Home → ushauri
→ NI VEMA UKAYAJUA HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA:
1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote.
2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa.
3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.
4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote.
5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.
6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na mtu asiye sahihi.
7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wagomvi.
Aina tano za wanawake wa kuepukwa;
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wachawi
(d) Wagomvi
(e) wasio tii
8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe na Ndoa yenye furaha.
9. Maneno matatu yanayojenga amani katika Ndoa:
(a) Nakupenda.
(b) Samahani.
(c) Asante.
10. Kupiga punyeto kwa mwanaume na kujichua kwa mwanamke ni kuharibu mwili wako mwenyewe.
11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama gari bila mafuta. Hamuwezi kufika popote.
12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu:
>Mungu mmoja
> Mume mmoja
> Mke mmoja.
13. Furaha ya kudumu maishani hutegemea na chaguo lako la mwenzi ktk Ndoa.
14. Usioe/kuolewa na pesa au mali. Oa/Olewa na mtu. Pesa/Mali hufilisika lakini utu hudumu milele.
15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa isiyo na amani wala furaha.
16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.
17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa sababu tu anakidhi haja zako kingono.
18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki wema. Vivyo hivyo kwa marafiki wabaya (Bad company corrupt good character)
19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali.
20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza...
""Mungu awabariki Sana"". Watumie na wengine wajifunze.!
NI VEMA UKAYAJUA HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA: 1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote. 2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa. 3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema. 4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote. 5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu. 6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na mtu asiye sahihi. 7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa: (a) Walevi (b) Wazinzi (c) Wagomvi. Aina tano za wanawake wa kuepukwa; (a) Walevi (b) Wazinzi (c) Wachawi (d) Wagomvi (e) wasio tii 8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe na Ndoa yenye furaha. 9. Maneno matatu yanayojenga amani katika Ndoa: (a) Nakupenda. (b) Samahani. (c) Asante. 10. Kupiga punyeto kwa mwanaume na kujichua kwa mwanamke ni kuharibu mwili wako mwenyewe. 11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama gari bila mafuta. Hamuwezi kufika popote. 12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu: >Mungu mmoja > Mume mmoja > Mke mmoja. 13. Furaha ya kudumu maishani hutegemea na chaguo lako la mwenzi ktk Ndoa. 14. Usioe/kuolewa na pesa au mali. Oa/Olewa na mtu. Pesa/Mali hufilisika lakini utu hudumu milele. 15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa isiyo na amani wala furaha. 16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa. 17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa sababu tu anakidhi haja zako kingono. 18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki wema. Vivyo hivyo kwa marafiki wabaya (Bad company corrupt good character) 19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali. 20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza... ""Mungu awabariki Sana"". Watumie na wengine wajifunze.!
Artikel Terkait
NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?  Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu. Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile. Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…...... Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo. Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani. Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish. Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye. Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni? Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala . Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu. Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali. Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake? Ushauri tafadhali........... ... Read More
Jinsi Ya Kufanya Mapenzi Na Mwanamke Bikra  Ubikra ni hali ya binadamu kuwa hajafanya mapenzi maishani mwake. Mwanamume au mwanamke ambaye hajawahi fanya ngono wote ni bikra. Imekuwa desturi kwamba wanawake ndio huwa mabikra pekee, ilhali pia wanaume. Umwagaji wa damu mara ya kwanza wa kushiriki ngono hutofaitiana kwa wanawake tofauti. Wanawake wengine huwa hawatoki damu kulingana na umbile la kizinda chao. ufanya mapenzi na mwanamke bikra kunaweza kuwa na matokeo mawili. Kuna wanawake ambao husikia uchungu kwa mara yao ya kwanza kushiriki ngono na kuna wale ambao huwa hawaiskii uchungu. Kupata uchungu ama kukosa kunalingana na mwanamume ambaye huyu mwanamke anatolewa ubikra naye. Mwanamume ambaye ni mtulivu na anazingatia ama anafanya mapenzi na huyu mwanamke kwa utaratibu huwa anamsaidia yule mwanamke kufurahia wakati wake wa kwanza katika ngono na anapotolewa ubikra. Mwanamke pia anajukumu upande wake la kufanya ili asipate maumivu ama yawe madogo wakati wa kutolewa ubikra. Kama unataka kumtoa mwanamke ubikra bila maumivu kuna mambo muhimu unafaa kuzingatia ili kufanya nyote muwe na wakati wenye raha na utamu; Mwanamke lazima ajiamini Hakikisha mwanamke yule bikra anajiamini na ashki yake. Wanawake wengi mabikra huwa hawana maelezo ama elimu ya ngono. Wengi wao huwa wana aibu sana wakati jambo la kujamiiana linapozungumziwa. Kwa sababu hii mwanamke anaweza kuwa na uoga kwa kufikiri vile mara ya kwanza itakuwa. Uoga ni jambo ambalo huchangia kwa mwanamke bikra kupata uchungu wakati wa kwanza. Uoga kumdhuru kisaikolojia na hufanya misuli yake ya uuke kukaza na husababisha uchungu mwingi wakati wa kujamiiana na mwanamume. Kama mwanamume, ni muhimu kumfanya mwanamke yule bikra kujiskia huru na kutulia ili kujamiiana kuwe kwenye raha na utamu. Kuamiiana Kuaminiana ni jambo pia linaloweza kuwasaidia wawili wanaojamiiana kupata raha na utamu katika tendo lile. Fanya hima kujua kama mwanamke yule bikra ako na wasiwasi wowote ama kuna kitu kinachomtatiza. Fanya kujua kama kuna jambo analotaka kufanya wakati mnapohusiana katika ngono. Kujali hisia na matarajio ya mwanamke yule utafanya akuamini na itamsaidia pia kutulia wakati unapomtoa ubikra na hatakuwa na uchungu. Fahamu kwamba nyote mwahitaji kupeana raha mnapojamiiana, kwa hivyo zingatia pia mwanamke anafaa kujifurahisha wakati wa ngono. Papasa mwanamke Mwili wa mwanamke uko na sehemu nyingi ambazo zinaweza kupandisha hamu yake ya ngono. Mwanamume anafaa kufahamu jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa kumpapasa. Jaribu kumpiga busu na kumpapasa shingoni, mdomoni, ili kuweza kumtuliza. Kujua sehemu ambayo unaweza kumpapasa mwanamke yule bikra utamsaidia mwanaume wakati wanapofanya mapenzi. Hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi hufanya uuke wake kutulia na mwanamke yule kuwa katika hali ya utulivu. Utulivu huu humsaidia kuwa tayari kwa kufanya mapenzi na pia kwa ubikra wako kutolewa. Pia utulivu huu utamsaidia kwamba hatapata kuskia uchungu wakati wa kujamiiana. Kusisimua uuke Wakati mnapofanya mapenzi na mwanamke bikra, jaribu kusisima uuke wake na mafuta nyororo. Kusisima uuke wake kutakusaidia wakati unapoingiza uume wako kwa uuke wake. Pia hii husaidia kupunguza uchungu wakati unapenya uuke wake. Unataka uzoefu wake wa kwanza uwe kitu ambacho atakumbuka, kwa hivyo kusisima uuke wake husaidia asiwe na uchungu unapompenya uuke wake. Kuwa mpole katika ngono Unapofanya mapenzi na mwanamke bikra, lazima uwe tayari kwenda pole pole na kuwacha kufanya mapenzi mwanamke anaposema hajiskii tena. Ni jambo la busara kutilia maanani kile mwanamke yule anachotaka kufanya. Akisema hayuko tayari, mpe wakati hadi atakapo sema ana hamu ya kufanya mapenzi. Usikasirike mwanamke anapokwambia uwache mnapoendelea kufanya mapenzi. Mwanamke hutaka kujua kwamba wampenda ili aweze kukubali kukupa ubikra wake. Kwa hivyo kutulia anaposema hajiskii kunaweza kuwa jambo linalo weza kumwonyesha kwamba wampenda. Kwa kufanya vile, utakuta mwanamke yule bikra atajitoa kwako kwa moyo wake wote na mnapofanya mapenzi nyote mtapata raha na utamu. Chukua usukani kama mwanamume Kwa vile wewe ndiye mwanamume wa kwanza ambaye unamuingiza kwa ngono kwa mara ya kwanza, unataka kufanya iwe kitu ambacho atakumbuka maishani. Kama mwanamume ni muhimu kuchukuwa usukani wakati mnataka kujamiiana. Mwanamke hupenda mwanamume anayejiamini kitandani. Hata unapochukuwa usukani zingatia anachotaka yeye na umwelekeze pole pole. Usije ukafa moyo kwa vile hana uzoefu lakini mfunze kile anachoweza kufanya ili ukipenya uuke wake aweze kusikia utamu na uchungu usiwe mwingi. Unataka kumfanya awe na nyege ya kufanya mapenzi na awe tayari kwa uume wako. Kinga katika ngono Kulala na mwanamke bikra hakumaanishi kwamba usahau kujikinga na kushika mimba ambao hakukutarajiwa na kueneza kwa magonjwa yanayotokana na kufanya mapenzi. Ni muhimu kama mwanaume kijikinga na kuchukuwa tahathari wakati wote wa kufanya mapenzi. Hakikisha unatumia mipira wakati wa kufanya mapenzi na madawa ya kukinga uzazi. Hii itawasaidia nyote wawili kupunguza majuto baada ya kufanya mapenzi. Kuwa mwepesi kwenye matarajio Kwa mwanamume, usije ukawa na tatumaini makubwa sana wakati wa kujamiiana na mwamake bikra kwa mara ya kwanza. Kitendo hicho kinaweza tokea kinyume na ulivyo tarajia. Unaweza fikiri utapata wakati rahisi kupandisha hamu yake na pia kupata wakati rahisi wakati wa kumpenya uuke wake. Unafaa kuweka matarajio yako wazi kwamba kitu chochote chaweza tokea. Kuweka wazi matarajio kutakusaidia kwa tukio lolote lile. Waweza pata kujifurahisha ama kupata raha unapofanya mapenzi na mwanamke yule bikra na pia unaweza kupata kuwa nyote hamkufurahia wakati ule. Kuwa tayari kwa uhusiano wa kimapenzi Mwanamume lazima awe tiyari kuwa katika mahusiano na yuel mwanamke bikra unayefanya mapenzi naye. Kila mtu hukumbuka wakati wake wa kwanza kufanya mapenzi, kwa hivyo ni muhimu kuifanya iwe ya dhamani. Kumbuka mnaenda kuwa katika uhusiano wa karibu, kuwa tayari kukuwa kwa uhuisano wa kimaisha kwani hisia zake zaweza kubadilika mnapofanya mapenzi. Kwa hivyo kama hutaki kuumiza mpenzi wako usifanye mapenzi naye kama huko tayari kuwa katika uhusiano naye kimaisha. Kufanya mapenzi ni kitu ambacho mwanamume na mwanamke hupenda. Cha muhimu kwanza ni kujikinga kutokana na magonjwa, na mimba ambazo hamkutarajia. Kwa kufanya mapenzi wawili hao huwa wameamua hupeanza uchi wao kwa mahaba. Kwa mwanamke bikra, yataka uwe mtu makini sana. Mwanamke bikra hana uzoefu wa funyanya ngono kwa hivyo unafaa kumpeleka pole pole na ukamfunza anachofaa kufanya wakati mnafanya mapenzi. Mwanamke bikra anafaa kufanywa ajiskie yuko huru na kuwachiwa kusema wanachotaka kufanya kwani ni wakati wao wa kwanza. Mwanamume lazima aweze kumweka mwanamke yule katika hanjam ya kufanya mapenzi naye, kwa kupapasa, kumpiga busu. Asiwe mtu mwenye kuharakisha kumpenya mwanamke bikra ila awe mtulivu. Mwanamke bikra akiona kwamba unazingatia masilahi yake atakuwa huru nawe na atakubali kukupa ubikra wake. Mwanamke aliyetulia na anayejua mwanamume anaujasiri na kujiamini kitandani atafanya tendo la kufanya mapenzi liwe la kufana sana kwa wote wawili. ... Read More
MAMBO 10 AMBAYO NI SUMU KATIKA MAPENZI  KATIKA harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi. Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi. 1. WIVU WA KUPINDUKIA Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomwona mpenzi wako akizungumza na mwanamume mwingine, au anapotoka na marafiki zake wa kike, au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa tayari umekunywa sumu ya mapenzi. Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana. Kama kweli unataka mpenzi wako akupende kwa dhati, mwoneshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda wao mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu. 2. KUTOMWACHIA NAFASI MPENZI Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumwona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa peke yake kwa ajili ya mambo yake binafsi. Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, lakini kwa hakika hiyo si ishara njema ya mapenzi ya kudumu. Hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka. Kwa hiyo, mpe mpenzi wako fursa ya kupumua. Namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kutaka kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu hiyo itaisha. 3. KUMWAMULIA MPENZI MAMBO YAKE Unaweza kujikuta ukisukumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini wakati gani, akutane na nani na kwa wakati gani au ale nini. Ukiona hivyo, fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia. Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa jinsia, hakuna mwanamke ambaye angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake. Kama ilivyodokezwa hapo juu, kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu. Kama utataka kumpangia kila kitu ni wazi kuwa utaishia kuishi peke yako. 4. KUMUULIZA MPENZI MASWALI Iwapo utajikuta ukimuuliza mpenzi wako maswali mengi yanayoonesha wasiwasi wako kuhusiana na mwenendo wake, fahamu kuwa kuna tatizo na tatizo hilo lisipopatiwa ufumbuzi utakuwa mwanzo wa mwisho wa uhusiano wenu. Mwanamke angependa umuulize maswali ya kawaida kuhusiana na jinsi siku yake ilivyokuwa na kama marafiki zake hawajambo au la, lakini kila jambo lina mpaka wake. Mwanamke hatarajii kuwa kila mnapokutana atakuwa kama ameingia kwenye chumba cha mtihani au usaili wa kazi. 5. KUTOAMINI ANACHOKWELEZA MPENZI Wakati mwingine watu hushindwa kuwaamini wenzao, lakini kwa sababu ambazo ni za msingi, lakini kuna wakati ambapo mtu hushindwa kumwamini mwenzake bila sababu yoyote ya msingi, au kwa sababu zisizo sahihi, kisingizio kikiwa ni mapenzi. Kuna tatizo la kisaikolojia la kujishuku au kuwashuku wenzako. Hili ni jambo ambalo linaweza kukuharibia mustakabali wako katika mapenzi, maana husababisha kujengeka kwa mazingira ya kutokuaminiana. Ili uweze kwenda sanjari na mpenzi wako, amini kila anachokweleza hadi pale utakapokuwa na sababu za msingi za kutokumwamini. Na hata unapokuwa umelithibitisha jambo, endelea kuwa katika uhalisia wako. 6. KUACHA HOBI, MARAFIKI Mahusiano ya kimapenzi mara nyingi huhusisha kila mmoja kuacha baadhi ya mambo yake kwa ajili ya mwenzake. Hata hivyo, lengo ni kuweka tu uwiano wa mahitaji, si kuacha kila kitu ulichokuwa nacho kwa ajili ya mwenzako, ama kwa shinikizo, au kwa kulewa penzi. Iwapo utabaini kuwa marafiki zako sasa wamekuwa ni marafiki zako wa zamani na hobi zako zimebaki tu katika kumbukumbu japo kwa hakika bado unahisi mapenzi katika hobi hizo, basi tambua kuwa huyo mrembo wako amekunywesha sumu ya penzi na sasa huwezi hata kuitumia vema mantiki yako. Mbaya zaidi, iwapo utabaini kuwa marafiki zako wapya ni marafiki wa siku zote wa mpenzi wako na hobi zako ni zile za mpenzi wako, basi tambua kuwa huna tena nafsi yako, bali umejisalimisha mzima mzima kwa mpenzi wako. Lakini msemo mmoja wa hekima unatwambia usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja. Yamkini unaelewa. 7. KUKUBALI KUPELEKESHWA Pengine unakumbuka kuwa kuna nyakati ambapo ulikuwa na uwezo wa kujikita katika jambo moja na kulifanya kwa umakini, huku ukiwa pia mwerevu, mjanja na unayejisimamia, lakini leo unayeyuka kirahisi tu kama barafu iliyowekwa juani! Hii ni hatari kwa mustakabali wa maisha yako. Mbaya zaidi ni pale utakapoiacha kazi yako inayokulipa vizuri na kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako. Ukifika hali hii ujue wewe mwenyewe kuwa hapo hakuna mwanamume. 8. UTAYARI WA KUFA KWA AJILI YAKE Umewahi kujisikia kuwa na utayari wa kufa kwa ajili ya mpenzi wako? Kama jibu ni “ndiyo”, basi fahamu kwa hakika kuwa hayo uliyo nayo si mapenzi bali ni upumbavu. Pengine huku ndiko kunywesha sumu ya mapenzi. Kwa hakika, hakuna mwanamke ambaye anastahili kumfanya mwanamume yeyote kufa kwa ajili yake. Yamkini wanaume wanaolengwa katika makala haya si wavulana wanaosoma sekondari, waliobalehe majuzi, ambao wakipenda au kupendwa hujiona kama wako katika sayari yao. Mwanamume aliyepevuka hujiamini na hayaweki maisha yake yote mikononi mwa mwanamke, hata kama mwanamke huyo angekuwa ndiye mrembo wa dunia. Iwapo, ama kwa ujinga au kwa kufahamu umewahi kumwambia mpenzi wako: “Ukiniacha nitajiua,” na ukawa unaamini hivyo kabisa, basi yamkini unahitaji kutafuta msaada wa ushauri nasaha, maana kwa hakika umepotoka. 9. MUDA WOTE UNAWASILIANA NAYE Vijana wa siku hizi ni watumiaji wazuri sana wa simu, lakini iwapo utabaini kuwa asilimia kubwa ya muda wako unautumia ama kwa kuongea au kuwasiliana kwa ujumbe mfupi na mpenzi wako, basi fahamu kuwa kuna tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka. Kumbuka kuwa mapenzi hayachukui nafasi ya kila kitu. Yamkini huyo mpenzi wako amekukuta unaishi na kuna mambo ya muhimu ya kufanya. Hebu achana na simu kwanza ufanye mambo ya muhimu kuhusiana na maisha yako. Kama mpenzi wako hakwelewi katika hili basi hakufai. 10. NDUGU ZAKE WANAKUFUATILIA Iwapo utabaini kuwa marafiki, ndugu na jamaa za mpenzi wako wanamtonya mpenzi wako kuhusiana na kile wanachokiita mwenendo wako mbaya, usipuuze hali hii. Kuna uwezekano mkubwa kuwa watu hawa wanayo sababu ya kuwa na wasiwasi na mwenendo wako, kwa hiyo jichunguze na kuangalia jinsi unavyoenenda. Hata hivyo, jambo hili si ishara njema ya mustakabali mwema wa uhusiano wenu. Iwapo mpenzi wako ataweka watu wake wakufuatilie, maana yake halisi ni kwamba hakuamini. Katika hali kama hii, haitarajiwi kuwa mustakabali wa uhusiano wenu utakuwa mzuri, kwani kutakuwa na uingilizi mwingi wa ndugu, jamaa na marafiki zake. Unaweza kukubali kuendelea kuishi katika hali hii kwa kisingizio cha mapenzi, lakini ukweli ni kwamba hayatakuwa mapenzi bali karaha. KUWA MAKINI Kama unavyoona, hizi ni baadhi tu ya dalili kuwa mapenzi yako kwa mwanamke sasa yanaelekea katika ulevi, mithili ya ule wa dawa za kulevya. Jambo moja la kukumbuka ni kwamba kweli mapenzi ni kitu kizuri, lakini pia mapenzi yanahitaji kuwa jambo linaloashiria mustakabali mwema kwa wahusika wawili. Yakiwapo mambo haya kumi hauwezi kuwapo mustakabali mwema katika mapenzi. ... Read More
Tatizo la Ugumba kwa wanawake  Ugumba ni hali ya mwanamke kushindwa kushika ujauzito. Linaweza kuwa tatizo pia kwa mwanaume lakini katika makala hii tutaona nini kinasababisha tatizo hili kwa upande wa wanawake. Nini husababisha ugumba kwa wanawake? Mayai kutokomaa ipasavyo: Tatizo la mayai kutokukomaa vema ndilo chanzo na sababu kuu ya wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito na hii inachukua karibu asilimia 30 ya wanawake wote wagumba. Habari njema ni kuwa tatizo hili linaweza kurekebishwa kirahisi ikiwa mwili utapewa vile viinilishe mhimu vinavyokosekana hadi kupelekea mayai kutokomaa vizuri. Vinavyosababisha mayai ya mwanamke kutokomaa vema: (1) Matatizo ya kihomoni Matatizo katika homoni ndicho chanzo kikuu cha mayai kutunga bila kukomaa vizuri. Hatua za ukomaaji wa mayai zinategemea uwiano mzuri wa homoni na namna zinavyotegemeana katika kufanya kazi. Jambo lolote linalovuruga homoni kubaki katika uwiano wake sawa na wa kutegemeana na wenye kufanya kazi ipasavyo linaweza kupelekea utungaji wa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Kuna sababu kuu mbili zinazosababisha matatizo katika homoni: Ufanyaji kazi usioridhisha wa hypothalamus Hypothalamus ni sehemu ya mbele ya ubongo ambayo ina jukumu la kutuma ishara (signals) kwenda katika tezi ya pituitari ambayo yenyewe tena hutuma uchochezi wa kihomoni kwenda kwenye ovari katika mfumo wa F.S.H na L.H ili kuanzisha ukomaaji wa mayai. Ikiwa hypothalamus inashindwa kufanya kazi zake vizuri kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa ndiyo kutakuwa ni matokeo yake. Tatizo hili linachukuwa asilimia 20 katika kesi za mayai kushindwa kukomaa kiasi kinachohitajika. Ufanyaji kazi usioridhisha wa tezi ya pituitari Kazi kubwa ya tezi ya pituitari ni kuzarisha na kutoa homoni mbili maalumu kwa ajili ya mfumo wa uzarishaji kufanya kazi zake vizuri ambazo zinajulikana kitaalamu kama ‘Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ na ‘Luteinizing hormone (L.H)’. Mayai yatashindwa kukomaa vizuri ikiwa ama L.H au F.S.H zinatengenezwa chache sana au nyingi sana kuliko inavyohitajika. Hili linaweza kutokea kama sababu ya ajari, uvimbe au kama usawa usio sawa wa kikemikali katika pituitari. (2) Kovu katika Ovari Uharibifu au ajari katika ovari unaweza kupelekea kuzalishwa kwa mayai ambayo hayajakomaa. Kwa mfano, upasuaji mkubwa, uvamizi au upasuaji wa mara nyingi wa uvimbe katika ovari unaweza kusababisha kapsuli ya ovari kupata majeraha au makovu na hivyo kwa namna moja ama nyingine kuweza kuzuia utungwaji wa mayai ambayo hayajakomaa vema. Pia maambukizi katika njia ya uzazi yanaweza kupelekea tatizo hili. (3) Dalili za mwanzo za kukaribia kufunga kuzaa (Menopause) Hii huchangia kwa asilimia chache na kwa sasa halielezeki kisawasawa. Kwamba wanawake wengi wanapokaribia umri wa kuacha kuzaa kuanzia miaka 40 kwenda juu baadhi yao hutokewa na tatizo la kutunga mayai ambayo hayajakomaa vema. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao mapema kabla ya umri uliozoeleka yaani miaka 40 kwenda juu. Kwa sababu hiyo inadhaniwa kwamba uwezo wao wa asili katika kuzalisha mayai unakuwa umepunguwa na wengi wao huwa ni wale walikuwa wakijihusisha zaidi na michezo ya kukimbia au wale wenye historia ya muda mrefu ya kuwa na uzito pungufu na wafanyaji sana wa mazoezi. Tatizo hili pia linaweza kuwa ni la kurithi. (4) Matatizo kwenye kijishimo yai (follicle) katika ovari: Ingawa kwa sasa bado hili nalo halielezeki, hiki kijishimo yai kwa kitaalamu kinajulikana kama ‘’follicle’’ ndicho hupasuka na yai kutoka. Kuna baadhi ya kina mama wanapata dalili za kijishimo yai kutokupasuka “unruptured follicle syndrome” na matokeo yake kila mwezi mama anazalisha yai kama kawaida lakini hiki kijishimo yai kinashindwa kupasuka. Hivyo yai linabaki ndani ya ovari na utungaji wa mimba unashindwa kufanyika. Kinachosababisha ufanyaji kazi dhaifu wa mirija ya uzazi (Fallopian Tubes): Magonjwa katika mirija ya uzazi yanahusika na ugumba kwa karibu ya asilimia 25 ya wanawake wote wagumba. Hali yenyewe inatofautiana toka kwa mmoja hadi kwa mwingine kutoka kugandana au kunatana kidogo hadi kuzibika kabisa kwa mirija. Matibabu ya mirija iliyozibika huhusisha upasuaji au usafishaji wa mwili kwa kula vyakula na vinywaji maalum kwa muda wa majuma kadhaa. Sababu kubwa zinazopelekea kuzibika au kunatana kwa mirija ya uzazi ni pamoja na zifuatazo: (A) Maaambukizi Maambukizi katika njia ya uzazi ambayo yamesababishwa ama na bakteria au virusi na ambayo kwa kawaida ni magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya tendo la ndoa, maambukizi haya kwa kawaida husababisha muwasho au kuungua na kupelekea makovu na uharibifu. Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na mengineyo yanaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa wanawake wengi hasa ikiwa hayatatibiwa mapema. (B) Magonjwa yasiyo ya kawaida Magonjwa yasiyo ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa kidole tumbo (appendicitis) na uvimbe katika utumbo mpana (colitis), magonjwa ambayo husababisha muwasho au kuungua chini ya uvungu wa utumbo mkubwa na kuiathiri mirija ya falopiani na kama matokeo yake makovu na kuzibika kwa mirija ya uzazi hutokea. (C) Upasuaji uliopita Upasuaji una chukua nafasi kubwa katika kusababisha ugumba kutokana na matokeo yake ya kusababisha magonjwa ya mirija ya uzazi na uharibifu utokanao na huo upasuaji. Upasuaji katika utumbo mkubwa unaweza kupelekea kunatana au kugandana kwa mirija ya uzazi kutakakopelekea mayai kushindwa kusafiri kirahisi katika mirija hiyo ya uzazi. (D) Mimba kutungwa nje ya mji wa uzazi: Hii ni wakati mimba inapotungwa katikati ya mirija ya uzazi yenyewe. Katika hali kama hii hata kama kutatokea bahati kiasi gani bado kunaweza kusababisha uharibifu katika mirija na hali hii ni moja ya hali mbaya sana kiafya na kimaisha. (E) Hali ya kurithi Kwa nadra au kwa asilimia fulani ndogo baadhi ya wanawake huzaliwa na hali ya kuwa na mirija isiyo ya kawaida kwa uzazi na kwa kawaida hali hii huambatana na mji wa uzazi usio wa kawaida pia. . (5) Sababu za kitabia: Inajulikana wazi kwamba baadhi ya tabia na namna tunavyoishi kunaweza kupelekea wanandoa wakashindwa kupata mtoto. Kwa bahati nzuri nyingi kama si zote ya hizo tabia zinaweza kurekebishika au kuachwa kabisa na kupelekea siyo tu kuwa na uwezo wa kuzaa bali pia kuwa na afya nzuri kwa ujumla. Sababu hizo za kitabia ni pamoja na zifuatazo: Lishe na mazoezi Ili mfumo wa uzazi uwe na uwezo mzuri unahitaji vitu viwili mhimu, lishe kamili na mazoezi. Wanawake wenye uzito uliozidi sana au wenye uzito pungufu sana wanaweza wakapatwa na tatizo la kutopata ujauzito kirahisi. Uvutaji sigara Uvutaji wa sigara una mchango mkubwa na ugumba. Uvutaji sigara husababisha uzarishwaji wa mbegu chache kwa mwanaume (lower sperm count) kwamba mwanaume anatoa mbegu chache sana ama pungufu wakati huo huo uvutaji sigara huchangia katika tatizo la kutoka kwa mimba, kuzaa kabla ya miezi 9 (njiti), na kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo kwa wanawake. Unywaji pombe Unywaji pombe kupita kiasi una mchango mkubwa sana katika ugumba na hii hata ikitokea mama akapata ujauzito kama bado anaendelea kunywa pombe inaweza kupelekea matatizo hata kwa mtoto mtarajiwa. Unywaji pombe pia huchangia uzarishwaji wa mbegu chache kwa wanaume. Madawa ya kulevya Utumiaji a madawa ya kulevya kama bangi na mengine ya kujidunga kwa sindano kunaweza kuwa sababu ya kuzalisha mbegu chache kwa wanaume. Utumiaji wa dawa za kulevya kama ‘Cocaine’ kwa mama mjamzito kunaweza kusababisha mtindio wa ubongo na matatizo katika figo kwa mtoto mtarajiwa. Matumizi ya madawa ya kulevya inafaa yaepukwe wakati wa kutafuta ujauzito na wakati wa ujauzito. Utowaji mimba Utowaji mimba wa mara kwa mara pia unahusika sana na tatizo la ugumba kwa karibu ya asilimia 20. Utowaji mimba unaweza kusababisha makovu katika mji wa uzazi na hata kuharibika kabisa kwa mji wa uzazi ikiwa utowaji huo haukufanyika kitaalamu au unafanyika mara kwa mara. (6) Sababu za ugumba za kimazingira: Uwezo wa kushika ujauzito unaweza pia kuathiriwa kutokana na kuwa karibu na baadhi ya kemikali au sumu katika maeneo ya kazi au makazi. Vitu viwezavyo kusababisha mabadiliko, dosari za kuzaliwa, utokaji mimba, au utasa huitwa ‘Sumu kwa mfumo wa uzazi’. Kamikali zifuatazo zinahusishwa na ugumba au utasa: Risasi (Lead) Kuwa karibu na kemikali au sumu zinazounda risasi kunaweza kuwa sababu ya ugumba. Risasi hupelekea kuzalishwa kwa mbegu zisizo za kawaida kwa wanaume zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘teratospermias’ na inafikirika pia kuhusika na utokaji mimba kusiko kwa asili (artificial abortion). Baadhi ya matibabu na madawa ya hospitalini Kuwekwa kwenye matibabu yanayohusisha mionzi (x-rays), mionzi ya kawaida au hata ile ya kutibia kansa (chemotherapy), kunaweza kusababisha matatizo katika uzarishwaji wa mbegu kwa mwanaume na wakati huo huo kuchangia kwa sababu kadhaa zinazopelekea kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Pia matumizi ya dawa za kuzuia ujauzito kwa muda mrefu yamekuwa yakihusishwa na ugumba kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado kuna mjadala mkubwa katika hili. Ethylene Oxide Hii ni kemikali inayotumika kusafishia vifaa vya upasuaji, pia hutumika katika kutengeneza baadhi ya sumu za kuua wadudu. Ethylene oxide inaweza kupelekea matatizo katika uzazi hasa katika miezi ya mwanzo mwanzo ya ujauzito na inahusishwa sana na tatizo la utokaji mimba katika miezi ya mwanzo ya ujauzito (early miscarriage). Dibromochloropropane (DBCP) Hii pia ni kemikali au dawa inayotumika katika kuua wadudu, ikiwa unafanya nayo kazi kila mara inaweza kusababisha kutungwa kwa mayai yasiyokomaa vizuri, kuelekea mapema kwa ukomo wa kutokuzaa kabla hata ya miaka 40 au 45 (early menopause) na kadharika. (7) Sababu zingine zinazoweza kusababisha ugumba kwa mwanamke: Karibu asilimia 10 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya mji wa uzazi usio wa kawaida (abnormal uterus). Hali zingine ni pamoja na uvimbe katika kizazi, kugandana au kunatana kwa mji wa uzazi na mirija ya uzazi. Karibu asilimia 3 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya matatizo ya ute usio wa kawaida katika mlango wa kizazi (femaleís cervical mucus). Ute ute huu unahitaji kuwa na hali fulani maalumu kwa mbegu za kiume kuweza kuogelea kirahisi katikati yake. Chanzo kikubwa cha tatizo hili ni usawa usio sawa wa homoni za kike ambapo homoni ya uzazi ya kike iitwayo ‘estrogen’ yaweza kuwa ni chache sana au homoni nyingine iitwayo ‘progesterone’ yaweza kuwa ni nyingi sana tofauti na inavyohitajika. Vitu vya kuepuka kwa mtu mwenye tatizo la ugumba: ChipsiVinywaji baridiKaffeinaNyama nyekunduVilevi ... Read More
NAOMBA MSIJE KWENYE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YANGU, NJOONI KWENYE MSIBA WANGU. Baada ya kukaa kwenye ndoa takriban miaka 10 kasoro miezi miwili wakafanikiwa kupata watoto wawili wa kwanza angel na wa pili baraka. jamaa akakaa na mkewe wakapanga mipango mizito sana kuhusiana na tukio lingine zito baada ya tukio lao la harusi.yaani kusheherekea miaka 10 ya ndoa yao. Lakini akajisemea, ngoja nipime kiwango cha uaminifu alichonacho mke wangu kabla ya hiyo sherehe haiwezekani kwamba kuna usalama kabisa maana ktk miaka yote nimekuwa MTU wa kazini,safarini in short sina muda mwingi wa kukaa na familia yangu....na kama atavuka hili jaribu basi naweka nadhiri mbele za mbingu nitamtafutia zawadi nzuri ambayo hajawahi kuona na hatokuja kuisahau Akawaambia marafiki zake nataka nifanye party ya kusheherekea miaka kumi ya ndoa yangu nahitaji kampani yenu,walifurahi sana marafiki zake hususani wafanyakazi wenzake. Kamati zikaundwa mara moja,lakini baba angel aliendelea na upelelezi wa kumjaribu mkewe pasipo kujua huyo mkewe aitwaye Elizabeth. Mama angel aliendelea kualika marafiki zake,wazazi wake wakawa wanasubiria kwa hamu kubwa hilo tukio wakimbariki mwenyezi Mungu kwa kuendelea kustawisha ndoa ya mtoto wao.huku asijue mmewe ana nini ndani ya moyo wake. Baba angel akafanya usajili wa line mpya ya tigo asiyoijua mkewe. Akasajili kwa kubuni jina la #Asajile_mwasilu ambaye alikuwa anahisi anatembea na mkewe maana mara kadhaa alishazikuta msg za ajabu kwenye simu ya mkewe kama za mtu na mpenzi wake na alipoichunguza kwenye tigo pesa usajili ukaonyesha jina la Asajile mwasilu. akawa akichat na mkewe mara kwa Mara, kupitia hiyo namba mpya...... siku moja mkewe akaangalia hiyo namba kwenye usajili akaona jina la "Asajile mwasilu" waooooo ooh my dear,akafurahi basi mwenyewe! Akaamua kupiga simu,mumewe hakupokea akakata akamwambia nitext niko mahali hatutaweza kuelewana. Kumbuka Wakati huo mumewe yupo kazini........akamwambia tuendelee kuchat My nikupendae uko wapi mpenzi wangu nikufuate sasa hivi,maana nilivyofrahi kuona SMS yako mungu anajua!namba zako zote baba angel alifuta kwenye simu yangu,na wewe ndio hujanitafuta tena..... baba angel akajibu, we taratibu,si unajua umeolewa wewe unifuate wapi? mumeo alinipigiaga simu kwamba angenifanya kitu kibaya Sana iwapo ningeendelea kuwa na mawasiliano na wewe basi nikaogopa mwenyewe ndio maana nikajikaliaga kimya. Ooh pole my sweet, ndio walivyo wanaume wasiojitambua hawa,yaani yeye anadhani anaweza kunichunga eti! Anasahau kwamba uanaume sio kuchunga mke uanaume ni kumhudumia vzur mkeo kitandani huo ndio ulinzi tosha. Yaani kusema ule ukweli,sijawahi kupata mwanaume wa kunihudumia vile nitakavyo zaidi yako,uko wapii? Mama angel akaendelea kufunguka. Mh!baba angel akajikuta anaishiwa pozi vibaya mno huku mapigo ya moyo yanayoambatana na ghadhabu yakikitesa kifua chake ambacho hata pumzi ilikuwa ni shida kutoka hakuamini kwamba huyo anaechat naye ni mkewe.......akamjibu kwa kicheko cha uongo Hahaaaaaa ina maana unataka kusema jamaa hayuko vzur kitandani?? Na vipi angel hajambo??? Ndio maana nakuuliza uko wapi this time nikufate?maana umelandisha mtoto mpaka sio vizuri,wewe mwanaume una damu kali,wakati mwingine mpaka naona aibu kumwita mume wangu baba angel maana ukweli Mimi ndio naujua....ila yeye hajui kitu anajua ni wake. Baba angel akawazaa wee huku mipango ya sherehe akiona ikiyeyuka taratibu kadri alivyokuwa akiendelea kuchati na mkewe... Akakaa katibu dakika 10 bila kusema chochote akiwaza je ni kweli angel sio wangu???mh! Hawa wanawake vipii?? akatazama saa yake akaona ni saa 8 za mchana akajisemea pale ofsini "hivi mke wangu ana roho mbaya kiasi hiki Kumbe nalea mtoto asie wangu?? Akafungua kwenye gallery akatazama picha za mtoto wake huyo mzur akaendelea kujipa moyo......... Akamrudia mkewe akamwambia Wacha buana uko naye angel hapo?? Mama angel akajibu yes, jamaa akajibu tena "Mi mwenyewe nimekumiss sana na nimemmis sana mwanangu natamani nimwone tu lakini naangalia usawa wa mfuko hauko sawa sana...... Mkewe akajibu hebu ngoja nipe dakika sifuri......... Haraka haraka mama angel akampigia simu mumewe kwa namba yake ya siku zote. "Samahani baby unamkumbuka neema msimamizi wa send off yangu?? Jamaa kwa unyonge huku akijikaza kusikiliza uongo wa mkewe akajibu ndio namkumbuka amefanya nini? Nilikuwa nampa taarifa ya party yetu kumbe alipata ajar yuko nyumbani, sasa nimeona wacha nikamwangalie kabisa sasa hivi naomba hela kidogo..........jamaa akamtumia tsh. laki moja na nusu na msg juu akimhimiza kuwahi kurudi. Vipi uko na angel hapo?? Mama akajibu ndio nikupe uongee naye?? basi akampa simu wakaongea na baba yake...... Akachukua simu mama yake akamwambia mumewe " halafu naenda nae angel mara moja! Jamaa akajibu hamna shida. Upesi mama angel akamwandikia sms anaedhani ni Asajile mchepuko wake kumbe ni mumewe huyo huyo akamtext sasa enda mahali tafuta guest nzur nakutumia elfu 80 sasa hivi Jamaa akajibu waooo ndio maana sijawahi kuacha kukupenda Elizabeth wangu.....basi ntakwambia nikipata. Ila uje na angel Baada ya dakika kama 30 Elizabeth akawa amejiandaa na kumuandaa mwanaye huku akimuahidi house girl kana kwamba atarudi saa 2 usiku....... Jamaa mida kama ya saa 10 jioni akamtext wife njoo hapa...........kuna Lodge inaitwa shelisheli unaijua?wife akaitikia yes.....basi njoo ni chumba namba 6 ghorofa ya 6 ila usimwache mtoto pls. Muda wote huo baba angel alikuwa ameshika kitambaa mkononi maana haipiti sekunde asipojifuta machozi machoni alikuwa akilia tu kwa jinsi alivyokuwa akimpenda mkewe.akajifikiria kuwa ,kwanini Mungu alimficha hilo jambo lililo moyoni mwa mkewe??kwanini Mungu ameruhusu alee mtoto asiye wake?? Kufika hapo Ni kama mwendo wa dakika 20 kwa toyo,basi Mama angel akaona achukue hiyo bodaboda awahi na kweli akawa amewahi.......akaingia hiyo hotel akaenda sehemu ya lift akafika chumba gorofa ya 6 akaenda chumba namba 6 Taratibu akafungua mlango mgongoni akiwa na angel akakuta hakuna mtu kumbe jamaa kaingia kidogo uani Dakika mbili hivi jamaa akawa anatokea kutoka uani Ile kufungua mlango Mama angel hakuamini alichokikuta maana tayari kwenye ubongo wake alikuwa amemtengeneza Asajile.....lakini sio Asajile aliyemkuta........ aligongana USO kwa USO na mumewe wanaetarajia kufanya sherehe ya ndoa yao wiki kama mbili zijazo. Mama angel alipiga yowe yesuuuuu huku akitaka kukimbia kutoka nje........mumewe akamkamata mkono wake akamtuliza na kumwambia "usiogope uko kwenye mikono salama ya baba wa watoto wako kaa utulie! Ooh my god sijui nimefanya nini Mimi!?mkewe alijisemea huku akionyesha kuchanganyikiwa. Wakati huo angel yuko kwa baba yake akistaajabu kuhusu kinachoendelea......... Ilimchukua kama dakika 20 mpaka kutulia mama angel Mumewe akaongea maneno mafupi tu..... MKE WANGU, USIJE UKADHANI MIMI NIPO GIZANI KABISA NISIJUE HATA HATA KIDOGO ULICHONACHO MOYONI MWAKO. AKAONGEA KILUGHA KUMKWEPESHA MTOTO ASIELEWE......LAKINI AKIWA NA MAANA KWAMBA TANGU HUYU MTOTO AMEZALIWA,MOYONI MWANGU NILIJUA SIO MTOTO WANGU,HATA WIFI ZAKO, shemeji zako WAZAZI WANGU WALINIAMBIA HILI JAMBO,NA LISEMWALO LIPO.......mama angel akazidi kupigwa butwaa Akaendelea kumsimulia mkewe....... SIKU MOJA NILIOTA NDOTO MTOTO ANAUMWA,NA TULIPOENDA HOSPITALI ETI KATIKA VIPIMO IKAONYESHA WANAPIMA DNA NIKAKASIRIKA,MBONA MNAMPIMA DNA WAKATI HUYU NI MGONJWA ANAHITAJI VIPIMO VINGINE? YULE DR AKANIAMBIA NITULIE KWANI ANAJUA AFANYACHO NIIKAMKA,NILIPOMPIGIA SIMU MTUMISHI WA MUNGU MMOJA AKANIAMBIA MTOTO SI WANGU LAKINI NISICHUKUE UAMUZI WOWOTE MBAYA BADALA YAKE NIENDELEE KULEA MAANA MALIPO NI KWA MUNGU. Elizabeth, umenitonesha tena kidonda mke wangu, Asante umemleta angel kwa baba yake Asajile lakini hayupo,bado nabaki Mimi ndiye baba yake Mungu atanilipa kwa uaminifu wangu......nashkur kwa uongo wako,asante kwa hela uliyonitumia ya chumba, nataka nikwambie nimefanya kama ulivyonipa maelekezo....... Wakati huo mama angel analia tu hakuna mfano,anaona hata aibu kusema nisamehe,alichojibu ktk kulia kwake ni "Naona nafsi yangu inahukumiwa mno kuliko maneno unayoniambia.....najua mwisho wa ndoa yangu ni hapa hakuna jinsi,siwezi kujitetea mume wangu!naiona jehanamu hii hapa,ninauona ubaya wa kufuga dhambi sasa,hapa ndio naamini hakuna siri duniani,haiwezekani ukafanya kitu ukajua haitajulikana. Niko tayari uniambie chochote na sitapinga,nimeaibika mbeke ya mwanangu Mwanangu nimeaibika mbele ya mume wangu anipendaye na nimeaibika mbele za mbingu na dunia..........nitaficha wapi USO wangu mie?? Jamaa akamwambia mkewe najuta kukujaribu mke wangu najuta kuupima uaminifu wako,ila namshukuru Mungu amenipa kifua kikubwa cha kukabiliana na mambo MAZITO. Lakini wakati mwingine namshukuru Mungu tu maana kila jambo lina makusudi....... Wakatoka pale hotelini wakaingia ndani ya gari ambayo baba angel alikuja nayo wakarudi nyumbani. Usiku mzima mwanamke hakulala usingizi akidhani labda mumewe angemuua hata mtoto........asubuhi kulipokucha jamaa alipowahi kazini mwanamke akaanza kupitia message walizokuwa wanachat na mmewe akaona ni kama yupo uchi tu.......akaenda kununua vidonge duka la dawa baridi akameza akafa huku akiacha ujumbe usemao KUHUSU KUFA KWANGU ASILAUMIWE MTU YEYOTE ILA NILAUMIWE MIMI NAPENDA NIWEKE HADHARANI KILA KITU,KUHUSU MTOTO WANGU ANGEL SIO WA MUME WANGU,JAPO KWA KIPINDI CHOTE ALIKUWA ANAJUA NI WAKE.......BABA YAKE ANAITWA ASAJILE MWASILU......ALINIPA MIMBA NIKIWA NDANI YA NDOA YANGU....... NATUBU KWA WAZAZI WANGU NA WAZAZI WA MUME WANGU MNIOMBEE NIENDAKO NIPUNGUZIWE ADHABU YA KABURI,MWISHO NAWAOMBA MSIJE KWENYE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YANGU,NJOONI MSIBANI. Mwisho sitaki kueleza nini kilitokea kwenye mazishi na msiba kwa ujumla wake Lakini jamaa anaendelea kulea mtoto asiye wake na mtoto wake. Kwenye mazishi alisikika akilia akisema najuta kwanini nilipima uaminifu na msimamo wa mke wangu,yamkini mpaka leo angekuwa hai............... BAADA YA MAZISHI MAKABURINI BABA ANGEL ALIMPELEKEA KARATASI KAKA YAKE AMBAYE NDIYO ANGETOA SHUKRANI KWA WATU NA MATANGAZO MACHACHE YA NINI KINGEENDELEA BAADA YA PALE,BASI AKASOMA ILE KARATASI KWAMBA "TUNAPENDA KUWATAARIFU KWAMBA ILE SHEREHE YA MIAKA 10 YA NDOA YA BABA ANGEL PAMOJA NA MKEWE AMBAYE NI MAREHEMU SASA ILE TAREHE IPO PALEPALE ATAFANYA NA WATOTO WAKE ITAAMBATANA NA KUMSHUKURU MUNGU KATIKA YOTE MAANA IMEANDIKWA "SHUKURUNI KWA KILA JAMBO"........... Siku ya sherehe yenyewe watu walifika kwa wingi sana hamna mfano na miongoni mwao ni baba angel original yaani Asajile....... Itaendelea next time Ila jueni kuwa shetani yuko kaz ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: