Home → ushauri
→ MAMBO 10 AMBAYO NI SUMU KATIKA MAPENZI

KATIKA harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi.
Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi.
1. WIVU WA KUPINDUKIA
Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomwona mpenzi wako akizungumza na mwanamume mwingine, au anapotoka na marafiki zake wa kike, au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa tayari umekunywa sumu ya mapenzi.
Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana. Kama kweli unataka mpenzi wako akupende kwa dhati, mwoneshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda wao mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu.
2. KUTOMWACHIA NAFASI MPENZI
Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumwona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa peke yake kwa ajili ya mambo yake binafsi.
Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, lakini kwa hakika hiyo si ishara njema ya mapenzi ya kudumu. Hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka. Kwa hiyo, mpe mpenzi wako fursa ya kupumua. Namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kutaka kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu hiyo itaisha.
3. KUMWAMULIA MPENZI MAMBO YAKE
Unaweza kujikuta ukisukumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini wakati gani, akutane na nani na kwa wakati gani au ale nini. Ukiona hivyo, fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia.
Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa jinsia, hakuna mwanamke ambaye angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake. Kama ilivyodokezwa hapo juu, kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu. Kama utataka kumpangia kila kitu ni wazi kuwa utaishia kuishi peke yako.
4. KUMUULIZA MPENZI MASWALI
Iwapo utajikuta ukimuuliza mpenzi wako maswali mengi yanayoonesha wasiwasi wako kuhusiana na mwenendo wake, fahamu kuwa kuna tatizo na tatizo hilo lisipopatiwa ufumbuzi utakuwa mwanzo wa mwisho wa uhusiano wenu.
Mwanamke angependa umuulize maswali ya kawaida kuhusiana na jinsi siku yake ilivyokuwa na kama marafiki zake hawajambo au la, lakini kila jambo lina mpaka wake. Mwanamke hatarajii kuwa kila mnapokutana atakuwa kama ameingia kwenye chumba cha mtihani au usaili wa kazi.
5. KUTOAMINI ANACHOKWELEZA MPENZI
Wakati mwingine watu hushindwa kuwaamini wenzao, lakini kwa sababu ambazo ni za msingi, lakini kuna wakati ambapo mtu hushindwa kumwamini mwenzake bila sababu yoyote ya msingi, au kwa sababu zisizo sahihi, kisingizio kikiwa ni mapenzi.
Kuna tatizo la kisaikolojia la kujishuku au kuwashuku wenzako. Hili ni jambo ambalo linaweza kukuharibia mustakabali wako katika mapenzi, maana husababisha kujengeka kwa mazingira ya kutokuaminiana. Ili uweze kwenda sanjari na mpenzi wako, amini kila anachokweleza hadi pale utakapokuwa na sababu za msingi za kutokumwamini. Na hata unapokuwa umelithibitisha jambo, endelea kuwa katika uhalisia wako.
6. KUACHA HOBI, MARAFIKI
Mahusiano ya kimapenzi mara nyingi huhusisha kila mmoja kuacha baadhi ya mambo yake kwa ajili ya mwenzake. Hata hivyo, lengo ni kuweka tu uwiano wa mahitaji, si kuacha kila kitu ulichokuwa nacho kwa ajili ya mwenzako, ama kwa shinikizo, au kwa kulewa penzi.
Iwapo utabaini kuwa marafiki zako sasa wamekuwa ni marafiki zako wa zamani na hobi zako zimebaki tu katika kumbukumbu japo kwa hakika bado unahisi mapenzi katika hobi hizo, basi tambua kuwa huyo mrembo wako amekunywesha sumu ya penzi na sasa huwezi hata kuitumia vema mantiki yako.
Mbaya zaidi, iwapo utabaini kuwa marafiki zako wapya ni marafiki wa siku zote wa mpenzi wako na hobi zako ni zile za mpenzi wako, basi tambua kuwa huna tena nafsi yako, bali umejisalimisha mzima mzima kwa mpenzi wako. Lakini msemo mmoja wa hekima unatwambia usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja. Yamkini unaelewa.
7. KUKUBALI KUPELEKESHWA
Pengine unakumbuka kuwa kuna nyakati ambapo ulikuwa na uwezo wa kujikita katika jambo moja na kulifanya kwa umakini, huku ukiwa pia mwerevu, mjanja na unayejisimamia, lakini leo unayeyuka kirahisi tu kama barafu iliyowekwa juani! Hii ni hatari kwa mustakabali wa maisha yako.
Mbaya zaidi ni pale utakapoiacha kazi yako inayokulipa vizuri na kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako. Ukifika hali hii ujue wewe mwenyewe kuwa hapo hakuna mwanamume.
8. UTAYARI WA KUFA KWA AJILI YAKE
Umewahi kujisikia kuwa na utayari wa kufa kwa ajili ya mpenzi wako? Kama jibu ni “ndiyo”, basi fahamu kwa hakika kuwa hayo uliyo nayo si mapenzi bali ni upumbavu. Pengine huku ndiko kunywesha sumu ya mapenzi. Kwa hakika, hakuna mwanamke ambaye anastahili kumfanya mwanamume yeyote kufa kwa ajili yake.
Yamkini wanaume wanaolengwa katika makala haya si wavulana wanaosoma sekondari, waliobalehe majuzi, ambao wakipenda au kupendwa hujiona kama wako katika sayari yao. Mwanamume aliyepevuka hujiamini na hayaweki maisha yake yote mikononi mwa mwanamke, hata kama mwanamke huyo angekuwa ndiye mrembo wa dunia.
Iwapo, ama kwa ujinga au kwa kufahamu umewahi kumwambia mpenzi wako: “Ukiniacha nitajiua,” na ukawa unaamini hivyo kabisa, basi yamkini unahitaji kutafuta msaada wa ushauri nasaha, maana kwa hakika umepotoka.
9. MUDA WOTE UNAWASILIANA NAYE
Vijana wa siku hizi ni watumiaji wazuri sana wa simu, lakini iwapo utabaini kuwa asilimia kubwa ya muda wako unautumia ama kwa kuongea au kuwasiliana kwa ujumbe mfupi na mpenzi wako, basi fahamu kuwa kuna tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka.
Kumbuka kuwa mapenzi hayachukui nafasi ya kila kitu. Yamkini huyo mpenzi wako amekukuta unaishi na kuna mambo ya muhimu ya kufanya. Hebu achana na simu kwanza ufanye mambo ya muhimu kuhusiana na maisha yako. Kama mpenzi wako hakwelewi katika hili basi hakufai.
10. NDUGU ZAKE WANAKUFUATILIA
Iwapo utabaini kuwa marafiki, ndugu na jamaa za mpenzi wako wanamtonya mpenzi wako kuhusiana na kile wanachokiita mwenendo wako mbaya, usipuuze hali hii. Kuna uwezekano mkubwa kuwa watu hawa wanayo sababu ya kuwa na wasiwasi na mwenendo wako, kwa hiyo jichunguze na kuangalia jinsi unavyoenenda.
Hata hivyo, jambo hili si ishara njema ya mustakabali mwema wa uhusiano wenu. Iwapo mpenzi wako ataweka watu wake wakufuatilie, maana yake halisi ni kwamba hakuamini. Katika hali kama hii, haitarajiwi kuwa mustakabali wa uhusiano wenu utakuwa mzuri, kwani kutakuwa na uingilizi mwingi wa ndugu, jamaa na marafiki zake. Unaweza kukubali kuendelea kuishi katika hali hii kwa kisingizio cha mapenzi, lakini ukweli ni kwamba hayatakuwa mapenzi bali karaha.
KUWA MAKINI
Kama unavyoona, hizi ni baadhi tu ya dalili kuwa mapenzi yako kwa mwanamke sasa yanaelekea katika ulevi, mithili ya ule wa dawa za kulevya. Jambo moja la kukumbuka ni kwamba kweli mapenzi ni kitu kizuri, lakini pia mapenzi yanahitaji kuwa jambo linaloashiria mustakabali mwema kwa wahusika wawili. Yakiwapo mambo haya kumi hauwezi kuwapo mustakabali mwema katika mapenzi.
MAMBO 10 AMBAYO NI SUMU KATIKA MAPENZI  KATIKA harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi. Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi. 1. WIVU WA KUPINDUKIA Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomwona mpenzi wako akizungumza na mwanamume mwingine, au anapotoka na marafiki zake wa kike, au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa tayari umekunywa sumu ya mapenzi. Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana. Kama kweli unataka mpenzi wako akupende kwa dhati, mwoneshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda wao mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu. 2. KUTOMWACHIA NAFASI MPENZI Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumwona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa peke yake kwa ajili ya mambo yake binafsi. Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, lakini kwa hakika hiyo si ishara njema ya mapenzi ya kudumu. Hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka. Kwa hiyo, mpe mpenzi wako fursa ya kupumua. Namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kutaka kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu hiyo itaisha. 3. KUMWAMULIA MPENZI MAMBO YAKE Unaweza kujikuta ukisukumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini wakati gani, akutane na nani na kwa wakati gani au ale nini. Ukiona hivyo, fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia. Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa jinsia, hakuna mwanamke ambaye angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake. Kama ilivyodokezwa hapo juu, kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu. Kama utataka kumpangia kila kitu ni wazi kuwa utaishia kuishi peke yako. 4. KUMUULIZA MPENZI MASWALI Iwapo utajikuta ukimuuliza mpenzi wako maswali mengi yanayoonesha wasiwasi wako kuhusiana na mwenendo wake, fahamu kuwa kuna tatizo na tatizo hilo lisipopatiwa ufumbuzi utakuwa mwanzo wa mwisho wa uhusiano wenu. Mwanamke angependa umuulize maswali ya kawaida kuhusiana na jinsi siku yake ilivyokuwa na kama marafiki zake hawajambo au la, lakini kila jambo lina mpaka wake. Mwanamke hatarajii kuwa kila mnapokutana atakuwa kama ameingia kwenye chumba cha mtihani au usaili wa kazi. 5. KUTOAMINI ANACHOKWELEZA MPENZI Wakati mwingine watu hushindwa kuwaamini wenzao, lakini kwa sababu ambazo ni za msingi, lakini kuna wakati ambapo mtu hushindwa kumwamini mwenzake bila sababu yoyote ya msingi, au kwa sababu zisizo sahihi, kisingizio kikiwa ni mapenzi. Kuna tatizo la kisaikolojia la kujishuku au kuwashuku wenzako. Hili ni jambo ambalo linaweza kukuharibia mustakabali wako katika mapenzi, maana husababisha kujengeka kwa mazingira ya kutokuaminiana. Ili uweze kwenda sanjari na mpenzi wako, amini kila anachokweleza hadi pale utakapokuwa na sababu za msingi za kutokumwamini. Na hata unapokuwa umelithibitisha jambo, endelea kuwa katika uhalisia wako. 6. KUACHA HOBI, MARAFIKI Mahusiano ya kimapenzi mara nyingi huhusisha kila mmoja kuacha baadhi ya mambo yake kwa ajili ya mwenzake. Hata hivyo, lengo ni kuweka tu uwiano wa mahitaji, si kuacha kila kitu ulichokuwa nacho kwa ajili ya mwenzako, ama kwa shinikizo, au kwa kulewa penzi. Iwapo utabaini kuwa marafiki zako sasa wamekuwa ni marafiki zako wa zamani na hobi zako zimebaki tu katika kumbukumbu japo kwa hakika bado unahisi mapenzi katika hobi hizo, basi tambua kuwa huyo mrembo wako amekunywesha sumu ya penzi na sasa huwezi hata kuitumia vema mantiki yako. Mbaya zaidi, iwapo utabaini kuwa marafiki zako wapya ni marafiki wa siku zote wa mpenzi wako na hobi zako ni zile za mpenzi wako, basi tambua kuwa huna tena nafsi yako, bali umejisalimisha mzima mzima kwa mpenzi wako. Lakini msemo mmoja wa hekima unatwambia usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja. Yamkini unaelewa. 7. KUKUBALI KUPELEKESHWA Pengine unakumbuka kuwa kuna nyakati ambapo ulikuwa na uwezo wa kujikita katika jambo moja na kulifanya kwa umakini, huku ukiwa pia mwerevu, mjanja na unayejisimamia, lakini leo unayeyuka kirahisi tu kama barafu iliyowekwa juani! Hii ni hatari kwa mustakabali wa maisha yako. Mbaya zaidi ni pale utakapoiacha kazi yako inayokulipa vizuri na kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako. Ukifika hali hii ujue wewe mwenyewe kuwa hapo hakuna mwanamume. 8. UTAYARI WA KUFA KWA AJILI YAKE Umewahi kujisikia kuwa na utayari wa kufa kwa ajili ya mpenzi wako? Kama jibu ni “ndiyo”, basi fahamu kwa hakika kuwa hayo uliyo nayo si mapenzi bali ni upumbavu. Pengine huku ndiko kunywesha sumu ya mapenzi. Kwa hakika, hakuna mwanamke ambaye anastahili kumfanya mwanamume yeyote kufa kwa ajili yake. Yamkini wanaume wanaolengwa katika makala haya si wavulana wanaosoma sekondari, waliobalehe majuzi, ambao wakipenda au kupendwa hujiona kama wako katika sayari yao. Mwanamume aliyepevuka hujiamini na hayaweki maisha yake yote mikononi mwa mwanamke, hata kama mwanamke huyo angekuwa ndiye mrembo wa dunia. Iwapo, ama kwa ujinga au kwa kufahamu umewahi kumwambia mpenzi wako: “Ukiniacha nitajiua,” na ukawa unaamini hivyo kabisa, basi yamkini unahitaji kutafuta msaada wa ushauri nasaha, maana kwa hakika umepotoka. 9. MUDA WOTE UNAWASILIANA NAYE Vijana wa siku hizi ni watumiaji wazuri sana wa simu, lakini iwapo utabaini kuwa asilimia kubwa ya muda wako unautumia ama kwa kuongea au kuwasiliana kwa ujumbe mfupi na mpenzi wako, basi fahamu kuwa kuna tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka. Kumbuka kuwa mapenzi hayachukui nafasi ya kila kitu. Yamkini huyo mpenzi wako amekukuta unaishi na kuna mambo ya muhimu ya kufanya. Hebu achana na simu kwanza ufanye mambo ya muhimu kuhusiana na maisha yako. Kama mpenzi wako hakwelewi katika hili basi hakufai. 10. NDUGU ZAKE WANAKUFUATILIA Iwapo utabaini kuwa marafiki, ndugu na jamaa za mpenzi wako wanamtonya mpenzi wako kuhusiana na kile wanachokiita mwenendo wako mbaya, usipuuze hali hii. Kuna uwezekano mkubwa kuwa watu hawa wanayo sababu ya kuwa na wasiwasi na mwenendo wako, kwa hiyo jichunguze na kuangalia jinsi unavyoenenda. Hata hivyo, jambo hili si ishara njema ya mustakabali mwema wa uhusiano wenu. Iwapo mpenzi wako ataweka watu wake wakufuatilie, maana yake halisi ni kwamba hakuamini. Katika hali kama hii, haitarajiwi kuwa mustakabali wa uhusiano wenu utakuwa mzuri, kwani kutakuwa na uingilizi mwingi wa ndugu, jamaa na marafiki zake. Unaweza kukubali kuendelea kuishi katika hali hii kwa kisingizio cha mapenzi, lakini ukweli ni kwamba hayatakuwa mapenzi bali karaha. KUWA MAKINI Kama unavyoona, hizi ni baadhi tu ya dalili kuwa mapenzi yako kwa mwanamke sasa yanaelekea katika ulevi, mithili ya ule wa dawa za kulevya. Jambo moja la kukumbuka ni kwamba kweli mapenzi ni kitu kizuri, lakini pia mapenzi yanahitaji kuwa jambo linaloashiria mustakabali mwema kwa wahusika wawili. Yakiwapo mambo haya kumi hauwezi kuwapo mustakabali mwema katika mapenzi.
Artikel Terkait
🎀MVUMBIKO WA KITUMBUWA 🎀 Mwanamke mvumbiko bibi 👌🏼 Unapomaliza period ukiosha ushapanga leo ni siku ya shoo unatakiwa kuvumbika KITUMBUA chako na Vitu Vya asili ili kuiweka k yko ktk mvuto wa hali Ya juu👌🏼 🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀 Matayarisho ya mvumbiko👇kwanza unatakiwa Usafishe k vzr kisha uwe na kitambaa cheupe kisafi kwa ajili ya kuekea mvumbiko wako👌🏼 🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀 Unatakiwa uwe na mpachor,mpompia,asmin,maward,sio miti mizima Mizima jmn hapana,kisha unachukua kitambaa Chako unaweka mchanganyiko wako kisha unavaa km pedi,lkn kabla ujaweka mchanganyiko wako kile kitambaa ukifukize vzr Ndio unaweka na kuvaa, 🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀 Lkn kama shoo usiku unaweka mcha na ili harufu ikolee vzr,ikifika usiku unatoa unajitayarisha kwa shoo mtoto wa kike na mnukio wako wa kitumbuwa uone bwana anavoila nyama yako rahaaaaaaa thannaaaaa👌🏼 Mwanamke mvumbiko. Mpo hapo? 🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀🎀 IMETOKA MWANAMKE NDOWA ... Read More
NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI? Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili). Jinsi yakutumia samahani kiusahihi Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali. Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya. Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa. Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena. Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha. Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa) Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe) Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea. Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja. ... Read More
Majina Ya Watoto Wa Kiume (26)  Katika tamaduni nyingi, majina ya watoto wa kiume hutokana na majira au matukio ya wakati wanapozaliwa. Kwa mfano, wakati mmoja, mwanamke Mwethiopia alijifungua mtoto wa kiume. Shangwe yake ikageuka kuwa majonzi alipoona mtoto wake akiwa amelala bila kusonga. Nyanya yake alipomchukua mtoto huyo ili amwoshe, kwa ghafla mtoto akaanza kusonga, kupumua na hata kulia. Hali hii ikawa chanzo cha jina la mtoto na hiyo wazazi wake wakaunganisha jina muujiza na neno linguine la Kiamhara na kumwita mvulana huyo Muujiza Umefanyika. Nchini Burundi, majina memgin yalitokana na wakati wa vita vilivyokuwemo mwanzo wa miaka ya tisini. Mtoto aliyezaliwa huku mzazi akijifichakutokana na machambulizi angepatiwa jina kama Manirakiza amabalo maana yake ni’Mungu Ndiye Anayeokoa’. Majina mengine ya wakati ule ni kama Twagirimana na Mwana wa Imana ambayo pia humaanisha mwana wa Mungu au mtu aliyeponea vita kwa muujiza wa Mungu. Desturi hii ya majina ya watoto wa kiume imeenea kote ulimwenguni ambapo kuna majina mengi yaliyo na maana ya nyakati kam wakati wa vita, njaa, shjrehe, makumbusho au tukio amabalo watu hupenda kukumbuka kwa kuwapa watoto majina. Kuna majina kadhaa amabyo ni mashuhuri sana ulimwenguni ;Noah, Liam, Mason, Jacob, William, Ethan, Michael, Alexander, James, Daniel na mengine. MAANA MAJINA TUKIZINGATIA HERUFI YA JINA LA KWANZA (KIUME) HERUFI A Watoto wenye jina linaloanza kwa herufi hii hupenda mambo makubwa,hujiamini sana na huwa na uwezo wa kutimiza malengo yao. Ni watoto wenye tahadhari,wachangamfu na hupenda matukio. Kwa kawaida hupenda kuheshimiwa,hupenda mamlaka,na ana kiburi,watoto wapenda hasira.Kidesturi herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI B Mwenye jina linaloanziana na herufi hii ni watoto wakarimu,waaminifu na hupenda kazi sana. Ni wajasiri, shujaa na wakatili katika vita au popote pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.Herufi hii huwakilisha nyota yangombe. HERUFI C Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni motto wa kubadilikana,ni washindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda.Ni watu wabunifu na wanapenda mawasiliano,herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha. HERUFI D Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni anayependa usawa,biashara ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi.Ni wajeuri na wenye msimamo. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa. HERUFI E Mwenye jina linaloanza na herufi ni mtu mwenye roho nzuri,mwenye mapenzi na huruma,mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Ubaya wake ni mtu asiyetegemewa na ni kigeugeu.Herufi hii huwakilishwa na nyota ya samba. HERUFI F Mwenye jina linaloanza na herufi hii n mtu mwenye mapenzi,huruma,roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu,ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke. HERUFI G Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni mtu mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho,ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. Ni mtu mwenye hisia kali,msomi,mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri kutoka kwa watu.Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani. HERUFI H Mwemye jina linaloanzia na herufi hii ni mtoto mwenye ubunifu na nguvu katika biashara,hupata faida kubwa katika anayopenda kutokana na bidii, ni mwenye mawazo mengi,mchoyo na mbinafsi.Herufi hii huwakilisha nge. HERUFI I Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda sharia,ana huruma na utu mzuri.Wakati mwingi ni mtoto mwenye kujiamini sana na mwenye hasira za haraka. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale. HERUFI J Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye matamanio,mkweli,mkarimu na mwerevu.Huwa asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa,wakati mwingine anakuwa ni mtoto mvivu na anayekosa mwelekeo. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi. HERUFI K Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto mjeuri,mwenye msimamo thabiti,mpenda umashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu, ana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana,ni mtoto asiyeridhika. Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo. HERUFI L Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto wa vitendo,mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha,hupatwa na misiba mara kwa mara.Herufi hii huwakilisha nyota ya samaki. HERUFI M Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kujiamini sana,mchapakazi na hupata mafanikio,ni mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI N Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mbunifu, mwenye hisia kali,hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ngombe. HERUFI O Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye subira,mvumilivu,na mwenye bidii ya kusoma.Ni mtoto mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.Herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha. HERUFI P Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye uwezo wa kuamuru na ana hekima kubwa.Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa. HERUFI Q Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtotto mwenye kupenda mambo ya asili,ni watu wasioelezeka,wako na uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya samba. HERUFI R Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mtulivu,mwenye huruma lakini mwenye hasira za haraka.Muda mwingi yeye ni mpenda amani. Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke. HERUFI S Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mvuto kali wa kuleta utajiri,ni mtoto mwenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani. HERUFI T Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda ushauri wa kiroho,anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu, ni watoto wenye hisia kali na wepesi sana kushawishika.Herufi hii huwakilisha nyota ya nge. HERUFI U Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye bahati kwa ujumla,anapenda uhuru katika mapenzi,ni mbinafsi,mwenye tama na anayekosa maamuzi. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale. HERUFI V Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mchapakazi,mwenye bidii asiye choka lakini ni watu wasiotabirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi. HERUFI W Mwemye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mawazo sana,mchangamfu sana,mwenye uwezo wa kutambua watu wabaya na wema, ni wenye tama na hufanya mambo hatari sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo. HERUFI X Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto asiyependa kuwekewa vizuizi hasa katika anasa na ni rahisi kwake kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI Y Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mpenda uhuru na hapendi kupingwa katika jambo lolote,ni watoto wanaokosa uamuzi na husababisha kupoteza bahati katika maisha. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI Z Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda matumaini na amani,ni wenye msimamo mkali japo ni wenye kukubali ushauri . Herufi hii huwakiisha nyota ya ngombe. ... Read More
KWA WANAWAKE TU! NJIA 14 ZA KUJIWEKA ILI WANAUME WATAMANI KUKUTONGOZA  Je umekuwa ukijiuliza kwa nini haukuwi approached na wanawaume kama unavyotaka? Mtandao wa Sayari ya Mapenzi umeamua kukuandalia mbinu na maujanja ya kutumia ili uonekane mwanamke ambaye anaweza kufukuziwa na mwanaume kwa urahisi. Owk.... Kando na itikadi ambazo umekuwa ukifikiria, kuapproachiwa ama kufukuziwa na mwanaume si gemu ya bahati nasimu ambayo mtu anaingojea ijitokezee. Na pia kando na itikadi nyingi za wanawake wanazozifikia, si lazima ufanye kitendo kikubwa ama cha inadi ili mwanaume aweze kukutongoza. Ukweli ni kuwa, kama unaielewa akili ya mwanaume na jinsi inavyofanya kazi kabla ya kuapproach mwanamke, unaweza kumfanya mwanaume yeyote kutaka kuongea na wewe dakika tano atakapokuja katika himaya yako. So mbinu zenyewe ndizo zipi? Zama nami... Njia za kujiweka ili mwanaume apate nafasi rahisi ya kukutongoza Kwanza jiweke nadhifu Hii ni muhimu katika yote kama wataka mwanaume akutambue. Mwanaume kitu cha kwanza anachokiangalia huwa ni mwonekano wa mwanamke. Mwanaume anapoingia katika chumba, inamchukua sekunde ndogo zana kuamua iwapo anataka kuapproach mwanamke mfani au la. Kama umevalia vizuri na unapendeza, itarahisisha kazi yako sana. Pili usionekane kama una shughli Usijishughlishe sana na simu yako, ama kitabu chako, ama kitu kingine. Unaweza kuwa umeboeka na unajaribu kujiweka buzy, lakini fursa iweza kuwa hivi, kufanya hivyo kunaweza kumfanya mwanaume anayetaka kukuapproach kuona ya kuwa uko buzy sana kiasi cha kuwa atashindwa kukufuata kwanu unaweza usiwe interested na maongezi yake. Tatu ni kuwa mko ligi moja? Hii inakinzana na hatua ya kwanza, lakini inaweza kuwa na tatizo iwapo unaoneka kama uko ligi tofauti na mwanaume. Kama utaoneka amakujiweka mtu wa hadhi ya juu wanawake watapenda kukuangalia lakini hawatakuaproach. Hii ni kwa sababu wanaume wengi hawapendi kudhalilishwa wakati wanapoamua kukuapproach....kiufupi ni kuwa ukiwa unavutia kupindukia wanaume watakuogopa. Lakini tena, kuna wale wanaume ambao wanajiamini kupindukia ambao wanajua thamani ya kukuapproach, nao ni wanaume alfa, wanaume diriki, na pia wale wanaume mapleya. Kama wataka kuteka atenshen ya mwanaume mzuri wa kawaida lakini anayeogopa kukuapproach, jaribu kutumia mbinu ya kuwa jamili na watu wanaokuzunguka. Huwa inasaidia. Ujanja wa kumfanya mwanaume aweze kukuakuaproach 1. Jinsi utakavyovalia Usivalie kana kwamba huna kitu cha kuficha. Utapata atenshen ya kila mtu lakini wanaume ambao wataamua kukuapproach ni wale ambao wanataka kulala nawe kwa usiku mmoja pekee. Enyewe kuvalia kwa kutamanisha kunasaidia kuteka atenshen ya mwanaume, lakini usivuke mipaka ya kawaida. Kumbuka kuwa si lazima uonyeshe viungo vyako vyote vya mwili ili uweze kuteka macho ya mwanaume. Kama unavutia inatosha kumfanya mwanaume akugundue. 2. Unavyomuangalia Mchungulie mara moja na nyingine, halafu mwangalie mara kwa mara. Hakikisha ya kuwa haujisahau ukamwangalia sana kupindukia ama atakuona kama wewe ni rahisi wa kuapproach na anaweza kukupuuza. 3. Mitindo ya kumwangalia Kuna mitindo miwili mikuu ya kumwangalia mwanaume ili kumuonyesha ya kuwa umevutiwa naye. Unaweza kutumia mbinu zote mbili kulingana na vile unataka. i) Kumwangalia polepole - wakati ambapo unaangalia pande zote, angalia upande wake na uyaangalie macho yake kwa sekunde kadhaa huku ukiweka tabasamu. Halafu pole pole zungusha kichwa chako uangalie kwingine. Mbinu hii ni ya kijasiri ya kumwonyesha mwanaume umevutiwa kwake. ii) Kumwangalia kwa uharaka - hii ni mbinu ya kumwangalia kwa uharaka. Anza kumuangalia, ukiona kama anataka kukuangalia, ghafla angalia kando halafu utoe tabasamu ukiangalia chini. Mbinu hii inampa confidence na kukuona wewe ukipendeza. 4.Mfanyie kazi iwe rahisi Inakuwa vigumu kwa mwanaume kumuapproach mwanamke sehemu ambapo yuko kundini na marafiki zake. Kama mawazo yako ni kufuatwa na mwanaume, hakikisha ya kuwa wakati mwingine unajipa time ukiwa pekeako ama zaidi uwe na rafiki yako wa kike mmoja. 5. Sehemu zifaazo Si kila sehemu ni nzuri kufanya maongezi na mtu. Kama unataka mwanaume akuapproach, chagua sehemu ambayo si kila mtu ataanza kujeuza kichwa chake kutaka kujua ni nini kinachoendelea kati yenu. Sehemu za mkawahawa, supermarket, ama bookshop ni sehemu nzuri zaidi za kukutana na mwanaume kupiga stori. 6. Mpatie nafasi aongee na wewe Hata kama uko katika group na marafiki zako halafu mwanaume akakugundua, mwonyeshe interest kwa kumuangalia kwa madakika. Ukiona kama yuko tayari kuongea na wewe, unaweza kujitenga na marafiki zako kwa muda. Aidha unaweza kuanza kuzunguka hio sehemu kiasi ama unaweza kujipeleka mahali ambapo itakuwa rahisi kwa mwanaume huyu kuzungumza na wewe. 7. Tabasamu Onekana jamili, na nafasi ya wewe kufuatwa na wanaume itaongezeka mara dufu. Kupendwa kwa mwonekano wa kwanza ni kama baraka kwa mwanamke yeyote yule ambaye anataka macho ya mwanaume yamwone. 8. Usiboe Kuwa mwanamke mwenye furaha na mwenye hisia chanya mahali popote pale utakapokua. Mwanamke mwenye shangwe huvutia mwanaume yeyote yule. Kama utaonyesha chembechembe za kuboeka, mwanaume anayetaka kukuapproach anaweza kuwa na maswali mengi ya kujiuliza kwani ataona ya kuwa maisha yako huboesha na yasiyo na mwanga. 9. Usiwe mjeuri Kama wewe ni mjeuri kwa yeyote, aidha weita ama mmoja wa rafiki yako, inaweza kutokea kuwa mwanaume ambaye anapania kukuapproach kusimamisha ari yake. Hakuna mtu anapenda mtu mjeuri, na hakuna mwanaume angependa kuapproach mwanamke ambaye anaweza kumpuuzia ama kumkataa. 10. Usitangamane na wanaume Hii ni muhimu kwa mwanamke yeyote aelewe. Usiwahi kamwe kutangamana na marafiki zako wa kiume kama unataka kukuwa approached na mwanaume. Haitafanya kazi kamwe. 11. Mwoneshe kuwa uko intrested Mwonyeshe kuwa uko interested kwake kwa kutaka kumjulia hali zaidi. Hata kama uko na marafiki zako mnaongea halafu amekaa karibu na wewe, mwangalie iwapo anakuangalia hata kama unawajibu rafiki zako. 12. Onyesha uanawake wako Mwangalie mara kwa mara, halafu ukishika macho yake, peta nywele zako nyuma ya sikio lako. Inaweza kuonekana kama jambo dogo kwako, lakini kwa mwanaume ni kama kugonga ndipo. 13. Mtege Pita mbele yake halafu mwangalie machoni mwake wakati unapompita. Mtese kihisia, ataipenda kuona atenshen yake. 14. Usilazimishe Utakuwa unajiaibisha iwapo unalazimisha mambo. Wanaume si mabubwi, hivyo ukiwaangalia mara moja na nyingine ama kuwatabamia, wanajua kuwa uko tayari kuapprochiwa. Ok hizi ni mbinu ambazo unafaa kuzitumia kama unataka mwanaume yeyote yule akunotice ama akufukuzie. ... Read More
Je Wajua Kwanini Wanawake Hula Vyakula vya Ajabu Ajabu Wakiwa Wajawazito?  Tabia hii inayojulikana kwa Kiingereza kama “Pica” inatokana na mtu kutamani kula vitu vyenye virutubisho kidogo sana au visivyo na virutubisho vya aina yoyote kwa mwili. Tamaa hizi huwa zinawapata watoto au mama mjamzito kutafuna vitu ambavyo kimsingi si chakula – kama udongo au chaki. Jina hili la pica ni aina ya ndege ambaye anajulikana kwakuwa anakula kitu chochote, hana anachochagua. Ni kweli kwamba wajawazito wengi hupata hamu ya kula vitu ambavyo si vyakula walivyozoea kula mara kwa mara wakiwa si wajawazito; wengi wao ni rahisi kuwaelewa kwa sababu hukimbilia mchele, barafu na vinginevyo ambavyo si vitu vibaya kula. Kwa watoto, hii ni tabia iliyozoelekakwakuwa inawatokea watoto wengi ambao ni kati ya asilimia 25 na 30% ya watoto wote; lakini kwa wanawake wajawazito, inatakiwa iwe kwa kiwango cha chini zaidi. Nini kinasababisha tabia hii kwa wajawazito? Sababu ya baadhi ya wanawake kuwa na tabia hii wakati wa ujauzito haijulikani hasa. Kwa sasa hakuna sababu maalumu, lakini kwa mujibu wa Jarida la Chama cha Watu Wanaoishi na Ugonjwa wa Kisukari nchini Marekani, tabia hii yawezekana ikasababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Baadhi wanadai kwamba hali hii inaashiria kwamba mwili unajaribu kupata vitamini na madini mengine yanayokosekana kwenye chakula cha kawaida ambacho mtu anakula. Muda wingine tabia hii yawezaikatokana na kuumwa viungo au akili kwa muda mrefu. Baadhi ya vitu vya ajabu ambavyo wajawazito hupenda kula Vitu vinavyopendwa zaidi na wajawazito wengi ni udongo, uchafu. Vitu vingine ni njiti za kiberiti zilizochomwa, mawe, mkaa, barafu, dawa ya meno, sabuni na mchanga. Mjamzito anapokula vitu hivi hujisikii raha kana kwamba amekula chakula chenye faida kubwa kwake na kwa mtoto aliye tumboni. Kuna hatari yoyote kwa mtoto aliye tumboni? Kula vitu ambavyo si vyakula kimsingi ni jambo linaloweza kusababisha madhara kwa mjamzito mwenyewe na mtoto aliye tumboni. Kula vitu hivi kunaweza kuharibu mfumo wa kawaida wa kunyonya virutubisho kutoka kwenye vyakula na kusababisha mwili wako upungukiwe na madini muhimu unayoyahitaji kwa afya yako na ya ukuaji wa mtoto vilevile. Tabia hii ni hatarishi sana kwakuwa vitu ambavyo si vyakula vinaweza kuwa na viambata ambavyo ni sumu au vyenye vijidudu vinavyoathiri mwili. Kudhibiti tabia hii Usihamaki unapojikuta unatamani vitu vya ajabu ajabu wakati wa ujauzito: inatokea sana na si jambo la kushangaza kwako pia. Jambo la muhimu ni kumjulisha muuguzi wako au wahudumu wa kliniki unayohudhuria kujua maendeleo yako ya mtoto tumboni ili akuelimishe na ahakikishe kwamba una uelewa kuhusu hatari zinazoambatana na tabia hiyo. Baadhi ya mbinu za kutumia kushinda tamaa hizo Mtaarifu mhudumu wako wa afya kwenye kliniki unayohudhuria na muangalie kumbukumbu za ukuaji wa mtoto tumboni pamoja na hali yako ya kiafyaFatilia kiwango chako cha madini ya chuma mwilini pamoja na kiwango cha vitamini na madini mengine unayotakiwa kulaOmba ushauri kuhusu kitu gani uwe unakula ili kubadili ili kuepuka vitu vya ajabu (waweza kumung’unya/ kutafuna vitu kama pipi au ‘big g’ isiyo na sukariMwambie hata rafiki yako mmoja kuhusu hamu hizi na umtake awe anakukataza unapokula vitu vya ajabu ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: