi kula kungu mtoto wa kike nilikula kungu jicho ukiniangalia utanionea huruma. Nilimaliza mafunzo salama, kabla ya kuanza kazi alinitafutia tena mwanaume mwingine naye alikuwa mmoja wa wale walioninanga mwanzo. Nilikuwa na imani alikuja akijua ni yule Manka wa mwaga msigo babangu kisha uondoke. Mafunzo niliyopata ya mwisho mtoto wa kiume chozi lilimtoka, kwenye maandalizi tu alilia zaidi ya mara tatu. Mtindo huu nilifundishwa kama sitaki kutumika sana kwanza namchosha mwanaume mwenye maandalizi. Hata ulipoingia baharini nusra anifie maji baada ya kushikwa na pumu katikati ya safari, machejo yalimfanya aifukuze Land Curuser VX kwa bajaj. Ilibidi niingie kazi ya kumpepea asinifie, baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida aliniangalia mara mbili. “Ni wewe Manka au naota” “Kwani vipi?” “Hata siamini, kumbe ulikuwa unafanya makusudi” “Ulikuwa vya chukuchuku sasa vimeungwa” ”Una maana gani?” “Si umeona mwenyewe si la kusimuliwa” “Nimekubali lazima nirudie” ”Mmh, cha kunifia kifuani hapa namefungulia injini moja katika injini nne si ungebadilika jina.” “Manka naomba nikuoe.” “Ni haraka sana vuta subra” “Lakini niwe mmoja wa watu wa mbele kufikiriwa.” “Hakuna tatizo” Yule kijana ambaye alikuwa kama mlevi aliniachia laki moja ya asante” Baada ya kuondoka Bi Shuu kama kawaida yake alitoa tathimini yake. “Mwali japo mpinzani wako hakuonesha upinzani lakini umejitahidi sana tena sana, sasa nina uwezo wa kukueleza kapambane na mtu yoyote. La muhimu kuzingatia niliyokueleza hakika kila atakayehusa lazima anate sasa hivi mwili wako ni asali yenye ulimbo” Maneno ya Bi Shuu yalinifanya nijiamini nimeanza kuiva kimapigano, kwa vile muda ulikuwa umekwisha jumatatu ilipofika nililipoti kazini kwangu. Nilimkuta aliyekuwa amenishikia, baada ya kunipokea alinielekeza kazi za kufanya na yeye kuendelea na majukumu mengine. Kuna kitu kimoja nilisahau kukueleza baada ya kukaa ndani kuchezwa nilipotoka nilitakata na kunawili mtoto wa kike. Nikiwa naendelea na kazi bosi wangu dear zilipendwa aliingia ofisini, ilionesha hakujua kama naanza kazi siku ile. Alipofika hakuniangalia alinisalimia. “Za saizi?” “Nzuri” “Ile kazi tayari?” “Ndiyo namalizia” ’Baada ya muda gani” ”Dakika kumi” “Ok, fanya haraka.” Baada ya kusema vile aliingia ofisini kwake, ilionesha hakujua kama nipo mimi. Baada ya kumaliza kazi niliyoikuta niliprinti na kumpelekea, alikuwa bado ameinama nilipofika mbele yake nilisema. “Bosi kazi tayari” Sauti yangu ilimshtua na kunyanyua macho, kwa mshangao wa ajabu alisema. “Ha! Manka umekuja saa ngapi?” “Toka asubuhi” “Ina maana nimekupita kwenye ofisi yako?” “Ndiyo bosi” “Ooh, samahani sana” “Kawaida tu bosi wala usijisikie vibaya,” mtoto wa kike nilikuwa nimekwenda kimitego na kumuomba Mungu Mateja ajichanganye sijui aonje kidogo. Niliapa ningefanya aliyofundishwa na mengine nisiyo yajua ili kuhakikisha anakutana na vitu vipya katika medani ya mapenzi. Mtoto jicho lilikuwa limelegea kidogo jicho lilionekana kwa kujipaka wanja chini na juu na kuongeza uzuri wangu. Japo nilijijua mi mzuri, lazima mzuri ujijue kabla hujasifiwa na watu, lakini mapungufu yangu Bi Shuu aliyamaliza mengi niliyokuwa nayo. Mateja ilionekana kama kuchanganyikiwa kuniona nimebadika nimependeza na ninavutia tena kimitego ya kike hasaa. “Manka ulikuwa unakula nini?” “Kwa nini bosi?” nilimuuliza kwa sauti laini huku nikimchanulia tabasamu ya kufa mtu huku jicho nalo likizungumza. “Hapana, umependeza na unavutia” “Nashukuru kwa hilo ila moja umesahau” “Lipi hilo?” “Sasa hivi si Manka chukuchuku ila Manka huyu kaungwa akaungika” “Una maana gani?” “Bosi nitakuomba kesho nikukaribishe chakula cha usiku” “Mmh, hakuna tatizo kwa vile wiki hii ni ya mwisho baada ya hapo nitakuwa katika maandalizi ya harusi.” “Hakuna tatizo kazi njema.” “Na wewe pia.” Baada ya kumkabidhi kazi yake nilirudi kuendelea na kazi yangu, moyoni niliapa kama kweli atakubali mwaliko wangu amekwisha.Muda wa mchana Mchumba wake alimuijia kama kawaida na kwenda naye kupata chakula cha mchana. Japo moyo uliniuma lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo kutokana na makosa kuyafanya awali. Jioni niliporudi nilimueleza Bi Shuu mwaliko niliompa Mateja kuja kula chakula cha usiku. “Mwali akiingia amekwisha, hakikisha anaisahau ndoa yake” “Bi Shuu la kuuliza hilo” “Nakuaminia mtu wangu.” “Naiona kama kesho inachelewa” “Itafika punguza munkari, usije yakakamia maji” “Si hivyo Bi Shuu nakuhakikishia kuyafanya yote kwa umakini mkubwa labda asije.” ***** Siku ya pili nilikwenda ofisini na kuendelea na kazi bosi alipokuja alinisalimia. “Mrembo hujambo” “Sijambo bosi simshindi wifi” “Manka mbona umefika mbali salamu umeijibu sivyo” “Samahani bosi, za nyumbani” “Mmh, salama sijui zako.” “Nami namshukuru Mungu, haya nipo ndani” “Sawa bosi” Kabla ya kuingia ofisini aligeuka na kuniuliza. “Mwaliko wa usiku upo vile vile au kuna mabadiliko” “Hakuna mabadiliko” “Haya,” alisema huku akifungua mlango na kuingia ofisini kwake. Baada ya kuingia ofisi nilibaki nilikuwa siamini kama nimesikia vizuri kuulizia mwaliko, niliona dalili njema zimeanza asubuhi jioni ni kumalizia tu. Huwezi amini siku hiyo nilifanya kazi kwa furaha ya ajabu kama Mateja amenikubali nirudiane naye. Jioni kabla ya kuondoka aliniaga na kuniahidi angekuja usiku. “Kweli Mateja utakuja?” “Kama siji ningekuambia” “Karibu sana mpe..” Mungu wangu nilitaka kujisahau kumwita mpenzi wakati tuliisha achana long time a go. “Niite tu mpenzi wala usijisikie vibaya,” “Hapana bosi” “Haya baadae” Mateja aliondoka na kuniacha nikipanga vizuri vitu vyangu kabla ya kurudi nyumbani. ********* Nilkipofika nyumbani Bi Shuu aliniomba siku ile aandae chakula cha mgeni, sikuwa na hiyana mtoto wa kike nilimuacha afanye mambo yake. Nilikiandaa chumba changu na kukiweka katika hali ya usafi wa hali ya juu, kama kawaida Bi Shuu alinipatia mafusho ya manukato mazuri. Baada ya kuhakikisha chumba changu kinapendeza niliingia kuoga mtoto wa kike na kujifusha utuli huku nikipaka wanja wa sina mume ambao lazima mwanaume barabarani akusalimie. Baada ya kusimama mbele ya kioo kujitathimini, nilizidi kujisifia mtoto wa kike kwa upendeleo niliopewa na mwenyezi. Baada ya kuhakikisha nipo sawa, nilikunywa kungu na kuanza kujisikia nikisisimka mtoto wa kike kama mamba mwenye njaa. Nikiwa nimekaa mkao wa kula kumsubiri Mateja, mara aliingia Bi Shuu na kuniongezea mambo fulani ya muhimu pindi Mateja akiingia chumbani kwangu. “Mwali nilitaka kusahau kwa vile anajua anakuja kula chakula na kuondoka cha kufanya akiingia tu, ukimvamia kwa kumkumbatia huku akimbusu hakikisha mikono yako inafanya kazi ya haraka kumvua nguo bila kuchelewa mpatie upande wa kanga. Wakati huo mimi nitakuwa tayari nimepeleka maji ya kuoga bafuni niliyoyawekea viungo. Nani alikuambia wanawake wa Tanga ndio wanajua mahaba, nataka Mateja akiondoka kila kitakachokuja mbele yake akione shombo.” “Nimekuelewa Bi Shuu.” “Sio umenielewa bahati hairudi mara mbili, itumie kubadili matokeo.” “Matokeo ya nini Bi Shuu?” “Ukimaliza kilicho tupotezea muda nitakwambia.” “Nitafuata maelekezo yako.” Baada ya kutoa maelekezo Bi Shuu alirudi kumalizia kutengeneza maajumati ya mgeni rasmi. Majira ya saa moja na nusu gari la Mateja lilisimama mbele ya nyumba yetu, ajabu usongo wote niliokuwa nao uliyeyuka kama donge la mafuta katika kikaango cha moto. Nilijikuta nikijawa na hofu juu ya nilichokipanga kumpa Mateja kama ataingia katika mtego wangu. Nilijihisi kupoteza ujasiri niliokuwa nao kabla ya Mateja hajaja, niliikandamiza mikono yangu kifuani na kubana pumzi na kukaa kwa muda kuvuta ujasiri kisha niliitoa na kushusha pumzi nzito. Baada ya kujipa ujasiri nilijitengeneza haraka haraka ili kujiweka sawa japo nilikuwa nimejiweka kimitego ya kike hasa. Ndani nilivalia kufuri la bikini la rangi nyekundu juu nilivalia kanga nyepesi ukituliza macho unaona kila kitu cha ndani. Wakati huo chumba kilikuwa kikinukia utuli kila kona mimi mwenyewe nilikuwa kama Hululaini malaika wa daraja la juu. Jicho mtoto lilikuwa lemelegea kwa kungu huku mwili ukisisimka kama nyoka mwenye hasira aliyepandisha sumu kwa ajili ya kumgonga mtu. Wakati nikifanya matayarisho ya mwisho kabla ya kumpokea Mateja mbele ya kioo, Bi Shuu muda huo alikuwa amempokea. “Wawooo mwanaume huyo.” “Niambie kipenzi changu?” Sauti ya Mateja ilisikika. “Niseme nini mkeo nawe umetupa jongoo na mti wake.” “Bi Shuu kama ningetupa leo ningeonekana hapa?” “Mateja kula nisishibe heri nisipewe.” “Bi Shuu heri nusu shari kuliko shari kamili na kidogo si haba kuliko kukosa kabisa.” “Nitakuwezea wapi mtoto wa Kisukuma aliyejifanya Mzaramo kwa kujifanya unajua kuyageuza maneno.” “Vipi nimewakuta?” Mateja aliuliza mimi ndani kiroho paa! “Umewakuta wamejaa tele wewe tu,” mmh, maneno ya Bi Shuu yalijaa nahau na misemo na kuzidi kuniweka njia panda. Wakati nikijua hodi itapigwa wakati wowote nilipandisha tena pumzi na kuzishusha kisha nilijiandaa kumpokea. Mara mlango uligongwa. “Hodi ndani?” “Karibu,” nilimkaribisha huku nikikaa mkao wa chura kuruka. Mara mlango ulifunguliwa na Mateja aliingia, mtoto wa kike nilijizoazoa na kumkumbatia. “Ooh, karibu mpenzi.” “Asante za hapa?” “Nzuri.” Mtoto wa kike niliutambaza mdomo wangu na kutua kwenye mdomo wa Mateja ambaye alikuwa bado amepigwa na butwaa, nikihema kama mgonjwa wa pumu. Mateja alinipokea na kubadilishana mate, mikono yangu alipata nafasi ya kumvua shati. Baada ya kumvua shati nilimsukumia kitandani na kumlalia juu, kwa haraka nilimalizia na vilivyokuwa vimebaki chini kisha nilimpatia upande wa kanga. Kila nililolifanya siku ile kwa Mateja kilikuwa kigeni kwake niliamini alijua bado Manka wa mwaka 47 hohehahe asiyejua chochote. Niliamini muda huo Bishuu alikuwa ameisha peleka maji yaliyochanganywa na viungo bafuni. Nilimshika mkono Mateja na kutoka naye nje kumpeleka bafuni kuoga, Bi Shuu kweli alikuwa amepania mlangoni nilikuta kuna ndala mpya. Mateja alivaa na kuongozana naye hadi bafuni. “Karibu mpenzi uoge.” “Asante.” Nilimwacha Mateja bafuni na kurudi ndani kujiandaa kumlisha vilivyoungwa na Bi Shuu. Kabla sijaweka tako chini Bi Shuu aliingia bila hodi na kusema kwa sauti ya juu. “Wee mwana, ndio unafanya nini?” Kauli ile ilinishtua sana. Kutokana na makosa ya kuruka baadhi ya sehemu katika hadithi ya wiki iliyopita kufikia hatua ya kuwachanganya wasomaji. Leo tutaelezea kwa ufupi toka Mateja alipomuona Manka ofisini mpaka kufikia hatua ya kumsubiri chumbani. Baada ya Mateja kushtuka kumuona Manka jinsi alivyopendeza kwa muda ambao hakuwepo kazini alimsifia kuwa amependeza mara dufu. Naye Manka alitumia nafasi ile kumkaribisha Mateja chakula cha jioni kwake. Mateja alimkubalia na kumuahidi angefika jioni kwa ajili ya chakula. Manka aliporudi nyumbani alimueleza Bi Shuu kuwa Mateja amekubali kuja kula chakula cha jioni. Bi Shuu alimueleza asiipoteze nafasi ile adimu ahakikishe kama atakubali kuvila vilivyoungwa basi achanganyikiwe. Bi Shuu alimuomba kazi ya kupika chakula aifanye yeye ya kuandaa chakula cha ujanani kwake pale alipokuwa akimtengenezea mpenzi wake. Baada ya makubaliano na Bi Shuu Manka aliingia ndani kujiandaa kwa ajili ya kumpokea Mateja kwa kufanya usafi wa mwili na chumba huku akifusha udi na asumini kumwagia kitandani. Yalikuwa mafunzo tosha ya Bi Shuu ambayo Manka aliyafanyia kazi. Baada ya kila kitu kuwa tayari Manka alimsubiri kwa hamu Mateja mpaka alipofika. Baada ya kumuandalia maji na kumuacha aoge peke yake ndipo Bi Shuu alipomfuata na kumuuliza amefanya nini. Ili kujua kosa lake nina imani mpaka sasa tupo pamoja, haya tuserereke pamoja… Kauli ya Bi Shuu ilinishtua na kujiuliza nimefanya kosa gani tena. “Bi Shuu nimefanya nini?” “Manka haya ndiyo makosa mnayafanya sana wanawake wengi, kwa nini umuache aoge peke yake. Nenda kaoge naye ikiwezekana anza kumliza kilio cha raha bafuni.” Mmh, mtoto wa kike haraka nilitelemsha nguo ya ndani na kubakia na upande wa kanga nyepesi na kumuwahi Mateja kabla hajajipaka sabuni. Nilipokaribia bafuni Mateja alikohoa kumaanisha kuna mtu. “Mm..mm..mmh.” Nilisukuma mlango na kumkuta amejipaka sabuni usoni, alipofumbua macho aliniona nipo mbele yake. “Aah, kumbe wewe?” “Ulidhani nani?” “Nilifikiri kuna mtu kaingia kwa bahati mbaya.” “Nilikwenda kutoa nguo ili tuje tuoge wote,” nilidanganya. “Sasa mbona hukuniambia kama tunaoga wote uliondoka kimya kimya.” “Nilijua nakuwahi.” “Haya tuoge.” ITAENDELEA ... Read More
HOUSE GIRL DIARY; NAITWA RAYA NI HOUSE GIRL MSTAAFU—SEHEMU YA TATU (ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI; Raya anarekodi Video ikimuonyesha yule Mama akimtesa mtoto wake wa kambo, akimpiga na kumfanyisha kazi. Anamkabidhi Baba Jack ili aone kinachoendelea. Je nini kitatokea ENDELEA.. Kama hujasoma sehemu ya pipi basi bonyeza hapa; Iddi Makengo Dada alimuona namna Baba anavyobadilika, namna ambavyo uso wake alikua anaukunja, ghafla nilimuona Baba machozi yanamtoka, nikitegemea kama atapandwa na hasira kama nillivyokua mimi na kuanza kumtandika Dada makofi niliona anamgeukia taratibu, alimuangalia kwa uchungu kama vile alikua anataka kusema kitu lakini maneno hayatoki. “Ni…ni nini hiki?” Alijitahidi kuuliza, wakati huo Dada alikua kimya akiangalia chini kwa aibu. “Nisamehe mume wangu ni hasira tu, huyu mtoto wakati mwingine ananiudhi nalazimika kumpiga…” Alijitetea. Mimi bado nilikua nashangaa ni kwanini Dada hakua amelala chini akitokwa damu kwa kipigo. “Hasira ndiyo unwe unampiga mtoto namna hii, hizi ni hasira gani?” Hapa Baba aliuliza kwa hasira kidogo, nilipata faraja labda atamtandika makofi lakini haikutokea. Dada alianza kulia, “Hata mimi sijui mume wangu, sijui hata nini kilinitokea siku hiyo nikampiga mtoto, mimi sina mkono wakupiga kabisa, wewe mwenyewe unanijua labda ni hii mimba…nikiwa katika hali hii nakua tofauti sana…” “Muongo, ni kila siku anampiga, hata haya anayoita mapele ni yeye. Hata chakula anamnyima, anamtukana, anamfanyisha makazi kama Mbwa, huyu si mwanamke ni shetani!” Niliongea huku nikinyanyuka kwa hasira, Baba alikua kama zezeta flani hivi, baada ya kutajiwa neno mimba ni kama alisahau kuwa yule mwanamke alikua ni shetani. Nilikua nasikia mambo ya limbwata lakini nilikua sijawahi kuona mtu kalogwa akalogeka. Kwa namna ile video ilivyokua mtu yeyote mwanye akili timamu hata kama asingekua mzazi wa Jack angekasirika na asingemsikiliza yule mwanamke. “Una mimba mke wangu, ina miezi mi ngapi? Mbona hukuniambia?” Alisahau kabisa kuhusu Jack na kuanza kuulizia upuuzi mwingine ambao nilijua kabisa ni uongo. “Hakluna cha mimba wala nini, hivi wewe huoni kama anataka kukuchota akili!” Niliongea kwa hasira, pale nilikua kama mfanyakazi ila kwa wakati ule nilijua kazi sina hivyo ilikua ni lazima kumtetea Jack na kuhakikisha haki inatendeka. Nilipiga kelele na harakaharaka nilitaja karibu kila kitu ambacho mimi nilikishuhudia Dada akimfanyia Jack. “Mume wangu unaona, huyu binti ndiyo sababu ya kila kitu. Hataki kufanya kazi, nyumba ikakua chafu na kamjaza mwanao kiburi, mbona kabla ya kuja tulikua tunaishi salama. Jack namfundisha kazi na ananisaidia kufanya kazi za ndani, kwa hali yangu hii siwezi kufanya chochote, wewe mwenyewe unakumbuka kilichotokea kipindi kile. Unajua namna tulivyohangaikia huyu mtoto, hivi kweli kumfundisha mtoto wa kike kazi za nyumbani ni kosa? Au kumchapa akikosea ni kosa? Au kwakua mimi sina kazi nipo hapa nyumbani, au kwakua mimi ni Mama wa kambo ndiyo mnaniona kama shetani. Huyu binti anajazwa maneno na Mama yake, kila siku wanaongea na ndiyo wanataka kutuvuruga. Mimi siwezi, mimi siwezi kama umenichoka niambie tu niondoke zangu!” Aliongea huku akilia, kila kitu kilikua ni uigizaji, wakati anaongea alianza kunyanyuka, alinyanyuka huku akishika tumbo kama vile ana maumivu tumboni. “Nini? Kuna nini kimetokea, tumbo linauma?” Baba alimuuliza lakini hakujibu zaidi ya kumuambia niache kama umeamua kumsikiliza huyo baki naye mimi naondoka. Alinyanyuka kwa kupepesuka kisha taratibu alidondoka chini. Niliona kabisa kafanya makusudi kwani hakudondokea sakafuni, alipiga jicho pembeni kisha akapepesa macho na kudondokea kwenye sofa, akawa kama kakaa kiupende kisha ndiyo akafika chini. Baba alipaniki, alianza kuhaha, simu alitupa pembeni na kuacha kuangalia, watoto wake nao walikuja kulia na kumlilia Mama yao. Ilikua ni kama maigizo flani, Baba alianza kuongea habari za Hospitali ndipo alijifanya kufungua macho na kulazimisha kupelekwa chumbani. Aliniambia nimsaidie kumnyanyua lakini sikua tayari, nilimshika Jack mkono na kuondoka naye mapaka chumbani, nilimuacha Baba akihangaika kumnyanyua ili kumpeleka chumbani, alisahau kabisa ishu ya mwanae. **** Usiku mzima sikulala, nilijua nafukuzwa lakini suala la kumuacha Jack pale halikuingia akilini. Nilimuambia Jack nimpeleke kwa Bibi yake lakini alikataa katakata. “Watakuja tu kunichukua, hata nikisema nini hakuna mtu wa kunisikiliza. Wewe dada ondoka tu uniache hapa, nimeshazoea kila dada anayekuja anachoka na kuondoka mimi naendelea tu kubaki. Baba hawezi kuruhusu niondoke, alishagombana na Bibi mara nyingi lakini anasema ananipenda na hawezi kukaa mbali na mimi. Kumbe sikua mimi peke yangu niliyeona yale mateso na kukerwa nayo, kulikua na wafanyakazi wengine wawili nyuma ambao walishafukuzwa kwaajili ya Jack ndiyo maana alikata tamaa. Mmoja alisema kwa Bibi yake Jack na mwingine alimpa chakula na alikua anawasiliana na Mama yake Jack. Asubuhi Baba aliamka kama kawaida, ni kama kulikua hakuna kitu kilichotokea, Dada alijifanya kuamka na kumuamsha Jack kwaajili ya shule, alijidai kumuandaa na kujifanya hana kinyongo. Waliwaaandaa na kuwapeleka shule, alipoondoka tu Dada aliniambia nikusanye kila kilicho changu na kuondoka. Alinitukana sana kwa kutaka kuingilia nyumba yake akiniambia kuwa pale hawezi kuondoka. Alitaka kunipiga lakini kwakua sikuwa nikihitaji kazi tena na nilishajua siwezi kubaki tena pale kumlinda Jack niliamua kumtolea hasira. Baba alishaondoka kwenda kazini hivyo tulibaki wawili tu, pamoja na mwili wangu mdogo lakini nilipitia mengi, maisha ya kupigana mtaani nilishayazoea. Nilimsubiri aliponipiga kofi la kwanza na la pili. Nilimuacha anogewe ndiyo nikaanza kumtandika, hakuamini. Nilimtandika kama vile mtoto mdogo, nilimpiga sana akapiga kelele lakini hakukua na mtu wa kumsikia. Baada ya hapo nilichukua kilicho changu na kuondoka. Nilimuambia naondoka lakini nitarudi, nitarudi kwaajili ya Jack. Alinyamaza kimya bila kusema chochote. Kumbe mtu mwenyewe alikua mayai mayai halafu anajifanya kuonea watu. Niliondoka na kwenda kwa kijana mmoja, huyo alikua ni X wangu, tulizinguana kitambo kabla sijaacha kazi nilipokua nikifanya mwanzoni, yeye alikua ni Kondakta wa daladala hivyo mchana alikua kazini. Mlango wake nilikua naujua vizuri hivyo niliufungua hata bila funguo. Sikua na pakwenda kwani sikua na ndugu Dar, ingawa sikuachana naye vizuri lakini nisingelala mtaani. Jioni alirudi na kunikuta, hata hakukasirika, alianza kucheka na kunitania kama siwezi kuishi bila yeye. Nilimuambia ishu yangu, nikamuonyesha ile video katika simu yangu, hata yeye pamoja na Bangi zake hakuamini kama kuna mtu anaweza kufanya vile tena kwa mtoto mdogo kama yule. “Huyo mwanaume kashatengenezwa, cha kufanya hapo ni kwenda Polisi, mbona siku mbili huyo akikaa ndani anakaa sawa…” Aliongea huku akinigusa, najua alitaka mapenzi lakini sikua katika mood kabisa, ila aliongea jambo amaalo sikuliwaza kabisa hapo awali. “Baba yake anaweza asijali lakini sidhani kama Polisi hawatajali.” Niliwaza kufanya hivyo lakini ulikua ni usiku, niliamua kusubiri mpaka asubuhi. Lakini niliwaza kama itakua vizuri nikienda na Jack kwani nilijua kuwa wakiangalia makovu yake basi utakua ni ushahidi tosha na watamuonea huruma. Lakini ningempataje wakati yuko shuleni, niliamua kwenda nyumbani kwao kumsubiri wakati anatoka shule. Wakati wanashushwa na gari kabla ya kuingia ndani nimchukue na kuondoka naye. Mchana muda wa wao kutoka shule nilichukua Bajaji, nilimuambia Dereva kupaki karibu na geti kabisa, Gari la shule lilipokuja na kuwashusha nilishuka na mimi. Wote waliniona, wale wengine walikimbilia ndani lakini Jack ambaye alikua anaogopa alisimama na kuniambia niondoke kwani atapigwa. Sikumsikiliza wala sikusubiri kumuelezea. Nilimshika na kumvuruta mpaka kwenye Bajaji, nikamuingiza kwa lazima kisha nikamuambia Dereva tuondoke. Kwakua nilishamuambia kila kitu aliwahsa Bajaji mpaka kituoni. Kule nilienda mpaka mapokezi, hakukua na watu wengi, nilianza kuelezea kila kitu, nikawaonyesha na Video. Kila askari aliyeiona alikasirika, tulipewa askari wa kike ambaye alienda kumkagua Jack. Alikua ni Mama mtu mzima, wakati anamkagua alianza kutokwa na machozi ingawa alijizuia sana. Mwanzoni Jack alikataa kusema lakini baada ya kuhakikishiwa usalama wake lielezea kila kitu. Niliandikisha maelezo kisha tukapewa PF3 ili akatibiwe, askari mmoja alitupeleka hospitalini na gari yake binafsi. Baada ya hapo ilitolewa RB, Dada na Baba wote walikamatwa na kufikishwa kituoni. Wote walikua na kesi, haikua ni ya mtu mmoja tena. Polisi waliwasiliana na ndugu wengine kwaajili ya kumchukua Jack na kukaa na wale watoto wengine kwani wote hawakupewa dhamana. Mimi niliondoka lakini nilikua naenda Hospitalini kumuangalia Jack mara kwa mara. Alilazwa kupatiwa matibabu kwa muda wa wiki moja hivi, Mama yake alikuja na baadaye kukabidhiwa mtoto wake. Baba na Dada walikaa mahabusu kwa wiki moja na kutoka kwa dhamana lakini cha kushangaza hawakupelekwa mahakamani. Sijui nini kilitokea lakini binafsi naamini walitoa pesa nyingi kwani Baba Jack alikua na pesa na kacheo flani. Kesi iliisha chinichini na mimi sikuweza kufuatilia, baada tu ya Jack kurudi na kukabidhiwa kwa Mama yake kwangu hilo lilitosha hayo mengine yalikua hayanihusu. Hela yenyewe ya kula ilikua ni shida nisingeweza kufuatilia maisha ya wengine. Sasa hivi imepita kama miaka miwili hivi tangu hili tukio litokee, nipo hapahapa Dar lakini nimehama mtaa. Sifanyi tena kazi za ndani, nimefungua Genge langu ambalo nauza mbogamboga na matunda. Bado nawasiliana na Jack kupitia Mama yake na anaendelea vizuri, wanaishi maisha ya kawaida sana lakini yenye furaha. Katika kazi yangu hii ya kuuza Genge wateja wangu wengi ni wadada wakazi ‘House Girl’ mengi wanayokutana nayo katika nyumba za watu ni kubwa. Kwa wa mama ambao ndiyo mabosi wetu kumbukeni hata sisi ni wanadamu kama nyinyi. ***MWISHO MAMA KWANI BABA YETU NDIYO HUYU HUYU AU SISI NI MAYATIMA? Baba yao ndiyo alikua na kila kitu, mali zote zilikua za kwao lakini kila akisafiri walikua wakiishi kama mashetani, Shangazi zao na Baba zao wadogo waliungana kuwachukia, Mama yao alikua akinyanyaswa na kutukanwa. Kila siku walimuambia yeye ni mzigo na hawezi kuchukua mali za Kaka yao. Bibi yao ambaye alitegemewa kuwa upande wao naye walimjaza maneno. Walimuambia huyu mwanamke kama Kaka akimuacha watagawana mali na Kaka akifa basi atachukua mali zote. Kilichopo hapa ni kuhakikisha Kaka hawi na kitu chochote cha yeye kuchukua…. JE UNATAKA KUJUA KISA HIKI KINAHUSU NINI…Kama kisa kilichopita kilikutoa machozi hiki kitakupigisha mayowe… Lakini nacho kimetokea niseme kinaendelea kutokea, unaweza kuwa na mali nyingi na wanao wakaishi kama mashetani hata kabla hujafa. Kama unataka kuwa wa kwanza kukisoma basi hakikisha umelike ukurasa ... Read More
Story - - - - - NI WEWE TU PENINA. BY GIVAN IVAN PHONE & WHATSAPP____0769673145 Karibuni tuianze story yetu hii mpya yenye kusisimua iliyojaa visa mbali mbali kuhusu mapenzi. Sehemu ya kwanza (1) Mapenzi ya vijana wawili walionza kupendana toka wakiwa wadogo mpaka Sasa wakiwa na umri wa miaka 25 kila mmoja, yalikuwa yakizidi kukolea kila siku na kuwa matamu zaidi na zaidi. Vijana Hawa ni Frank pamoja na Penina. "nahisi kuvurugwa nahisi kufa kufa yaani najiona kama napepea juu juu kwa jinsi navyompenda mpenzi wangu Penina." alikuwa frank akiongea maneno hayo mbele ya wazazi wake pamoja na mdogo wake Wa kike aitwaye Angel. "na siku si nyingi utakuwa chizi wewe sio kwa kupenda huko kaka yangu." akaongea Angel kumuambia Frank. "acha niwe chizi tu mdogo wangu, lakini sio chizi wa kutembea uchi barabarani bali chizi wa kupenda." akaongea Frank maneno hayo na kuwafanya wazazi wake wacheke sana. "lakini mwanangu Sasa inabidi mfanye taratibu mfunge ndoa Sasa." aliongea baba yake Frank. "Hamna shida baba usijali yote hayo yatafanyika muda mfupi ujao. " Akaongea Frank ambaye muda wote furaha ilijaa usoni mwake. *wakati huo huo Penina mpenzi wake Frank naye alikuwa katika moja saloon akitengeneza nywele zake ikiwa ni maandalizi ya kwenda kukutana na mpenzi wake Frank. " Dada nitengeneze vizuri tafadhali maana napenda muda wote niwe navutia mbele ya mpenzi wangu." aliongea Penina kumwambia mwanadada aliyekuwa akimtengeneza nywele. "usijali dada nitakutengeneza vizuri mpaka mwenyewe ufurahi." Dada yule akamjibu Penina na kumfanya atabasamu. Baada ya dakika kadhaa Penina alimaliza kutengenezwa nywele zake na moja kwa moja akazama kwenye pochi yake na kutoa simu yake, kisha akatafuta Jina lililoandikwa my love Frank na moja kwa moja akazipiga namba hizo. * Frank akiwa bado anaongea na wazazi wake ghafla simu yake ilianza kuita, akatoa na kuangalia mpigaji ni Nani. Frank alianza kutabasamu baada ya kukuta mpigaji ni Penina kipenzi cha moyo wake. "haloo mke wangu mtarajiwa mambo vip?" akaongea Frank baada ya kupokea simu. "poa tu mpenzi wangu nimekumiss hadi nahisi kizunguzungu." akajibu Penina. "Asante mpenzi wangu yaani kuachana Jana tu ndio kunimiss hivyo?" " yeah nimekumis sana hebu jiandae nakupitia Sasa hivi tukale bata kidogo. " akaongea Penina kumwambia Frank. " waoow ok najiandaa Sasa hivi utanikuta tayari my love." akajibu Frank na simu ikakatwa. Frank aliwaacha wazazi wake pale sebuleni kisha yeye akaenda kujiandaa kwa ajili ya kutoka na mpenzi wake. Penina naye baada ya kukataa simu aliingia kwenye gari yake nyeupe aina ya rava4 na kuanza kuelekea nyumbani kwa Frank. Tumfahamu Penina vizuri. Penina ni mwanamke mrembo sana aliyebarikiwa na Mungu kuwa na kila kitu kizuri katika mwili wake. Popote pale Penina alipopita aliacha gumzo kwa wanaume ambao walikuwa wakimmezea mate. Penina ametoka katika familia ya kitajiri yenye watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume ambao ni Nolan, Penina na Irene. Penina amefanikiwa kusoma mpaka elimu ya juu kabisa na kufanikiwa kuwa mfanyabiashara mdogo anayechipukia kwa kasi sana. Penina alianza uhusiano wa kimapenzi akiwa kidato cha tatu, na alianza uhusiano na kijana aliyeitwa Frank ambao mpaka Sasa wapo pamoja. Lakini kitu kimoja ambacho kanalitia dosari penzi tamu kabisa la Penina na Frank, ni baba yake Penina kutopenda mwanawe aolewe na Frank. Baba yake Penina hakutaka kabisa mtoto wake aolewe na Frank, yeye alitaka mtoto wake aolewe na mzungu kutokana na uwezo wao wa kipesa. Mama yake Penina pamoja na Nolan kaka yake Penina ndio Watu pekee waliokuwa wanayaunga mkono mapenzi ya Penina na Frank katika familia yao. Lakini Irene mdogo wake Penina pamoja na baba yake Penina ndio watu pekee ambao walikuwa hawataki kabisa kuyaona mapenzi ya Penina na Frank yakiendelea. * Frank yeye anatoka katika familia yeye hali ngumu kimaisha, hawakuwa na uwezo hata wa kuwa na nyumba nzuri kama wenzao. Frank aliishia kidato cha pili kutokana na wazazi wake kutokuwa na uwezo wa kumuendeleza zaidi. Kadhalika pia Angel mdogo wake Frank naye aliishia darasa La saba kutokana na Wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza zaidi. * Baada ya dakika kadhaa Penina aliwasili nyumbani kwa kina Frank, akapaki gari yake pembeni na kushuka Kisha akaingia katika nyumba ya kina Frank ambayo ilikuwa imechoka Sana. "waoow mkwe wetu karibu Sana." mama yake Frank ndio alimpokea Penina kwa furaha Sana. "Asante Sana mama yangu nimekaribia." akajibu Penina huku akiketi pembeni ya mama yake Frank. "eeh mwanetu lete habari." akaongea mama yake Frank. "Sina hata mpya nimekuja kumchukua mtoto wenu." akajibu Penina. Na Muda huo huo Frank akajitokeza akiwa tayari ameshajiandaa. Licha ya umaskini uliopo katika familia Yao, bado Frank alijitahidi Sana katika kuupendezesha mwili wake ili aweze kuendana na mpenzi wake Penina ambae Muda wote alikuwa mtu wa kupendeza tu. "waoow my love mwaaa." Penina ndio alinyanyuka na kumkumbatia Frank na kumuachia busu Zito la shavu. Frank naye hakuwa nyuma alimpokea mpenzi wake kwa furaha pia. Penina pamoja Na Frank waliaga na kutoka nje, wakaingia kwenye gari na kuondoka. "tunaelekea wapi Sasa mpenzi wangu?" akahoji Frank. "surprise my love sikuambii tunaelekea wapi." Penina akamjibu Frank huku akitabasamu. "haya bhana bas nafunga macho mpaka tufike." akaongea Frank na kumfanya Penina azidi kutabasamu.* Katika bar moja iliyopo maeneo ya sinza kikao kimoja kilikuwa kikiendelea, na huku kilichokuwa kikipangwa Katika kikao kile ni namna ya kulivunja na kuliharibu penzi la Penina na Frank. Mzee Joel ambaye ni baba yake Penina, pamoja na Angel ambaye ni mdogo wake Penina pamoja na vijana wengine watatu wa kiume na mmoja wa kike, ndio waliokuwa wahusika wakuu wa kikao kile. .... Itaendelea ... Read More
CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA TATU (03) ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI : kas0ro Niram peke yake ambae alisema, "wala sina mpango huo, ntampeleka wapii mimi, ila nimemsifiatu! sababu katika wavulana niliowai kuwaona, kwa hapa mtanzania, yule kaka ni handsome sanaa" alisema Niram huku anawaangalia marafiki zake, ambao wakakubaliana nae, kwakiikisa vicwavyao juu chini, na wakati huo kengele ya darasani ikagongwa, wakasimama tayari kwa kuanza safari ya kuingia darasani, ENDELEA....... Waliingia darasani, na vipindi vikaedelea kama kawaida. Niram alitafakari sana maneno ya rafiki zake,,akujua hata kwanini awazia lile jambo, maana hata sababu ya kuliwazia akuiona. "mmh mimi sasa ntakuwa nataka kurukwa na hakili haki ya Mungu" alijisemea kimoyo moyo Niram. Ila akaamua aachane na fikra zile, ambazo mwenyewe alizoziona za kipuuzi, na kuendelea na ratiba zake nyengine. ****** "hallo mmewangu nimekumisi mno utakuja lini?".ilikuwa sauti ya mama niram, aliye kuwa amepozi kwenye moja ya kochi zuri huku ameweka miguu juu ya meza. "ooh mkewangu kipenzi ratiba zinabana kazi zimekuwa nyingi mno hata mi nimekumisi kipenzi ila sina la kufanya mama".ilisikika sauti upande wa pili, ikiongea kwa masikitiko na mapenzi makubwa kwa mkewe. "ooh darling uwezi kuomba ruhusa ukaja hata kwa siku chache tu?".aliongea kwa kudeka mama niram huku akimpachika na swali mumewe huyo,aliyekuwa mbali na nchi ya Tanzania. "ooh sitawahi, unajua natakiwa kwenda india kuna Mahafali ya Razaki".ilisisitiza sauti ya baba niram. "ooh Mungu wangu nilisahau nasikitika sitoenda kwenye mahafali ya mwanangu".aliongea mama niram kwa unyonge ilionyesha hakuwa na furaha kuikosa hiyo sherehe ya mtoto wake wakiume. "usijali mke wangu, najua uwezi kuja sababu niramu hatokuwa na wakubaki nae wacha niende kukuwakilisha mimi sawa mamaa".aliongea kwakubembeleza baba niram huku akimfariji mkewe ili asijione mkosefu. "oky honey kazi njema nitafute baadae utapomaliza kazi".alisisitiza mama niram, "oky honey byeee ilove you"."love u too mume wangu byee". Waliagana mtu na mumewe, mama niramu akanyanyuka kuelekea jikoni,kuangalia kama msichana wake kama ameshamaliza kupika chakula cha mchana. ********* "eeeh ujue vincent ukumalizia story".alisikika suma akimuambia vicent, wakati huo walikuwa katika uwanja wa mpira, wakiangalia watu wanaofanya mazoezi, akiwemo Richard, yeye alikuwa akifanya mazoezi ya mpira wa kikapu, vicent na suma walikuwa wakimuangalia rafiki yao huyo, ambae alijua kuutumia uwanja vizuri aliku Hodari kweli kweli katika mchezo huo, "hahhhhah suma wewe mshkaji wangu mmbeya sana duuuh! yani kumbe ulisubiri tutoke tu!, yani wewe sikuwezi" aliongea vicent, vikafata vicheko vikaliii, suma alikuwa hana mbavuuu, ungewaona ungesema walikuwa wameona jambo la kuchekesha hapo walipo, "sasa mi nimesubiri we unihadithie naona kimya nikaona bora niseme yanini nife kiholo".aliongea suma huku anakalisha tako vizuri akimgeukua mlengwa. Basi vicent alimuadithia mwanzo mwisho, jinsi alivyokutana nae mpaka ilipofikia kusahau kumuomba namba. "hahahhhah hizo ndoto ndugu yangu yani ndo maana ukamzingua vanessa?".aliongea suma kwa mbwembwe, huku akumuona rafiki yake huyo kama anaota ndoto za mchana kweupe. "sikia suma vanessa mimi simpendi bora tu akate tamaa mapema kuliko nikaja kumuumiza zaidi huko mbele na kuhusu huyo dem ata asiponipenda baridi tu! ilimradi mi nimuekeze hisia zangu tu".aliongea vicent kwa msisitizo akimaanisha anachokisemaa. "aaah naona mnakula tu ubuyu". Aliingia Richard, katikati ya mazungumzo, mwili ukiwa umelowa jasho, aka kaa pembeni yao ilionyesha ashamaliza kufanya mazoezi ******* "mama simu inaita".aliita msichana wa kazi wakina Vincent, akimpelekea simu bosi wake ambae alikuwa amekaa nje kwenye bustani. "asante karunde kaendelee na kazi". Alisema mama yake vicent huku anaweka mkonga sikioni. "hallow magreth niambia rafiki yangu".aliongea mama vicent, aikusikika upande wapili,mara mama vicent akaongea na kuaga"aaah! Sawa basi usijali ntakuambia tarehe ikufika nikutakie siku njema".simu ikakatwa.******** "hahahhhh!! Yani na wewe huo ubuyu tule tumekuwa shilawadu?".aliongea vicent huku anacheka, mabega yote yakifanya kazi ya kunesanesa."yani we acha tu katuchukuliaje huyu sijui huyu bwege".alijibu suma huku akimpiga kofi la bega la kiutani utani. "aaah!bac kausheni vipi ile story ya asubuh nimalizie basi mwana".aliongea Richard huku anajiweka sawa kusikiliza. Vilifwata vicheko hatari. "kumbe na wewe shilawadu" aliongea suma baada ya kumaliza kucheka. Basi story zikaanza upyaa, visent akampa fully data. Richard Akuwa na la kuchangia zaidi ya kumtia moyo na kumwambia akaze buti. mara wakasikia ...... Itaendelea......CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA NNE (04) ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU: "aaah! basi kausheni vipi ile story ya asubuh nimalizie basi mwana".aliongea Richard huku anajiweka sawa kusikiliza. Vilifwata vicheko hatari. "kumbe na wewe shilawadu" aliongea suma baada ya kumaliza kucheka. Basi story zikaanza upyaa, visent akampa fully data. Richard Akuwa na la kuchangia zaidi ya kumtia moyo na kumwambia akaze buti. mara wakasikia... endelea....... mara wakasikia, kama kuna vishindo vinakuja mahali walipo wao .ilibidi wakatishe story yao.nakuangalia mbele palipotokea,sauti ya viatu."mmmmh!!", alishusha pumnzi vicent baada ya kumuona mtu huyo aliyekuwa anakuja usawa waliokuwepo wao. Hakuwa mwengine bali ni vanessa, vanessa alizidi kuiongea taratibu kuja mahali pale, walipokuwepo wakina vicent.hatimae alifika."mambo zenu". Aliwasabahi huku akisubiri atajibiwa kwa hali gani salamu yake."nzuri vp vanessa"alijibu suma, mara kabla ajamaliza kuitikia suma, alidakia richard pia."tuambie shemela wa ukweli".kauli hii ili mchukiza, sana vicent alijikuta anamkata jicho moja kali rafiki yake huyo.ila vanessa alipotezea japo vicent,hakujibu salamu yake. "mi niko poa sana samahanini shemeji zangu nilikuwa naomba mnipishe kidogo nna mazungumzo na vicent".aliongea vanesa, huku akiwaangalia shemeji zake hao kwa zamu."ooh!!usijali mama suma eeh tuwapishe wapendanao".aliongea tena richard safari hii huku anatabasamu tabasamu la kichokozi,maana alijua ni jinsi gani anamkera rafiki yake." twenzetu mwanangu uwanja wenu jamani".aliongea suma huku ananyakua kibegi, chake kilicho kuwa pembeni yake, amesimama na kuanza kuondoka,wakati huo richard alikuwa ameshatanguli mbele." oyaa wanangu msifike mbali mnisubiri maana sitachukua mda mwingi hapa".aliongea vicent huku akiwa bize anatazama walipo kuwa wana tokomea wenzie. " poa".walijibu wote kwa pamojaa na kuendelea kutokomea mbele. "nakusikiliza unaweza kuongea" aliongea vicent bila kupepesa macho, akiwa mkavu kabisa." vincent kwani una nini mbona sikuelewi baba"aliongea vannesa huku anakaa pembeni ya vincent. Ila akupata jibu toka upande wapili."vincent si naongea na wewe au kuna kitu nimekukosea niambie ili nijue nikuombe radhi baba,nakupenda sitaki tukosane".aliongea vanesa kwa huzuni huku machozi yakiwa yanalengalenga kwenye macho yake. "sikia vanessa naomba usipoteza muda wako kwa ajili yangu focus katika masomo ujui kuwa tuna karibia mitihani ya kuhitimu kidato cha Sita ".alisema visent bila alama ya uoga,usoni kwake."najua baba lakini hiyo siyo sababu ya kufanya uwe serious ni kuelewana tu" alilalama vanessa huku akijisigeza karibu na vicent."oky basi ndo hivyo vanessa tuzingatie masomo now mapenzi yasimame kwanza".alimaliza vicent huku akijifuta vumbi, kwenye makalio tayari kwakuondoka. "vicent ntawezaje kukuchunia siwezi ntajitahidi nisome kwa bidii ila tusisitishe uhusiano wetu nakupenda sana". "vanessa tuelewane basi au nimefanya kosa kukusikiliza hapa?". Aliuliza vicent,pasipo kusubiri jibu akaanza,kuondoka.ila vanessa alimdaka mkono,na kumvuta asiondoke.daaaaah!! Lilikuwa kosa kubwa maana alisukumwa,akadondoka kama mzigo wa kuni pwaaaaaaah!!.aisee!! Vanessa aliumia akaanza kulia, maana alijiona kama mtu asiekuwa na thamani tena, aliumia kupita kiasi. Kitendo kile, kilimfanya vicent aingiwe na huruma, akaghairisha alipokuwa anakwenda, maana alijiona ana hatia sana. "nyanyuka mpenzi sikuzamilia kufanya hivyo nisamehe mama ". Alisema vicent huku akiinama, kumnyanyua vanessa na kwa bahati nzuri, hakuna alieliona tukio lile. "pole mama nisamehe sana". Alisisitiza vicent akionyeshwa kuchukizwa, na tukio alilolifanya." usijali vicent najua aikuwa kusudio lako kuna vitu haviko sawa kwako". Alijibu vanessa huku anajifuta vumbi, akisaidiwa na vicent. Baada ya hapo vicent alimchukua na kumkalisha chini. " vanessa siyo kama sikupendi laah hasha!! Nakupenda ila nielewe unatakiwa tusome kwanza tukimaliza mitihani tutaendelea, nafanya haya kwaajili yetu mama".aliongea vicent,siyo kama alimaanisha ila aliona si busara, kumuhukumu mtu kisa kampenda ni dhambi kubwa sana. " sawa ila niahidi tutakuwa tuna ongea hata mara moja moja, kwani bila kusikia sauti yako au kukuona sitaweza kusoma". Aliongea kwa kudeka, huku akijiegemeza kwa vicent. " sawa mama itakuwa hivyo ila naona muda unatutupa mkono, sitaki kuwachosha wenzangu wananisubiri". Alisema vicent huku akisimama tayari kwa kuondoka. "oky bby tutawasiliana ukifika".alisema Vanessa huku akiachia, busu matata shavuni mwa vicent. Basi waliagana na vicent akawafata washkaji zake, safari ikaanza..****** Nyumbani kwa kina niramu, palipoa alifika moja kwa moja mpk nyumbani kwao, akamsalimia dada wa kazi " da anna mamy yuko wapi?" aliuliza huku ana jibwaga juu ya kochi, begi akilitupia juu ya meza kubwa ya kioo, " ametoka kaniaga anaenda supermarket kununua bidhaa zimepungua".alijibu anna msichana wao wa kazi.niramu akajizoazoa kivivu, akaliokota begi lake, akaelekea chumbani kwake. Anna aliondoka kuendelea na shughuli zake.******* Vanessa alifika kwao, alikuwa amechoka, alifika akamkuta baba yake, ametulia kwenye kochi,akisoma gazeti. Nyumba yao ilikuwa, kubwa kiasi yenye uzuri wa kawaida.baba yake alikuwa daktari hospitali ya muhimbili, mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya msingi.walizaliwa watano yeye ni watatu kati ya wanaume wawili, na wasichana watatu, wakwanza ni kaka yao.alipita akamsalimia baba yake, na kupitiliza chumbani. Hakika alijikuta anawaza sana matukio, yaliyomtokea shule. " mmh!! Au vicent amepata msichana mwengine?". Alijiuliza."kama ni kweli sitakubalii kwanza sina imani hiyo, labda atakuwa na jambo lingine, ila shule ile nzima, hakuna anaenikamata kwa uzuri".alijiwazia mwenyewe,akijiuliza na kujipa majibu mwenyewe. Ila gafla aka...... Itaendelea SEHEMU YA TANO (05) ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE: wakwanza ni kaka yao.alipita akamsalimia baba yake, na kupitiliza chumbani. Hakika alijikuta anawaza sana matukio, yaliyomtokea shule. " mmh!! Au vicent amepata msichana mwengine?". Alijiuliza."kama ni kweli sitakubalii kwanza sina imani hiyo, labda atakuwa na jambo lingine, ila shule ile nzima, hakuna anaenikamata kwa uzuri".alijiwazia mwenyewe,akijiuliza na kujipa majibu mwenyewe. Ila gafla aka...... ENDELEA. Ila gafla akakumbuka kitu. "mmh si alisema kuwa, tunawasiliana kama kawaida ngoja tuone kama itakuwa hivyo kweli". Alijisemea peke yake, vanessa huku akijiuliza, na kujipa majibu mwenyewe.kiufupi mapenzi yalisha mchanganya, hakujua afanye nini, kumueka vicent kwenye mstari. Aliwaza sana, mpka akapitiwa na usingizi,akasahau hadi kwenda kula chakula.. ****** Niram akiwa bado yupo chumbani, alikuwa ana mfikiria sana vicent, mpka akawa anajiuliza,ni kwa nini amfikirie kama vile. " mmh mbona sasa nawaza upuuzi, kipi ambacho kinanifanya nikumbuke lile tukio la asubuhi".ila gafla kuma kitu akakumbuka, kikamfanya aangue kicheko siyo cha nchi hii. "hahhhhhhahhh!! hhhah!! uwiiii mama weeeeh hhh!!". Alicheka niram kama kichaa. " hivi sasa kilichokuwa kimemgandisha mpka asiondoe gari ni nini?".alijiuliza kisha akaendelea. "maana mtu aliduwaa kama kaona ela alafu yupo pekee yake anavizia jinsi ya kuikwapua hahhhah!!".alijisemesha mwenyewe kisha akacheka tena kwanguvu. Mala mlango ukafunguliwa, Akaingia mama yake ,inaelekea ndo kwanza alikuwa anafika,maana kipochi kilikuwa kwapani. " Eeeeh!! Mwenzetu vipi unaumwa ukichaa, mbona unacheka peke yakoo?".aliuliza mama yake,huku akiwa amesimama mlangoni, kwenye chumba cha binti yake.Niram alishtuka, maana hakutegemea uwepo wa mama yake eneo lile. Ila aliuficha mshtuko wake. "Eeeeeh!! Mama bwana kuna mwalimu wetu alianguka, wakati anaingia darasani, basi nikikumbuka nachekaaa".alivunga niram huku akijifanya kuwa makini na anachokingea. "wewe mtoto shetani si bure mwalimu kaanguka ndo unacheka hivyoo haaahhhhah hatarii, haya vua hizo nguo ukale, maana nakujua wewe hapo ulipo ujala ". Aliongea mama niramu, huku anapiga hatua kwenda nje. "sawa mama naja". Alijibu niram, mara ukasikika mlango paaaaah!, alikuwa mama niramu anafunga mlango . "uhhhhhhhhuh!!"alishusha punzi ndefu niramu, maana akutegemea kama angeweza kudanganya, haraka hivyo. Alibadili nguo nakutoka kwenda kuchukua chakula.. ******* Vicent alikuwa chumbani kwake, akichezea laptop yake.huku ana kula lakini mawazo mengi, yalikuwa kwa niramu. Alijiuliza kwanini ametumbukia juu ya mapenzi ya msichana, wakihindi hakika chakula hakikulika ,alikuwa na mawazo ya hatari yaliyo mfanya, chakula aone kichungu. " ntajitahidi kumtafuta naimani ntampata tu".alijiwazia kimoyomoyo, asijue aanzie wapi, amalizie wapi.ila gafla akiwa kwenye dimbwi la mawazo, alisikia simu yake inaitaaa. Ngrrrrrrrri ngrirrrrrrr!! "nani tena huyoo?". Alijiuliza huku akijiinua kuifata ,kwenye kochi maana yeye alikuwa kitandani. " daaaah!! Anataka nini tena huyuuu aaah!!".alilalamika vicent huku anaipokea simu. "hellow vanessa". Aliongea " yes bby nimekumic nikaona nikupigie". Ilisikika simu upande wa pili alikuwa vaness. " Oooh!! Kumbe niambie". "vicent nilikuwa na kukumbusha lile ombi langu nililokuomba". " lipi hilo?".alihoji vicent huku akimsikiliza kwa makini. "ni lini utanipa penzi lako?, nashindwa kujizuia vicent". Alilalama vanessa huku akisubiria, jibu upande wa pili. "Vanessa hivi kumbe jini wako apendi amani eeh!!?".aliuliza vicent, na kabla ajajibiwa akaongeza neno. " hivi leo nilitoka kukuambia nini hivi upo serious kweli wewe?, naomba usinitibue kama unawaza ngono badala ya kusoma ni wewe mimi naomba unikaushie kabisa".aliongea kwa jazba vicent, huku mikunjo kwenye paji la uso,likionyesha ni jinsi gani amechukia. "ooh nisamehe bby, mi nilikueleza tu hisia zangu wala sitaki tugombane".alijitetea vannesa maana alijua ashaharibu. " oky nikutakie jioni njema kesho mungu akipenda" aliongea vicent, na bila kusubiri jibu simu ikakatwa. Kiukweli vanessa, alijilaumu kwanini aliongea vile, aliilaani ile siku kwani aliiona siku mbaya kuliko zote. Baada ya kukata simu, vicent alikirudia kitanda na kujibwaga bado kidogo angemwaga chakula, kwenye kitanda. " Oooohsh!! Yote sababu ya huyu mwanamkee aaah!!". Alilalama vicent, huku lawama zote akimtupia vanessa. Eti wadau ukipenda sana unaonekana msumbufuu eeeh?.. Tuendeleee.. Basi vicent akachukua kile chakula na kukiweka chini akaendelea na ratiba zake . ******** Ilikuwa muda wa saa mbili kamili usiku(02.00) vanessa alikuwa yupo selbeni na mdogo wake wa mwisho wa kike, aliitwa juliana.kifupi unaweza mwita juli, walikuwa wanaangalia tv.wengine wakiwa na mishemishe zao, huku wazazi wao wakiwa wameshaingia chumbani,maana hata muda wa kuangalia taharifa ya habari aukuwepo, kutwa watoto wanaangalia movie zao. Ndio maana mzee wao anaamua ajununulie gazeti.. Muda wote wapo sebleni ila vanessa alikuwa kimya, kama anawaza jambo. Ila juli aliiona hali tofauti aliyokuwa nayo dada yake .. "vipi dada unaumwa mbona ueleweki leo?". Swali la juli lilimshtua vanessa ,kwenye dimbwi la mawazo akawa hana jibu sahihi la kumpa akabaki, kumbabaisha tu " hamna juli mdogo wangu nawaza mitihani sijui itakuwa migumu?".alivunga vanessa na kujifanya kuuliza ili kupoteza mada. " mmmh!! Dada usiwaze mbona nakuaminia itakuwa ya kawaida muhimu usome ". Alimjibu juli, vanessa akatingisha kichwa kukubali. Ila hakukaa sana akamuaga nduguye akaingia ndani kwake. ********* Siku ya pili, vicent alitoka mapema nyumbani, aliwahi shule kabla hata ya rafiki zake. Hii yote ni kutokana hata usingizi haukupatikana,kutokana na mawazo aliyo nayo. Alikuta baadhi ya wanafunzi wapo darasani, Alifika akakaa kwenye kiti na kufungua begi,kuchukua kitabu na kuanza kusoma. Ila hata sijui nini kilimtuma kutazama mbele maaana alijikuta anatoa macho......itaendelea ... Read More
Story....... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya nane (8) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp....... 0769673145 Ilipoishia........ Lakini Sasa watu wale ambao walikuwa ni wakina Zaza hawakujua wanamfuata nani. Wazimu wa wazimu Nolan naye alifungua mlango na kutoka kwenye gari Lake na kuanza kuwafuata wakina Zaza bila kuwa na uoga wowote.* *************Endelea ********* Zaza pamoja na wenzake walishtuka kuona Nolan anashuka kwenye gari na kuona anawafuata bila wasi wasi wowote. Na baada ya sekunde chache Nolan alikuwa mbele yao. "mnataka nini mbona tunapotezeana Muda?" Nolan akawauliza wakina Zaza huku akiwa amesimama mbele yao. "hahahaaaa Nolan kwa siku ya leo huna bahati leo umeingia pabaya." akaongea zaza huku akimsogelea Nolan. "leo hakika tutakufunza adhabu." akaongea zaza na kumshushia Nolan fimbo ya mgongo, lakini kabla fimbo Ile haijamfikia Nolan aliidaka na kuivunja. Kitendo kile kilimshtua Zaza na kumfanya akasirike kwa fimbo yake kuvunjwa. Zaza alimrushia Nolan ngumi ya uso lakini nayo pia ilikingwa vizuri na Nolan. "acha kupoteza Muda wako kupigana na mimi hata mkiwa ishirini bado hamtaniweza." akaongea Nolan kumwambia Zaza. Lakini zaza hakusikia, akachomoa kisu na kutaka kumchoma Nolan cha tumbo, lakini Nolan alimkamata mkono ule wenye kisu Kisha akamtandika ngumi tatu tumboni za haraka haraka na Kisha akauosokota ule mkono wenye kisu na kuuvunja. Zaza alijikuta akipiga kelele kwa maumivu aliyoyapata. Wale vijana wengine kuona mkubwa amevunjwa mkono nao wakachomoa visu vyao na kuanza kumfuata Nolan kwa kasi. Nolan akawaangalia na kuwapigia hesabu za haraka haraka. "wewe nitakupiga teke la tumbo, wewe wa pili nitakupiga ngumi mbili za kichwa alafu wewe wa tatu na wa mwisho nitatukutoboa kwenye paja la mguu na kisu chako mwenyewe." hizo ni hesabu za haraka haraka ambazo Nolan aliwapigia vijana wale. Na wakati huo huo vijana wale walimkaribia Nolan, na kama Nolan alivyowapigia hesabu aliwafanya vile vile na kila mmoja akadondokea upande wake. "nyie ni kina nani na mnataka nini?" Nolan akamuuliza kijana mmoja kati ya wale wanne aliowapiga. "sijui hata sisi ni wakina nani" akajibu kijana yule. "nitakuvunja shingo jibu swali nililokuuliza." Nolan akamuamrisha kijana yule. "si nimesema sijui sisi ni wakina nani." akajibu kijana yule jibu hilo ambalo lilimpelekea apokee ngumi nzito ya uso kutoka kwa Nolan. Lakini kumbe wakati Nolan anamuhoji kijana yule, kulikuwa na mwanamke mmoja ambaye ni dereva wa kina Zaza yeye alibaki kwenye gari na Nolan hakumuona. Mwanamke yule alishuka kwenye gari taratibu akachomoa kisu chake na kuanza kumsogelea Nolan taratibu bila yeye kujua. Mwanamke yule alipofika sehemu ile aliyokuwa Nolan akimuhoji kijana yule alikinyanyua kisu chake juu kwa mikono miwili na kukusanya nguvu Zake zote na kuanza kuhesabu moja mpaka tatu kwa ajili ya kumshushia Nolan kisu kile cha kichwa. Nolan akiwa bado pale chini akimhoji kijana yule ghafla alishangaa kumuona kijana yule akianza kucheka, kumbe kijana yule alimuona yule Mwanamke ambaye ni mwenzao akijiandaa kummaliza Nolan. Lakini kucheka kwa yule kijana kulimfanya Nolan ahisi kitu. Lakini kidogo hivi Nolan aliona kivuli cha mtu pembeni yake, akageuka haraka kuangalia ni nini kipo nyuma, lakini Ile kugeuka Nolan alikutana na kisu kikija kwa kasi kichwani kwake. Nolan alipojaribu kukikwepa kisu alikuwa tayari ameshachelewa, lakini kwa bahati nzuri kisu kile hakikumpata Nolan kichwani, kwani Ile kugeuka nyuma kulimfanya alindishe kichwa kidogo hivyo kisu kile kikampata Nolan bega karibu na shingo. Nolan alisikia uchungu ambao hajawahi kusikia Katika maisha yake. Lakini mwanamke yule alidhamiria kummaliza Nolan, kwani alikichomoa kisu kile kwenye bega la Nolan na kukirudishia tena pale pale na kumfanya Nolan azidi kupiga kelele kwa maumivu aliyoyapata. Mwanamke yule alikichomoa tena kisu kile na kutaka kummaliza Sasa Nolan kwa kumkata shingo. Mwanamke yule alipotaka kumkata Nolan shingo, Nolan alijijaza licha maumivu aliyokuwa nayo alikikamata kisu. Lakini kwa kukimata kisu kile alijikuta akipokea teke Zito kutoka kwa yule yule Mwanamke na kutupwa mbali. Lakini kwa kupigwa teke lile ilikuwa kama vile Nolan ameamshwa kutoka usingizini. Nolan alinyanyuka na kusimama na kumtizama mwanamke yule huku akiapa lazima amuue. "umenipiga Sana hata wewe Sasa umeisha." akaongea Nolan na kuanza kutoka mbio kumfuata yule Mwanamke. Yule Mwanamke naye akatoka mbio na kuanza kumfuata Nolan huku akiwa na kisu chake mkononi. Walipokaribiana yule Mwanamke akaruka juu huku akiwa amekielekeza kisu kichwani kwa Nolan, Nolan kuona vile naye akaruka juu zaidi ya yule Mwanamke na kupita juu kidogo ya kichwa cha Mwanamke yule na kutua nyuma ya Mwanamke yule. Bila kupoteza hata sekunde moja Nolan aligeuka na kuruka juu na kurusha teke Zito ambalo lilimpata sawia kabisa Mwanamke yule la kichwa na kumuweka chini. Nolan hakusubiri yule Mwanamke anyanyuke, akaruka tena juu na kukunja miguu na kutua kwa magoti mgongoni mwa yule Mwanamke yule na kumvunja mgongoni huku wenzake wakishuhudia lakini wasiweze kufanya lolote kwa kuwa nao walikuwa hoi kwa kichapo walichokipata kutoka kwa Nolan. "wewe lazima nikuue umenijeruhi Sana ngombe wewe." Nolan ndio alimwambia Mwanamke yule Kisha akammaliza kwa kumtandika ngumi nzito ya shingo ambayo ilimpandisha ndege ya kuzimu. Baada ya Nolan kummaliza Mwanamke yule naye alijikuta akidondoka chini na kuzimia kutokana damu nyingi iliyomwangika kutoka kwenye mwili wake. Taarifa zilienea kila mahali kwa mauaji yale yaliyotokea sehemu ile huku wengine wakiwa hoi bin taabani. Polisi pamoja na kikosi cha kutoa huduma ya kwanza kilifika pale na bila kupoteza muda, Nolan pamoja na wakina Zaza wakabebwa na kupelekwa hospital.* Mzee Joel akiwa ametulia nyumbani kwake akipata moja baridi moja ya moto, aliweza kupata taarifa Ile ambayo ilimshangaza Sana. "inakuaje wakina Zaza wako hoi na pia Nolan yupo hoi, kuna nini kilitokea?" akajiuliza mzee Joel bila kupata jibu. Huzuni ilianza upya tena kwa Penina baada ya kupata taarifa ya Nolan mtu pekee ambaye alikuwa akimtegemea kwa chochote, kuwa na yeye yuko hoi bin taabani hospitalini. Bila kupoteza Muda Penina aliingia kwenye gari Lake na kuanza safari ya kuelekea Katika hospital aliyolazwa Nolan, Penina alihisi kuchanganyikiwa hasa akifikiria mambo anayotendewa na baba yake, na pia kupotea kwa mpenzi wake Frank. Hali hiyo ilimfanya Penina akose umakini barabarani na akiwa amebakiza mita chache kufika Katika hospital aliyopo Nolan, Penina alijikuta akikosa balance na kupoteza mwelekeo na kutoka nje ya barabara na kwenda kugonga mti uliokuwa pembeni ya barabara Ile. Pale pale Penina alipoteza fahamu baada ya kugonga mti ule, na alipokuja kushtuka alijikuta yupo hospitalini. Taarifa ilimfikia mzee Joel kwamba Penina amepata ajali Muda mchache uliopita. "shit ni bora afe mtu yoyote lakini sio Penina, utajiri wangu upo kwa Penina." akaongea mzee Joel huku akitoka ndani haraka haraka na kuingia kwenye gari na kuanza kuwahi hospitalini kwenda kumuangalia binti yake Penina.* Baada ya kubangaiza huku na kule kwa siku kadhaa hatimaye Frank alifanikiwa kupata pesa ambayo aliihitaji, na bila kupoteza sekunde, dakika wala masaa, moja kwa moja Frank aliianza safari ya kurudi dar es salam huku mawazo yake yote yakiwa kwa Penina tu Mwanamke aliyempenda kwa moyo wake wote. .......... Itaendelea ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: