Home → ushauri
→ ❤FAIDA 15 ZA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA❤
Tendo la ndoa tangu uumbaji lililengwa kati ya mwanaume na mwanamke waliofunga ndoa,
sasa hivi dunia imebadilika sana kiasi kwamba tendo hili sio lazima kuliita la ndoa tena. watu wengi wamekua wakishiriki tendo la ndoa bila kufungua ndoa .. vile vile kutokujua faida zake.lakini tendo la ndoa lina faida nyingi sana kiafya na kisaikolojia.
Hivyo kama wewe una mke, mchumba au mpenzi halafu kila siku unampa sababu za kutoshiriki basi huenda hujui faida zake. hebu tuzisome kama ifuatavyo..
👉🏿 HUONDOA MSONGO WA MAWAZO;
kipindi cha tendo la ndoa mwili hutoa hormone inayoitwa kitaalamu kama endophirn ambayo huleta furaha.kila aliyeshiriki tendo la ndoa atakua shahidi kama una msongo wa mawazo sana ukaenda kufanya tendo hili utajikuta unajisikia vizuri sana,
👉🏿 HUPUNGUZA PRESHA YA DAMU;
wakati wa tendo la ndoa damu inapita kwa kasi sana kwenye mishipa ya damu na kuondoa vikwazo kama mafuta, lehemu na kunyoosha mishipa iliyosinyaa.utafiti unaonyesha tendo la ndo hushusha presha ya chini kitaalamu kama diastolic pressure.
👉🏿 HUONGEZA KINGA YA MWILI;
askari wa mwili kwa jina immunoglubin hutolewa na mwili kupambana na magonjwa wakati wa tendo la ndoa, kama huamini basi shiriki tendo la ndoa ukiwa na mafua na baadae utashindwa kuelewa mafua yameenda wapi.
👉🏿 HUIMARISHA MAHUSIANO;
kuna homoni ya furaha na uzazi inaitwa oxytocin homoni, homoni hii hutengenezwa na mwili kipind cha tendo la ndoa.kama umekaa kwenye mahuasiano muda mrefu utagundua kwamba ikitokea umegombana na mpenzi wako halafu mkafanya tendo la ndoa basi ugomvi unaisha bila hata kuongelea swala lililowagombanisha.
👉🏿 HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KANSA YA TEZI DUME;
utafiti uliofanyika nchini australia uligundua kwamba wanaume wanaoshiriki tendo la ndoa angalaua mara 21 kwa mwezi wako kwenye hatari ndogo sana ya kupata kansa ya tezi dume kuliko wale wasioshiriki hivyo kama mpenzi au mke wako hakupi ushirikiano basi atakuletea kansa.
👉🏿 HUSAIDIA KUPATA HEDHI KWA WAKATI;
tendo la ndoa huweka homone za uzazi kitaalamu kama oestrogen na progesterone kwenye kiwango sawa. hii husaidia kupata siku zako kwa wakati na bila maumivu.kimsingi tendo la ndoa husaidia sana kuliko vidonge vya uzazi ambavyo humezwa na watu ambao hawaoni siku zao.
👉🏿 HULETA USINGIZI WA KUTOSHA;
hii haihitaji ubishi au ushahidi mara nyingi baada ya kushiriki tendo la ndoa hata kama ni mchana kila mtu hupata uchovu fulani na kujikuta unapitiwa na usingizi kwa muda mrefu.
👉🏿 NISEHEMU YA MAZOEZI;
tendo la ndoa lina faida zote ambazo mtu anayefanya mazoezi anazipata ikiwemo kupungua uzito, kua na afya bora hata kuondoa kitambi kwani wakati wa tendo la ndoa mapigo ya moyo huongezeka, kasi ya upumuaji hua juu na kua sawa na mtu wa mazoezi.
👉🏿 HUKUFANYA UISHI MUDA MREFU;
moja ya sababu kuu zinazofanya watu wafe mapema ni kukosa furaha ya maisha, na kua na afya ambayo sio nzuri.watu wanaoshiriki tendo la ndoa wanapata faida za kua na afya bora na furaha.
👉🏿 HUONGEZA NGUVU ZA KIUME NA UWEZO WA KUFANYA TENDO;
watu wengi wenye umri zaidi ya miaka 40 huanza kupungukiwa nguvu za kiume. hii ni sababu ya damu kidogo ambayo inafika kwenye uume. tendo la ndoa mara kwa mara hupeleka damu nyingi kwenye uume na kukufanya ue na uume imara na wenye nguvu.
👉🏿 HUKIFANYA UONEKANE MDOGO KIUMRI;
tendo la ndoa mara kwa mara hukufanya mwili uwe bize kumwaga homoni mbalimbali mwilini ambazo humfanya mtu aonekane mdogo kwa miaka kumi ukilinganisha na umri wake halisi.
👉🏿 HUIMARISHA AFYA YA MOYO;
tendo la ndoa huchoma mafuta ambayo ni sumu kwa moyo, mafuta mengi huweza kuziba mishipa ya moyo na kusababisha shambulio la moyo kitaalamu kama heart attack.
👉🏿 HUONGEZA NGUVU KWENYE MISULI YA NYONGA;
katika umri fulani mkubwa wanawake hupata matatizo ya kushindwa kuzuia mkojo sababu ya kuzaa mara kwa mara. kipindi cha tendo la ndoa wakati mwanamke anafika kileleni uke wake unabana sana na kufanya misuli yake ya nyonga kua na nguvu.
👉🏿 HUPUNGUZA MAUMIVU;
utafiti uliofanywa na madaktari bingwa wa mifupa umegundua kwamba wagonjwa wa baridi yabisi au athritis ambao wanashiriki tendo la ndoa mara kwa mara hawasumbuliwi sana na maumivu kama hao wasio shiriki.
❤FAIDA 15 ZA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA❤ Tendo la ndoa tangu uumbaji lililengwa kati ya mwanaume na mwanamke waliofunga ndoa, sasa hivi dunia imebadilika sana kiasi kwamba tendo hili sio lazima kuliita la ndoa tena. watu wengi wamekua wakishiriki tendo la ndoa bila kufungua ndoa .. vile vile kutokujua faida zake.lakini tendo la ndoa lina faida nyingi sana kiafya na kisaikolojia. Hivyo kama wewe una mke, mchumba au mpenzi halafu kila siku unampa sababu za kutoshiriki basi huenda hujui faida zake. hebu tuzisome kama ifuatavyo.. 👉🏿 HUONDOA MSONGO WA MAWAZO; kipindi cha tendo la ndoa mwili hutoa hormone inayoitwa kitaalamu kama endophirn ambayo huleta furaha.kila aliyeshiriki tendo la ndoa atakua shahidi kama una msongo wa mawazo sana ukaenda kufanya tendo hili utajikuta unajisikia vizuri sana, 👉🏿 HUPUNGUZA PRESHA YA DAMU; wakati wa tendo la ndoa damu inapita kwa kasi sana kwenye mishipa ya damu na kuondoa vikwazo kama mafuta, lehemu na kunyoosha mishipa iliyosinyaa.utafiti unaonyesha tendo la ndo hushusha presha ya chini kitaalamu kama diastolic pressure. 👉🏿 HUONGEZA KINGA YA MWILI; askari wa mwili kwa jina immunoglubin hutolewa na mwili kupambana na magonjwa wakati wa tendo la ndoa, kama huamini basi shiriki tendo la ndoa ukiwa na mafua na baadae utashindwa kuelewa mafua yameenda wapi. 👉🏿 HUIMARISHA MAHUSIANO; kuna homoni ya furaha na uzazi inaitwa oxytocin homoni, homoni hii hutengenezwa na mwili kipind cha tendo la ndoa.kama umekaa kwenye mahuasiano muda mrefu utagundua kwamba ikitokea umegombana na mpenzi wako halafu mkafanya tendo la ndoa basi ugomvi unaisha bila hata kuongelea swala lililowagombanisha. 👉🏿 HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KANSA YA TEZI DUME; utafiti uliofanyika nchini australia uligundua kwamba wanaume wanaoshiriki tendo la ndoa angalaua mara 21 kwa mwezi wako kwenye hatari ndogo sana ya kupata kansa ya tezi dume kuliko wale wasioshiriki hivyo kama mpenzi au mke wako hakupi ushirikiano basi atakuletea kansa. 👉🏿 HUSAIDIA KUPATA HEDHI KWA WAKATI; tendo la ndoa huweka homone za uzazi kitaalamu kama oestrogen na progesterone kwenye kiwango sawa. hii husaidia kupata siku zako kwa wakati na bila maumivu.kimsingi tendo la ndoa husaidia sana kuliko vidonge vya uzazi ambavyo humezwa na watu ambao hawaoni siku zao. 👉🏿 HULETA USINGIZI WA KUTOSHA; hii haihitaji ubishi au ushahidi mara nyingi baada ya kushiriki tendo la ndoa hata kama ni mchana kila mtu hupata uchovu fulani na kujikuta unapitiwa na usingizi kwa muda mrefu. 👉🏿 NISEHEMU YA MAZOEZI; tendo la ndoa lina faida zote ambazo mtu anayefanya mazoezi anazipata ikiwemo kupungua uzito, kua na afya bora hata kuondoa kitambi kwani wakati wa tendo la ndoa mapigo ya moyo huongezeka, kasi ya upumuaji hua juu na kua sawa na mtu wa mazoezi. 👉🏿 HUKUFANYA UISHI MUDA MREFU; moja ya sababu kuu zinazofanya watu wafe mapema ni kukosa furaha ya maisha, na kua na afya ambayo sio nzuri.watu wanaoshiriki tendo la ndoa wanapata faida za kua na afya bora na furaha. 👉🏿 HUONGEZA NGUVU ZA KIUME NA UWEZO WA KUFANYA TENDO; watu wengi wenye umri zaidi ya miaka 40 huanza kupungukiwa nguvu za kiume. hii ni sababu ya damu kidogo ambayo inafika kwenye uume. tendo la ndoa mara kwa mara hupeleka damu nyingi kwenye uume na kukufanya ue na uume imara na wenye nguvu. 👉🏿 HUKIFANYA UONEKANE MDOGO KIUMRI; tendo la ndoa mara kwa mara hukufanya mwili uwe bize kumwaga homoni mbalimbali mwilini ambazo humfanya mtu aonekane mdogo kwa miaka kumi ukilinganisha na umri wake halisi. 👉🏿 HUIMARISHA AFYA YA MOYO; tendo la ndoa huchoma mafuta ambayo ni sumu kwa moyo, mafuta mengi huweza kuziba mishipa ya moyo na kusababisha shambulio la moyo kitaalamu kama heart attack. 👉🏿 HUONGEZA NGUVU KWENYE MISULI YA NYONGA; katika umri fulani mkubwa wanawake hupata matatizo ya kushindwa kuzuia mkojo sababu ya kuzaa mara kwa mara. kipindi cha tendo la ndoa wakati mwanamke anafika kileleni uke wake unabana sana na kufanya misuli yake ya nyonga kua na nguvu. 👉🏿 HUPUNGUZA MAUMIVU; utafiti uliofanywa na madaktari bingwa wa mifupa umegundua kwamba wagonjwa wa baridi yabisi au athritis ambao wanashiriki tendo la ndoa mara kwa mara hawasumbuliwi sana na maumivu kama hao wasio shiriki.
Artikel Terkait
UMESOMA HADITHI NYINGI ZA MAPENZI, LAKINI HII ITAKUSISIMUA KULIKO ZOTE, UTATUMIA DAKIKA 2 KUSOMA LAKINI...  1st year nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo. Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why 2nd year Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia "asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. 3rd year Siku moja kabla ya Tamasha la muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia "Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as "bestfriends".hivyo tukaenda. katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Graduation Day siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but she didn't notice me like that,and i knew it. kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia "you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Miaka michache baadae Nikiwa kanisani Yule Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be mine,but she didn't see me like that,and i knew it. but before she drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Kwenye Mazishi Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo' Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I wish he would tell me he loved me! Nilipiga magoti huku nikilia nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo nae tena katangulia mbele za haki i cried!! Vunja ukimya ... Read More
Jinsi ya Kuomba Msamaha MACHAGUO YA UPAKUAJI Podikasti Makala Nyinginezo SOMA KATIKA Amkeni! | Septemba 2015 UNAWEZA KUWA NA FAMILIA YENYE FURAHA Fuata Mwongozo wa Mungu ili Uwe na Ndoa Yenye Furaha Kujiuliza maswali mawili rahisi kunaweza kuisaidia ndoa yako. AMKENI! Viwango Vinavyomfaa Kila Mtu, Nyakati Zote—Upendo Upendo unaotajwa mara nyingi katika Biblia si ule wa kimahaba au kimapenzi. HABARI NJEMA KUTOKA KWA MUNGU! Kanuni za Biblia Zinatunufaishaje? Yesu alieleza kwa nini tunahitaji mwongozo na ni kanuni gani mbili za Biblia zina umuhimu mkubwa. Kuwafundisha Watoto Unyenyekevu Je, Inafaa Kujihatarisha Kwa Kusudi la Kujisisimua? Watoto Wanapoondoka Nyumbani Umuhimu wa Kazi za Nyumbani Kuomba msamaha kunaweza kuzuia ugomvi CHANGAMOTO Muda mfupi tu uliopita wewe na mwenzi wako mmetoka kubishana. Kisha unajiambia hivi: ‘Sihitaji kumwomba msamaha. Kwa sababu si mimi niliyeanzisha ugomvi!’ Mmeacha kuzungumzia jambo hilo, lakini hali si shwari. Unafikiria kuomba msamaha lakini unaona huwezi kusema, “samahani.” KWA NINI HILO HUTUKIA Kiburi. “Wakati mwingine si rahisi kusema ‘samahani’ kwa sababu sitaki kujishushia heshima,” anakiri mume anayeitwa Charles. * Kiburi kinaweza kukufanya uone aibu kukubali kwamba umechangia tatizo. Mtazamo. Unaweza kuhisi kwamba kuomba msamaha kunahitajika tu pale unapokosea. Mke anayeitwa Jill anasema hivi: “Ni rahisi kwangu kusema ‘samahani’ ninapojua kwamba nimesababisha tatizo. Lakini, ikiwa sote tulisema mambo yasiyofaa, ni vigumu kufanya hivyo. Kwa nini niombe msamaha ikiwa sote tuna makosa?” Unaweza kujitetea ikiwa unahisi kwamba mwenzi wako ndiye mwenye makosa. “Unapoamini kabisa kwamba hujafanya kosa lolote, unaonyesha huna hatia kwa kukataa kuomba msamaha,” anasema mume anayeitwa Joseph. Malezi. Huenda ulilelewa katika familia ambayo halikuwa jambo la kawaida kuomba msamaha. Ikiwa ndivyo, huenda hukujifunza kukubali makosa yako. Kwa kuwa hukuzoea kufanya hivyo tangu utotoni, ni vigumu kwako kuomba msamaha ukiwa mtu mzima. MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA Mfikirie mwenzi wako. Jaribu kukumbuka jinsi ulivyohisi vizuri ulipoombwa msamaha na mtu fulani. Kwa nini basi usimfanye mwenzi wako ahisi hivyo? Hata ikiwa huamini kwamba ulikosea, unaweza kuomba msamaha kwa ajili ya maumivu ambayo mwenzi wako amepata au kwa sababu ya usumbufu wowote uliotokana na matendo yako. Maneno hayo yanaweza kumsaidia mwenzi wako ahisi vizuri.— Kanuni ya Biblia: Luka 6:31 . Zingatia ndoa yako. Ona kuomba msamaha kuwa ushindi katika ndoa yako na si kushindwa. Zaidi ya yote, mtu anayeendelea kukasirika ni “mgumu kuliko mji wenye nguvu,” inasema Methali 18:19 . Inaweza kuwa vigumu kurudisha amani katika hali hiyo. Pia, unapoomba msamaha unazuia kosa kuwa kikwazo. Ukifanya hivyo, unatanguliza ndoa yako badala ya hisia zako.— Kanuni ya Biblia: Wafilipi 2:3 . Uwe mwepesi kuomba msamaha. Ni kweli kwamba ni vigumu kuomba msamaha ikiwa hujakosea. Lakini makosa ya mwenzi wako hayapaswi kuwa kisingizio cha kuendelea kuwa na tabia mbaya. Hivyo, usisite kuomba msamaha ukifikiri kwamba muda ukipita kosa hilo litasahaulika. Unapoomba msamaha unafanya iwe rahisi pia kwa mwenzi wako kuomba msamaha. Na kadiri unavyoomba msamaha ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kufanya hivyo tena wakati mwingine.— Kanuni ya Biblia: Mathayo 5:25 . Onyesha kwamba unajali hisia za mwenzi wako. Kutetea kosa lako si sawa na kuomba msamaha. Kusema kwa kejeli, “samahani kwa kuwa naona unakwazika haraka kwa sababu ya jambo hili,” si njia ya kuomba msamaha hata kidogo! Kubali makosa yako na utambue kwamba umemuumiza mwenzi wako, hata kama unaona hakuwa na sababu ya kukwazika. Tambua ukweli. Kubali kwamba utafanya makosa. Kwa kweli, kila mtu hukosea! Hata kama unafikiri huna hatia, tambua kwamba kuna uwezekano umechangia jambo hilo. Biblia inasema hivi: “Mtu wa kwanza katika kesi yake ni mwadilifu, mwenzake huingia naye hakika humchunguza kwa undani.” ( Methali 18:17 ) Itakuwa rahisi kwako kuomba msamaha ikiwa una maoni yaliyosawazika kuhusu mapungufu yako ... Read More
JIFUNZE KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPENZI YA DHATI NA WEWE: Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi". Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. MTU AMBAYE HAKUPENDI KWA DHATI: ==> Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako. ==> Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?" Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo". Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu. ==> Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo. ==> Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie. ==> Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. ===> Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo. MTU ANAYEKUPENDA KWA DHATI: ==> Hachoki kukwambia NAKUPENDA, kwani anajisikia raha sana pale atamkapo neno hilo juu yako kwahiyo unaweza ukawa kama wimbo wake kwako. ==> Anajivunia kuwa na wewe na atapenda kukupa sifa nzuri kila mara, yani Hachoki kukusifia. Atakushauri pale unapokosea ili uwe katika njia nzuri. Unaponuna atajua cha kufanya ili wewe ufurahi na kurudi kwenye hali ya kawaida. ==> Hachoki kukuombea mema na kukutakia mafanikio. ==> Atapenda kukueleza ukweli kila mara ili uweze kujenga uaminifu na imani juu yake. ==> Wewe utakuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake, atakuthamini na kukujali. Tatizo lako litakuwa sawa na tatizo lake, atakupa ushauri bila kuchoka. ==> Kabla ya kumuuliza swali kuwa "je unanipenda?" atakuwa ameshakujibu tena kwa hisia nzito kuwa "nakupenda sana mpenzi wangu". ==> Hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, kwakuwa wewe ndiye furaha yake. ====> Thamani yako ni kubwa sana kwake, anakuona mpya kila siku na hachoki kuvutiwa na wewe. Anakupenda kwa kumaanisha na si kukupenda kimazoea tu. Neno NAKUPENDA litamtoka moyoni na ataridhihirisha kwa kinywa chake. Mtambue mtu huyu kuwa anakupenda kwa dhati. NB: Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Si vyema kutumia mapungufu ya mwenzio kama fimbo katika mapenzi, cha muhimu ni kumuelimisha na kumuelekeza ili muweze kwenda sambamba. Nadhani baadhi ya maswali ya wadau yatakuwa yamejibiwa na hiyo mada. Kama kuna nyongeza au swali lolote kuhusiana na hiyo mada tuambiane hapa na kupatiana majibu hapa hapa wadau. ... Read More
MADHARA YA MWANAMKE KUZAA MFULULIZO BILA KUPUMZIKA.  Ni wazi vifo vya uzazi vimekuwa vikisababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo ya mwanamke kuzaa mfululizo bila kupumzika hivyo kutokana na hali hiyo ipo haja kwa wakuu wa mikoa ya kanda ya magharibi, kanda ya ziwa na kwingineko kuongeza juhudi zaidi katika kuwaelimisha wananchi wake umuhimu wa kutumia njia ya uzazi wa mpango. Wakuu hao wana kazi ya kuondoa mila na desturi za wananchi wa ukanda huo ili waondokane na mila hizo zilizopitwa na wakati kwa kutumia njia sahihi za uzazi wa mpango katika kuwezesha taifa kukua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi, Takwimu za nchi zinaonyesha kanda ya magharibi inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya kuzaana na kufikiwa asilimia 7.1 ikifuatiwa na kanda ya ya kati na kufuatiwa na kanda ya ziwa hali hii pia inachangia ongezeko la vifo vya uzazi kwa wanawake kutopumzika. Kuna haja wananchi kuelimishwa kuwa matumizi mazuri ya njia ya uzazi hayana madhara mwilini ili waweze kuzaa kwa mpango na kupunguza vifo vya uzazi.  Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alizindua mpango mkakati ulioboreshwa wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na kuwataka watendaji wake katika mikoa yote nchini, ambao ni wakuu wa mikoa kuwa wahakikishe wanapunguza vifo vya watoto na akinamama wanaokufa kwa matatizo ya uzazi. ... Read More
Kanuni Kumi '10' Muhimu za Kuwa Mke Mwema Katika Ndoa....Ikizishindwa Imekula Kwako  UHALISI WA MAISHA: Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo; UVUMILIVU: Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo. UPENDO WA DHATI: Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni Upendo wa dhati na uhalisia. UTII KWA KWA JAMII: Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa. UAMINIFU KATIKA JAMII: Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote. UNYENYEKEVU WA KWELI: Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima. UWAJIBIKAJI WA DHATI: Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake. USHIRIKIANO WA DHATI: Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora. UTARATIBU WA KAZI/MPANGILIO: Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako. KUFANYA TATHIMINI: Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku, pengine ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima n.k kama mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta faida/hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka. Ukiona faida ni kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka katika nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza wakati. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: