Home → ushauri
→ #Mwanaume akiwa unafanya haya usilalamike kwa mkeo
Ikifikia mke kukusaliti kwanza unahitaji kujiuliza kuna tatizo gani mpaka akafikia kukusaliti? Mwanamke anaekupenda sio rahisi kumsaliti ampendae hata akitongozwa na Sharobaro, Mzee Yussuf, Diamond hata Reginal Mengi.
Ikitokea mkeo kakusaliti kuna kitu nyuma ya pazia lako, ingawa wengi wetu tunasema hela na Gari vinawalainisha wanawake. Wengi waliosalitiwa basi hizi ndio kasoro zao:-
1 Kaowa mwanamke wa mtu (mwanamke alikuwa na mpenzi wake lakini jamaa kaingia wakati mwanamke anatamani ndoa)
2 Alikuwa na hela sasa kafulia hana kitu au alijifanya alikuwa na hela lakini baada ya kuowa mke anagutuka mume mchovu.
3 Humtoshelezi kwenye tendo la ndoa( humkojozi) kama umeowa mke ameshawahi kufikishwa kilima cha kilimanjaro pole yako fanya maujuzi umpeleke kilima cha Everest.
4 Ubahili hapa wengi wa wanaume ndio hupigiwa sana wake zao, mke anahitaji matumizi yake binafsi sio kula na kulala tu au kumnunulia madira na chocolate za kichina. kuna matozi wanahonga mpaka malaki na milioni halafu unawacha hela ya ugali unapikiwa pilau ukimaliza kula unakwenda kulala, bwege kama wewe lazima uchapiwe dadeki zako.
5 Huna muda wa maongezi na mkeo hujui hata nini anapenda,nini leo kimemkuta,wala huna future plan kwenye familia wewe ukali,mpira,vijiwe,kazi na marafiki tuu wakati rafiki yako wa kweli(mkeo) huna muda wa maongezi nae.
6 Kuwaachia marafiki kuzoweana sana na shemegi yao, sio kama vibaya kutaniana na shemegi yao lakini kuna mataani mengine hupitiliza. utakuta mpaka baadhi ya rafiki wanampigia simu shemegi yao wanaongea kwa masaa na vicheke kibao.
7 Kujifanya mkali kila wakati wewe uso umeukunja kama ngozi za pumb..u hujulikani kijana au mzee hujulikani leo umefurahi au umenuna. Tokea umuowe mkeo hujawahi kumtania hata siku moja.
8 Kuchepuka kuna baadhi ya wanaume walioowa nishawahi kuwauliza kwanini wanachepuka jibu lao kubwa wanasema hawajui. HUbaki kumalizia kusema eti hawa wanawake watakuwa na sumaku
Kuna baadhi ya mambo husababisha sisi wenyewe wake zetu kufikia kuchukua uamuzi wa kutusaliti, Kama ukali unafanya kazi mbona simba na ukali wake lakini kazungukwa na mabebez kibao
#Mwanaume akiwa unafanya haya usilalamike kwa mkeo Ikifikia mke kukusaliti kwanza unahitaji kujiuliza kuna tatizo gani mpaka akafikia kukusaliti? Mwanamke anaekupenda sio rahisi kumsaliti ampendae hata akitongozwa na Sharobaro, Mzee Yussuf, Diamond hata Reginal Mengi. Ikitokea mkeo kakusaliti kuna kitu nyuma ya pazia lako, ingawa wengi wetu tunasema hela na Gari vinawalainisha wanawake. Wengi waliosalitiwa basi hizi ndio kasoro zao:- 1 Kaowa mwanamke wa mtu (mwanamke alikuwa na mpenzi wake lakini jamaa kaingia wakati mwanamke anatamani ndoa) 2 Alikuwa na hela sasa kafulia hana kitu au alijifanya alikuwa na hela lakini baada ya kuowa mke anagutuka mume mchovu. 3 Humtoshelezi kwenye tendo la ndoa( humkojozi) kama umeowa mke ameshawahi kufikishwa kilima cha kilimanjaro pole yako fanya maujuzi umpeleke kilima cha Everest. 4 Ubahili hapa wengi wa wanaume ndio hupigiwa sana wake zao, mke anahitaji matumizi yake binafsi sio kula na kulala tu au kumnunulia madira na chocolate za kichina. kuna matozi wanahonga mpaka malaki na milioni halafu unawacha hela ya ugali unapikiwa pilau ukimaliza kula unakwenda kulala, bwege kama wewe lazima uchapiwe dadeki zako. 5 Huna muda wa maongezi na mkeo hujui hata nini anapenda,nini leo kimemkuta,wala huna future plan kwenye familia wewe ukali,mpira,vijiwe,kazi na marafiki tuu wakati rafiki yako wa kweli(mkeo) huna muda wa maongezi nae. 6 Kuwaachia marafiki kuzoweana sana na shemegi yao, sio kama vibaya kutaniana na shemegi yao lakini kuna mataani mengine hupitiliza. utakuta mpaka baadhi ya rafiki wanampigia simu shemegi yao wanaongea kwa masaa na vicheke kibao. 7 Kujifanya mkali kila wakati wewe uso umeukunja kama ngozi za pumb..u hujulikani kijana au mzee hujulikani leo umefurahi au umenuna. Tokea umuowe mkeo hujawahi kumtania hata siku moja. 8 Kuchepuka kuna baadhi ya wanaume walioowa nishawahi kuwauliza kwanini wanachepuka jibu lao kubwa wanasema hawajui. HUbaki kumalizia kusema eti hawa wanawake watakuwa na sumaku Kuna baadhi ya mambo husababisha sisi wenyewe wake zetu kufikia kuchukua uamuzi wa kutusaliti, Kama ukali unafanya kazi mbona simba na ukali wake lakini kazungukwa na mabebez kibao
Artikel Terkait
Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati ANAVYOKUTAZAMA Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda. MIPANGO Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu. ATAONESHA HUZUNI Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. ATAKUAMINI Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake. ATAKUPA NAFASI Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake. UTAKUWA MWANAFAMILIA Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao. ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo. ATAKUSAIDIA Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani. ATAJITOLEA Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati. ATAAMBATANA NAWE Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu. KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!! ... Read More
MUNGU ATANILIPIA: Nakumbuka nililazimishwa kuolewa ila nilikubali ili kutii amri ya wazazi. Nikabahatika kupata mtoto wa kike niliyempenda sana, kwani sikuwa na raha ya kuishi na mume wangu aliyekuwa mzee sana kwa bahati mbaya mume wangu alikufa kwa ugonjwa wa kisukari. Nikabaki mimi na binti yangu kwakweli sikutaka kuolewa tena niliamua kukaa na kulea mwanangu huyu. Kweli nilimlea na kumsomesha binti yangu, alipofika chuo ndipo mambo yalipoanza kubadilika. Binti yangu akanitaarifu kuwa amepata mchumba na akaja nae nyumbani kumtambulisha kwa ushamba wangu nikashangaa kweli ile gari ya mchumba wa mwanangu na nikaona raha kwa binti yangu kumpata mwanaume mwenye pesa kama yule, ilikuwa ni kipindi cha likizo na yule bwana alikuwa akija mara kwa mara kutusalimia huku akibeba zawadi tofauti tofauti, sikuwa na shaka naye hata akiniambia anataka kutoka na mwanangu nilimpa ruhusu wanaenda halafu anamrudisha nyumbani. Siku moja ambayo siwezi kuisahau kamwe katika maisha yangu, mwanangu akaniaga kuwa anataka kutoka na mchumba ake ila atarudi kesho yake nikamkatalia na kumwambia asifanye hivyo kwani ataonekana hana thamani tena. Badae kidogo alifika mpenzi wake huyo na kuniomba, mwanzoni nilimkatalia ila baada ya kunisihi sana nikakubali kuwa waende basi mwanangu na yule mpenzi wake wakaondoka pale nyumbani nikitegemea mwanangu kurudi kesho yake. Kesho ikafika hadi jioni mwanangu hakurudi, hofu ikaanza kunitawala moyoni mwangu hadi kunakucha mwanangu hakuwa nyumbani pa kuanzia sijui kwani yule kijana ni mgeni kwetu. Siku hiyo nikiwa kwa mbali namwona mwanangu akijikongoja kwa kujivuta, nilimkimbilia mpaka pale alipo nikambeba hadi nyumbani, naye akaniambia maneno haya "mama nakupenda sana ila naomba nikwambie ujumbe huu uwafikishie mabinti wote. Mama, yule kijana nilikutana naye wakati naenda chuo akanipa lifti na kuchukua namba yangu. Mawasiliano yetu yalianzia hapo ila sijui anapoishi wala ndugu zake, aliniomba nije nae nyumbani kumtambulisha kipindi hiki cha likizo na ndio nikafanya hivyo, nilizoea kuzunguka nae hotel, bar, cinema na majumba yote ya starehe. Ila alichonitenda hivi karibuni ni cha kustaajabisha, nilipoondoka naye hapa alinifunga kitambaa machoni na kusema anaenda kunifanyia suprise nilishangaa tukielekea mahali pasipojulikana huko nilienda kupata mateso makubwa mengine hata hayasimuliki ila kuna hili la kunifunga mimi kamba kwenye miti, mikono na miguu ikiwa imetanuliwa halafu wakanifanyisha mapenzi na mbwa watatu, ikiwa hiyo haitoshi lililetwa joka kubwa ambalo liliingizwa sehemu zangu za siri, sijui lilienda kufanya vitu gani ila nilipata maumivu ambayo hayaelezeki nililia hadi kuzimia, nilipozinduka nikajikuta nipo nje ya nyumba yetu nimetupwa ila kabla ya yote waliniambia kuwa sitakiwi kusema chochote kile kwa mtu yoyote kwani nitakufa." Alipomaliza kusema hayo nilikuwa natetemekd mwili mzima kwani nilimuona mwanangu akinyooka na kufa mikononi mwangu. Hata nikieleza maumivu yangu hakuna atakayenielewa, ila niliumia kupita maelezo. Yote namwachia Mungu. Tangu kifo cha mwanangu nimekuwa kama mtu nisiyejielewa, natoa wosia kwa mabinti wengine tafadhari sana angalieni kwa makini wachumba mlionao isije ikawa kama yaliyomkuta binti yangu, wazazi wote kuweni makini. Naumia kumpoteza binti yangu mpenzi tena aliyekufa kwa maumivu makubwa. Ila najua Mungu atatenda jambo. Hadi leo sielewi kwanini mwanangu alitendwa hivi. Kama ujumbe huu umekugusa, dondosha LIKE yako hapo au SHARE ukiweza ili na wengine wapate kitu. ... Read More
SABABU YA KWELI WANAWAKE KUENDELEA KUTEMBEA NA WANAUME WALIO OA  Jane ni mwanamke mwenye mafanikio, anamiliki kampuni ya kutengeneza mifuko ya plastic, ana studio. Ana akili , anavutia na ni mwenye ujasiri. Pia anatembea na mume wa mtu. Amekuwa akiwauliza rafiki , familia yake ambao wanafahamu kuwa kitu gani kinamfanya mwanamke mwenye mafanikio, akili na ujasiri kutembea na mume wa mtu kwa miaka zaidi ya mitatu? Hamu ndio Inayoanza Mwanaume ambaye ameoa anapomkaribia mwanamke , anakuwa na hatari— hatari ambayo inaonyesha kumuhitaji zaidi. Kuwa na muda naye. Huenda kwa meseji au kupata chakula pamoja kwa siri, au kulala nae kwa siri. Huonyesha kuwa na majukumu kama mwanaume single. Lakini mwanaume single huandaa date. Huwa na sababu nyingi za kufanya hivyo, na ukiri wao huwa ni wa makini na huonyesha kuwa hawako interested. Hujikuta wameingia kwenye majukumu ambayo hakuwa amejiandaa. Kwa ushindani, kazi ya mwanaume aliyeoa Inamlinda kutokana na nia yake kwa mwanamke single ili kuonyesha hamu yake. Kama hataweza kuonyesha hisia zake kwa kumtazama macho yake, sauti yake, kumsugua mwanamke mgongo wake, kumfanyia massage kwenye mabega, mwanamke atajuaje kama anamtaka? Na ataendeleaje kubaki nae kama hamtimizii haja zake? Kwa kufanya hayo anaweza kumuwekea ulinzi, mahusiano yao kukomaa na kuwa mazuri na kuwa ya kawaida. Lakini akili Itakuja. Marafiki aliowaambia watamkumbusha.Ni mume wa mtu. Familia watamuuliza , bado yuko na mke wake? Wakati anapoanza kujiuliza ndani yake , mume alienae, Ataanza kuwa na njia mbili. Kwa wanawake wengi, hio imepitwa na wakati. Kwa wengine mchezo utaendelea—kwa kufahamu maamuzi haya…tuangalie sasa 1.Wakati mwanaume anapotoka nje, uwezekano mkubwa hana furaha ndani ya nyumba yake. 2Talaka zinaongezeka . ndoa zinafikia mwisho, na wanaume wanaoa tena. 3.Uzinzi unaongezeka kwa wanaume. Huenda kuishi muda mrefu peke yao sio mpango mzuri. Kwa mtu kama Jane kuishi maisha kama hayo, huenda ni katika kumpata mtu sahihi na kumuondoa kwa mke wake hata kama kutakuwepo hatari katika hisia zake. Mwanamke kama Jane ni wepesi wa kujifunza zaidi kuhusu tabia za wanaume ambao wanacheat kabla ya kuamua kuingia kwenye mahusiano ya kudumu. Wengi wa wanaume wanasema , sababu kubwa ya kucheat ni kukosa sex Ni kiasi kidogo sana cha wanaume ambao hupotea katika mapenzi ya nje Baadhi ya wanaume wanaocheat walitoa taarifa kuwa wanafanya hivyo kwa wenza wengi karibu miaka yote Kwa kulinganisha wanawake na wanaume. Wanawake wao huingia kwenye mahusiano kwa mwanaume aliyeoa kwa sababu ya kuwapenda. Lakini sio nzuri kama mtu ameoa ni bora kujiheshimu na kumuheshimu mke wake , Na kama kuna tatizo ni vizuri kurekebisha kuliko kwenda kutafuta majibu ya tatizo lako nje.Kwa nini nasema hivi , ni kwa sababu ipo siku mwanamke huyo atahitaji kuwekwa wazi , utafanyaje na wewe ulikuwa ni mwizi. kwa upande wa mwanamke Utavunjika moyo, inapofika wakati kama huo.Maumivu ya kuachwa na mwanaume aliyeoa ni makubwa kuliko ya kuachwa na mwenza ambaye ni wako kabisa. Black woman hugging her knees 1.Utajisikia kama mkosaji mara mbili. Kwamba hukuweza kumpata mtu ambaye tayari kwanza alikuwa ameoa na amekuacha baada ya kuridhika kwake. 2.Wasaliti wanaokatiza mahusiano huwa wanaonyesha kabisa kuwa hawana hisiana za kutosha kwako. Wanakuchukulia kama wewe ni msichana mkubwa, na unaelewa kitu gani unachokifanya. 4.Mfumo unaompa support unaweza ukawa upo gizani. HUenda ni aibu au hamu ya kumlinda msaliti au vyote. Hakuna mtu ambaye anafahamu. Kama wapo basi ni wa katibu sana. Kwa hio watu kama Jane wataepuka vipi hatari inayotokana na aina hii ya mahusiano? Ukweli ni kwamba, ufahamu una nguvu.Kama msomaji unahusika na mume wa mtu, rudia tena kusoma makala hii kwa makini kabla hujaendelea zaidi. Maisha ni mafupi.Muda wa kumsaidia mume wa mtu ambaye amekosa kitu fulani kwa mwenza wake umekwisha. Mwache akatengeneze kwa mwenza wake. Wanaume Single wako wengi wanakusubiri na hawana hatari kama hizo. Hata kama atakuonyesha kuwa wako cool mwanzoni usidanganyike. ... Read More
JIFUNZE KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPENZI YA DHATI NA WEWE: Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi". Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. MTU AMBAYE HAKUPENDI KWA DHATI: ==> Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako. ==> Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?" Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo". Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu. ==> Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo. ==> Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie. ==> Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. ===> Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo. MTU ANAYEKUPENDA KWA DHATI: ==> Hachoki kukwambia NAKUPENDA, kwani anajisikia raha sana pale atamkapo neno hilo juu yako kwahiyo unaweza ukawa kama wimbo wake kwako. ==> Anajivunia kuwa na wewe na atapenda kukupa sifa nzuri kila mara, yani Hachoki kukusifia. Atakushauri pale unapokosea ili uwe katika njia nzuri. Unaponuna atajua cha kufanya ili wewe ufurahi na kurudi kwenye hali ya kawaida. ==> Hachoki kukuombea mema na kukutakia mafanikio. ==> Atapenda kukueleza ukweli kila mara ili uweze kujenga uaminifu na imani juu yake. ==> Wewe utakuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake, atakuthamini na kukujali. Tatizo lako litakuwa sawa na tatizo lake, atakupa ushauri bila kuchoka. ==> Kabla ya kumuuliza swali kuwa "je unanipenda?" atakuwa ameshakujibu tena kwa hisia nzito kuwa "nakupenda sana mpenzi wangu". ==> Hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, kwakuwa wewe ndiye furaha yake. ====> Thamani yako ni kubwa sana kwake, anakuona mpya kila siku na hachoki kuvutiwa na wewe. Anakupenda kwa kumaanisha na si kukupenda kimazoea tu. Neno NAKUPENDA litamtoka moyoni na ataridhihirisha kwa kinywa chake. Mtambue mtu huyu kuwa anakupenda kwa dhati. NB: Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Si vyema kutumia mapungufu ya mwenzio kama fimbo katika mapenzi, cha muhimu ni kumuelimisha na kumuelekeza ili muweze kwenda sambamba. Nadhani baadhi ya maswali ya wadau yatakuwa yamejibiwa na hiyo mada. Kama kuna nyongeza au swali lolote kuhusiana na hiyo mada tuambiane hapa na kupatiana majibu hapa hapa wadau. ... Read More
Jinsi ya Kuomba Msamaha MACHAGUO YA UPAKUAJI Podikasti Makala Nyinginezo SOMA KATIKA Amkeni! | Septemba 2015 UNAWEZA KUWA NA FAMILIA YENYE FURAHA Fuata Mwongozo wa Mungu ili Uwe na Ndoa Yenye Furaha Kujiuliza maswali mawili rahisi kunaweza kuisaidia ndoa yako. AMKENI! Viwango Vinavyomfaa Kila Mtu, Nyakati Zote—Upendo Upendo unaotajwa mara nyingi katika Biblia si ule wa kimahaba au kimapenzi. HABARI NJEMA KUTOKA KWA MUNGU! Kanuni za Biblia Zinatunufaishaje? Yesu alieleza kwa nini tunahitaji mwongozo na ni kanuni gani mbili za Biblia zina umuhimu mkubwa. Kuwafundisha Watoto Unyenyekevu Je, Inafaa Kujihatarisha Kwa Kusudi la Kujisisimua? Watoto Wanapoondoka Nyumbani Umuhimu wa Kazi za Nyumbani Kuomba msamaha kunaweza kuzuia ugomvi CHANGAMOTO Muda mfupi tu uliopita wewe na mwenzi wako mmetoka kubishana. Kisha unajiambia hivi: ‘Sihitaji kumwomba msamaha. Kwa sababu si mimi niliyeanzisha ugomvi!’ Mmeacha kuzungumzia jambo hilo, lakini hali si shwari. Unafikiria kuomba msamaha lakini unaona huwezi kusema, “samahani.” KWA NINI HILO HUTUKIA Kiburi. “Wakati mwingine si rahisi kusema ‘samahani’ kwa sababu sitaki kujishushia heshima,” anakiri mume anayeitwa Charles. * Kiburi kinaweza kukufanya uone aibu kukubali kwamba umechangia tatizo. Mtazamo. Unaweza kuhisi kwamba kuomba msamaha kunahitajika tu pale unapokosea. Mke anayeitwa Jill anasema hivi: “Ni rahisi kwangu kusema ‘samahani’ ninapojua kwamba nimesababisha tatizo. Lakini, ikiwa sote tulisema mambo yasiyofaa, ni vigumu kufanya hivyo. Kwa nini niombe msamaha ikiwa sote tuna makosa?” Unaweza kujitetea ikiwa unahisi kwamba mwenzi wako ndiye mwenye makosa. “Unapoamini kabisa kwamba hujafanya kosa lolote, unaonyesha huna hatia kwa kukataa kuomba msamaha,” anasema mume anayeitwa Joseph. Malezi. Huenda ulilelewa katika familia ambayo halikuwa jambo la kawaida kuomba msamaha. Ikiwa ndivyo, huenda hukujifunza kukubali makosa yako. Kwa kuwa hukuzoea kufanya hivyo tangu utotoni, ni vigumu kwako kuomba msamaha ukiwa mtu mzima. MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA Mfikirie mwenzi wako. Jaribu kukumbuka jinsi ulivyohisi vizuri ulipoombwa msamaha na mtu fulani. Kwa nini basi usimfanye mwenzi wako ahisi hivyo? Hata ikiwa huamini kwamba ulikosea, unaweza kuomba msamaha kwa ajili ya maumivu ambayo mwenzi wako amepata au kwa sababu ya usumbufu wowote uliotokana na matendo yako. Maneno hayo yanaweza kumsaidia mwenzi wako ahisi vizuri.— Kanuni ya Biblia: Luka 6:31 . Zingatia ndoa yako. Ona kuomba msamaha kuwa ushindi katika ndoa yako na si kushindwa. Zaidi ya yote, mtu anayeendelea kukasirika ni “mgumu kuliko mji wenye nguvu,” inasema Methali 18:19 . Inaweza kuwa vigumu kurudisha amani katika hali hiyo. Pia, unapoomba msamaha unazuia kosa kuwa kikwazo. Ukifanya hivyo, unatanguliza ndoa yako badala ya hisia zako.— Kanuni ya Biblia: Wafilipi 2:3 . Uwe mwepesi kuomba msamaha. Ni kweli kwamba ni vigumu kuomba msamaha ikiwa hujakosea. Lakini makosa ya mwenzi wako hayapaswi kuwa kisingizio cha kuendelea kuwa na tabia mbaya. Hivyo, usisite kuomba msamaha ukifikiri kwamba muda ukipita kosa hilo litasahaulika. Unapoomba msamaha unafanya iwe rahisi pia kwa mwenzi wako kuomba msamaha. Na kadiri unavyoomba msamaha ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kufanya hivyo tena wakati mwingine.— Kanuni ya Biblia: Mathayo 5:25 . Onyesha kwamba unajali hisia za mwenzi wako. Kutetea kosa lako si sawa na kuomba msamaha. Kusema kwa kejeli, “samahani kwa kuwa naona unakwazika haraka kwa sababu ya jambo hili,” si njia ya kuomba msamaha hata kidogo! Kubali makosa yako na utambue kwamba umemuumiza mwenzi wako, hata kama unaona hakuwa na sababu ya kukwazika. Tambua ukweli. Kubali kwamba utafanya makosa. Kwa kweli, kila mtu hukosea! Hata kama unafikiri huna hatia, tambua kwamba kuna uwezekano umechangia jambo hilo. Biblia inasema hivi: “Mtu wa kwanza katika kesi yake ni mwadilifu, mwenzake huingia naye hakika humchunguza kwa undani.” ( Methali 18:17 ) Itakuwa rahisi kwako kuomba msamaha ikiwa una maoni yaliyosawazika kuhusu mapungufu yako ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: