Home → ushauri
→ NIMEZALISHWA NA KUTELEKEZWA JE NAWEZA KUPATA MWANAUME WA KUNIPENDA MIMI NA MWANANGU? NINI CHA KUFANYA?
kumpata mwanaume ambaye atampenda huyo mwanao kuliko hata kawaida na ukawa na furaha. lakini hembu usikae na kusubiri mwanaume wa kukusaidia kulea mwanao, hapana hembu anza kusema hapana namlea mwenyewe.
Anzisha familia yako, kama bado unaishi kwenu basi tafuta kazi, tafuta biashara anza kujitegemea na huko wakati ukiendelea na maisha yako basi ndiyo utakutana na huyo mwanaume unayemtaka wewe na atakua mume wako. Lakini ni namna gani utakutana na mwanaume wa namna hiyo? Ni namna gani wewe utapata mwanaume wakati wale ambao hawajazaa tu kupata wanaume ni shida?
Kitu cha kwanza unatakiwa kujua kuwa, kupata mume hakuna uhusiano na kua na mtoto au la? Lakini jambo la pili nikua kama utajiamini na kuanza kumuona mtoto wako kama baraka na si laana basi itakua rahisi kwako kumpata mwanaume. Hembu jiamini, unapokutana na mwanaume, wakati wa mazungumzo hembu jivunie kuwa na mtoto.
Ndiyo sio upite ukitangaza hapana, lakini wakati wa mazungumzo akikuuliza kuhusu wewe muambie, mimi ni mtu flani nafanya kazi flani au biashara, nina mtoto mmoja wa kiume au wakike au nina watoto wawili. Baba yao tulishindwana kidogo ila now ana maisha yake na mimi nina yangu.
Usiongelee alivyo kutenda, alivyokuumiza, alivyokutelekeza hapana, haimhusu na hakuna mtu anayetaka mtu aliyetelekezwa. Muambie tu unamlea mwanao mwenyewe na unafuraha, ndiyo usilielie kama una matatizo, msongo wa mawazo au nini, hakuna mtu anayependa watu wenye matatizo. Unaweza hata kuenda mbali kidogo na kutoa picha ya mwanao kwenye wallet na kumuonyesha, ndiyo jivunie kuwa na mtoto na wengine hawataona shida.
Lakini kama ukimficha ficha, ukaficha ficha kama una mtoto basi hata huyo mwanaume hatampenda kama wewe mwenyewe humpendi na unamuona kama ni kikwazo badala ya baraka. Muhimu nikuwa usimuonyeshe kila mwanaume kama una mtoto, hapana muonyeshe yule ambaye kakuvutia na unaangalia unasema hapana huyu naweza kuwa naye kama mume.
Achana na wale wa siku moja, kanyaga twende, wale usiwaambie mambo mengi ila kama unaona ni mtu ambaye umemtamani hata kama yeye huoni kama anataka kitu siriasi kama moyo wako umemdondokea basi muamini na muambie. Hii ikimaanisha kuwa hata kama akikukataa sababu ya mtoto akukatae kabla hujampa moyo wako.
Lakini hata kama akija kukukataa huko mbeleni, au mkavunjana na kisha akakupotezea wala usiwaze kama ni sababu ya mtoto, kuna wengi sana ambao huachwa na bikira zao wapya kabisa hivyo kuachwa na mwanaume kusiipeleke akili yako kuwa ni sababu una mtoto. Furahia mahusiano yako furahia kuwa na mtoto na utona wengine nao hufurahia.
Usmsingizie mtoto kwa kushindwa kuwa na mtu, hapana wapo wengi ambao hawana wati na wala hata hawajaanza mapenzi na wapo wenye watoto mpaka watatu na wanaume wanawahangaikia kila siku. Muhimu acha kuwa mtu wahuzuni, kukatakata tamaa na kulia lia hapana ukiwa mtu wa majonzi basi utawakimbiza wanaume, badilika.
#SHARE #ShuleRafiki #ChaguaFuraha
NIMEZALISHWA NA KUTELEKEZWA JE NAWEZA KUPATA MWANAUME WA KUNIPENDA MIMI NA MWANANGU? NINI CHA KUFANYA? kumpata mwanaume ambaye atampenda huyo mwanao kuliko hata kawaida na ukawa na furaha. lakini hembu usikae na kusubiri mwanaume wa kukusaidia kulea mwanao, hapana hembu anza kusema hapana namlea mwenyewe. Anzisha familia yako, kama bado unaishi kwenu basi tafuta kazi, tafuta biashara anza kujitegemea na huko wakati ukiendelea na maisha yako basi ndiyo utakutana na huyo mwanaume unayemtaka wewe na atakua mume wako. Lakini ni namna gani utakutana na mwanaume wa namna hiyo? Ni namna gani wewe utapata mwanaume wakati wale ambao hawajazaa tu kupata wanaume ni shida? Kitu cha kwanza unatakiwa kujua kuwa, kupata mume hakuna uhusiano na kua na mtoto au la? Lakini jambo la pili nikua kama utajiamini na kuanza kumuona mtoto wako kama baraka na si laana basi itakua rahisi kwako kumpata mwanaume. Hembu jiamini, unapokutana na mwanaume, wakati wa mazungumzo hembu jivunie kuwa na mtoto. Ndiyo sio upite ukitangaza hapana, lakini wakati wa mazungumzo akikuuliza kuhusu wewe muambie, mimi ni mtu flani nafanya kazi flani au biashara, nina mtoto mmoja wa kiume au wakike au nina watoto wawili. Baba yao tulishindwana kidogo ila now ana maisha yake na mimi nina yangu. Usiongelee alivyo kutenda, alivyokuumiza, alivyokutelekeza hapana, haimhusu na hakuna mtu anayetaka mtu aliyetelekezwa. Muambie tu unamlea mwanao mwenyewe na unafuraha, ndiyo usilielie kama una matatizo, msongo wa mawazo au nini, hakuna mtu anayependa watu wenye matatizo. Unaweza hata kuenda mbali kidogo na kutoa picha ya mwanao kwenye wallet na kumuonyesha, ndiyo jivunie kuwa na mtoto na wengine hawataona shida. Lakini kama ukimficha ficha, ukaficha ficha kama una mtoto basi hata huyo mwanaume hatampenda kama wewe mwenyewe humpendi na unamuona kama ni kikwazo badala ya baraka. Muhimu nikuwa usimuonyeshe kila mwanaume kama una mtoto, hapana muonyeshe yule ambaye kakuvutia na unaangalia unasema hapana huyu naweza kuwa naye kama mume. Achana na wale wa siku moja, kanyaga twende, wale usiwaambie mambo mengi ila kama unaona ni mtu ambaye umemtamani hata kama yeye huoni kama anataka kitu siriasi kama moyo wako umemdondokea basi muamini na muambie. Hii ikimaanisha kuwa hata kama akikukataa sababu ya mtoto akukatae kabla hujampa moyo wako. Lakini hata kama akija kukukataa huko mbeleni, au mkavunjana na kisha akakupotezea wala usiwaze kama ni sababu ya mtoto, kuna wengi sana ambao huachwa na bikira zao wapya kabisa hivyo kuachwa na mwanaume kusiipeleke akili yako kuwa ni sababu una mtoto. Furahia mahusiano yako furahia kuwa na mtoto na utona wengine nao hufurahia. Usmsingizie mtoto kwa kushindwa kuwa na mtu, hapana wapo wengi ambao hawana wati na wala hata hawajaanza mapenzi na wapo wenye watoto mpaka watatu na wanaume wanawahangaikia kila siku. Muhimu acha kuwa mtu wahuzuni, kukatakata tamaa na kulia lia hapana ukiwa mtu wa majonzi basi utawakimbiza wanaume, badilika. #SHARE #ShuleRafiki #ChaguaFuraha
Artikel Terkait
Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi. MSOME SAIKOLOJIA YAKE Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira. MRUHUSU AKUJIBU Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. EPUKA MARUMBANO Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano. MUOMBE MSAMAHA Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.” Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako. ... Read More
NJIA RAHISI 13 ZA KUWA NA FURAHA KILA SIKU  Mabadiliko yalio mepesi kwenye tabia zako za kila siku yatakuweka kwenye mstari wa furaha unayoitaka Umejikuta uko kwenye siku tofauti, story hizo hizo, imekuwa ni kawaida yako? Basi muda huu , sio kesho , sio wiki ijayo, ni wakati wa kubadilisha historia yako. ni za haraka, rahisi na hazina gharama unapofanya hivyo na matokeo yatakupa furaha unayoitaka. 1.Pata masaa 7 mpaka 8 ya kulala usiku. Kulala usingizi wa kutosha unapata furaha, utaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi zako , na utakuwa na mahusiano mazuri. weka simu yako mbali unapoenda kulala, usitumie chakula kingi wakati wa jioni. 2.Amka mapema , dakika 30 kabla . Kama wewe ni mfanya kazi wa kuajiriwa na una tabia ya kuchelewa kazini, jaribu kuamka mapema dakika 15 au 30 kila siku kwa ajili ya kujiandaa vizuri na kukumbuka vitu vyote vya kufanya, kuchukua siku hio. utaona tofauti ya tabia yako. 3.Meditate. Hii ni kubwa. meditate kwa muda wa dakika 10 au 20, utapata faida nyingi zaidi ya furaha, pamoja na kuwa muwazi, kuwa na malengo ya siku nzima. Anza siku yako na meditation. utajiepusha na tress na wasiwasi na hutachanganyikiwa na kazi zako. 4.Jipe nafasi wengi wetu huwa tunajaza vitu nyumbani, ofisini hata vile ambavyo havina kazi, hatuvitumii. inaharibu mfumo mzima wa akili yako, hisia zako, na mwili wako. Ondoa vitu ambavyo huvitumii, tupa nje au gawia watu ambao wanahitaji kuwa navyo, hali yako ya furaha itaboreka. Na hutalemewa na kazi nyingi. 5.Jifunze kitu kipya Jitahidi kujifunza kitu kipya kila siku, kwa sababu hio ndio changamoto itakayokupa furaha, kujifunza kitu kipya inaboresha afya yako ya mwili na akili, kujifunza utajenga ujasiri pia na utakuwa sharp. 6.Tembea mara kwa mara Kutembea kwa dakika 30 kwa siku moyo wako utakuwa unafanya kazi vizuri, utapunguza hasira, hutakuwa na chuki. Kama unaona ni ngumu kwako kutembea , hasa kama una gari , jifunze kupaki gari yako mahali mbali na ofisi , tembea . anza kutumia maji ya kutosha. utapata faida nyingi . 7.Usijihusishe na mambo ya mitandao. Ni rahisi kuingia instagram, facebook na zingine, lakini wachunguzi wanasema kwamba ukizidisha kujihusisha na mitandao unaweza kuharibu afya yako ya akili. badala ya kutumia nusu saa kwenye mitandao, unaweza kufanya kitu kingine unachokipenda, au kusoma kitabu, kujifunza mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiboresha mwenyewe kuwa mwenye afya. 8.Kuwa mwema. Ukarimu unakuongoza kwenye furaha yako mwenyewe na utakuwa mwenye afya bora. vitu ambavyo vinavyo chochea furaha ni kutoa , na kuwa mkweli , utapata faida , na utajisikia vizuri kuwa sehemu ya baraka kwa mtu fulani. kujitolea kufanya kitu, au kumwachia mtu kiti kwenye daladala. Sehemu ngumu? lakini nzuri. 9.Kaa na watu wenye furaha. Angalia watu unaoshinda nao, unaofanya nao kazi, ni watu wa aina gani. kwa sababu kuna msemo unasema kuwa ukikaa na ua rose utanukia hata kama ulikuwa hunukii. Fanya hivyo na utaweza kufungua mlango mpya kwa ajili yako maishani. utaiona furaha ikitiririka kama mto. 10.Don’t gossip. Kuseng’enya, umbeya, itakusababishia maradhi ya misongo na kukosa furaha. mtu mmbeya hawezi kusaidia kitu. wakati mwingine jitenge na watu kama hawa, au unapoona kuna kutoelewana na wafanya kazi wenzako, jaribu kutulia kwanza , badilisha negative to positive. Sema kitu kizuri kuhusu mtu. ni vizuri. kwa sababu utajiwekea alama nzuri kwako. 11.Tumia muda wako na watu unaowapenda Unapoongea na familia au marafiki kwenye simu , inatia moyo. mawasiliano hayo yanakupa afya na furaha.Fikiri ilivyo vizuri kama utaenda kula na rafiki yako mahali fulani, au kuamua kupika nyumbani , au kucheza na watoto wako kitu kama game, mpira, inafurahisha. 12.Journal Kuandika vitu vya kufanya kwa siku, au kuandika vitu unavyotaka kuvipata, Lengo hili dogo litaongeza IQ yako na kuleta utulivu wa kuboresha ujasiri wako, ukiwa na tabia hii kila siku , furaha haitakosekana kwako na utapata faida ya akili na hisia zako zitakuwa bora. 13.Jizoeze kujijali. Unapojijali ,Utaona faida zake, pamoja na kuondoa stress na wasiwasi, utakuwa mtu wa kuwaza mazuri na utaboresha immunity.pata muda kila siku kufanya kitu kwa ajili ya furaha, kama vile mazoezi, kupika chakula kizuri, kusoma . utaanza kushangaa jinsi ilivyo rahisi kuwa na furaha unapojijali na utaboresha akili yako na mwili wako, na roho yako. Kama unavyojua , kuna njia nyingi zinazotushambulia kwa siku, Ondoka mahali ambapo panaharibu ratiba yako. sasa, kama kitu kingine chochote,mafanikio ni kufanyia kazi. kwa hio pick one, and let the fun begin! ... Read More
UNAJUA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO????  Kama inavyoeleweka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la "Tantric Sex." Kama inavyoelewaka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la “Tantric Sex.” As if hii duinia, especially hii century haiko overloaded na information kuhusu mambo ya mapenzi, jinsi ya kufanya mapenzi and whats hot in the bedroom, whats in and whats not. So, lately nimeona a lot of tzmoms readers wamekuwa wakitembelea sana na kusoma page ya “mapenzi baada ya ujauzito” na “kufanyamapenzi wakati wa ujauzito.” And I thought well, writing about Tantric Sex will be nyongeza kwa kila mmoja, aliye mama na mbaye bado damu inachemka katika mambo ya mapenzi. Anyhu, kama “SEX/MAPENZI” yangekuwa yanaweza kuyu-nite the world/countries/makabila/people I think hii fani ingeshinda. Well, so kama umeshawahi kujifungua ama kama wewe ni mama, you definitely understand ni jinsi gani ni vigumu kuwa upbeat kuhusu mapenzi ama kumfurahisha mumeo/mpenzio everyday. Well, once in a while maybe but not everyday. Ila kama we ni mdada/binti ambaye hujazaa bado well, damu yako bado inachemka so energy bado ipo nyingi ya kukurupushana na mpenzio. Having said that, si maanishi mtu ukishazaa ndo fani ya kuenjoy mapenzi imekwisha but nguvu zinapungua for sure however, kuna vitu vingi tuu ambavyo vinaweza kusaidia kuleta nguvu ya kutaka kukurupushana chumbani lol. Kukosa nguvu/energy to wanna work it all the time its not because mwanamke ni mvivu but hutokana na kuwa na mambo mengi sana ya kutend nyumbani i.e. kuhakikisha watoto wako taken care of, labda kazini pia unahitajika, etc una kuta hupati muda wa kujifurahisha mwenyewe ama na mpenzi wako. Therefore, mara nyingi before you know mupenzi anaanza kulalamika or hata mwanamke mwenyewe unaweza kufeel like you are not doing enough so mambo ndo hivyo yanaanza kwenda south chumbani. Hivyo basi, lets dig in tuone Tantric Sex inatoa msaada wa aina gani ili kurevamp mapenzi. Kwanza kabisa, FYI tantric sex can be weird at the beginning ila nitajitahidi kutoingia so indepth ili kusave miyoyo ya watu wengine. Kwamaana hii ni soft porn “according to me.” Lol. so usishtuke ama kushangaa sana. Well, anythign “sex” can be unconfortable anyways. Okay, so, kwanza kabisa, with Tantric Sex, mtu na mpenziwe wanatakiwa kuwa; SPIRITUALLY CONNECTED (usishtuke sio kidini lol).. Hii inamaainisha kwamba wewe na patner wako kwa pamoja mnajua mnataka nini emotionally and physically. Kwa kufanya hivi inasaidia kuwafanya kwa pamoja kuwa “FREE” na kuondoa wasiwasi wa labda mwenzangu atanijudge kwamba labda mimi ni malaya ama fuska etc. In other words hii process inaitwa “Dropping the Veil, between “Self” and “Other/patner.” THE ENVIRONMENT/mazingira. Wakati mnapractice tantric sex of course, just like when you are in the bedroom unaweza ukavaa lingerie/kuo za ndani zinazovutia or “kuwa kama mlivyotoka tumboni mwa mama zenu” (you know what i mean). Tatu, wapenzi wanaanza kupapasana lol, but in a way kwamba you are feeling the energy of the other person. Na hii energy unaweza kuifeel kwasababu mko free hamna anayemjudge mwingine/there are no worries. You are just in your own created world. Nne, wakati wa kufeel energy ya mwingine lazima wapenzi wawe wana pumua heavely yaani just feeling every move made but the other person mpaka mnapofikia mahali were you are breathing so hard and you are feeling each other. then you start kissing the lips, and then deeper for minutes even hours. Then mengineyo yanaweza kuendelea. So, all this time kumbuka its not about going straight into sex with your partner rather its about getting high by touching and feeling connected with each other. hivyo basi, once in a while take that time and revamp your intimacy, dress good, feel sexy and heey have fun!!. By 🅱 ... Read More
NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI? Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili). Jinsi yakutumia samahani kiusahihi Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali. Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya. Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa. Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena. Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha. Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa) Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe) Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea. Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja. ... Read More
JIFUNZE KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPENZI YA DHATI NA WEWE: Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi". Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. MTU AMBAYE HAKUPENDI KWA DHATI: ==> Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako. ==> Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?" Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo". Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu. ==> Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo. ==> Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie. ==> Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. ===> Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo. MTU ANAYEKUPENDA KWA DHATI: ==> Hachoki kukwambia NAKUPENDA, kwani anajisikia raha sana pale atamkapo neno hilo juu yako kwahiyo unaweza ukawa kama wimbo wake kwako. ==> Anajivunia kuwa na wewe na atapenda kukupa sifa nzuri kila mara, yani Hachoki kukusifia. Atakushauri pale unapokosea ili uwe katika njia nzuri. Unaponuna atajua cha kufanya ili wewe ufurahi na kurudi kwenye hali ya kawaida. ==> Hachoki kukuombea mema na kukutakia mafanikio. ==> Atapenda kukueleza ukweli kila mara ili uweze kujenga uaminifu na imani juu yake. ==> Wewe utakuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake, atakuthamini na kukujali. Tatizo lako litakuwa sawa na tatizo lake, atakupa ushauri bila kuchoka. ==> Kabla ya kumuuliza swali kuwa "je unanipenda?" atakuwa ameshakujibu tena kwa hisia nzito kuwa "nakupenda sana mpenzi wangu". ==> Hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, kwakuwa wewe ndiye furaha yake. ====> Thamani yako ni kubwa sana kwake, anakuona mpya kila siku na hachoki kuvutiwa na wewe. Anakupenda kwa kumaanisha na si kukupenda kimazoea tu. Neno NAKUPENDA litamtoka moyoni na ataridhihirisha kwa kinywa chake. Mtambue mtu huyu kuwa anakupenda kwa dhati. NB: Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Si vyema kutumia mapungufu ya mwenzio kama fimbo katika mapenzi, cha muhimu ni kumuelimisha na kumuelekeza ili muweze kwenda sambamba. Nadhani baadhi ya maswali ya wadau yatakuwa yamejibiwa na hiyo mada. Kama kuna nyongeza au swali lolote kuhusiana na hiyo mada tuambiane hapa na kupatiana majibu hapa hapa wadau. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: