Home → ushauri
→ B professional love
SABABU ZA KUTOKA HARUFU MBAYA UKENI NA NAMNA YA KUJIKINGA
Tarehe September 8, 2014
Wanawake na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchavu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili… Kihalisi, badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua… Japokuwa ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga
VISABABISHI
i. Bacteria
Tatizo hili husababishwa na Bakteria kwa asilimia kubwa. Kwa asili, ukeni huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni kufanya mazingila ya uke kuwa katika hali nzuri. Kutokana na njia mbaya za kusafisha uke, hasa kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia sabuni zenye dawa, husababisha bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake kuchukuliwa na aina zingine za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha tatizo hili.
Pia kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna hatari ya kuhamishia bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na kuwaamishia ukeni ambapo watazaliana na kukuletea madhala haya.
ii. Kuvu(fungus)
Hii mara nyingi huambatana na uchafu mzito utokao ukeni mfano wa maziwa mgando(mtindi)
iii. Magonjwa ya zinaa(STIs)
Kwa asilimia kubwa husababisha na Chlamyidia na kisonono(gonorrhoea). Yote mawili hutibika kirahisi, ila husababisha madhala makubwa zaidi yasipotibiwa kwa wakati. Tukio baya ni kuwa mwanamke anaweza akawa na magonjwa haya na asione dalili yoyote. Ila mara nyingine mwanamke anaweza kujisikia maumivu anapokojoa, na mara nyingine mkojo unakuwa kama una ukungu, vikiambatana na harufu mbaya.
iv. Maambukizi ya via vya uzazi vilivyo ndani ya nyonga[Pelvic Inflammatory Diseases(PID)]
Hii husababishwa na bacteria waambukizwao kwa njia ya ngono wanapofanikiwa kufika kwenye tumbo la uzazi na hata pia mirija ya mimba na hata kokwa(ovaries), hasa chlamydia. Mara nyingi mwanamke anaweza asijisikie chochote hadi pale atakapojisikia maumivu yasiyokwisha ya tumbo(chini ya kitovu), au itakapoingiliana na utungaji wa mimba. Na kama atajisikia, mara nyingi huwa ni maumivu ya nyonga, harufu mbaya, uchafu mzito ukeni, homa, maumivu wakai wa kukojoa na hata maumivu wakati wa kujamiiana.
Tatizo hili lisipotibiwa mapema laweza kusababisha utasa, ama mimba kutunga nje ya mji wa mimba.
v. Kansa ya uke na kansa ya shingo ya kizazi
Asilimia chache sana ya wanawake inaweza ikawa ni kutokana na kansa ya shingo ya kizazi ama ya uke. Hapa ndipo inapoonyesha kuwa tatizo hili siyo la kufumbia macho, na umuhimu wa kuwahi kwa wataalam wa tiba kwa uchunguzi wa mapema na kabla tatizo halijawa kubwa.
vi. Uchafu
Usipokuwa msafi kwa kiwango kikubwa utakuwa unakaribisha wadudu kuzaliana na kukuletea madhala. Pia unatakiwa kuwa makini wakati wa hedhi, na pia uchaguzi wa pedi, kwani kuna pedi ambazo zina kemikali za kukata harufu zinaweza kukudhulu.
JINSI YA KUJIKINGA
• Usiwe unaosha ukeni kupita kiasi kwani husababisha kuondoa bacteria wa asili wa ukeni(Lactobacilli) na kukaribisha bacteria wenye madhala.
• Pia epuka sabuni zenye dawa(antibacterial soap) usafishapo ukeni, kwani hii pia huua bacteria wa asili wa ukeni.
• Hii haimaanishi usiwe unasafisha ukeni. Usafi ni muhimu, kwani uchafu pia hukaribisha vimelea vya magonjwa.
• Kama tatizo limeshajitokeza, wahi haraka kwa wataalam wa tiba wakufanyie uchunguzi na kujua ni kipi kati ya vilivyotajwa hapo juu kilichosababisha. Daktari atakuchunguza na kujua kama ni bacteria, fungus ama ni dalili za awali za kansa na kuchukua hatua mapema kuepusha madhala zaidi.
• Kumbuka kujisafisha kupindukia si suluhisho kama tatizo limeshajitokea, kwani kunaweza kuzidisha tatizo badala ya kusuluhisha.
B professional love SABABU ZA KUTOKA HARUFU MBAYA UKENI NA NAMNA YA KUJIKINGA Tarehe September 8, 2014 Wanawake na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchavu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili… Kihalisi, badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua… Japokuwa ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga VISABABISHI i. Bacteria Tatizo hili husababishwa na Bakteria kwa asilimia kubwa. Kwa asili, ukeni huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni kufanya mazingila ya uke kuwa katika hali nzuri. Kutokana na njia mbaya za kusafisha uke, hasa kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia sabuni zenye dawa, husababisha bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake kuchukuliwa na aina zingine za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha tatizo hili. Pia kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna hatari ya kuhamishia bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na kuwaamishia ukeni ambapo watazaliana na kukuletea madhala haya. ii. Kuvu(fungus) Hii mara nyingi huambatana na uchafu mzito utokao ukeni mfano wa maziwa mgando(mtindi) iii. Magonjwa ya zinaa(STIs) Kwa asilimia kubwa husababisha na Chlamyidia na kisonono(gonorrhoea). Yote mawili hutibika kirahisi, ila husababisha madhala makubwa zaidi yasipotibiwa kwa wakati. Tukio baya ni kuwa mwanamke anaweza akawa na magonjwa haya na asione dalili yoyote. Ila mara nyingine mwanamke anaweza kujisikia maumivu anapokojoa, na mara nyingine mkojo unakuwa kama una ukungu, vikiambatana na harufu mbaya. iv. Maambukizi ya via vya uzazi vilivyo ndani ya nyonga[Pelvic Inflammatory Diseases(PID)] Hii husababishwa na bacteria waambukizwao kwa njia ya ngono wanapofanikiwa kufika kwenye tumbo la uzazi na hata pia mirija ya mimba na hata kokwa(ovaries), hasa chlamydia. Mara nyingi mwanamke anaweza asijisikie chochote hadi pale atakapojisikia maumivu yasiyokwisha ya tumbo(chini ya kitovu), au itakapoingiliana na utungaji wa mimba. Na kama atajisikia, mara nyingi huwa ni maumivu ya nyonga, harufu mbaya, uchafu mzito ukeni, homa, maumivu wakai wa kukojoa na hata maumivu wakati wa kujamiiana. Tatizo hili lisipotibiwa mapema laweza kusababisha utasa, ama mimba kutunga nje ya mji wa mimba. v. Kansa ya uke na kansa ya shingo ya kizazi Asilimia chache sana ya wanawake inaweza ikawa ni kutokana na kansa ya shingo ya kizazi ama ya uke. Hapa ndipo inapoonyesha kuwa tatizo hili siyo la kufumbia macho, na umuhimu wa kuwahi kwa wataalam wa tiba kwa uchunguzi wa mapema na kabla tatizo halijawa kubwa. vi. Uchafu Usipokuwa msafi kwa kiwango kikubwa utakuwa unakaribisha wadudu kuzaliana na kukuletea madhala. Pia unatakiwa kuwa makini wakati wa hedhi, na pia uchaguzi wa pedi, kwani kuna pedi ambazo zina kemikali za kukata harufu zinaweza kukudhulu. JINSI YA KUJIKINGA • Usiwe unaosha ukeni kupita kiasi kwani husababisha kuondoa bacteria wa asili wa ukeni(Lactobacilli) na kukaribisha bacteria wenye madhala. • Pia epuka sabuni zenye dawa(antibacterial soap) usafishapo ukeni, kwani hii pia huua bacteria wa asili wa ukeni. • Hii haimaanishi usiwe unasafisha ukeni. Usafi ni muhimu, kwani uchafu pia hukaribisha vimelea vya magonjwa. • Kama tatizo limeshajitokeza, wahi haraka kwa wataalam wa tiba wakufanyie uchunguzi na kujua ni kipi kati ya vilivyotajwa hapo juu kilichosababisha. Daktari atakuchunguza na kujua kama ni bacteria, fungus ama ni dalili za awali za kansa na kuchukua hatua mapema kuepusha madhala zaidi. • Kumbuka kujisafisha kupindukia si suluhisho kama tatizo limeshajitokea, kwani kunaweza kuzidisha tatizo badala ya kusuluhisha.
Artikel Terkait
Kwa wanawake tu! Jinsi ya kujisafisha uke  Naomba kufahamishwa na wanawake jinsi ya kujisafisha kwenye papuchi(mwanaume atakaye shauri naomba awe doctor au mwenyewe experience ya kutosha kuhusu maumbile ya mwanamke) Mimi huwa nikienda kuoga natumia sabuni ya jamaa kusafisha juu kabisa ya papuchi yaani kwenye mapaja na pale juu kwenye nyw**le...then natumia maji mengi kujisuuza na kuingiza kidole ndani kidogo ya K kutoa uchafu either wa period kama niko P na sometimes nakuta kuna ule uchafu mweupe wanaita(utoko) but huo uchafu huwa ni mweupe kama barafu na pia haunuki kabisaa..... Sasa swali ni kwamba kuna watu wanadai hatupaswi kutoa huo uchafu eti ni bacteria wa kukinga K isipate madhra so hupaswi kuingiza kidole kabisa.... tuoshe juujuu tu...... Second wengine wanasema tusinawe na sabuni kabisaa(japo kama nilivyosema mimi sabuni napitisha kwa juu kabisa tena nikiwa nimesimama ili isiweze kuingia kwenye K coz siamin kama kujisafisha bila sabuni harufu ya mkojo, harufu ya P na jasho itaisha kwa kunawa na maji tu.....na situmii sabuni zenye chemical). Naomba wanake wenzangu mnipe experience zenu juu ya hili ... Read More
Mbinu za kufufua penzi lenu 1. Badilisha mavazi yako . Ikiwa bidhaa za kampuni unayoipenda zinabadilika baada ya miaka michache ili kupata umaruufu kwa wateja wake,pia wewe badilisha sura yako kwa kubadilisha mavazi na mfumo wa nywele ili umfurahishe mpenzi wako. Hata kama umekuwa ukipendeza kwa mavazi yako, mpenzi wako tayari amekuzoea hivyo. Nunua nguo mpya, chupi mpya, jaribu mtindo mwingine wa kutengeneza nywele ndiposa mpenzi wako akuone kama mgeni vile. 2. Hamia nyumba mpya Ukiwa umekuwa ukiishi katika mtaa mmoja kwa miaka mingi ,badilisha maeneo yako. Gura kwenda kwenye mtaa mpya, hili litakusaidia Kubadilisha mazingira na itaisisismua akili na kufurahia mukiwa pamoja. 3. Badilisha mfumo wa chumba chako cha kulala. Panga vitu upya,ondoa vitu za kitambo,nunua vitu vipya,paka rangi tofauti tofauti kwenye ukuta wako. Chumba cha kulalia kinapaswa kuwa cha kuvutia mno, badilisha mipangilio ya chumba chako mukiwa pamoja na mpenzi wako ndivyo nyiyi wote mumiliki mabadiliko hayo. 4. Omba msamaha nawe umsamehe. Ni vigumu kuwa na urafiki wakati masuala tata kati yenu hayajatatuliwa. Usipuuze maswala ambayo ni kawaida katika uhusianio,upendo wa dhati sio eti kwa sababu hamgombani wewe na mpenzi wako Upendo wa dhati ni uwezo wa kusuluhisha matatizo kati yenu. Omba msamaha wakati umekosea nawe msamehe wakati umekosewa. 5. Endeni mjivinjari kwa tarehe Endeni likizo au tokeni nje pamoja. Mkiwa nyote kwenye kwenye mazingira mapya inaweleta nyote pamoja. 6.Kataeni hamu ya kutizama picha za kujamiana. Watu wengi wanaohusiano hudhani kuwa kuangalia picha hizo za kujamiana ni kitu kizuri ilhali ni jambo hatari sana. Jiulize mbona watu huangalia picha hizi? Kwa ajili ya kusisimua hali yao ya ngono?. Kutegemea picha hizi kusisimua fataki kati yenu inamyang'anya mpenzi wako mamlaka ya kukusisimua mwenyewe. Je inammanisha kuwa mpenzi wako hawezi kukusisimua? Kama ni hivyo picha hizi hazisaidi kutengeneza hali zinaharibu. Picha hizi zinafanya mapenzi yawe duni ilhali ni mmoja wapo wa kuwa na mapenzi. Rudisha mapenzi na uwacha picha hizo mbaya ndiposa mpenzi wako aweze kujisalamisha kwako na ni jukumu lenu kusisimuana hisia kali za mahaba ile umruhusu awe spesheli kwako nawe kwake. 7. Jisalimishe upya Kama fataki katika yenu yamekuwa yakididimia tatizo ni lenu. Je unampenda kama awali? Je unanipenda kweli? Ondoa hofu hizo kwa kumhakikishia penzi lenu. Hii ndiyo sababu wapenzi husherekea penzi lao. 8. Weka mtoto mbali na maswala yenu ya Huba. Ni vizuri kuwa na watoto na kuwa karibu nao lakini wakti mwengine ni vyema watoto kuwa mbali na wazazi ili waweze kuwa na mda wao wa kipekee . Tunza watoto kutokana na penzi lenu, penzi lenu likiingiiliwa kati basi uwezo wenu kama wazazi utaadhirika. 9. Epuka kuumiza mwenzako Punguza visa vya kumuudhi na kumumiza mwenzako. Roho iliyoumizwa ni vigumu kupenda. 10. Mbusu mpenzi wako zaidi. Mabusu huleta watu pamoja. Unavyo mbusu zaidi ndivyo munavyo chochea penzi. 11. Omba Mungu anajali kuhusu penzi lenu na ndoa yenu. Ombeni kwa pamoja kuhusu shida za penzi lenu. 12. Tenga wakati wa Faragha Tenga wakati mahsusi kwa mpenzi wako. Wanandoa wengi huwa na wakati mgumu sana kutenga muda maalum kuwa na wapenzi wao kutokana na majukumu ya maisha kama vile kazi safari watoto na kadhalika lakini Jitahidi uweke kando muda maalum ambao utakaa karibu naye msemezane Mkumbatiane mkumbushane haswa mlikotoka na mnakokwenda . Ni muhimu sana. 13. Usilete majukumu yako ya kikazi nyumbani. Ni vyema kufanya kazi ili kujipatia riziki yako na familia yako lakini kazi hiyo isalie kule afisini wala isiletwe nyumbani kamwe. Usije na kazi yako ndani ya chumba chenyu cha kulala au ufanye mpenzi wako ahisi kuwa unamnyanyasa kwa sababu licha ya kuwa ulimuuowa mpenzi wako lakini umeoleka kwa kazi yako. 14. Weka teknolijia mbali Teknolojia ni nzuri maanake inakupasha yanayojiri papo hapo . Pia inawakutanisha hata mkiwa mbalimbali ,lakini ukiwa na mpenzi wako mbona usiiweke hiyo simu ama Kompyuta mbali ? Mpenzi wako anataka kuongea nawe,kukubusu,kukumbatia kuwa karibu yako anataka kuisikia sauti yako lakini macho yako yanijishughulisha na kuongea kwa simu,mtandao wa kijamii ama unachapisha ujumbe . Je nayeye akianza kuienzi kompyuta yake kuwasabahi jamaa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii kutakuwepo na ndoa ? Ukiwa nyumbani na mpenzi wako jiepushe na Teknolojia . 15. Chezeni pamoja Kucheza pamoja kunaimarisha mahaba. Haijalishi kama mpenzi wako anajua kupiga densi zaidi yako au la , Mkiwa pamoja weka mziki anaoupenda kisha mwite aje mpige naye rhumba,salsa Bongo flava, reggae ,hip hop hata Chakacha kama ni mwenyeji wa pwani ! Chezeni miili yenu ikigusana! 16 Kaeni msemezane Mkiwa kitandani na mpenzi wako mnazungumza ? Unamwambia nini kitandani ? Unazungumzia kuhusu madeni yako? Usidhubutu ,mwambie kuhusu mahitaji yenu ya kimahaba ,mwambie unampenda na kuwa haujui ungelikuwa wapi bila yeye . 17. Andikianeni barua za kimapenzi. Mwandikie barua za kimapenzi na uiache kwenye gazeti au kwenye tarakilishi ,kitu ambayo itamfanya afurahie,kutoka kwa mwandiko wako. 18. Puuza watu ambao watakuvuruga amani kati yenu Hao watu wanaokutongoza kupitia kwenye mitandao ya kijamii ima ni Facebook,WhatsApp wazuie wasikutumie ujumbe wa moja kwa moja. Ni mahasidi hao,wala hawakupendi Ng'ooooo!!!! Wao wangalikupenda kweli hawangejaribu kukuletea huzuni kwa kuvunja penzi/ndoa yenu. Kujihusisha nao inapunguza makali ya penzi lenu ukidanganyika kuwa unapendwa ilhali ni Wanafiki tu 19.Nunua marashi mapya Mnunulia mpenzi wako marashi yanayonukia vyema yatakayo fanya mpenzi wako afurahie kuwa nawe. 20.Jiachilie Kuwa na uwazi wa mawazo ukiwa na mpenzio Jaribu njia tofauti za kufanya mapenzi Zungumzeni kama ambao mnaigiza sinema za mahaba Mchezee shere Mtanie mpenzi wako ... Read More
MASWALI 60 YA KUMUULIZA MPENZI WAKO , YANAWEZA KUWA YA KUCHEKESHA& KUFURAHISHA:  Mawasiliano hujenga mahusiano mazuri, bila hivyo kutakuwa na tofauti fulani kati ya wawili wapendanao .watu wengi wanaamini kuwasiliana kunajenga uhusiano mzuri, hebu fikiria kama una rafiki yako mnaopendana hakutafuti hata kama umekuwa mbali kwa muda mrefu , si inaboa sana? nikupe mfano mmoja , wanandoa wakiwa pamoja nyumbani , siku hiyo wameamua wasiende mahali popote, unafikiri wangekalia kufanya tendo la ndoa siku nzima? jibu ni hapana. lakini wanakuwa na mawasiliano ya aina yake , Hapa nakuletea maswali unayotakiwa kumuuliza mpenzi wako mkiwa mko mmekaa jioni , au katika mapumziko yenu, lakini uwe makini hapa kuna wengine hawapendi umdadisi, ile kuna wengine ni waelewa na watakuelewa. mwanaume mwenye kukupenda atakuelewa. MASWALI YA KUMUULIZA KIJANA UMPENDAE. 1.Unakumbuka nini cha utotoni ambacho uliwahi kufanya? 2.kwenye hii tamthilia unampenda mwigizaji gani? 3.nafikiri nimepoteza namba yangu ya simu , naweza chukua ya kwako? 4.ni kipi kinachoweza kukufanya ucheke zaidi katika maisha yako? 5.kwa mfano wewe ungekuwa muhudumu ungechagua watu wa jinsia gani wa kuwahudumia ? 6.umewahi kutuma maombi ya urafiki kwa rafiki wa kike? 7.kabla ya mimi umewahi kuwa na nani? 8. je unaweza kukosa kitu unachokipenda kwa ajili yangu? 9.kama ukijikuta umeangukia kwa mwanamke , utaitumiaje hio siku wewe kama wewe? 10.wewe ni wangu? 11.unampenda nani? 12. unaamini kama kuna mungu? 13.unawezaje kumjua mtu kama ni rafiki wa kweli? 14.Unapenda kuwa smart au ni vyovyote tu? 15.je unweza kukaa na mtu usiempenda? 16.Unajisikiaje unapokuwa na mimi? 17. Utamjuaje mchumba wa kweli? 18.Unatafuta kitu gani kwa msichana? 19.Utajielezeaje wewe mwenyewe? 20.je, utaweza kunielezea mimi? 21.Kuna tatizo gani umewahi kukumbana nalo? 22.ni mzuri au ni mbaya? 23.umewahi kumwacha msichana? 24.umewahi kujihusisha na kitu chochote kibaya? 25.busu la kwanza kabisa ulimbusu nani? 26.ulifanikiwa? 27. Unapenda staili ipi ya mapenzi?kitandani. 28. Tamthilia ipi unaipenda? 29.Unapenda chakula gani? 30.unapenda rangi gani? 31.unapenda mziki gani ? 32.ukiwa mtoto ulikulia wapi? 33.Ulipendelea kucheza mchezo gani wakati wa utoto? 34. unashangilia timu gani ya mpira? 35.mwigizaji gani unamkubali sana duniani? 36. tamthilia ipi ni nzuri? 37.unawafurahia marafiki zangu? 38.unaipenda kazi yako? 39.unategemea kubadilisha nininkatika maisha yako? 40.Kuna kitu chochote ambacho huwa nakuudhi hata kama ni cha kijinga ambacho hujawahi kujaribu kuniambia? MASWALI MENGINE YA KINDANI ZAIDI YA KUULIZA UNAPOKUWA NA MTU ANAYEKUTHAMINI. 41.Ukipoteza nguvu zako wakati wa usiku , je ni kitu kipi utanieleza ili niridhike? 42.Ni sehemu gani ya mwili wangu , macho yako yakiona utashangaa kama hujawahi kuniona nikiwa uchi? 43.Umewahi kusikia mwili wangu ukinuka? 44.kama nakuhitaji, natupo pamoja wakati huo, unawezaje kunielewa, wengine husema unawezaje kunisoma,je unafikiri utajua dalili? 45.umewahi kuota uko na mwanamke ukifanya mapenzi? 46.umewahi kucheza kama dactari wakati wa utoto? 47. ni aina gani ya mapenzi ungependa kuwa nayo katika maisha yako? 48.Umewahi kufumwa ukiwa uchi? 49.je una uzoefu gani katika mahusiano? 50.unaweza kuniambia vitu vya kuchekesha ulivyofanya wakati wa utoto? 51.Kama ungetaka kubadili jinsia ni sehemu ipi ungependelea,na kwa nini? 52.Kuna siri yeyote hujaniambia? 53.UTU. je unafikiri umbo la mtu lina tatizo katika mahusiano? 54.tukipata watotro mimi na wewe ungependa watoto wetu wafuate tabia zetu? 55.unapenda staili ipi ya chini au ya juu? 56. umewahi kumpiga mtu kofi? 57.je wewe ni mkweli? 58.kitu gani unachokipenda ambacho hujawahi kuniambia? 60 .Nikimwangalia mwanaume mwingine na kumsifia utaudhika?je kuna tabia yeyote ya udanganyifu ambayo hujaipenda kwangu?unaweza kuacha kitu unachokipenda kwa kumsaidia rafiki? fuatilia maswali mengine mengi yatakuja. toa maoni yako katika maswali haya. ... Read More
JIFUNZE KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPENZI YA DHATI NA WEWE: Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi". Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. MTU AMBAYE HAKUPENDI KWA DHATI: ==> Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako. ==> Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?" Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo". Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu. ==> Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo. ==> Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie. ==> Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. ===> Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo. MTU ANAYEKUPENDA KWA DHATI: ==> Hachoki kukwambia NAKUPENDA, kwani anajisikia raha sana pale atamkapo neno hilo juu yako kwahiyo unaweza ukawa kama wimbo wake kwako. ==> Anajivunia kuwa na wewe na atapenda kukupa sifa nzuri kila mara, yani Hachoki kukusifia. Atakushauri pale unapokosea ili uwe katika njia nzuri. Unaponuna atajua cha kufanya ili wewe ufurahi na kurudi kwenye hali ya kawaida. ==> Hachoki kukuombea mema na kukutakia mafanikio. ==> Atapenda kukueleza ukweli kila mara ili uweze kujenga uaminifu na imani juu yake. ==> Wewe utakuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake, atakuthamini na kukujali. Tatizo lako litakuwa sawa na tatizo lake, atakupa ushauri bila kuchoka. ==> Kabla ya kumuuliza swali kuwa "je unanipenda?" atakuwa ameshakujibu tena kwa hisia nzito kuwa "nakupenda sana mpenzi wangu". ==> Hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, kwakuwa wewe ndiye furaha yake. ====> Thamani yako ni kubwa sana kwake, anakuona mpya kila siku na hachoki kuvutiwa na wewe. Anakupenda kwa kumaanisha na si kukupenda kimazoea tu. Neno NAKUPENDA litamtoka moyoni na ataridhihirisha kwa kinywa chake. Mtambue mtu huyu kuwa anakupenda kwa dhati. NB: Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Si vyema kutumia mapungufu ya mwenzio kama fimbo katika mapenzi, cha muhimu ni kumuelimisha na kumuelekeza ili muweze kwenda sambamba. Nadhani baadhi ya maswali ya wadau yatakuwa yamejibiwa na hiyo mada. Kama kuna nyongeza au swali lolote kuhusiana na hiyo mada tuambiane hapa na kupatiana majibu hapa hapa wadau. ... Read More
Wanawake: Mumeo akikukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana  Usiku kama mumeo kakukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana, hata malaika baraka hawawezi shuka kwenu. Huyo ulionae amezaliwa kwao kaja na tabia zake na wewe umezaliwa kwenu una tabia zako. Sasa ukitaka kila kitu kiwe wewe unavyotaka atakuwa mwanao tena huyo sio mumeo samehaneni kwa kila mnalofanyiana. Usiweke vinyongo tena ukajua unamkomoa mana unavyonuna ndo mchepuko unavopata chance ya kuwasiliana na si kila mwanaume anamchepuko wengine washkaji tu sasa ukijitia umenuna kisa umemuona kachat, sijui umekuta meseji sijui nini utakonda uzikwe na presha na unavyotiwa kaburini tu huku wenzio wanamtext pole kazi ya Mungu mpenzi. Gangamala mtoto wa kike sio kidogo kununa kama unga wa ngano ulokosa amira. Tabasamu njia nzuri na sahihi ya kumuua mtu akikosea ukatabasamu ataanza kutafuta mchawi kumbe mchawi mwenyewe, ataanza kutoka kujua kwanini hujakasirika atatulia tu akiamini anakuvizia kumbe anajivizia. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: