Home → ushauri
→ MBINU MPYA ZA WANAWAKE WA SIKU HIZI WANAO SAKA NDOA KWA NGUVU...NI NOMA SANA
Siku ya kwanza atakuja na chupi 2, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi
anaondoka...
Siku ya 2 anakuja na khanga,anaivaa usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka...
Siku ya 3 anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia 'Hny nitunzie nimesahau hereni zangu mezani
Siku ya 4 anakuja na nguo 2 na vipedo vya kubadilisha na viatu pea 2,anavua high heels anaweka kwenye Shoe rack,asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo. Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na vitu kadha wa kadha,na ole wako uvihamishealipoacha,kesi zinaanza...
Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza...Anahamia taratibu.. Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa
ina perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa hereni na 'Foundation'... My Brother,huna haja ya kuuliza,NDO KASHAHAMIA HUYO....
Kifuatacho utaambiwa,''Honey I miss my days',Zamaninilijua ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed Calls, Siku hizi kuna Missed days,ukiambiwa hivi tu ju imekula kwako, inawindwa ndoa...
MBINU MPYA ZA WANAWAKE WA SIKU HIZI WANAO SAKA NDOA KWA NGUVU...NI NOMA SANA Siku ya kwanza atakuja na chupi 2, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi anaondoka... Siku ya 2 anakuja na khanga,anaivaa usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka... Siku ya 3 anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia 'Hny nitunzie nimesahau hereni zangu mezani Siku ya 4 anakuja na nguo 2 na vipedo vya kubadilisha na viatu pea 2,anavua high heels anaweka kwenye Shoe rack,asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo. Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na vitu kadha wa kadha,na ole wako uvihamishealipoacha,kesi zinaanza... Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza...Anahamia taratibu.. Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa ina perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa hereni na 'Foundation'... My Brother,huna haja ya kuuliza,NDO KASHAHAMIA HUYO.... Kifuatacho utaambiwa,''Honey I miss my days',Zamaninilijua ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed Calls, Siku hizi kuna Missed days,ukiambiwa hivi tu ju imekula kwako, inawindwa ndoa...
Artikel Terkait
UMESOMA HADITHI NYINGI ZA MAPENZI, LAKINI HII ITAKUSISIMUA KULIKO ZOTE, UTATUMIA DAKIKA 2 KUSOMA LAKINI...  1st year nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo. Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why 2nd year Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia "asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. 3rd year Siku moja kabla ya Tamasha la muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia "Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as "bestfriends".hivyo tukaenda. katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Graduation Day siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but she didn't notice me like that,and i knew it. kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia "you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Miaka michache baadae Nikiwa kanisani Yule Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be mine,but she didn't see me like that,and i knew it. but before she drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Kwenye Mazishi Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo' Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I wish he would tell me he loved me! Nilipiga magoti huku nikilia nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo nae tena katangulia mbele za haki i cried!! Vunja ukimya ... Read More
NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?  Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu. Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile. Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…...... Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo. Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani. Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish. Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye. Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni? Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala . Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu. Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali. Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake? Ushauri tafadhali........... ... Read More
Tatizo la Ugumba kwa wanawake  Ugumba ni hali ya mwanamke kushindwa kushika ujauzito. Linaweza kuwa tatizo pia kwa mwanaume lakini katika makala hii tutaona nini kinasababisha tatizo hili kwa upande wa wanawake. Nini husababisha ugumba kwa wanawake? Mayai kutokomaa ipasavyo: Tatizo la mayai kutokukomaa vema ndilo chanzo na sababu kuu ya wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito na hii inachukua karibu asilimia 30 ya wanawake wote wagumba. Habari njema ni kuwa tatizo hili linaweza kurekebishwa kirahisi ikiwa mwili utapewa vile viinilishe mhimu vinavyokosekana hadi kupelekea mayai kutokomaa vizuri. Vinavyosababisha mayai ya mwanamke kutokomaa vema: (1) Matatizo ya kihomoni Matatizo katika homoni ndicho chanzo kikuu cha mayai kutunga bila kukomaa vizuri. Hatua za ukomaaji wa mayai zinategemea uwiano mzuri wa homoni na namna zinavyotegemeana katika kufanya kazi. Jambo lolote linalovuruga homoni kubaki katika uwiano wake sawa na wa kutegemeana na wenye kufanya kazi ipasavyo linaweza kupelekea utungaji wa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Kuna sababu kuu mbili zinazosababisha matatizo katika homoni: Ufanyaji kazi usioridhisha wa hypothalamus Hypothalamus ni sehemu ya mbele ya ubongo ambayo ina jukumu la kutuma ishara (signals) kwenda katika tezi ya pituitari ambayo yenyewe tena hutuma uchochezi wa kihomoni kwenda kwenye ovari katika mfumo wa F.S.H na L.H ili kuanzisha ukomaaji wa mayai. Ikiwa hypothalamus inashindwa kufanya kazi zake vizuri kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa ndiyo kutakuwa ni matokeo yake. Tatizo hili linachukuwa asilimia 20 katika kesi za mayai kushindwa kukomaa kiasi kinachohitajika. Ufanyaji kazi usioridhisha wa tezi ya pituitari Kazi kubwa ya tezi ya pituitari ni kuzarisha na kutoa homoni mbili maalumu kwa ajili ya mfumo wa uzarishaji kufanya kazi zake vizuri ambazo zinajulikana kitaalamu kama ‘Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ na ‘Luteinizing hormone (L.H)’. Mayai yatashindwa kukomaa vizuri ikiwa ama L.H au F.S.H zinatengenezwa chache sana au nyingi sana kuliko inavyohitajika. Hili linaweza kutokea kama sababu ya ajari, uvimbe au kama usawa usio sawa wa kikemikali katika pituitari. (2) Kovu katika Ovari Uharibifu au ajari katika ovari unaweza kupelekea kuzalishwa kwa mayai ambayo hayajakomaa. Kwa mfano, upasuaji mkubwa, uvamizi au upasuaji wa mara nyingi wa uvimbe katika ovari unaweza kusababisha kapsuli ya ovari kupata majeraha au makovu na hivyo kwa namna moja ama nyingine kuweza kuzuia utungwaji wa mayai ambayo hayajakomaa vema. Pia maambukizi katika njia ya uzazi yanaweza kupelekea tatizo hili. (3) Dalili za mwanzo za kukaribia kufunga kuzaa (Menopause) Hii huchangia kwa asilimia chache na kwa sasa halielezeki kisawasawa. Kwamba wanawake wengi wanapokaribia umri wa kuacha kuzaa kuanzia miaka 40 kwenda juu baadhi yao hutokewa na tatizo la kutunga mayai ambayo hayajakomaa vema. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao mapema kabla ya umri uliozoeleka yaani miaka 40 kwenda juu. Kwa sababu hiyo inadhaniwa kwamba uwezo wao wa asili katika kuzalisha mayai unakuwa umepunguwa na wengi wao huwa ni wale walikuwa wakijihusisha zaidi na michezo ya kukimbia au wale wenye historia ya muda mrefu ya kuwa na uzito pungufu na wafanyaji sana wa mazoezi. Tatizo hili pia linaweza kuwa ni la kurithi. (4) Matatizo kwenye kijishimo yai (follicle) katika ovari: Ingawa kwa sasa bado hili nalo halielezeki, hiki kijishimo yai kwa kitaalamu kinajulikana kama ‘’follicle’’ ndicho hupasuka na yai kutoka. Kuna baadhi ya kina mama wanapata dalili za kijishimo yai kutokupasuka “unruptured follicle syndrome” na matokeo yake kila mwezi mama anazalisha yai kama kawaida lakini hiki kijishimo yai kinashindwa kupasuka. Hivyo yai linabaki ndani ya ovari na utungaji wa mimba unashindwa kufanyika. Kinachosababisha ufanyaji kazi dhaifu wa mirija ya uzazi (Fallopian Tubes): Magonjwa katika mirija ya uzazi yanahusika na ugumba kwa karibu ya asilimia 25 ya wanawake wote wagumba. Hali yenyewe inatofautiana toka kwa mmoja hadi kwa mwingine kutoka kugandana au kunatana kidogo hadi kuzibika kabisa kwa mirija. Matibabu ya mirija iliyozibika huhusisha upasuaji au usafishaji wa mwili kwa kula vyakula na vinywaji maalum kwa muda wa majuma kadhaa. Sababu kubwa zinazopelekea kuzibika au kunatana kwa mirija ya uzazi ni pamoja na zifuatazo: (A) Maaambukizi Maambukizi katika njia ya uzazi ambayo yamesababishwa ama na bakteria au virusi na ambayo kwa kawaida ni magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya tendo la ndoa, maambukizi haya kwa kawaida husababisha muwasho au kuungua na kupelekea makovu na uharibifu. Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na mengineyo yanaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa wanawake wengi hasa ikiwa hayatatibiwa mapema. (B) Magonjwa yasiyo ya kawaida Magonjwa yasiyo ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa kidole tumbo (appendicitis) na uvimbe katika utumbo mpana (colitis), magonjwa ambayo husababisha muwasho au kuungua chini ya uvungu wa utumbo mkubwa na kuiathiri mirija ya falopiani na kama matokeo yake makovu na kuzibika kwa mirija ya uzazi hutokea. (C) Upasuaji uliopita Upasuaji una chukua nafasi kubwa katika kusababisha ugumba kutokana na matokeo yake ya kusababisha magonjwa ya mirija ya uzazi na uharibifu utokanao na huo upasuaji. Upasuaji katika utumbo mkubwa unaweza kupelekea kunatana au kugandana kwa mirija ya uzazi kutakakopelekea mayai kushindwa kusafiri kirahisi katika mirija hiyo ya uzazi. (D) Mimba kutungwa nje ya mji wa uzazi: Hii ni wakati mimba inapotungwa katikati ya mirija ya uzazi yenyewe. Katika hali kama hii hata kama kutatokea bahati kiasi gani bado kunaweza kusababisha uharibifu katika mirija na hali hii ni moja ya hali mbaya sana kiafya na kimaisha. (E) Hali ya kurithi Kwa nadra au kwa asilimia fulani ndogo baadhi ya wanawake huzaliwa na hali ya kuwa na mirija isiyo ya kawaida kwa uzazi na kwa kawaida hali hii huambatana na mji wa uzazi usio wa kawaida pia. . (5) Sababu za kitabia: Inajulikana wazi kwamba baadhi ya tabia na namna tunavyoishi kunaweza kupelekea wanandoa wakashindwa kupata mtoto. Kwa bahati nzuri nyingi kama si zote ya hizo tabia zinaweza kurekebishika au kuachwa kabisa na kupelekea siyo tu kuwa na uwezo wa kuzaa bali pia kuwa na afya nzuri kwa ujumla. Sababu hizo za kitabia ni pamoja na zifuatazo: Lishe na mazoezi Ili mfumo wa uzazi uwe na uwezo mzuri unahitaji vitu viwili mhimu, lishe kamili na mazoezi. Wanawake wenye uzito uliozidi sana au wenye uzito pungufu sana wanaweza wakapatwa na tatizo la kutopata ujauzito kirahisi. Uvutaji sigara Uvutaji wa sigara una mchango mkubwa na ugumba. Uvutaji sigara husababisha uzarishwaji wa mbegu chache kwa mwanaume (lower sperm count) kwamba mwanaume anatoa mbegu chache sana ama pungufu wakati huo huo uvutaji sigara huchangia katika tatizo la kutoka kwa mimba, kuzaa kabla ya miezi 9 (njiti), na kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo kwa wanawake. Unywaji pombe Unywaji pombe kupita kiasi una mchango mkubwa sana katika ugumba na hii hata ikitokea mama akapata ujauzito kama bado anaendelea kunywa pombe inaweza kupelekea matatizo hata kwa mtoto mtarajiwa. Unywaji pombe pia huchangia uzarishwaji wa mbegu chache kwa wanaume. Madawa ya kulevya Utumiaji a madawa ya kulevya kama bangi na mengine ya kujidunga kwa sindano kunaweza kuwa sababu ya kuzalisha mbegu chache kwa wanaume. Utumiaji wa dawa za kulevya kama ‘Cocaine’ kwa mama mjamzito kunaweza kusababisha mtindio wa ubongo na matatizo katika figo kwa mtoto mtarajiwa. Matumizi ya madawa ya kulevya inafaa yaepukwe wakati wa kutafuta ujauzito na wakati wa ujauzito. Utowaji mimba Utowaji mimba wa mara kwa mara pia unahusika sana na tatizo la ugumba kwa karibu ya asilimia 20. Utowaji mimba unaweza kusababisha makovu katika mji wa uzazi na hata kuharibika kabisa kwa mji wa uzazi ikiwa utowaji huo haukufanyika kitaalamu au unafanyika mara kwa mara. (6) Sababu za ugumba za kimazingira: Uwezo wa kushika ujauzito unaweza pia kuathiriwa kutokana na kuwa karibu na baadhi ya kemikali au sumu katika maeneo ya kazi au makazi. Vitu viwezavyo kusababisha mabadiliko, dosari za kuzaliwa, utokaji mimba, au utasa huitwa ‘Sumu kwa mfumo wa uzazi’. Kamikali zifuatazo zinahusishwa na ugumba au utasa: Risasi (Lead) Kuwa karibu na kemikali au sumu zinazounda risasi kunaweza kuwa sababu ya ugumba. Risasi hupelekea kuzalishwa kwa mbegu zisizo za kawaida kwa wanaume zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘teratospermias’ na inafikirika pia kuhusika na utokaji mimba kusiko kwa asili (artificial abortion). Baadhi ya matibabu na madawa ya hospitalini Kuwekwa kwenye matibabu yanayohusisha mionzi (x-rays), mionzi ya kawaida au hata ile ya kutibia kansa (chemotherapy), kunaweza kusababisha matatizo katika uzarishwaji wa mbegu kwa mwanaume na wakati huo huo kuchangia kwa sababu kadhaa zinazopelekea kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Pia matumizi ya dawa za kuzuia ujauzito kwa muda mrefu yamekuwa yakihusishwa na ugumba kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado kuna mjadala mkubwa katika hili. Ethylene Oxide Hii ni kemikali inayotumika kusafishia vifaa vya upasuaji, pia hutumika katika kutengeneza baadhi ya sumu za kuua wadudu. Ethylene oxide inaweza kupelekea matatizo katika uzazi hasa katika miezi ya mwanzo mwanzo ya ujauzito na inahusishwa sana na tatizo la utokaji mimba katika miezi ya mwanzo ya ujauzito (early miscarriage). Dibromochloropropane (DBCP) Hii pia ni kemikali au dawa inayotumika katika kuua wadudu, ikiwa unafanya nayo kazi kila mara inaweza kusababisha kutungwa kwa mayai yasiyokomaa vizuri, kuelekea mapema kwa ukomo wa kutokuzaa kabla hata ya miaka 40 au 45 (early menopause) na kadharika. (7) Sababu zingine zinazoweza kusababisha ugumba kwa mwanamke: Karibu asilimia 10 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya mji wa uzazi usio wa kawaida (abnormal uterus). Hali zingine ni pamoja na uvimbe katika kizazi, kugandana au kunatana kwa mji wa uzazi na mirija ya uzazi. Karibu asilimia 3 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya matatizo ya ute usio wa kawaida katika mlango wa kizazi (femaleís cervical mucus). Ute ute huu unahitaji kuwa na hali fulani maalumu kwa mbegu za kiume kuweza kuogelea kirahisi katikati yake. Chanzo kikubwa cha tatizo hili ni usawa usio sawa wa homoni za kike ambapo homoni ya uzazi ya kike iitwayo ‘estrogen’ yaweza kuwa ni chache sana au homoni nyingine iitwayo ‘progesterone’ yaweza kuwa ni nyingi sana tofauti na inavyohitajika. Vitu vya kuepuka kwa mtu mwenye tatizo la ugumba: ChipsiVinywaji baridiKaffeinaNyama nyekunduVilevi ... Read More
Kufanya Mapenzi Kwa Wiki Mara 3 Kunapunguza Kupata Shambulio La Moyo (Heart Attack) Kwa Asilimia 50%  Utafiti umebainisha kwamba kufanya mapenzi angalau mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupatwa Heart Attack (Shambulio la Moyo) kwa 50% ukilinganishwa na yule ambaye anapitisha wiki nzima bila kupiga mambo yetu. Pia utafiti huo unasisitiza ya kwamba mwenye Kufanya Mapenzi killa siku anaondoa uwezekano wa kupata Heart Attack kwa Asilimia 100% ZIJUE FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI Kiafya Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75. Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani. Kuongeza mwendo wa damu Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji. Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili. Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol) Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini. Kupunguza maumivu Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa. Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate. Kupunguza mfadhaiko wa moyo Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi. Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen) Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo. Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular). Hupunguza baridi na mafua Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa. Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa. NB: Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa HAYA KWA WANA NDOA FANYENI MAPENZI JAPO KWA WIK MARA 3 MUPATE FAIDA ZA TENDO LA MAPENZI NDANI YA NDOA. KWA WALE WASIOWA HAWAPATI HIZI FAIDA SHAURI YENU MSIE OWA OWENI MUPATE FAIDA ZA TENDO LA NDOA ... Read More
AINA 10 ZA WANAUME AMBAO WANAWAKE HUJUTIA WAKIWA NAO  1. Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband). HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea. 2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake. 3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband). Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke. 4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband). Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida. 5. Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband). Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao. 6. Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband). Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena. 7. Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband). Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa. 8. Mume Mtalii (Visiting Husband). Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto. 9. Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke. 10. Mwanaume Mbahili (Miserly Husband). Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: